Saturday, 2 May 2020

Joe Biden ambaye ni Mpinzani wa Trump uchaguzi wa Mwaka Huu Marekani akanusha madai ya kumdhalilisha kingono msaidizi wake

Mgombea urais nchini Marekani katika tiketi ya chama cha Democratic, Joe Biden, amekanusha vikali madai ya kumdhalilisha kingono Tara Reade ambaye alikuwa afisa wake wa zamani, huku akiongeza kuwa kisa hicho ambacho mwathiriwa anadai kilitendeka mwaka 1993, hakikutokea. 

Akihojiwa na kituo cha televisheni cha MSNBC, Biden amekivunja kimya chake cha mwezi mmoja kuhusu suala hilo kwa kusema kuwa hajawahi kutenda uhalifu huo.

 Aidha, taarifa ya Biden imesema waliokuwa wasaidizi wake wakuu mnamo wakati kisa hicho kinadaiwa kutokea, wamekanusha kufahamu tukio hilo.

 Mgombea huyo wa Democrat amesema ataiomba idara ya taifa inayohusika na kuweka rekodi kuchunguza ikiwa kuna rekodi yoyote ya malalamiko hayo. 

Reade ni miongoni mwa wanawake ambao wamelalamika kwamba Biden aliwabusu na kuwashika kwa njia isiyofaa. 

Joe Biden atakiwakilisha chama cha Demokratic katika mchuano wa Urais  nchini Marekani Novemba Mwaka huu ambapo atachuana na Rais wa sasa  Rais Donald Trump


Share:

PICHA: Mwili wa aliyekuwa Waziri wa Katiba na Sheria, Balozi Dkt. Augustine Mahiga ukiwasili nyumbani kwake

Mwili wa aliyekuwa waziri wa katiba na sheria Balozi Dkt. Augustine Mahiga, ukishushwa nyumbani kwake Gangilonga mjini Iringa kwaajili ya taratibu za kuuaga kabla ya kuelekea eneo alipozaliwa Tosamaganga nje kidogo ya mji wa Iringa kwa ibada ya  mazishi.



Share:

Waziri Mkuu wa Urusi akutwa na virusi vya Corona

Waziri Mkuu wa Russia Mikhail Mishustin amesema amekutwa na maambukizi ya virusi vya Corona.

Taarifa iliyotolewa na Makao Makuu ya Serikali ya Urusi imesema, Mishustin alimwambia rais wa nchi hiyo Vladmir Putin kwa njia ya video kuwa, amepimwa na kukutwa na virusi vya Corona. 

Amesema amejitenga nyumbani kwake na kufuata maelekezo ya madaktari, na kuongeza kuwa, serikali itaendelea kufanya kazi kama kawaida.

Naibu wa kwanza wa Waziri Mkuu huyo Andrei Belousov atakaimu kwa muda kazi za waziri mkuu huyo, kufuatia hatua iliyoidhinishwa na rais Putin.


Share:

Ratiba Ya Mazishi Ya aliyekuwa Waziri wa Katiba na Sheria Balozi Dkt Augustine Mahiga

Makamu wa Rais,Mama Samia Suluhu Hassan, leo  Mei 2, 2020,  ataongoza mazishi ya aliyekuwa Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt Augustine Mahiga, aliyefariki dunia jana. 

Dkt. Mahiga mwanadiplomasia mkongwe aliyeitumikia nchi kwa weledi, atazikwa alasiri Tosamaganga, Iringa.

Msemaji Mkuu wa Serikali.Dkt. Hassan Abbas ametoa taarifa hiyo.


Share:

Kiongozi Wa Korea Kaskazini Ajitokeza Hadharani Kwa Mara Ya Kwanza Baada ya Uvumi Kwamba Yuko Mahututi

Kim Jong Un amejitokeza hadharani kwa mara ya kwanza baada ya kutoonekana kwa takribani wiki tatu hadi kupelekea uvumi wa kwamba anaugua na huenda amefariki.

 Shirika la Habari la Korea Kaskazini(KCNA) limesema Kim  Jana May 01, 2020 alikata utepe kwenye uzinduzi wa kiwanda cha mbolea eneo la sunchon.


Share:

Dkt. Kalemani : TANESCO Kateni Umeme Kwa Wadaiwa Sugu Muongeze Mapato

Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani ameliagiza Shirika la Umeme nchini( TANESCO) kuendelea kukata umeme kwa wadaiwa sugu ili kukusanya mapato zaidi na kulipa madeni ya shirika hilo.

Dkt. Kalemani alisema hayo, Aprili 30, 2020, Jijini Dodoma, alipokutana na  Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa TANESCO, kuzungumzia tathimini ya miaka mitano ya utekelezaji wa miradi mbalimbali, baada ya kufanya ziara ya kukagua ujenzi wa upanuzi wa kutuo cha kupoza na kuzambaza umeme cha Zuzu.

Katika kikao hicho, mambo mbalimbali yalijadiliwa kuhusiana na nishati ya umeme inayozalishwa nchini kwa lengo la kuleta manufaa makubwa zaidi kiuchumi kwa nchi, Shirika na watumiaji wa umeme huo ikiwemo viwanda, wafanyabiashara na matumizi mengine.

Dkt. Kalemani aliiagiza TANESCO, kulipa madeni yote inayodaiwa na kutoongeza madeni mapya, vilevile wadaiwa sugu wakumbushwe madeni yao,na endapo hatawalipa, TANESCO iwakatie umeme, kwa kufanya hivyo kutamaliza tatizo la wadaiwa sugu.

“TANESCO inadaiwa madeni makubwa, pia ina wateja wengi sana ambao ni wadaiwa sugu wanaodaiwa fedha nyingi sana na hawalipi ,zimo Taasisi, Mashirika ya Umma na binafsi, pamoja na watumiaji wa kawaida, ninawaagiza nendeni mkawakatie umeme! narudia tena mkakate umeme! mkishaukata, wahusika watalipa na wataonyesha ushirikiano mkubwa, tofauti na kumdai kawaida tu”, alisema Dkt. Kalemani.

Kuhusu wizi na uhujumu wa miundombinu ya umeme, Dkt. Kalemani, aliitaka TANESCO, Bodi ya TANESCO na Watendaji wa Wizara ya Nishati, kushirikiana kwa pamoja kutafuta njia sahihi naya kisasa zaidi  ya kubaini wizi wa umeme,unaofanywa na watu wasiowaaminifu na kusababisha hasara kwa shirika na kupoteza mapato ya taifa.

“Wizi wa umeme upo na haukubaliki, tuweke mfumo sahihi wa kisasa kubaini wahusika, tuache na hii tabia ya kukimbizana kimbizana na wezi, pia sisi watumishi tuwe wazalendo,na wasimamizi wazuri wa miundombinu yetu,vilevile tuwe na walinzi wenye weledi katika miradi yetu bila kujali niya serikali au mtu binafsi, jukumu la ulinzi ni letu sote faida ya Taifa kwa jumla”,alisisitiza Dkt. Kalemani.

Aidha aliwataka kuendelea kufanya tathmini na uwiano wa gharama za kutengeneza nguzo za Zege na nguzo zinazotumika sasa,ili kuangalia uwezekano wa kutumia nguzo za zege katika maeneo yote nchini lakini kwa gharama nafuu, kwa lengo la kukabiliana na changamoto ya kuoza ama kuungua kwa nguzo katika maeneo mbalimbali.

Hata hivyo aliweka wazi kuwa katika baadhi ya maeneo machache ambayo ni korofi nguzo za zege zimeanza kutumika japo ni za gharama kubwa.

Vilevile alitaka kuongezeka kwa idadi ya wateja wa umeme katika kila sekta, kuharakisha uunganishaji wa umeme kwa mteja pale anapomaliza kulipia gharama husika, pamoja na kutatua changamoto za wateja kwa wakati sahihi ili kuvutia wateja wengi zaidi na kuondoa malalaliko.

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu aliwataka TANESCO kuangalia uwezekano wa kutoa zawadi kubwa kwa wasamaria wema wanaotoa taarifa za siri kuhusu wanaohujumu na kuiba umeme tofauti na ile inayotolewa sasa, ambayo pia huchukuwa muda mrefu kuikabidhi kwa mhusika.

Mgalu alikitaka  kitengo husika kitunza siri za watoa taarifa,pia kifanye uchunguzi wa kina na kutoa adhabu kwa mtumishi yeyote atakayetiliwa shaka, au kuhusika na wizi pamoja na kuhujumu miundombinu ya umeme kama inavyofanywa kwa wahisika wengine wanaobainika.

Vilevile kuwe na uhamasishaji wa kuwavutia watoa taarifa ili kupata matokeo chanya kunusu wizi na uhujumu wa miundombinu ya umeme nchini.

Naye Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Mhandisi Zena Said, alieleza kuwa ili kukabiliana na changamoto ya wizi na uhujumu wa miundombinu ya umeme, watashirikiana na Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa,(TAMISEMI) kuimarisha ulinzi kuanzia ngazi za Kaya.

Mhandisi Said, alisema kwa kufanya hivyo kutasaidia sana kubaini wezi na wahujumu miundombinu ya umeme kwa kuwa watu hao wasio wazalendo huwa wanaoneka na hata kufahamika katika maeneo yao.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa TANESCO, Dkt. Alexander Kyaruzi, aliishuruku Wizara ya Nishati kwa kuwapa ushirikiano mkubwa katika kutekeleza majukumu yao na kuyafanyia kazi yale waliokuwa wakiishauri wizara hiyo, katika kipindi chote cha miaka mitano

Dkt.Kiyarunzi, alikiri kwa kuwa kazi ya kusambaza umeme si jambo jepesi, hivyo wanajivunia kuona maendeleo makubwa katika sekta ya nishati ya kuongeza wigo wa usambazaji wa umeme vijijini, kujenga miradi mikubwa ya kuzalisha, njia za kusafirisha na kusambaza umeme pamoja na vituo vya kupoza na kusambaza umeme nchini.

Awali kabla ya kufanyika kwa kikao hicho, Uongozi wa Wizara na Wajumbe wa Bodi hiyo walifanya ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa upanuzi wa Kituo kikubwa zaidi nchini cha Kupoza na kusambaza umeme cha Zuzu kilichopo jijini Dodoma.

Kwa mujibu wa Dkt. Kalemani, ujenzi wa kituo hicho utakamilika mwishoni mwa mwezi huu wa Mei, 2020 na kitakuwa na uwezo wa kuzalisha Megawati 648 tofauti na vituo vingine.

Na kituo hicho kitaimarisha upatikanaji wa umeme kwa Jijiji la Dodoma ambalo linaendelea kukuwa kwa kasi na  kitakuwa ndiyo kitovu cha vituo vyote vya kupoza kuzambaza umeme katika mikoa yote nchini na kuupeleka nchi jirani pale itakapohitajika kufanya hivyo.


Share:

Tathmini Ya Ununuzi Wa Pamba Kufanyika Kabla Msimu

Serikali imesema inafanya tathmini ya hali ya ununuzi wa zao la pamba msimu wa mwaka 2019 ili kuondoa changamoto zilizojitokeza kabla msimu mpya wa ununuzi kuanza mwaka huu.

Akizungumza na viongozi wa wilaya ya Chato mara baada ya kutembelea viwanda vya kuchambua pamba, Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Gerald Kusaya amesema msimu mpya wa ununuzi utatangazwa mara baada ya tathmini ya msimu uliopita kufanyika.

“ Wizara imegundua kuwa hali ya mazao shambani kwa pamba bado ,kwani hata vitumba bado havijapasuka kutokana na uwepo mvua nyingi ,hivyo baada ya ziara hii kwenye mikoa ya kanda ya ziwa serikali itakaa na watalaam ili kuamua lini wakulima wataanza kuuza pamba yao kupitia Vyama Vya Ushirika vya Msingi (AMCOS) “ alisema Kusaya

Aliongeza kusema kabla msimu haujafunguliwa serikali itahakikisha madeni ya wakulima,wanunuzi na ushuru wa AMCOS, halmashauri pamoja na mfuko wa pembejeo yanalipwa.

“Kila mwananchi atalipwa madai yake na jitihada za serikali ni kuona madeni haya yanalipwa kabla ya msimu mpya wa ununuzi wa pamba kuanza” alisitiza Katibu mkuu
 
Katika hatua nyingine Chama Kikuu cha Ushirika Chato( CCU) kimetakiwa kuhamasisha wakulima wengi zaidi kuzalisha zao la pamba ili ipate malighafi za kutosha kutumika kwenye kiwanda chake cha kuchambua pamba.

Kusaya alitoa wito huo kufuatia taarifa ya Meneja Mkuu wa Chama hicho Joseph Masingiri kusema kiwanda kimeshindwa kuendelea na uchakataji marobota kutokana na uhaba wa pamba ambapo msimu wa 2019 ni  kilo milioni 13.6 ,000 tu zilinunuliwa wakati uwezo wake ni kilo milioni 30.

Ili kukabiliana na changamoto za zao hilo,Katibu Mkuu Kusaya amewataka wataalam wa halmashauri na wa chama kikuu  kuhamasisha wakulima kuzalisha mazao ya mkonge na korosho ili kuwa na uhakika wa kipato pale zao la  pamba linapoyumba.

“ Tulime pamba na mazao mengine ya biashara kama mkonge na korosho yanayostawi vizuri kwenye mkoa huu wa Geita na kanda ya ziwa yote .Wizara ya kilimo ipo tayari kuleta mbegu bora za mkonge na korosho toka taasisi za utafiti ili zigawiwe kwa wakulima “ Kusaya.

Kusaya alitaja faida za zao la mkonge kuwa katika kipindi cha miaka mitatu  baada ya kupanda mkulima ataanza kuvuna na kuendelea hadi miaka kumi na tano huku akiendelea na kilimo cha mazao mengine .

Katika kuhakikisha mkoa wa Geita unaongeza uzalishaji wa mazao nchini,Katibu Mkuu huyo ameelekeza mkoa uwasilishe wizarani maandiko ya miradi ya kipaumbele ya umwagiliaji ili serikali itafute wadau wa kuitekeleza.

Nae Katibu Tawala Mkoa wa Geita Dennis Bandisa aliyeshiriki ziara hiyo aliishukuru wizara ya kilimo kwa kuonesha nia ya kusaidia kukuza kilimo cha umwagiliaji na kuwa kuahidi kuwa maandiko atayawasilisha wizarani ndani ya kipindi kifupi.

Taarifa ya  Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chato Eliurd Mwaiteleke kuhusu sekta ya kilimo ilisema wilaya hiyo ina eneo la hekta 10,810 zinazofaa kwa umwagiliaj lakini ni hekta 3,416 tu sawa na asilimia 31.6 zinamwagiliwa.

Katika msimu wa mwaka 2019 jumla ya kilo milioni 10.8 za pamba mbegu zilinunuliwa wilayani Chato kupitia AMCOS zenye thamni ya shilingi Bilioni 13.06 ililipwa kwa wakulima.


Share:

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumamosi May 02



















Share:

Friday, 1 May 2020

Mwenyekiti wa Soka la Wanawake Mkoa wa Dar es Salaam Dkt. Maneno Tamba Afariki Dunia.....TFF Waomboleza

Mwenyekiti wa Soka la Wanawake Mkoa wa Dar es Salaam na mmiliki wa timu ya soka ya wanawake ya Mburahati Queens, Dkt. Maneno Tamba amefariki dunia leo mchana.



Share:

CCM Watuma Salamu Za Rambirambi Kifo Cha Waziri Augustine Mahiga




Share:

KAMPUNI YA AGORA WOOD PRODUCT YAKABIDHI VIFAA VYA KUKABILIANA NA CORONA KWA JESHI LA POLISI IRINGA


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Juma Bwire (kulia) akipokea vifaa vya kujikinga dhidi ya Virusi ya Covid 19 kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Agora Wood Product, Elisha Edson, vyenye thamani Tsh Milioni 6. 5 kuwasaidia askari Polisi kujilinda afya zao. (Picha na Datus Mahendeka wa Jeshi la Polisi)

Share:

Wenye Virusi Vya Corona Nchini Kenya Wafika 411....Ni Baada ya Wengin 15 Kuongezeka

Watu 15 zaidi wameambukizwa ugonjwa wa corona  nchini Kenya ndani ya masaa 24.

Waziri wa Afya Mutahi Kagwe amesema leo Ijumaa, Mei 1, wakati wa kikao na wanahabari 

Idadi hiyo sasa inafikisha watu walioambukizwa virusi hivyo nchini Kenya kuwa 411. 

Aidha watu wanne pia wamefarikina kufikisha idadi ya waliofariki  kuwa 21.


Share:

Trump: Virusi vya Corona vilitengenezwa katika maabara ya China

Rais wa Marekani Donald Trump amedai kuwa ameona ushahidi kwamba virusi vya corona vilitoka katika maabara ya China.

Trump amesema hayo huku akitishia kuongeza ushuru kwa China kutokana na ilivyolishughulikia janga la corona ambalo limeukumba ulimwengu mzima.

 Hata hivyo, madai hayo ya Rais Trump yamekosa kutiwa uzito baada ya maafisa wa intelijensia pamoja na waziri wake wa mambo ya nje, Mike Pompeo, kusema kuwa hawajui kwa  ni wapi virusi hivyo vilianzia.

Ukosoaji wa hivi karibuni wa Trump dhidi ya China umejiri, huku takwimu zinaonesha kwamba Wamarekani milioni 30 wamepoteza ajira kufuatia masharti ya kutotoka nje. 


Share:

Kampuni Zaununuzi Wa Tumbaku Ushetu Zaingia Mitini Wakulima Wakidai Zaidi Ya Shilingi Milioni 80

SALVATORY NTANDU
Baada ya kuwepo kwa Malalamiko ya Wakulima wa tumbaku kutolipwa fedha na kampuni za ununuzi wa zao hilo katika msimu wa 2019/20 katika Halmashauri ya Ushetu wilayani Kahama mkoani Shinyanga, Baraza la Madiwani  la  Halmashauri hiyo limeagiza kufanyika kwa uhakiki wa madai hayo kabla kufanyika kwa Masoko  mapya ya mwaka 2020/21.

Uamuzi huo ulitolewa Aprili 30 na Mwenyekiti wa Halmashauri ya hiyo, Juma Kimisha katika kikao cha kawaida cha robo ya tatu ya mwaka wa fedha 2019/20 kuanzia Januari hadi Marchi baada ya kupokea taarifa mbalimbali za maendeleo zilizotekelezwa na serikali.

Alisema kuwa katika vyama vya Msingi Kangeme,Tumaini na Ilomelo wakulima wake wanazidai kampuni za ununuzi wa zao hilo zaidi ya Milioni 80 baada ya kuchukua mazao yao katika Msimu uliopita na hadi sasa hawajui ni lini watapata stahiki zao.

“Diwani wa Kata ya Ulowa Paschal Mayengo aliwasilisha malalamiko ya wakulima wake hapa ya kutolipwa fedha na  kampuni za Jaspay na Magepa ambazo zinafikia Dola elfu 35000 ambazo mpaka hivi sasa hawajalipwa huku msimu mpya ukitarajiwa kufunguliwa Mwezi Mei mwaka huu,”alisema Kimisha.

Nae Diwani wa kata ya Igunda Tabu Katoto alishauri ofisi ya Mkurugenzi kufuatilia kwa kina Madai yao ili kudhibiti vitendo vya unyanyasaji vinavyofanywa na baadhi ya kampuni hizo ambazo hazina nia ya kuwakomboa wakulima wa Ushetu.

“Tuweke msisitizo kwa kampuni zote za ununuzi wa zao hili zihakikishe zinajenga  ofisi ili wakulima wetu wasiwe wanahangaika na itasaidia kwabana viongozi wake ikilinganishwa na hivi sasa ambako hatujui wamiliki wake na ni wapi wapatikana,”alisema Katoto.

Akipokea Maelekezo ya kikao hicho Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Michael Matomora alikiri kuwepo kwa madai ya wakulima hao na kuomba kupewa muda kwaajili ya kufanya uhakiki ili kujua uhalali wake.

“Nipeni muda ili niwezekufanya kazi hii kwa ukamilifu niwaahidi nitatoa taarifa kwa kina katika kikao cha Kamati ya fedha ambacho kitaketi hivi karibuni,”alisema Matomora.

Mwisho.


Share:

“sijaridhishwa Na Utendaji Kazi Wa Chama Kikuu Cha Ushirika Geita” - Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo

Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo ametembelea Chama Kikuu cha Mkoa wa Geita (Geita Cooperative Union-GCU) kilichopo Kasamwa wilaya ya Geita  na kutoridhishwa na hali ya kiwanda cha kuchambua pamba kushindwa kufanya kazi muda mrefu.

Ametoa kauli hiyo leo (01.05.2020) wakati alipotembelea na kukagua shughuli za taasisi zilizo chini ya wizara yake na kusema kiwanda cha kuchambua pamba (ginnery) Kasamwa kimeshindwa kujiendesha kutokana na mitambo na majengo yaliyopo kuwa ya kizamani yaliyotumika toka mwaka 1956

“Nimekagua na sijaridhishwa na jinsi kiwanda (ginnery) hii ya Kasamwa kuona haina hata mtambo mmoja unaofanya kazi hali inayopekea pamba ya ya wakulima kuchakatwa kwenye viwanda binafsi “ alisema Kusaya

Amewaagiza viongozi wa Chama kikuu cha ushirika Geita kushirikiana na serikali ya mkoa na wadau kufufua kiwanda hicho ili kitumike kuongeza thamani ya zao la pamba inayozalishwa wa wakulima wa Geita kwa kutafuta mitambo ya kisasa.

Awali Katibu Mkuu Kusaya  alikagua kiwanda cha Matongo Farming Limited cha Geita na kukuta  kimesimama kuzalisha marobota ya  pamba kutokana na upungufu wa malighafi.

Kiwanda hicho kinachomilikiwa na Samson Ng’walida kilianzishwa mwaka 2018 na kina  uwezo wa kuzalisha marobota 450 kwa siku na kuchambua pamba mbegu tani 270 kwa siku.

“Uwezo wa kiwanda ni kuchambua tani 48,600 kwa mwaka na msimu huu wa 2019/2020 tumefanikiwa kuzalisha jumla ya robota 9,412 za pamba nyuzi sawa na asilimia 19 ya uwezo wa kiwanda” alisema Mwalida Samson ambaye ni Mkurugenzi Msaidizi wa kiwanda cha Matongo Ginery.

Kufuatia hali hiyo Katibu Mkuu Kusaya alitoa wito kwa mikoa yote 17 inayozalisha pamba nchini kutengeneza mazingira rafiki kwa wananchi na wawekezaji ili waongeze uzalishaji wa pamba kukidhi malengo ya Serikali ya awamu ya Tano kukuza uchumi kupitia sekta ya viwanda.

 “Napenda kuona uchakataji wa pamba unafanyike mwaka mzima badala ya miezi mitatu au minne ya  sasa kutokana na ukosefu wa malighafi  hali inayosababisha ajira kupungua na serikali kukosa mapato kutokana na viwanda kutozalisha bidhaa za pamba” alisema Kusaya.

Amewataka wataalam wa kilimo nchini kuwasaidia wakulima kupata ya mbegu bora za pamba zinazozalishwa kituo cha utafiti TARI Ukiriguru pamoja na matumizi ya pembejeo na mbolea ili kuongeza tija na uzalishaji wa zao hilo.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Bodi ya Pamba Tanzania Marco Mtunga alisema takwimu zinaonesha mkoa wa Geita umezalisha kilo milioni 33 za pamba katika msimu wa 2019 kiasi ambacho ni kidogo kulingana na mahitaji makubwa ya viwanda vilivyopo mkoani humo.

Aliongeza kusema uwezo wa viwanda vya ndani nchini kwa sasa ni kuchakata pamba ni tani milioni 1.2 wakati uzalishaji umefikia tani 348,910 na kusema bodi yake itaendelea kubuni mikakati mizuri ili uzalishaji pamba uongezeke.

Mwisho
Imetolewa na :
Kitengo cha mawasiliano Serikalini,
Wizara ya Kilimo


Share:

FULL POWER, ZATI 50 NI KIBOKO YA TATIZO LA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME NA UUME MDOGO

Zati 50
Full Power
Sababu za upungufu wa nguvu za kiume na maumbile madogo ya uume:


⇒Ngiri,

⇒Henia

⇒Kisukari

⇒Tumbo kujaa gesi

⇒Kutopata choo vizuri

⇒Utumiaji madawa kwa muda mrefu

⇒Unywaji wa pombe kupita kiasi

⇒Msongo wa mawazo 



⇮⇒Haya yote hupelekea mwili kutokuzalisha homoni ya gesrtogine au kuwa chache na kushindwa kupata mzunguko mzuri wa damu na vichocheo vingine kama madini ya zinki ambayo hukufanya kuwa na msisimko  na kufanya kuwa na muda  mrefu na nguvu za kutosha.



FULL POWER



⇨Ni dawa ya vidonge ya miti shamba inaongeza nguvu za kiume na kutibu kabisa tatizo hilo.

⇨Inaongeza hamu ya tendo la ndoa
⇨Inakufanya uchelewe kufika kileleni zaidi ya Dakika 30 na kurudia tendo zaidi ya mara nne na zaidi.

Zati 50

⇨ Inarutubisha maumbile ya uume  na kunenepesha urefu nchi 6,unene sentimita 4

⇨Dawa hii ni ya kutibu kabisa tatizo hilo.

Pia tunatibu Magonjwa mengine Kama

Matatizo ya pumu,Bawasiri, vidonga vya tumbo,Kisukari,Magonjwa sugu ya zinaaa,Kaswende,U.T.I , kiuno,miguu kuwaka moto, Fangasi sehemu za Siri, kupunguza unene wa mwili,tumbo kuunguruma,kujaa gesi, matatizo ya uzazi kwa wanawake, kurutubisha mbegu za uzazi kwa akina baba, matatizo ya meno tunatibu bila kungoa

Kliniki yetu inapatikana Zanzibar, Dar es salaam na Shinyanga.

Wasiliana nasi kwa simu namba 071770 22 27
Share:

HUYU NDIYO AUGUSTINE MAHIGA...WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA TANZANIA ALIYEFARIKI DUNIA GHAFLA DODOMA


Balozi Dkt Augustine Mahiga alizaliwa Agosti 28, 1945, Kijiji cha Tosamaganga mkoani Iringa, alisoma elimu yake ya Msingi na Sekondari hapa nchini na baadaye mwaka 1968, alijiunga na Chuo Kikuu cha Afrika Mashariki, DSM na kuhitimu Shahada ya Sanaa akibobea kwenye Elimu mwaka 1971.

Marehemu Balozi Dkt Augustine Mahiga, aliyekuwa Waziri wa Katiba na Sheria.

Baadaye alipata ufadhili wa masomo yake nchini Canada, katika Chuo Kikuu cha Toronto na kuhitimu Shahada ya Sanaa na baadaye aliendelea na masomo katika chuo hicho hicho akijikita katika uhusiano wa Kimataifa na kuhitimu mwaka 1975 .

Mwaka 1980 hadi 1983, Balozi Dkt Mahiga alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa, baadaye pia aliteuliwa kuwa mwakilishi wa kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Kimataifa akifanya kazi Geneva - Uswisi, ambapo baadaye mwaka 1992 na 1994 aliteuliwa kuwa kiongozi mwakilishi wa Shirika la Kuhudumia Wakimbizi Duniani (UNHRC).

Balozi Dkt Mahiga ni Mwanadiplomasia wa Tanzania na Waziri wa zamani wa Mambo ya Nje wa Tanzania kutoka 2015-2019 na hapo awali aliwahi kuwa Mwakilishi wa kudumu wa Tanzania kwa Umoja wa Mataifa, kutoka 2003 hadi 2010 na kama Mwakilishi Maalum wa Umoja wa Mataifa (UN) na Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Umoja wa Mataifa kutoka Somalia 2010 hadi 2013.

Mnamo Machi 03, 2019, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, alimteua Balozi Dkt Augustine Mahiga kuwa Waziri wa Katiba na Sheria, akichukua nafasi ya Profesa Palamagamba Kabudi, na aliapishwa Machi 4, 2019

Balozi Dkt Augustine Mahiga ameaga Dunia mapema leo Mei 1, 2020, Jijini Dodoma, baada ya kuugua ghafla.

Mungu ailaze roho ya Marehemu Balozi Dkt Augustine Mahiga, mahala pema peponi. Amina.

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger