Wednesday, 1 April 2026

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMATANO APRILI 1,2026

 

Magazeti

                                

Share:

Tuesday, 31 March 2026

Tanzia : BWEGE AFARIKI DUNIA



Chama cha ACT Wazalendo kimetangaza kwa masikitiko kifo cha mwanachama wake, Ndugu Seleman Bungara maarufu kama Bwege, kilichotokea ghafla wakati akiwa hospitalini akipatiwa matibabu ya kusafisha figo (dialysis).

Kupitia taarifa iliyotolewa na kiongozi wa chama, Dorothy Semu, chama kimetoa pole kwa familia ya marehemu, ndugu, jamaa na wanachama wote walioguswa na msiba huo.

ACT Wazalendo imemtaja marehemu Bungara kama mwanasiasa wa upinzani aliyekuwa mstari wa mbele katika kupigania haki na demokrasia nchini.

 Chama hicho kimesema kitashiriki kikamilifu katika mazishi na kuwataka wanachama kuungana na familia katika kipindi hiki kigumu.


Share:

WMA YATOA MSAADA WA VIFAA VYA UJENZI KWA WAHITAJI DODOMA


Katika kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia, Wakala wa Vipimo (WMA) imetoa misaada ya vifaa vya ujenzi wa jiko la kisasa katika Kituo cha kulelea watoto wenye mahitaji maalumu Cha RAHMAN ORPHANAGE CENTER kilichopo Chang'ombe jijini Dodoma.
Akizungumza baada ya kutoa misaada hiyo Meneja wa WMA Mkoa wa Dodoma Said Ibrahimu amesema suala la mazingira safi ya kupikia ni haki ya kila mmoja ndio maana wameamua kama Wakala kutoa misaada hiyo itakayowezesha upishi wa kisasa katika mazingira safi na salama ikiwemo usalama wa chakula kwani kituo hicho wamekuwa wakipika kwa kutumia kuni na mazingira ya Nje ambayo sio salama kwa afya ya watoto hao.

"tunamuunga mkono Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuhakikisha nishati safi ya kupikia inakuwa katika mazingira safi na salama ndio maana leo kwa niaba ya wafanyakazi wa WMA tumekabidhi Sementi, Marumaru na vifaa vingine vitakavyosaidia ujenzi wa jiko hilo, "amesema Meneja Said
Kadhalika, Mkurugenzi wa kituo hicho Bi. Rukia Abdallah ameishukuru WMA kwa misaada hiyo itakayokwenda kuboresha mazingira ya mapishi katika Kituo hicho chenye idadi ya watoto 120 huku akiomba wadau wengine kujitokeza kuchangia kituo hicho ikiwemo suala la usafiri ili watoto hao waweze kutembelea maeneo mbalimbali kwa ajili ya kujifunza zaidi.

Mmoja wa watoto wanaolelewa katika Kituo hicho Hazra Ramadhan ameipongeza Wakala wa Vipimo kwa kuona umuhimu wa kuwasaidia na kuwaomba kuendelea kuwakumbuka kila mara ili waweze kutimiza malengo yao.
Share:

Monday, 30 March 2026

TUNAHITAJI MATOKEO YA UTEKELEZAJI WA MRADI WA PAMOJA.DKT JINGU




Na WMJJWM – Dar Es Salaam

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. John Jingu amasisizitiza kasi katika utekelezaji wa mradi wa kukuza usawa wa kijinsia pamoja na kuleta matokeo yenye tija kwa jamii.

Dkt. Jingu amesema hayo Machi 27, 2026, Jijini Dar es Salaam wakati akiongoza kikao cha Kamati elekezi ya utekelezaji wa mradi wa Kukuza Usawa wa Kijinsia Tanzania (PAMOJA) kwa lengo la kujadili na kuimarisha uratibu na uendeshaji wa mradi huo.

Dkt. Jingu amesema katika utekelezaji wa mradi huo, kila mmoja ahakikishe anatimiza majukumu yake kwa ufanisi kwa nafasi aliyonayo, ili kuleta matokeo tarajiwa ili hatimaye mradi uache alama chanya kwa jamii.

Kwa upande wake Katibu wa Kamati hiyo ambaye ni Mkurugenzi wa Sera na Mipango kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wanawaka na Makundi Maalum Victor Nkya amesema mradi huo utawanufanisha wanawake kwa kupitia mikopo ili kuendesha shughuli za kiuchumi na kuongeza kipato cha familia.

“Mradi huu utawafikia wanawake wajasiriamali ili kukuza na kuimaridha Uchumi wa kaya jamii na familia kupitia mikopo yenye masharti nafuu, kutoa elimu ya kupinga ukatili wa kijinsia kuipitia vikundi vya wanawake mtaani na sokoni, pamoja na kuimarisha malezi hatimaye kutakuwa na Watoto wenye maadili na wenye kuleta tija katika jamii” amesema Nkya.

Mradi wa PAMOJA unatekeleza kwa Tanzania bara na Zanzibar, ukilenga kuimarisha usawa wa kijinsia, kupunguza na kutokomeza vitendo vya ukatili wa kijinsia, kuongeza fursa za kiuchumi kwa wanawake, kupinga na kutokomeza ukatili wa kijinsia na kuimarisha malezi nchini.





Share:

Sunday, 29 March 2026

SOAT YAZINDULIWA, YAAHIDI KUONGEZA MAPATO YA UTALII KUFIKIA BILIONI 790

Na Mussa Juma,Arusha.

Jumuiya ya Wawekezaji Mahiri katika maeneo ya Wanyamapori(SOAT) imezinduliwa rasmi jijini Arusha, huku wawekezaji hao wakiahidi kushirikiana na serikali  kuendeleza  Utalii na kuhakikisha ndani ya miaka 20 wanaingizia taifa kiasi cha shilingi Bilioni 790 kutokana uwekezaji wao.

Akizungumza katika Uzinduzi huo, Mtendaji mkuu wa SOAT, Erasmus Tarimo alisema wanachama wa SOAT wanatarajia kuwekeza katika miradi mbali mbali kwa jamii kwa kiasi cha USD 50 milioni kwa kipindi cha miaka ishirini sawa na shilingi bilioni 125.

Tarimo alisema kutakuwa na uwekezaji katika ulinzi wa usiopungua dola milioni 20  ili kukabiliana na majangili kwa kipindi cha miaka 20 na  uwekezaji katika utafiti dola milioni 7.

Alisema SOAT,  inatarajia Kuimarisha mfumo wa udhibiti ili kuhakikisha usimamizi imara na mazingira yanayotabirika ya uwekezaji wa muda mrefu unaotegemea utalii wa wanyamapori.

“ Mheshimiwa mgeni rasmi Dira yetu sisi ni kuunganisha wanyamapori, jamii na Utalii kwa ajili mafanikio endelevu ya kiuchumi  na Misheni ni Kushirikiana kulinda wanyamapori, kuinua jamii katika kuhifadhi na kuendeleza utalii endelevu”,alisema.

Tarimo alisema, Malengo ya jumuiya hiyo kuongeza wigo wa chaguo kwa wateja kuhusiana na shughuli za matumizi na sisizo za matumizi, kutekeleza uwekezaji bunifu kaatika utalii na kuhimiza uwekezaji mbadala na kuendeleza na kutangaza bidhaa za utalii Pamoja na kudumisha ubora wa maeneo ya uhifadhi.

“ Pia tunakusudia kuendeleza uwekezaji toshelezi ili kuwekeza katika kujenga miundombinu stahiki katika maeneo ya hifadhi,kuimarisha uhifadhi , manufaa ya kijamii na kiuchumi pamoja kuzalishamapato zaidi na kutumia rasilimali za wanyamapori kwa kutoa shughuli mbalimbali endelevu za matumizi ya wanyamapori”, alisema.

Akizindua umoja huo, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TAWA, Meja Jenerali ( Mstaafu) Hamis Semfuko alipongeza wawekezaji hao wa maeneo la Uwekezaji mahiri wa wanyamapori(SWICA) kuanzisha umoja huo ambao utasaidia sana kuimarisha mawasiliano na serikali.

Alisema tangu kuanza utaratibu wa SWICA  Serikali imekuwa ikinufaika sana na uwekezaji mahiri katika maeneo ya Wanyamapori zaidi ya mara tisa kwa sasa.

Alisema Mfumo wa uwekezaji mkakati wa SWICA ulianza kutekelezwa kwa kuanzia na wawekezaji sita Kwa kiasi cha uwekezaji wenye thamani ya USD milioni 278 sawa na shilingii bilioni 696 .

Meja Generali mstaafu , Semfuko alisema awali SWICA ilikuwa na  wawekezaji  sita na sasa kuna wawekezaji 13 na wapo wengine ambao wanataka kuwekeza hatua ambayo inaonesha umuhimu wa uwekezaji huu mahiri katika sekta ya Utalii.

Alisema Rais Samia Suluhu Hassan amekuwa akifuatilia sana uwekezaji katika SWICA na anaamini kuwa unakwenda kulinufaisha sana Taifa lakini pia kuchangia kupunguza migogoro baina ya wanyamapori na binaadamu na kuongeza ajira na mapato.

Awali Kaimu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori(TAWA), Mlage Yussuf Kabange alisema alisema maeneo ya SWICA yapo ndani ya maeneo ya TAWA hivyo,SOAT itapewa ushirikiano mkubwa kuhakikisha inafikia malengo yake.

Kamishna  Kabange alisema TAWA inaamini kukiimarishwa ushirikiano, lengo la Serikali kufikisha watalii milioni nane ifikapo mwaka 2030 litafanikiwa.

Akizungumza kwa niaba ya Mwenyekiti wa SOAT, Makamu Mwenyekiti Martha Lucumay  alisema wamejipanga kufanyakazi na serikali lakini wanaomba pia changamoto kadha ikiwepo za kikodi kufanyiwa kazi.

Akizungumza katika uzinduzi huo,mmoja wa Wakurugenzi wa kampuni ya Mwiba Holdings Ltd ambayo ni miongoni mwa wanachama waanzishilishi wa SOAT.Nicolaus Negri alishukuru Serikali kufika katika uzinduzi huo na kuahidi SOAT itafanyakazi kwa kushirikiana na Serikali.

Negri pia aliwashukuru viongozi wa chama cha mawakala wa Utalii nchini(TATO) chama cha Wawindaji wa Utalii nchini(TAHOA), Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori(TAWIRI) na wadau wengine wa Utalii kushiriki katika uzinduzi huo amba oni muhimu katika kuboresha sekta ya uhifadhi na Utalii nchini.

Maeneo ambayo yanawekezwa kupitia SWICA  ni Eneo la kaskazini la pori la akiba la Maswa,Maswa Kimali ,Maswa Mbono;Mapori ya akiba ya Grumeti na Ikorongo;.Pori la akiba la Mkungunero,Pori Tengefu la Ziwa Natroni na Kitalu cha LL1 katika pori la akiba la Selous.

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger