Friday, 25 August 2023

UKUNGU KUZALISHA MAJI SAFI NA SALAMA MBULU



Mkuu wa wilaya ya Mbulu Kheri James ameongoza msafara wa kukagua mradi wa kuvuna ukungu na maji uliopo mkoani Manyara wilaya ya Mbulu.

Ziara hiyo ilifanyika Leo Agost 23,2023 ikiongozwa na mkuu wa wilaya akiambatana na wakurugenzi, wataalamu wa mradi pamoja na watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Mbulu na Mbulu mji.

Mkuu wa Wilaya Kheri alisema kuwa wilaya ya Mbulu ni miongoni mwa wilaya ambayo inanufaika na mradi wa uvunaji wa maji kupitia ukungu.

"Kama ilivyotaratibu zetu viongozi inabidi kujengewa uwezo ni namna gani mradi huu utafanyika na mazingira ya mradi yatakuwaje, kwa busara ya kawaida Leo viongozi wote na watumishi kwa uwakilishi tumeona tufike hapa Babati ambapo mradi huu unafanya kazi vizuri, kwa tija kubwa sana na unasaidia upatikanaji wa maji safi kwa ajili ya wanafinzi wa shule ya sekondari Qameyu,matumizi ya laboratory na matumizi mengine ambayo shule itahitaji." Alisema Mkuu wa Wilaya.

Mheshiwa Mkuu wa Wilaya aliendelea kusema kuwa jitihada kubwa zinafanywa na serikali katika kuhakikisha maji safi na Salama yanapatikana, jitihada hizi zinafanywa na serikali pamoja na wadau, na wadau wanaongeza nguvu kwa sababu kubwa moja, hakuna namna tutaleta maendeleo ya watu wetu bila maji safi na Salama.

"Mradi sasa unapokwenda kuanza tumeshajifunza baadhi ya mambo ya kuanza nayo wakati wa kuanza, lakini mambo ya kufanya wakati wa mradi unaendelea, na mambo ya kufanya ili kuulinda mradi ili kuleta tija inayokusudiwa." Alisema Kheri James

Kwa upande wa Professor Karoli Njau wa Chuo Kikuu Cha Nelson Mandela ambae ni Mshauri mwelekezi wa mradi alisema kuwa wanatumia neti kudaka maji yaliyo kwenye ukungu.Ambapo alizungumza kuwa ukungu una majimaji na unaposhuka chini sana unaweza kutumia teknolojia hiyo iliyowekwa ambayo tunaiona.

"Hii ni teknolojia mpya sana kwa ajili ya kupata maji.Na hii teknolojia ya hizi neti inadaka ule ukungu na ule ukungu unaelekezwa mpaka unafika sehemu za chini ambazo zinakusanya na yale maji yanakusanywa pamoja yanaingizwa kwenye matenki." Alisema Prof. Njau.

Manager wa mradi wa Catching Clouds Dennis Wolter kutoka Ujerumani alisema anashukuru kwa mapokezi makubwa ambayo hakuyategemea, alisema wanakazi kubwa ambayo ipo mbele yao lakini wamejidhatiti na wana shauku kubwa kuifanya.

" Tuna uelewa kwamba tutakutana na changamoto lakini tunavyoona viongozi mnajitoa ni alama kubwa kwamba tunaweza kufanya kazi hii pamoja na tutahakikisha kwa ubora wetu kwamba mradi huu utakuwa wenye tija kubwa kwa jamii.

Kwa upande wa Mkurugenzi mtendaji wa Wilaya ya Mbulu Ndugu, Abubakar Kuuli alihitimisha kwa kutoa shukrani kwa Mkuu wa Wilaya kwa niaba ya watumishi pamoja na wananchi wote wa Halmashauri ya wilaya ya Mbulu, na kueleza kuwa miradi hiyo ni mizuri sana, ule wa kuvuna ukungu na wa kuvuna maji ya mvua. Amewakaribisha wawekezaji na ameahidi kutoa ushirikiano mzuri pale utakapohitajika.


Share:

Thursday, 24 August 2023

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO IJUMAA AGOSTI 25,2023































Share:

MERIDIANBET KASINO MFAHAMU CLEOPATRA MTAWALA WA MISRI!!

 
Je, ulikosa simulizi za kale kuhusu Misri? Ikiwa ni kweli, tuna jambo sahihi kwa ajili yako. Safari hii, kiongozi aliyejipatia umaarufu nchini Misri, Bi Cleopatra, anachukua jukumu kuu. Ni wewe tu kufurahia mzuka huu kwenye kasino ya mtandaoni ya Meridianbet.

 

Cleos Gold ni sloti ya kasino ya mtandaoni kutoka kwa mtoa huduma Platiplus Casino. Mchezo huu wa sloti una bonasi kadhaa ambazo utafurahia. Kuna alama za wild za kuvutia na pia kuna aina tatu ya mizunguko ya bure.

 

Jinsi ya Kucheza Cleos Gold

 

Cleos Gold ni mchezo wa sloti unaopatikana kasino ya mtandaoni, mchezo wenye nguzo tano zilizopangwa katika safu tatu na mistari 20 ya malipo. Ili kupata ushindi wowote,

 

Unahitaji kupata alama tatu au zaidi zinazofanana kwenye mstari wa malipo.

Mchanganyiko wowote wa ushindi huhesabiwa pekee kutoka kushoto kwenda kulia kuanzia nguzo ya kwanza kushoto.

 

Unaweza kupata ushindi mmoja kwa kila mstari wa malipo. Ikiwa una mchanganyiko wa kushinda zaidi kwenye mstari mmoja wa malipo, utalipwa mchanganyiko wenye thamani kubwa.

 

Jumla ya ushindi inawezekana ikiwa utaziunganisha kwenye mistari kadhaa wakati huo huo.

 

Kubonyeza kitufe cha Line Bet kinafungua menyu ambapo utaweza kuweka kiasi cha dau kwa kila mstari wa malipo. Utaweza kuona kiasi cha dau kwa mzunguko katika uwanja wa Jumla ya Dau.

 

Pia kuna chaguo la Kiotomatiki, unaloweza kuanzisha wakati wowote. Kupitia chaguo hili unaweza kuweka hadi mizunguko 100. Kupitia chaguo hili, unaweza kuweka kikomo kwa kupoteza na kwa faida iliyopatikana.

 

Ikiwa unapenda mchezo wa haraka zaidi, unaweza kuamsha mzunguko wa haraka kwa kubofya uwanja wenye picha ya mshale. Unaweza kurekebisha kiwango cha sauti kwenye kona kushoto chini ya nguzo.

 

Alama za mchezo wa Cleos Gold

 

Linapokuja suala la alama za mchezo huu was loti ya kasino mtandaoni, alama za karata zinaleta malipo ya chini zaidi: 10JQK na A. Zinagawanywa katika vikundi viwili, hivyo K na A zinakuletea malipo kidogo zaidi.

 

Baada ya hapo, inakuja alama ya msalaba, na mara baada yake utaona alama ya jicho linaloleta malipo makubwa zaidi.

 

Alama ifuatayo ni alama ya ndege ndiye alama inayofuata kwa thamani ya malipo. Tano za alama hizi katika mchanganyiko wa ushindi zitakuletea mara 750 ya dau lako.

 

Utakutana na alama ya Anubis inayoleta malipo makubwa zaidi. Ikiwa utashikiza alama tano za hizi kwenye mstari wa malipo utashinda mara 800 ya dau lako.

 

Alama ya Scarab ni mojawapo ya alama za msingi zenye thamani kubwa. Ikiwa unapatanisha alama tano za hizi katika mfuatano wa kushinda, utashinda mara 900 ya dau lako.

 

Alama ya msingi yenye thamani kubwa zaidi ya mchezo ni Cleopatra mwenyewe. Tano za alama hizi kwenye mstari wa malipo zitakuletea mara 1,000 ya dau lako.

 

Alama ya Joker inawakilishwa na piramidi inayobeba nembo ya Wild. Inachukua nafasi ya alama zote, isipokuwa nembo ya scatter, na kuwasaidia kuunda mchanganyiko wa kushinda.

 

Inaonekana kwenye nguzo ya pili, ya tatu, ya nne, na ya tano.

 

Michezo ya bonasi

 

Nembo ya scatter inawakilishwa na farao inayobeba nembo ya bonasi. Inaonekana kwenye nguzo ya pili, ya tatu, na ya nne. Tatu za alama hizi kwenye fremu zitakupa mizunguko ya bure.

 

Unachagua moja kati ya aina tatu zifuatazo za mizunguko ya bure:

Mizunguko mitano ya bure na alama wild zinazobaki mahali hadi mwisho wa mchezo wa bonasi.

 

Mizunguko 10 ya bure na alama za wild zinazopo ongezeka, alama wild inaongezeka kwenye nguzo nzima kila inapoonekana. Mizunguko 15 ya bure na alama ya wild za jumla.

 

NB: Ukijisajili Meridianbet unapewa bonasi ya mizunguko ya bure kucheza michezo ya kasino ya mtandaoni. Jisajili na Cheza.

 



Share:

MKUU WA WILAYA AWAHIMIZA WANA-BUSEGA KUTOA MAONI KWA UWAZI BEI ZA MAJI





Mkuu wa Wilaya ya Busega, Mhe. Anna Joram Gidarya, amewataka wananchi wa Wilaya ya Busega kutoa maoni kwa uhuru kuhusu ombi la kurekebisha bei za maji na usafi wa mazingira kutoka Mamlaka ya Maji Busega wakati wa mkutano wa kutafuta maoni uliofanyika mjini Lamadi, Wilayani Busega, leo 24 Agosti 2023.

“Serikali imewaamini EWURA na kuwatuma hapa kupokea maoni yetu wana-Busega  ili tuweze kupata bei za huduma ya maji na kuilinda Mamlaka yetu isife, hivyo niwasihi sana mtoe maoni kwa uwazi na bila woga,” alisema. 

Mhe  Gidarya ameitaka EWURA kuendelea kuisimamia BUSEWASA kwa umakini, kwani Serikali inaamini katika utendaji mahiri wa mdhibiti  ili kuhakikisha huduma za maji bora zinaendelea kupatikana na kwa wananchi wa Busega.

Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa EWURA katika mkutano huo, Bw. George Mhina ambaye pia Meneja wa EWURA Kanda ya Ziwa, alisema EWURA itaendelea kutekeleza wajibu wake kwa mujibu wa sheria.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji Busega, Mha. Romanus Thomas, alieleza sababu za kuomba marekebisho ya  bei za maji ni kuongeza mtandao wa usambazaji huduma za majisafi na usafi wa mazingira, kuongezeka gharama za uendeshaji ikiwamo gharama  za umeme na gharama za kutibu maji.

Mwisho.

Share:

Video Mpya : NTEMI OMABALA - BHABHA

 

Share:

DKT. BITEKO AWATAKA WATUMISHI MADINI MTWARA KUSHIRIKIANA





Waziri wa Madini Dkt. Doto Biteko leo Agosti 24, 2023 ametembelea na kuzungumza na watumishi wa Ofisi ya Madini Mkazi Mkoa wa Mtwara.

Aidha, Dkt.Biteko amekutana na kuzungumza na Uongozi wa Wachimbaji Wadogo wa madini Mkoani Mtwara.



Taarifa rasmi itawasilishwa. Zifuatazo ni baadhi ya picha katika kikao hicho kifupi.

Share:

TAKUKURU YABAINI MADUDU MATENGENEZO BARABARA SHINYANGA


Kaimu Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Shinyanga Mwamba Masanja.


Na Marco Maduhu, SHINYANGA

TAASISI ya kuzuia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Shinyanga, imembana Mkandarasi kutoka Kampuni ya Brampem Global Investment LTD, kurudia matengenezo ya barabara aliyojenga chini ya kiwango, pamoja na kukatwa fedha kutokana na kuchelewesha matengenezo hayo kinyume cha Mkataba, huku ikitatua kero ya ukosefu wa madawa na vifaa tiba zahanati ya Kisuke halmashauri ya Ushetu.


Kaimu Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Shinyanga Mwamba Masanja, amebainisha haya leo Agost 24, 2023 wakati akitoa taarifa kwa vyombo vya habari kwa kipindi cha robo ya Nne ya mwaka wa fedha 2022/2023.


Amesema kwa kipindi hicho walifanya ufuatiliaji wa miradi mbalimbali ikiwamo ya matengenezo ya barabara, zilizopo katika Manispaa ya Shinyanga chini ya usimamizi wa TARURA ili kuona utekelezwaji wa miradi hiyo kama imezingatia ubora na viwango vinavyotakiwa.

Amesema katika ufuatiliaji wa matengenezo ya barabara hizo kwa uboreshaji wa vipande vya barabara katika Kata ya Chamaguha, Ngokolo, Ndembezi, Kambarage na Mwasele, walibaini Mkandarasi kutekeleza ujenzi wa barabara hizo chini ya kiwango.
Kaimu Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Shinyanga Mwamba Masanja,akitoa taarifa kwa waandishi wa habari.


“Mkandarasi huyu kutoka Kampuni ya Brampem Global Investment mbali na uchelewashaji wa ukamilishaji wa mradi, ametekeleza kazi chini ya kiwango kwa kutochonga barabara kwa usahihi, kina chatabaka la kifusi kutofika kiwango na kutoshindiliwa ipasavyo, na uchongaji wa Mitaro isiyoridhisha,”amesema Masanja.


Aidha, amesema Mkandarasi huyo kwa sasa yupo kwenye kipindi cha makato ya fedha ikiwa ni adhabu ya kuchelewesha mradi kwa mujibu wa Mkataba, kwamba alipaswa akamilishe mradi huo Aprili 27 mwaka huu lakini licha ya kuongezewa siku 75 bado mradi huo wa matengenezo ya barabara haukukamilika.


Amesema Takukuru ilimshauri msimamizi wa mradi wa matengezo ya barabara hizo ambaye ni Tarura, imtake Mkandarasi arudie kazi zote alizotekeleza chini ya kiwango ili thamani ya fedha ionekane, na ushauri huo ulifanyiwa kazi na mpaka sasa marekebisho yamefanyika yenye thamani ya Sh.milioni 76 na thamani nzima ya mradi ni Sh.milioni 236.6.
Kaimu Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Shinyanga Mwamba Masanja,akitoa taarifa kwa waandishi wa habari.


Masanja amesema miradi mingine ya maendeleo ambayo waliifuatilia yenye thamani ya Sh.bilioni 5.6 katika Sekta ya Elimu, Maji, Kilimo na Ujenzi. walibaini kuwapo na dosari ndogo ndogo kwenye miradi miwili ya ujenzi wa shule mpya ya msingi Ibadakuli na Shule mpya ya Msingi Igaga na kurekebishwa.


Katika hatua nyingine amesema kupitia Proramu ya Takukuru Rafiki, walipokea malalamiko kutoka kwa wananchi wa Kata ya Kisuke Halmashauri ya Ushetu juu ya ukosefu wa vifaa tiba na madawa katika Zahanati ya Kisuke, na ukosefu wa Maji kwenye vijiji vya Ididi na Mutongi, na kero hizo zilifanyiwa kazi na wananchi kupata huduma.


Amesema kwa upande wa dawati la uchunguzi kwa kipindi hicho walipokea taarifa 35 za malalamiko, zilizohusu rushwa ni 26 na zinatoka katika Sekta mbalimbali, Elimu rushwa 7, Serikali za Mitaa 6,Ardhi 5, Polisi 2, Afya 2, Maji Moja na GPSA Moja, na uchunguzi wa taarifa hizo unaendelea.


Ametoa wito kwa wananchi wa Mkoa wa Shinyanga, kuendela kutoa ushirikiano kwa Taasisi hiyo kwa kutoa taarifa pale wanapoona viashiria vya rushwa au ubadhilifu wa fedha kwenye miradi ya maendeleo ili hatua zichukuliwe.
Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO ALHAMISI AGOSTI 24,2023



























Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger