Saturday, 14 October 2023

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI OKTOBA 14,2023





Share:

𝗧𝗨𝗞𝗢 𝗧𝗔𝗬𝗔𝗥𝗜 𝗞𝗨𝗦𝗛𝗜𝗥𝗜𝗞𝗜𝗔𝗡𝗔 𝗡𝗔 𝗦𝗘𝗞𝗧𝗔 𝗕𝗜𝗡𝗔𝗙𝗦𝗜: 𝗲-𝗚𝗔

Na Mwandishi Wetu. 

Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA), imeahidi kushirikiana na Benki ya NMB ili   kuimarisha, kukuza na kuendeleza ujuzi na vipaji kwa vijana wa Kitanzania wabunifu na wale wanaosoma fani ya TEHAMA, katika Vyuo Vikuu mbalimbali nchini, kupitia programu maalum ya mafunzo kwa vitendo inayotolewa na e-GA kupitia Kituo chake cha Utafiti, Ubunifu na Uendelezaji wa Serikali Mtandao (eGOVRIDC).

Kauli hiyo ilitolewa hivi karibuni na Mkurugenzi Mkuu wa e-GA Mha. Benedict Ndomba, wakati wa kikao cha pamoja kati ya e-GA na Benki ya NMB kilichofanyika katika Makao Makuu ya ofisi za e-GA jijini Dodoma, kwa lengo la kujadili namna taasisi hizo zinavyoweza kushirikiana katika maeneo mbalimbali ya teknolojia.

Maeneo hayo ni pamoja na utafiti, matumizi ya teknolojia za kisasa, kuvumbua vipaji na kuviendelea kwa wavijana wabunifu wa Kitanzania, pamoja na kutoa fursa kwa vijana wavumbuzi na wabunifu ikiwa ni sehemu ya kuendeleza Sekta ya TEHAMA nchini. 

Ushirikiano huo unatarajiwa kuongeza na kukuza fursa za ajira kwa vijana sambamba na kuimarisha uhusiano mzuri kati ya Serikali na sekta binafsi kwenye eneo la TEHAMA, alisema Ndomba .  

“e-GA imekuwa ikishirikiana na Vyuo Vikuu mbalimbali nchini  katika kuwapata vijana wenye ujuzi, hivyo makubaliano hayo kati ya e-GA na NMB ni muendelezo wa ushirikiano mazuri uliopo kati ya e-GA na wadau mbalimbali wa TEHAMA”, alifafanua Ndomba.

Aliongeza kuwa, katika kikao hicho taasisi hizo zimekubaliana kushirikiana na kuandaa mkataba wa makubaliano (MOU) ambapo baada ya kukamilika kwa mkataba huo, pande zote mbili zitakutana na kujadiliana namna ya utekelezaji wa makubaliano hayo. 

“e-GA imekuwa ikiwatengeneza vijana wanaoshiriki programu maalum ya mafunzo kwa vitendo pamoja na utaratibu wa kujitolewa (interns and volunteering) kupitia kituo chetu cha utafiti na ubunifu, kwa kuwajengea uwezo zaidi ili kwenda sambamba na soko la ajira pamoja na mabadiliko ya sayansi na teknolojia yanayoibuka kila siku”, alisema Ndomba.

Aidha, Ndomba aliishukuru Benki ya NMB kwa kuona umuhimu wa kutengeneza wataalamu wazawa wa TEHAMA   kupitia programu hiyo na kuwa,  e-GA ipo tayari kushirikiana na benki nyingine zenye dhamira ya kuijenga Tanzania ya kidijitali katika sekta zote za serikali na binafsi.

Naye Meneja eGovRIDC Dkt. Jaha Mvulla alisema, e-GA ipo tayari kushirikiana na Benki ya NMB katika maeneo mbalimbali yanayolenga kukuza matumizi ya TEHAMA nchini ikiwemo eneo la rasilimali za miundombinu na vifaa vya TEHAMA vya kufanyia mazoezi na majaribio, ubunifu hasa maeneo ya teknolojia mpya, kujenga uwezo na uzoefu kwa vijana, mafunzo kwa vitendo, utafiti na machapisho, maonesho, mashindano mbalimbali ya kidigitali kwa ajili ya kuvumbua vipaji, na maeneo mengine yanayohusiana na jitihada za Serikali Mtandao na teknolojia za kifedha.

“e-GA ipo tayari kufanya kazi na NMB kupitia programu maalumu ya mafunzo kwa vitendo inayoendeshwa na eGovRIDC, ili kuchochea ubunifu katika matumizi ya teknolojia mpya zinazoibuka duniani ikiwemo Akili Bandia (AI), Machine Learning,  Blockchain na matumizi yake kama vile kujenga ulewa wa teknolojia kama za Digital Currency na FinTech, Utengenezaji wa mifumo (System Development) kwa ajili ya kutatua changamoto zetu nchini na usalama mtandaoni (Cyber Security)”, alisema Dkt.Jaha.

Mkuu wa Kitengo cha Rasilimali Watu- Kituo cha Taaluma NMB Bi. Joanitha Rwegasira alisema kuwa, Benki ya NMB imeandaa programu hiyo ili kuongeza idadi ya vijana wabobezi kwenye masuala ya TEHAMA watakaofanya kazi katika sekta za umma na binafsi kwa lengo la kukuza taifa la kidijitali.

Programu hiyo itasaidia kufanya majaribio ya teknolojia mpya  zinazoibuka ikiwemo Sarafu ya mtandaoni na kutoa suluhu kwenye maeneo mbalimbali yenye changamoto katika utendaji kazi na utoaji wa huduma kwa wananchi ikiwemo matishio ya usalama mtandaoni, ubunifu wa mifumo n.k, alisema Rwegasira

Aidha, aliishukuru Mamlaka kwa kuonyesha utayari wa kushirikiana na NMB na kwamba watatumia fursa hiyo katika kuhakikisha wanaboresha huduma za kibenki hususani huduma zinazotolewa kidijitali.

Share:

Friday, 13 October 2023

MRADI KITUO CHA KUPOZA UMEME CHALINZE WAFIKIA ASILIMIA 84.3


Na Mwandishi wetu,Pwani.

*Asisitiza Watanzania wanataka umeme*

*Atoa Pongezi kwa wafanyakazi kwenye mradi huo

*TANESCO wapongezwa kwa hatua ya ujenzi*

Mradi wa ujenzi wa Kituo cha Kupoza Umeme wa Msongo wa kilovoti 400/220/132/33 wa kituo cha Chalinze umefikia asilimia 84.3 na hivyo kuleta matumaini ya kuboresha hali ya upatikanaji wa umeme. 

Hayo yameelezwa leo Oktoba 12, 2023 na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt. Doto Biteko alipotembelea na kuzungumza na wafanyakazi wa  kituo hicho cha Chalinze Mkoani Pwani, kujionea maendeleo ya ujenzi wa mradi huo. 

"kwa sasa  ujenzi umefikia asilimia. 84.3 na unatarajiwa kukamilika ifikapo tarehe 31 Disemba, 2023. Mradi huu unakwenda kupunguza changamoto ya umeme kwa kiasi kikubwa hususan katika mkoa huu wa Pwani," amesema Dkt. Biteko.

Ameongeza kuwa, mara baada ya Mradi huo kukamilika, kituo hicho kitakuwa na uwezo wa kupokea Megawatt 2115 kutoka katika Bwawa la kuzalisha Umeme wa Maji la Julius Nyerere na kitasambaza Megawati 850 kwenye mikoa ya Morogoro, Dar es Salaam na Pwani na kuimarisha hali ya upatikanaji umeme katika mikoa hiyo. 

Akizungumza na wafanyakazi wanaofanya kazi katika mradi huo amewataka wafanye kazi kwa bidii kwa kuwa Serikali imewapa ushirikiano ili mradi huo ukamilike kwa wakati. 

Meneja wa Mradi wa kituo hicho Mhandisi Newton Livingstone Mwakifwamba amesema kuwa Serikali imetoa ushirikiano mkubwa katika utekelezaji hususan katika mazingira mazuri ya wafanyakazi. Amesema mradi huo utakamilika kwa muda uliopangwa ifikapo mwezi Desemba 2023.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge amesema toka kuanza kwa mradi huo hakuna changamoto iliyojitokeza kukwamisha mradi huo. Amempongeza Dkt. Biteko kwa kutembelea mradi huo kujionea maendeleo yake.

Naye, Mbunge wa Jimbo la Chalinze Mhe. Ridhiwani Kikwete ambaye ni Naibu Waziri Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora amesema kuwa, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya kazi kubwa katika utekelezaji wa mradi huo na kusisitiza kuwa mradi utakapokamilika utakua ni msaada mkubwa wa mkoa wa Pwani.

Mradi huo ulianza rasmi tarehe 6 Septemba, 2021 ambapo kazi za ujenzi zilianza tarehe  11 Oktoba, 2021 na unahusisha ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme kutoka JNHPP hadi Chalinze pamoja na kituo cha kupoza umeme na kusafirisha umeme kuelekea mikoa ya kaskazini kwa kuingizwa Kenya Gridi ya Taifa.

Ziara hiyo ilihudhuriwa na  Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Mipango na Uwekezaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Decklan Mhaiki, Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Mhe. Halima Okash na Viongozi Mbalimbali wa Chama cha Mapinduzi mkoa wa Pwani na Watumishi wa mradi huo

Share:

KAMISHNA BENEDICT WAKULYAMBA AKAGUA MRADI WA UJENZI WA UWANJA WA NDEGE


Na: Zainab Ally – Mikumi

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Kamisha Benedict Wakulyamba amesema Miradi ya Ujenzi wa Viwanja vya ndege vinavyoendelea kujengwa katika Hifadhi za Taifa za Mikumi na Ruaha itaenda kuongeza kasi ya ukuwaji katika Sekta ya Utalii hasa katika ukanda wa Kusini mwa Tanzania.

Naibu Kamishna Benedict Wakulyamba amebainisha hayo alipotembelea Hifadhi ya Taifa ya Mikumi Oktoba 12, 2023 na kukagua ujenzi na Ukarabati wa uwanja wa ndege wa Kikoboga wenye urefu wa Kilomita 1.8 utakaozingatia taratibu zote za Ujenzi wa Viwanja vya ndege Duniani.

Aidha Wakulyamba amesema Ujenzi wa Kiwanja hicho ni mapinduzi makubwa katika Sekta ya Utalii ikizingatiwa changamoto za miundombinu mbalimbali zimeanza kutafutiwa ufumbuzi wa kudumu ili kuchagiza maendeleo katika Sekta hiyo.

Kwa upande wake Mhifadhi Mwandamizi ambaye ni Mratibu wa Mradi wa REGROW Kutoka Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) Michael Joseph alisema uwanja huo utakuwa na uwezo wa kutua ndege zenye ukubwa wa Q 300 na uwezo wa jengo litakalopokea abiria 140 pamoja na maegesho ya ndege 7.

Awali, wakati akitoa taarifa za Ujenzi wa uwanja huo kwa Naibu Katibu Mkuu, Bw. Michael alisema ujenzi wa mradi huo hauathiri shughuli zozote za utalii katika hifadhi hiyo kwa kutumia uwanja wa zamani, ambapo ndege za kitalii zinaingia kupitia uwanja wa zamani.

Naye, Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Mikumi Kamishna Msaidizi Mwandamizi Ignasi Gara alitolea ufafanuzi juu ya kasi kubwa ya kuongezeka kwa idadi ya watalii katika hifadhi hiyo ambapo mafuriko ya Watalii wa ndani wamezidi kuongezeka kutokana na kuboreshwa kwa miundombinu mbalimbali.

“Kwa mwaka Uliopita tulitazamia kupata watalii elfu 60,000, lakini kwa bahati nzuri baada ya kuanza kwa matengenezo ya uwanja takapata watalii Zaidi 100,000 ambapo tulivuka malengo, Tunaamini hata mwaka huu tutaendelea kupata idadi ya watalii wengi Zaidi” Alisema Kamishna Msaidizi Gara.

Kwaupande Naibu Kamishana wa Uhifadhi na maendeleo ya Biashara Helman Bathiho alisema ukarabati wa Miundombinu ya Barabara pamoja viwanja vya ndege katika Hifadhi za Taifa za Mikumi, Ruaha pamoja na Nyerere kunatajwa kutoa fursa kwa Watanzania katika kuwekeza katika ujenzi wa Hoteli za Kisasa ili kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla

Aidha Hifadhi ya Taifa ya Mikumi imeweka mikakati madhubuti kuhakikisha inaendelea kuboresha huduma rafiki ndani ya hifadhi ikiwemo kuongeza maeneo ya malazi pamoja na kuongeza bidhaa mpya za utalii ili kuchagiza ukuaji katika sekta hiyo.


Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO IJUMAA OKTOBA 13, 2023

 





















Share:

Thursday, 12 October 2023

SERIKALI KUONGEZA WODI MAALUM 100 ZA UANGALIZI WA WATOTO NJITI



Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel,akizungumza wakati akifungua Kongamano la kwanza la Afya ya Mtoto Tanzania na mkutano wa 24 wa Madaktari Bingwa wa Watoto Tanzania unaoendelea jijini Dodoma kwa lengo la kuangalia ustawi wa mtoto kuanzia anapozaliwa mpaka kukua kwake.


Mshauri Mkuu Mwandamizi wa Sera na mipango kutoka USAID Tanzania, Jema Bisimba,akizungumza wakati wa Kongamano la kwanza la Afya ya Mtoto Tanzania na mkutano wa 24 wa Madaktari Bingwa wa Watoto Tanzania unaoendelea jijini Dodoma kwa lengo la kuangalia ustawi wa mtoto kuanzia anapozaliwa mpaka kukua kwake.


Sehemu ya washiriki wakimsikiliza Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel (hayupo pichani) wakati akifungua Kongamano la kwanza la Afya ya Mtoto Tanzania na mkutano wa 24 wa Madaktari Bingwa wa Watoto Tanzania unaoendelea jijini Dodoma kwa lengo la kuangalia ustawi wa mtoto kuanzia anapozaliwa mpaka kukua kwake.


Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufungua Kongamano la kwanza la Afya ya Mtoto Tanzania na mkutano wa 24 wa Madaktari Bingwa wa Watoto Tanzania unaoendelea jijini Dodoma kwa lengo la kuangalia ustawi wa mtoto kuanzia anapozaliwa mpaka kukua kwake.

Na. WAF - Dodoma

Serikali kupitia Wizara ya Afya katika kuboresha Huduma za afya nchini imejenga wodi maalum za uangalizi wa watoto njiti 128 na kwa mwaka huu imepanga imepanga kujenga wodi nyingine 100 ili kuhakikisha vifo vya watoto wachanga vinapungua na kuisha kabisa.

Hayo yamebainishwa na Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel wakati akifungua Kongamano la kwanza la Afya ya Mtoto Tanzania na mkutano wa 24 wa Madaktari Bingwa wa Watoto Tanzania unaoendelea jijini Dodoma kwa lengo la kuangalia ustawi wa mtoto kuanzia anapozaliwa mpaka kukua kwake.

Dkt. Mollel amesema kuwa Serikali chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan imewekeza fedha nyingi katika uangalizi wa watoto njiti lengo likiwa ni kuwapatia huduma bora na uangalizi maalum mpaka watakapofikia uzito unaostahili.

“Uwekezaji huu ni pamoja na kuwa na madaktari Bingwa wa watoto (Madaktari wa Mama Samia), kuboresha miundombinu katika Hospitali zote zenye wodi ya uangalizi maalum kwa watoto njiti ( NICU)”. Ameeleza Dkt. Mollel.

Dkt. Mollel amesema serikali imeamua kuwekeza katika eneo hilo kwani mtoto kuanzia anapozaliwa mpaka kutimiza miaka 18 anahitaji uangalizi wa karibu ili kupata ustawi mzuri na kuwa na taifa la kesho imara.

Aidha, ametoa wito kwa Madaktari Bingwa wa Watoto nchini kuendelea kufanya kazi nzuri ya kuwahudumia watoto wanaozaliwa kabla ya siku na wale wanaozaliwa kawaida kwani wote wanahitaji uangalizi wa karibu katika ukuaji.

“Kwa niaba ya Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu tunawapongeza sana kwa kazi nzuri mnayofanya ya kuhakikisha mnapunguza vifo vya watoto wachanga nchini, na kwa mantiki hiyo niwahakikishie kuwa tutakuwa bega kwa bega na nyie ili kuhakikisha mnatekeleza majukumu yenu kwa ufasaha”. Amesema Dkt. Mollel.

Kwa upande wake Mshauri Mkuu Mwandamizi wa Sera na mipango kutoka USAID Tanzania, Jema Bisimba amesema kuwa hivi karibu watazindua programu ya USAID Tuwajali watoto yenye lengo la kusaidia watoto wanaoishi na virusu vya UKIMWI kuanzia miaka sifuri hadi miaka 17 kwa kuwawezesha Huduma zote zinazohusu mambo ya watoto.


Bisimba amesema kwa kupitia programu hiyo watasaidia Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan kupitia Wizara ya Afya kufikia lengo la kumaliza maambukizi ya virusi vya UKIMWI kwa watoto fufikia 2030
Share:

TEA YASHIRIKI MAONESHO YA ELIMU YA WATU WAZIMA KIBAHA


Mamlaka ya Elimu nchini TEA imesema inajivunia kuwa na wanufaika zaidi ya 49,000 nchi nzima walionufaika na mafunzo ya kuongeza ujuzi yaliyoendeshwa na vyuo mbalimbali chini ya mfuko wa kukuza ujuzi unaoratibiwa na mamlaka hiyo.

Akizungumza wakati wa kilele cha Juma la Elimu ya Watu Wazima ambalo maonesho yake kitaifa yanafanyika wilayani Kibaha mkoani Pwani, afisa habari wa Mradi wa Kuendeleza Ujuzi (SDF) Bi. Eliafile Solla amesema kuwa wengi wa wanufaika hao kwa sasa wamejiajiri na waliosalia wameajiriwa kutokana na mafunzo waliyoyapata.

“Kwa wale waliojiajiri wameendelea kukuza wigo wa ajira kwa kuendelea kuajiri watu wengine kwenye shughuli zao za kibiashara”

Mafunzo ya kuongeza ujuzi yanayotolewa na vyuo mbalimbali vyenye ithibati kutoka wizara ya elimu, sayansi na teknolojia yamejikita kwenye maeneo sita ya kipaumbele ya kilimo na kilimo uchumi, uchukuzi, ujenzi, teknolojia ya habari na mawasiliano, utalii na huduma za ukarimu.

Maadhimisho ya “Juma la Elimu ya Watu Wazima” linatarajiwa kufikia tamati Ijumaa, Oktoba 13 mwaka huu huku idadi ya watu wazima wanaojua kusoma na kuandika ikitajwa kuongezeka.



Wadau mbalimbali wa masuala ya Elimu wakipata Elimu kwenye banda la Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) katika maonesho ya Juma la Elimu ya Watu Wazima yanayoendelea Wilayani Kibaha, mkoani Pwani. Maonesho hayo yameanza Octoba 9 na yatafungwa rasmi Octoba 13, 2023
Share:

MRADI KITUO CHA KUPOZA UMEME CHALINZE WAFIKIA ASILIMIA 84.3


Na Mwandishi wetu,Pwani.

*Asisitiza Watanzania wanataka umeme*

*Atoa Pongezi kwa wafanyakazi kwenye mradi huo

*TANESCO wapongezwa kwa hatua ya ujenzi*

Mradi wa ujenzi wa Kituo cha Kupoza Umeme wa Msongo wa kilovoti 400/220/132/33 wa kituo cha Chalinze umefikia asilimia 84.3 na hivyo kuleta matumaini ya kuboresha hali ya upatikanaji wa umeme. 

Hayo yameelezwa leo Oktoba 12, 2023 na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt. Doto Biteko alipotembelea na kuzungumza na wafanyakazi wa  kituo hicho cha Chalinze Mkoani Pwani, kujionea maendeleo ya ujenzi wa mradi huo. 

"kwa sasa  ujenzi umefikia asilimia. 84.3 na unatarajiwa kukamilika ifikapo tarehe 31 Disemba, 2023. Mradi huu unakwenda kupunguza changamoto ya umeme kwa kiasi kikubwa hususan katika mkoa huu wa Pwani," amesema Dkt. Biteko.

Ameongeza kuwa, mara baada ya Mradi huo kukamilika, kituo hicho kitakuwa na uwezo wa kupokea Megawatt 2115 kutoka katika Bwawa la kuzalisha Umeme wa Maji la Julius Nyerere na kitasambaza Megawati 850 kwenye mikoa ya Morogoro, Dar es Salaam na Pwani na kuimarisha hali ya upatikanaji umeme katika mikoa hiyo. 

Akizungumza na wafanyakazi wanaofanya kazi katika mradi huo amewataka wafanye kazi kwa bidii kwa kuwa Serikali imewapa ushirikiano ili mradi huo ukamilike kwa wakati. 

Meneja wa Mradi wa kituo hicho Mhandisi Newton Livingstone Mwakifwamba amesema kuwa Serikali imetoa ushirikiano mkubwa katika utekelezaji hususan katika mazingira mazuri ya wafanyakazi. Amesema mradi huo utakamilika kwa muda uliopangwa ifikapo mwezi Desemba 2023.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge amesema toka kuanza kwa mradi huo hakuna changamoto iliyojitokeza kukwamisha mradi huo. Amempongeza Dkt. Biteko kwa kutembelea mradi huo kujionea maendeleo yake.

Naye, Mbunge wa Jimbo la Chalinze Mhe. Ridhiwani Kikwete ambaye ni Naibu Waziri Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora amesema kuwa, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya kazi kubwa katika utekelezaji wa mradi huo na kusisitiza kuwa mradi utakapokamilika utakua ni msaada mkubwa wa mkoa wa Pwani.

Mradi huo ulianza rasmi tarehe 6 Septemba, 2021 ambapo kazi za ujenzi zilianza tarehe  11 Oktoba, 2021 na unahusisha ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme kutoka JNHPP hadi Chalinze pamoja na kituo cha kupoza umeme na kusafirisha umeme kuelekea mikoa ya kaskazini kwa kuingizwa Kenya Gridi ya Taifa.

Ziara hiyo ilihudhuriwa na  Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Mipango na Uwekezaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Decklan Mhaiki, Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Mhe. Halima Okash na Viongozi Mbalimbali wa Chama cha Mapinduzi mkoa wa Pwani na Watumishi wa mradi huo

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger