INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Monday, 30 June 2014
Sunday, 29 June 2014
TANGAZO LA ORODHA YA MAJINA YA KUITWA KAZINI 27 JUNI 2014,KWA WAOMBAJI WALIOFANYA USAILI TAR.05 HADI 06 JUNE
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY1
SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA
Kumb. Na. EA.7/96/01/G/30 27 Juni, 2014 KUITWA KAZINI
SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA
Kumb. Na. EA.7/96/01/G/30 27 Juni, 2014 KUITWA KAZINI
Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma inapenda kuwataarifu waombaji kazi wa nafasi mbalimbali waliofanya usaili kuanzia tarehe 05 hadi 06 Juni, 2014 kuwa walioorodheshwa katika tangazo hili wamefaulu usaili na wanatakiwa kuripoti kwa Mwajiri kama ilivyoonyeshwa katika tangazo hili. Aidha, wanatakiwa kuripoti katika vituo vyao vipya vya kazi katika muda ambao umeainishwa katika barua zao za kupangiwa vituo vya kazi wakiwa na vyeti halisi (Originals Certificates) vya masomo kuanzia kidato cha nne na kuendelea ili vihakikiwe na mwajiri kabla ya kupewa barua ya ajira. Kwa Waombaji Kazi walioitwa katika Wizara ya Maliasili na Utalii wote kwa pamoja wanatakiwa kuripoti Chuo Cha Taifa cha Utalii Tandika, Wilayani Temeke tarehe 14/07/2014 Saa 2:00 Asubuhi Bila kukosa.
Barua za kuwapangia vituo vya kazi kwa walioitwa katika Taasisi ya Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania zimetumwa kupitia anuani zao. Aidha, wale ambao majina yao hayakuonekana katika tangazo hili watambue kuwa hawakupata nafasi/hawakufaulu usaili, hivyo wasisite kuomba mara nafasi za kazi zitakapotangazwa tena. ANGALIA MAJINA HAYO...HAPA CHINI
MAJINA MAPYA YA VIONGOZI CUF TAIFA BAADA YA UCHAGUZI MKUU
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
1.MWENYEKITI PROFESA IBRAHIM LIPUMBA
2.KATIBU MKUUU......MAALIM SEIF
3. Naibu Katibu Mkuu (Bara), Mhe. Magdalena Sakaya.
4. Naibu Katibu Mkuu (Zanzibar), Mhe. Nassor Ahmed Mazrui.
2.KATIBU MKUUU......MAALIM SEIF
3. Naibu Katibu Mkuu (Bara), Mhe. Magdalena Sakaya.
4. Naibu Katibu Mkuu (Zanzibar), Mhe. Nassor Ahmed Mazrui.
HOTUBA YA MH.MIZENGO PINDA-WAZIRI MKUU WAKATIA AKIFUNGA SHUGHULI ZA BUNGE JANA DODOMA
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

UTANGULIZI
a) Masuala ya Jumla
Mheshimiwa Spika,
1. Naomba nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu mwenye wingi wa Rehema kwa kutupatia uzima na afya hadi kufikia siku ya leo. Tumekuwepo hapa kwa takriban miezi miwili ambapo tumeweza kupokea na kujadili Taarifa za Mapitio ya Utekelezaji wa Kazi za Serikali kwa mwaka 2013/2014 na Mwelekeo kwa mwaka 2014/2015 kwa Wizara mbalimbali na hatimaye kupitisha Bajeti ya Serikali kwa mwaka 2014/2015.

2.
Napenda kutumia nafasi hii ya awali kuwapongeza Waheshimiwa Wabunge
wote kwa kazi nzuri ya kutukuka ambayo wameifanya kwa nidhamu na ufanisi
mkubwa, hususan wakati wa Mjadala wa Bajeti ya Serikali na Mafungu ya
Wizara za Kisekta. Kipekee niwashukuru Wajumbe wa Kamati ya Bajeti chini
ya Uongozi mahiri wa Mheshimiwa Mtemi Andrew John Chenge, Mbunge wa
Jimbo la Bariadi Magharibi kwa kazi yao nzuri ya kuchambua Bajeti ya
Serikali na Sheria zinazoambatana na masuala ya Bajeti. Changamoto
zilikuwa nyingi, lakini kwa pamoja tumekubaliana na
kuafikiana. Kazi kubwa iliyoko mbele yetu ni kwenda kushirikiana na
Wananchi katika utekelezaji wa Bajeti hii ili kuwaletea maendeleo.
Mheshimiwa Spika,
3. Katika kipindi hiki tukiwa hapa Bungeni, yapo matukio ya kusikitisha yaliyotokea ambapo baadhi ya Waheshimiwa Wabunge walipoteza Wapendwa wao. Aidha, yapo matukio ya Kitaifa yaliyosababisha kupoteza maisha ya Ndugu, Jamaa na Marafiki. Napenda kutumia nafasi hii kuwapa pole Waheshimiwa Wabunge na Watanzania wote waliofikwa na misiba na majanga mbalimbali, ikiwa ni pamoja na wote waliopotelewa na Ndugu, Jamaa na Marafiki.

4. Kipekee niwape pole ndugu, jamaa na marafiki waliopotelewa na ndugu zao na wote waliopata majeraha wakati kulipotokea Mlipuko wa Bomu pale Darajani, Zanzibar. Tukio hili la kusikitisha halipendezi kwa Nchi yetu. Niwaombe Wananchi wote kwa umoja wetu tushirikiane kuwa Walinzi katika maeneo yetu na kuwezesha kuwatambua mapema wale wote wenye nia mbaya ya kuharibu amani na utulivu katika Taifa letu.

Saturday, 28 June 2014
MATOKEO BRAZIL NA CHILE:BRAZIL YATINGA ROBO FAINALI KWA MATUTA,HONGERA CHILE
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
WENYEJI Brazil wameitoa Chile kwa penalti 3-2 katika mchezo wa hatua ya 16 Bora Kombe la Dunia mjini Uwanja wa Belo Horizonte, kufuatia sare ya 1-1 ndani ya dakika 120.
WENYEJI Brazil wameitoa Chile kwa penalti 3-2 katika mchezo wa hatua ya 16 Bora Kombe la Dunia mjini Uwanja wa Belo Horizonte, kufuatia sare ya 1-1 ndani ya dakika 120.
AJALI YA NOAH SINGIDA-WATATU WAFARIKI,KUMI WAJERUHIWA
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Watu
watatu wamekufa na wengine kumi wamejeruhiwa baada ya gari walilokuwa
wakisafiria aina ya Noha kupasuka tairi ya nyuma na kubingirita mara
tatu katika kijiji cha Januka manispaa ya Singida.
ADA VYUO VYA UALIMU JUU,YAPANDA ZAIDI
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

\Serikali imepandisha maradufu ada kwa wanafunzi wanaosomea ualimu kwenye vyuo vya ualimu nchini kuanzia muhula ujao wa masomo.
BARCELONA YAMWINDA SUAREZ

Licha ya
kukabiliwa na marufuku ya FIFA ya miezi minne kwa kumng'ata mlinzi wa
Italia Giorgio Chiellini Barcelona ya Uhispania haijakata tamaa ya
kumsajili mshambulizi machachari wa wa Uruguay Luiz Suarez.