Thursday, 18 February 2021

BALOZI KIJAZI KUZIKWA TANGA JUMAMOSI FEBRUARI 20

...
Balozi John Kijazi enzi za uhai wake

Na Aurea Simtowe - Mwanchi

 Katibu mkuu Ikulu, Dk Moses Kasiluka amesema aliyekuwa katibu mkuu kiongozi, Balozi John Kijazi atazikwa Jumamosi Februari 20, 2021 wilayani Korogwe Mkoa wa Tanga.


Amesema ibada ya kuaga mwili wa Balozi Kijazi aliyefariki dunia jana Jumatano Februari 17, 2021 katika hospitali ya Benjamin Mkapa mkoani Dodoma itafanyika kesho asubuhi katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam na kuongozwa na Rais John Magufuli.

Amesema leo shughuli ya kuaga mwili wa Balozi Kijazi ilifanyika katika Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom) na kisha mwili ukasafirishwa hadi jijini Dar es Salaam.

“Utasafirishwa kwenda Dar es Salaam nyumbani wake na utalala hapo na kesho asubuhi kutakuwa na ibada itakayoongozwa na Rais Magufuli na viongozi wengine wa Serikali.”

“Baada ya kukamilisha shughuli ya kuaga ratiba tuliyonayo ni kuwa atazikwa siku ya Jumamosi, Korogwe nyumbani kwao, tunawakaribisha wote wanaoweza kushiriki kumsindikiza kiongozi wetu,” amesema Dk Kasiluka.

Via Mwananchi

Share:

Related Posts:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © 2025 MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger