Waziri wa Viwanda na biashara Dkt Ashatu Kijaji azungumza na wafanyakazi wa kiwanda cha 21st Century Textiles Limited kinachojihusisha na kuchakata mkonge leo Juni 17,2022 Jijini Dar es Salaam Waziri wa Viwanda na biashara Dkt Ashatu Kijaji akitoka katika ofisi za kiwanda cha 21st Century Textiles Limited mara baada ya kufanya ziara katika kiwanda hicho kinachojihusisha na kuchakata mkonge leo Juni 17,2022 Jijini Dar es Salaam Baadhi ya wafanyakazi wa kiwanda cha 21st Century Textiles Limited kinachojihusisha na kuchakata mkonge wakimsikiliza Waziri wa Viwanda na biashara Dkt Ashatu Kijaji (hayupo pichani) baada ya kufanya ziara kwenye kiwanda hicho leo Juni 17,2022 Jijini Dar es Salaam Waziri wa Viwanda na biashara Dkt Ashatu Kijaji akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kufanya ziara katika kiwanda cha 21st Century Textiles Limited kinachojihusisha na kuchakata mkonge leo Juni 17,2022 Jijini Dar es Salaam
(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)
*************************
NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
Waziri wa Viwanda na biashara Dkt Ashatu Kijaji amesema serikali ishaanza kuchukua hatua za kutatua changamoto za viwandani vinavyozalisha bidhaa za katani hapa nchini ili viweze kujiendesha katika mazingira sahihi.
Akizungumza jijini Dar es Salaam mara baada ya kufanya ziara katika kiwanda cha 21st Century Textiles Limited kinachojihusisha na kuchakata mkonge, Dkt Kijaji amesema katika kutatua changamoto hizo serikali imeondoa kodi ya ongezeko la thamani kwenye mazao yote yanayotokana na zao hilo ikiwa ni lalamiko lao kubwa la wenye viwanda.
Pia Amesema wameona ushindani ambao si mzuri unatokana na mazao ya nyuzi za lailoni na zingine zinatoka nje ya nchi hivyo wizara inaendelea kulishughulikia ili kuweza kuliondoa tatizo hilo ambalo linasababisha viwanda hivyo kutokufanikiwa ipasavyo.
Aidha amesema kuwa changamoto zinazowakabili wafanyakazi wa viwanda hivyo nazo wanazighulikia ili kuweza kuhakikisha kila mfanyakazi anafanya kazi katika mazingira mazuri na kazi kuendelea.
Amewahakikisha wafanyakazi wa kiwanda hicho cha 21st Century Textiles Limited kwamba kiwanda hicho hakitafungwa kwani changamoto zinazowakabili wanaenda kuzitatua mara moja hivyo kila mfanyakazi atapata haki yake na kuendea na kazi.
"Katika Mwaka wa fedha ujao Serikali inatarajia kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili sekta ya Viwanda ili kila muhusika wa eneo hiyo ananufaika katika sekta hiyo hatimaye kuongeza ajira na uchumi kwa ujumla hapa nchini". Amesema Waziri Kijaji.
0 comments:
Post a Comment