Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano kwa Umma wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Semu Mwakyanjala, amesema matumizi ya bei mpya ya vifurushi yamesitishwa kwa muda akieleza kuwa uamuzi huo utahusu vifurushi vya data pekee huku vile vya ujumbe mfupi wa maneno na kupiga zitaendelea kama ilivyotangazwa leo.
Friday, 2 April 2021
SERIKALI YATANGAZA KUSITISHA BEI MPYA ZA BANDO 'VIFURUSHI' VILIVYOZUA GUMZO LEO
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano kwa Umma wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Semu Mwakyanjala, amesema matumizi ya bei mpya ya vifurushi yamesitishwa kwa muda akieleza kuwa uamuzi huo utahusu vifurushi vya data pekee huku vile vya ujumbe mfupi wa maneno na kupiga zitaendelea kama ilivyotangazwa leo.
ONGEZEKO VIFURUSHI 'BANDO' KILIO KILA KONA... STEVE NYERERE ATAKA WAZIRI ASEME WALAU NENO MOJA TU
FUNDI AFARIKI KWA KUPIGWA SHOTI AKICHOMELEA GARI
TAZAMA HAPA FILAMU YA YESU KWA LUGHA YA KISUKUMA (The Jesus Film - Sukuma / Kisukuma Language (Tanzania)
GEKUL AHAIDI KUIMARISHA USHIRIKIANO KWA WADAU WA TASNIA YA HABARI NCHINI
Rais Samia Suluhu Hassan akimwapisha Pauline Gekul kuwa Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo katika hafla iliyofanyika katika Ikulu ya Chamwino Jijini Dodoma jana.
Waziri wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Innocent Lugha Bashungwa (asiye na Miwani) akizungumza na Viongozi Wakuu wa Wizara; kushoto ni Naibu wake Mhe. Pauline Gekul, kulia ni Katibu Mkuu na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbas na wa kwanza ni Naibu Katibu Mkuu, Dkt. Ally Possi, mara baada ya hafla ya uapisho iliyofanyika katika Ikulu ya Chamwino Jijini Dodoma jana.Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Pauline Gekul na Naibu Katibu Mkuu, Dkt. Ally Possi (katikati) na Mkurugezi wa Utawala wa Wizara hiyo Bernard Marcelline mara baada ya hafla ya uapisho iliyofanyika katika Ikulu ya Chamwino Jijini Dodoma jana.
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Pauline Gekul akizungumza na Katibu Mkuu na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbas(mwenye suti ya bluu) na Naibu Katibu Mkuu, Dkt. Ally Possi, mara baada ya hafla ya uapisho iliyofanyika katika Ikulu ya Chamwino Jijini Dodoma jana.
· Bashungwa amshukuru Mhe.Rais
Na John Mapepele, Dodoma
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Pauline Gekul ameahidi kuimarisha ushirikiano kwa wadau wa tasnia za Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ili kutimiza ahadi za Ilani ya Chama cha Mapinduzi na ahadi alizozitoa Mheshimiwa, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan wakati wa Kampeni za Uchaguzi Mkuu mwaka 2020.
Mhe. Gekul ameyasema haya muda mfupi baada ya kuapishwa kuwa Naibu Waziri kwenye tasnia hizo na Mhe. Rais kwenye Ikulu ya Jijini Dodoma jana ambapo amewahakikishia wadau wote nchini kuendeleza ushirikiano ili kuleta mapinduzi makubwa katika Wizara hiyo kwa kushirikiana na Waziri mwenye dhamana hiyo Mhe. Innocent Bachungwa.
“ Nitatoa ushirikiano kwa Waziri wangu lakini pia kwa wadau wote wa tasnia hii ya Wizara yetu ili kuhakikisha michezo, utamaduni, habari, Sanaa kila jambo liende kulingana na ahadi alizotoa mama yetu mpendwa Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan ” amesisitiza Gekul
Amesema katika kutenda kazi hii mpya pia atazingatia miongozo aliyoitoa Mhe. Rais kwenye hotuba yake awali ambapo alielekeza mambo mahususi ya kuyafanyia kazi.
Akizungumzia uteuzi wa Naibu Waziri Gekul mara baada ya kukamilisha zoezi la kuwaapisha Katibu Mkuu Kiongozi, Mawaziri na Manaibu Mawaziri, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan amesema. “Nimemtoa Wizara ya Mifugo, pengine anajua mambo ya mifugo mifugo, lakini nikaona aende kwenye michezo awasaidie wanawake”
Amesema wanawake wamefanikiwa kuleta vikombe vitatu hapa nchini na hawatajwi kama ilivyo kwa upande wa wanaume ambapo ameeleza kuwa awali yeye ndiye alipewa kazi hiyo kwenye kipindi cha kwanza cha Awamu ya Tano na Hayati, Rais Magufuli hivyo amempa Mhe. Gekul kwa matarajio makubwa.
Amefafanua kuwa wanawake wamekuwa akifanya vizuri kwenye michezo mbalimbali hivyo aende akasimamie hilo kikamilifu
“Wanawake kwenye michezo wanafanya vizuri, hawasifiwi lakini wanaume wakishinda tu, katia goli huku viwanja vinagawiwa” ameongeza Mhe. Rais Samia.
Naye Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Innocent Bashungwa amemshukuru Mhe. Rais kwa kuwa na Imani nao na kuendelea kuwateua kusimamia tasnia hizo na kumuahidi kufanya kazi kwa ushirikiano, uadilifu na ubunifu mkubwa ili kutimiza ahadi za Serikali kwa wananchi wake.
“Kipekee ninamshukuru sana Rais wangu, Mama Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutuamini naomba kumhakikishia kuwa tutafanya kazi bila kuchoka na kwa ushirikiano mkubwa baina yetu sote, sisi na wadau wetu wote ili kukamilisha ahadi katika kipindi kifupi” ameongeza Mhe. Bashungwa
WANANCHI NYALIGONGO WAKABIDHI MSAADA WA MADAWATI SHULENI, DC MBONEKO AONYA WAZAZI KURUBUNI WATOTO KUFELI MTIHANI
ICT OFFICER II at Tanzania Tobacco Board
This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content
RE: ADVERTISEMENT OF TRANSFER VACANCIES Ref. No. TTB/P.3/VOL.II/143 Introduction The Tanzania Tobacco Board (TTB) invites applications from suitably qualified Public Servants who wish to transfer their employment to fill 8 vacant posts in various post/designations. Establishment of TTB The history of TTB goes back to 1960’s during the then Tanganyika Tobacco Board. In 1970 the […]
This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details
RECORDS MANAGEMENT ASSISTANT II 3 posts at Tanzania Tobacco Board

PERSONAL SECRETARY II at Tanzania Tobacco Board

Chief, Procurement, P-4 at IRMCT
This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content
Org. Setting and Reporting This position is located in the Arusha branch of the Mechanism. The incumbent reports to the Chief Administrative Officer. Responsibilities Within delegated authority the incumbent will be responsible for the following duties: • Serves as a senior procurement and contracting expert with responsibility for the supervision of a geographically separated team […]
This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details
Project Executant at WWF
This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content
VACANCY: PROJECT EXECUTANT – CORAL REEF RESCUE INITIATIVES (CRRI) & FISHERIES WWF is seeking to hire a competent and motivated Project Executant – Coral Reef Rescue Initiatives (CRRI) & Fisheries for its office in Tanzania, based in Dar es salaam. Main Tasks Under the technical guidance of Marine Programme Coordinator, The Project Executant-Coral Reef Initiative will […]
This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details
VIJANA WA KIUME WADAI UCHUMI WA NG’OMBE UNACHOCHEA NDOA UTOTONI
Picha ya ng'ombe
Na Deogratius Temba, Kahama
Vijana wameaswa kutafuta vyanzo mbadala vya uwekezaji ili kujukwamua kimaisha badala ya kutegemea kuwaoza wasichana wa shule ili wapate mahari ya ng’ombe.
Wakizugungumza katika mdahalo wa wanaume juu kubadili mtazamo na mila na desturi zinazochangia Ukatili wa Kijinsia, katika kata za Shilela na Lunguya , Halmashauri ya wilaya ya Msalala, ulioendeshwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), kwa kushirikiana na Halmashauri ya Msalala na Shirika la Kimataifa la Idadi ya watu (UNFPA), wanaume kutoka katika vikundi mbalimbali zaidi ya 300 waliokutana katika mdahalo huo, wamesema jamii inahitaji mabadiliko makubwa ya kimtazamo ili kuondokana dhana ya uchumi wa ng’ombe na kuwekeza katika sekta nyingine za uzalishaji mali.
Akizungumza mwezeshaji kutoka TGNP, Deogratius Temba, aliwaasa vijana kuunda vikundi vya kuweka akiba na kukopeshana, kujifunza ujasiriamali na kuchukua mikopo ya uwezeshaji vijana ya asilimia nne (4) inayotolewa na Halmashauri ili kuwa na vyanzo vyao wenyewe vya mapato badala ya kutegemea ng’ombe wa wazazi kulipia mahari pindi wanapotaka kuoa.
Katika mjadala huo, vijana walidai kuwa wakati mwingine, wasichana wadogo wanasukumwa kuolewa ili mahari yatakayopatikana yasaidie kumlipia kaka yake mahari kutokana na vijana wa kiume kutokuwa na fedha au kutokumiliki ng’ombe wa kutosha kulipa mahari.
“Unajua hapa kwetu, kama kuna msichana nyumbani, sisi vijana wa kiume tunaomba ajitokeze mtu wa kumlipia mahari ili sehemu ya ng’ombe wake tupewe nasisi tukalipe mahari… sasa kama kijana huna kazi, ajira huna, unategemea utapata wapi mahari?” alisema Fautine Shau (32) mkazi wa kata ya Lunguya.
Kwa upande wake Mtendaji wa kata ya Lunguya, Lusajo Manase, aliwaasa vijana kuhakikisha wanasimama imara katika kubalidili mtazamo, kuacha kurithi mila na desturi ambazo zinasababusha vitendo vya udhalilishaji na ukatili wa kijinsia.
“Tunayo bahati ya kipekee kukutana na nyie vijana wa kiume wa kata yetu. Hawa wenzetu wamekuja ili tubadilishane mawazo, tuboreshe mahusiano yetu ili tukitoka hapa tuwe na mkakati unaotekelezeka wa kutokomeza kabisa Ukatili wa Kijinsia”, alisema Lusajo.
Shabaha za kiutendaji kwa Mpango Kazi wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili wa Kijinsia (MTAKUWWA), ni Kuongeza uwiano wa halmashauri zenye programu za kijamii za kuzuia ukatili dhidi ya wanawake kutoka asilimia 0 hadi asilimia 20, Kuongeza uwiano wa wanakaya wenye umri kati ya miaka 15-49 waliopata taarifa kuhusu ukatili dhidi ya wanawake, kutoka asilimia 0 hadi asilimia 55 (iv) Kupunguza ukatili wa kingono kutoka asilimia 17.2 hadi asilimia 8.
Aidha ni kupunguza ukatili wa kimwili dhidi ya wanawake wenye umri kati ya miaka15-49 toka asilimia 39 hadi asilimia 10 na kupunguza ukatili wa kihisia kutoka asilimia 36.3 hadi asilimia 18.
Sambamba na kupunguza ukatili dhidi ya Watoto unaosababishwa na mila na desturi kama mimba za utotoni kutoka asilimia 27 hadi asilimia 5, Kupunguza kiwango cha ukeketaji kutoka asilimia 32 hadi asilimia 11 na Kupunguza ndoa za utotoni kutoka asilimia 47 hadi asilimia 10.
Regional Emergency Director – Great Lakes at International Rescue Committee
This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content
Requisition ID: req14096 Job Title: Regional Emergency Director – Great Lakes Sector: Emergency Response Employment Category: Fixed Term Employment Type: Full-Time Open to Expatriates: Yes Location: Dar es Salaam, Tanzania Job Description This role can be based in Tanzania, Burundi, Central African Republic or DRC. As Regional Emergency Director (RED), you will provide strategic and operational leadership to building emergency […]
This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details
UFUNGUO PROJECT MANAGER at UNDP
This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content
Background UNDP Tanzania’s inclusive growth programme 2016 – 2021. The overarching goal is to support Tanzania to accelerate inclusive economic growth with a focus on poverty reduction, job creation and environmental sustainability, in line with the principal objectives set out in the Tanzania Development Vision 2025 and Zanzibar Vision 2020, which aim to eradicate extreme […]
This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details
Senior Accountant at Pathfinder International
This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content
Pathfinder Overview Pathfinder International is driven by the conviction that all people, regardless of where they live, have the right to decide whether and when to have children, to exist free from fear and stigma, and to lead the lives they choose. Since 1957, we have partnered with local governments, communities, and health systems in […]
This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details
Thursday, 1 April 2021
JESHI LA POLISI TANZANIA: HATUTEGEMEI KUONA SHEREHE NA SHAMRASHAMRA ZOZOTE SIKUKUU HII YA PASAKA
Kama mnavyofahamu Taifa letu bado lipo kwenye siku 21 za maombolezo baada ya kifo cha aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Dkt John Pombe Joseph Magufuli. Pamoja na tukio hilo kubwa la majonzi napenda kuwajulisha kuwa hali ya ulinzi na usalama nchini ni shwari ingawa kuna matukio machache ya kiuhalifu wa kijinai na ajali za usalama barabarani zilizotokea ambapo kwa pamoja yanaendelea kushughulikiwa na baadhi ya wahalifu waliohusika kutenda matukio hayo wameshakamatwa.
Ndugu Wanahabari,
Kufuatana na kalenda ya kila mwaka, inapofikia wakati kama huu waumini wa dini ya kikristu husheherekea sikukuu ya Pasaka. Sikukuu hiyo hutanguliwa na mfungo na unapokaribia kumalizika juma la mwisho huwa na ibada mbalimbali ikiwa ni pamoja na ibada ya Ijumaa Kuu, Jumamosi ibada ya usiku na Jumapili ambayo ndiyo sikukuu ya Pasaka tarehe 4.4.2021. Siku hizi tatu waumini wa dini za kikristu hukusanyika kwa wingi katika nyumba za ibada kwa ajili ya sala.
Nipende kuwajulisha kuwa Jeshi la Polisi nchini limejipanga vizuri kuhakikisha kuwa waumini hao wanashiriki ibada hizo katika mazingira ya amani, utulivu na usalama na hata wananchi wengine kuendelea na shughuli zao kama kawaida.
Wito wa Jeshi la Polisi Tanzania ni kuomba ushirikiano kutoka katika kamati za ulinzi na usalama katika nyumba za ibada na sehemu zingine katika suala zima la kudumisha amani, ulinzi na usalama.
Ndugu Wanahabari,
Aidha, tunatoa rai na maelekezo kwa waendesha vyombo vya moto na watumiaji wote wa barabara kuzingatia sheria za usalama barabarani ili kuepuka ajali ambazo kutokana na tafiti mbalimbali zilizowahi kufanyika zimeonyesha asilimia 75 ya ajali zinachangiwa na uzembe wa binadamu. Ajali zinaweza kuepukika kwa kiasi kikubwa kama kila mwananchi atafuata na kuzingatia sheria za usalama barabarani ikiwa ni pamoja na kuepuka mwendo kasi,kutumia kilevi wakati wa kuendesha chombo cha moto, kutokuzingatia alama za tahadhari za barabarani, kutokuvaa kofia ngumu (helmet) na kupakia mishikaki .
Makamanda wa Polisi wa Mikoa na Vikosi wameshajipanga vizuri kuhakikisha hali ya usalama inaendelea kuimarika na kuwachukulia hatua kali wale wote watakaovunja sheria za usalama barabarani katika kipindi hiki kwani Makao Makuu ya Polisi imeshawapatia maelekezo na mikakati ambayo kila mmoja ataitekeleza kulingana na mazingira ya eneo lake na mipango ya kamati za usalama za himaya husika.
Tuna imani kama kila mwananchi atazingatia na kufuata sheria na kujiepusha na vishawishi vya kufanya vitendo vya kihalifu, ibada za Pasaka zitamalizika salama tukizingatia kuwa bado tupo katika kipindi cha maombolezo na hatutegemei zile sherehe na shamrashamra tulizozizoea kipindi cha miaka ya nyuma kuwepo katika kipindi hiki.
Ahsanteni kwa kunisikiliza.
Imetolewa na:
David A. Misime – SACP
Msemaji wa Jeshi la Polisi
Makao Makuu ya Polisi
Dodoma, Tanzania.