Friday, 8 March 2019

LOWASSA KUTIKISA ARUSHA...ZIARA YAKE YA KWANZA BAADA YA KUREJEA CCM

...


Wakazi wa Jiji la Arusha na viunga vyake kesho Machi 9, 2019, watampokea aliyekuwa mgombea wa Urais kwa tiketi ya Chadema katika uchaguzi mkuu wa 2015, Edward Lowassa ambaye sasa anaingia mkoani humo akiwa na utambulisho mpya wa kada wa Chama cha Mapinduzi (CCM).

Lowassa ambaye ni Waziri mkuu Mstaafu, alijiunga na Chadema Julai 28, 2015 lakini Machi Mosi, 2019, alirejea rasmi CCM na kuwaambia viongozi na wananchi waliofika kushuhudia kurejea kwake katika ofisi ndogo za makao makuu ya CCM Lumumba, jijini Dar es Salaam “nimerudi nyumbani.”

Inaelezwa kuwa Lowassa ataondoka Dar es Salaam saa tano asubuhi na kuwasili Arusha saa sita na atapokewa na viongozi wa CCM ngazi ya mkoa na kisha ataelekea wilayani Monduli.

Akiwa Monduli, atapokewa na uongozi wa wilaya na baadaye atahutubia mkutano.

Na Lilian Timbuka, Mwananchi
Share:

Related Posts:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © 2025 MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger