Thursday, 30 September 2021

SEMA SINGIDA YAZINDUA MRADI WA KILIMO BIASHARA

Mkuu wa Wilaya ya  Manyoni Rahabu Mwagisa akizindua mpango wa uboreshaji wa maisha ya jamii kupitia mradi wa "Kilimo Biashara" unaosimamiwa na Shirika la SEMA mkoani Singida.


Na Edina Malekela,Singida
MKUU wa Mkoa wa Singida Dkt. Binilith Mahenge amesema Mkakati wa kitaifa wa kuondoa umaskini ni jukumu la Serikali,Sekta binafsi,Asasi zisizo za kiserikali (NGO'S) na washirika mbalimbali wa maendeleo ambapo unahitaji kuzingatia na kushughulikia kwa usahihi changamoto zinazowakabili wakulima wadogo.

Dkt. Mahange alisema hayo jana alipowakilishwa na Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Rahabu Mwagisa katika uzinduzi wa mpango wa uboreshaji wa maisha ya jamii kupitia mradi wa "Kilimo Biashara" unaosimamiwa na Shirika la SEMA mkoani Singida.

Alisema tafiti kadhaa zilizofanywa kuhusu umasikini zimebaini watu wengi masikini wanaishi vijijini na ni wakulima wadogo hivyo mikakati ya kitaifa ya kuondoa umasikini huo unahitaji kutatua kwa usahihi changamoto zinazowakabili wakulima hao.

Alisema mradi huo umeanza wakati muafaka ambapo mkoa kwa sasa unafikiria kuanzisha utekelezaji wa mpango wa kukuza uzalishaji wa zao la Alizeti unaolenga kuongeza uzalishaji wa mafuta yatokanayo na zao hilo kutoka tani 90,000 hadi tani 242,500 sawa na 54% ya jumla uagizaji wa mafuta hayo hapa nchini.

"Mpango huu wa uzalishaji utajumuisha washikadau wakiwemo wakulima wadogo,Vyama vya ushirika, Asasi za kiraia, wakulima wakubwa,Wizara ya Kilimo na Sekta binafsi." alisema na kuongeza.

"Matarajio yetu Mkoa na Wizara ya Kilimo katika utekelezaji wa mpango wa uboreshaji wa maisha ya jamii kupitia mradi wa Kilimo cha kibiashara ambao SEMA wanautekeleza utainua Uchumi wa wakulima wadogo wadogo kupitia kuongeza kwa tija ya mazao yatakayowezeshwa na mradi huu." alisema Dkt Mahenge.

Awali kabla ya kuzungumza Mkuu wa Mkoa Meneja Mkuu wa SEMA Ivo Manyaku alisema lengo la mradi huo ni kuwajengea uwezo wakulima waweze kujiunga kwenye vikundi vya kuweka na kukopa waweze kutunza mazao yao ili waje kuyauza kwa pamoja jambo litakalo wasaidia kuwa na sauti moja ya soko.

"Wakulima wengi wanauza mazao yao yakiwa shambani ili kukidhi mahitaji yao kutokana na kutokuwa na akiba hivyo ili wapate mahitaji wanayoyahitaji wanajikuta wanauza kwa bei ya hasara." alisema Manyaku.

Alisema kupitia mradi huo wanalenga kuyaongezea thamani mazao yanayozalishwa na wakulima,kuongeza mnyororo wa thamani ambapo mikakati ni kuwa na mashamba darasa,maonyesho ya Vijiji ya kibiashara ambapo watawaunganisha wasambazaji wa pembejeo ,maafisa Kilimo, wakulima na wanunuzi ili waone kila mmoja anahitaji nini jambo litakalosaidia mkulima kuwa na uhakika wa soko.

Meneja alisema mradi huo umewapa kipaumbele Wanawake na Vijana kwa zaidi ya 70% na utatekelezwa katika Wilaya tatu za mkoa huu ambazo ni Iramba, Ikungi na Manyoni huku ukitarajiwa kuboresha maisha ya wakulima wadogo 6,000 kwa kuimarisha miundombinu ya kusaidia biashara na mnyororo wa thamani wa mazao ya Mahindi,Mbaazi,Mtama pamoja na Alizeti.
Mkuu wa Wilaya ya  Manyoni Rahabu Mwagisa katikati  akiwa na viongozi wengine wakitembelea mabanda ya wajasiliamali kabla ya kuzindua mapanho wa uboreshaji wa maisha ya jamii kupitia mradi wa  kilimo biashara.

Meneja Mkuu wa SEMA Ivo Manyaku akizungumza kwenye ghafla hiyo.
Mkuu wa Wilaya ya  Manyoni Rahabu Mwagisa akizungumza kabla ya kuzindua mradi huo.
Share:

Chui auawa baada ya kujeruhi wanne Wilaya Ya Hai, Kilimanjaro


Watu wanne wamejeruhiwa na chui wilayani Hai mkoani Kilimanjaro, baada ya chui huyo kuvamia zahanati ya Huruma iliyopo wilayani humo.

Kamanda wa polisi wa mkoa wa Kilimanjaro, Simon Maigwa amesema chui huyo anayedaiwa kutoka Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro, alionekana majira ya asubuhi katika eneo la Bomang’ombe.

Amewataja waliojeruhiwa kuwa ni  Emmanuel Usara,  Jesca Nnko, Urusula Cosmas na Maliki Sakia wote wakazi wa Bomang’ombe wilayani Hai.

Hata hivyo askari kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) walifanikiwa kumdhibiti na baadaye kumuua chui huyo kabla hajaleta madhara zaidi.


Share:

FCS YAZINDUA MPANGO MKAKATI MPYA KUSAIDIA WANANCHI... DKT. TENGA ATAKA ASASI ZA KIRAIA KUSHIKAMANA

Rais wa Taasisi ya Foundation For Civil Society (FCS) Dkt. Stigimana Tenga amezitaka Asasi za kiraia nchini kushikamana kwa pamoja na kuhakikisha wanazisemea kazi wanazofanya katika Taasisi zao ili ziweze kufahamika kwa wananchi na jamii kwa ujumla.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mpango Mkakati mpya wa Foundation For Civil Society (FCS) Dkt. Tenga amesema Asasi za Kiraia zinapaswa kujengwa kutokana na kwamba ni muhimili mkubwa wa maendeleo nchini na wananchi wanapaswa kuzifahamu.

Pia amezitaka Asasi hizo kuhakikisha zinaangalia mifumo mbalimbali inayowaongoza ambayo ndiyo miundombinu ya uwajibikaji katika kazi zao hususani katika kutatua matatizo ya wananchi.

“Tuisemee sekta hii na yale yote ambayo sekta hii inayafanya kwenye jamii, yasemeeni mnayoyafanya ili yajulikane msione aibu yeyote,”alisema Dkt. Tenga.

Aliongeza kuwa Asasi zinapaswa kutatua matatizo ya wananchi na kusaidia kuyaondoa hilo ndiyo lengo kubwa la FCS katika Dira yake.

“Tujenge uwajibikaji katika misingi ya ubinadamu na utu bila kujali kuna nini, bali kuwashirikisha wenzetu matatizo ambayo sekta ya Asasi za kiraia nchini inapitia ambayo yanahitaji kutatuliwa kwani ni matatizo yanayojikita katika mifumo,” aliongeza Dkt. Tenga.

Aidha alisema hawapaswi kutatua matatizo kwa mbinu zile zile za zamani ambazo sio mbinu za kujenga mifumo bali ni mbinu za kutoa huduma.

“Tusipoangalia hivyo tutazidi kuona hizo mbinu zinaongezeka na kuwa kubwa sana na kuhakikisha wanaangalia mifumo ambayo ndio miundombiniu ya uwajibikaji katika asasi,” alisema.

Kwa Upande wake,Mkurugenzi Mtendaji wa FCS Francis Kiwanga alisema wamezindua mpango mkakati mpya wa FCS ambao unalenga kushuka chini hususani vijijini katika kuwasaidia wananchi.

Alisema kupitia mpango huo, Taasisi yao itaendelea kufanya kazi na Asasi mbalimbali za kiraia ambao ndiyo wadau wao muhimu katika kuwafikia wananchi.

Alisema falsafa ya Taasisi yao inaamini kuwa umaskini,hali ya kutokuwa na haki katika jamii,hali ya ukandamizaji watu wengine ni tatizo kubwa na ni adui wakubwa wa maendeleo.

Alisema katika rasilimali zao takribani asilimia 90 zinakwenda vijijini kuhudumia wananchi.

“Rasilimali zetu tunayogawa kila mwaka asilimia 90 inakwenda vijijini ,tunaamini waliopo Dar es Salaam ,Taasisi nyingi zinaweza kufanya kazi na watu wengine kokote duniani kuliko waliopo vijijini” alisema Kiwanga.

Pia aliongeza kwa kusema kuwa katika mpango kazi wao wanazingatia usawa wa kijinsia,kufanya kazi na wadau wao kuwapa heshima inayostahili na kuwaheshimu kwani wao ndio wabia wao wakubwa na kwamba sauti yao ina ukubwa wa kuweza kuwafikia wananchi.

Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Asasi za kiraia, Dkt. Richard Samabiga aliipongeza FCS kwa hatua hiyo ya kuzindua mpango mkakati huo ambao unaonyesha dira ya kusaidia wananchi katika maeneo mbalimbali.

Alisema mpango huo unaleta matumaini makubwa kwa Asasi za kiraia katika kufanya kazi zao za kusaidia wananchi.

Mpango mkakati huo umejikatika katika kutekeleza miradi ya utawala bora, usawa wa kijinsia na watu wenye ulemavu, kukuza uchumi na kujenga amani na utatuzi wa migogoro.
Rais wa FCS Dkt. Stigimana Tenga akizungumzia mpango huo mara baada ya kuzinduliwa rasmi mwishoni mwa wiki Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa FCS Francis Kiwanga (wa tatu kulia) akiwa na Rais wa Taasisi hiyo Dkt. Stigimana Tenga (katikati) na mwenyekiti wa Bodi ya FCS Dkt. Richard Samabiga (wa kwanza kulia) wakiangalia mpango mkakati utakaotekelezwa kwa kipindi cha miaka mitano mara baada ya kufanyika uzinduzi rasmi wa mpango huo uliofanyika mwishoni mwa wiki kwenye Ofisi za FCS Jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mtendaji wa FCS Francis Kiwanga akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi huo akielezea namna ambavyo FCS itavyotekeleza majukumu yake katika kuusimamia mpango huo.
Baadhi ya watumishi wa FCS na wageni mbalimbali waalikwa wakiwa kwenye hafla ya uzinduzi huo.



Share:

350 Jobs Opportunities at Tanzania Immigration Department (Ajira uhamiaji)

350 Jobs at Tanzania Immigration Department (Ajira uhamiaji) September, 2021. The Immigration Services Department is established under Section 4(1) of the Immigration Act of 1995 Chapter 54 as amended by Act No.8 of 2015.  It gives the Department the authority to control and facilitate immigration issues in the United Republic of Tanzania. The Department is […]

This post 350 Jobs Opportunities at Tanzania Immigration Department (Ajira uhamiaji) has been posted by Udahiliportaldaily

Get more post by visiting Udahiliportal.com

know more details about Udahiliportal.com by visiting Udahiliportal.com - Find Jobs & Ajira mpya leo, ajira portal Tanzania, ajira yako, brighter Monday, mabumbe, mwananchi ajira, secretariet ya ajira, tamisemi ajira za afya, wizara ya afya, ajira Tanzania - selection za vyuo , selection, second selection vyuo, second selection, tamisemi selection, selection form one 2020/2021

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

Share:

Global Compliance Manager at Pathfinder

Pathfinder Overview   Pathfinder International is driven by the conviction that all people, regardless of where they live, have the right to decide whether and when to have children, to exist free from fear and stigma, and to lead the lives they choose. Since 1957, we have partnered with local governments, communities, and health systems […]

This post Global Compliance Manager at Pathfinder has been posted by Udahiliportaldaily

Get more post by visiting Udahiliportal.com

know more details about Udahiliportal.com by visiting Udahiliportal.com - Find Jobs & Ajira mpya leo, ajira portal Tanzania, ajira yako, brighter Monday, mabumbe, mwananchi ajira, secretariet ya ajira, tamisemi ajira za afya, wizara ya afya, ajira Tanzania - selection za vyuo , selection, second selection vyuo, second selection, tamisemi selection, selection form one 2020/2021

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

Share:

JUA BANDIA KUFANYA KAZI MWAKA 2035


Picha ya mradi wa International Thermonuclear Experimental Reactor (ITER)
 ****
China ni miongoni mwa mataifa yaliyopiga hatua kwenye upande wa Teknolojia na hivi karibuni wameweka rekodi mpya baada ya kufanikiwa kutengeneza ‘Plasma’ ya nyuzi joto Milioni 120 kwa sekunde 101 na joto la Milioni 160 Celsius kwa sekunde 20.

Kituo hicho cha utafiti ni sehemu ya mradi mkubwa wa dunia “International Thermonuclear Experimental Reactor” (ITER), ambapo nchi nyingi zinashiriki kufanya majaribio ya kutengeneza nishati salama inayotokana na ‘nuclear fusion’ na itaanza kufanya kazi mwaka 2035 kwenye nchi kama 35.
Share:

General Trade Executive at TotalEnergies

Description Du Poste   HSEQ   Respect of the Golden rules and all the HSE rules and standards of TOTAL by all the staff, contractors, customers…   PLANNING   Implements the affiliate marketing strategy Participates in the development of affiliate marketing plans on General Trade on the basis of GT in the box master plan, […]

This post General Trade Executive at TotalEnergies has been posted by Udahiliportaldaily

Get more post by visiting Udahiliportal.com

know more details about Udahiliportal.com by visiting Udahiliportal.com - Find Jobs & Ajira mpya leo, ajira portal Tanzania, ajira yako, brighter Monday, mabumbe, mwananchi ajira, secretariet ya ajira, tamisemi ajira za afya, wizara ya afya, ajira Tanzania - selection za vyuo , selection, second selection vyuo, second selection, tamisemi selection, selection form one 2020/2021

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

Share:

6 Job Opportunity at Sikonge District Council and MDH

Share:

IT Officer Cum Software Developer at MDH

POSITION: IT Officer Cum Software Developer (1 Post)   LOCATION:        Dar es Salaam REPORTS TO:    IT Manager Job Summary:  IT Officer Cum Software Developer will be responsible to study existing systems and procedures and develop software applications to automate various MDH programmatic and operations activities. She/He will design and develop software applications […]

This post IT Officer Cum Software Developer at MDH has been posted by Udahiliportaldaily

Get more post by visiting Udahiliportal.com

know more details about Udahiliportal.com by visiting Udahiliportal.com - Find Jobs & Ajira mpya leo, ajira portal Tanzania, ajira yako, brighter Monday, mabumbe, mwananchi ajira, secretariet ya ajira, tamisemi ajira za afya, wizara ya afya, ajira Tanzania - selection za vyuo , selection, second selection vyuo, second selection, tamisemi selection, selection form one 2020/2021

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

Share:

Serikali Kuendelea Kuboresha Mazingira Ya Watu Wenye Ulemavu


NA MWANDISHI WETU, DODOMA
SERIKALI imesema inaendelea na utaratibu wa kujenga na kukarabati vyuo vya watu wenye ulemavu kwa lengo la kuwasaidia wenye ulemavu kupata ujuzi ili kujikomboa kiuchumi.

Akizungumza Jijini Dodoma baada ya kupokea msaada wa vifaa visaidizi kwa ajili ya wenye ulemavu vyenye thamani ya shilingi milioni 13.9 ambavyo ni viti mwendo 55 na fimbo nyeupe 50 za wasioona kutoka kwa Taasisi ya kutoa huduma ndogo za kifedha (ASA Microfinance Company Limited), Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya watu wenye ulemavu Mhe. Ummy Nderiananga alisema dhamira ya Serikali ni kuhakikisha kila mtanzania anapata haki yake bila vikwazo.

Aliongeza kuwa ipo mikakati madhubuti ya kuhakikisha masuala ya wenye ulemavu yanapewa kipaumbele ikiwemo uboreshwaji wa vyuo ikiwemo Chuo cha Mwanza ambacho ujenzi wake unatarajiwa kukamilika kuanzia mwezi Januari mwakani kuwawezesha vijana kupata mafunzo ambayo yatawasaidia kufanya shughuli zao za uzalishaji na kushiriki katika maendeleo ya Taifa kwa ujumla.

“Kwasasa Wizara inaratibu kwa kasi ujenzi wa vyuo vya watu wenye ulemavu na ufufuaji wa vile ambavyo vipo.Tunaendelea kufanya hivyo katika Chuo cha Yombo Dar es salam, tumezindua Chuo kingine Tabora ambacho kilikuwa kimefungwa kwa miaka 10 na kumalizia ujenzi wa chuo cha kisasa Mkoa wa Tanga,” alisema Naibu Waziri Ummy.

Pia Naibu Waziri huyo alibainisha kuwa Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan imeweka mkazo kuwasaidia watu wenye ulemavu kwa kuendelea kutoa fedha ya elimu bila malipo ambapo watu wenye ulemavu nao hunufaika na mfumo huo huku akieleza kuwa Serikali inatambua changamoto zinazowakabili watu wenye ulemavu.

“Serikali kupitia bohari kuu ya dawa inaendelea kuagiza mafuta ili kuwakinga dhidi ya saratani ya Ngozi kwa watu wenye ualbino sambamba na kuzitaka Halmashauri kuendelea kutenga fedha za mapato ya ndani kupitia asilimia 10 inayotolewa na kila Halmashauri kwa wanawake, vijana na wenye ulemavu kwa sababu hii inawasaidia kupambana na umasikini,”alieleza.

Hata hivyo aliishukuru kampuni hiyo kwa moyo wake wa kujitoa na kuiunga mkono serikali katika juhudi za kuwaletea ustawi wananchi wake na kuwahimiza wadau wengine wa maendeleo kujitokeza kuwasaidia watu wenye ulemavu hatua itakayofanya kujiona wana thamani na kutambulika ndani ya jamii.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa ASA Microfinance Limited , Muhammad Shah Newaj alieleza kwamba wametoa msaada huo wenye thamani ya Sh. milion 13.9 kama sehemu ya kutambua mchango wa watu wenye ulemavu katika maendeleo kuanzia ngazi ya familia hadi Taifa akisema wana uwezo wa kufanya kazi kama watu wengine endapo watapewa fursa na kuhudumiwa katika mahitaji yao wataendelea kushirikiana na Serikali kuhakikisha wanaisaidia jamii kuepukana na umaskini.

Naye Afisa Sheria kutoka ASA Microfinance Limited, Zephania Paul alifafanua kwamba vifaa hivyo ni sehemu ya kutoa huduma kwa jamii na awamu hiii ni yapili kufanyika akisema awamu ya kwanza ilifanyika jijini Dar es salaam huku akibainisha kuwa taasisi hiyo ipo katika Mikoa nane ya Tanzania Bara na Zanzibar na hadi sasa wamewafikia wanawake 1,600 na kutoa ajira .

Akitoa shukrani zake mama wa mtoto mwenye ulemavu Martha Mshama aliishukuru serikali kwa kushirikiana na wadau kuendelea kuwajali watu wenye ulemavu akieleza kuwa kiti alichopewa kitamsaidia kufanya kazi zake kwani awali alikuwa akitumia muda mwingi kuwa karibu na mtoto akihofia kuanguka na kupata madhara.

” Tunaishukuru serikali kwa kutupatia viti mwendo ambapo ni msaada mkubwa kwangu maana nilikuwa nikihofia usalama wa mtoto wangu kuna wakati anaweza kuanguka natakiwa kuwa naye karibu sana lakini sasa walau nitaweza kufanya kazi zangu nawashukuru sana Mungu awabariki,”alishukuru Martha.

Naye Selina Nigangwa (mwenye ulemavu wa miguu) mkazi wa Swaswa aliishukuru serikali kwa kuwapatia msaada huo na kushauri wakati mwingine kutoa viti vya kuendesha kwa kutumia mikono.

“Tunashauri serikali wakati mwingine watoe viti vya kuendesha kwa mikono ili tuweze kuendesha wenyewe bila kumtegemea mtu,” alieleza Selina.


Share:

HUYU NDIYO MTU MCHAFU KULIKO WOTE DUNIANI..HUYU ' MWAMBA' HAJAOGA ZAIDI YA MIAKA 60, ANAVUTA KINYESI KAMA SIGARA



Je, wewe huwa unapenda kuoga au hupendi kuoga. Kama hupendi kuoga basi nadhani leo utafarijika baada ya kufahamu kuwa yupo mtu asiyependa kuoga kuliko wewe.

Unasema hupendi kuoga lakini huwezi kupitisha wiki bila kuoga, acha kutudanganya wewe unapenda kuoga. Kama hupendi kuoga kweli unaonaje miezi au miaka kadhaa ikapita bila ya mwili wako kugusa maji? Usijali hutakufa.

Yupo mtu ambaye hajaoga kwa miongo kadhaa lakini bado anaishi, yaani tunaweza kusema kwamba yeye ni mchafu kuliko uchafu wenyewe, lakini hilo kwake halimsumbui na huyu si mwingine bali ni mzee ajulikanaye kama Amou Haji.

Haji anaogopa maji, kwa hivyo anachukia kuoga, anaamini ataugua ikiwa ataoga na hii imemzuia kuoga kwa zaidi ya miongo sita.

 Amou Haji, raia wa Irani mwenye umri wa miaka 83 ametajwa kama mtu mchafu zaidi ulimwenguni kwani hajaoga katika kipindi cha miaka 65.

Maisha katika jangwa la Irani, na nyama ya nungu nungu iliyooza ikiwa kama chakula chake akipendacho, ndio amezoea. Maisha yake ni uchafu kuanzia anachokula anapoishi na hata mwili wake binafsi.

Ili kuwa na afya hunywa lita tano za maji kutoka kwenye kopo la mafuta lenye kutu kila siku. Pia anapenda kuvuta sigara lakini mtindo wake wa kuvuta sigara unajumuisha kuvuta kinyesi kikavu cha ng’ombe badala ya tumbaku lo! Hutatamani kuwa karibu naye.

Wenyeji wanaamini kuwa moyo uliovunjika ndio sababu Amou Haji alichagua mtindo huu wa maisha. Lakini, bado hajakata tamaa ya kupata upendo.

Haji hana nyumba, anazurura karibu na kijiji kilichotengwa cha Dejgah katika mkoa wa Kusini mwa Irani wa Fars na anaishi kwenye mashimo yaliyotengenezwa jangwani nje ya kijiji. Ingawa wanakijiji walimjengea kibanda lakini alichagua kutoishi hapo.

Amekuwa na rangi inayotaka kufanana na ardhi inayomzunguka na anajichanganya kabisa na mazingira yake. Wenyeji wanasema mara nyingi huwa wanamfanisha na mwamba wakati anapokuwa ametulia kimya. Haji hajali raha za ulimwengu na anaridhika kuishi maisha ya uchafu na ya kuhamahama.
Share:

MZEE NATABAY AFARIKI AKIWA NA UMRI WA MIAKA 127...FAMILIA YAOMBA AINGIE KWENYE KITABU CHA GUINNESS WORLD RECORDS


Mzee mmoja aitwaye Natabay Tinsiew huko nchini Eritrea amefariki akiwa na umri wa miaka 127, familia yake imesema.

Aidha familia hiyo imesema ina matumaini kwamba Natabay Tinsiew atapata nafasi ya kuandikwa kwenye kitabu cha Guinness World Records kama mtu aliyewahi kuishi miaka mingi zaidi.

"Uvumilivu, ukarimu na maisha ya furaha" ndio siri ya mzee huyo kuishi kwa muda mrefu, mjukuu wake Zere Natabay aliiambia BBC Tigrinya.

Bwana Natabay alifariki siku ya Jumatatu akiwa na amani katika kijiji chake, Azefa - ambacho kina idadi ya watu takribani 300 na kipo kwenye korongo lililozungukwa na milima.

Mjukuu wake amesema rekodi za kanisa - pamoja na cheti chake cha kuzaliwa - kinaonesha kuwa alizaliwa mnamo mwaka 1894 - na ndio mwaka ambao alibatizwa - na hivyo kumfanya awe amefariki akiwa na miaka 127.

Lakini familia ya Bw. Natabay inaamini kuwa mzee huyo alizaliwa mnamo mwaka 1884, lakini alibatizwa miaka 10 baadaye, wakati mapadre walipokuja karibu na kijijini kwao.Kulikuwa na mapadre wachache wakati huo, na watu walikuwa wakiwasubiri watembelee kijiji chao.

Padre Mentay, wa kanisa katoliki ambaye alihudumu katika kijiji hicho kwa miaka saba, alithibitisha kwamba rekodi zilionesha kwamba Bwana Natabay alizaliwa mnamo 1894. Alisema alikuwepo wakati wanakijiji wakisherehekea alipotimiza miaka 120 mnamo 2014.

Bwana Zere aliiambia BBC kuwa tayari alikuwa amewasiliana na Guinness World Record ili kuthibitisha hati rasmi za kuzaliwa kwa babu yake, na alikuwa akingojea kusikia kutoka kwao.

Katika kitabu cha Guinness World Records kimemrekodi mwanamke wa Ufaransa Jeanne Calment, aliyekufariki mnamo 1997 akiwa na miaka 122, kama mtu aliyeishi miaka mingi zaidi.

Bwana Natabay alioa mnamo mwaka 1934, mke wake alifariki mwaka 2019 akiwa na umri wa miaka 99.

Wakati wa maisha yake, Bwana Natabay alikuwa mfugaji, mwenye ng'ombe wengi, mbuzi na nyuki.

Vilevile alifanikiwa kuishi na kuona vizazi vitano vya familia yake vikikua.

Bwana Zere alisema babu yake atakumbukwa kama "mtu wa kushangaza", ambaye alikuwa mwema, anayejali na mchapa kazi.
Share:

GGML YATOA MILIONI 800 KUKARABATI HOSPITALI YA RUFAA GEITA



Baadhi ya madaktari ambao ni wanachama wa Chama cha Madaktari Tanzania (MAT), wakishirikiana na wadau mbalimbali kutoa huduma za afya bure kwa wakazi wa mji wa Geita. Mpango huo maalumu wa siku tatu umefadhiliwa na GGML chini ya uratibu wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita na chama hicho.
 ***
Na Mwandishi Wetu 
Kampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML) kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Geita na Chama cha Madaktari Tanzania (MAT) imetoa kiasi cha Shilingi milioni 800 kukarabati Hospitali ya Rufaa Geita.

Pia imesaidia uchunguzi wa bure wa matibabu kwa watu wa Geita kwa siku tatu kuanzia tarehe 27 Septemba 2021 hadi 29 Septemba 2021.

Akizungumzia program hiyo ya matibabu bure, Rais wa Chama cha Madaktari (MAT), Dk. Shadrack Mwaibambe alisema chama chake kina utamaduni wa kutoa huduma za afya bure kwa jamii kabla ya mkutano wao wa kila mwaka.

"Kwa kawaida MAT huwa na mizunguko tofauti katika mikoa yote inayotoa huduma za matibabu bure kwa jamii. Hii ni mara yangu ya kwanza kuja katika mji wa Geita na kupata vifaa vya kisasa vya matibabu ambavyo vilitolewa kama msaada kutoka GGML kwenda kwa Hospitali ya Rufaa ya Geita. Msaada huu umetusaidia sana katika uchunguzi wa awali wa wagonjwa wetu.

"Wakazi wa Geita wanapaswa kujivunia uwekezaji huu wa GGML katika hospitali hii kwani vifaa vingi vinavyopatikana hapa pia vinapatikana katika hospitali kuu kama Bugando na Muhimbili. Mchango wa GGML kwa vifaa hivi vya kisasa unapaswa kupongezwa, "alisema.

Aidha, Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa katika Hospitali ya Rufaa ya Geita Dk. Michael Mashallah alikiri msaada wa GGML na wadau wengine waliohusika katika mradi huo utainufaisha vilivyo jamii ya wana Geita.

"Huu ni msaada ambao umma wa aina yoyote ungependa kupata kwa sababu upatikanaji wa huduma za afya ni muhimu sana kwa sababu inaweza kuokoa maisha.

“Nawashukuru wadau wote kwa msaada wao, haswa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Geita, GGML, MAT, AMREF, CORDET, NELICO, Fhi360, MNH, BMC, ORCI, JKI, TANCDA, Maria Stope, MDH na SHDEPHA, "alisema Dk. Mashallah.

Kwa upande wake Makamu wa Rais wa GGML, Simon Shayo alisema kama raia na mshirika wa maendeleo, GGML imejitolea kushirikiana na serikali kuhakikisha huduma za afya zinazopatikana katika mkoa wa Geita.

Alisema kuwa GGML imetoa Shilingi milioni 800 kwa Hospitali ya Rufaa ya Geita kwa lengo la kuhudumia zaidi ya wakazi milioni 1.7 wanaoishi katika mji huo.

"GGML imekarabati majengo mbalimbali ya Hospitali ya Mkoa ya Geita, ambayo yalijengwa mwaka 1957. Pia imewapa vifaa vya matibabu vinavyoiwezesha hospitali kutoa huduma za uchunguzi wa moyo na meno.

“Msaada huu utahakikisha wan- Geita wanaanza kupata huduma za matibabu ya kibingwa kama zile zilizokuwa zinatolewa kule kwenye Hospitali ya Rufaa Moi jijini Dar es Salaam.

“Msaada huo umejumuisha ununuzi wa mashine ya ECG, jenereta ya dharura ya vifaa vya meno na ujenzi wa majengo ya kisasa ya dharura na kwa watoto wanaozaliwa kabla ya muda yaani njiti," alisema.

Alisema mkoa wa Geita unakua haraka na ndoto ya GGML ni kujenga vituo vya afya vya kisasa ndani jamii inayowazunguka.

“GGML imetekeleza miradi kadhaa ya afya, hasaa ujenzi wa zahanati huko Nyamalembo, Nyakahongola, Kasota na Kakubiro ambazo kila moja iligharimu zaidi ya Sh milioni 260.

“Mwaka wa 2019, GGML pia ilitoa vifaa vya matibabu kwa vituo vya afya vyenye thamani ya Sh milioni 142 kusaidia zahanati za Katoro na Bukoli huko Geita. Katika mwaka huo huo, GGML pia ilitoa darubini mbili za kisasa zenye thamani ya takriban Sh milioni 13 kwa Mkuu wa Mkoa wa Geita.

“Mwaka jana, GGML ilitoa vifaa na vifaa vya matibabu, pamoja na vifaa vya upasuaji wa mifupa, mashine ya ECG na kifaa cha kuangazia, kwa idara ya mifupa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Sekou Toure.
Baadhi ya madaktari ambao ni wanachama wa Chama cha Madaktari Tanzania (MAT), wakishirikiana na wadau mbalimbali kutoa huduma za afya bure kwa wakazi wa mji wa Geita. Mpango huo maalumu wa siku tatu umefadhiliwa na GGML chini ya uratibu wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita na chama hicho.
Share:

HUAWEI YAWAPIGA MSASA WATALAAM 19 WA TEHAMA KUENDANA NA MABADILIKO YA TEHAMA


Mwakilishi kutoka Huawei Tanzania, Yohana Mathias (kulia) akimkabidhi cheti Rweyemamu Barongo ambaye ni mmoja wa washiriki mafunzo ya uchakataji wa data kubwa yaliyotolewa jijini Dar es salaam na Kampuni ya Huawei Tanzania kwa kushirikiana na Tume ya Taifa ya Tehama kwa muda wa siku saba. Kushoto ni Msimamizi wa shughuli za uendeshaji wa Tehama kutoka katika Tume hiyo, Mhandisi Jasson Ndanguzi.
Mwakilishi kutoka Huawei Tanzania, Yohana Mathias (kulia) akimkabidhi cheti Catherine Teodor ambaye ni mmoja wa washiriki mafunzo ya uchakataji wa data kubwa yaliyotolewa jijini Dar es Salaam na Huawei Tanzania kwa kushirikiana na Tume ya Taifa ya Tehama kwa muda wa siku saba. Kushoto ni Msimamizi wa shughuli za uendeshaji wa Tehama kutoka katika Tume hiyo, Mhandisi Jasson Ndanguzi.
Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya uchakataji wa data kubwa yaliyoratibiwa na Kampuni ya Huawei Tanzania kwa kushirikiana na Tume ya Taifa ya Tehama jijini Dar es Salaa. Jumla ya watalaam 19 wa Tehama wamepatiwa mafunzo hayo ya siku saba.
Msimamizi wa shughuli za uendeshaji wa Tehama kutoka katika Tume hiyo, Mhandisi Jasson Ndanguzi akizungumza na washiriki wa mafunzo ya uchakataji wa data kubwa yaliayofanyika jijini Dar es Salaam kwa muda wa siku saba.
Mwakilishi kutoka Huawei Tanzania, Yohana Mathias akizungumza na washiriki wa mafunzo ya uchakataji wa data kubwa yaliayofanyika jijini Dar es Salaam kwa muda wa siku saba.
Washiriki mafunzo ya uchakataji wa data kubwa yaliyotolewa na Kampuni ya Huawei kwa kushirikiana na Tume ya Taifa ya Tehama kwa muda wa siku saba jijini Dar es salaam wakiwa katika picha ya pamoja.
**


Na Mwandishi wetu
Kampuni ya Huawei Tanzania kwa kushirikiana na Tume ya Tehama imetoa mafunzo kwa wataalamu 19 wa Tehama kutoka katika sekta ya umma na binafsi kwa lengo la kuwaongezea ujuzi watalaam wazalendo.

Akifunga mafunzo hayo jijini Dar es Salaam hivi karibuni, Mwakilishi wa uongozi kutoka Kampuni ya Huawei Tanzania, Yohana Mathias amesema mafunzo hayo ni chachu katika kuendelea kuibua ubunifu mpya kwenye sekta ya Tehama.

Amesema mafunzo hayo yaliyofanyika kwa siku saba ni kielelezo tosha namna Huawei inashirikiana na Serikali katika kunoa Watanzania wengi waweze kumudu kufanya kazi kubwa zinazohusu uchakataji wa data badala ya kwenda kuchukua watalaam kutoka nje ya nchi.

“Huawei kila mara tumekuwa tukishirikiana na Serikali kutoa mafunzo ya aina hii kwa sababu tunaamini Tehama ni sekta ambayo inakua kwa kasi hivyo ni vema kuwaandaa Watanzania kuendana na mapinduzi ya nne ya viwanda duniani,” amesema.

Aidha, Msimamizi wa shughuli za uendeshaji wa Tehama kutoka Tume ya Taifa ya Tehama, Mhandisi Jasson Ndanguzi pamoja na kuishukuru kampuni ya Huawei kwa jitihada hizo, amesema mafunzo hayo ni moja ya mikakati ya Tume hiyo katika kutengeneza mpango wa Taifa wa miaka mitatu wa maendeleo.

Amesema mpango huo pia unalenga kuwasajili watalaam wa Tehama, pamoja na kuwaendeleza kwa kuwajengea uwezo ili kuenenda na maendeleo ya Tehama duniani.

“Ndani ya mapinduzi ya nne ya viwanda kunatumika teknolojia ya hali ya juu ndio maana Tume tumeona kuna haja ya kuwajengea uwezo mpya kwa sababu inawezekana teknolojia wanazotumia zinapitwa na wakati…na hii ndio sababu tunawashukuru sana wenzetu wa Huawei kwa jitihada zao katika kufanikisha mpango huu,’’

“Kwa hiyo mbali na mafunzo tunawasajili ili tuweze kujua tuna wanataalam wangapi kama nchi na watalaam hao kila mwaka na kila siku wanajiendeleza kivipi ili kama nchi tujue tuna ujuzi kiasi gani na tunaweza kunufaika vipi na fursa zilizopo kwenye Tehama,” amesema.

Ameongeza kuwa Serikali imekuwa ikiboresha miundombinu ya Tehama lakini sasa inaanza kuweka mkazo kwenye uboreshaji wa rasilimali watu ili Tanzania iwe na watalaam wa kutosha.

“Kwa hiyo mafunzo haya yanahusu big data analysis yaani uchakataji wa data kubwa ambazo zinaweza kusaidia kutoa taarifa sahihi na kuwezesha kufanya maamuzi sahihi ya kiutawala na kimaendeleo,” amesema.

Amesema tangu wazindua mpango wa mafunzo hayo Aprili mwaka huu, jumla ya washiriki 157 wamefaidika na kuongezewa ujuzi katika maeneo ya uchakataji wa data kubwa, usimamizi wa miradi ya Tehama, Cyber security na mafunzo mengine.

Aidha, Mmoja wa wakufunzi wa mafunzo hayo kutoka Huawei, Oscar Mashauri amesema Mwalimu amesema mafunzo hayo ni muarobaini kwa watalaam hao ambao walikuwa wanashindwa kuchakata data kubwa kwenye ofisi zao kwa kuwa hawakuwa na mbinu wala utalaam wa kuzichakata.

“Wameridhika na mafunzo kutoka Huawei kwa sababu wamegundua wanaweza kufanyia kazi wakiwa kwenye maofisi yao,” amesema.

Aidha, mmoja wa washiriki wa mafunzo hayo Rweyemamu Barongo ambaye ni mtaalam wa Tehama kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BOT), amesema mafunzo hayo yanakwenda kuwapeleka kwenye ulimwengu mpya.

“Tuna imani yatatusaidia kwenye maeneo yetu ya kazi na kuonggeza ubunifu mpya kwa manufaa yetu na manufaa ya nchi kwa ujumla…na zaidi niishukuru sana kampuni ya Huawei kwa kufanikisha hili,” amesema.

Share:

KIJANA AUAWA KWA VISU KISHA KUNING'INIZWA JUU YA MTI WA MPARACHICHI



Kijana Melkezedik Robert mwenye umri wa miaka 35, mkazi wa kijiji cha Nyerezi, Arumeru mkoani Arusha, amekutwa amekufa huku mwili wake ukiwa umening’inizwa juu ya mti ya mparachichi.

Mwenyekiti wa ulinzi wa wa Kitongoji cha Achi, aliyejitambulisha kwa jina moja la Agesmun, amesema walikuta mwili wa kijana huyo ukiwa umekatwakatwa visu katika maeneo mbalimbali mgongoni.

Alisema mara baada ya polisi kufika, waliwashikilia baba na mdogo wa marehemu ambaye inasadikika alikuwa na ugomvi na marehemu kaka yake.
Share:

Retention Officer (RO) at MDH

POSITIION: Retention Officer (RO) (8 Posts)   LOCATION:        Geita, Kagera, Tabora and Dar es Salaam REPORTS TO:    District Project Manager/ Regional Retention Manager Job Summary: The Retention Manager (RO) is responsible for the day to day implementation of MDH’s retention and continuity of care programs and services. She/he work with Council Health […]

This post Retention Officer (RO) at MDH has been posted by Udahiliportaldaily

Get more post by visiting Udahiliportal.com

know more details about Udahiliportal.com by visiting Udahiliportal.com - Find Jobs & Ajira mpya leo, ajira portal Tanzania, ajira yako, brighter Monday, mabumbe, mwananchi ajira, secretariet ya ajira, tamisemi ajira za afya, wizara ya afya, ajira Tanzania - selection za vyuo , selection, second selection vyuo, second selection, tamisemi selection, selection form one 2020/2021

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

Share:

Community ART Officer (CAO) at MDH

POSITION: Community ART Officer (CAO) (8 Posts)   LOCATION:        Kagera, Geita & Dar es Salaam REPORTS TO:    District Community Services Manager (DCSM) Job Summary:  The Community ART Officer (CAO) is responsible for the day-to-day field implementation of MDH’s community ART program and services. She/He will work with the Council Health Management Teams […]

This post Community ART Officer (CAO) at MDH has been posted by Udahiliportaldaily

Get more post by visiting Udahiliportal.com

know more details about Udahiliportal.com by visiting Udahiliportal.com - Find Jobs & Ajira mpya leo, ajira portal Tanzania, ajira yako, brighter Monday, mabumbe, mwananchi ajira, secretariet ya ajira, tamisemi ajira za afya, wizara ya afya, ajira Tanzania - selection za vyuo , selection, second selection vyuo, second selection, tamisemi selection, selection form one 2020/2021

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

Share:

TAMISEMI: Call for Work at Benjamin Mkapa Foundation (BMF) Released Today 29th September, 2021 | Download All Names Here

Overview   The Benjamin William Mkapa Foundation (BMF) is a non- profit Trust, established in 2006 with the vision towards healthy lives and well-being for all, in Tanzania and the rest of Africa. Its strategic focused results areas include to combat HIV and AIDS, TB, Malaria and Reproductive, Maternal New Born, Child and Adolescent Health […]

This post TAMISEMI: Call for Work at Benjamin Mkapa Foundation (BMF) Released Today 29th September, 2021 | Download All Names Here has been posted by Udahiliportaldaily

Get more post by visiting Udahiliportal.com

know more details about Udahiliportal.com by visiting Udahiliportal.com - Find Jobs & Ajira mpya leo, ajira portal Tanzania, ajira yako, brighter Monday, mabumbe, mwananchi ajira, secretariet ya ajira, tamisemi ajira za afya, wizara ya afya, ajira Tanzania - selection za vyuo , selection, second selection vyuo, second selection, tamisemi selection, selection form one 2020/2021

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

Share:

TB/HIV Officers at MDH

POSITION: TB/HIV Officers (6 Posts)   LOCATION:        Geita, Kagera & Tabora REPORTS TO:    TB/HIV Manager Job Summary:  The TB/HIV Officer works with and supports the MDH RTB-HIV Manager to ensure efficient implementation, M&E and reporting of TB/HIV services in her/his respective region including direct field coordination of key program priorities such as […]

This post TB/HIV Officers at MDH has been posted by Udahiliportaldaily

Get more post by visiting Udahiliportal.com

know more details about Udahiliportal.com by visiting Udahiliportal.com - Find Jobs & Ajira mpya leo, ajira portal Tanzania, ajira yako, brighter Monday, mabumbe, mwananchi ajira, secretariet ya ajira, tamisemi ajira za afya, wizara ya afya, ajira Tanzania - selection za vyuo , selection, second selection vyuo, second selection, tamisemi selection, selection form one 2020/2021

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

Share:

Maternal and Child Health (MCH) Officers at MDH

POSITION: Maternal and Child Health (MCH) Officers (7 Posts)   LOCATION:        Geita, Kagera, Tabora & Dar Es Salaam REPORTS TO:    Regional Maternal and Child Health (MCH) Manager Job Summary:  The Maternal and Child Health (MCH) officer works with and supports the MDH RMCH Manager to ensure efficient implementation, M&E and reporting of reproductive, maternal, […]

This post Maternal and Child Health (MCH) Officers at MDH has been posted by Udahiliportaldaily

Get more post by visiting Udahiliportal.com

know more details about Udahiliportal.com by visiting Udahiliportal.com - Find Jobs & Ajira mpya leo, ajira portal Tanzania, ajira yako, brighter Monday, mabumbe, mwananchi ajira, secretariet ya ajira, tamisemi ajira za afya, wizara ya afya, ajira Tanzania - selection za vyuo , selection, second selection vyuo, second selection, tamisemi selection, selection form one 2020/2021

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

Share:

Grants Manager at MDH

POSITION:   Grants Manager (1 Post)   LOCATION:   Dar es Salaam REPORTS TO:    Director of Grants and Compliance Job Summary:  Reporting to the Director of Grants and Compliance, the Grants Manager is responsible for overall oversight and coordination of donor engagement and proposal development. She/He will work with all other staff to develop and submit high […]

This post Grants Manager at MDH has been posted by Udahiliportaldaily

Get more post by visiting Udahiliportal.com

know more details about Udahiliportal.com by visiting Udahiliportal.com - Find Jobs & Ajira mpya leo, ajira portal Tanzania, ajira yako, brighter Monday, mabumbe, mwananchi ajira, secretariet ya ajira, tamisemi ajira za afya, wizara ya afya, ajira Tanzania - selection za vyuo , selection, second selection vyuo, second selection, tamisemi selection, selection form one 2020/2021

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

Share:

Wednesday, 29 September 2021

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO ALHAMISI SEPTEMBA 30, 2021
















Share:

SERIKALI YADHAMIRIA KUENDESHA SEKTA YA SANAA KIBIASHARA


Serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imedhamiria kuendesha sekta ya Sanaa kibiashara na kuongeza tija ikiwa ni pamoja na kuwezesha sekta hii kutumika kama nyenzo ya kuhamasisha na kuelimisha jamii kuhusu masuala ya kiuchumi, kijamii na kisiasa.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Exaud Kigahe Septemba 29, 2021 wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Sekta ya Sanaa 2021 ambao lengo lake ni kujadili kwa Pamoja masuala yanayohusu Sekta ya Sanaa kati ya Serikali na wadau ili kufikia lengo la kuifanya sekta hii kuendeshwa kibiashara ambapo kauli mbiu ya mkutano huo ni “Sanaa Biashara”

“Serikali imejipanga kuweka mazingira wezeshi ya kukuza Sanaa zetu ili kufikia viwango vya kimataifa na kuboresha mbinu na Mikakati ya Utekelezaji wa sera na Sheria za kuimalisha kazi za Sanaa nchini kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa Sanaa hususani wasanii” amaeeleza Mhe. Exaud Kigahe

Aidha, Mhe. Exaud Kigahe ameeleza kuwa Wizara ya Viwanda na Biashara ni mdau mkubwa wa Wizara ya Sanaa, Utamaduni na Michezo kwani Sekta ya Sanaa ni kiwanda kinachozalisha bidhaa na huduma za sanaa ambazo zinahitaji mchango mkubwa wa Wizara ya Viwanda na Biashara katika kuweka sera, sheria, kanuni na miongozo mbalimbali ya kusimamia uendeshaji wake na kuiendeleza kama inavyofanyika katika Sekta nyingine za kiuchumi hapa nchini.

Kwa upande wake, Dkt. Emmanuel Ishengoma Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Sanaaa wa Wizara ya Sanaa, Utamaduni na Michezo ameeleza kuwa ili kuendesha Sanaa kibiashara, Serikali imeanzisha mfuko wa Utamaduni na Sanaa ambao utasaidia kuimarisha sekta hiyo kwa kudhamini mafunzo vilevile kutoa mkopo kwa mashariti nafuu ya kusaidia Sanaa na utamaduni na mpaka sasa Serikali imeshatoa billioni moja na milioni mia tano za kuwezesha mfuko huo.
Share:

WAZIRI MHAGAMA AKAGUA MIFUMO YA USALAMA NA AFYA MGODI WA SHANTA


Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge,Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama (Mb) akikagua maeneo ya mgodi mpya wa dhahabu wa Shanta uliopo Wilayani Ikungi Mkoani Sindiga alipofanya ziara ya kukagua usimikaji wa mifumo Usalama na Afya katika mgodi huo kabla ya kuanza rasmi shughuli za uchimbaji zinazotarajiwa kuanza mwakani. Alioambatana nao ni Meneja Mkuu wa Mgodi huo Mhandisi Jiten Divecha (Kushoto), Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki, Miraji Mtatulu (Kulia) pamoja na viongozi wa Wilaya ya Ikungi na baadhi ya wafanyakazi wa mgodi huo.


Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge,Kazi, Vijana,Ajira na wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama (Mb), akizungumza na baadhi ya wafanyakazi wa Mgodi mpya wa Dhahabu wa Shanta Singida pamoja na viongozi mbalimbali wa Wilaya ya Ikungi, wakati wa ziara yake katika mgodi huo iliyolenga kukagua usimikaji wa mifumo Usalama na Afya katika mgodi huo kabla ya kuanza rasmi shughuli za uchimbaji dhahabu zinazotarajiwa kuanza mwakani. Wengine ni Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki, Miraji Mtatulu (Kulia) na Kaimu Katibu Tawala wa Wilaya ya Ikungi Dijovison Ntangeki (Kushoto).


Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana,Ajira na wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama (Mb), akizungumza na baadhi ya wafanyakazi wanaojenga miundombinu mbalimbali katika Mgodi wa Dhahabu wa Shanta Singida alipotembelea maeneo mbalimbali ya mgodi huo yanayoandaliwa kwaajili ya uchimbaji wa dhahabu unaotarajiwa kuanza rasmi mwakani. Waziri Jenista aliambatana na viongozi mbalimbali wakiwemo Mkurugenzi wa Usalama na afya kutoka OSHA, Mhandisi Alexander Ngata (wakwanza kushoto kwa Mhe. Waziri), Kaimu Katibu Tawala wa Wilaya ya Ikungi Dijovison Ntangeki (Mwenye koti la suti) pamoja na Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki, Miraji Mtatulu (wakwanza kulia) na Meneja Mkuu wa Mgodi huo Mhandisi Jiten Divecha (wapili kushoto).


Mkurugenzi wa Usalama na afya kutoka OSHA, Mhandisi Alexander Ngata, akitoa taarifa juu ya hali ya utekelezaji wa Sheria ya Afya na Usalama na Afya ya mwaka 2003 katika Mgodi wa Dhahabu wa Shanta Singida katika kikao baina ya Waziri pamoja na menejimenti na wafanyakazi mgodi huo wakati wa ziara ya Waziri iliyokuwa na lengo la kukagua usimikaji wa mifumo Usalama na Afya katika mgodi huo kabla ya kuanza rasmi shughuli za uchimbaji dhahabu.


Mkurugenzi wa Usalama na afya kutoka OSHA, Mhandisi Alexander Ngata (mwenye kofia ya bluu) na Kaimu Meneja wa Kanda ya Kati, Venance Buliga (mwenye barakoa nyeupe), wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama (Mb), alipokuwa akizungumza na menejimenti pamoja na wafanyakazi wa Mgodi wa Dhahabu wa Shanta Singida alipofanya ziara katika mgodi huo

******************************

Na Mwandishi Wetu

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu), Jenista Mhagama, amefanya ziara katika Mgodi wa Dhahabu wa Shanta uliopo Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida kwa lengo kukagua usimikaji wa mifumo ya Usalama na Afya katika hatua za awali za maandalizi ya uchimbaji madini katika mgodi huo.

Waziri amesema ni muhimu kwa sehemu mbalimbali za kazi zinazoanzishwa hapa nchini ikiwemo migodi kuwahusisha wataalam wa Usalama na Afya katika hatua za awali za ujenzi wa miundombinu ili waweze kupata ushauri utakaowawezesha kujenga miundombinu inayozingatia viwango vya Usalama na Afya mahali pa kazi na hivyo kuepuka kuweka miundombinu ambayo ipo kinyume na Sheria na kanuni za usalama na afya mahali pa kazi.

“Kwetu sisi na wenzangu wa OSHA tutakachojitahidi ni kuendelea kuwapa elimu ya kutosha kuhusu masuala ya usalama na afya mahali pa kazi ili mbobee kwenye eneo hilo kusudi muondoshe migogoro katika eneo lenu la kazi na ndio maana ninaomba muwaruhusu hapa wawe na tawi la wafanyakazi. Lakini tutawasadia pia kukagua na kuangalia mifumo yenu ya usalama na afya kama itaweza kulinda afya za wafanyakazi hususan pale mtakapoanza rasmi uzalishaji kwani tunatambua kwamba shughuli hizi za uchimbaji madini huambatana na vihatarishi vingi vya usalama na afya ambavyo vinahitaji mifumo madhubuti ya kukabiliana navyo,” amesema Jenista Mhagama.

Akiwa ameambatana na Waziri Mhagama katika ziara hiyo, Mkurugenzi wa Usalama na Afya wa Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA), Mhandisi Alexander Ngata, ametoa wito kwa makampuni makubwa ambayo yanafanya kazi na makampuni saidizi (sub-contractors) kuhakikisha kwamba makampuni hayo yanazingatia Sheria na kanuni za usalama na afya mahali pa kazi.

Awali akiwasilisha taarifa yake kuhusu hali ya usalama na afya katika mgodi huo mbele ya Waziri, Mkurugenzi wa Usalama wa OSHA, Mhandisi Ngata alieleza kwamba kampuni hiyo imekuwa ikijitahidi kutekeleza matakwa yote ya Sheria ya Afya na Usalama Mahali pa Kazi kama ambavyo wamekuwa wakielekezwa na wataalam kutoka OSHA. Aidha, alibainisha kwamba changamoto iliyopo ni kwa makampuni saidizi (sub-contractors) yanayofanya kazi na Shanta ambayo bado hayazingatii utekelezaji wa Sheria tajwa.

Kwa upande wake Kaimu Meneja wa Kanda ya Kati inayojumuisha mikoa ya Dodoma, Singida, Tabora na Kigoma, Venance Buliga, amesema wamekuwa wakishirikiana ipasavyo na uongozi wa mgodi huo katika hatua mbalimbali za ujenzi wa miundombinu ya uchimbaji madini katika mgodi huo ambapo wamekuwa wakifanya ukaguzi na kutoa ushauri wa kitaalam kuhusu namna bora ya kujenga miundombinu inayozingatia afya na usalama wa wafanyakazi.

Aidha, menejimenti ya mgodi huo pamoja na wafanyakazi wameeleza kuwa usalama na afya kwa wafanyakazi ni miongoni mwa vipaumbele vya kampuni hiyo.

“Tunafanya kazi kwa kuzingatia misingi mitatu ambayo ni biashara, mahusiano na jamii inayotuzunguka pamoja na afya na usalama wa watu wetu kama kama tulivyoeleza katika taarifa yetu kwa Mheshimiwa Waziri na yeye pamoja na wataalam wa OSHA wamethibitisha hilo walipotembelea sehemu mbalimbali katika mgodi,” amesema Mhandisi Jiten Divecha, Meneja Mkuu wa Mgodi wa Shanta wa Ikungi Mkoani Singida.

“Kwa masuala ya usalama na afya hapa Shanta tuko vizuri sana, kila sehemu ambayo watu wanafanya kazi masuala ya matumizi sahihi ya vifaa kinga yanazingatiwa ipasavyo na pia wakaguzi wa OSHA huwa wanatutembelea kuangalia namna tunavyofanya kazi na kutushauri kuboresha endapo tunakuwa kinyume na taratibu za usalama na afya mahali pa kazi,” amesema Ferdinand Cyprian, Mfanyakazi wa Mgodi wa Shanta-Ikungi katika kitengo cha upakaji rangi majengo.

Taasisi ya OSHA ambayo ipo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu) ina dhamana ya kusimamia utekelezaji wa Sheria ya Afya na Usalama Mahali pa Kazi ya mwaka 2003 pamoja na kanuni zake ambayo pamoja na mambo mengine inawataka wamiliki wa sehemu za kazi nchini kusajili maeneo yao na OSHA, kufanyiwa ukaguzi wa usalama na afya, kuchunguza afya za wafanyakazi pamoja na kuwapa mafunzo ya usalama na afya mahali pa kazi.
Share:

DKT. NDUMBARO AWATAKA WATUMISHI WA UMMA KUUTUMIKIA UMMA KWA UZALENDO, UADILIFU NA WELEDI


Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro akifungua kikao kazi cha ofisi yake na Taasisi zinazosimamia Maadili na vyama vya kitaaluma chenye lengo la kubadilishana uzoefu wa usimamizi wa maadili, kilichofanyika Ukumbi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI Mtumba jijini Dodoma.


Baadhi ya washiriki wa kikao kazi cha Taasisi zinazosimamia Maadili na vyama vya kitaaluma chenye lengo la kubadilishana uzoefu wa usimamizi wa maadili wakimsikiliza Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI Dkt. Laurean Ndumbaro (hayupo pichani) wakati akifungua kikao kazi hicho kilichofanyika Ukumbi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI Mtumba jijini Dodoma.


Mkurugenzi wa Idara ya Ukuzaji Maadili, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bi. Leila Mavika (wa kwanza kushoto) akitoa neno la utangulizi wakati wa ufunguzi wa kikao kazi cha ofisi yake na Taasisi zinazosimamia Maadili na vyama vya kitaaluma chenye lengo la kubadilishana uzoefu wa usimamizi wa maadili, kilichofanyika Ukumbi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI Mtumba jijini Dodoma.


Baadhi ya washiriki wa kikao kazi cha Taasisi zinazosimamia Maadili na vyama vya kitaaluma chenye lengo la kubadilishana uzoefu wa usimamizi wa maadili, wakifuatilia moja ya mada iliyowasilishwa na Mkurugenzi wa Idara ya Ukuzaji Maadili, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bi. Leila Mavika katika kikao kazi hicho kilichofanyika Ukumbi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI Mtumba jijini Dodoma.


Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa kikao kazi cha Taasisi zinazosimamia Maadili na vyama vya kitaaluma chenye lengo la kubadilishana uzoefu wa usimamizi wa maadili mara baada ya kukufungua kikao kazi hicho, kilichofanyika Ukumbi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI Mtumba jijini Dodoma.

*********************************

Na Veronica Mwafisi-DODOMA

Tarehe 29, Septemba, 2021



Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro amewataka Watumishi wa Umma nchini kuutumikia umma kwa uzalendo, uadilifu na weledi ili kutimiza azma ya Serikali ya kutoa huduma bora kwa wananchi.

Dkt. Ndumbaro ametoa wito huo wakati akifungua kikao kazi cha siku mbili cha taasisi simamizi za maadili na vyama vya kitaaluma chenye lengo la kubadilishana uzoefu wa usimamizi wa maadili, kilichofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya RaiS-UTUMISHI Mtumba, jijini Dodoma.

Dkt. Ndumbaro amesema uzalendo, uadilifu na utendaji kazi unaozingatia weledi ndio nguzo kuu ya utendaji kazi wa Watumishi wa Umma ikiwa ni pamoja na ustawi wa taifa.

Ameongeza kuwa, ofisi yake imekuwa na utamaduni endelevu wa kushirikiana na taasisi zinazosimamia maadili na vyama vya kitaaluma ili kujenga taifa imara lenye Watumishi wa Umma wazalendo na waadilifu.

“Ushirikiano uliopo kati ya ofisi yangu na taasisi simamizi za maadili na vyama vya kitaaluma, utasaidia kujenga uadilifu kwenye utumishi wa umma na jamii kwa ujumla”, Dkt. Ndumbaro amefafanua.

Dkt. Ndumbaro amesema, Watumishi wa Umma nchini wanao wajibu wa kuunga mkono kwa vitendo azma ya Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan ya kuujenga Utumishi wa Umma kuwa wenye kuzingatia uadilifu, uwajibikaji, Kanuni, Sheria, Taratibu na miongozo iliyopo.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Idara ya Ukuzaji Maadili, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bi. Leila Mavika amesema lengo kuu la kikao kazi hicho ni kukumbushana uzingatiaji wa maadili, kujadili changamoto za usimamizi wa maadili katika Utumishi wa Umma na kuzitafutia ufumbuzi.

Mwanasheria wa Bodi ya Wataalamu ya Ununuzi na Ugavi, Bw. Suleiman Mzava ambaye ni mmoja wa washiriki wa kikao kazi hicho amesema, kikao kazi hicho kitasaidia kujenga uadilifu miongoni mwa taasisi za umma hivyo ameipongeza Serikali kwa kuweka nguvu kubwa katika usimamizi wa maadili.

Watumishiwa Umma wa wakizingatia uzalendo, uadilifu na weledi katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku, watatoa huduma bora kwa wananchi na kutoa mchango mkubwa katika maendeleo ya taifa.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger