Thursday 19 October 2017

JE UNATAKA KUBADILI KOZI ULIYOCHAGULIWA CHUO KIKUU?SOMA>>NJIA KUU TATU ZITAKAZOKUFANYA UAME KOZI KIURAHISI

...
 Image result for TCU.GO.TZ
Habari yenu wadau wapendwa wa blog hii ya MASWAYETU BLOG wadogo hamjambo?wakubwa shikamoni.

Kwanza kabisa nipende kuwapongeza wale wote waliochaguliwa kujiunga na vyuo mbalimbali ndani na nje ya Bongo yetu hii.Hongereni sana kwani nyie ni baadhi ya vijana wengi waliokosa nafasi hizo;


Leo napenda kuzungumzia mada kubwa kuhusu ubadilishaji wa kozi uingiapo chuoni,Kutokana na vijana wengi kuchaguliwa kozi ambazo hawazitaki,mfano mtu alikuwa anataka kusomea ualimu akajikuta kachaguliwa hotel management au mwingine alikuwa anataka kusomea udakatari akajikuta kachaguliwa Ualimu LEO nitaelezea njia ambazo unaweza kuzifanya ili uweze kuadilisha kozi na kusoma kozi unayoitaka;
Zifuatazo ni njia hizo;

1.KUBADILI KOZI SIKU YA KWANZA YA REGISTRATION
   UFIKAPO CHUONI.
-Hii ni kati ya njia ambazo ni nyepesi sana ambayo itakufanya usome kozi unayotaka kusoma tofauti na uliyochaguliwa,ukifika
siku ya kwanza chuoni.Wakati wa kusajiliwa utakuta kila kozi na sehemu yake,wewe nenda moja kwa moja sehemu wanayosajili kozi utakayotaka kuhamia,then ongea na yule anaesajili mwombe kwa upole atakusikiliza tu,usifanye papara kusajili,MADHARA ya njia hii ni kwamba itaweza ikakupa usumbufu kwenye mkopo baadae.
2.KUBADILI KUPITIA TCU.

   -Hii pia inaweza ikakufanya uame kozi unayotaka kuhama na kuhamia unayotaka kusoma,cha kufanya fata maelekezo waliyotoa tcu jinsi ya kuhama chuo kwa kubonyeza hapa>>>>>TARATIBU ZA KUHAMA CHUO 

3.NJIA YA TATU NI KUANDIKA BARUA
-Njia hii ndio njia inayokubalika kiofisi lakini kuhamishwa kwake kiukweli ni vigumu sana kwani unaweza ukakauta wanaohamishwa kati ya wanafunzi 2000 ni 20 tu,na nikati ya njia ngumu na ndefu sana kwani inaweza kukuchukua takribani wiki 4 hadi kuhamishwa.KIKUBWA FIKA MAPEMA  CHUONI HAPO.
Makala hii imeandaliwa na; 
INNOCENT THE BLOGGER BOY(hata mimi nilifanikiwa kubadilisha kozi niliyochaguliwa)
MMILIKI HALALI WA MASWAYETU BLOG

Kama unaswali Ni follow instagram,then ni inbox,search>>>>MASWAYETU BLOG
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger