Tuesday, 11 July 2023

TBS YATOA ELIMU KWA WADAU SABASABA KUHUSU MASUALA YA UDHIBITI UBORA

...


****************

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS) limeendelea kutoa huduma kwa wajasiriamali ,wafanyabiashara na wadau mbalimbali wa Viwango katika Maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam ambapo wamekuwa wakiwapa taarifa ya huduma ambazo wanazitoa ikiwemo uandaaji wa viwango,usajili wa bidhaa na majengo ya vyakula na vipodozi,upimaji,ugezi,uthibitishaji wa mifumo na udhibiti ubora wa bidhaa zinazozalishwa nchini na nje ya nchi.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Julai 10,2023 Jijini Dar es Salaam, Afisa Udhibiti Ubora Mwandamizi Bw.Hassan Juma amesema wameweza kupata wadau mbalimbali wakiwemo wajasirimali wadogo ambao wameweza kupata elimu namna ya bidhaa zao zinavyotakiwa kuthibitishwa ubora na Shirika hilo kupitia SIDO.

"Kwenye Maonesho ya kipindi hiki wajasiriamali wengi wameonesha nia ya kuthibitisha bidhaa zao baada ya kupata elimu ya kutosha kuhusu umuhimu wa kuthibitisha bidhaa zao ambazo wamekuwa wakizizalisha pamoja na kuagiza". Amesema

Pamoja na hayo Bw.Juma amesema kuwa kupitia Maonesho hayo wameweza kutoa elimu kwa makampuni makubwa mbalimbali kuhusiana na uthibitishaji wa mifumo yao ambao wameridhishwa na huduma zinazotolewa na shirika hilo.

TBS inaendelea kuwakaribisha wadau kutembelea banda lao lililopo kwenye banda la Wizara ya Viwanda na Biashara ili kupata huduma hizo papo kwa hapo.

Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger