Sunday, 8 October 2023

BANDOLA SALUMU ACHANGIA SHILINGI MILIONI 1000,000 UJENZI WA MADRASA NDEMBEZI SHINYANGA

Katibu wa Elimu , Malezi na Mazingira Jumuiya ya Wazazi CCM Mkoa wa Shinyanga Mhe. Bandola Salum akichangia ujenzi wa madrasa Ndembezi.

Na Mwandishi wetu Malunde 1 Blog Shinyanga

Katibu wa Elimu , Malezi na Mazingira Jumuiya ya Wazazi CCM Mkoa wa Shinyanga Mhe. Bandola Salum amechangia kiasi cha shilingi milioni moja kwa ajili ya ujenzi wa jengo la madrasa ,Jengo linalo jengwa katika mtaa wa Mabambasi kata ya Ndembezi Halmashauri ya  Manispaa ya Shinyanga.

Bandola ametoa mchango huo katika  harambee ya kuchangia ujenzi wa jengo la madrasa ikiwa nisehemu ya kuandaa mazingira mazuri ya kuwafundishia watoto elimu ya dini.

Pia Bandola amewasii wadau wengine wamaendeleo kujitoa kuchangia ujenzi wa jengo hilo ili liweze kukamilika na  watoto wapate sehemu ya kujifunzia maandiko matakatifu.

Katika Harambee hiyo zaidi ya Shilingi Milioni 7 zimechangwa na waumini pamoja na wadau mbalimbali kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa jengo hilo ambalo kwa sasa lipo usawa wa linta.
Katibu wa Elimu , Malezi na Mazingira Jumuiya ya Wazazi CCM Mkoa wa Shinyanga Mhe. Bandola Salum akichangia ujenzi wa madrasa Ndembezi.

Shekh MSafari Kitumbo akiwa na katibu wa Elimu , Malezi na Mazingira Jumuiya ya Wazazi CCM Mkoa wa Shinyanga Mhe. Bandola Salum wakichangia ujenzi wa madrasa Ndembezi. 

Mfanya biashara Rajabu Moshi akishiriki katika harambee ya kuchangia ujenzi wa Madrasa Ndembezi.
Shaban Abdalla akishiriki katika harambee ya kuchangia ujenzi wa Madrasa Ndembezi.

Share:

KAIRUKI ATAJA TAREHE ZA ONESHO LA SITE 2024

Na John Mapepele

Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Angellah Kairuki ametangaza tarehe ya maonesho ya nane ya Swahili International Tourism Expo - S!TE, 2024 kuwa ni Oktoba 11-13 na kuwataka waandaaji kuyaboresha zaidi ili kupata washiriki wengi kutoka sehemu mbalimbali duniani.

Mhe. Kairuki ametoa kauli hiyo leo Oktoba 8,2023 katika siku ya mwisho ya Maonesho ya Saba ya Swahili International Tourism Expo- S!TE 2023 wakati akifunga maonesho hayo jijini Dar es Salaam.

Amewashukuru wadau wote walioshiriki kwenye maonesho yam waka huu ambapo amesema bila ushiriki wao lisingeweza kufanyika kwa kiwango na ubora mkubwa kama lilivyofanyika.

Ameipongeza Mamlaka ya Wanyamapori Tanzania (TAWA) kwa kupamba maonesho haya kwa kuandaa bustani ya wanyama hai pori ambayo imekuwa kivutio kikubwa kwa watu waliotembelea.

Aidha amewaomba wadau kutoa maoni kuhusu maonesho ya mwaka huu ili yasaidie kuboresha maonesho ya mwakani na kuyafaya kuwa ya kimataifa.

“Maboresho haya yatatujenga na kutusaidia kutuingiza katika maonesho makubwa ya kimataifa kama vile world tourism Market.” Amefafanua Mhe. Kairuki

Awali Mhe. Kairuki alisema pamoja na kazi kubwa ya kuboresha miundombinu iliyofanywa na kusaidia kuleta watalii pia alifafanua kuwa ongezeko kubwa la watalii nchini limetokana na kazi nzuri iliyofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kupitia filamu ya “The Royal Tour”. Filamu hii ilionyeshwa katika vituo vingi vya televisheni vinavyotambulika nchini Marekani na kwingineko duniani ili kutangaza vivutio vya utalii vya Tanzania.
Share:

SERIKALI KUJENGA MELI MPYA YA MIZIGO KUIONGEZEA UWEZO BANDARI YA KAREMA

Serikali inakusudia kujenga Meli mpya ya Mizigo, Barabara ya Lami na Reli ili kuwezesha Bandari ya Karema iliyopo Wilaya ya Tanganyika Mkoani Katavi, iliyokamilika Ujenzi wake kwa Asilimia 100, kufanya kazi kwa uwezo wake wote.

Ahadi hiyo ya Serikali imetolewa na Waziri wa Uchukuzi Mhe. Prof. Makame Mnyaa Mbarawa alipotembelea Bandari hiyo Jumapili Oktoba 08 2023.

“Nimefurahi kuona Bandari hii nzuri sana, yenye miundombinu ya kisasa na nafasi ya kutoa huduma bora za kibandari kwa Wananchi na Wafanyabiashara wa Nchi za Tanzania, Zambia na Congo DRC”. Amesema Waziri Prof. Mbarawa.

Mhe.Waziri amesema, ili uwekezaji wa Serikali wa shilingi Bilioni 47.9 uweze kuleta tija, ni lazima ipatikane Meli kubwa ya Mizigo sambamba na ujenzi wa Barabara ya Lami na Reli km. 110 kutoka Mpanda hadi Karema.

Kwa Upande wake Mbunge wa Mpanda Vijijini ambae pia na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu Mhe. Moshi Selemani Kakoso amesema, Wananchi wa Mikoa ya Katavi, Rukwa na Kigoma wanamshukuru Mhe.Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa mradi mkubwa wa Bandari ya kimkakati ya Karema ambayo itainua Uchumi wa Mikoa hiyo kwa kiasi kikubwa ikiwa ni pamoja na kutoa fursa za Ajira kwa Wananchi.

Kwa upande wake Meneja wa Bandari za Ziwa Tanganyika Bw. Edward Mabula amesema, tangu kuanza kutumika kwa Bandari ya Karema tarehe 01.09.2022, Abiria 4900 na Tani 1500 za mizigo zimehudumiwa.

Tarehe 11 Oktoba 2023, Serikali kupitia Wizara ya Uchukuzi itasaini Mikataba ya Ujenzi wa Meli mbili za Mizigo zitakazotoa huduma katika Maziwa Victoria na Tanganyika sanjari na Mktaba wa ujenzi wa Karakana ya Meli. Hafla ya utiaji saini huo inafanyika Mkoani Kigoma.

Share:

SERIKALI KUSHIRIKIANA NA WADAU KUKUBILIANA NA CHANGAMOTO YA AFYA YA AKILI

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Prof. Joyce Ndalichako, akiwahutubia wanamichezo walioshiriki katika Bonanza la Waajiri lililoandaliwa na Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) na kufanyika katika Viwanja vya Leaders jijini Dar es Salaam.

*******************

Na Mwandishi Wetu

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imejipanga kushirikiana na wadau mbali mbali kukabiliana na changamoto ya afya ya akili ambayo inawakumba watanzania wengi kwasasa hususan kwenye maeneo ya kazi.

Mpango huo wa serikali umewekwa wazi na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Prof. Joyce Ndalichako, alipokuwa akiwahutubia wanamichezo walioshiriki katika Bonanza la Waajiri lililoandaliwa na Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) na kufanyika katika Viwanja vya Leaders jijini Dar es Salaam.

Amesema serikali itaendelea kushirikiana kikamilifu na wadau kuweka mipango ya kisera na kuimarisha miundombinu ya utoaji huduma kwa wananchi ikiwa ni pamoja na kujenga vituo vya afya nchi nzima na kuongeza watalam wa afya ya akili kwenye vituo hivyo.

“Ninafahamu licha ya uwepo wa changamoto ya afya ya akili, wafanyakazi katika maeneo yao ya kazi wamekuwa wakikabiliwa na tishio la magonjwa yasiyoambukiza kama vile, saratani, magonjwa ya moyo na kisukari. Magonjwa haya kwa kiasi kikubwa yamekuwa yanasababishwa na mtindo wa maisha tunayoishi sambamba na kutokuwa na tabia ya kufanya mazoezi ya viungo vya miili yetu,” ameeleza Waziri Ndalichako na kuongeza:

“Hivyo niwaombe sana tuwekeze katika afya zetu kwa kufuata mitindo mizuri ya afya ikiwemo kula milo kamili na kufuata ushauri wa wataalamu wetu wa afya. Niwahimize Waajiri kuendelea kuwekeza katika michezo na program mbalimbali zinazojenga tabia ya kufanya mazoezi ya viungo.”

Akimkaribisha Waziri katika tukio hilo, Katibu Mkuu katika Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mhandisi Cyprian Luhemeja, pamoja na kuwapongeza ATE kwa kuandaa Bonanza hilo, amesema:

“Bonanza hili ni changamoto kwetu kama Wizara yenye dhamana ya masuala ya Ajira na Vijana ambapo ndio tulipaswa kuandaa vitu kama hivi hivyo nasi tutakwenda kujipanga na kuona ni kwa namna gani tutaweza kuwa na matukio kama haya kwa lengo la kuwaendeleza vijana katika nchi yetu.”

Akizungumza katika bonanza hilo kwa niaba ya Taasisi chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA), Bi. Khadija Mwenda, amesema kutokana na ukubwa wa changamoto ya magonjwa yasiyo ambukiza miongoni mwa waajiri na wafanyakazi kwasasa ni wakati mwafaka kwa wadau na serikali kushirikiana katika kushughulikia changamoto hiyo.

“Kwa mujibu wa takwimu tulizozikusanya kwenye maeneo ya kazi kwa mwaka wa fedha 2022/2023 jumla ya wafanyakazi 350,000 walipimwa afya na OSHA ambapo asilimia 40 ya idadi hiyo walikuwa na uzito uliozidi wastani, hali inayowaweka katika hatari ya kupata magonjwa ya kuambukiza ikiwemo kisukari, shinikizo la juu la damu na saratani,” amesema Bi. Mwenda.

Kwa upande wake Afisa Mtendaji Mkuu wa ATE, Bi. Suzanne Ndomba-Doran, amesema ATE wameendelea kushirikiana na OSHA kutoa elimu kwa waajiri kupitia vikao vya wadau kuhusiana na masuala ya usalama na afya ili kuongeza tija katika uzalishaji.

“Bonanza la mwaka huu limebeba Kauli Mbiu ni: “Kuimarisha Afya ya Akili ili Kuongeza Tija Mahali pa Kazi”, lengo ni kuendelea kuhamasisha umuhimu wa kuimarisha afya ya akili mahali pa kazi na kuibua mjadala. Mazingira salama na yenye afya kazini yanapelekea kuwa na wafanyakazi wenye afya njema ambao ndio msingi mkuu wa uzalishaji mahali pa kazi. Kwahiyo sisi tumeendelea kufanya hilo kwa vitendo ambapo hivi karibuni tumeshirikiana na OSHA kufanya vikao 10 vya kisekta kwa lengo la kutoa elimu kwa wadau pamoja na kusikiliza na kutatua changamoto zao kuhusiana na huduma zetu,” alieleza Mtendaji Mkuu wa ATE.
Mtendaji Mkuu wa OSHA, Bi. Khadija Mwenda, akitoa salamu kwa niaba ya Taasisi chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu katika Bonanza la Waajiri lililofanyika Viwanja vya Leaders Dar es Salaam.
Afisa Mtendaji Mkuu wa ATE, Bi. Suzanne Ndomba-Doran, akiwatambulisha wageni waliohudhuria Bonanza la Waajiri kwa mwaka 2023 katika Viwanja vya Leaders Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA), Bw. Herry Mkunda, akiwasilisha salamu za wafanyakazi ka katika Bonanza la Waajiri lililofanyika Viwanja vya Leaders Dar es Salaam.
Timu za mpira wa pete kutoka makampuni mbali mbali zikishiriki michezo katika Bonanza la Waajiri lililofanyika Viwanja vya Leaders Dar es Salaam.
Timu ya mpira wa miguu ya OSHA ikichuana na timu ya Kampuni ya Niajiri katika michezo ya Bonanza la Waajiri katika Viwanja vya Leaders Dar es Salaam.
Mtendaji Mkuu wa OSHA, Bi.Khadija Mwenda, akionesha cheti cha shukrani alichokabidhiwa na Mgeni Rasmi baada ya Taasisi yake kudhamini Bonanza la Waajiri lililoandaliwa na ATE.
Katibu Mkuu katika Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mhandisi Cyprian Luhemeja, akimkaribisha Waziri Ndalichako kuzungumza na wanamichezo katika Bonanza la Waajiri ambapo Waziri huyo alikuwa Mgeni Rasmi.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Prof. Joyce Ndalichako, akipiga shuti mpira kuashiria kuzindua michezo katika Bonanza la Waajiri lililoandaliwa na Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) na kufanyika katika Viwanja vya Leaders jijini Dar es Salaam.
Share:

JE UNGEPENDA KUJIUNGA NA CHAMA CHA WAANDISHI WA HABARI VIJIJINI TANZANIA 'RUJAT'?? MAELEKEZO HAYA HAPA

Bofya <<Hapa>> Kujaza Fomu ya kujiunga na Chama cha Waandishi wa Habari Vijijini (The Rural Journalists Association of Tanzania). RUJAT imesajiliwa kwa mujibu wa sheria za usajili wa vyama vya hiyari chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAPILI OKTOBA 8,2023

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive

Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger