INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Friday, 11 September 2015
Thursday, 10 September 2015
Wednesday, 9 September 2015
MATOKEO YA USAILI ULIOFANYIKA TAREHE 04/09/2015
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
MATOKEO YA USAILI ULIOFANYIKA TAREHE 04/09/2015
MATOKEO YA USAILI ULIOFANYIKA TAREHE 04/09/2015
Sunday, 06 September 2015 14:25 | ||||
Wasailiwa waliochaguliwa kuendelea na usaili wa mahojiano wanatakiwa kufika kwa muda na tarehe kama ilivyopangwa kwenye ratiba. Wasailiwa wanakumbushwa kufika na vyeti vyao halisi (Original Certificates)
|
Tuesday, 8 September 2015
Monday, 7 September 2015
Sunday, 6 September 2015
Magufuli: Nikiwa Rais Nitachukua Mashamba Yasiyotumika
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
MGOMBEA urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk John Magufuli ameahidi kunyang’any’a mashamba ambayo yamehodhiwa na watu bila kutumiwa kwa ufugaji wala kilimo, na kuyagawa kwa wakulima na wafugaji wasio na maeneo ya kilimo.
Alisema hayo alipozungumza na wananchi wa wilaya za Ulanga na Kilombero mkoani Morogoro jana.
MGOMBEA urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk John Magufuli ameahidi kunyang’any’a mashamba ambayo yamehodhiwa na watu bila kutumiwa kwa ufugaji wala kilimo, na kuyagawa kwa wakulima na wafugaji wasio na maeneo ya kilimo.
Alisema hayo alipozungumza na wananchi wa wilaya za Ulanga na Kilombero mkoani Morogoro jana.
Dk
Magufuli alisema akiwa rais, kuna mambo mengi anaweza kufanya,
kukabiliana na migogoro ya ardhi kati ya wakulima na wafugaji na
mojawapo ni kutoa ardhi zaidi kwaajili ya wakulima na wafugaji, ili
kuondoa uhaba wa ardhi, unaosababisha ugomvi wa maeneo ya kulishia
mifugo na kulima.
Alisema
kuna watu wanamiliki maelfu ya eka za ardhi bila kulima na kwamba
atanyang’any’a mashamba hayo ambayo yamehodhiwa na watu hao bila
kutumiwa kwa ufugaji wala kilimo.
Akihutubia maelfu ya wananchi, pia Dk Magufuli alisema kuwa anajivunia uzoefu wa marais wastaafu wa Awamu ya Pili mpaka Awamu ya Nne na wa Zanzibar, kwamba ndio atakaowafuata kwa ushauri akikwama popote.
Akihutubia maelfu ya wananchi, pia Dk Magufuli alisema kuwa anajivunia uzoefu wa marais wastaafu wa Awamu ya Pili mpaka Awamu ya Nne na wa Zanzibar, kwamba ndio atakaowafuata kwa ushauri akikwama popote.
Alisema hiyo ni moja ya tofauti kubwa kati yake na wagombea wengine wa urais.
“Nitaingia Ikulu nikiwa na washauri wazuri, nikikwama mahali nitakwenda kwa Rais Jakaya Kikwete, nikikwama nitaenda kwa mzee Benjamin Mkapa, nikikwama tena nakwenda kwa mzee Ali Hasan Mwinyi.
“Nitaingia Ikulu nikiwa na washauri wazuri, nikikwama mahali nitakwenda kwa Rais Jakaya Kikwete, nikikwama nitaenda kwa mzee Benjamin Mkapa, nikikwama tena nakwenda kwa mzee Ali Hasan Mwinyi.
“Wako
wengi, upo ushauri nitauchukua kutoka kwa mzee Salmin Amour (Rais
Mstaafu wa Zanzibar), Dk Ali Mohamed Shein na kwa Amani Abeid Karume,”
alisema.
Kutokana na fursa hiyo ya kiuongozi aliyonayo ndani ya Chama Cha Mapinduzi, Dk Magufuli aliomba Watanzania wote bila kujali vyama vya siasa, makabila wala dini kumpa kura kwa wingi kwa kuwa atakuwa na washauri wazuri wenye uzoefu.
Kutokana na fursa hiyo ya kiuongozi aliyonayo ndani ya Chama Cha Mapinduzi, Dk Magufuli aliomba Watanzania wote bila kujali vyama vya siasa, makabila wala dini kumpa kura kwa wingi kwa kuwa atakuwa na washauri wazuri wenye uzoefu.
Alisema
wagombea wengine, akiwemo wa Chadema anayeungwa mkono na vyama
vinavyounda Ukawa, Edward Lowassa, hawataweza kupata ushauri wa washauri
hao kama ilivyo rahisi kwake.
Kutokana
na uhakika huo wa washauri wazoefu, Dk Magufuli alisema ndio maana
baadhi ya wagombea hao wanaweza kuja na ahadi za uongo, ikiwemo ya
kuondoa nyumba za tembe na za nyasi.
Aliwataka
wananchi kuwapima wagombea hao katika ahadi zao, kwa kuwa baadhi
walikuwepo ndani ya Serikali kwa muda mrefu, lakini walishindwa kuondoa
nyumba hizo katika majimbo walikotokea.
Dk
Magufuli alisema yeye hataahidi kuondoa nyumba hizo, bali anaahidi
kushusha bei ya vifaa vya ujenzi hasa saruji, mabati na misumari, ili
wananchi wanaofanya kazi wajenge nyumba bora.
Katika
kuongeza idadi ya Watanzania wanaofanya kazi ili kufikia lengo hilo, Dk
Magufuli alisema katika kila mtaa na kijiji, serikali yake itatoa Sh
milioni 50 kwa ajili ya kuanzisha na kukuza biashara ndogo za wanawake
na vijana.
Alisema
atataka kila anayefanya kazi apate kipato kizuri kitakachomsaidia
kukabiliana na mahitaji ya maisha yake, ikiwemo kujenga nyumba bora
kutokana na kushushwa kwa bei za bidhaa za ujenzi.
Kwa wakulima, alisema atahakikisha pembejeo sahihi zinatolewa kwa wakati na mazao yatakayovunwa, itakuwa marufuku kwa Serikali kukopa mazao yao.
Kwa wakulima, alisema atahakikisha pembejeo sahihi zinatolewa kwa wakati na mazao yatakayovunwa, itakuwa marufuku kwa Serikali kukopa mazao yao.
Dr. Slaa Aishambulia CHADEMA Kwa Mara ya Pili.......Asisitiza Kuwa Lowassa ni Fisadi
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
ALIYEKUWA Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk Wilbrod Slaa amejitokeza hadharani kwa mara nyingine na kujibu watu waliojitokeza kuponda hotuba yake, aliyoitoa hivi karibuni kuwa hawana hoja zaidi ya kumtukana.
ALIYEKUWA Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk Wilbrod Slaa amejitokeza hadharani kwa mara nyingine na kujibu watu waliojitokeza kuponda hotuba yake, aliyoitoa hivi karibuni kuwa hawana hoja zaidi ya kumtukana.
Akizungumza
kupitia kituo kimoja cha Televisheni jijini Dar es Salaam, Dk Slaa
alisema madai yote, yaliyotolewa juu yake na baadhi ya watu wakiwemo
viongozi wa Chadema na vyama vinavyounda Ukawa, baada ya hotuba
aliyoitoa, hayana msingi wowote na kwamba ni kuishiwa hoja, ndio maana
walimtukana badala ya kujibu hoja.
“Nashukuru
hoja zangu zote hawajazijibu, sasa wanapiga tu propaganda, hata Rostam
Aziz alijaribu kujibu, lakini akatukana tu kama alivyonitukana mwaka
2007 badala ya kujibu hoja na mimi nasema ufisadi ni hoja,” alisema Slaa.
Aidha,
Dk Slaa alisema hawezi kumpeleka mahakamani Rostam ambaye ni kada wa
CCM, ambaye amemtaka Dk Slaa ampeleke mahakamani kama anao ushahidi kuwa
anaunga mkono mgombea urais kwa tiketi ya Chadema, Edward Lowassa.
Slaa amesema yuko tayari kutoa ushahidi wake pale Jamhuri itakapomfungulia mashitaka. “Wale
ambao hawaelewi taratibu za kesi, kuna kesi za madai ambapo mtu binafsi
anafungua kesi na kesi za jinai ambazo mtu binafsi hawezi kufungua ila
Jamhuri, kesi za Jamhuri mtu huwezi kufungua, wewe ni shahidi… mimi
nikiitwa nitakwenda kutoa ushahidi dhidi ya Rostam Aziz,” alisema Dk Slaa.
Aidha,
alisema ni kweli vijana wanataka mabadiliko na ni hoja ya msingi na pia
wakulima ambao hawafaidiki na kilimo chao, wanataka mabadiliko, vivyo
hivyo kwa makundi mengine.
“Nimesema mimi Lowassa hafai, leo, lini ameanza kuwa rafiki wa masikini?
“Nimesema mimi Lowassa hafai, leo, lini ameanza kuwa rafiki wa masikini?
"Lini ameanza kuwa safi?Watanzania waache ushabiki usiofaa wapime kwa vigezo, ushabiki usio na tija utatuangamiza,”
alisema Dk Slaa, akijibu hoja mbalimbali ambazo zimejitokeza baada ya
hotuba yake hiyo, aliyoitoa mwanzoni mwa wiki hii baada ya kutangaza
kuachana na mambo ya siasa na kubaki mshauri wa wananchi.
Akijibu
shutuma dhidi yake baada ya kutuhumiwa kutoa habari za upotoshaji juu
ya maaskofu, Slaa alisema alichokieleza siku ile anatangaza kujiengua
kwenye siasa ni alichoambiwa na Mchungaji wa Kanisa la Ufufuo na Uzima,
Josephat Gwajima kwamba maaskofu 30 kati ya 34 walihongwa.
“Tatizo
halikuwa fedha bali askofu anaona sifa mimi kumuunga mkono mtu ambaye
alitumia fedha kununua maaskofu, na Watanzania nawaomba mtulie
msikurupuke na maneno bila kuyachambua, taifa linaangamia kwa sababu ya
ushabiki usio na tija, nimeshtushwa na kauli yake, kiongozi anayepaswa
kukemea rushwa, maovu… baba askofu piga magoti Mungu wako atazame
dhamira yako,” alisema.
Dk
Slaa alisema yeye ana uwezo wa kupambanua siasa na mambo mengine na
kwamba ni kweli alikutana na Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe
katika Hoteli ya Serena na hiyo ni katika kupata taarifa alizozihitaji
kwa ajili ya kazi yake ya utafiti na kwamba Mwakyembe ni chanzo cha
taarifa cha kwanza na kwamba hakufanya kwa siri.
Akizungumzia
picha yake ambayo ilizunguka kwenye mitandao ya kijamii, ikimuonesha
yeye akiwa na Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba na Mwenyekiti wa
CUF, Profesa Ibrahim Lipumba alisema picha hiyo ni wakati wa mkutano wa
vyama vya siasa na Rais wa Ujerumani, Joachim Gauck alipokuja kwenye
ziara ya kikazi Februari mwaka huu.
“Kwenye
picha hizo ambazo zinatuonesha mimi, Mwigulu na Profesa Lipumba
tukimpokea Rais wa Ujerumani alipotembelea Tanzania, leo ndio zinaletwa
kuonesha eti haya ndiyo mazungumzo ya kumng’oa Slaa, naomba niwaambie
warudi nyuma waangalie hizo picha ni za lini hazina uhusiano na mimi
kujiondoa,” alisema Dk Slaa.
Aidha,
Dk Slaa alisema kuwa kuna propaganda nyingine ambayo imetumika ambapo
watu wametuma pia picha ambazo zinamuonesha akiwa kwenye ndege,
ikisemekana kwamba ametoroka nchini baada ya hotuba, sio kweli.
Alikiri
kusafiri lakini sio kwa kutoroka, kama ambavyo imedaiwa na baadhi ya
watu na kwamba amekuwa akipiga picha na watu kwenye ndege na kwamba
picha hiyo ni ya safari ambayo alishasafiri na kurudi.
“Magazeti
na mitandao wanasema Dk Slaa hayuko nchini, lakini nadhani sasa
Watanzania wanaona sasa niko hapa studio Dar es Salaam na siko
Marekani,” alisema Dk Slaa na kuongeza kuwa uongo huo unaonesha ni aina gani za siasa zilizopo hapa nchini.
Alisema hoja ya wapi amepata fedha kwenda Serengeti na kuishi hotelini ni hafifu. “Nilikwenda
Marekani na kukaa kwa zaidi ya miezi 12 na kutembelea majimbo 13 na
sikulipiwa na mtu yoyote zaidi ya chama changu kulipia shilingi 500,000
kwa mshauri aliyeandaa nyaraka ya kunisaidia katika ziara hiyo, mbona
hawakuniuliza nimepata wapi fedha hizo?”
Lembeli Aanika MAOVU Yaliyofichwa Wakati wa Operesheni Tokomeza
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
MGOMBEA ubunge wa jimbo la Kahama, James Lembeli kupitia tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ameishambulia serikali ya CCM na kueleza kwamba serikali hiyo haiwezi kuwapatia wananchi maendeleo kutokana na kuwa na mfumo mbovu wa kiutawala.
MGOMBEA ubunge wa jimbo la Kahama, James Lembeli kupitia tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ameishambulia serikali ya CCM na kueleza kwamba serikali hiyo haiwezi kuwapatia wananchi maendeleo kutokana na kuwa na mfumo mbovu wa kiutawala.
Mbali
na hilo Lembeli alisema serikali ya CCM ndiyo serikali pekee yenye
mfumo kandamizi, viongozi wake ni walaghai wakubwa na imekuwa na mfumo
mchafu wa kulindana mafisadi kwa mafisadi huku wananchi wa kawaida
wakiendelea kutaabika.
Lembeli
ambaye awali alikuwa mbunge wa CCM jimbo la Kahama na baadaye kutimkia
Chadema, alitoa kauli hiyo wakati wa uzinduzi wa kampeni za Chadema
zilizofanyika katika viwanja vya Freeman Mbowe ambapo uwanja huo
ulijengwa na mbunge anayemaliza muda wake na kutetea jimbo hilo Prof
Kulikoyela Kahigi.
Kiongozi
huyo ambaye alikuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa kampeni hizo
alitonesha vidonda vya wafugaji wa jimbo hilo kwa kueleza kwamba
serikali imekalia ripoti ya uchunguzi wa Tume iliyoundwa na bunge kwa
ajili ya Operesheni tokomeza.
Alisema
sababu kubwa ya serikali kushindwa kuweka hadharani taarifa hiyo ambayo
Lembeli alikuwa mwenyekiti ni kutokana na vitendo vingi vilivyofanywa
vilikuwa vikihusisha vigogo wa serikali na ndiyo maana kuna hali ya
kulindana licha ya kuwa wapo watu ambao wamepata vilema na wengine
kupoteza maisha.
Alisema
katika taarifa hiyo kuna mambo mengi ya kutisha ambayo yalifanywa na
watumishi wa serikali ikiwa ni pamoja na kudhalilisha utu wa mtu, mauaji
pamoja na uharibifu wa mali za wananchi hususan wafugaji.
“Ndugu
zangu wana Bukombe kuna msemo usemao siri ya mtungi aijuaye kata, sasa
mtungi ni CCM na kata ni mimi (Lembeli) mimi nimetoka CCM baada ya kuona
kwamba hakuna chama dharimu, kandamizaji, kinachotumia migogo ya
wanyonge masikini kujinufaisha.
“Sijaona
chama chenye viongozi ambao wanalinda ufisadi wa kutisha, wizi wa
kutisha pamoja na watu ambao hata upeo wa kufikiri umekwisha bali
wamekuwa watu wa kupokea vitisho vya hali ya juu na hatima yake
wanatugeuza kuwa wapumbavu na malofa,” amesema Lembeli.
Akizungumzia
ahadi za mgombea urais kupitia CCM, Dk. John Magufuli, Lembeli amesema
kwamba mgombea huyo kwa sasa amekuwa akiwalaghai wasukuma kwa madai
kwamba atawapatia maendeleo pale tu atakapochaguliwa.
Amesema kauli hiyo ni ya uongo na unafiki kamwe Dk. Magufuli awezi hata kuwatetea wasukuma wenzake.
“Nawapa
mifano miwili tu wakati Dk. Magufuli akiwa waziri wa mafugo aliwasaidia
nini wafugaji wakati mifugo ikiteketea na kukosekana kwa soko.
“Mbali
na hilo alipochaguliwa kuwa waziri wa mifugo na uvuvi ni nani ambaye
alikuwa akichoma kokolo za wavuvi kwa madai hazifahi, alikuwa wapi
kushika nyavu hizo zikiwa madukani na kuzipiga marufuku wakati huo huo
aliendelea kuchoma nyavu hizo, hapo kweli ana nia ya kuwakomboa
watanzania hususani wakulima na wafugaji,” alihoji Lembeli.
Saturday, 5 September 2015
Friday, 4 September 2015
MKUTANO WA LOWASSA MPANDA-KATAVI-RUKWA
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania katika mwamvuli wa
UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward