Saturday, 24 January 2026

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI JANUARI 24, 2026




magazetini








Share:

Friday, 23 January 2026

TUTACHUKUA HATUA KALI KWA WATAKAOTUMIA TAARIFA BINAFSI ZA WATU KINYEMELA- PDPC



Tume ya taarifa ya ulinzi wa Taarifa binafsi Tanzania PDPC imetangaza kuanza mara moja kwa ukaguzi wa uzingatiaji wa sheria kwa Taasisi za umma na za binafsi, zinazokusanya na kuchakata taarifa binafsi.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Alhamisi Januari 22, 2026, Mkurugenzi Mkuu wa Tume hiyo Dkt. Emmanuel Mkilia amesema zoezi hilo linafanyika mara baada ya muda wa hiari kuisha kulingana na tangazo la Tume hiyo lililoweka ukomo wa Aprili 8, 2026 kwa Taasisi husika kukamilisha usajili wao.

"Ukaguzi huu utahusisha kubaini Taasisi za umma na za binafsi zinazokusanya, kuhifadhi kuchakata na kusafirisha taarifa binafsi nje ya nchi bila kuzingatia matakwa ya sheria ya ulinzi wa taarifa binafsi sura ya 44 na kanuni zake na PDPC tutachukua hatua kali za kisheria dhidi ya yeyote, taasisi ama kampuni itakayokiuka sheria hii ikiwa ni pamoja na faini, kifungo, fidia kwa waathirika ama vyote kwa pamoja." Amesema Dkt. Mkilia.

Aidha PDPC imesema mtu ama Taasisi itakayobainika kutumia taarifa ya mtu binafsi bila ridhaa yake au kinyume na taratibu zilizowekwa kisheria, Taasisi hiyo itawajibishwa Ipasavyo bila ya kujali hadhi ama ukubwa wa Taasisi itakayokiuka misingi ya sheria katika ulinzi wa taarifa binafsi.

Pamoja na mafanikio yanayotokana na ukuaji wa TEHAMA duniani, kumekuwepo na changamoto mbalimbali ikiwemo ulinzi wa taarifa binafsi ambazo zimekuwa zikikusanywa, zikichakatwa na wakati mwingine kusafirishwa kutoka nchi moja kwenda nyingine bila kuzingatia utaratibu na misingi ya ulinzi wa taarifa binafsi iliyokubalika kisheria.


Share:

Thursday, 22 January 2026

MASLAHI YA TAIFA KWANZA: MAPINDUZI YA KIFIKRA NA KIUCHUMI KATIKA KULINDA RASILIMALI

Katika ulimwengu wa sasa unaotawaliwa na ushindani mkali wa kidiplomasia na kiuchumi, Tanzania na mataifa mengine ya Afrika yanapita katika kipindi cha kihistoria kinachohitaji mabadiliko makubwa ya kifikra ili kulinda rasilimali na mustakabali wa vizazi vijavyo. 

Kupitia mjadala mzito uliofanyika hivi karibuni, wasomi na viongozi wabobezi nchini wakiongozwa na Profesa wa Uchumi, Samuel Wangwe, Kanali Mstaafu Joseph Simbakalia na mwanasiasa mkongwe Hamad Rashid Mohammed, wametoa msisitizo ambao unapaswa kuwa dira ya maendeleo ya taifa letu. 

Hoja kuu inayopaswa kueleweka kwa kila mwananchi ni kuwa maslahi ya kitaifa ni kitu kitakatifu ambacho hakipaswi kuchezewa au kuamuliwa kwa misingi ya itikadi za vyama vya siasa, ukabila wala dini, bali kwa kuangalia faida ya muda mrefu ya taifa zima.

Profesa Samuel Wangwe ameweka wazi kuwa taifa linalolenga maendeleo ya kweli ni lile ambalo wananchi wake wanaunganishwa na msimamo mmoja wa kizalendo, hususan katika usimamizi wa rasilimali. 

Ili kufikia hatua hii, kuna haja kubwa ya kuongeza thamani ya rasilimali zetu badala ya kuziuza kama malighafi pekee, jambo ambalo linawezekana tu kwa kuwekeza kwa vijana kupitia teknolojia. Profesa Wangwe anazitaja nchi za India, China na Malaysia kama mifano ya kuigwa kwani zimepiga hatua kwa kuwapeleka vijana wao kujifunza nje ya nchi na kurudi kukuza uchumi wa viwanda wa ndani. Hii ina maana kuwa ufunguo wa utajiri wa Tanzania haupo tu kwenye madini au ardhi, bali upo kwenye akili za vijana walioandaliwa kiteknolojia kuongoza mageuzi ya kiuchumi.

Ukombozi wa kifikra ni nguzo nyingine muhimu iliyosisitizwa na Kanali Mstaafu Joseph Simbakalia, ambaye amewataka Waafrika kuacha kutegemea mataifa ya Magharibi kuamua mustakabali wao. 

Simbakalia anafafanua kuwa kudhani kuwa mataifa ya nje yana mamlaka ya mwisho juu ya matumizi ya rasilimali zetu ni aina ya utumwa wa kifikra unaorudisha nyuma maendeleo. Ili Afrika iweze kujenga uchumi imara, viongozi wanapaswa kutanguliza uadilifu na kuwajibika kwa wananchi bila kuathiriwa na shinikizo za nje au migogoro ya kikanda inayochelewesha umoja. 

Hoja ya utambulisho na utamaduni imeguswa kwa uzito na Hamad Rashid Mohammed, ambaye anakumbusha kuwa ukoloni haukuishia tu kwenye utumwa wa kimwili bali uliingia kwenye mioyo ya Waafrika kwa kuwafanya wadharau tamaduni zao. Siasa za kimataifa kwa sasa zinatumia taasisi za kifedha kama mbinu mpya ya utawala, jambo ambalo linaweza kupingwa tu ikiwa tutaimarisha utamaduni wetu wa kupendana, kusikilizana na kudhibiti rasilimali zetu wenyewe. 

Mkakati wa kuelimishana juu ya umuhimu wa kujitambua kama Waafrika ndio utakaotuwezesha kusimamia maendeleo yetu bila kuyumbishwa na misaada yenye masharti magumu yanayominya uhuru wetu wa kiuchumi.

Ujumbe huu wa pamoja kutoka kwa wabobezi hawa unatoa funzo kubwa kwa vijana, wafanyakazi na wafanyabiashara nchini Tanzania kuwa maendeleo ya nchi ni jukumu la pamoja. Serikali ya Awamu ya Sita tayari imeanza kutekeleza misingi hii kwa kufungua fursa za kibiashara na mataifa makubwa kama Marekani huku ikisisitiza tija na ajira kwa wazawa. Ni wajibu wa kila mwananchi kuelewa kuwa tunapozungumzia uwekezaji katika madini ya kimkakati au mikopo ya halmashauri kwa vijana, tunazungumzia utekelezaji wa maslahi ya taifa kwa vitendo. Maamuzi yoyote tunayoyafanya leo katika ngazi ya familia, halmashauri au serikali kuu lazima yapimwe kwa mizani ya kama yanajenga au yanabomoa umoja na utajiri wetu wa pamoja kama taifa.

Share:

ILALA TUNAJIVUNIA RAIS SAMIA, AMETULETEA MAENDELEO- MAMBO


Na Jonas Jovin, Dar

Wananchi wa Wilaya ya Ilala Jijini Dar Es Salaam wameeleza kufurahishwa na kazi kubwa inayotekelezwa na Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan hasa katika Ujenzi wa mundombinu ya barabara za ndani, Vyumba vya madarasa katika shule za msingi na Sekondari pamoja na ujenzi wa miundombinu katika sekta ya afya na maji Wilayani humo.

Kwa kuitaja, wananchi hao wameeleza kuhusu ujenzi wa barabara za ndani kupitia miradi mbalimbali ikiwa ni pamoja na mradi wa DMDP, ikiwemo barabara ya Nyeburu- Miti mirefu pamoja na barabara ya Kigezi- Njianne kuelekea Majohe, wakisema awali ilikuwa ni ngumu kuona barabara za ndani zikijengwa kwa kiwango cha lami nchini.

Bw. Othman Hassan Mambo, Mkazi wa Nyeburu, ameitaja miradi ya ujenzi wa madarasa katika shule za msingi na sekondari ikiwemo katika shule za Msingi Nyeburu na Kaliani pamoja na ujenzi wa shule mpya ya Sekondari Kigezi.

"Mama Samia hakuishia hapo kwenye elimu pia ameipandisha hadhi shule ya Sekondari Nyeburu, na sasa ina kidato cha kwanza mpaka cha sita. 

Haya ni matunda ambayo Mhe. Rais ameyafanya, sisi tumpongeze kwa kazi hii kubwa iliyotukuka na sisi tunamuombea dua Mungu aendelee kumuweka na kumjalia afya njema." Amesema Bw. Mambo.

Katika hatua nyingine, mwananchi huyo pia ameeleza kuhusu urahisi wa sasa wa wananchi kupata Vitambulisho vya Taifa (NIDA) kupitia programu maalumu iliyoanzishwa ngazi ya Kata pamoja na kasi ya ujenzi wa tenki kubwa la maji Bangulo, akisema yote hayo ni sehemu ya jitihada za serikali za kuondoa changamoto zote zinazowakwaza wananchi.

Ameeleza pia kuhusu fursa za uwezeshaji wananchi kiuchumi kupitia Mikopo ya Halmashauri inayotolewa kwa Vijana, wanawake na wenye ulemavu, akisisitiza wajibu wa kila mmoja kulinda amani ili kuruhusu utekelezaji wa miradi ya maendeleo na ustawi wa wananchi.
Share:

WANANCHI WA UKONGA WAMSHUKURU RAIS SAMIA KWA KUDUMISHA AMANI NA USALAMA





Na Mwandishi wetu, Dar

Wananchi wa Ukonga Mkoani Dar Es Salaam wametoa pongezi na Shukrani kwa Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuimarisha amani, utulivu na usalama katika Jimbo lao la Ukonga, suala ambalo limewezesha shughuli za kiuchumi na kijamii kuendelea.

Kwaniaba ya wananchi wengine wa Jimbo hilo wakati akizungumza na Chombo chetu cha habari, Bw. Salum Issa Salum, Mkazi wa Kata ya Buyuni ameeleza kuwa licha ya kupitia baadhi ya changamoto mwishoni mwa mwaka jana, hali kwasasa ni shwari na hatua za maendeleo zimeendelea kushuhudiwa katika Kata hiyo na maeneo mengine kote Tanzania.

"Nisemee zaidi katika miundombinu, Mama amesikia kilio chetu na sasa barabara nyingi zimejengwa kwa kiwango cha lami kupitia miradi mbalimbali ikiwemo mradi wa DMDP kutoka hapa kwetu kwenda Kivule." Amesema Bw. Salum.

Katika maelezo yake, Mwananchi huyo amemuombea uhai zaidi na afya njema Rais Samia, akisisitiza pia umuhimu wa kila mwananchi kushiriki kikamilifu katika kuilinda amani ya Tanzania ili kutoa fursa ya Taifa na kila mwananchi kupiga hatua za kimaendeleo.
Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO ALHAMISI JANUARI 22,2026

Share:

Wednesday, 21 January 2026

Tanzia : MUASISI NA MWENYEKITI WA KWANZA WA CHADEMA EDWIN MTEI AFARIKI DUNIA







Mwasisi na Mwenyekiti wa kwanza wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Edwin Mtei amefariki Dunia usiku wa Januari 19, 2026.




Share:

Tuesday, 20 January 2026

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMATANO JANUARI 21, 2026

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger