Tuesday 31 October 2017

HAYA HAPA MAJINA YA WATANZANIA WALIOPANGIWA KAZI KADA YA AFYA OCTOBER 30 2017

...
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA




OFISI YA RAIS
Anuani ya Simu: “TAMISEMI”
Tawala za MKOA na
Simu Na: (026) 2322848, 2321607
Serikali za Mitaa,
2322853, 2322420
Jengo la Mkapa,
Nukushi: (026) 2322116, 2322146
2 Barabara ya hospitali,
2321013

S.L.P. 1923,
Barua pepe: ps@tamisemi.go.tz
41185 DODOMA.




Unapojibu tafadhali taja:

Kumb. Na. CD. 162/355/01
30 Oktoba, 2017



TANGAZO LA KUITWA KAZINI


OR TAMISEMI kwa kushirikiana na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto inapenda kuwataarifu waombaji kazi wa nafasi mbalimbali za kada za Afya walioomba kazi kuanzia tarehe 25/07/2017 hadi tarehe 30/08/2017 kuwa mchakato wa kuwapangia vituo vya kazi umekamilika.

Aidha, mnatakiwa kuripoti katika vituo vya kazi mlivyopangiwa katika muda wa siku kumi na nne (14) kuanzia tarehe ya tangazo hili mkiwa na vyeti halisi (Originals Certificates) vya masomo kuanzia kidato cha nne na kuendelea kwa ajili ya kuhakikiwa na mwajiri kabla ya kupewa barua ya ajira.

Orodha ya majina ya waliopangiwa vituo vya kazi inapatikana kupitia tovuti ya OR TAMISEMI www.tamisemi.go.tz. Hakutakuwa na mabadiliko ya vituo, watakaoshindwa kuripoti katika muda uliopangwa, nafasi zao zitajazwa na waombaji wengine wa kada husika.

Kwa wale ambao majina yao hayakuonekana katika tangazo hili watambue kuwa hawakupata nafasi hivyo wasisite kuomba kwa mara nyingine nafasi za kazi zitakapotangazwa. Nafasi za Wauguzi na Wahudumu wa Afya zitatangazwa mara baada ya kukamilisha zoezi la uchambuzi na uhakiki wa vyeti.

Waajiri wote mnaelekezwa kuwapokea, kuhakiki vyeti na kuwafanyia mafunzo elekezi (Induction Course) kabla ya kuwapangia vituo vya kazi.



Limetolewa na:-

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini

OR – TAMISEMI


30/10/2017

KUYAONA MAJINA HAYO

Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger