Saturday, 21 November 2020

Waziri Mkuu atoa siku 15 kukamilika kwa Hospitali ya Uhuru


Na. Angela Msimbira OR-TAMISEMI

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Mjaliwa (Mb) ametoa siku 15 kwa Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino, Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) na Suma JKT kuhakikisha ujenzi wa Hospitali ya Uhuru unakamilika ifikapo disemba 5, 2020.

Akikagua maendeleo ya ujenzi wa Hospitali hiyo jana Jijini Dodoma Mhe. Majaliwa amesema Hospitali ya Uhuru ni moja kati ya miradi ya kimkakati ya Serikali ya Awamu ya Tano ya kuimarisha utoaji huduma katika Sekta ya afya ambayo inaanzia kuboresha kuanzia ngazi ya zahanati, vituo vya Afya, Hospitali za Wilaya, Hospitali za Rufaa na Hospitali za Magonjwa makubwa.

Anaendelea kufafanua kuwa Serikali imekuwa mstari wa mbele kuhakikisha inaboresha huduma za afya kwa lengo la kutoa huduma bora kwa wananchi, hivyo imejikita katika kuhakikisha miradi yote ya kimakakati inakamilika kwa wakati ili ianze kutumika

“ Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino, Wakala wa majengo (TBA), Suma JKT, hakikisheni ujenzi wa Hospitali hii unakamilika kwa wakati, fanyeni kazi usiku na mchana, jengeni vibanda na kuhamia kwenye eneo la ujenzi, ongezeni wafanyakazi ili kukamilisha ujenzi kwa wakati uliopangwa” amesisitiza Mhe. Majaliwa

Mhe. Majaliwa amesema miradi ya Kimakakati inatakiwa ikamilike kwa wakati na Watanzania wanahamu ya kuona miradi inakamilika na kuanza kutoa huduma hivyo fanyeni kazi kwa weledi ili kuweza kukamilisha ujenzi wa Hospitali hiyo muhimu kwa jamii

Akitoa taarifa ya maendeleo ya ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Chamwino, Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhandisi Joseph Nyamhanga amesema ujenzi wa Hospitali ya Uhuru imekadiriwa kutumia zaidi ya shilingi bilioni 3.995 na kiasi kilichotengwa ni shilingi bilioni 3.410 ambapo zaidi ya shilingi milioni 995 zilikuwa ni fedha za maadhimisho ya siku ya uhuru wa Tanganyika na shilingi bilioni 2.415 ni gawio la kampuni ya simu ya Airtel.

Naye Msaidizi wa Mkuu wa JKT Colonel Laurence Angelo Lupenge amesema mradi wa ujenzi wa Hospitali ya Uhuru umefikia asilimia 92 na kazi zilizofanyika ni kusafisha eneo la mradi,kuchimba na kujenga msingi, kujenga “frame” ya jengo pamoja na kuta, kupiga “plaster” kuta pamoja na” skimming”, kuweka njia za mifumo ya umeme,kupaua na kufunga gypsum board,kuchimba mashimo ya maji taka na kuweka “rough floor” kwa ajili ya kuweka vigae




Share:

MFUMO WA KUUZA NA KUNUNUA HISA KWA NJIA YA SIMU ZA MKONONI WAZINDULIWA


Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka hiyo, CPA Nicodemus Mkama akizundua mfumo wa kuuza na kununua hisa kwa njia ya simu za mkononi katika Soko la Hisa la Dar es Salaam leo jijini Dar Es Salaam.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka hiyo, CPA Nicodemus Mkama akizungumza mbele ya Wageni waaalikwa wakati wa kuzindua mfumo wa kuuza na kununua hisa kwa njia ya simu za mkononi katika Soko la Hisa la Dar es Salaam leo jijini Dar Es Salaam.
Baadhi ya Wageni waalikwa mbalimbali wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri wakati wa uzinduzi huo leo jijini Dar es salaam

Na Mwandishi Wetu, Michuzi TV

MAMLAKA ya Masoko ya Mitaji na Dhamana(CMSA)imezindua mfumo wa kuuza na kununua hisa kwa njia ya simu za mkononi katika Soko la Hisa la Dar es Salaam huku ikiwataka watanzania wote waliopo ndani na nje ya nchi kutumia mfumo huo mpya kwani sasa huduma imeletwa mikononi mwetu kupitia Hisa Kiganjani.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa mfumo huo, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka hiyo, CPA Nicodemus Mkama amesema mfumo wa hisa kiganjani ni matokeo chanya ya ushirikiano wa wadau katika sekta ya masoko ya mitaji, wenye lengo la kuunga mkono juhudi za Serikali ya awamu ya tano chini ya uongozi madhubuti wa Rais John Magufuli kuhakikisha wanawezesha wananchi wetu kiuchumi kwa kuwafikishia huduma popote walipo, mijini na vijijini, hivyo kuinua vipato vyao hususani wananchi wenye kipato cha chini.

Aidha mfumo huu ni matokeo ya utekelezaji wa mpango mkakati wa Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) na Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA) yenye lengo la kufikisha huduma kwa wanchi wengi zaidi hususani wa kipato cha chini walio vijijini ambapo huduma hii hapo awali ilikuwa haipatikani. 

Amesema hatua hiyo ni muhimu kwani inatarajia kuongeza idadi ya wawekezaji katika masoko ya mitaji na kuchangia utekelezaji wa Mpango Jumuishi wa Huduma za Kifedha hapa nchini yaani National Financial Inclusion Framework.

"Ninayo furaha kutamka mfumo wa uuzaji hisa kwa kutumia simu za mkononi umeidhinishwa na Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana baada ya kukidhi matakwa ya kisheria, vigezo na kanuni za usimamizi wa masoko ya mitaji ikiwa ni pamoja na kanuni za usimamizi wa masoko ya mitaji kimataifa zinazotolewa na Taasisi ya Usimamizi wa Masoko ya Mitaji Ulimwenguni yaani International Organisation for Securities Commission (IOSCO).

"Kwa mantiki hiyo, napenda kutumia fursa hii kuipongeza Bodi na Menejiment ya Soko la Hisa la Dar es Salaam kwa kufanikisha shughuli za uundwaji wa mfumo huu. Nawapongeza pia wote waliohusika katika kufanikisha uundwaji wa mfumo huu ikiwa ni pamoja na Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA), Idara ya Malipo Mtando (GePG), Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Taaasi ya Kuendeleza Sekta ya Fedha (FSDT), Kampuni ya MagillaTech, Benki washirika na Kampuni za Simu, na wengine wote walioshiriki kwa namna moja au nyingine,"amesema.

Ameongeza uwepo wa Mfumo wa Kuuza na Kununua Hisa kwa Kutumia Simu za Mkononi unatarajiwa kuleta matokeo chanya katika kujenga Sekta Jumuishi ya Fedha. Kwa mujibu wa utafiti wa Finscope Tanzania wa mwaka 2017, zaidi ya asilimia 60 ya watu wazima wanatumia huduma za fedha kwa njia ya simu za mkononi. 

Aidha amesema kwa mujibu wa takwimu za Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) za kipindi cha robo mwaka kilichoishia Septemba 2020, idadi ya watanzania wanaotumia simu za mkononi ni milioni 49.2 na watanzania wanaotumia huduma za fedha kwa njia ya simu ni milioni 30.5 ambapo thamani ya miamala katika kipindi hicho ilikuwa Shilingi trilioni 11.5 yenye wastani wa Shilingi 377,795 kwa kila muamala. 

"Inatarajiwa uwepo wa mfumo wa kuuza na kununua hisa kwa njia ya simu za mkononi kutawavutia wananchi wanaofanya miamala hii kuwekeza sehemu ya fedha hizi kwenye soko la hisa, na hivyo kufanikisha utekelezaji wa Mpango wa Sekta ya Masoko ya Mitaji katika Mpango wa Kitaifa wa Huduma Jumuishi za Kifedha 2018 – 2022 unaolenga kuongeza kwa asilmia 50, wawekezaji katika masoko ya mitaji. 

"Kwa kuwa mfumo huu unatarajia kuwezesha kuongezeka kwa miamala katika Soko la hisa, inatarajiwa kwamba ukwasi wa Soko la hisa utaongezeka. Ukwasi mkubwa wa Soko ni kiashiria muhimu cha ubora wa soko kinachovutia wawekezaji wengi wa ndani na wa kimataifa,"amesema

Ameongeza Mfumo huo wa Hisa Kiganjani unatarajiwa kuongeza mchango katika jitihada za kuongeza uelewa na elimu ya fedha kwa umma, zinazofanywa na DSE na CMSA. Baadhi ya jitihada hizo ni pamoja na mipango ya Shindano la Masoko ya Mitaji Kwa Wanafunzi wa Vyuo Vikuu na Taasisi za Elimu ya Juu .Shindano la Uwekezaji kwa Wanafunzi linaloendeshwa na Soko la Hisa la Dar es Salaam; na Mpango wa DSE wa Kuendeleza Biashara yaani the DSE Enterprise Acceleration Program.Matumizi ya Mfumo huu yatawezesha kufikiwa kwa haraka zaidi kwa malengo ya mipango hii. 

Ametoa rai kwa soko la Hisa na Wadau wote katika Masoko ya Mitaji kuhakikisha kuwa mfumo huu unaleta tija na manufaa yafuatayo yakiwemo ya kupunguza gharama za shughuli za uwekezaji, kuondoa changamoto ya ulazima wa wawekezaji kuwa karibu na Soko au watoa huduma za kununua na kuuza hisa.

Pia kuongeza hamasa ya uwekezaji kwa kundi la vijana ambao ndio wengi katika jamii, kuwezesha Watanzania waliopo nje ya nchi kushiriki katika uwekezaji hapa nyumbani na kujenga utamaduni wa wananchi kuwekeza kutokana na urahisi wa namna ya kuwekeza katika soko la hisa.
"Ili kufikia malengo hayo, natoa mwito kwa Uongozi wa Soko la Hisa la Dar es Salaam na kampuni zote zenye leseni kutoka Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana kuhamasisha matumizi ya Mfumo huu ikiwa ni pamoja na kuingiza elimu ya matumizi yake kwenye mipango yao ya kila mwaka ya elimu kwa umma.

"Napenda kutumia fursa hii kuwataka watanzania wote, waliopo ndani na nje ya nchi, kutumia mfumo huu mpya kwani sasa huduma imeletwa mikononi mwetu kupitia HISA KIGANJANI. Kama sote tunavyoolewa matumizi ya huduma za kifedha ni moja ya nyenzo kuu ya kupata maendeleo ya mtu mmoja na Taifa kwa ujumla. 

"Muitikio wa Watanzania utaleta hamasa kwa Serikali na Wadau wake ikiwa ni Pamoja na Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana katika kuongeza juhudi zaidi katika kutafuta mbinu bora zaidi za huduma na bidhaa za masoko ya hisa kwa Wananchi,"amesema.

Ametoa msisitizo kwa Soko la Hisa, Taasisi zinazotoa huduma katika soko la hisa, na Wadau wa Sekta ya Masoko ya Mitaji kuwa Dunia hivi sasa ipo kwenye Mapinduzi ya Nne ya Viwanda.

"Shughuli nyingi ulimwenguni na kimataifa, kwa sasa, zinafanyika kwa kutumia TEHAMA. Hivyo basi, wadau wote wa sekta ya masoko ya mitaji wanapaswa kwenda na kasi hiyo ya kukua kwa sekta ya mawasiliano ya Tehama. Kwa mantiki hiyo wadau wote mnapaswa kubuni bidhaa na huduma zinazoendana na kasi ya kukua kwa sekta ya mawasiliano ya Tehama ulimwenguni.

"Serikali kupitia Mamalaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana(CMSA) itaendelea kujenga mazingira wezeshi na shirikishi kwa lengo la kufikia azma hiyo kwa maendeleo ya masoko ya mitaji hivyo kuchochea ukuaji wa uchumi wetu hapa nchini,"amesema.
Share:

TBS NA ZBS WAANDAA TUZO YA UBORA YA SADC KWA WAFANYABIASHARA NA WAZALISHAJI WA BIDHAA

  

Afisa Viwango Mkuu kutoka Shirika la Viwango Tanzania (TBS),Bw.Nickonia Mwabuka akizungumza na waandishi wa habari leo Makao Makuu ya Shirika hilo Jijini Dar es Salaam


Wafanyabiashara na wazalishaji wa bidhaa nchini wametakiwa kushiriki katika shindano la utoaji tuzo bora kwa makampuni ya uzalishaji na watoa huduma itakayofanyika Machi mwaka 2021 nchini Msumbiji katika mkutano wa mwaka unaoshughulikia vikwazo katika biashara kwenye Jumuiya ya SADC (SADCTBT-Cooperation Structures).

Akizungumza na wandishi wa habari Jijini Dar es Salaam, Afisa Viwango Mkuu kutoka Shirika la Viwango Tanzania (TBS),Bw.Nickonia Mwabuka amesema tuzo hizo ni kuangalia bidhaa zetu zinakidhi ubora katika utengenezaji na utumiaji kwaajili ya wananchi na biashara pamoja na kukuza uchumi kwa jumuiya ya SADC.

"Tunawaomba wadau wote katika uzalishaji na kutoa huduma kutumia nafasi hii ya kushindana iliyotolewa na SADC, kujaza fomu husika kwa kuangalia vigezo vilivyowekwa na kutuma TBS kwa mtandao uliowekwa, kama upo karibu unaweza kuleta mwisho ni Jumatano saa 10 jioni".Amesema Bw.Mwabuka.

Aidha Bw.Mwabuka amesema makundi yote yatakayo shiriki watajaza fomu maalumu iliyoandaliwa ambayo ipo kwenye tovuti ya TBS- www.tbs.go.tz, ZBS- www.zbs.go.tz na kuirejesha kwa kutumia email qualityawards@tbs.go.tz Novemba 25 mwaka huu.

Pamoja na hayo Bw.Mwabuka amesema mshindi wa kwanza katika kila kundi atapewa cheti cha ushindani na kombe.

"Washindi hao pia watashiriki katika mkutano wa SADCTBT utakaofanyika Machi 2021 Maputo nchini Msumbiji ambaye ndiye atakuwa Mwenyekiti wa SADC". Amesema Bw.Mwabuka.

Hata hivyo amesema kuwa faida ya kushiriki katika mashindano hayo ni pamoja na kufanya bidhaa na huduma zetu kwa ujumla kujulikana katika soko la SADC.

Sambamba na hayo amesema kuwa makundi ambayo yatashiriki ambayo ni kundi la wajasiriamali chini ya watu 100,Wazalishaji wakati ma wakubwa zaidi ya wafanyakazi 100,mtu binafsi anayezalisha/kutoa huduma inayokidhi ubora.

Amesema utoaji wa tuzo kwa makampuni ya uzalishaji na watoa huduma ni utaratibu ambao hufanyika kila mwaka kwa wanachama wa SADC kwa lengo la kutambua mchango wa matumizi ya viwango katika kukidhi ubora wa bidhaa na huduma kwa jamii ya SADC.

Tuzo ya hizo zimeandaliwa na Shirika la Viwango TBS na Shirika la Viwango Zanzibar (ZBS) wakishirikiana na taasisi za sekta binafsi bara na visiwani.

Share:

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumamosi Novemba 21



Share:

Friday, 20 November 2020

Special Assistant to the Registrar, P4 at IRMCT / UN

Org. Setting and Reporting This position is located in the Immediate Office of the Registrar of the International Residual Mechanism for Criminal Tribunals (IRMCT), Arusha Branch. The incumbent will report to the Registrar.   Responsibilities •Undertake comprehensive research and provide specialized legal advice and support to the Registrar on legal issues related to the work […]

The post Special Assistant to the Registrar, P4 at IRMCT / UN appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Regional Emergency Coordinator at Danish Refugee Council (DRC)

Overall purpose of the role:  The Regional Emergency Coordinator (REC) assists in the development and strengthening of emergency preparedness and response within the region through the provision of technical support and quality assurance to all emergency programmes within the East Africa and Great Lakes (EAGL) region on a need and request basis. The role envisions […]

The post Regional Emergency Coordinator at Danish Refugee Council (DRC) appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

SUPPLIES ASSISTANT II at IJA

POST SUPPLIES ASSISTANT II – 1 POST POST CATEGORY(S) HR & ADMINISTRATION PROCUREMENT & LOGISTIC MANAGEMENT EMPLOYER Institute of Judicial Administration (IJA) APPLICATION TIMELINE: 2020-11-18 2020-12-01 JOB SUMMARY N/A DUTIES AND RESPONSIBILITIES i. To file transaction documents; ii. To arrange stocks in the shelves or storage area according to their nature and sensitivity; iii. To […]

The post SUPPLIES ASSISTANT II at IJA appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Director Of Finance And Business Development at Tanzania Standard (Newspaper) Ltd

Applications are invited from suitably qualified persons to fill the following post: – DIRECTOR OF FINANCE AND BUSINESS DEVELOPMENT The Director of Finance shall be the Head of Directorate of Finance and Business Development and is responsible to the Director General. He shall direct and coordinate the organization’s financial resources. In Finance Supervises the implementation of […]

The post Director Of Finance And Business Development at Tanzania Standard (Newspaper) Ltd appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Senior Manager; Mass Affluent at NMB Bank

Job Purpose To lead a team of Relationship Managers in growing the Mass Affluent book by providing holistic financial advice and deepen client relationships by identifying broader product and service solutions that meet their investment, savings and credit needs. Main Responsibilities HESLB LOAN ALLOCATION (HESLB LOAN BENEFICIARIES) 2020/2021 Identify potential new clients and work with […]

The post Senior Manager; Mass Affluent at NMB Bank appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Specialist; ATM & POS Support at CRDB

Job Purpose Responsible to provide pro-active, efficient and cost effective second level technical support to ensure highest ATM and POS terminal services uptime to customers. Key Responsibilities Branch User support responsibilities: Train branch ATM custodians how to operate the ATMs correctly and efficiently, e.g. Cash replacement, operator control panel, clear note jams and recycle bins, replacement of […]

The post Specialist; ATM & POS Support at CRDB appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Senior Specialist; Networks Security at CRDB

Job Purpose Plan, organize and lead a team to deliver cost effective and efficient IT security controls to protect and defend the bank’s network infrastructure against any internal and external threats (e.g. unauthorized access, cyber-attacks, etc.). Key Responsibilities Protects network infrastructure by defining access privileges, control structures, and resources. Manage and ensure optimal security configurations […]

The post Senior Specialist; Networks Security at CRDB appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Specialist; Data Centers at CRDB

Job Purpose Monitor, troubleshoot, and maintain the bank’s Data Centers Power Cooling, Fire Detection and suppression, Physical security, access control and other low voltage systems. Key Responsibilities Daily monitoring, troubleshooting, resolve or escalate to vendors incidents related to the Data Centers Power (Utility feeds, Generator systems, UPS, battery string, etc.), Cooling (HVAC, chiller), Fire Detection & suppression (FM200 Pre-action […]

The post Specialist; Data Centers at CRDB appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Manager; Data Centers Operations at CRDB

Job Purpose Responsible of planning, organizing and leading a team to deliver cost effective and efficient   data centers facilities services (power, cooling, fire prevention/suppression systems) that meet and exceed business and customers’ expectations (availability, recoverability, security and continuous improvement). Key Responsibilities Responsible for availability, recoverability and security of Data centers facilities (Power Utility feeds, Generator systems, […]

The post Manager; Data Centers Operations at CRDB appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Senior Manager; Networks at CRDB

Job Purpose Responsible for selection and implementation of the best network technology solutions & suppliers, maintaining highest uptime of all networks. Quickest response & resolution of network incidents & problems escalated from Level 1 Support (Service Management Department). Ensure excellent management of Service Level Agreement (SLA) with Network Service providers, cost effective maintenance of network […]

The post Senior Manager; Networks at CRDB appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

DSE YAZINDUA MFUMO WA HISA KIGANJANI DAR ES SALAAM

 

Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA), Nikodemus Mkama akigonga kengele kuashiria uzinduzi wa mfumo wa kuuza na kununua Hisa kwa njia ya simu za mkononi (Hisa Kiganjani) jijini Dar es Salaam Novemba 20 2020. Kutoka (kulia) ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE), Moremi Marwa, Afisa Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Kuendeleza Sekta ya Fedha (FSDT), Sosthenes Kewe na Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA), Ricco Boma.  (Picha zote na Robert Okanda)
Mgeni rasmi wa uzinduzi wa mfumo wa kuuza na kununua Hisa kwa njia ya simu za mkononi (Hisa Kiganjani), ambaye ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA), Nikodemus Mkama akitoa hotuba yake wakati wa hafla ya uzinduzi huo jijini Dar es Salaam Novemba 20 2020. Kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Kuendeleza Sekta ya Fedha (FSDT), Sosthenes Kewe na Afisa Mtendaji Mkuu wa Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE), Moremi Marwa.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE), Moremi Marwa akiongea na waandishi wa habari wakati wa wakati wa hafla ya uzinduzi wa mfumo wa kuuza na kununua Hisa kwa njia ya simu za mkononi (Hisa Kiganjani) jijini Dar es Salaam Novemba 20 2020.   
Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA), Nikodemus Mkama wa pili kulia) akiwa katika picha ya pamoja na madalali wa DES wakati wa hafla ya uzinduzi wa mfumo wa kuuza na kununua Hisa kwa njia ya simu za mkononi (Hisa Kiganjani) jijini Dar es Salaam Novemba 20 2020. Kutoka (kulia) ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE), Moremi Marwa, Afisa Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Kuendeleza Sekta ya Fedha (FSDT), Sosthenes Kewe na Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA), Ricco Boma. 

Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA), Nikodemus Mkama (wa pili kulia) akiwa katika picha ya pamoja na sehemu ya wafanyakazi wa Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) wakati wa hafla ya uzinduzi wa mfumo wa kutumia kuuza na kununua hisa kwa njia ya simu za mkononi katika soko la hisa Dar es Salaam Novemba 20 2020. Kulia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa (DSE), Moremi Marwa,  Afisa Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Kuendeleza Sekta ya Fedha (FSDT), Sosthenes Kewe (wa pili kushoto) na Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA), Ricco Boma.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA), Nikodemus Mkama (mwenye tai nyekundu) akiagana na Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA), Ricco Boma. Kulia (pia) ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE), Moremi Marwa akiagana na  Afisa Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Kuendeleza Sekta ya Fedha (FSDT), Sosthenes Kewe wakati wa kuhitimisha hafla ya uzinduzi huo.

Na Robert Okanda

Tanzania leo imezindua mfumo wa kuuza na kununua hisa kwa njia ya simu za mkononi unaoitwa Hisa Kiganjani, hatua inayolenga kuongeza wigo wa ushiriki wa wananchi na wawekezaji katika uwekezaji kupitia masoko ya mitaji na hivyo kuchochea ukuaji wa sekta ya fedha na uchumi wa wananchi na nchi kwa ujumla.

Uzinduzi wa mfumo huo umefanywa makao Makuu ya Soko la Hisa Dar es Salaam (DSE), na Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA), Nicodemus Mkama ambapo amesema uwepo wa mfumo wa kununua na kuuza hisa kwa njia ya mtandao, unatarajiwa utoe matokeo chanya katika sekta jumuishi ya kifedha, baada ya tafiti kuonyesha asilimia 60 ya Watanzania wanatumia huduma za fedha kwa njia ya simu za mkononi, ikiwa ni pia ni kuunga jitihada zinazoendelea za kutoa elimu kwa makundi mbalimbali ya kijamii kujenga utamaduni wa kuwekeza kwenye masoko ya hisa na mitaji.

Kwa mujibu wa Mtendaji huyo, Mfumo huo umeidhinishwa na Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana baada ya kukidhi matakwa ya kisheria, vigezo na kanuni za usimamizi wa masoko ya mitaji kimataifa zinazotolewa na Taasisi ya Usimamizi wa Masoko ya Mitaji ulimwenguni yaani ''International Organaization for Securities Commission (IOSCO).

Bwana Mkama aliongeza kusema kwamba mfumo huo unatarajia kuwezesha kuongezeka kwa miamala katika soko la hisa na inatarajiwa kwamba ukwasi wa soko la hisa utaongezeka. 'Ukwasi Mkubwa wa soko ni kiashiria muhimu cha ubora wa soko kinachovutia wawekezaji wengi wa ndani na wa kimataifa' 

Aidha Mfumo huo unatarajiwa pia kuongeza mchango katika jitihada za kuongeza uelewa na elimu ya fedha kwa umma zinazofanywa na DSE na CMSA
Alizitaja baadhi ya jitihada hizo ni pamoja na mipango na shindano la Masoko ya Mitaji kwa wanafunzi wa Vyo Vikuu na Taasisiza elimu ya juu yaani (Capital Market  Universities and Higher Learning Institutions
Challenge linaloendeshwa na CMSA; na shindano la Uwekezaji kwa Wanafunzi yaani; DSE Scholar Investiment Challenge linaloendeshwa na soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) na mpango wa DSE wa kuendeleza biashara yaani, DSE Enterprise Acceleration Program. 
    
Awali Afisa Mtendaji Mkuu wa DSE Bwana. Moremi Marwa, amesema mfumo huo umebuniwa ili kuongeza idadi ya wawekezaji kwenye taasisi hiyo kutoka laki tano na nusu ya sasa ambayo ni sawa na asilimia moja ya Watanzania wote lakini pia huduma za DSE kuwafikia watu wengi sehemu waliko ndani na nje ya nchi tofauti na sasa ambapo huduma hizo zinapatikana jijini DSM pekee.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa kuendeleza Sekta ya Fedha Tanzania (FSDT), Sosthenes Kewe amesema baada ya Tanzania kupata mafanikio ya kuingia uchumi wa kati, hivi sasa inaingia katika uchumi shindani unaohitaji ushiriki mpana wa jamii katika masuala ya kuinua uchumi.

Share:

SHIRIKA LA OPE LATOA PEMBEJEO ZA KILIMO KUHAMASISHA ZAO LA MTAMA WILAYANI KISHAPU




 Na Marco Maduhu, Kishapu.

Shirika lisilokuwa la kiserikali la Organization of People Empowerment (OPE) la Mkoani Shinyanga, limetoa msaada wa Pembejeo za kilimo kwa wananchi wa Kata ya Busangwa wilayani Kishapu, kwa ajili ya kuhamasisha kilimo cha zao la Mtama.

Zoezi la ugawaji wa pembejeo hizo za kilimo, limefanyika leo eneo la Shule ya Msingi Ng’wajipugila Kata ya Busangwa, na kuhudhuliwa na mgeni rasmi afisa kilimo wa halmashauri ya wilaya ya Kishapu George Kesyy, akimwakilisha Mkurugenzi wa halmashauri hiyo.

Afisa miradi kutoka Shirika hilo la OPE, Joseph Kasya, amesema Pembejeo hizo wamezitoa katika vikundi vinne, ambavyo vilipewa mafunzo kwa ajili ya kulima mashamba darasa ya zao la Mtama, ambayo yatakuwa chachu kwa wakulima kwenye Kata hiyo ya Busangwa, na hatimaye kulima kilimo chenye tija na kupata mavuno mengi.

“Shirika la OPE tumepokea Ruzuku kutoka Shirika la Tanzania Development Trust (TDT) la uingereza, kwa ajili ya kuingia ubia na jamii katika kuhamasisha kilimo cha zao la Mtama, ili kuongeza upatikanaji wa chakula cha kutosha kwa wananchi”, amesema Kasya.

“Katika mradi huu tumetoa mafunzo kwa wakulima kutoka vikundi Vinne vya Kata ya Busangwa, ili wakalime mashamba darasa ya zao la Mtama, na kufundisha wenzao namna ya kulima zao hili kisasa, na leo tumekuja kutoa Pembejeo kwa ajili ya kuwezesha wananchi kulima Mtama, ambapo tumetoa mbegu bora kabisa pamoja na majembe,”ameongeza.

Naye mgeni huyo Rasmi afisa kilimo wilayani Kishapu George Kessy, amelipongeza Shirika hilo kwa kushirikiana na Serikali, kuhamasisha wananchi kulima mazao ambayo yanasatahimili ukame, ili wapate mavuno mengi na kuondokana na baa la njaa hapo baadae.

Amesema ni vyema wananchi wilayani Kishapu katika msimu wa kilimo wa mwaka huu (2020-2021), wakajikita kulima mazao ambayo yanastahimili ukame, kutokana na taarifa za hali ya hewa kuwa hakutakuwa na mvua za kutosha , hivyo ni vyema wakaanza kuchukua tahadhari mapame na kulima mazao hayo.

Ametaja mazao pendekezwa ambayo yanastahimili ukame na kulimwa kwenye ardhi ya Kishapu, kuwa ni Mtama, Choroko, Dengu, Alzet, Viazi Lishe, vitamu, pamoja na mazao ya biashara Pamba na Mkonge.

Nao baadhi ya wanufaika na pembejeo hizo akiwamo Rebeka Ruchagula, ameshukuru kwa kupewa mafunzo hayo ya kilimo cha kisasa cha zao la Mtama pamoja na Pembejeo, na kuahidi kwenda kulima zao hilo na kutoa elimu kwa wenzao ili wanufaike na kupata mavuno mengi.

TAZAMA PICHA HAPA CHINI


Afisa miradi kutoka Shirika la OPE Joseph Kasya, akizungumza kwenye makabidhiano ya Pembejeo kwa vikundi vinne vya Shamba darasa kwa ajili ya kulima zao la Mtama Kata ya Busagwa wilayani Kishapu.

Mgeni Rasmi Afisa kilimo wilayani Kishapu George Kessy, akizungumza kwenye makabidhiano ya Pembejeo kwa vikundi vya Shamba Darasa la zao la Mtama Kata ya Busangwa wilayani humo.
Afisa kilimo wilyani Kishapu George Kessy, akisisitiza wananchi wote wilayani humo, kuwa mwaka huu wajikite kulima Mazao yanayostahimili ukame.
Wanavikundi wa kilimo cha zao la Mtama kutoka Kata ya Busangwa wilayani Kishapu, wakiwa kwenye zoezi la kukabidhiwa Pembejeo za kilimo kwa ajili ya kulima zao hilo la Mtama kwenye Mashamba darasa.

Wanavikundi wa kilimo cha zao la Mtama kutoka Kata ya Busangwa wilayani Kishapu, wakiwa kwenye zoezi la kukabidhiwa Pembejeo za kilimo kwa ajili ya kulima zao hilo la Mtama kwenye Mashamba darasa.

Wanavikundi wa kilimo cha zao la Mtama kutoka Kata ya Busangwa wilayani Kishapu, wakiwa kwenye zoezi la kukabidhiwa Pembejeo za kilimo kwa ajili ya kulima zao hilo la Mtama kwenye Mashamba darasa.

Wanavikundi wa kilimo cha zao la Mtama kutoka Kata ya Busangwa wilayani Kishapu, wakiwa kwenye zoezi la kukabidhiwa Pembejeo za kilimo kwa ajili ya kulima zao hilo la Mtama kwenye Mashamba darasa.
Afisa kilimo halmashauri ya wilaya ya Kishapu George Kessy. (kulia) akikabidhi Pembejeo za kilimo ili kuhamasisha kilimo cha zao la Mtama.
Zoezi la kukabidhi Pembejeo likiendelea.

Zoezi la kukabidhi Pembejeo likiendelea.
Zoezi la kukabidhi Pembejeo likiendelea.
Pembejeo, ambazo ni Majembe, na Mbegu za zao la Mtama zikiwa ndani ya mfuko.

Picha ya pamoja mara baada ya kumalizika kwa zoezi la kukabidhi Pembejeo kwa wakulima.
Picha ya pamoja mara baada ya kumalizika kwa zoezi la kukabidhi Pembejeo kwa wakulima.

Na Marco Maduhu- Kishapu.

Share:

AFARIKI DUNIA KWA KUGONGWA NA TRENI AKIIDANDIA MALAMPAKA SIMIYU


Kamanda wa Polisi, mkoa wa Simiyu, ACP Richard Abwao.

Na Sitta Tumma - Simiyu
Mtu mmoja, Galula Luhende, mkazi wa Malampaka, Wilaya ya Maswa, Mkoa wa Simiyu, amefariki dunia baada ya kugongwa na Treni.

Mtu huyo anayekadiriwa kuwa na umri wa kati ya miaka 45 na 50, miguu yake yote miwili pia ilikatwa na Treni baada ya kumkanyaga.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu, ACP Richard Abwao, amethibitisha akisema ajali hiyo imetokea jana, saa 3:00 usiku.

Kamanda Abwao amesema Treni hiyo ilikuwa ikitokea jijini Mwanza kwenda Dar es Salaam, kwamba kabla ya ajali ilisimama Malampaka kupakia abiria.

"Marehemu alikuwa akidandia Treni hiyo iliyokuwa imeanza kuondoka, ndipo alipoteleza na kuanguka na kukanyagwa miguu.

"Marehemu huyo kabla ya kufariki dunia, alikimbizwa Kituo cha Afya Malampaka na baadaye kuhamishiwa Hospitali ya Wilaya ya Maswa kwa matibabu," ACP Abwao amenukuriwa.


Kulingana na tukio Hilo, Jeshi la Polisi limetoa wito kwa raia kuwa na tahadhari ya kiusalama, punde wawapo eneo la Stesheni ya Treni.


Kamanda Abwao ametoa rai hiyo pia kwa wananchi wakati wanapokuwa karibu na njia ya Gari Moshi (Treni).
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger