Tuesday 25 July 2023

MSITOE DAWA KWA WAGONJWA KAMA HANA CHETI CHA DAKTARI-DKT SHEKALAGHE

...

KATIBU Mkuu wa Wizara ya Afya Dkt Seif Shekalaghe akizungumza  wakati akifungua kongamano la mrejesho wa Tafiti za Kukinga na kudhibiti Maambukizi na Usugu wa dawa za Antibiotic lililofanyika katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa NIMR Prof. Said Shehe Aboud  na kulia ni Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga -Bombo
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) Prof. Said Shehe Aboud  akizungumza wakati wa  kongamano la mrejesho wa Tafiti za Kukinga na kudhibiti Maambukizi na Usugu wa dawa za Antibiotic lililofanyika katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo 
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga -Bombo Dkt Naima Yusuf akizungumza wakati wa kongamano hilo
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga -Bombo Dkt Naima Yusuf akizungumza wakati wa kongamano hilo
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Dkt Seif Shekalaghe akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) Prof. Said Shehe Aboud  mara baada ya kuwasili katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga -Bombo kushoto wa kwanza ni Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa mkoa wa Tanga Bombo Dkt Naima Yusuf 



Na Oscar Assenga,TANGA

KATIBU Mkuu wa Wizara ya Afya Dkt Seif Shekalage amewataka wenye maduka ya dawa nchini wafuate taratibu zilizowekwa na Serikali wasitoe dawa kwa wagonjwa kama hawajakwenda na cheti kilichoandikwa na daktari.

Dkt Seif aliyasema hayo Jijini Tanga wakati akifungua kongamano la mrejesho wa Tafiti za Kukinga na kudhibiti Maambukizi na Usugu wa dawa za Antibiotic lililofanyika katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo.

Alisema jambo hilo ni la msingi na Serikali wameweka sheria kali mtu akimakatwa anachukuliwa hatua lakini sasa wanazungumza wanaofanya kwa njia za siri ambao hawajagundulika wanasababisha tatizo linakuwa kubwa.

“Katika hili napenda kusisitiza hili kwa wenye maduka ya dawa nchini wafuate taratibu zilizowekwa na Serikali wasitoe dawa kwa wagonjwa kama hawajakwenda na karatasi iliyoandikwa daktari”Alisema

Alisema jambo jingine ni wenzao wanaoshirikiana nao wanaouza dawa za mifugo mtu anakwenda anasema kuku wake anatatizo fulani anatoa dawa lakini ushauri unatolewa kwa wahusika kwamba huyo kuku anaumwa nini na anapaswa kutibiwa vipi.

Katibu Mkuu huyo alisema wanahitaji waandishi wa habari kutumia kalamu zao kuweza kutoa elimu kwao waandihi wa habari kila mkoa kuewaeleza athari za dawa na mambo mengine na kuifikisha jamii na hivyo kuweza kuondosha kasumbua hiyo kwa jamii.

Alisema zipo dawa ambazo mtu anajisikia anaumwa na kichwa kununua panado kwa sababu ya kutuliza kichwa iili uende kwa daktari akakupe dawa hilo ndio jambo la msingi sana

Alisema waanajua zipo dawa muhimu zilizowekwa kwenye maduka lakini dawa za antibayotiki wananchi wasitumie tu kwa sababu wanapotumia dawa bila kupata ushauri kwa daktari dawa za aina gani kwa sababu kufanya hivyo wanatengeneza mwili wao kuwa na usugu vimelea vinavyokupata kuweza ku kutibiwa na zile dawa ambazo ni sahihi kwa sababu umeshatengeneza usugu wa kuweza kutrumia tu dawa,

Awali akizungumza Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) Prof. Said Shehe Aboud alitoa wito kwa wananchi wasiende kwenye duka la dawa kununua bila cheti cha daktari kwani kumekuwa na mazoezi wananchi kwenda kujinunulia dawa bila kujua kama kweli wanahitaji kutumia hizo au la.

Alisema pia vilevile wanapoandikiwa dawa za daktari wahakikishe wanatumia dozi kamili na wanatumia kwa mujibu ilivyoandikwa na Daktari.

Aidha aliwataka pia kuhakikisha kwamba pale wanapokwenda kununua kwenye duka la dawa na mambo ya kujitibu wenyewe wanapopata tatizo la kiafya waende hospitalini waonwe madaktari wapimwe wapate vipimo vya maabara na vikapaporudi kwa daktari ndio wanaweza kujua wanapaswa kutumia dawa ya aina gani.

Naye kwa upande wake Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Dkt Naima Yusuf alisisitiza wananchi kuacha kutumia dawa bila kujua wanaumwa na nini kwani kufanya hivyo zinaweza kuwasababishia madhara mbalimbali.

Alisema katika utafiti huo walichofanya walichukua sampuli kutoka kwa mama na mtoto aliyezaliwa na kama amezaliwa kwa njia ya kawaida au upasuaji na vifaa vilivyotumika.

“Tupo hapa kwa ajili ya kusisitiza wananchi wasitumie dawa bila kujua wanaumwa na nini kwani kuna tabia unaumwa kidogo unakwenda duka la dawa unachukua dawa mwishowe zile dawa zinaacha kufanya kazi”Alisema

Dkt Naima alisema kwa sababu utakwenda kununua kwa hela ulionayo anunua dozi ambayo haijakamilika na unanunua dawa hujui unaumwa na nini ni vijidudu gani vimesababisha hali hiyo”Alisema

Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger