Friday, 19 February 2021

RAIS MAGUFULI AONGOZA WAOMBOLEZAJI KUAGA MWILI WA BALOZI KIJAZI DAR

...

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akiwa amekaa kwa majonzi wakati mwili wa Aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Injinia John Kijazi ulipowasili kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam leo Ijumaa Februari 19,2021 ambako anaongoza shughuli za kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa Marehemu Mara baada ya kumalizika kwa ibada ya kuaga.
Rais mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Jakaya Kikwete wa pili kutoka kushoto , Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim Juma, Naibu Spika wa Bunge Mh.Dk. Tulia Ackson Makamu wa pili wa Rais Zanzibar Mh. Hemedi Suleiman Abdallah kulia ni miongoni mwa waombolezaji waliojitokeza kuaga mwili wa Aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Injinia John Kijazi kwenye viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam leo Ijumaa Februari 19,2021.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Dk.Bashiru Ali na Waziri wa Sheria na Katiba Dk.Mwigulu Nchemba wakiwa katika viwanja vya Karimjee kwa ajili ya kuaga mwili wa Aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi Marehemu Balozi Injinia John Kijazi.
Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii na Kamishna mkuu wa Shirika la hifadhi za Taifa TANAPA Allan Kijazi kulia akiwa pamoja na Ndugu na jamaa wakati wa kuaga mwili wa ndugu yao mpendwa Marehemu Injinia Balozi John Kijazi kwenye viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam leo.
Mwili wa Marehemu Balozi Injinia John Kijazi ukiwasili kwenye viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam ambapo shughuli za kuaga zinafanyika kabla ya kwenda Korogwe Mkoani Tanga kwa mazishi.
Mwili wa Marehemu Balozi Injinia John Kijazi ukiwasili kwenye viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam ambapo shughuli za kuaga zinafanyika kabla ya kwenda Korogwe mkoani Tanga kwa mazishi.
Baadhi ya Makatibu wakuu wa Wizara mbalimbali wakipita na kutoa heshima zao za mwisho kwa Aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi Marehemu Balozi Injinia John Kijazi.
***
Rais wa Tanzania John Magufuli anaongoza waombolezaji katika kuaga mwili wa katibu mkuu kiongozi John Kijazi.

Shughuli hiyo inafanyika katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam.

Baada ya kuagwa kwa taratibu za kiserikali, mwili utasafirishwa hadi Korogwe mkoani Tanga ambapo atazikwa siku ya Jumamosi.

Balozi Mhandisi John William Herbert Kijazi amekuwa mwakilishi wa Tanzania nchini India, Singapore, Sri Lanka, Bangladesh na Nepal mwenye makazi yake jijini New Delhi, India kuanzia mwaka 2007 - 2016 na hivyo kumfanya kuwa Mkuu wa Mabalozi wote wanaowakilisha Tanzania nje ya nchi.

Kabla ya kuwa balozi, Mhandisi Kijazi alikuwa Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi na baadaye Wizara ya Maendeleo ya Miundombinu kuanzia mwaka 2002 hadi 2006, baada ya kuteuliwa kuwa Balozi ndani ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano waKimataifa na hatimaye kupangiwa kituo cha New Delhi, India.
Share:

Related Posts:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © 2025 MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger