Friday, 28 March 2014
Siri ya CCM kung’ang’ania Serikali mbili kikatiba
Siri ya CCM kung’ang’ania Serikali mbili kikatiba
- Msimamo huo ni kinyume na mapendekezo au matakwa ya wengi kama ilivyoainishwa kwenye Rasimu ya Pili ya Katiba iliyoandaliwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba
Katika maisha ya kawaida, binadamu ana msimamo wake na hata uamuzi asiopenda ubadilike.
Katika medani ya siasa nchini msimamo wa Chama Cha
Mapinduzi ( CCM) kuhusu Muungano na muundo unafahamika. Ni muundo wa
kutaka Serikali mbili ambao chama hicho unakipigania kwa udi na uvumba.
Hata hivyo, msimamo huo ni kinyume na mapendekezo
au matakwa ya wengi kama ilivyoainishwa kwenye Rasimu ya Pili ya Katiba
iliyoandaliwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba.
Tume hiyo iliyokuwa chini ya Jaji Joseph Warioba
ilikusanya maoni ya wananchi na ilipendekeza muundo wa Muungano wa
Serikali tatu.
Hivi karibuni akifungua Bunge Maalumu la Katiba,
Rais Jakaya Kikwete akaunga mkono msimamo wa chama chake, jambo
lililoibua mjadala unaoendelea hadi sasa.
Hoja ya Serikali mbili
Kwanini CCM wanataka Serikali mbili na siyo tatu
au moja kama ilivyo maoni ya wananchi walio wengi kwa mujibu wa maelezo
ya Tume ya Warioba? Makala haya yanachambua hoja hiyo.
Profesa Bakar Mohammed ni Mhadhiri Mwandamizi na
Mkuu wa Idara ya Siasa na Utawala ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam,
anayesema msimamo wa CCM wa kudai Serikali mbili unatokana na hofu ya
uhafidhina wa kuogopa mabadiliko.
Anasema viongozi wengi wa CCM wanasumbuliwa na
hofu na woga wa mabadiliko na kwamba wanakuwa wagumu kuyakubali
yanapotaka kutokea.
“Kama mtu unaangalia madaraka zaidi, lazima
kunakuwa na woga, na hii ni hulka ya binadamu kuwa na woga wa kuacha
kile ulichokizoea… Lakini ukiangalia masilahi ya nchi na kuacha yale
yanayokusukuma kusingekuwa na wasiwasi huu unaoonekana sasa,” anasema.
Anasema CCM inachofanya ni kuhakikisha haking’oki
madarakani, huku viongozi wake wakiamini kuwa wana sifa za kuongoza na
siyo wengineo.
Profesa Bakari anailinganisha hofu ya sasa ya CCM
na ile waliyokuwa nayo viongozi wa chama hicho miaka ya 1990 zilipoanza
vuguvugu za mabadiliko ya siasa za vyama vingi. Anasema CCM kiliendesha
propaganda kuwa mfumo wa vyama vingi haukuwa na tija na ungeleta vita.
Seif: Hatuko tayari kujadili serikali mbili
Zanzibar. Makamu wa Kwanza wa
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad amesema chama
chake cha CUF hakiko tayari kujadili mfumo wa Muungano wa serikali mbili
kama inavyotetewa na wabunge wa CCM na Rais Jakaya Kikwete.
Amesema tayari amewaandikia barua Rais Kikwete na Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein kuwaeleza juu ya msimamo huo.
Maalim Seif alitoa msimamo huo jana kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Kibandamaiti mjini Unguja.
Isitoshe, alisema CUF imebaini kuwa kuna njama za
kufuta kipengele katika Katiba ya Zanzibar kinachosema; “Zanzibar ni
nchi” na kwamba hiyo ni sawa na kutwanga maji kwenye kinu kwa kuwa
Wazanzibari kamwe hawatakubali kufanya hivyo.
Maalim Seif alisema haikuwa mwafaka kwa Rais
Kikwete kukosoa mapendekezo ya Rasimu ya Katiba yanayotaka mfumo wa
Muungano kuwa wa serikali tatu.
Alisema Jaji Warioba aliweka kando itikadi yake ya
CCM katika utendaji wake kwenye Tume ya Mabadiliko ya Katiba na kuja na
uamuzi huo kwa vile ndiyo tiba ya kero za Muungano wa Tanganyika na
Zanzibar.
“Mapendekezo yaliyowasilishwa na Jaji Warioba
hayakuwa maoni yake, yale ni maoni ya wananchi, Tanganyika imevaa koti
la Muungano, ametoa ushahidi wake ili kujenga mwafaka katika kuendeleza
Muungano wenye mfumo wa serikali tatu,” alisema Maalim Seif.
Alisema Muungano wa serikali mbili hauvumiliki na
kama kuna watu wanaendelea kuutetea mfumo huo, Zanzibar inaweza kutumia
sheria yake ya kura ya maoni kuwauliza wananchi wanaotaka na wasiotaka
jambo hilo.
“Nimemwandikia barua Rais Kikwete, nakala
nimempelekea Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein, Tanzania Bara
wanataka Zanzibar iondoe kifungu cha Katiba kinachosema Zanzibar ni
nchi, jambo hilo halitapita...tutafanya kampeni wananchi walikatae,”
alieleza Katibu Mkuu huyo wa CUF.
Alisema ni jambo la kusikitisha katika hotuba yake
alijisahau kama ni mkuu wa nchi na analihutubia Bunge Maalumu badala
yake akaegemea kuwa mwenyekiti wa CCM.
Alisema haikuwa sahihi kutoa vitisho na kutaja
ikiwa Serikali ya Muungano chini ya Serikali tatu italegalega, jeshi
litachukua madaraka ya nchi.
“Rafiki na ndugu yangu Kikwete, usifikiri huu ni
wakati ule wa Julius Nyerere, akisema yeye hakuna wa kumpinga. Mambo
yamebadilika, usijifanye ni Nyerere mpya, hakuna atakayekusikiliza na
kubabaika,” alisisitiza Maalim Seif.
ROSE NDAUKA ADAIWA KUMTIBULIA DILI BATULI
ROSE NDAUKA ADAIWA KUMTIBULIA DILI BATULI
Akizungumza na Ijumaa kwa sharti la kutotajwa jina lake, chanzo kilisema, wazo la project ile alikuwa nalo Batuli lakini Rose akaingilia kati, hali iliyosababisha Batuli amnunie mwenzake.…

Mastaa wawili, Yobnesh Yusuph ‘Batuli’ na Rose Ndauka wamedaiwa kuwa kwenye bifu chanzo kikidaiwa ni Rose kumtibulia mwenzake dili la ile project ya kusafisha jiji iliyofanyika hivi karibuni.
Akizungumza na Ijumaa kwa sharti la kutotajwa jina lake, chanzo kilisema, wazo la project ile alikuwa nalo Batuli lakini Rose akaingilia kati, hali iliyosababisha Batuli amnunie mwenzake.
Alipopigiwa Batuli kwanza aling’aka lakini akasema hapendi kuzungumzia mambo hayo kwani yameshapita huku Rose akieleza kuwa, wazo la project hiyo alikuwa nalo kabla hajajifungua hivyo haoni kama kamtibulia Batuli dili lake.
HIVI NDIVYO MVUA ILIVYOHARIBU MAZINGIRA JIJINI DAR
HIVI NDIVYO MVUA ILIVYOHARIBU MAZINGIRA JIJINI DAR
Maji yakiwa yametuhama…
Maji yakiwa yametuhama kwenye shimo stendi ya mabasi Ubungo.
Mvua iliyonyesha usiku wa kuamkia jana na
leo imesababisha maafa kwenye baadhi ya maeneo ya jiji la Dar es Salaam
ambapo katika mizunguko ya kamera yetu imenasa eneo la nje ya stendi
ya Mkoa, Ubungo maji yakiwa yamejaa kila pande huku wafanyabiashara
wadogo wanaofanyia kazi eneo hilo, miavuli yao na vitendea kazi
vikisombwa na maji huku mashimo yaliyokuwa yamechibwa katika
utengenezaji wa barabara yakizidi kuporomoka.
Friday, 21 March 2014
WAALIMU BINZA SHULE YA MSINGI,WAKANA KUWAZOMEA WALIMU WA SHANWA SHULE YA MSINGI
WAALIMU BINZA SHULE YA MSINGI, WAKANA KUWAZOMEA WAALIMU
WA SHULE YA MSINGI SHANWA KATIKA WILAYA YA MASWA
Waalimu wa
shule ya Msingi katika Wilaya ya Maswa wamekanusha vikali juu kudaiwa kuwazomea Waalimu wenzao wa shule ya Msingi Shanwa zote
zikiwa katika Mji mdogo wa Maswa
Kwa mujibu
wa Mwalimu mkuu msaidizi Shule ya msingi Binza Bibi Iviri Swai alisema kuwa Ofisi
yake pamoja na Walimu wenzake wamesikitishwa mno na taarifa zilizo andikwa na gazeti
la Tanzainia daima la Feburuari 12,2014 toleo Namba 3357 kuwa si za kweli hata
kidogo jambo hilo halipo shuleni kwake
Mwalimu Swai
katika maelezo yake kwa mwandishi habari hizi alisema kuwa anachofahamu ujio wa
Afisa Elimu msingi kufika katika shuleni yake alikuwa na ujumbe wa kuwaeleza Walimu wa Shule
ya Binza na Shanwa juu ya ujio wa Rais Jakaya Kikwete katika Wilaya Maswa wala
hapakuwa na maelekezo mengine
Aidha alipo
ulizwa mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Shanwa Gilda Gogadi yeye kwa upande wake
alisema amesikitishwa na taarifa hizo zilizo andikwa na gazetii la Tanzania daima kuwa zilikuwa na
lengo la kuwachonganisha kati uongozi wa shule ya msingi Binza na Shule yake ya
Shanwa
“Inawezekana
mwadishi huyu hana madili ya uandishi wa habari na si dhani kama ni Mwandishi
wa habari anaye fahamu wajibu wake huyu ni mzushi na kama ameshindwa kazi ya
uandishi wa habari atafute kazi ingine au akandikie magazeti ya udaku hayo
ndiyo kazi yake umbeya na uzushi tu”alisema Mwalimu Gogadi
“Hata hivyo
pamoja na kuandika habari za uongo na kumchafua Afisa Elimu wetu ambaye
kimsingi bado ni mgeni katika Wilaya Maswa si kwamba ametuchafua sisi hiyo
amewachafua Walimu wote wa Halimashauri ya Maswa na Jamii nzima”alisema Gogadi
Kwa upande
wake Afisa Elimu katika Halimashauri ya Wilaya ya Maswa Mabeyo Bujimu
aliyehamia kutoka Halimashauri ya Kibondo mkoani Kigoma alisema kuwa
kazi yake ni kusimamia taaluma na Waalimu wote wa Shule za Msingi katika
Halimashauri ya Wilaya ya Maswa na Si vingenevyo
Bujimu
alibainisha zaidi kwamba kitendo cha kuandikwa na baadhi ya vyombo vya habari
hususani gazeti la Tanzania Daima ni kitendo cha kutaka kumdalisha na kudalisha
taaluma ya elimu kwa ujumla “sisi
Wataalamu[Walimu]hatuko katika majukwa ya kisiasa kazi yetu ni moja kuelimisha
watoto basi”alisisitiza Bujimu
“ Hivi
mwandishi kwa uelewa wako mimiDEO mzima] nitoe magizo kwa Walimu wa Binza wakazomee Walimu wa Shanwa nimeanza
jana kazi ya ualimu?huyu mwandishi ana
elimu ndogo yupo yupo tu nenda katika shule zote mbili Binza na Shanwa ukweli
utaupata huko”alisema kwa kujiamini Bujimu.
WAALIMU BINZA SHULE YA MSINGI, WAKANA KUWAZOMEA WAALIMU
WA SHULE YA MSINGI SHANWA KATIKA WILAYA YA MASWA
Waalimu wa
shule ya Msingi katika Wilaya ya Maswa wamekanusha vikali juu kudaiwa kuwazomea Waalimu wenzao wa shule ya Msingi Shanwa zote
zikiwa katika Mji mdogo wa Maswa
Kwa mujibu
wa Mwalimu mkuu msaidizi Shule ya msingi Binza Bibi Iviri Swai alisema kuwa Ofisi
yake pamoja na Walimu wenzake wamesikitishwa mno na taarifa zilizo andikwa na gazeti
la Tanzainia daima la Feburuari 12,2014 toleo Namba 3357 kuwa si za kweli hata
kidogo jambo hilo halipo shuleni kwake
Mwalimu Swai
katika maelezo yake kwa mwandishi habari hizi alisema kuwa anachofahamu ujio wa
Afisa Elimu msingi kufika katika shuleni yake alikuwa na ujumbe wa kuwaeleza Walimu wa Shule
ya Binza na Shanwa juu ya ujio wa Rais Jakaya Kikwete katika Wilaya Maswa wala
hapakuwa na maelekezo mengine
Aidha alipo
ulizwa mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Shanwa Gilda Gogadi yeye kwa upande wake
alisema amesikitishwa na taarifa hizo zilizo andikwa na gazetii la Tanzania daima kuwa zilikuwa na
lengo la kuwachonganisha kati uongozi wa shule ya msingi Binza na Shule yake ya
Shanwa
“Inawezekana
mwadishi huyu hana madili ya uandishi wa habari na si dhani kama ni Mwandishi
wa habari anaye fahamu wajibu wake huyu ni mzushi na kama ameshindwa kazi ya
uandishi wa habari atafute kazi ingine au akandikie magazeti ya udaku hayo
ndiyo kazi yake umbeya na uzushi tu”alisema Mwalimu Gogadi
“Hata hivyo
pamoja na kuandika habari za uongo na kumchafua Afisa Elimu wetu ambaye
kimsingi bado ni mgeni katika Wilaya Maswa si kwamba ametuchafua sisi hiyo
amewachafua Walimu wote wa Halimashauri ya Maswa na Jamii nzima”alisema Gogadi
Kwa upande
wake Afisa Elimu katika Halimashauri ya Wilaya ya Maswa Mabeyo Bujimu
aliyehamia kutoka Halimashauri ya Kibondo mkoani Kigoma alisema kuwa
kazi yake ni kusimamia taaluma na Waalimu wote wa Shule za Msingi katika
Halimashauri ya Wilaya ya Maswa na Si vingenevyo
Bujimu
alibainisha zaidi kwamba kitendo cha kuandikwa na baadhi ya vyombo vya habari
hususani gazeti la Tanzania Daima ni kitendo cha kutaka kumdalisha na kudalisha
taaluma ya elimu kwa ujumla “sisi
Wataalamu[Walimu]hatuko katika majukwa ya kisiasa kazi yetu ni moja kuelimisha
watoto basi”alisisitiza Bujimu
“ Hivi
mwandishi kwa uelewa wako mimiDEO mzima] nitoe magizo kwa Walimu wa Binza wakazomee Walimu wa Shanwa nimeanza
jana kazi ya ualimu?huyu mwandishi ana
elimu ndogo yupo yupo tu nenda katika shule zote mbili Binza na Shanwa ukweli
utaupata huko”alisema kwa kujiamini Bujimu
Mwandishi wa
habari hizi alipo hojiana na baadhi ya Waalimu kutoka Shule ya msingi Binza na
Shanwa ambao majina yao yame[ hifadhiwa]
kwa kwa sasa kwa nyakati tofauti walisema wanatarajia kuitisha kikao kwa shule
zote mbili [Shanwa na Binza] ili kutoa tamko lao hatua za kuchukua dhidi ya
Mwandishi wa habari na na chombo anacho andikia.
Thursday, 13 March 2014
DOGO JANJA WAVUNJA UCHUMBA WA MTU MTWARA
DOGO JANJA, ASLAY WAVUNJA UCHUMBA WA MTU MTWARA
Na Chande Abdallah na Nyemo ChilonganiMADOGO wanaotikisa katika ulimwengu wa muziki Bongo, Abdulaziz Chende ‘Dogo Janja’ na Asilahi Isihaka ‘Aslay’ wamedaiwa kuvunja uchumba wa jamaa aliyefahamika kwa jina la Fikiri Chodas na Farida.
Tukio hilo lilitokea usiku wa Machi 7, mwaka huu, Newala mkoani Mtwara wakati wasanii hao walipokuwa wamekwenda kufanya ziara ya kimuziki.
Kwa mujibu wa chanzo makini, baada ya madogo hao kufanya shoo kali mjini humo, Farida aliwang’ang’ania wasanii hao waliokuwa wakijiandaa kwenda kulala katika hoteli waliyofikia ndipo Fikiri alipokasirika.
Uvumilivu ulimshinda Fikiri, akamvaa Dogo Janja na kumtaka aachane na mpenzi wake, mchumba wake huyo naye akaja juu na kuhamia kwa Aslay ndipo vurugu ilipotokea ambapo Fikiri alihangaika kumkwida ili kumuokoa mpenzi wake asiondoke na wasanii hao.
Kuonesha mwanamke huyo alikuwa ‘amekolea’ kwa wasanii hao, alianza kumporomoshea mpenzi wake matusi ya nguoni na kudai amuache kwani ‘wametembea’ naye siku moja tu.
Fikiri alipoona mpenzi wake huyo anamkana, aliamua kutangaza kummwaga papo hapo.
Jitihada za mapaparazi wetu kufuatilia sakata hilo kwa undani zilizaa matunda baada ya kufanikiwa kunasa video ya timbwili hilo (litarushwa hewani kupitia Global Online TV).
Mapaparazi wetu walimtafuta Dogo Janja kwa njia ya simu, alipopatikana alifunguka:
“Kweli siku ile tulipomaliza shoo tu tulimuona huyo demu (Farida) anakuja kwetu. Ghafla jamaa akatokea na kuanza kugombana. Sisi tuliondoka sasa kama jamaa kamuacha mpenzi wake ni yeye mwenyewe, sisi hatukuondoka naye,” alisema Dogo Janja.
ALI KIBA KUTISHIWA KUUAWA, DIAMOND KUHOJIWA POLISI
ALI KIBA KUTISHIWA KUUAWA, DIAMOND KUHOJIWA POLISI

SAKATA la staa wa Bongo Fleva, Ally Saleh ‘Ali Kiba’ kunusurika kuuawa na watu wasiojulikana kwa kutumia bastola limechukua sura mpya, safari hii, Nasibu Abdul ‘Diamond’ amefunguka kuwa amejiandaa kuhojiwa na polisi.
Kwa mujibu wa chanzo chetu katika jeshi hilo jijini Dar, Diamond ambaye amekuwa akitajwa sana katika sakata hilo kupitia mitandao ya kijamii ataitwa kuhojiwa.
“Unajua ile kesi ipo hapa Central, awali ilitokea Polisi Msimbazi, sasa mpelelezi wake amekuwa akifikiria kumwita Diamond ili amhoji maana anatajwa sana,” kilisema chanzo hicho.
Hivi karibuni, Ali Kiba alivamiwa usiku na watu zaidi ya watano nyumbani kwao, Kariakoo jijini Dar ambapo waliruka ukuta na kuingia ndani huku kila mmoja akiwa na bastola.
Ilidaiwa kuwa, mmoja kati ya watu hao ambao ilisemekana walitumwa kumuua msanii huyo, aliibua mzozo wa makusudi kwa wenzake ili kumpa mwanya Kiba kutoroka kwa vile hakufurahishwa na kitendo hicho.
Habari zinasema walipoingia ndani huku kelele za mbwa zikasaidia kumshtua staa huyo, ule mzozo ulioanzishwa na wavamizi hao ulimsaidia Kiba kutoroka ingawa walimkosakosa risasi.
Ikasemekana baada ya msanii huyo kukimbia, jamaa ambaye alimkingia kifua alimpigia simu na kumfungukia watu waliohusika huku ikidaiwa kuwa baadhi yao ni mastaa wenzake.
“Alinitajia tu majina lakini nilishindwa kuthibitisha moja kwa moja hivyo nikayafikisha Kituo Kikuu cha Polisi (Central) kwa ajili ya uchunguzi,” alisema Ali Kiba huku akikataa kutaja hata jina moja.
Hata hivyo, mengine yaliibuka hasa kwenye mitandao ya kijamii kuwa, miongoni mwa wasanii waliohusika katika tukio hilo eti ni na Diamond.
Amani lilimsaka afande mmoja ambaye anajua mwenendo wa kesi hiyo ambaye alikiri kesi hiyo kuwepo Central lakini alisema mambo yote ni siri ya kazi.
“Nani atahojiwa, nani hatahojiwa ni siri ya kazi yetu,” alisema.
Juzi, paparazi wetu walimtafuta staa huyo wa Wimbo wa Number One ili kusikia anazungumziaje manenomaneno hayo ya kwenye mitandao na vinywa vya watu.
“Nimeshasikia nikitajwa katika hilo, kimsingi ni madai mazito lakini mimi nipo tayari kuhojiwa ili sheria ichukue mkondo wake kwani najua si kweli na sijui lolote,” alisema Diamond.
Akandelea: “Mimi na Kiba kuna ugomvi gani hadi nifikie hatua hiyo. Kwanza sina moyo wala uwezo wa kufanya hivyo.”
AUNT ,WEMA WALA KICHAPO

KIMEWAKA! Habari zilizothibitishwa zinaeleza kuwa, sura mbili za mauzo kwenye sinema za Kibongo, Wema Isaac Sepetu na Aunt Ezekiel Grayson wanadaiwa kula kichapo kutoka kwa msanii mwenzao, Adam Kuambiana, Amani limeinyaka.
Tukio hilo lililoshuhudiwa na ‘shushushu’ wetu lilijiri mchana kweupe maeneo ya Mikocheni, Dar, hivi karibuni baada ya kuibuka timbwili lenye ujazo wa kilo kadhaa baina ya mastaa hao.
ALIANZA WEMA
Kwa mujibu wa chanzo, Wema ndiye aliyeanza kummwagia Kuambiana maneno ya shombo akimwambia kuwa ahakikishe siku hiyo haipiti bila kukata kucha za miguuni kwani ni ndefu na zinatisha.
“Mwanzoni ilikuwa kama utani tu. Wema alimwambia Kuambiana akate kucha, tena itabidi atumie mkasi wa kukatia michongoma maana kwa wembe hazikatiki.
“Pia Wema alimwambia yeye hawezi kumwacha mpenzi wake na kucha ndefu kama hizo za Kuambiana,” kilisema chanzo chetu.
Ilizidi kudaiwa kwamba wakati Wema akiendelea ‘kumpaka’ Kuambiana, Aunt aliyekuwa amejilaza chini alidakia na kusikika akisema kuwa ni kweli msanii huyo mwenye uwezo wa juu katika fani anatakiwa kukata kucha hizo huku akizungumza maneno ya shombo kwa jamaa huyo.
HASIRA
“Baada ya kuona imekuwa ‘too much’, Kuambiana alipandwa na hasira, akanyanyuka kwenye kochi na kumfuata Wema kwa lengo la kumpa kipigo,” kilisema chanzo hicho.
MARTIN KADINDA AMUOKOA
Habari zilidai kwamba, Kuambiana alipomfikia Wema alianza kumpiga vibao hadi meneja wake, Martin Kadinda akaingilia kati kumuokoa mwanadada huyo ambaye pia ni meneja wake.
KIBAO CHAMGEUKIA AUNT
Chanzo kilieleza kwamba baada ya kuachana na Wema, msaanii huyo ambaye pia ni ‘dairekta’ wa sinema mbalimbali za Bongo alimfuata Aunt na kuanza kumlamba makofi ya kutosha.
Tukio hilo lilizua tafrani na kuwafanya wasanii wengine waliokuwa eneo hilo wakimbie na kushindwa kuwatetea Aunt na Wema kwa kuogopa kugeuziwa kibao.
KUAMBIANA ANASEMAJE?
Baada ya kuinyaka ishu hiyo, mapaparazi wetu walimtafuta Kuambiana na kumuuliza kulikoni kugeuka bondia na kuwapiga warembo hao ambapo alikiri kutokea kwa ishu huyo.
Alisema kuwa, Wema na Aunt ni kama wadogo zake, tena yeye kama dairekta wao walipaswa kumheshimu na siyo kumvunjia heshima.
“Akina Wema ni wadogo zangu, wanahitaji kuniheshimu na mimi ndiye mwongozaji wa filamu yao, kwa nini wanikosee heshima? Hata kama wamekasirika lakini nimewashikisha adabu,” alisema Kuambiana kwa ile sauti yake nzito.
WEMA & AUNT
Kwa upande wao, walipoulizwa Aunt na Wema kuhusiana na kichapo walichopewa walisema walishamzoea jamaa huyo, lakini kwa alilolifanya la kuwapiga makofi aliwakwaza kwa sababu hata kama ni mwongozaji wa filamu yao lakini alikuwa pale kwa ajili yao.
HISTORIA YA KUAMBIANA
Ukiachana na tuki hilo, Kuambiana anadaiwa kuwa na mkono mwepesi hasa anapokuwa ‘lokesheni’ ambapo mwaka jana, aliwahi kumtia mikononi staa mwingine wa filamu za Bongo, Rose Ndauka walipokuwa wakirekodi filamu visiwani Zanzibar.
Siku ya tukio hilo, Kuambiana alikuwa akidairekti Filamu ya Distress in Zanzibar. Alimshutumu Rose kuvaa mavazi tofauti na maagizo yake, katika kujibishana akamuwasha makofi.
HATA MITAANI!
Juni, mwaka jana, Kuambiana alimshushia kipigo Fadhili Joseph ambaye alimdai fedha za bia alizokunywa kwenye baa yake, Sinza, Dar es Salaam.
Kuambiana aliposhindwa kulipa aliacha laptop (kompyuta mpakato), siku iliyofuata alirudi na kushusha kichapo huku akiitaka laptop hiyo.
Kuambiana alikamatwa na Polisi Kawe, Dar kwa faili la malalamiko KW/RB/5761/2012 SHAMBULIO. Kesi hiyo ikahamishiwa Kituo cha Polisi Kijitonyama ‘Mabatini’ kwa vile ndiyo kituo cha karibu na eneo la tukio.
MADAIREKTA WAKOJE?
Mbali na Kuambiana, staa mwingine ambaye pia ni dairekta wa muvi za Bongo, Issa Musa ‘Cloud’ naye aliwahi kutoa kipigo cha bakora kwa msanii Blandina Chagula ‘Johari’ kwa kosa la kuchelewa kufika sehemu ya kurekodia filamu.
PINGAMIZI LA MGOMBEA UBUNGE CHADEMA CHALINZE
TAARIFA YA PINGAMIZI LA MGOMBEA WA UBUNGE JIMBO LA CHALINZE FABIAN LEONARD SKAUKI – MGOMBEA CHAMA CHA WANANCHI –CUF
DHIDI YA
MATHAYO MANG’UNDA TORONGEY – MGOMBEA CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO - CHADEMA
13.03.2014
MATHAYO MANG’UNDA TORONGEY – MGOMBEA CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO - CHADEMA
13.03.2014
Mimi FABIAN L. SKAUKI, Mgombea Ubunge wa
Uchaguzi mdogo Jimbo la CHALINZE kwa tiketi ya THE CIVIC UNITED FRONT
(CUF) ninamwekea Pingamizi mgombea wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(CHADEMA) kwamba amepoteza sifa za kuwa mgombea kwa sababu zifuatazo:
1. Ndugu MATHAYO M. TORONGEY amejaza
taarifa za uongo kwenye fomu yake kwamba kazi anayoifanya ni BIASHARA.
Sio kweli, kwa sababu hajaweka vielelezo vya yeye kufanya hiyo kazi.
Hajulikani anafanya kazi gani.
2. Ndugu MATHAYO M. TORONGEY amejaza
katika fomu kwamba anajua kusoma na kuandika Kiswahili na kiingereza.
Taarifa hizi ni za uongo, mgombea huyu hajui kusoma wala kuandika
Kiswahili wala kiingereza, na kwamba amedanganya na amepoteza sifa za
kuwa mgombea.
3. Ndugu MATHAYO M. TORONGEY
amedanganya kwa kughushi/kufoji sahihi za wadhamini, ambao
amewaorodhesha kwenye fomu ya kuomba kuthibitishwa kuwa mgombea. Ambapo
katika fomu hizo wadhamini wote sahihi zao zimefojiwa na hazifanani na
zile zilizokuwepo kwenye daftari la kudumu la wapiga kura na kwamba
sahihi zote hizi zimesainiwa na mtu mmoja ambaye sio muhusika. Hivyo
anapoteza sifa ya kuendelea kuwa mgombea.
4. Ndugu MATHAYO M. TORONGEY ameshindwa
kutimiza mahitaji ya kisheria ya kuwa na wadhamini wasiopungua 25,
badala yake amedhaminiwa na wadhamini 28 ambao kati yao wadhamini 7 sio
wapiga kura halali wa Jimbo la CHALINZE, na kwamba Taarifa zao na namba
zilizojazwa hazifanani.
Hivyo anabakiwa na wadhamini halali 21 ambao kisheria hawatoshi kutimiza matakwa ya kisheria.
Majina ya wadhamini hao ambao hawakidhi matakwa ya kisheria na namba zao ni:
JINA LA MDHAMINI NAMBA YA KADI KURA
1. HABIBU ALLY SAIDI *16886275*
2. MOHAMMED RAMADHANI *30376567*
3. ABDULKADIR ALLY *49264905*
4. SHABANI SULEYMAN *16984045*
5. JUMA MRISHO *48759563*
6. RAJABU ALLY *16872368*
7. MANENO MIRAJI *16872059*
1. HABIBU ALLY SAIDI *16886275*
2. MOHAMMED RAMADHANI *30376567*
3. ABDULKADIR ALLY *49264905*
4. SHABANI SULEYMAN *16984045*
5. JUMA MRISHO *48759563*
6. RAJABU ALLY *16872368*
7. MANENO MIRAJI *16872059*
Wananchi wenye namba na majina hayo hapo
juu waliojazwa kama wadhamini kuanzia namba 1 hadi 7 kwenye fomu yake
hawana sifa za kupiga kura kwenye maeneo ambayo wamejazwa wanatokea.
Hii ni kutokana na ukweli kwamba idadi
halali ya wadhamini wanaobaki ukiwaondoa hao saba watabaki 21, hawakizi
vigezo vya kuwa wadhamini.
5. Ndugu MATHAYO M. TORONGEY
amedanganya uraia wake na kwamba yeye si Mtanzania wa kuzaliwa ndio
maana hana vielelezo halali vinavyohusu uraia wake. Hivyo anakosa sifa
ya kuwa mgombea.
Hivyo ninaomba Tume ya Uchaguzi kutengua
uteuzi wa mgombea wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), ndugu
MATHAYO M. TORONGEY kwa kuwa anakosa sifa za yeye kuendelea kuwa
mgombea.
Wako katika ujenzi wa taifa,FABIAN LEONARD SKAUKI
……………………………………………………..
MGOMBEA UBUNGE JIMBO LA CHALINZE.
THE CIVIC UNITED FRONT
Wednesday, 12 March 2014
BWAWA LA MAGEREZA MASWA

Magugu maji
katika lambo la mwantonja Maswa
MAGUGU MAJI YAVAMIA LAMBO LA MWANTONJA MASWA
MAGUGU MAJI YAVAMIA LAMBO LA MWANTONJA MASWA
Na Isaack
Mbwaga Maswa Machi 11,2014
Mhariri Habari Mwananchi
Mimea aina
ya magugu maji yanatishia kufunika kabisa Lambo la maji la Mwantonja mini Maswa Lambo linalo hudumia
vitongoji 10 vinavyo zunguka lambo hilo maji yake yatumika kwa kiwango kikubwa wakati
wa kiangazi shughuli za kibinadmu kama vile umwagiliaji katika
bustania,kujengea na kunyweshea Mifugo
Wakiongea na
gazeti hili kwa nyakati tofauti lilipo tembelea eneo la Lambo la Mwantonja na
kujionea hali halisi jinsi mimea hiyo ilivyo stawi na kufunika karibu eneo lote
la Lambo kwa ktishia uhai wa Lambo
Mkazi wa
kitongoji cha Unyanyembe Njile Washa
alisema magugumaji hayo yamezidi kuongeka kadiri siku zinavyo songa mbele na
suala la kufurika kwa magugumaji katika
Lambo siyo geni viongozi wa vitongoji
karibu vyote vinavyo lizunguka Lambo wanayo taarifa na wanaona lakini hakuna
hatua zinazo chukuliwa kuyaondoa magugu hayo
Njile aliongeza
kusema kuwa endapo juhudi hazitafanyika kuanzia sasa kuyatoa huenda magugu hayo
yakanza kusafiri hadi mto simiyu ambayo maji yake yanasafiri hadi ziwa Victori
mkoani Mwanza
Naye
Mwenyekiti wa Kitongoji cha Unyanyembe katika mji mdogo wa Maswa Nkuba Shimi
alipo ongea na gazeti hili alisema kuwa taarifa za kuwepo kwa magugu maji katika lambo la Mwantonja Ofisi ya Idara ya mifugo na Uvuvi wanazo
taarifa tatizo ni ukosefu wa nyenzo za kuvunia magugu hayo
Alizitaja
nyenzo hizo kuwa ni pamoja rasimali fedha kwa ajili ya kuajiri watu, mitumbwi
mitatu na visu vya kutosha ili watu watakao fanya kazi ya kuyaondoa magugumaji kazi iwe rahisi kwao na bila kuhatarisha
maisha yao ama kuzama endapo italetwa mitumbwi mibovu
Aidha
uchunguzi uliofanywa na gazeti hili
umebaini katika baadhi ya visima vya maiji na malambo kadhaa ya maji kuwepo kwa
mimea hiyo ambo inatishia uhai wa viumbe wengine kama vile samaki
Endapo
mamlaka hazita chukua hatua za haraka kulikabili na kuyaondosha magugumaji hayo
katika malambo na visima vilivyo vamiwa na mimea aina ya magugu maji iko hatari ya kukosa maji kabisa kiangazi kwa
ajili shughuli za kibinadamu kama vile Kilimo cha mbogamboga,kunyweshea Mifugo
na matumizi ya Binadamu
Tatizo la
kuoneka na kuota kwa magugu maji kwa mara ya kwanza lilianza kuijitokeza mwaka 1994 ambapo mimea hiyo ilikuwa
inasafishwa na wafanya biashara wa samaki kutoka Mwanza kuja kuuza katika Soko
kuu la Nyalikungu katika mji wa Maswa
Masalia ya
mimea ya magugu maji ambayo yalikuwa yanatumika kufunika Samaki kutoka ziwa Victoria baada ya kutua mzigo wa
Samaki majani ya magugu hayo yalikuwa
yanatupwa ovyo bila ungalizi karibu na Malambo ama visima vya maji wakati wana
fanya usafi wa vyombo vyao vilivyo kuwa vinatumika kusafirishia Samaki
Serikali ya
Halimashauri ya Wilaya ya Maswa [Idara ya Mifugo na Uvuvi] inao wajibu wa
kuhakikisha juhudi zinafanyika haraka za kuyavuna magugu hayo kabla hajasambaa
na kuenea maeneo mengi katika Halimashauri yote ya Wilaya ya Maswa na Wilaya
Jirani zinazo pitiwa na mto Simiyu
Kufutia
kuwepo kwa Mradi wa LIVEMP II kwa Halimashauri tano za
Itilima,Magu,Kwimba,Meatu na Maswa ambapo Halimashauri ya Maswa ina wahamasisha
Watu binafsi,Taasisi na Vikundi mbalimbali kuchimba mabwawa ya kufugia
Samaki kwa ajili ya matumizi ya nyumbani
na biashara
Saturday, 8 March 2014
AFISA ELIMU AWAPA SOMO WALIMU WAKUU
WAKUU WA
SHULE ZA SEKONDARI MASWA” WAFUNDWA”NA AFISA ELIMU SEKONDORI –NTAGAYE
Waalimu wa
shule za Sekondari katika Halimashauri ya Wilaya ya Maswa wameagizwa
kuhakikisha na wanafuatilia kwa ukaribu ufundashaji wa Wanafunzi katika Shule
zao ili kuinua kiwango cha ufaulu Wanafunzi
Kauli hiyo
alitolewa hivi karibuni na Afisa Elimu Sekondari wa Halimashauri ya Wilaya ya
Maswa Paulina Ntagaye wakati alipokuta na
Waalimu Wakuu wa Shule za Sekondari
katika Ukumbi wa Halimashauri ya Maswa kwa lengo la kuwekeana mikakati ya
kuboresha elimu ya Sekondari kwa mwaka 2014
Ntagaye
pamoja na mambo mengine alisema kufuatia tamko la Serikali kuwa na mpango wa
matokeo makubwa sasa[BRN] ni wajibu wa Waalimu wakuu kwa kila shule kusimamia
kwa dhati kazi ya ufundishaji na kila Mwalimu wa Somo ahakikishe anawajibika
kadri anavyoweza ili tupate matokeo makubwa
Hata hivyo
Mkuu wa Shule ya Sekondari ya kutwa ya Binza Focus Nchiyiki alisema kuwa ili
elimu yapatikane matokeo makubwa sasa ni wajibu wa Serikali kuhakikisha ina
sambaza vitabu vya kianda na ziada vya kutosheleza kwa Wanafunzi sambamba na ujenzi wa maabara kama ilivyo kwa
Shirika la Umeme[TANESCO]wanavyo sambaza umeme vijijini
“Tunaona
karibu kila siku maroli ya nguzo za Umeme na nyaya zinazambazwa katika vijiji
mbalimbali vilivyo pendekezwa kupata nishati ya Umeme lakini Wizara ya Elimu na
mafunzo Wanafunzi wana uhaba wa vitabu hakuna maabara za kutosha pia na Waalimu
ni nwachache katika baadhi ya shule za Sekondari”alisema
Afisa Elimu
wa Sekondari katika Halimashauri ya
Maswa Paulina Ntagaye alizipongeza shule kumi bora zilizo fanya vizuri katika
mtihani wa kidato cha Pili 2013 ambazo
ni Lalago Sekondari,Ipililo Sekondari,Kulimi Sekondari,Senani Sekondari,Mwabayanda
Sekondari, shule zingine ni Nyabubinza,Kadoto Sekondari,Ng’wanza Sekondari na
Salagi
Wakati huo huo Ntagaye hakusita kuwanyoshea
vidole Wakuu wa Shule kumi duni ambazo
matokea yake ni mabaya mtihani wa kidato cha pili kuwa Ofisi yake hata sita kuwa
chukulia hatua kali endepo shule hizo zitaendea kufanya vibaya katika mitihani
yake mbalimbali ya ndani na kitaifa alisema kwa msisitizo Afisa Elimu huyo
Shule ya
Sekondari ya Kata ya Ipililo imeshika na nafasi ya kwanza kwa shule za Serikali
kati ya shule 36 za Serikali ingawa
shule ya Sekondari ya Wazazi ya Lalago imeshika nafasi ya kwanza kati shule 38
za Serikali na binafsi wakati za binafsi ni Ng’wanza Sekondari na Lalago Sekondari









