Thursday, 11 February 2021

MTOTO WA MIAKA 9 ACHOMWA MOTO KWA TUHUMA YA KUIBA KARANGA SHINYANGA

...

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba,kushoto ni mfano wa karanga

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Jeshi la Polisi mkoa wa Shinyanga linamshilikilia mwanamke aliyejulikana kwa jina la Christina Mwagi (29) kwa tuhuma ya kumjeruhi kwa kumchoma moto sehemu mbalimbali za mwili wake mtoto wake mwenye umri wa miaka 9 akishirikiana na mme wake (baba wa kambo) Yohana Michael (34) kwa tuhuma za kuiba karanga.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba amesema tukio hilo limetokea Februari 7,2021 majira ya saa saba mchana katika kijiji na kata ya Usule wilaya ya Shinyanga.

Amesema Peter Mahona (45) ambaye ni mwenyekiti wa kitongoji cha Usule aligundua mtoto huyo wa kike mwenye umri miaka 09 ambaye ni mwanafunzi darasa la tatu katika shule ya msingi Usule kufanyiwa vitendo vya ukatili kwa kujeruhiwa kwa kuchomwa na moto sehemu mbalimbali za mwili wake.

“Aliyetekeleza tukio hilo Christina Mwagi ambaye ni mama mzazi na Yohana Michael ambaye ni baba wa kambo”,amesema Kamanda Magiligimba.

Amesema chanzo cha mtoto huyo kuchomwa moto sehemu mbalimbali za mwili wake ni mtoto huyo kuiba karanga.

Ameongeza kuwa madhura anapatiwa matibabu katika hospitali ya rufaa mkoa wa Shinyanga na hali yake ni mbaya na kwamba watuhumiwa watafikishwa mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilika.

Kamanda Magiligimba anatoa wito kwa wananchi wa mkoa wa Shinyanga kuendelea kutoa taarifa za ukatili dhidi ya watoto kwa Jeshi la polisi ili kukomesha vitendo hivyo.
Share:

Related Posts:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © 2025 MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger