Thursday, 30 July 2026

RC SHINYANGA AFANYA ZIARA YA UKAGUZI MIRADI YA MAENDELEO KISHAPU

Na Sumai Salum – Kishapu
  • ARIDHISHWA NA HATUA YA MIRADI YA MAENDELEO KISHAPU

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Mboni Mhita, Julai 29, 2026 amefanya ziara ya kukagua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo wilayani Kishapu mkoani humo, ikiwa ni pamoja na mradi wa sekta za elimu, afya, maji, miundombinu ya barabara, miradi inayotekelezwa kwa ushirikiano na wadau wa maendeleo pamoja na unufaishaji wa mikopo ya asilimia 10 ya Halmashauri. 

Akiwa katika ziara hiyo, Mhita amesema maendeleo yanayoonekana ni matokeo ya amani, utulivu na demokrasia ya kiuchumi inayowavutia wadau wa maendeleo na wawekezaji kushirikiana na Serikali kuboresha maisha ya wananchi.


Mhita amesema Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imeendelea kuwekeza katika sekta ya elimu kwa kujenga vyumba vya madarasa na kuboresha miundombinu ya shule ili kuhakikisha kila mtoto anapata haki ya elimu katika mazingira bora, ikiwa ni pamoja na kuongeza uwiano wa madarasa na matundu ya vyoo kulingana na idadi ya wanafunzi. Aidha, amepongeza vikundi vilivyonufaika na mikopo ya asilimia 10 ya Halmashauri, ikiwemo kikundi cha Wachapakazi kilichotumia mkopo huo kununua trekta kwa ajili ya kuongeza tija katika shughuli za uzalishaji.

Hata hivyo mmoja wa wananchi kutokea Kata ya Mwataga Patricia Nkana ameipongeza Serikali kwa kuendelea kuboresha huduma za afya na upatikanaji wa maji safi na salama, akisema ujenzi na uboreshaji wa zahanati na upanuzi wa upatikanaji wa maji safi na salama umeongeza usalama wa akina mama wajawazito wakati wa kujifungua na kuinua ustawi wa wananchi kwa ujumla na kuchochea kuimarisha afya ya ndoa zao.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Mboni Mhita akizungumza wakati wa ziara yake ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo wilayani Kishapu ikiwa ni pamoja na mradi wa sekta za elimu, afya, maji, miundombinu ya barabara, miradi inayotekelezwa kwa ushirikiano na wadau wa maendeleo pamoja na unufaishaji wa mikopo ya asilimia 10 ya Halmashauri Julai 29, 2026
Katibu Tawala mkoani Shinyanga Cp. Salum Hamduni akiwa kwenye ziara ya Mkuu wa Mkoa huo Mhe. Mboni Mhita Wilayani Kishapu Julai 29, 2026
Mkuu wa Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga Mhe Peter Masindi akizungumza wakati wa ziara ya Mkuu wa Mkoa huo Mhe. Mboni Mhita Wilayani humo ya kukagua miradi mbalimbali ikiwa ni pamoja na miradi ya sekta za elimu, afya, maji, miundombinu ya barabara, miradi inayotekelezwa kwa ushirikiano na wadau wa maendeleo pamoja na unufaishaji wa mikopo ya asilimia 10 ya Halmashauri Julai 29, 2026 Katibu Tawala wilayani Kishapu mkoani Shinyanga Fatma Mohamed akiwa kwenye ziara ya Mkuu wa Mkoa huo Mhe. Mboni Mhita Wilayani Kishapu Julai 29, 2026
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga Emmanuel Johnson
Mwananchi wa Kata ya Mwataga wilayani Kishapu mkoani Shinyanga Patricia Nkana akielezea namna wanavyonufaika na uboreshaji wa miundombinu hasa ya Elimu, Afya, Maji na Nishati ya Umeme hadi Vijijini Julai 29,2026 wakati wa ziara ya Mkuu wa Mkoa huo Mhe Mboni Mhita wilayani humo

Tazama picha za matukio mbalimbali👇👇👇























































































































































































Share:

Wednesday, 29 July 2026

SANGU: WADAU TUCHANGIE MADAWATI




Na Mwandishi wetu, Sumbawanga

Wadau wa maendeleo ndani na nje ya mkoa wa Rukwa wamehamasishwa kuchangia upatikanaji wa madawati kwa ajili ya kuwezesha watoto kusoma kwenye mazingira wezeshi kwa ustawi wa taaluma.

Wito huo umetolewa hivi karibuni na Mbunge wa Jimbo la Kwela ambaye pia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira na Mahusiano Mhe. Deus Sangu wakati alipokabidhi madawati kwa shule za msingi katika jimbo hilo alipofanya ziara ya kikazi.

Katika ziara hiyo sangu alikabidhi madawati  zaidi ya 100 kwa shule za msingi sita (6) yenye thamani ya shilingi Milioni 60 ambayo ameyapata kupitia ufadhili ya Benki ya Taifa ya Biashara (NBC).

Waziri Sangu akizungumza kwenye moja ya mikutano yake na wananchi wa kijiji cha Nankanga tarafa ya Kipeta na kijiji cha Ilemba alisema ametoa msaada huo kuunga mkono jitihanda za wananchi katika kuchangia maendeleo ya elimu.

“ Nimekuja hapa kukabidhi zawadi ndogo kwa Watoto.Leo nimewaletea madawati 20 ambapo yatasaidia Watoto 60 kutoendelea kukaa chini” alisema Waziri Sangu.

Mbunge huyo aliongeza kuwaambia wananchi kuwa yeye ni mbunge wa vitendo na kwamba anapenda vitu vinavyoonekana ambapo aliitumia fursa hiyo kushukuru uongozi wa Benki ya NBC kwa kuguswa na shida za wanaKwela .

“Ninashukuru benki ya NBC kwa msaada wao waliotupatia madawati haya yanayokwenda kupunguza tatizo la watoto kukaa chini. utatuzi huu wa kero za wananchi ni sehemu ya maelekezo tuliyopewa na Rais  Dkt. Samia Suluhu Hassan kwetu wabunge” alisema Sangu alipoongea na wananchi wa Kijiji cha Msia kata ya  Milepa huku akitoa wito kwa wadau wengine wa maendeleo kuchangia madawati kwa ajili ya jimbo la Kwela.

Miongoni mwa shule zilizopokea madawati hayo na idadi yake kwenye mabano ni shule ya msingi Kalumbaleza (20), Msia (20), Kimambo (15), Ilemba (20) , Nankanga (20) na Deusi Sangu sekondari madawati (30).

Akizungumza kwa niaba ya wananchi, Diwani wa kata ya  Mwadui Mahmood Leonce Mgweno alisema amepokea madawati toka Ofisi ya Mbunge na kwa tayari amefikisha shuleni na kumpongeza Mbunge Sangu kwa msaada.

Nao wananchi wametumia fursa ya ziara ya mbunge Sangu kueleza kufurahishwa kwao na jitihada anazozifanya kuchangia maendeleo ya jimbo hilo ikiwemo msaada wa madawati.

Nae Bwa.Thomas Nsandale ameishukuru Ofisi ya Mbunge kwa kuwezesha wa upatikanaji wa  madawati ikiwa ni miongoni mwa vingi walivyopatiwa katika kipindi chote Mhe.Sangu akiwa Mbunge wa Jimbo la Kwela 

“Sangu amefanya mambo mengi ambayo yanatufanya sisi wananchi kutokupunguza upendo juu yake na tunamuomba pia Madawati haya yasiwe ya mwisho kwa wananchi wake wa Kwela Bali iwe sababu ya muendelezo wa Maendeleo haya” amesema Nsandale.

Waziri Sangu alikuwa jimboni Kwela wilaya ya Sumbawanga kukagua shughuli za maendeleo pamoja na kuzungumza na wananchi.

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger