Monday, 25 April 2022

Picha : UCHAFUZI WA MAZINGIRA WAHATARISHA AFYA ZA WANANCHI DIDIA...DIMBWI HATARI KWENYE DAMPO SOKO KUU BALAA

Hili ni dimbwi la maji machafu lililopo kwenye dampo la uchafu jirani na soko kuu la Didia katika halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga ambalo linalalamikiwa na wakazi wa eneo hilo kuwa linahatarisha afya zao.


Wakizungumza na Malunde 1 blog iliyofika katika eneo hilo mapema leo Aprili 25,2022,wakazi wa Didia wamesema dimbwi hilo linakusanya maji machafu kutoka maeneo mbalimbali ya Mji wa Didia yakiwemo ya chemba za vyoo hali inayosababisha uhalifu wa mazingira.


Mbali na kueleza kuwa dimbwi hilo limekuwa kituo kikuu cha kuzalisha mbu waenezao malaria lakini pia pindi maji hayo yanapokauka kumekuwa na harufu mbaya kwani maji hayo yamechanganyikana na uchafu wa dampo lililopo eneo hilo.


Aidha wameomba hatua zaidi zichukuliwe kufukia madimbwi mbalimbali yaliyozagaa katika Mji wa Didia.


Nao wafanyabiashara wa Soko Kuu la Didia lenye zaidi ya miaka 50 wameziomba mamlaka zinazohusika kujenga choo katika soko hilo kwani hakipo hali inayochangia uchafuzi wa mazingira jirani na soko hilo huku wengine wakilazimika kwenda kujisaidia kwenye vyoo vya watu binafsi
Muonekazo wa dimbwi la maji machafu lililopo kwenye dampo la uchafu jirani na soko kuu la Didia katika halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga ambalo linalalamikiwa na wakazi wa eneo hilo kuwa linahatarisha afya zao. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Muonekazo wa dimbwi la maji machafu lililopo kwenye dampo la uchafu jirani na soko kuu la Didia katika halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga ambalo linalalamikiwa na wakazi wa eneo hilo kuwa linahatarisha afya zao.
Muonekazo wa dimbwi la maji machafu lililopo kwenye dampo la uchafu jirani na soko kuu la Didia katika halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga ambalo linalalamikiwa na wakazi wa eneo hilo kuwa linahatarisha afya zao.
Dampo la uchafu jirani na soko kuu la Didia katika halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga ambapo pia kuna dimbwi ambalo linalalamikiwa na wakazi wa eneo hilo kuhatarisha afya zao.
Dampo la uchafu jirani na soko kuu la Didia katika halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga ambapo pia kuna dimbwi ambalo linalalamikiwa na wakazi wa eneo hilo kuhatarisha afya zao.
Dampo la uchafu jirani na soko kuu la Didia katika halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga ambapo pia kuna dimbwi ambalo linalalamikiwa na wakazi wa eneo hilo kuhatarisha afya zao.
Dampo la uchafu jirani na soko kuu la Didia katika halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga ambapo pia kuna dimbwi ambalo linalalamikiwa na wakazi wa eneo hilo kuhatarisha afya zao.
Soko kuu la Didia ambalo lipo jirani Dampo la uchafu jirani na soko kuu la Didia katika halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga ambapo pia kuna dimbwi ambalo linalalamikiwa na wakazi wa eneo hilo kuhatarisha afya zao.
Soko kuu la Didia ambalo lipo jirani Dampo la uchafu jirani na soko kuu la Didia katika halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga ambapo pia kuna dimbwi ambalo linalalamikiwa na wakazi wa eneo hilo kuhatarisha afya zao.
Soko kuu la Didia ambalo lipo jirani Dampo la uchafu jirani na soko kuu la Didia katika halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga ambapo pia kuna dimbwi ambalo linalalamikiwa na wakazi wa eneo hilo kuhatarisha afya zao.

