Monday, 4 March 2019

RUBANI WA MAKAMU WA RAIS AFARIKI KWA AJALI YA HELIKOPTA

...

Rubani wa Makamu Rais wa Kenya Williamu Ruto amekufa kwenye ajali ya helikopta akiwa na abiria wane raia wa Marekani mara baada ya ndege hiyo kuanguka eneo la Lobolo.

Kwa mujibu wa polisi Rubani huyo aliyefahamika kwa jina la Mario Magonga akiwa na abiria wake hao walipata ajali hiyo leo saa mbili asubuhi.

‘’Polisi waliichukua miili ya watu watano ambayo ilipatikana eneo hilo ambapo mmoja wapo ni raia wa Kenya rubani wa makamu wa Rais Mario Magonga’’alisema taarifa ya polisi

Taarifa hiyo ilisema mpaka sasa chanzo cha ajali hiyo bado hakijafahamika lakini mpaka baadaye uchunguzi unaofanywa na polisi utabainika nini hasa chanzo cha ajali hiyo.

Share:

Related Posts:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © 2025 MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger