Monday, 17 October 2022
KARIM BENZEMA ASHINDA TUZO YA BALLON D'OR

Karim Benzema ameshinda tuzo ya Ballon d'Or kwa mara ya kwanza, baada ya kufurahia mwaka bora wa kikazi akiwa Real Madrid mnamo 2022.
Fowadi huyo wa Ufaransa alikuwa katika hali ya kuvutia katika msimu wote wa 2021/22, na kuiongoza Los Blancos kwa utukufu wa ndani na bara.
Benzema alifunga mabao 44 na asist 15 katika mechi 46 katika michuano yote akiwa na Madrid, akiwa na wastani wa mchango wa mabao kila baada ya dakika 66.4 huku klabu hiyo ikishinda La Liga na kombe lingine la UEFA Champions League.
Kiwango chake katika Ligi ya Mabingwa, haswa, ndicho kimemfanya kuwa mshindi anayestahili wa Ballon d'Or mnamo 2022. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 34 alifunga mabao 15 katika mashindano hayo pekee, huku 10 kati ya hayo yakiingia katika raundi ya mtoano peke yake.
Muhimu katika kampeni hiyo ya Ligi ya Mabingwa kwa Benzema ni pamoja na hat-trick yake ya ajabu dhidi ya PSG na kuipatia timu yake ushindi wa muujiza, na mabao machache muhimu dhidi ya Manchester City kwenye nusu fainali.
Benzema amekuwa mchezaji wa kwanza wa Ufaransa kushinda Ballon d'Or tangu Zinedine Zidane nyuma mwaka 1998 na mshindi wa tano wa Ufaransa kwa jumla - akiungana na Zidane, Michel Platini, Jean-Pierre Papin na Raymond Kopa kama washindi.
Via _ Lango la Habari
KAMPASI YA MUHAS KUJENGWA KIGOMA
Na Mwandishi wetu,KIGOMA..
SERIKALI kupitia mkopo wa Benki ya Dunia imetenga kiasi cha dola za Marekani milioni 45.5 kwa ajili ya ujenzi wa kampasi ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) ambapo kati ya fedha hizo, kiasi cha dola za Marekani milioni 15 zitatumika kwenye ujenzi wa miundombinu katika kampasi ya Kigoma.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda ameyasema hayo 17 Octoba 2022 Wilayani Kasulu wakati wa ziara ya kikazi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan Mkoani Kigoma na kueleza kuwa Kampasi hiyo itajengwa katika Halmashauri ya Ujiji mkoani Kigoma.
Amefafanua kuwa "Kampasi hiyo itajengwa katika eneo la ekari 47.3 ambalo linapakana na eneo litalojengwa Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Magharibi,Kampasi hii inatarajiwa kuwa na miundombinu itakayotoa mazingira bora ya ufundishaji na kujifunzia, utafiti pamoja na utoaji wa huduma kwa jamii,"amesema
Waziri huyo pia amemshukuru Rais Samia kwa kuzindua majengo mapya ya Chuo cha Ualimu Kabanga ambayo ni moja kati ya Miradi iliyotekelezwa na Wizara ikiwa ni Mkakati wa Serikali wa kuboresha Mazingira ya utoaji wa Elimu ya Ualimu nchini.
Prof. Mkenda amesema kuwa Ujenzi huo umefadhiliwa na Serikali ya Canada kupitia Mradi wa Kuendeleza Elimu ya Ualimu nchini (Teachers Education Supports Project – TESP).
Mradi wa ujenzi wa Chuo cha Ualimu Kabanga ulianza tarehe 26/03/2019 na ulikamilika tarehe 22/04/2022.
Ujenzi umetekelezwa na Mkandarasi SUMA JKT Kanda ya Magharibi chini ya Usimamizi wa Mshauri Elekezi Bureau for Industrial Cooperation (BICO) wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Aidha, kazi ya utengenezaji na uwekaji wa Samani katika majengo haya inaendelea.
TEA YASHIRIKI MAADHIMISHO YA JUMA LA ELIMU YA WATU WAZIMA
Mnufaika wa SDF katika sekta ya Uchukuzi akitoa elimu kuhusu matengenezo ya pikipiki na bajaji aliyopata kupitia ruzuku ya SDF.

*****************
Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) inashiriki katika maadhimisho ya Juma la Elimu ya Watu wazima katika viwanja vya Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam - DUCE kwa lengo la kuonyesha mchango wa Elimu isiyo katika mfumo rasmi kwa jamii.
Maadhimisho hayo yanafanyika sambamba na maonyeho ambapo yameanza rasmi leo Oktoba 17 hadi Oktoba 21.
TEA inashiriki maadhimisho na maonyesho hayo kupitia Mfuko wa Kuendeleza Ujuzi (SDF) ambao unalenga kutoa mafunzo ya Ujuzi na Stadi za Kazi katika sekta sita za kipaumbele ambazo ni Ujenzi, Utalii na Huduma za Ukarimu, Teknolojia ya Habari na Mawasiliano, Kilimo na Kilimo Biashara, Uchukuzi pamoja na Nishati.
Mfuko wa Kuendeleza Ujuzi (SDF) ni sehemu ya Programu ya Kuendeleza Elimu ya Ujuzi na Mafunzo ya Stadi za Kazi zenye kuleta Tija katika Ajira (ESPJ) na Mpango Mkakati wa Kitaifa wa Kukuza na Kuendeleza ujuzi nchini (NSDS) chini ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ambayo inasimamiwa na Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) na inafadhiliwa na Serikali pamoja na Benki ya Dunia (WB)
Zaidi ya wananchi 36,870 wamenufaika na ruzuku ya Mfuko wa Kuendeleza Ujuzi ili kuwawezesha kuajiriwa au kujiajiri wenyewe. Awamu ya kwanza ya SDF ilianza kutekelezwa mwaka wa fedha 2018/2019 ambapo Taasisi 15 zilifadhiliwa kwa jumla ya Shilingi Bilioni 3.1 wakati katika awamu ya pili Taasisi 81 zimenufaika kwa ufadhili wa kiasi cha Shilingi Bilioni 9.7 zikitumika kuendesha programu za mafunzo ya ujuzi.
WATUMISHI WA CHUO CHA KOLANDOTO WAENDELEA KUTEMBELEA VIVUTIO VYA UTALII...TAZAMA HAPA WAKIWA KATIKA MGODI WA MWADUI
Eneo linalochimbwa madini ya Almasi katika mgodi wa Mwadui uliopo Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga
**
Watumishi wa Chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto Shinyanga wameendelea kufanya ziara ya mafunzo katika maeneo mbalimbali hapa nchini.
Ziara hii imekuwa ikifanyika kila mwaka majira kama haya, kwa lengo la kujifunza kazi zinazofanywa na wenzao, kutembelea vivutio vya utalii vilivyopo hapa nchini kwa lengo la kuvitangaza vivutio hivyo,kukitangaza chuo chao pamoja na kujenga mahusiano ya kazi.
Katika ziara hizo wamewahi kutembelea hifadhi ya Ngorongoro,hifadhi ya Ruaha, na kwa mwaka huu ziara hii imekuwa ya tofauti ambapo siku ya Alhamisi ya 13 Oktoba 2022 walitembelea Mgodi wa almasi Mwadui uliopo wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga na leo 17 October wameanza safari ya kwenda mikoa ya kanda ya kaskazini mwa Tanzania, ambapo watapanda Mlima Kilimanjaro,watatembelea maporomoko ya maji yaliyopo Marangu na Hifadhi ya Taifa ya Arusha.
Watumishi wa Chuo cha sayansi za Afya Kolandoto Shinyanga wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Wafanyakazi wa Mgodi wa Almasi wa Mwadui uliopo wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga kwenye sanamu la Williamson
Watumishi wa Chuo cha sayansi za Afya Kolandoto Shinyanga wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Wafanyakazi wa Mgodi wa Almasi wa Mwadui uliopo wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga kwenye sanamu la Williamson
Watumishi wa Chuo cha sayansi za Afya Kolandoto Shinyanga wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Wafanyakazi wa Mgodi wa Almasi wa Mwadui uliopo wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga
Watumishi wa Chuo cha sayansi za Afya Kolandoto Shinyanga wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Wafanyakazi wa Mgodi wa Almasi wa Mwadui uliopo wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga
Watumishi wa Chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto Shinyanga wakipewa mafunzo na Mhandisi Mkuu wa Mgodi wa Almasi wa Mwadui uliopo wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga Eng. Shagembe Mipawa
Watumishi wa Chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto Shinyanga wakipewa mafunzo na Mhandisi Mkuu wa Mgodi wa Almasi wa Mwadui uliopo wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga Eng. Shagembe Mipawa
Watumishi wa Chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto Shinyanga wakipewa mafunzo na Mhandisi Mkuu wa Mgodi wa Almasi wa Mwadui uliopo wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga Eng. Shagembe Mipawa
Watumishi wa Chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto Shinyanga wakipewa mafunzo na Mhandisi Mkuu wa Mgodi wa Almasi wa Mwadui uliopo wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga Eng. Shagembe Mipawa
Eneo linalochimbwa madini ya Almasi katika mgodi wa Mwadui uliopo Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga
Mafunzo yakiendelea
Mafunzo yakiendelea
Mafunzo yakiendelea
Mafunzo yakiendelea
MWAMBA AOMBEWA KANISANI APATE NGUVU ZA KIUME

Nabii Jeremiah akimuombea muumini wake
Mchungaji mmoja nchini Kenya anayejiita Nabii Jeremiah Kioko, imesambaa video yake mitandaoni ikimuonesha akimuombea mwanaume mmoja ili apate nguvu za kiume kwa kumsukuma kisha kumshika nyeti zake.
Video hiyo imesambaa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii, ambapo Nabii huyo mara baada ya kufanya maombi hayo, muumini wake alisikika akisema tayari nguvu zake zimerejea na kumtaka mke wake ajiandae.
"Ruka juu kwanza achana na nguvu za kiume, nguvu za kiume simamama kuja, mimi naitwa Jeremiah nakupatia nguvu simama, mimi ni transformer wacha nimgawie mtazamaji nasikia ipo kabisa haaa, Bibi yako (mke wako) anakutazama hapa?," aliuliza Nabii Jeremiah
Ambapo mara baada ya maombi hayo muumini huyo alisikika akijibu ,"Nakuja kesho niko chonjo nitakuja ku-kiss na ku-hug,".
Aidha video hiyo pia ipo kwenye akaunti ya TikTok ya mchungaji huyo.
Sunday, 16 October 2022
RAIS SAMIA AIPA KONGOLE SIMBA SC!

“Kongole Simba kwa ushindi wa 1-0 (ushindi wa jumla 4-1) mlioupata dhidi ya timu ya Primeiro De Agosto ya Angola na hivyo kufanikiwa kuingia hatua ya makundi ya klabu bingwa Barani Afrika. Nawatakia kila kheri katika michuano inayofuata,”
RAIS SAMIA SULUHU ASALIMIA WANANCHI WA RUNZEWE-GEITA, NYAKANAZI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Wananchi wa Runzewe wakati akihitimisha ziara yake Mkoani Geita tarehe 16 Oktoba, 2022.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Waziri wa Nishati January Makamba pamoja na viongozi wengine wakivuta kitambaa kuzindua miradi sita ya umeme, ikiwemo Njia ya kusafirisha umeme wa msongo Kv 220 kutoka Nyakanazi -Geita, Nyakanazi Rusumo, Kituo cha kupokea, kupoza na kusambaza umeme cha Nyakanazi pamoja na njia kubwa za kusafirisha umeme kwenda Mkoa wa Kigoma tarehe 16 Oktoba, 2022 Mkoani Kagera.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Waziri wa Nishati January Makamba pamoja na viongozi wengine wakati akikata utepe kuzindua miradi sita ya umeme katika Kituo cha kupokea, kupoza na kusambaza umeme kwenda Mkoani Kigoma na Geita kwenye hafla iliyofanyika Nyakanazi mkoani Kagera 16 Oktoba, 2022 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akitembelea na kukagua miundombinu mbalimbali ya Kituo cha kupokea, kupoza na kusambaza umeme kwenda Mkoani Kigoma na Geita kwenye hafla ya uzinduzi iliyofanyika Nyakanazi mkoani Kagera 16 Oktoba, 2022 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Wananchi wa Nyakanazi mkoani Kagera wakati akielekea Mkoani Kigoma tarehe 16 Oktoba, 2022
SIMBA SC YAONESHA UBABE YAFUZU HATUA YA MAKUNDI LIGI YA MABINGWA AFRIKA
******************
NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
KLABU ya Simba imefanikiwa kutinga hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kuichapa timu ya Primeiro de Agosto ya nchini Angola 1-0 na kuwa jumla ya mabao 4-1 baada ya mechi ya kwanza Simba Sc kushinda 3-1 ugenini.
Mechi hiyo ambayo imepigwa katika dimba la Benjamini Mkapa, Simba Sc imefanikiwa kutawala mchezo na kuwafanya mashabiki ambao waliujaza uwanja kufurahia kandanda safi kutoka kwa mastaa wa timu hiyo.
Ni Moses Phiri ambaye amekuwa moto katika mechi za hivvi karibu amepachika bao safi ambalo liliwafanya Simba Sc kuwahakikishia kufuzu hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika














