Muonekano wa madimbwi katika moja ya mitaa katika mji wa Didia
Muonekano wa madimbwi katika moja ya mitaa katika mji wa Didia
Muonekano wa madimbwi katika moja ya mitaa katika mji wa Didia
Muonekano wa madimbwi katika moja ya mitaa katika mji wa Didia
Muonekano wa madimbwi katika moja ya mitaa katika mji wa Didia
Muonekano wa madimbwi katika moja ya mitaa katika mji wa Didia
Muonekano wa madimbwi katika moja ya mitaa katika mji wa Didia

Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Share:

DC MAGU : BAKWATA SISITIZENI ELIMU DUNIA NA DINI

Mkuu wa Wilaya Magu, Salum Kalli amewahimiza waumini wa dini ya kiislamu kutoa nafasi sawa kwa watoto wao kupata elimu ya dini pamoja na elimu dunia ili kutoa fursa kwa Taifa kuwa na wataalamu wa kada mbalimbali.

Kalli alitoa rai hiyo Jumapili Aprili 24, 2022 wakati akizungumza kwenye kongamano la ‘malezi bora, tabia njema na misngi ya ndoa’ lililofanyika katika msikiti mkuu wa BAKWATA wilayani Magu.


Alishauri viongozi wa BAKWATA kuwahimiza waumini waumini wao kutafuta elimu dunia na elimu dini kwani kwa kufanya hiyo itasaidia Taifa kuwa na jamii ya watu walioelimika na wanaozingatia maadili ya pande zote mbili na hivyo kutimiza ipasavyo wajibu wao ikiwemo malezi bora na kujiletea maendeleo.


Aisha Kali aliwahimiza wananchi wakiwemo waumini wa dini ya kiislamu kushiriki ipasavyo kwenye zoezi la Sensa ya watu na makazi linalotarajiwa kufanyika mwezi Agosti mwaka huu 2022 ambapo alitoa rai kwa viongozi wa dini kuendelea kuelimisha waumini wao kujiandaa na zoezi hilo.


Naye Sheikh wa Mkoa Mwanza, Hassan Kabeke alisema elimu dunia pia ni jambo la msingi kwa jamii ya waislamu akisema “tuna mkakati wa kujenga vituo vya afya kila wilaya mkoani Mwanza, bila kusomesha watoto tutawapa wapi madaktari, manesi na wafamasia”.


Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la KIVULINI, Yassin Ally alisema ni vyema BAKWATA ikasisitiza wanafunzi kwenda shule katika siku za wiki (Jumatatu hadi Ijumaa) na siku za wikendi (Jumamosi na Jumapili) wakaenda madrasa hatua itakayosaidia kushindana vyema kielimu na wenzao.


Makongamano ya ‘malezi bora, tabia njema na misingi ya ndoa yanafanyika katika Wilaya zote mkoani Mwanza yakiandaliwa na BAKWATA kwa kushirikiana na KIVULINI kwa lengo la kuelimisha jamii kupinga ukatili wa kijinsia, maelewano ndani ya ndoa, wazazi kulea watoto wao ili kuondoa utoro mashuleni na watoto wa mitaani ambapo maoni yanayokusanywa yatawasilishwa kwa Katibu Tawala Mkoa Mwanza ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya MTAKUWWA kwa ajili ya utekelezaji zaidi.

Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mkuu wa Wilaya Magu, Salum Kalli akizungumza kwenye kongamano hilo.
Waumini wa dini ya kiislamu wilayani Magu wakifuatilia kongamano hilo.
Mkurugenzi Mtendaji Shirika la KIVULINI, Yassin Ally akiwasilisha mada ya malezi kwenye kongamano hilo.
Mkurugenzi Mtendaji Shirika la KIVULINI, Yassin Ally akiwasilisha mada wakati wa kongamano hilo.
Mkurugenzi Mtendaji Shirika la KIVULINI, Yassin Ally akizungumza kwenye kongamano hilo.
Sheikh wa Mkoa Mwanza, Hassan Kabeke akisisitiza jamii kurejesha maadili kama ilivyokuwa zamani hatua itakayosaidia kuondoa mifarakano kwenye ndoa.
Sheikh wa Mkoa Mwanza, Hassan Kabeke (katikati) akizungumza kwenye kongamano hilo.
Waumini wa dini ya kiislamu wilayani Magu wakifuatilia kongamano la 'malezi bora, tabia njema na misingi ya ndoa' lililofanyika katika Msikiti Mkuu wa BAKWATA wilayani humo.
Sheikh wa Wilaya Magu, Nuhu Zaidi alitoa rai kwa jamii kuzingatia mafundisho yaliyowasilishwa kwenye kongamano hilo.
Viongozi mbalimbali wakifuatilia kongamano hilo.
Waumini wa dini ya kiislamu wilayani Magu wakifuatilia kongamano hilo.
Waumini wa dini ya kiislamu wilayani Magu wakifuatilia kongamano la malezi bora lililoandaliwa na BAKWATA Mkoa Mwanza kwa kushirikiana na shirika la KIVULINI katika kipindi hiki cha mwezi wa Ramadhani ambapo makongamano ya aina hiyo yanafanyika katika Wilaya zote za Mkoa Mwanza.
Waumini wa dini ya kiislamu wilayani Magu wakifuatilia kongamano hilo.

Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMATATU APRILI 25,2022



i
















Share:

Sunday, 24 April 2022

WAZIRI BITEKO ATOA WIKI MBILI FEDHA ZA CSR ZILIZOZUILIWA ZITOLEWE KUTEKELEZA MIRADI MARA


Waziri wa Madini  Doto Biteko
Waziri wa Madini  Doto Biteko

Na Dinna Maningo, Tarime

WAZIRI wa Madini ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Bukombe Doto Biteko ametoa wiki mbili kwa Serikali ya mkoa wa Mara ambayo imeuzuia Mgodi wa North Mara kutoa fedha za Uwajibikaji wa makampuni kwa Jamii ( CSR) kwa ajili ya kujenga miradi katika vijiji vinavyozunguka Mgodi,kuhakikisha fedha zinatolewa ili ziendelee kutekeleza Miradi ya maendeleo.

Biteko ameyasema hayo Februari,24,2022 wakati alipotembelea bomba la maji taka katika mgodi huo lililopasuka maeneo ya barabara binafsi ya mgodi na kuzua taharuki kwa wananchi.


"RC tumeongea nae kasema baada ya wiki mbili watakuwa wamekamilisha uchunguzi na miradi itaanza kutekelezwa,viongozi wasikilizeni watu wa chini hata kama hajui kiswahili wekeni mkalimani,watu wana maswali lakini hakuna anayewajibu.

"Kitu kinachojenga mahusiano kati ya wananchi na mgodi ni fedha za CSR mna Bilioni 5.6 bado na ya mwaka jana Bilioni moja zipo tu wakati kule halmashauri ya Bukombe kupata Bilioni moja ni kazi,nyie mnakaa na fedha za miradi,fedha zitolewe miradi itekelezwe",amesema Biteko.


Biteko amesema kuwa kutotolewa kwa fedha hizo ni kuusababishia mgodi kulaumiwa na wananchi wakati tatizo lipo kwa viongozi jambo ambalo linavunja mahusiano baina ya mgodi na vijiji vinavyozunguka mgodi.

Biteko ameutaka mgodi kujenga mahusiano mazuri na wananchi nakwamba nafasi kubwa za uongozi katika mgodi zinaongozwa na watanzania "kama afisa mahusiano wa mgodi hawezi,toa weka wengine,meneja wa huu mgodi ni mtanzania na tumewaweka kwakuwa ndiyo wanajua tamaduni zetu,tumeachiwa mgodi kuendesha wenyewe tatizo likitokea tusiwalaumu wazungu"


Mbunge wa Jimbo la Tarime vijijini Mwita Waitara amesema kuwa kitendo cha RC Mara kuzuia fedha kumekwamisha miradi mbalimbali kutotekelezwa baada ya kukosekana kwa fedha ukiwemo mradi wa maji kijiji cha Nyangoto unaonjengwa kwa fedha za CSR sh.Milioni 998,uliosimama baada ya mkandarasi kampuni ya Gokona kutolipwa fedha za ujenzi licha ya kuanza ujenzi kwa fedha zake ujenzi uliofikia asilimia 34.


"Tunamshukuru Waziri Biteko kufika na mwafaka kautoa kilio chetu ilikuwa ni pesa zilizozuiliwa zitolewe zifanye kazi wakati huo serikali ya Mara ikiendelea na uchunguzi wake wa matumizi mabaya ya fedha za CSR",amesema Waitara.


Mkuu wa mkoa wa Mara Ally Hapi amesema kuwa yeye anachopambana nacho ni utoaji wa fedha zinazolenga kwenye miradi lakini zinaishia kwenye matumbo ya watu akisisitiza kuwa fedha za CSR zilizopita ni wizi mtupu na kwamba Serikali ya mkoa huo itasimama imara.


"Tunachotaka tukikubaliana mradi ujengwe,ujengwe sisi tunajenga kituo cha afya kwa milioni 300 lakini kuna kijiji kimejenga kituo cha afya kwa Milioni 800 hakijakamilika,wananchi msitumike kama kichaka,fedha zinatumika nyingi kuliko mradi,nataka fedha zifanye kazi fedha za CSR za 2019 kuna fedha milioni 300 zilitengwa kutekeleza mradi hazijatumika unaomba tena fedha"amesema Hapi.


RC Hapi amesema kuwa wamejipanga vizuri ndani ya muda mfupi miradi itatekelezwa ukiwemo mradi wa maji Nyangoto ambao ameambiwa kuwa umeshafanyiwa usanifu na utajengwa na kwamba yeye hawezi kubariki wizi hivyo watu waache janjajanja na watekeleze miradi kwa ufanisi na kwa haraka.
Share:

POLISI KAGERA WAKAMATA MABOKSI 66 YENYE VIFAA VYA KUSAFIRISHIA UMEME LAINI KUBWA

Kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Kagera ACP Maketi Msangi

Na Mbuke Shilagi Kagera.

Jeshi la Polisi Mkoani Kagera limekamata maboksi 66 yenye vifaa vya kusafirishia umeme kwenye laini kubwa vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 18.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoani Kagera ACP Maketi Msangi, wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake amesema kuwa maboksi hayo yamekamatwa kwa nyakati tofauti wakati wa zoezi la oparesheni iliyofanyika kati ya tarehe 18 hadi 20 mwezi Aprili mwaka huu.

ACP Msangi amesema kuwa maboksi 11 yalikuwa yametelekezwa kwenye shamba la Kahawa katika kijiji cha Kanazi katika halmashauri ya wilaya ya Bukoba, maboksi 37 yalikamatwa katika nyumba ya kulala wageni iliyopo mtaa wa Jamuhuri kata ya Bilele Manispaa ya Bukoba na maboksi mengine 18 yalikuwa yametelekezwa kituo kikuu cha mabasi ya abiria kilichoko katika manispaa hiyo ya Bukoba.


Kaimu kamanda huyo amesema kuwa jeshi la polisi linaendelea na juhudi za kuwasaka watuhumiwa ili kuwafikisha mahakamani.

Share:

KIJANA MBARONI KWA TUHUMA ZA KUBAKA MWANAFUNZI WA MIAKA 16


Kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Kagera ACP Maketi Msangi

Na Mbuke Shilagi -Kagera

Jeshi la Polisi mkoani Kagera linamshikilia Stide Joackim (34) mkazi wa kijiji Kyaka kata Kyaka Wilaya ya Misenyi kwa tuhuma za kumbaka mwanafunzi wa sekondari mwenye umri wa miaka 16.

Kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Kagera ACP Maketi Msangi amesema kuwa mtuhumiwa huyo alitenda tukio hilo mnamo tarehe 18 Aprili mwaka huu majira ya saa 5:30 usiku katika kijiji cha Kyaka kata ya Kyaka wilayani humo, na mnamo tarehe 20 Aprili mwaka huu majira ya saa 8:30 mchana alikamatwa akiwa katika kijiji cha Bulfani pia kilichopo katika kata hiyo.

ACP Msangi amesema kuwa, chanzo cha tukio hilo ni tamaa za mwili na kwamba mtuhumiwa atafikishwa mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilika.


Ametoa wito kwa wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa kutoa taarifa za wahalifu, ili hatua zichukuliwe kabla ya madhara kutokea.
Share:

BI. HARUSI ALIYEWAWEKEA WAGENI BANGI KWENYE CHAKULA SIKU YA HARUSI AKAMATWA


Danya Svoboda bi. harusi ambaye anashikiliwa na Polisi kwa kosa la kuwawekea wageni bangi kwenye chakula.

DANYA SVOBODA ni bibi harusi ambaye yeye na mhudumu wake, Joycelyn Bryan wamekamatwa na Polisi huko Florida nchini Marekani baada ya kubainika ni kweli waliongeza bangi kwenye chakula ambacho kilitolewa kwa wageni wa harusi yake.


Mmoja ya wageni waalikwa katika harusi hiyo alitoa ushahidi kwa kusema; “Nilianza kuhisi tofauti baada ya kula, nilijisikia kama mlevi hivi…

“Nilimpomuuliza bibi harusi kama waliongeza bangi, akajibu ndiyo na akasisimka…”

Siku ya tukio hilo ilibidi maofisa wa Polisi kuitwa kwenye sherehe ya harusi hiyo kusaidia wageni ambao walisema walihisi kama walikuwa wamepewa dawa za kulevya na baadhi kupoteza fahamu.


Baada ya vipimo vya vyakula na vinywaji vya sherehe hiyo, viligundulika kuwa na chembechembe za bangi.
Madawa ya Kulevya aina ya bangi

Bibi harusi huyo pamoja na mhudumu wake wanakabiliwa na mashtaka ya kufanya maamuzi ya kizembe na kulisha watu bangi bila ridhaa yao.


Huko Florida, inasemekana bangi ni halali kama ikitumika kimatibabu, lakini si kwa matumizi ya dawa hiyo kwa burudani, tofauti na katika baadhi ya majimbo ya Marekani.

Cc; @sifaelpaul
Share:

Video Mpya : ELVIS KASHUMBA - UPENDO



Mwimbaji wa nyimbo za Injili Elvis Kashumba anakualika kutazama video ya wimbo wake mpya unaitwa Upendo...Tazama hapa chini
Share:

WAZIRI GWAJIMA ATOA CHETI KWA SHIRIKA LA ICS KWA KUANZISHA MFUMO WA KUTOA ELIMU YA MALEZI NA MAKUZI BORA YA MTOTO KWA NJIA YA KIDIJITALI


Waziri Wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima Ametoa Cheti cha Pongezi kwa Shirika la Wekeza kwa Mtoto na Kuimarisha Familia ICS la Mjini Shinyanga linalo tekeleza Miradi ya Kijamii katika Kupinga Ukatili wa Wanawake na Watoto Kupitia Utoaji wa Elimu ya Malezi na Makuzi Bora kwa Mtoto Baada ya kufanikiwa Kuanzisha Mfumo wa Elimu kwa Njia ya Mtandao kwa kutumia Simu Janja kwa lengo la kuhamasisha jamii itambue umuhimu wa Malezi Bora kwa Ustawi wa Watoto.

Soma pia: 

ICS YAJA NA MKAKATI WA KUTOA ELIMU YA MALEZI NA MAKUZI BORA YA MTOTO KWA NJIA YA KIDIJITALI


Aidha wengine waliopata vyeti vya Pongezi ni pamoja na  Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema, Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, Afisa Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Shinyanga Ndugu Tedson Ngwale pamoja na Afisa Ustawi wa Mkoa huo Bi. Lyidia Kwesigabo kwa mshikamamo na uongozi mzuri wa wadau uliofanikisha kudhibiti Mauaji ya kinyama kwa Wazee kutokana na imani potofu za Kishirikina kuwa kila Mzee mwenye macho mekundu eti ni Mchawi.

Dkt.  Gwajima amesema Kuwa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi amaalumu ina mpango wa Kuanzisha Tuzo ya Siku ya Mashujaa wa Mapinduzi ya Kutokomeza Ukatili Kwa Wanawake, Watoto na Wazee ili Kuongeza Hamasa Kwa Jamii inayoshiriki Kupinga Vitendo Vya Ukatili wa Kijinsia hapa Nchini.


Kwa Upande wake Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu-(Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) ambaye Pia ni Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Patrobas Katambi amesema kuwa Jamii inapaswa Kubadilika kuwa na Malezi bora kwa watoto ili kujenga Taifa lenye maadili mema

Mkurugenzi wa Shirika la ICS Kudely Sokoine amesema kuwa Shirika lina mpango wa kufikia watu laki sita (600,000) katika Mikoa ya Shinyanga, Mwanza, Kilimanjaro na Simiyu kwa lengo la Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto


Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger