Sunday, 6 September 2020

Tundu Lissu Leo Atazindua kampeni Kanda ya Kusini katika Uwanja wa Sabasaba, mjini Mtwara.

...
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CHADEMA  Tundu  Lissu leo Septemba 6, 2020. atazindua kampeni Kanda ya Kusini (Lindi, Mtwara na Ruvuma) katika Uwanja wa Sabasaba, mjini Mtwara.

Jana alikuwa Kanda ya Nyasa, katika viwanja vya Nzovwe, jijini Mbeya ambapo pamoja na mambo mengine aliahidi kujenga maeneo maalum kwa ajili ya shughuli za Machinga na Mamalishe  ambayo yatakuwa wazi usiku na mchana. 

Lissu alisema baadhi ya wananchi huwa wanachelewa kufika kwenye miji yao wanapokuwa wametoka safarini na hivyo kukosa huduma za kununua mahitaji kwenye masoko kutokana na masoko hayo kufungwa .

“Tutajenga masoko maalum kwa kushirikiana na sekta binafsi kwenye maeneo mbalimbali ili machinga wetu wafanye biashara hapo kwa uhuru na kila mmoja atakuwa na chumba chake,” aliahidi.

Vilevile, Lissu alisema serikali yao itajenga majengo maalumu kwenye maeneo ya stendi za mabasi kwa ajili wa wauzaji vyakula, maarufu mamalishe na babalishe, ili wafanyie biashara zao huko kwa uhuru.


Share:

Related Posts:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © 2025 MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger