Friday, 12 February 2021

Tanzia : MBUNGE ATASHASHTA NDITIYE AFARIKI DUNIA

...

Mbunge wa Muhambwe mkoani Kigoma na ambaye pia alikuwa Naibu Waziri wa Wizara ya Uchukuzi, Atashasta Justus Nditiye amefariki dunia leo Ijumaa Februari 12,2021 saa 4:00 asubuhi.

Spika wa Bunge Job Ndugai amethibitisha habari hizo akisema Nditiye alifariki wakati akipatiwa matibabu baada ya ajali ya gari aliyopata Februari 10, 2021 eneo la Nanenane Nzuguni mkoani Dodoma.

Kutokana na kifo hicho, Ndugai ameahirisha shughuli za Bunge hadi kesho Jumamosi wakati itakapotolewa taarifa za taratibu za kuaga mwili na maziko.

Nditiye anakuwa mbunge wa pili kufariki katika Bunge la 12 baada ya Martha Umbulla, aliyekuwa mbunge wa viti maalum (CCM), kufariki hivi karibuni.
Share:

Related Posts:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © 2025 MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger