Tuesday, 6 July 2021

Research Assistant at Baylor College of Medicine Children’s Foundation

Baylor College of Medicine Children’s Foundation – Tanzania is a non-government organization (NGO) dedicated to supporting the provision of high-quality, comprehensive HIV/AIDS care and treatment to HIV – exposed and infected children and adolescents in the Lake and Southern Highlands Zones of Tanzania. Baylor-Tanzania is funded by the United State Agency for International Development (USAID), […]

This post Research Assistant at Baylor College of Medicine Children’s Foundation has been posted by Udahiliportaldaily

Get more post by visiting Udahiliportal.com

know more details about Udahiliportal.com by visiting Udahiliportal.com - Find Jobs & Ajira mpya leo, ajira portal Tanzania, ajira yako, brighter Monday, mabumbe, mwananchi ajira, secretariet ya ajira, tamisemi ajira za afya, wizara ya afya, ajira Tanzania - selection za vyuo , selection, second selection vyuo, second selection, tamisemi selection, selection form one 2020/2021

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

Share:

Assistant Hatchery Manager – Poultry at Evolve People Solutions

Assistant Hatchery Manager – Poultry   Our client is looking for a highly organized and result oriented Assistant Hatchery Manager to be  responsible for all activities in the assigned Hatchery’s Department and for achieving set targets as per  SOPs. The successful candidate will gain valuable experience in a fast paced environment and have the  ability to […]

This post Assistant Hatchery Manager – Poultry at Evolve People Solutions has been posted by Udahiliportaldaily

Get more post by visiting Udahiliportal.com

know more details about Udahiliportal.com by visiting Udahiliportal.com - Find Jobs & Ajira mpya leo, ajira portal Tanzania, ajira yako, brighter Monday, mabumbe, mwananchi ajira, secretariet ya ajira, tamisemi ajira za afya, wizara ya afya, ajira Tanzania - selection za vyuo , selection, second selection vyuo, second selection, tamisemi selection, selection form one 2020/2021

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

Share:

Zari ampiga chini mpenzi wake maarufu kwa jina la King Bae

Mfanyabiashara na Mzazi mwenza wa staa wa Bongofleva na bosi wa Wasafi Media, Diamond Platnumz, Zarina Hassan maarufu kama ‘Zari the boss lady’ameamua kumpiga chini mpenzi wake maarufu kwa jina la King bae au Dark Stallion, baada ya kuona hana manufaa naye.

Zari ambaye anaishi Afrika Kusini pamoja na watoto wawili wa Mondi, aliandika ujumbe kwenye insta story yake,kuwa mwanaume huyo inabidi amuache kwani hana faida yoyote kwake.

“Nimemmisi, lakini inanibidi nimuache aondoke. Kwa sababu kama hanijengi, hana faida kwangu siwezi kuendelea naye,” ameandika Zari

Kufuatia hali hiyo baadhi ya mashabiki wamedai kuwa hii inaweza kuwa muda muafaka kwa Mondi kurudisha majeshi kwa Zari baada ya Dark Stallion ambaye alikuwa raia wa Nigeria kutimuliwa.

Share:

Wawili wafariki dunia, 15 wanusurika kifo baada ya kula chakula chenye sumu

Watoto wawili wamefariki dunia na wengine 15 wamenusurika kifo baada ya kula chakula ambacho kinadhaniwa kuwa na sumu.

Taarifa hiyo imetolewa jana na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Henry Mwaibambe, wakati akizungumza na waandishi wa habari, amewataja waliofariki kuwa ni Manyirizu Joseph (6) na Bertha Mateso (5) ambao wote ni wakazi wa Ikobe wilayani Mbogwe.

Kamanda Mwaibambe amesema watoto hao na wengine waliojeruhiwa walikula mabaki ya chakula (kiporo) ambacho ni wali na nyama ya kondo na kuanza kutapika pamoja na kuharisha.

Aidha, Kamanda huyo amesema hali ya manusura wanaendelea na matibabu katika kituo cha afya Iboya wilayani Mbogwe mkoani humo na hali zao zinaendelea vizuri.

Share:

Serikali Na Unesco Wazindua Mradi Mpya Wa Kisayansi Utakaosaidia Nchi Kimaendeleo

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Profesa James Mdoe amesema kuwa mpaka sasa hakuna sera ya sayansi , teknolojia na ubunifu zaidi ya kuwa na sera ya sayansi ilitungwa mwaka 1996 ambayo ndio inatumika kwa sasa.

Prof. Mdoe aliyasema hayo jana mjini Morogoro wakati akizindua mradi wa kuboresha mifumo ya sayansi, teknolojia na ubunifu kwa ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Uswidi (SIDA) kwa ushirikiano wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknololojia pamoja na Tume ya Taifa ya UNESCO.

Alisema kuwa kama nchi na kwa kutambua umuhimu wa sayansi, teknolojia na ubunifu kwa sasa mchakato wa kuandaa sera ya sayansi, teknolojia na ubunifu unaendelea na kwamba wizara iko tayari kushirikiana na wadau mbalimbali katika kukamilisha uandaaji wa sera hiyo.

“Covid imetufundisha tuwe tunajitegemea wenyewe kwa kuwekeza kwenye tafiti za kisayansi na kama nchi mradi huu utasaidia tuko wapi na tunaelekea wapi,” alisema Prof. Mdoe.

Awali akitambulisha mradi huo Mkuu wa kitengo cha Sayansi asilia kutoka UNESCO Keven Robert alisema kuwa mradi huo utawezesha kusaidia nchi kuimarisha mifumo ya sayansi, teknolojia na utafiti.

Aidha mradi huo pia utasaidia kuimarisha taasisi za kisayansi kufanya tafiti na kuweka mazingira wezeshi ya kufanya tafiti za kisayansi ambazo zitasaidia katika kutatua changamoto za wananchi, kukabiliana na majanga yakiwemo magonjwa mbalimbali na pia kufikia malengo ya maendeleo endelevu.

Robert alisema kuwa mradi huo utakuwa na maeneo10 ya utekelezaji ambapo baadhi ya maeneo ni pamoja na kuangalia uwekezaji katika tafiti za kisayansi ambapo matokeo ya tafiti hizo zinapouzwa zinaweza kuimarisha uchumi ya nchi.

“Mfano katika kipindi hiki cha janga la Corona yapo mataifa yaliyofanya tafiti za kisayansi na kutengeneza chanjo hivyo zinapouzwa mataifa hayo yamekuwa yakipata fedha na kukua kiuchumi,” alisema Robert.

Alitaja maeneo mengine yatakayoangaliwa katika mradi huo kuwa ni kwa namna gani tafiti za kisanyansi zinasaidia wananchi na kwa namna gani wananchi wanashirikishwa kwenye tafiti kwa kuzingatia usawa wa kijinsia.

Kwa upande wake mwakilishi wa Mkurugenzi mkazi wa UNESCO Faith Shayo alisema kuwa mradi huo utakuwa wa awamu mbili na matarajio ya mradi huo ni kuona nchi inazingatia maazimio 10 ambayo yaliazimiwa mwaka 2017 baada ya maazimo ya awali ya mwaka 1974 kufanyiwa maboresho.

Share:

Wawili Wakamatwa Kwa Madai ya kumiliki karakana ya kutengeneza silaha za kienyeji

Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma linawashikilia watu wawili kwa tuhuma za kumiliki karakana ya kutengeneza silaha za kienyeji aina ya gobole bila kibali na kuziuza kwa wahalifu.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Onesmo Lyanga, amesema kufuatia msako uliofanyika katika Kijiji cha Chilendu, Kata na Tarafa ya Kibakwe Wilaya ya Mpwapwa walikamatwa watuhumiwa hao, ambao majina hayakutajwa, wakimiliki karakana ya kutengenezea silaha za kienyeji aina ya gobole bila kibali.

Lyanga amesema watuhumiwa walikamatwa wakiwa na gobole tano zilizo tayari, baruti gramu 408, goroli vipande vya chuma 40, fremu za silaha mbili na vifaa mbalimbali vya uchongaji wa silaha hizo.

Share:

Atiwa Mbaroni Kwa Kumbaka Mtoto Wake wa Kambo

Jeshi la Polisi wilayani Geita linamshikilia Vicent Said (27) mkazi wa Kata ya Magenge kwa tuhuma za kumbaka mwanaye wa kambo mwenye umri wa miaka saba.

Taarifa hiyo imetolewa na Kamanda wa Polisi Henry Mwaibambe, wakati akizungumza na waandishi wa habari amesema, tukio hilo limetokea Julai 2, mwaka huu katika kijiji cha sobora ambapo mtuhumiwa huyo anadaiwa kumrubuni mtoto huyo kwa maandazi na juisi ya shilingi 500.

Kamanda Mwaibambe amesema mtuhumiwa amekamatwa na atafikishwa mahakamani wakati wowote kuanzia sasa.

Aidha, Kamanda huyo amesema baada ya tukio hilo kuna watu wanaotaka kuharibu ushahidi ili mtuhumiwa aachiwe huru na kuwatahadharisha kuziacha juhudi hizo mara moja kwani polisi hawatozifumbia macho ili haki itendeke.

Akizungumza na chombo kimoja cha habari, mtoto huyo aliyefanyiwa kitendo hicho, amesema baba yake huyo amekuwa akimfanyia kitendo hicho mara kwa mara na pindi anapomfanyia humfunga mdomo na akimaliza humnunulia maandazi na juisi.

Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMANNE JULAI 6,2021

Magazetini June 6 2021

Share:

Monday, 5 July 2021

Ofisi Ya Msajili Wa Hazina Yaagizwa Kuibua Miradi Mipya

Na. Josephine Majura na Sabato Kosuri,  Dar es Salaam

NAIBU Waziri wa Fedha na Mipango, Mhandisi Hamad Yussuf Masauni ameiagiza Ofisi ya Msajili wa Hazina kushirikiana na Idara ya Ubia baina ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi ya Wizara ya Fedha na Mipango na pia Kituo cha Uwekezaji (TIC), kuanzisha miradi mipya ambayo Serikali itaweka hisa zake.

Ametoa maagizo hayo jijini Dar es Salaam alipotembelea Ofisi ya Msajili wa Hazina ambapo alikutana na kufanya mazungumzo na Menejimenti na Wafanyakazi wa ofisi hiyo akiwa katika mwendelezo wa ziara yake ya kutembelea Taasisi zote zilizo chini ya wizara hiyo.

Alisema faida ya kuongezeka kwa miradi mipya ni kuifanya Serikali kupata gawio kubwa zaidi ambapo fedha hizo zitaisaidia Serikali kutekeleza miradi ya maendeleo na mashirika yanayoendesha miradi hiyo kuongeza uwezo wake wa kiutendaji.

“Pamoja na agizo la kuhakikisha kunakuwa na miradi mipya, nataka mfanye ufuatiliaji wa matumizi ya kila Shirika au Taasisi ili kupata uhalisia wa utendaji kazi na matumizi yao ili kupunguza matumizi yasiyo kuwa ya lazima lengo likiwa ni kuongeza faida na kurudisha sehemu ya faida hiyo kama gawio kwa Serikali” alisisitiza Mhandisi Masauni.

Aidha, ameiagiza Ofisi ya Msajili wa Hazina kupitia Kitengo cha Utafiti kuendelea kufanya tafiti mbalimbali zenye kuibua changamoto za uendeshaji wa mashirika na kuzitafutia ufumbuzi ili yaweze kujiendesha kwa faida ili kuepuka hasara kwa Serikali.

Akizungumzia baadhi ya Mashirika kutokuwa na Bodi, Masauni, aliipongeza Ofisi ya Msajili wa Hazina kwa kuanzisha Mfumo wa Usimamizi na Ufuatiliaji wa Bodi za Taasisi na Mashirika ya Umma, ambao unatumika kutambua hali za Bodi na kusaidia kupata wajumbe wa Bodi kwa wakati.

Alieleza kuwa ni vema kuwa na Bodi hizo kwa kuwa husaidia kujenga uwajibikaji na utawala bora katika mashirika na taasisi za umma.

Masauni amesema kuwa, Ofisi ya Msajili wa Hazina inatakiwa kushiriki katika kutoa maoni na ushauri kwenye majadiliano yanayohusiana na mikataba mbalimbali ya miradi mikubwa kwa kuwa Msajili wa Hazina ndiye mlezi wa mashirika hayo na mwenye dhamana ya kulinda maslahi ya umma katika miradi mbalimbali nchini.

Kwa upande wake Msajili wa Hazina, Bw. Athumani Mbuttuka, alisema katika miradi ambayo Serikali ina hisa na inaendeshwa kwa tija, imeendelea kuweka mikakati madhubuti ya kufanya tathimini na upelembaji, akitolea mfano katika kiwanda cha Sukari Kilombero kuwa uchambuzi wa upanuzi wa kiwanda hicho umeweza kusaidia kuokoa kiasi cha takribani Dola za Marekani 69.5 milioni ambazo ni zaidi ya Shilingi bilioni 161 kabla ya kutoa gharama za awali.

Pia uchambuzi na majadiliano na kampuni ya Inflight umewezesha kupatikana kwa gawio la Dola za Marekani takribani 687,516 sawa na shilingi bilioni 1.6 ambazo zitaanza kulipwa mwezi huu.

Mbuttuka aliahidi kufanyia kazi maagizo yote yaliyotolewa na Mheshimiwa Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhandisi Masauni ili kuongeza uwajibikaji katika ofisi hiyo.

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhandisi Masauni yupo jijini Dar es Salaam katika ziara yake ya kikazi ambapo atatembelea ofisi zilizo chini ya Wizara ya Fedha na Mipango.

Share:

PAPA FRANCIS AFANYIWA OPERESHENI BAADA YA KULAZWA

PAPA FRANCIS

Papa Francis

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko, Jumapili tarehe 4 Julai 2021 majira ya jioni alilazwa kwenye Hospitali ya Gemelli iliyoko mjini Roma kwa ajili ya kufanyia operesheni kubwa kwenye utumbo mpana.

 Operesheni hii imeongozwa na Prof. Sergio Alfieri huku akisaidiwa na Prof. Luigi Sofo, Prof. Antonio Tortorelli pamoja na Prof. Roberta Menghi. Wengine katika jopo hili la madaktari ni Prof. Massimo Antonelli, Prof. Liliana Sollazzi pamoja na Madaktari Roberto De Cicco na Maurizio Soave. Kwenye chumba cha upasuaji, walikuwepo pia Prof. Giovanni Battista Doglietto pamoja na Prof. Roberto Bernabei.

Taarifa ya madaktari wa Hospitali ya Gemelli inaonesha kwamba, operesheni hii imefanikiwa na Baba Mtakatifu Francisko anaendelea vyema. Kama kawaida yake katika hali ya unyenyekevu, Baba Mtakatifu Francisko, baada ya sala ya Malaika wa Bwana kwenye Uwanja wa Kanisa kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican, Jumapili tarehe 4 Julai 2021 majira ya jioni alipelekwa Hospitalini Gemelli kama wagonjwa wengine na kulazwa ghorofa ya 10 katika chumba ambazo kwa muda mrefu Mtakatifu Yohane Paulo II alikitumia wakati wa matibabu hospitalini hapo. Prof. Sergio Alfieri, mwenye umri wa miaka 55 ndiye daktari mkuu wa kitengo cha magonjwa ya mfumo wa chakula.

Takwimu zinaonesha kwamba, kama daktari amekwisha kufanya operesheni za magonjwa ya mfumo wa chakula zipatazo 9, 000 tangu mwaka 2010. Prof. Sergio Alfieri ni kati ya wanafunzi waliofundwa na kufundika kutoka katika Jopo la Madaktari bingwa Francesco Crucitti, ambaye katika historia anatambulikana kama Daktari aliyemfanyia Mtakatifu Yohane Paulo II, operesheni tatu. Alifundwa pia na Profesa Giovanni Battista Doglietto. Radio Vatican itaendelea kukujuza yale yanayojiri katika afya ya Baba Mtakatifu Francisko ambaye kwa sasa anapumzika Hospitalini Gemelli baada ya kufanyiwa upasuaji mkubwa kwenye utumbo mpana.

Share:

MAZISHI YA TB JOSHUA KUFANYIKA IJUMAA JULAI 11... TUKIO LA KUWASHA MISHUMAA KUPEPERUSHWA LIVE

Maelezo ya picha,TB Joshua
Temitope Balogun JoshuaJe maarufu TB Joshua

Tukio la kuwasha mishumaa litaanzisha utararibu wa mazishi ya aliyekuwa muhubiri mashuhuri wa Nigeria, na muasisi wa kanisa la Synagogue Church of All Nations (SCOAN) aliyefariki mwezi uliopita.

Mchungaji TB Joshua alifariki tarehe 5 Juni,2021 akiwa na umri wa miaka 57, siku chache kabla ya kuadhimisha siku yake ya kuzaliwa.

 Mazishi yake yanatarajiwa kuwa ya faragha Ijumaa Julai 11, 2021.

Hata hivyo kanisa lake bado halijafichua ni nini kilichosababisha kifo chake.

Taarifa iliyotolewa na kanisa lake - Synagogue Church of All Nations imesema: "Mungu amemchukua mtumishi wake Nabii TB Joshua nyumbani - sawa na mapenzi yake. Aliutumia muda wake wa mwisho duniani katika huduma ya Mungu. Alifanya alichopaswa kufanya, akakiishi na amekufa kwa ajili yake ."

"Nabii TB Joshua ameacha urithi wa huduma na kujitolea kwa ajili ya ufalme wa Mungu ambao utaendelea kuishi kwa vizazi ambavyo havijazaliwa ."

Mchakato wa kuwasha mishumaa utakuwa utakuwa ni sherehe ya kibinafsi , limesema kanisa la Synagogue Church of All Nations.

Tukio hilo linatarajiwa kuanza saa kumi na mbili unusu jioni Jumatatu kwa saa za Nigeria.

Litapeperushwa pia moja kwa moja kwenye chaneli ya TV ya kanisa hilo.

Kulingana na taarifa hiyo Kanisa hilo limewataka watu kubeba mishumaa kama ishara ya kuungana katika mpango wa ‘’kumheshimu’’ mtumishi wa Mungu - TB Joshua."

Chanzo - BBC Swahili
Share:

KAMPUNI YA MADINI YA BARRICK, WAJASIRIAMALI WANAOISHI JIRANI YA MGODI WA BULYANHULU WASHIRIKI MAONYESHO YA BIASHARA YA SABASABA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mh.Dk.Philip Mpango (wa pili kutoka kulia) akipita katika banda la Barrick wakati alipotembelea maonesho ya Sabasaba.
***
Kampuni ya madini ya Barrick, inashiriki katika maonesho ya 45 ya kimataifa ya Biashara (SabaSaba) yanayoendelea jijini Dar es Salaam, ambapo banda lake la maonesho linaendelea kutembelewa na viongozi mbalimbali wa Serikali pamoja na wananchi ambao wanapata fursa ya kuelewa kwa undani shughuli za kampuni hiyo.

Mbali na ushiriki kampuni ya Barrick, pia imewezesha wajasiriamali kutoka vijiji vinavyozunguka mgodi wa Bulyanhulu uliopo mkoani Shinyanga, kwa ajili ya kuonesha bidhaa zao kwa lengo la kupata masoko zaidi na kupata maarifa kutoka kwa wajasiriamali wengine wanaoshiriki kwenye maonesho hayo.

Barrick imekuwa ikiwezesha wajasiriamali hao kwa kuwapatia elimu ya ukuzaji biashara zao, na kwa wale wanaoshughulika na kilimo wamekuwa wakipatiwa mbegu bora na mbolea.
Waziri wa Madini, Mh.Doto Biteko, akipatiwa maelezo ya shughuli za kampuni ya Barrick, kutoka wa wafanyakazi wa kampuni hiyo alipotembelea banda la kampuni hiyo katika maonyesho ya Sabasaba
Waziri wa Madini, Mh.Doto Biteko, akipatiwa maelezo ya shughuli za kampuni ya Barrick, kutoka wa wafanyakazi wa kampuni hiyo alipotembelea banda la kampuni hiyo katika maonyesho ya Sabasab
Waziri wa Madini, Mh.Doto Biteko, akipatiwa maelezo ya shughuli za kampuni ya Barrick, kutoka wa wafanyakazi wa kampuni hiyo alipotembelea banda la kampuni hiyo katika maonyesho ya Sabasab
Wafanyakazi wa Barrick katika banda la wajasiriamali kutoka Bulynhulu wanaoshiriki maonyesho ya biashara ya SabaSaba kwa ufadhili wa kampuni hiyo.
Share:

English Teacher Secondary level at Dar es Salaam Independent School

English Teacher Secondary level    DAR ES SALAAM INDEPENDENT SCHOOL Registration Numbers S. 2544 and DS/02/7/037 VACANCIES FOR THE SCHOOL YEAR 2021/22 We need the following staff to start in AUGUST 2021: SECONDARY: Position Title: English Teacher ALL TEACHERS APPLYING FOR POSITIONS AT DIS should have   At least five years teaching experience. Experience of Cambridge […]

This post English Teacher Secondary level at Dar es Salaam Independent School has been posted by Udahiliportaldaily

Get more post by visiting Udahiliportal.com

know more details about Udahiliportal.com by visiting Udahiliportal.com - Find Jobs & Ajira mpya leo, ajira portal Tanzania, ajira yako, brighter Monday, mabumbe, mwananchi ajira, secretariet ya ajira, tamisemi ajira za afya, wizara ya afya, ajira Tanzania - selection za vyuo , selection, second selection vyuo, second selection, tamisemi selection, selection form one 2020/2021

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

Share:

Mathematics Teacher Primary level at Dar es Salaam Independent School

Mathematics Teacher Primary level     DAR ES SALAAM INDEPENDENT SCHOOL Registration Numbers S. 2544 and DS/02/7/037 VACANCIES FOR THE SCHOOL YEAR 2021/22 We need the following staff to start in AUGUST 2021: PRIMARY: Position Title: Mathematics Teacher ALL TEACHERS APPLYING FOR POSITIONS AT DIS should have   At least five years teaching experience. Experience of Cambridge […]

This post Mathematics Teacher Primary level at Dar es Salaam Independent School has been posted by Udahiliportaldaily

Get more post by visiting Udahiliportal.com

know more details about Udahiliportal.com by visiting Udahiliportal.com - Find Jobs & Ajira mpya leo, ajira portal Tanzania, ajira yako, brighter Monday, mabumbe, mwananchi ajira, secretariet ya ajira, tamisemi ajira za afya, wizara ya afya, ajira Tanzania - selection za vyuo , selection, second selection vyuo, second selection, tamisemi selection, selection form one 2020/2021

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

Share:

Mathematics Teacher Secondary level at Dar es Salaam Independent School

Mathematics Teacher Secondary level     DAR ES SALAAM INDEPENDENT SCHOOL Registration Numbers S. 2544 and DS/02/7/037 VACANCIES FOR THE SCHOOL YEAR 2021/22 We need the following staff to start in AUGUST 2021: SECONDARY: Position Title: Mathematics Teacher ALL TEACHERS APPLYING FOR POSITIONS AT DIS should have   At least five years teaching experience. Experience of Cambridge […]

This post Mathematics Teacher Secondary level at Dar es Salaam Independent School has been posted by Udahiliportaldaily

Get more post by visiting Udahiliportal.com

know more details about Udahiliportal.com by visiting Udahiliportal.com - Find Jobs & Ajira mpya leo, ajira portal Tanzania, ajira yako, brighter Monday, mabumbe, mwananchi ajira, secretariet ya ajira, tamisemi ajira za afya, wizara ya afya, ajira Tanzania - selection za vyuo , selection, second selection vyuo, second selection, tamisemi selection, selection form one 2020/2021

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

Share:

Financial Accountant Officer at Caliber First Group Limited

JOB TITLE:  Financial Accountant Officer (Immediately) JOB LOCATION: Dar Es Salaam Tanzania Company Name: Caliber First Group Limited (CFGL) Caliber First Group Limited (CFGL) seeks a Financial Accountant Officer. S/he will play a key role in finance and accountants management and ensure that staff and management receive high quality, professional and responsive services. S/he will also implement […]

This post Financial Accountant Officer at Caliber First Group Limited has been posted by Udahiliportaldaily

Get more post by visiting Udahiliportal.com

know more details about Udahiliportal.com by visiting Udahiliportal.com - Find Jobs & Ajira mpya leo, ajira portal Tanzania, ajira yako, brighter Monday, mabumbe, mwananchi ajira, secretariet ya ajira, tamisemi ajira za afya, wizara ya afya, ajira Tanzania - selection za vyuo , selection, second selection vyuo, second selection, tamisemi selection, selection form one 2020/2021

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

Share:

Embroidery Machine Operators at Caliber First Group Limited

JOB TITLE:  EMBROIDERY-MACHINE OPERATORS (5) POSTS – FREE LANCERS JOB LOCATION: Dar es Salaam Tanzania Company Name: Caliber Publishers Caliber Publishers deals with printing services of all promotional items. Its services cut across Embroidery, digital printing, Offset printing, large format printing among others. It has been in operations since 2017, and is growing its market shares and Customers […]

This post Embroidery Machine Operators at Caliber First Group Limited has been posted by Udahiliportaldaily

Get more post by visiting Udahiliportal.com

know more details about Udahiliportal.com by visiting Udahiliportal.com - Find Jobs & Ajira mpya leo, ajira portal Tanzania, ajira yako, brighter Monday, mabumbe, mwananchi ajira, secretariet ya ajira, tamisemi ajira za afya, wizara ya afya, ajira Tanzania - selection za vyuo , selection, second selection vyuo, second selection, tamisemi selection, selection form one 2020/2021

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive

Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger