Monday, 21 August 2023

TANZANIA KUWA KITOVU CHA UCHAKATAJI MADINI BARANI AFRIKA - DKT. KIRUSWA






#Dkt. Kiruswa Afungua Maonesho ya Madini na Fursa za Uwekezaji Lindi

Ruangwa - Lindi

Imeelezwa kuwa, Serikali inaandaa Mkakati wa kuwezesha uongezaji thamani madini kwa lengo la kuzalisha bidhaa mbalimbali zinazotokana na madini utakaopelekea Tanzania kuwa kitovu cha uchakataji madini kwa lengo la kuvutia wawekezaji wa ndani na nje.

Hayo yamebainishwa na Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa wakati akifungua rasmi  Maonesho ya Madini na Fursa za Uwekezaji yanayokwenda sanjari na Kongamano la Wadau wa Madini ya Chumvi Mkoani Lindi leo Agosti 21, 2023

"Serikali inaendelea kuhimiza uongezaji thamani madini nchini ikiwa ni pamoja na uzalishaji wa bidhaa zinazotokana na madini. Katika kuhakikisha kuwa kusudio hilo linafikiwa, nawaomba wawekezaji kuendelea kuwekeza katika viwanda vya uongezaji thamani madini," amesema Dkt. Kiruswa
 
Aidha amesema, Serikali imeendelea kuweka mazingira wezeshi ya uwekezaji na biashara nchini ili kuvutia mitaji kutoka ndani na nje ya nchi, amesema katika kutekeleza azma hiyo, Serikali imeendelea kufanya mapitio ya Sera mbalimbali zinazosimamia Uwekezaji, Viwanda na Biashara nchini.

"Ninapenda kutumia nafasi hii kuwashukuru wadau wote wakiwemo washirika wetu wa Maendeleo wa ndani na nje ya nchi, napenda pia kuwashukuru washiriki wote mliotoka sehemu mbalimbali mliojumuika na wananchi wa Mkoa wa Lindi hii leo, hakika uwepo wenu unadhihirisha umuhimu wa maonesho haya kwamba sio tu kwa watu wa Lindi bali ni dhamira ya Serikali yetu ambayo ina nia kubwa ya kuendelea kuona Mkoa wa Lindi na Mikoa mingine ya Ukanda huu wa Kusini inafunguliwa kiuchumi," amesema Dkt. Kiruswa

Vile vile, Serikali itaendeleza jitihada za kujenga na kuimarisha misingi thabiti ya uchumi kwa kuvutia wawekezaji na ujenzi wa viwanda kama ilivyobainishwa katika Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Lindi Zainabu Telack amesema kuwa kupitia maonesho haya wawekezaji wanajionea fursa mbalimbali za rasilimali madini ikiwa pamoja na kutangaza fursa nyingine za kiuchumi zinazopatikana mkoani Lindi.

Kaulimbiu ya maonesho hayo ni *"Wekeza Lindi kwa Ukuaji wa Uchumi wa Maendeleo ya Jamii"*. Maonesho hayo yamehudhuriwa na wadau mbalimbali wa Sekta ya Madini waliopo ndani na nje ya nchi yanayoendelea hadi Agosti 26 mkoani Lindi.
Share:

MIGODI MIKUBWA YENYE UBIA NA SERIKALI YACHANGIA SHILINGI TRILIONI 1.53 KUFIKIA JUNI, 2023







 
*Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge Nishati, Madini ataka STAMICO iongezwe nguvu*

*Katibu Mkuu Mahimbali aeleza Mipango Kabambe kuendeleza Sekta ya Madini, aeleza Miradi Mingine Mbioni kupewa Leseni*

*Dodoma*

Katibu Mkuu Wizara ya Madini Kheri Mahimbali ameieleza Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini kuwa hadi kufikia Juni, 2023 miradi ya uchimbaji mkubwa wa madini ambayo Serikali ina hisa imechangia mapato ya Serikali ya jumla ya Shilingi *Trilioni 1.53* ambayo yametokana na tozo na kodi mbalimbali.

Mahimbali ameyasema hayo Agosti 21, 2023 jijini Dodoma kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini wakati akiwasilisha taarifa kuhusu hali ya uendeshaji wa migodi ambayo Serikali ina hisa na mkakati wa Serikali wa kuhakikisha inahuisha mikataba katika migodi mikubwa ili iendane na mabadiliko yaliyofanyika kwenye Sheria ya Madini pamoja na Sheria ya Mamlaka ya Nchi kuhusiana na Umiliki wa Maliasili, 2017.

Ameongeza kwamba, mbali ya kuchangia kodi, migodi hiyo imewezesha kutoa ajira zipatazo *3,110* kwa  watanzania na kuchangia kiasi cha shilingi *21, 045, 546,929.42* ikiwa ni mchango  kutokana na Wajibu wa Kampuni kwa Jamii (CSR) pamoja na kutumia jumla ya shilingi *2, 893,423, 283, 326.05* kwa ajili ya ununuzi wa bidhaa na huduma nchini.

Ameitaja migodi hiyo  kuwa ni  North Mara, Buzwagi, na Bulyanhulu inayochimba madini ya dhahabu  kupitia   Kampuni ya Twiga Minerals Corporation Limited , kampuni ya Tembo Nickel Corporation Limited inayojihusisha na uchimbaji wa madini ya nikeli katika eneo la Kabanga wilayani Ngala, Faru Graphite Corporation Limited itakayojihusisha na uchimbaji wa madini ya Kinywe wilayani Mahenge na Mamba Minerals inayojihusisha na uchimbaji wa madini adimu yaani ( Rare Earth  Elements ) katika eneo la Nguala mkoa wa Songwe.

‘’Mhe. Mwenyekiti migodi mingine yenye hisa na Serikali iliyochangia mapato hayo ni kampuni ya Sotta Mining Limited kupitia mgodi wa Nyanzaga uliopo Wilayani Sengerema, na kampuni ya Williamson Diamond Limited (WDL) kupitia mgodi wa  Mwadui uliopo Mkoa wa Shinyanga.

Aidha, Mahimbali ameieleza kamati hiyo  kwamba,  katika kuhakikisha Serikali inanufaika  na uwekezaji katika Sekta ya Madini nchini na kusimamia utekelezaji kulingana na matakwa  ya Sheria  ya Madini,  Serikali inatarajia kutoa leseni za uchimbaji wa madini kwa  kampuni za Duma TanzGraphite na Nyati Minerals Sand Limited zitakazofanya uchimbaji mkubwa pamoja na Kudu Graphite Limited  itakayofanya uchimbaji wa Kati na kuongeza kwamba, Serikali itakuwa na umiliki wa hisa za asilimia 16 kwa kila mradi.

Katika hatua nyingine, Katibu Mkuu Mahimbali ameieleza Kamati hiyo mikakati ya Wizara kuiendeleza  Sekta ya Madini ikiwa ni pamoja na kuhakikisha inaifungamanisha Sekta ya Madini na Sekta nyinigne za kiuchumi na kuzitaja baadhi kuwa ni Kilimo ambapo rasilimali madini hutumika katika uzalishaji wa mbolea kwa matumizi ya kilimo. Aidha, ametumia fursa hiyo  kuishukuru kamati hiyo kutokana na ushauri na maelekezo  yake ambayo yameiwezesha  Sekta ya Madini kuendelea kufanya vizuri ikiwemo kupata tuzo tatu  zilizotolewa na  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Agosti  Agosti, 2023 kwa taasisi zilizofanya vizuri ambapo  Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) na Kampuni ya Twiga zilipata ushindi wa kwanza kupitia vipengele mbalimbali .

Akijibu hoja iliyotolewa na Kamati kupitia kwa Mwenyekiti wa Kamati hiyo  Dunstan Kitandula na wajumbe wengine la kuiwezesha STAMICO kusimama kwa niaba ya Serikali katika kampuni za uchimbaji mkubwa na wa kati  wa madini badala ya kuanzisha kampuni nyingine tanzu,  amesema kuwa Serikali imeyachukua maelekezo hayo na pia  wizara ina mpango  wa kuiwezesha STAMICO kuwa na ushindani na kampuni kubwa za nje ikiwemo kuiwezesha kuvuka mipaka ya ndani na kuwekeza katika mataifa mbalimbali  barani Afrika.

‘’ Mhe. Mwenyekiti suala hili litafuatiliwa kwa umakini na kwa kuzingatia taratibu, maelekezo haya ni dhabiti na yataongeza tija kwenye Sekta ya Madini.’’amesema Mahimbali.

Kuhusu suala la kuhakikisha miradi ya madini inatekelezwa hususan ile inayotarajia kuanza utekelezaji, amesema Wizara imeweka mazingira ambayo yatawasaidia wawekezaji kuweza kufanya shughulli zao kikamilifu kulingana na muda uliopangwa.

Akizungumza katika kamati  hiyo, Mwenyekiti Kitandula ameitaka Wizara kuendelea kuwajengea wajumbe wa kamati hiyo uelewa kuhusu shughuli na miradi inayotekelezwa na wizara na wadau ili kupata uelewa wa pamoja na kuiwezesha kamati hiyo kusimamia na kuishauri Sekta ya Madini kikamilifu.
Share:

WAZIRI AWESO AMTEUA BI.NELLY MSUYA KUWA KAIMU MKURUGENZI MTENDAJI MWAUWASA

Share:

MSITU WENYE HELA MERIDIANBET NI KASINO YA JUNGLE SPIN!!

 

Ninakuleta tena kwenye safari isiyoweza kuepukika katikati ya msitu wa mvua. Utapata kuona kila kitu ambacho msitu wa mvua unaweza kukuoa mtonyo mwingi sana, Ili kuongeza uzuri wa mambo, kuna mshangao maalum ambao utaongeza ladha kwenye burudani hii ya kasino ya mtandaoni.

 

Jungle Spin ni mchezo wa kasino ya mtandaoni ambao unatolewa na mtoa huduma Platipus. Katika mchezo huu, kuna aina kadhaa za bonasi. Kuna nembo za mara mbili na mara tatu ambazo zitawashawishi wengi. Kwa bahati nzuri, unaweza kushinda hadi mizunguko 100 ya bure.

 

Sifa Kuu ya Mchezo Huu.

 

Jungle Spin ni kasino ya mtandaoni wa Meridianbet wenye nguzo tano zilizopangwa kwa mistari mitatu na ina mistari 50 ya malipo iliyowekwa. Ili kupata ushindi wowote, lazima uungane nembo tatu au zaidi kwenye mstari wa malipo.

Vivuli vyote vya ushindi huchukuliwa tu kutoka kushoto kwenda kulia, kuanzia nguzo ya kwanza upande wa kushoto.

 

Kwenye mstari mmoja wa malipo, unaweza kupata ushindi mmoja tu. Ikiwa una vivuli vingi vya ushindi kwenye mstari mmoja wa malipo, utalipwa kwa vivuli vyenye thamani kubwa zaidi.

 

Inawezekana kuunganisha ushindi ikiwa unaweka vivuli kwenye mistari mingi ya malipo kwa wakati mmoja.

 

Ndani ya sehemu ya Line Bet, kuna menyu ambayo unachagua thamani ya dau kwa kila mstari wa malipo. Thamani jumla ya dau kwa mzunguko inaonyeshwa kwenye sehemu ya Total Bet.

 

Pia kuna chaguo la kucheza moja kwa moja (Autoplay) ambalo unaweza kuweka wakati wowote. Kupitia chaguo hili, unaweza kuweka mizunguko hadi 100.

 

Ikiwa unapenda mchezo wa haraka na mizunguko ya haraka, unaweza kuamsha mizunguko hiyo kwa kubofya kitufe chenye picha ya mishale miwili.

Unaweza kurekebisha athari za sauti katika kona ya chini kushoto chini ya nguzo.

 

Alama za Jungle Spin

 

Alama za mchezo huu, vivuli vya thamani ndogo zaidi vinalletwa na kadi za kawaida: 10, J, Q, K, na A. Kati yao, K na A vina thamani kubwa kuliko zingine.

 

Nembo zingine za kawaida zinaweza kuonekana kama nembo moja au nembo mara mbili. Kwa hivyo, kuna uwezekano wa kuunda ushindi kutoka kwa nembo 10, yaani nembo tano mara mbili.

 

Chui ndiye nembo inayofuata yenye thamani ya malipo, na malipo sawa yanapewa na sokwe. Kuunda ushindi na nembo kumi kama hizi kwenye mfululizo kutakuletea mara 2,000 zaidi ya thamani yako kwa mstari wa malipo.

 

Kunguru mwekundu na mweupe wanafuata kwa thamani ya malipo, na wanatoa malipo makubwa zaidi. Ikiwa utaunda ushindi na nembo kumi mara mbili kwenye safu, utashinda mara 5,000 zaidi ya thamani yako kwa mstari wa malipo.

 

Hata hivyo, kuna nembo moja maalum inayostahili kutajwa, na hiyo ni kunguru mwenye rangi. Anaweza kuonekana kama nembo moja, nembo mbili, au hata nembo tatu. Ikiwa nembo tano za kunguru wenye rangi mara tatu zitaonekana kwenye mstari wa malipo, utashinda mara 50,000 zaidi ya thamani ya dau lako kwa mstari wa malipo.

 

Tumia fursa hii na pata ushindi mkubwa! Michezo ya Bonasi na Kasino ya mtandaoni ya Meridianbet. Fanya kugusa hapa.

 

Nembo ya Wild imeonyeshwa na nembo ya Jungle Wild. Inachukua nafasi ya nembo zote, isipokuwa nembo za kupandikiza, na inasaidia kuunda ushindi.

Inaonekana kwenye nguzo ya pili, ya tatu, na ya nne.

 

Nembo ya Scatter inawakilishwa na kipepeo na pia inaweza kuonekana kama nembo moja au nembo mbili.

 

Unaweza kuamsha mizunguko ya bure kulingana na sheria zifuatazo:

 

Vitambulisho vitano vya kupandikiza - mizunguko mitano ya bure

Vitambulisho sita vya kupandikiza - mizunguko 10 ya bure

Vitambulisho saba vya kupandikiza - mizunguko 15 ya bure

Vitambulisho nane vya kupandikiza - mizunguko 20 ya bure

Vitambulisho tisa vya kupandikiza - mizunguko 50 ya bure

Vitambulisho kumi vya kupandikiza - mizunguko 100 ya bure

 

Kwa maneno mengine, unaweza kushinda hadi mizunguko 100 ya bure kutoka kwa mzunguko mmoja tu!

 

 

NB: Ukijisajili Meridianbet unapewa bonasi ya mizunguko ya bure kucheza michezo ya kasino ya mtandaoni. Jisajili na Cheza.

 


Share:

MCHENGERWA- ZOEZI LA KUHAMISHA WATU NGORONGORO KUKAMILIKA MACHI 2024


Na John Mapepele

Serikali imesema zoezi la kuhama kwa hiari wananchi wanaoishi kwenye Hifadhi ya Ngorongoro kwenda Msomela mkoani Tanga litakamilika Machi 30 mwakani ili kupisha uhifadhi wa raslimali katika eneo hilo.

Kauli hiyo ameitoa Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mohamed Mchengerwa leo Agosti 21,2023 kwenye kikao baina ya Wizara na Kamati ya kudumu ya Bunge ya Ardhi,Maliasili na Utalii wakati kamati hiyo ikipokea na kujadili taarifa za serikali kuhusu utendaji wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania(TAWA) na utekelezaji wa zoezi la hiari la kuwahamisha wenyeji kutoka ndani ya Hifadhi ya Ngorongoro.

“Naomba kutoa taarifa kwa kamati yako mwenyekiti kuwa taratibu zote za uhamishaji wananchi kwa hiari awamu ya pili kutoka kwenye hifadhi ya Ngorongoro zimekamilika na kwamba Serikali imeshatoa fedha kwa ajilin ya zoezi hilo hivyo zoezi hilo litafanyika kama lilivyopangwa”. Amesisitiza Mhe. Mchengerwa

Amewaelekeza watendaji wote kuhakikisha kuwa wanasimamia zoezi hilo kwa weledi, wakitanguliza uzalendo huku akionya kwa mtendaji yoyote ambaye anakwenda kinyume atachukuliwa hatua za kisheria.


Akizungumzia kuhusu utendaji wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania(TAWA) na namna wizara ilivyojipanga kukabiliana na na changamoto za Wanyama waharibifu Mhe. Mchengerwa amesema wizara yake inakwenda kuwekeza katika teknolojia ya kisasa ili kudhibiti wanyama waharibifu.

Aidha amesema tayari Wizara katika kipindi kifupi imeshafanya marekebisho makubwa ya sheria na kanuni kadhaa za sekta zake zote ili ziendane na hali halisi ya sasa.

Amefafanua kuwa changamoto nyingi zinazoikabili baadhi ya masuala ya sasa ikiwa ni pamoja na wanyama waharibifu kama Tembo ni kutokana na matatizo ambayo yalitengenezwa kwa kufanya jambo moja bila kuzingatia masuala mengine kama mipango ya matumizi bora ya ardhi.

Amemtaka Naibu Katibu Mkuu Kamishna Benedict Wakulyamba ambaye ndiye msimamizi wa uhifadhi katika wizara kuhakikisha changamoto ya wanyama wahalibifu inapata suluhisho la kudumu.

Pia Mhe. Mchengerwa amesema kwa sasa Wizara imeshatoa ridhaa ya wawindaji wenyeji kufanya uwindaji ambapo pia wametoa ridhaa ya kufanya uwekezaji wa zoo za Wanyama.

“Tumeshaandaa block tatu upande wa kaskazini ambazo zitakuwa chini ya Serikali na tunaendelea kutengeneza miundombinu ili iwe bora na kutoa fursa kwa watu kuwinda”. Ameongeza Waziri Mchengerwa

Naye Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe.Timetheo Mzava kwa niaba ya Kamati yake ameipongeza Wizara kwa kazi nzuri inayofanya katika kipindi hiki huku akiitaka kuongeza juhudi za kukabili changamoto zinazowakabili wananchi hususan Wanyama waharibifu.

“Sote tumeona pamoja na kazi nzuri na mikakati mliyojiwekea tunawapongeza sana na tunataka mfanye vizuri zaidi”. Amesisitiza Mhe. Mzava wakati akikifunga kikao hicho

Aidha amesema katika siku za nyuma wizara ilikuwa haifanyi vizuri ukilinganisha na kipindi hiki kwa kuwa ilikuwa inachukuwa muda mrefu katika kufanya maamuzi

“Maamuzi yamekuwa yanachelewa sana, vitu kama vipepeo vya amani, suala la kusafirisha viumbe hai na mambo mengine yamekuwa yakichukua muda mrefu” ameongeza
Share:

SAFARI YA SIAH MALLE KATIKA UHANDISI INAVYOIBUA VIPAJI VIPYA VYA WANAWAKE WENYE NDOTO KUBWA


Siah Malle akitoa tathmini ya miradi ya kiuhandisi iliyobuniwa na wahandisi vijana wa kike katika na Maonesho na Kongamano la 8 la Wanawake Wahandisi Tanzania (TAWECE) yaliyofanyika Zanzibar.

***




Na Mwandishi Wetu

Siah Malle ni mfano mzuri wa mwanamke ambaye amefanikiwa kuvunja dhana iliyojengeka na kuwagawa wanawake na wanaume kwenye uwanja wa taaluma mbalimbali duniani. Safari yake ya kuwa jaji katika Kongamano na Maonesho ya 8 ya Wanawake Wahandisi Tanzania (TAWECE) ni uthibitisho tosha kuwa ari na bidii yake katika tasnia ya uhandisi imezidi kumuinua.



Alipokuwa anakua, Siah alivutiwa na ulimwengu wa sayansi na teknolojia. Kaka yake ambaye ni mhandisi wa ujenzi, alichochea shauku yake katika kuingia kwenye tasnia ya uhandisi na alidhamiria kufuata nyayo zake.



Lakini pia kwa kutiwa moyo na walimu wake, alisoma sayansi na hisabati katika elimu ya sekondari na kufanikiwa kufaulu vizuri katika masomo hayo.



Baadaye Siah aliendelea na elimu yake katika kozi ya uhandisi ngazi ya stashahada ambayo alisoma kwa muda wa miaka mitatu katika Chuo cha Ufundi Arusha.



Mmoja wa walimu wake aliyefahamika kwa jina la John Mbando, alitambua uwezo wake mapema na kumtia moyo katika fani hiyo kisha kumshawishi kuachana na uhandisi wa ujenzi na kubobea katika uhandisi wa mitambo.



Mbando alimshawishi kuwa uhandisi wa mitambo kuwa una manufaa mengi, ikiwa ni pamoja na kuajiriwa, manufaa na kubuni vitu mbalimbali ambavyo vinatatua changamoto au matatizo yanayoikumba jamii.



Hali hiyo ilisababisha mapenzi ya Siah katika uhandisi wa mitambo kuongezeka na alidhamiria kuingia katika taaluma hii.



Baada ya kuhitimu vizuri stashahada yake, Siah alisoma kwa miaka mitatu katika Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya ambako alihitimu Shahada ya Kwanza ya Uhandisi Mitambo na kupata alama zenye wastani wa (GPA) 4.3 na kutunukiwa tuzo ya Mwanafunzi Bora wa Kike aliyehitimu mwaka wa kuhitimu 2019.



Mwalimu wa Siah, Mbando ndiye aliyefanikisha safari muhimu ya mwanadada huyu ambaye sasa ni mhandisi mbobevu.

Hakumfundisha tu ujuzi wa kiufundi wa uhandisi wa mitambo, lakini pia alimjengea dhima nzima ya umuhimu wa kuzingatia maadili, mawasiliano na kufanya kazi kwa pamoja.

Alimhimiza kufuata ndoto zake na kamwe asikate tamaa, hata anapokabiliwa na changamoto. Uzoefu wa Siah ni ushuhuda wa nguvu ya ushauri na athari ambayo mwanamke au mtu yeyote anaweza kuwa nayo kwenye kazi na maisha ya kila siku.



Baada ya kumaliza masomo yake, Siah aliajiriwa na kampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML) kwa ajili ya mafunzo ya ufundi mitambo kama mhandisi wa mitambo.

Leo, anafanya kazi kama Mratibu 2 – katika idara ya inayoundwa na timu ya wahandisi. Anafurahi kuwa sehemu ya kampuni hiyo inayojitolea kuwajibika kwa kwa jamii kwa namna mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuwajengea uwezo zaidi wafanyakazi wake bila kujali jinsia huku ikiendelea na shughuli za uchimbaji madini mkoani Geita.



Katika GGML, Siah amepata fursa ya kufanya kazi katika miradi mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kubuni na kutekeleza ufumbuzi wa nishati endelevu.


Akiwa jaji katika maonesho hayo ya TAWECE 2023 yaliyofanyika Visiwani Zanziba, Siah alitunukiwa jukumu hilo muhimu katika kukuza usawa wa kijinsia na kuwawezesha wanawake vijana kutimiza ndoto zao katika fani ya uhandisi.

Alikagua miradi ya uhandisi iliyowasilishwa na wahandisi wachanga wa kike na kutoa maoni na mwongozo muhimu kwao ili kupiga hatua kumfikia n ahata zaidi yake.



Siah alifurahishwa na mawazo ya kiubunifu yanayoibua suluhu kwa matatizo mbalimbali ya jamii. Alishuhudia mawazo muhimu ya kibunifu kama vile miradi ya uzalishaji wa nishati ya inayotokana na jua (solar power), pikipiki za kiubunifu za matairi mawili zinazotumika katika kusafirisha abiria mijini na programu nyingine za kurahisisha maisha kwa binadamu.



Miradi hii ilionyesha uwezo wa uhandisi kushughulikia changamoto za ulimwengu halisi na kuboresha maisha ya watu.



Siah alijivunia kuwa sehemu ya hafla hiyo iliyopinga dhana potofu za kijinsia na kuvunja vizuizi dhidi ya wanawake kuingia kwenye fani ya uhandisi.



Siah anaamini kwamba matukio kama vile TAWECE ni muhimu katika kuhamasisha wanawake na wasichana wengi zaidi kufuata taaluma ya uhandisi, kuondokana na dhana potofu za kijinsia ya kwamba baadhi ya fani zinatakiwa kuhusishwa na wanaume pekee.



Ili kuwa mhandisi aliyefanikiwa, unahitaji kuwa na ujuzi na sifa kadhaa muhimu.




Hizi ni pamoja na ujuzi wa kiufundi, ujuzi wa kutatua matatizo, ubunifu na uvumbuzi, ujuzi wa mawasiliano, mawazo bora, usimamizi dhabiti wakati mnafanya kazi ya pamoja.



Pia Siah anasisitiza umuhimu wa uadilifu, uwazi na maendeleo ya kitaaluma, pamoja na haja ya wahandisi kufahamu maendeleo ya sasa yanayoendena na mabadiliko ya teknolojia.



Kama mfano wa kuigwa kwa wahandisi wanawake wanaotarajia kubobea kwenye fani hiyo, malengo ya Siah ni kuboresha ufanisi wa kazi, kuendeleza uvumbuzi na teknolojia, na kutafuta elimu na mafunzo zaidi.




Mradi wa ndoto yake ni kubuni mfumo ambao utaibua utatuzi changamoto mbalimbali zinazoikwamisha sekya ya madini… mradi ambao pia mbali na kuongeza ufanisi kwenye sekta hiyo pia utainufaisha GGML na sekta ya madini kwa ujumla.



Lakinin pia amedhamiri kujiendeleza kielimu, kuwatia moyo wasichana na wanawake wachanga kufuata taaluma ya uhandisi.



Safari ya Siah kama mhandisi wa kike ni msukumo chanya kwa wanawake wote. Kwa msaada wa walimu wake, washauri na mwajiri, ameshinda changamoto na kutekeleza ndoto zake, akiwawezesha wengine waliotaka kuishia njiani.




Historia yake ni ushuhuda wa ushauri unaweza kuwa na nguvu ya kubadilisha maisha ya mtu pindi anapoamua kujitolea na kuongeza bidi katika maisha ya kia siku.




Ushauri alioupata Siah ni kama ukumbusho kwamba wanawake wanaweza kufaulu katika nyanja zinazotawaliwa na wanaume kama vile uhandisi kwenye sekta ya madini.

Share:

WAZIRI AWESO AMUONDOA MKURUGENZI MTENDAJI WA MWAUWASA

Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMATATU AGOSTI 21,2023

































Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger