Sunday 23 July 2023

WAZIRI AWESO ATAKA WANANCHI VIJIJI PEMBEZONI MWA ZIWA VICTORIA VIPATE HUDUMA YA MAJI

...



Na Mariam Kagenda _ Kagera

Wataalamu wa Wizara ya Maji wameelekezwa kuweka mpango mkakati wa kuhakikisha vijiji ambavyo vipo pembezoni mwa ziwa Victoria vinanufaika na uwepo wa ziwa hilo ili wananchi wapate suluhisho la kudumu na kupata maji safi na salama.


Maelekezo hayo yametolewa na Waziri wa Maji Jumaaa Aweso wakati akizungumza na wananchi wa Jimbo la Nkenge katika halmashauri ya wilaya ya Misenye ambapo kabla ya mkutano wake wa adhara na wananchi hao alizindua mradi wa maji Katolerwa_Ishozi ambao unahudumia wananchi wapatao 7278 uliopo kata ya Ishozi.


Waziri Aweso amesema kuwa mkoa wa Kagera una ziwa Victoria, mto Kagera hivyo maeneo ya vijiji ambavyo vimeambatana na uanda wa ziwa Victoria hivyo lazima mpango mkakati uwekwe kwa ajili ya kuhakikisha wananchi wananufaika na Ziwa hilo.




Amesema kuwa maelekezo hayo yanatakiwa kufanyiwa kazi na lazima vijiji hivyo vinufaike kwasababu ni maelekezo pia ya Rais Dkt Samia Suruhu Hassan katika dhana yake ya kumtua mama ndoo kichwani.


Kwa upande wake mbunge wa Jimbo la Nkenge halmashauri ya wilaya ya Misenye Frolent Kyombo amesema kuwa kata ya Ishozi haikuwai kuwa na mradi wa maji huo ni wakwanza ambapo hapo awali wananchi walikuwa wanatumia vyanzo vya maji.


Ameishukuru serikali ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuwakumbuka wananchi wa wilaya hiyo hasa kwa kutatua changamoto ya maji.


Naye Meneja wa Ruwasa ambao ni wakala wa maji na usafi wa Mazingira Vijijni Injinia Andrew Kilembe wakati akisoma taarifa ya mradi wa maji Katolerwa_Ishozi amesema kuwa ujenzi wa mradi huo ulianza January 25 2022 na kwa sasa mradi huo umekamilika.


Aidha mradi huo unahudumia wananchi wa vijiji vya Nyarugongo 2543,Katano 1365,Luhano 1708 na Katolerwa 1662 ambapo kwa sasa shughuli zinazoendelea ni kuunganisha maji majumbani.



Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger