Tuesday, 31 December 2019

Picha : MBUNGE MASELE ACHANGIA MILIONI 9 KUSAIDIA UJENZI WA SOKO LA NDALA, ZAHANATI YA MWAWAZA NA MASEKELO

...
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Stephen Julius Masele amechangia shilingi milioni 9 kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa soko la kata ya Ndala,ujenzi wa zahanati ya Mwawaza na Masekelo katika Manispaa ya Shinyanga.


Akizungumza leo Jumanne Desemba 31,2019 wakati wa akiendelea na ziara yake ya kukagua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo katika jimbo lake la Shinyanga Mjini ,Mhe. Masele amesema fedha hizo zitasaidia kuchochea maendeleo kwa wananchi.

“Kupitia fedha za Mfuko wa Jimbo la Shinyanga Mjini,naahidi kuchangia shilingi milioni tano kwa ajili ya kusaidia kumalizia ujenzi wa soko la Ndala,lakini pia shilingi milioni mbili kwa ajili kusaidia ujenzi wa zahanati ya Mwawaza na shilingi milioni mbili kwa ajili ya ujenzi wa zahanati ya Masekelo”,amesema Masele.

Akiwa katika kata ya Mwawaza Masele ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Bunge la Afrika (PAP),amesema serikali inaendelea kutekeleza miradi miradi mbalimbali ikiwemo ya barabara na maji ambapo tayari jumla ya shilingi milioni 400 zimeshapelekwa katika Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Mjini Shinyanga (SHUWASA) kwa ajili ya kupeleka maji Mwawaza.

Katika hatua nyingine,Masele amewahimiza wakazi wa Mwawaza kulinda ardhi yao kwa kupima mashamba yao katika mfumo wa viwanja na kutunza hati za ardhi kwani ardhi ina thamani kubwa.

“Mji wa Shinyanga unapanuka,hapa Mwawaza imejengwa hospitali ya mkoa wa Shinyanga,naomba mpime ardhi yenu,mpate hati na siku mkiamua kuuza basi muuze kwa ridhaa yenu,sitaki kusikia mtu anawadhulumu ardhi yenu kwani kwenye baadhi ya maeneo kwenye jimbo nilihangaika kutatua migogoro ya ardhi kutokana na maeneo kutokuwa katika mpangilio mzuri”,ameeleza Masele.

Mhe. Masele akiwa ameambatana na Wajumbe wa kamati wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Shinyanga mjini,leo Desemba 31,2019 ametembelea kata tatu ambazo ni Mwawaza,Masekelo na Ndala.

ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Stephen Julius Masele akizungumza katika kata ya Mwawaza leo Desemba 31,2019 na kuahidi kuchangia shilingi milioni mbili kusaidia ujenzi wa zahanati ya Mwawaza wakati akiendelea na ziara yake kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika jimbo lake la Shinyanga Mjini. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Stephen Julius Masele akielezea mikakati mbalimbali inayofanywa na serikali kuwaletea maendeleo wananchi huku akiwaahidi wananchi wa Mwawaza kuwa huduma ya maji kutoka Ziwa Victoria imeanza kutekelezwa kwani tayari serikali imetoa shilingi milioni 400 ili kuwapatia huduma ya maji wananchi wa Mwawaza.
Wajumbe wa halmashauri wa Chama Cha Mapinduzi CCM kata ya Mwawaza wakiwa katika kikao na Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Stephen Masele.
Wajumbe wa halmashauri wa Chama Cha Mapinduzi CCM kata ya Mwawaza wakiwa katika kikao na Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Stephen Masele.
Katibu Msaidizi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Shinyanga mjini Rashid Mnunduma akizungumza wakati wa ziara ya Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Stephen Julius Masele katika kata ya Mwawaza.
Diwani wa kata ya Mwawaza Juma Nkwabi akizungumza wakati wa ziara ya Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Stephen Julius Masele.
Mwenyekiti wa CCM kata ya Mwawaza Dotto Mamboleo akisoma taarifa fupi ya Chama na serikali kata ya Mwawaza ambapo alizitaja changamoto wanazokabiliana nazo kuwa ni umeme,maji,barabara na zahanati.
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Stephen Julius Masele akizungumza katika kata ya Ndala leo Desemba 31,2019 na kuahidi kuchangia shilingi milioni tano kusaidia kukamilisha ujenzi wa soko la Ndala.Kulia ni Katibu Msaidizi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Shinyanga mjini Rashid Mnunduma,kushoto ni Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana CCM (UVCCM) wilaya ya Shinyanga Mjini Dotto Joshua. 
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana CCM (UVCCM) wilaya ya Shinyanga Mjini Dotto Joshua akizungumza wakati wa ziara ya Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Stephen Julius Masele katika kata ya Ndala.
Mwenyekiti wa UWT wilaya ya Shinyanga Mjini Shumbuu Katambi akizungumza wakati wa ziara ya Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Stephen Julius Masele.
Afisa Mtendaji wa kata ya Ndala Lucas Magandula akisoma taarifa ya utekelezaji wa miradi mbalimbali katika kata ya Masekelo.
Wajumbe wa halmashauri wa Chama Cha Mapinduzi CCM kata ya Ndala wakiwa katika kikao na Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Stephen Masele.
Wajumbe wa halmashauri wa Chama Cha Mapinduzi CCM kata ya Ndala wakiwa katika kikao na Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Stephen Masele.
Soko la Ndala ambalo ujenzi wake bado haujakamilika ambapo Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Stephen Julius Masele ameahidi kuchangia shilingi milioni 5 ili kukamilisha ujenzi huo.
Mwenyekiti wa CCM kata ya Ndala Rashid Mahene akizungumza wakati wa ziara ya Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Stephen Julius Masele.
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Stephen Julius Masele akizungumza na Wajumbe wa halmashauri wa Chama Cha Mapinduzi CCM kata ya Masekelo.
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Stephen Julius Masele akizungumza na Wajumbe wa halmashauri wa Chama Cha Mapinduzi CCM kata ya Masekelo ambapo aliahidi kuchangia shilingi milioni mbili kusaidia ujenzi wa zahanati ya Masekelo.
Katibu Msaidizi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Shinyanga mjini Rashid Mnunduma akizungumza wakati wa ziara ya Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Stephen Julius Masele katika kata ya Masekelo.
Katibu wa CCM kata ya Masekelo Peter John akisoma taarifa ya utekelezaji wa ilani ya CCM katika kata ya Masekelo.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM wilaya ya Shinyanga Mjini Esha Stima akizungumza wakati wa ziara ya Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Stephen Julius Masele.
Katibu wa Mbunge Jimbo la Shinyanga Mjini Mwajuma Radhia akizungumza wakati wa ziara ya Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Stephen Julius Masele.
Mwenyekiti wa CCM kata ya Masekelo Rashida Mahega akizungumza wakati wa ziara ya Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Stephen Julius Masele.
Wajumbe wa halmashauri wa Chama Cha Mapinduzi CCM kata ya Masekelo wakiwa katika kikao na Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Stephen Masele.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger