Thursday, 30 April 2020

MAMA ALIYEWAPIKIA MAWE WATOTO WAKE APATA MSISIMUKO WA AJABU



Boma la Penina Bahati mtaa wa Mishomoroni, kaunti ya Mombasa.
Prisca Momanyi akiwa na simu mpya ya Penina, pia alimsaidia kufungua akaunti kwenye benki.
***

Mjane Penina Bahati kutoka Mishomoroni eneo la Mlango Saba, kaunti ya Mombasa nchini Kenya ambaye aliwapikia wanawe mawe baada ya kukosa chakula ana sababu ya kutabasamu baada ya kupokea msaada kutoka kwa Wakenya.

Penina Bahati aliamua kupika mawe akiwa na tumaini wanawe ambao walikuwa wanalia njaa watalala hata hivyo hivyo, hatua yake haikufaulu baada ya mwanawe mmoja kuamka na kugundua alikuwa akiwahadaa.

 Baada ya Mtandao wa TUKO.co.ke kuangazia masaibu  ya Penina Bahati Kitsao, wengi walijitokeza na kumpa msaada wa chakula na pesa ambapo sasa anaweza kuwapa wanawe lishe angalau mara tatu kwa siku. 


Akiwa mwingi wa furaha, mama huyo mwenye umri wa miaka 45 alisema watoto wake sasa wanaweza pata mlo angalau mara tatu kwa siku, ambapo kwake ilisalia kuwa ndoto baada ya mumewe kuaga dunia 2019.

 "Nina furaha isiyo na kifani. Siamini Wakenya wanaweza kuwa na roho safi hivi. Nimepokea simu kutoka kote nchini, wengi walitaka kujua jinsi wanaweza kunisaidia," mama huyo alifichua.

 Kupitia kwa msamaria mwema ambaye pia ni jirani yake, Prisca Momanyi, Penina alipata simu na kufunguliwa akaunti ambapo wengi walikuwa wakiitisha ili wamtumie msaada.


"Sijawahi kuwa na akaunti ya benki wala simu, hii ni mara yangu ya kwanza na ninaona ni kama muujiza," aliongeza.

 Prisca alisema aliamua kumsaidia Penina baada ya kupokea habari za kusikitisha kwamba aliwapikia wanawe wanane waliokuwa na njaa mawe.

 Penina ana watoto wanane, kifungua mimba wake ana miaka 28 na kitinda mimba akiwa na miezi mitano.


Penina alisema kwamba mwanawe wa kiume mwenye umri wa miaka mitano ndiye alimshinikiza kupika mawe kwani alikuwa akilia njaa. 

"Watoto wengine ni wazima na wanaelewa wakati hamna chakula, hata hivyo huyu wa kiume ni mgumu hawezi elewa kabisa, alishinda kulia hapa kutwa nzima na ndipo sasa akanifanya nikachukua hatua hiyo," aliongeza.
Chanzo- TUKO NEWS
Share:

WAKILI ALBERT MSANDO ASHIKILIWA NA POLISI KWA KUTOA KAULI ZA UCHOCEZI KUHUSU CORONA

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, ACP Koka Moita, amesema kuwa wanamshikilia Wakili wa kujitegemea Albert Msando, baada ya kutoa kauli za uchochezi dhidi ya Serikali juu ya ugonjwa wa COVID-19 kwa madai ya kuwa mkoani humo hali ya maambukizi ni mbaya ili hali yeye hana mamlaka hayo.


Kamanda Moita ameyabainisha hayo leo Aprili 30, 2020, na kusema kuwa Msando alikuwa anaelezea hali mbaya ya ugonjwa wa Corona ndani ya Mkoa wa Arusha kupitia video yake iliyokuwa ikisambaa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii, huku akiwataka waandishi wa habari wawe mstari wa mbele katika kutoa taarifa za ugonjwa huo.

"Hali hii ilitoa wakati mgumu kwa wananchi waliokuwa wanasikiliza, kauli hii aliitoa wakati anatoa vifaa vya kujikinga na Corona katika eneo la kaloleni katika ofisi za Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Arusha, na Serikali ilikwishatoa  maelekezo kuwa mwenye mamlaka ya kutoa tarifa hizo ni Waziri Mkuu, Waziri wa Afya na Mganga Mkuu, hii kauli lazima iheshimiwe" amesema Kamanda Moita.


Share:

Afrika Kusini Yaripoti Maambukizi Mapya ya Corona 354 Ndani ya Masaa 24....Waliombukizwa Hadi Sasa Nchini Humo ni 5350

Idadi ya maambukizi ya virusi vya Corona nchini Afrika Kusini imefika watu 5,350 baada ya visa vipya 354 kuthibitishwa, huku idadi vifo ikifikia watu 103

Taarifa kutoka wizara ya afya imesema visa vipya 354 ni vya juu kuwahi kuripotiwa  nchini humo chini ya kipindi cha saa 24.

Takriban wiki sita zimepita tangu kisa cha kwanza cha Covid 19 kuripotiwa nchini Afrika Kusini, na idadi ya maambukizi imekuwa ikiongezeka .

Hivi karibuniAfrika Kusini ilichukuwa mikakati mipya kupambana dhidi ya Corona katika magereza mbalimbali nchini humo, baada ya wafungwa 59 na wafanyakazi wa gereza 29 kuthibitishwa kuambukizwa katika kipindi cha majuma mawili.



Share:

Rais wa zamani wa Sudan Omar al-Bashir Aomba Kuhamishwa Gereza Baada ya Msaidizi Wake wa Zamani Kupata Corona

Rais wa zamani wa Sudan Omar al-Bashir ametaka kuhamishwa gereza kufuatia habari kwamba mmoja wa wasidizi wake wa zamani ameambukizwa virusi vya Corona. 

Bashir amefungwa katika gereza la Kober pamoja na ofisa wa zamani wa Wizara ya mambo ya ndani Bw. Ahmed Hrouna, ambaye alihamishwa katika hospitali ya gereza baada ya kuthibitishwa kuambukizwa virusi vya Corona. 

Mkuu wa timu ya ulinzi wa Bashir Bw. Mohamed al-Hassan al-Amin amesema, hali ya Bw. Haroun si mbaya sana.


Share:

Trump Aituhumu China Kwamba Inafanya Kila Mbinu Ili Asichaguliwe Tena Kuwa Rais wa Marekani

Rais wa Marekani Donald Trump amesema kwamba China inampango wa kutumia kila njia ili kumfanya asichaguliwe  tena kwenye uchaguzi mkuu wa Urais unaotarajiwa kufanyika mwaka huu

Katika mahojiano yaliofanyika katika Ikulu ya Whitehouse na chombo cha habari cha Reuters, amesema kwamba China inakabiliwa na athari chungu nzima kutoka kwa Marekani kutokana na mlipuko wa virusi vya corona.

Anasema China ilificha kuhusu ugonjwa wa Corona na hivyo kuufanya usambae dunia nzima na kuleta madhara makubwa. 

Hata hivyo, Trump yeye mwenyewe amekuwa akikosolewa vikali  kwa Jinsi anavyokabiliana na tatizo hilo.

Mlipuko wa virusi vya corona umeharibu uchumi wa Marekani ambao Trump alikuwa akitumia  kama kinga kujipigia debe ili kuchaguliwa tena katika uchaguzi wa mwezi Novemba mwaka huu.

"China inafanya kila mbinu za kutaka nishindwe katika uchaguzi ujao. Wanataka mpinzani wangu mkuu kutoka chama cha Democrat Joe Biden ndo ashinde uchaguzi wa mwezi Novemba."-Trump

Aidha, Trump amepinga vikali utafiti uliofanyika nchini humo na kutoa maoni kwamba mpinzani wake  Biden  ana asilimia kubwa za kuibuka  mshindi.

"Siamini kura hizo za maoni....Naamini  raia wa taifa hili ni watu werevu. Na sidhani kama watamchagua mtu ambaye hawezi kuwasaidia kutatua  changamoto zao''. -Trump


Share:

Mahakama Yaamuru Zitto Kabwe Akamatwe

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, inatarajia kusoma hukumu ya Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe Mei 29 mwaka huu huku ikitoa hati ya kumkamata kwa kutohudhuria kwenye shauri lake bila taarifa.

Amri hiyo ya kumkamata Zitto ambaye anakabiliwa na mashtaka matatu ya uchochezi, ilitolewa jana mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi.

Hukumu ilipangwa kusomwa Mei 29 mwaka huu, baada ya upande wa mashtaka na utetezi kufunga ushahidi na kuwasilisha majumuisho ya mwisho kwa kuirahisishia mahakama kufikia uamuzi.

Wakili wa Serikali Mkuu, Tumaini Kweka, alidai shauri lilitajwa kwa ajili ya kupanga tarehe ya hukumu ambapo mshtakiwa hakuwepo na hakuna taarifa kuhusu kushindwa kufika kwake mahakamani.

”Mheshimiwa Hakimu mshitakiwa hayupo na muda wa mahakama unafahamika ni saa tatu asubuhi na hakuna taarifa yoyote ingawa mshtakiwa hana tabia ya kushindwa kufika mahakamani,” alidai.

Baada ya kudai hayo, Hakimu Shaidi alisema hati ya kukamatwa itolewe, kesi iliahirishwa hadi Mei 29, mwaka huu kwa ajili ya hukumu.

Katika kesi hiyo inadaiwa Oktoba 28 mwaka juzi, Zitto  aliitisha mkutano wa waandishi wa habari uliofanyika ofisi za Makao Makuu ya ACT Wazalendo, akiwa na lengo la kuleta chuki kwa raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kinyume na sheria na kwamba alitoa maneno ya uchochezi dhidi ya Jeshi la Polisi.


Share:

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Mghwira Athibitisha Kuambukizwa Ugonjwa wa Corona

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Mghwira ametangaza kuwa ameambukizwa virusi vya corona vinavyosababisha homa ya COVID-19.

Kiongozi huyo amesema, hafahamu ameambukizwa lini virusi hivyo na kwamba aliamua kupima kwa sababu kazi anazofanya zinahusisha muingiliano mkubwa na watu.

“Nimepima na matokeo yamekuja yameonesha nimeambukizwa virusi vya corona, sioni dalili za ugonjwa sina homa sikohoi lakini vipimo vimeonesha, hii ni dalili kwamba Watu wengi tunaweza kuwa tunetembea tukiamini tuko salama kumbe hatuko salama, sijui niliambukizwa lini “ – RC Mghwira


Share:

Maambukizi ya virusi vya Corona yapindukia 500 Jamhuri ya Demokrasia ya Congo

Visa 500 vya maambukizi vya virusi vya corona vimethibitishwa nchini Jamhuri ya Demokrasia ya Congo, watu 31 wakifariki huku watu 279 wakipona.

Kwa mijibu wa kamati iliyobuniwa kukabiliana na mlipuko huo, gereza la Ndolo limeathirika na mlipuko wa virusi hivyo, huku visa 4 vya maambukizi vikiripotiwa katika gereza hilo na wafungwa wengine 25 wakifanyiwa vipimo.

Mkoa wa Kinshasa unaongoza kwa wagonjwa wengi wa Corona, ukifuatiwa na Mkoa wa Kivu Kaskazini.

Hivi karibuni serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo iliwarejesha raia wake 165 walio kuwa wanaishi ugenini na ambao walikuwa wamezuiliwa kurejea nchini humo baada ya nchi nyingi kufunga mipaka kutokana na kuibuka kwa janga la Corona.


Share:

Picha : KASHWASA YATOA MSAADA WA MAPIPA KUONGEZA NGUVU MAPAMBANO DHIDI YA CORONA WILAYA YA SHINYANGA


Mkurugenzi Mtendaji wa KASHWASA Mhandisi Joshua Mgeyekwa (kushoto) akimkabidhi Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko mapipa 20 yenye lita 210 kwa ajili ya kukabiliana Virusi Vya Corona ‘Covid – 19’ katika wilaya ya Shinyanga.

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira katika mji wa Kahama na Shinyanga (Kahama Shinyanga Water Supply and Sanitation Authority(KASHWASA) inavyozalisha na kusambaza maji nchini imetoa msaada wa mapipa 20 yenye lita 210 kwa ajili ya kuunga juhudi za serikali katika mapambano dhidi ya Virusi Vya Corona ‘Covid – 19’ kwenye maeneo huduma za kijamii katika wilaya ya Shinyanga.

Mapipa hayo yamekabidhiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa KASHWASA Mhandisi Joshua Mgeyekwa kwa Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko leo Alhamis Aprili 30,2020.

Mhandisi Mgeyekwa amesema KASHWASA itaendelea kushirikiana na serikaliH katika mapambano dhidi ya Virusi vya Corona kwani Corona inaweza kuathiri shughuli za kijamii na kiuchumi.

“Tumekabidhi mapipa 20 yenye ujazo wa lita 410 kila moja ambayo yatawekwa kwenye maeneo ya watu wengi katika wilaya ya Shinyanga kwa ajili ya kukabiliana na maambukizi ya Virusi vya Corona”,amesema Mhandisi Mgeyekwa

“Katika kuunga juhudi za serikali kwenye mapambano dhidi ya Corona, KASHWASA imechangia mapipa 140 yenye thamani ya shilingi Milioni 11.8 kwa ajili ya wilaya 8 za mikoa ya Shinyanga,Mwanza na Tabora ambako KASHWASA inafanya kazi zake ambapo kati ya mapipa hayo 140, 20 ni kwa wilaya ya Shinyanga”,ameeleza Mhandisi Mgeyekwa.

Akipokea Mapipa hayo, Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko ameishukuru KASHWASA kwa mchango huo akibainisha kwa utasaidia kuongeza nguvu katika mapambano dhidi ya Virusi vya Corona.

“Kwa niaba ya wananchi wa wilaya ya Shinyanga ninawashukuru sana kwa kutupatia mapipa haya. Tutayapeleka katika Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga ili yakatumike kwenye maeneo ambayo yana mikusanyiko ya watu wengi ikiwemo minada na masoko”,amesema Mhe. Mboneko.

“Mkurugenzi wa halmashauri hakikisheni mapipa/madumu haya yanakuwa masafi na yawe na maji muda. Simamieni pia wananchi wasiweke ndoo tupu bila maji na wanawe kwa maji na sabuni muda wote”,ameongeza Mboneko.

Aidha amesema serikali inaendelea kutoa elimu kuhusu Corona kwa njia mbalimbali huku akiwasisitiza wazazi na walezi kuzuia watoto wasizurure mtaani na wafanyabiashara wasipandishe bei ya vifaa vinavyotumika katika mapambano dhidi ya virusi vya Corona.

Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Mhe. Hoja Mahiba ameahidi kutunza mapipa hayo na kwamba yatawekwa kwenye maeneo yenye huduma za kijamii ikiwemo minada,masoko,zahanati na vituo vya afya.


ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira katika mji wa Kahama na Shinyanga (Kahama Shinyanga Water Supply and Sanitation Authority(KASHWASA) inavyozalisha na kusambaza maji katika maeneo mbalimbali nchini Tanzania, Mhandisi Joshua Mgeyekwa akimkabidhi Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko mapipa 20 yenye lita 210 kila moja kwa ajili ya kuunga juhudi za serikali katika mapambano dhidi ya Virusi Vya Corona ‘Covid – 19’ kwenye maeneo huduma za kijamii katika wilaya ya Shinyanga leo Alhamis Aprili 30,2020. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko (kulia) akijaribu kufungua koki ya moja ya mapipa 20 yenye lita 210 kila moja yaliyotolewa na KASHWASA kwa ajili ya kuunga juhudi za serikali katika mapambano dhidi ya Virusi Vya Corona ‘Covid – 19’ kwenye maeneo huduma za kijamii katika wilaya ya Shinyanga. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa KASHWASA Mhandisi Joshua Mgeyekwa.
Kulia ni Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akizungumza wakati wa kupokea mchango wa mapipa 20 yaliyotolewa na KASHWASA kwa ajili kukabiliana na Maambukizi ya Virusi vya Corona katika wilaya ya Shinyanga. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa KASHWASA Mhandisi Joshua Mgeyekwa.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akiishukuru KASHWASA kwa mchango wa mapipa 20 kwa ajili kukabiliana na Maambukizi ya Virusi vya Corona katika wilaya ya Shinyanga ambapo alisema mapipa hayo yatapelekwa katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira katika mji wa Kahama na Shinyanga (Kahama Shinyanga Water Supply and Sanitation Authority(KASHWASA) Mhandisi Joshua Mgeyekwa akizungumza wakati akimkabidhi Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko (kulia) mapipa 20 kwa ajili ya kuunga juhudi za serikali katika mapambano dhidi ya Virusi Vya Corona ‘Covid – 19’ katika wilaya ya Shinyanga.
Mkurugenzi Mtendaji wa KASHWASA Mhandisi Joshua Mgeyekwa akizungumza wakati akimkabidhi Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko (kulia) mapipa 20 kwa ajili ya kuunga juhudi za serikali katika mapambano dhidi ya Virusi Vya Corona ‘Covid – 19’ katika wilaya ya Shinyanga.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko (katikati) akimkabidhi Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Mhe. Hoja Mahiba (kulia) mapipa 20 yaliyotolewa na KASHWASA ili yakatumike kwenye maeneo yenye huduma za kijamii katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa KASHWASA Mhandisi Joshua Mgeyekwa.
Kulia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Mhe. Hoja Mahiba akizungumza baada ya kupokea mapipa 20 yaliyotolewa na KASHWASA ili yakatumike kwenye maeneo yenye huduma za kijamii katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga. Kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko.
Muonekano wa mapipa yaliyotolewa na KASHWASA kwa ajili ya mapambano dhidi ya Virusi vya Corona katika wilaya ya Shinyanga.
Mkurugenzi Mtendaji wa KASHWASA Mhandisi Joshua Mgeyekwa (kushoto) akimpa zawadi ya Kalenda za KASHWASA Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko baada ya kukabidhi mapipa 20 kwa ajili ya kuunga juhudi za serikali katika mapambano dhidi ya Virusi Vya Corona ‘Covid – 19’ katika wilaya ya Shinyanga.
Mkurugenzi Mtendaji wa KASHWASA Mhandisi Joshua Mgeyekwa (kulia) akimpa zawadi ya Kalenda za KASHWASA Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Mhe. Hoja Mahiba baada ya kukabidhi mapipa 20 kwa ajili ya kuunga juhudi za serikali katika mapambano dhidi ya Virusi Vya Corona ‘Covid – 19’ katika wilaya ya Shinyanga.
Picha ya pamoja baada ya makabidhiano ya mapipa 20 yaliyotolewa na KASHWASA kwa ajili ya kuunga juhudi za serikali katika mapambano dhidi ya Virusi Vya Corona ‘Covid – 19’ katika wilaya ya Shinyanga.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Share:

BMT kuandaa muongozo kuhusu ukomo wa wachezaji wa Nje nchini.

Na Shamimu Nyaki, WHUSM-Dodoma
Serikali haijatoa ukomo wa wachezaji kutoka nje kushiriki michezo hapa nchini bali imeibua mjadala kwa wadau ili watoe maoni yao.
 
Hayo yamesemwa Jijini Dodoma na Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo Bw.Yusuph Singo kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ikiwa ni hatua ya kuboresha na kuimarisha sekta ya michezo nchini. 
 
Ili kutekeleza mjadala huo, Baraza la Michezo la Taifa (BMT) limepewa jukumu la kuendelea kuandaaa mwongozo utakaotumika kukusanya maoni kutoka kwa wadau kuhusu ukomo wa wanamichezo wa nje hapa nchini.
 
“Katika Hotuba ya Bajeti iliyosomwa hivi karibuni Bungeni jijini Dodoma na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe, hakuongolea idadi ya wachezaji kutoka nje wanaotakiwa kucheza nchini, bali aliagiza BMT kuandaa mjadala mpana katika kukusanya maoni kwa wadau wa michezo kuhusu namna bora ya kusajili wachezaji wa kigeni katika michezo yote hapa nchini” alisema Bw. Singo.
 
Pamoja na hayo, Mkurugenzi huyo ambainisha kuwa Mhe.Waziri Dkt. Mwakyembe alisisitiza kuwa wanamichezo wote kutoka nje ya nchi wanaosajiliwa hapa nchini ni lazima wawe na ubora pamoja na viwango vinavyotakiwa.
 
Akifafanua suala hilo Bw. Singo amesema kuwa michezo yote ya kulipwa kwa sasa imeendelea kukua duniani kote na nchi yetu pia inayo wachezaji wengi wanaocheza michezo hii ikiwemo Mpira wa Kikapu (Basketball), Kriketi, Mpira wa Miguu na michezo mingine, hivyo, Serikali haijatoa maelekezo ya ukomo wa usajili wa idadi ya wachezaji bali inataka kuwepo kwa mjadala wa wazi utakaotoa mwongozo wa ukomo wa idadi ya usajili wa wachezaji wa kigeni.
 
Aidha, Mkurugenzi huyo alitoa rai kwa wadau wa michezo nchini watakapopata fursa ya kuchangia au kutoa maoni katika mjadala huo wasiegemee katika timu wanazoshabikia, bali watoe maoni ambayo yatasaidia kuendeleza michezo na kuendeleza vipaji vya wanamichezo wetu pamoja na kukuza michezo nchini.
MWISHO






Share:

CCM Watuma Salam za Rambirambi Kifo cha Mbunge Richard Ndassa




Share:

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi April 30



















Share:

Wednesday, 29 April 2020

MAJAMBAZI WAVAMIA KANISA KATOLIKI KATOLIKI PAROKIA YA MODEKO MOROGORO..KANISA LAFUNGWA KWA KUFURU

Na Angela Kibwana, Morogoro Na P. Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.
Mheshimiwa Padre Lazarus Vitalis Msimbe, S.D.S., Msimamizi wa Kitume wa Jimbo Katoliki la Morogoro nchini Tanzania amefunga Kanisa la Parokia ya Bikira Maria Mtakatifu baada ya kuwasiliana na Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania na Ubalozi wa Vatican nchini Tanzania. 

Kuanzia tarehe 27 Aprili 2020 Kanisa la Parokia ya Modeko limefungwa na halitaweza kutumika kwa sasa hadi pale, Tabernakulo mpya itakapowekwa wakfu.

 Ibada hii inatarajiwa kuadhimishwa wakati wa Sherehe ya Ekaristi Takatifu, fursa makini kwa waamini kutangaza na kushuhudia imani ya Kanisa kuhusu Fumbo la Ekaristi Takatifu, yaani uwamo wa Kristo katika maumbo ya Mkate na Divai. 

Mababa wa Kanisa wanathibitisha kwamba, kwa nguvu ya imani ya Kanisa na uwezo wa Neno la Kristo Yesu, na tendo la Roho Mtakatifu, kwamba, mageuzo ya Mkate na Divai yanakuwa ni Mwili na Damu Azizi ya Kristo.

Padre Nikodemas Masong, Paroko wa Parokia ya Modeko, Jimbo Katoliki la Morogoro amesema, watu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi tarehe 27 Aprili 2020 walivamia na kuvunja mlango wa Kanisa la Parokia ya Modeko na kufanikiwa kuiba Tabernakulo iliyokuwa inahifadhi Ekaristi Takatifu na kutokomea mahali kusikojulikana. 

Walivunja pia milango ya ofisi za Parokia na kufanikiwa kuiba kiasi cha shilingi laki tatu na nusu, mali ya Chama cha Watumishi wa Altare Parokiani hapo. Walifanikiwa pia kuiba “Mixer” inayotumika kwa ajili ya mawasiliano Parokiani hapo.

 Familia ya watu wa Mungu ndani na nje ya Jimbo Katoliki la Morogoro imesikitishwa sana na kufuru hizi dhidi ya mahali na mambo matakatifu yanayogusa undani wa imani ya watu.


Via Vatican News
Share:

WAZIRI JAFO ATOA MAELEKEZO KUHUSU MPANGO WA UFUNDISHAJI WANAFUNZI KIELEKTRONIKI

Nteghenjwa Hosseah – OR-TAMISEMI
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI)Selemani Jafo amelitaka Baraza la Mitihani Tanzania(NECTA) na Taasisi ya Elimu Tanzania(TET), kuhakikisha utaratibu wa kufanya marejeo ya mitihani ulioanza kwa kidato cha sita uhusishe madarasa yote yanayotarajia kufanya mitihani ya Taifa.

Aidha, amewataka wanafunzi kuzingatia ratiba ya masomo inayotolewa ili wasikose vipindi vinavyorushwa kwenye redio,runinga na mitandao ya kijamii.

Jafo alitoa kauli hiyo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu utaratibu wa masomo kwa njia ya runinga,redio na mitandao ya kijamii.

Alitaka taassi hizo kuangalia utaratibu huo wa marejeo kwa madarsa mengine kama kidato cha pili,cha nne,darasa la saba na la nne ili nao wawe na umahiri katika kujibu mitihani yao.

Alisema Serikali kupitia wadau mbalimbali imetoa fursa hiyo muhimu ambayo inapaswa kuzingatiwa na watu wote wakiwemo wazazi,walimu na wanafunzi wenyewe.

“Niwatake wanafunzi wote hasa wa kidato cha sita ambao sasa maandalizi ya kufanya marejeo yanafanyika,tutumie fursa hii vizuri ya kujiandaa kwa utaratibu mpya utakaotumika kuanzia mwaka huu wa kupima umahiri tofauti na ule wa awali wa kuulizana maswali tuliouzoea,”alisema Jafo.

Aliongeza kuwa “Wanafunzi tumieni fursa hii iliyoletwa kwenu,zingatia ratiba,jipimeni uwezo wenu ili wenzio wasikuache nyuma pindi mkirudi shuleni,someni kwa bidii kwa maana tunataka kuelekea kwenye Taifa lenye uchumi imara.”

Aliwataka walimu kutumia fursa hiyo kujijengea uwezo wao wenyewe pia lakini kuwawezesha kuwa na uelewa zaidi ili wanafunzi wao watakapohitaji msaada pale watakapokwama wawe wanajua nini kinachoendelea.

“Walimu wetu najua mtu huwezi kuwa mkamilifu kwenye maeneo yote,kwa upande wenu hii pia ni fursa ya kujijengea uwezo kupitia walimu waliopo kwenye program hii ili ukirudi shuleni unakuwa umeongeza kitu kipya,lakini mwanafunzi wako anaweza kukupigia simu ameshindwa kuelewa sehemu Fulani hivyo inakuwa rahisi kumuelewesha,”alisema Jafo.

Waziri Jafo alisema kama Waziri anayesimamia elimu ya awali,msingi na sekondari amefarijika kuanza kwa utaratibu huo na ni imani yake kuwa pengo la vijana waliokuwa wanakaa nyumba bila ya msaada wowote wa kimasomo linaenda kuzibika.

“Wazazi wapeni nafasi watoto wenu ya kushiriki vipindi vyote vinavyotolewa, inawezekana vipindi vinaendelea wewe mzazi umempa mtoto wako kazi nyingine anafanya hilo sio sahihi, toa ushirikiano wa kutosha kuhakikisha watoto wanasoma na kufanya mazoezi yote yanayotolewa na walimu,”alisisitiza Jafo.

Jafo alivitaja vyombo vya habari ambavyo vinashiriki kikamilifu katika mpango huu wa ufundishaji wa vipindi kwa njia ya Televisheni na Radio kuwa ni TBC, ZBC, Azam Tv, Channel Ten, Clouds Fm, Global Tv, Gel Tv na Radio mbalimbali.

Pia aliwakumbusha wazazi na wanafunzi wote kuwa vipindi hivyo vitakua vinarushwa kupitia mtandao wa Youtube kwa ajili ya marudio ili kujenga uelewa zaidi.

“Mitandao ya Youtube itakayokuwa inarusha vipindi hivyo ni ya Baraza la Mitihani – NECTA, Taasisi ya Elimu Tanzania – TEA, Global Education Link – GEL, Global Tv, Azam Tv, ZBC TV na EATV” alisisitiza Jafo.

Alizipongeza taasisi zote binafsi zilizoshirikiana na Serikali kuhakikisha lengo lake linatimia katika kipindi hiki cha mpito cha ugonjwa wa Corona unaosababisha homa kali ya mapafu(COVID 19).

Alizataja Taasisi hizo kuwa ni Mawakala wa Vyuo Vikuu Nje ya Nchi yaan Global Education Link (GEL), UNESCO na Taasisi ya Elimu Solution.


Share:

LHRC YAZINDUA RIPOTI YA HAKI ZA BINADAMU TANZANIA 2019


Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC, Anna Henga (katikati), Afisa Utafiti, Fundikila Wazambi (kushoto) na Mkurugenzi wa Uwajibikaji na Uwezeshaji wa Kituo hicho, Felista Mauya (kulia) wakionesha nakala za Ripoti ya Haki za Binadamu Tanzania 2019 mara baada ya uzinduzi leo Jumatano  leo Aprili 29, 2020 katika ofisi za LHRC jijini Dar es Salaam na wadau kufuatilia kwa njia ya mtandao.
Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC, Anna Henga (katikati) akikata utepe kama ishara ya uzinduzi wa Ripoti ya Haki za Binadamu Tanzania 2019. Uzinduzi huo uliofanyika  leo Aprili 29, 2020 katika ofisi za LHRC jijini Dar es Salaam na wadau kufuatilia kwa njia ya mtandao.

***
Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kimezindua Ripoti ya Haki za Binadamu Tanzania 2019 inayoangazia hali ya haki za binadamu kwa mwaka 2019 na kufanya ulinganisho wa hali ilivyokuwa mwaka 2018. 

Uzinduzi huo umefanyika leo Jumatano, Aprili 29, 2020 kwa njia ya mtandao kufuatia mlipuko wa virusi vya Corona. 

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC amesema ripoti hiyo inahusisha matukio ya ukiukwaji wa haki za binadamu sambamba na mapendekezo kwa ajili ya uboreshaji wa sera, sheria na utendaji katika jamii. 

Anna amesema ripoti hiyo inaangazia hali ya haki za binadamu katika nyanja za haki za kiraia na kisiasa; haki za kiuchumi, kijamii na kiutamaduni; haki za makundi yaliyo hatarini; mifumo ya Ulinzi wa Haki za binadamu na haki za kijumla.

“Ripoti hii ni matokeo ya taarifa mbalimbali zilizokusanywa na LHRC ikiwemo taarifa kutoka kwa waangalizi wa haki za binadamu walio nchi nzima, wasaidizi wa kisheria walio katika wilaya mbalimbali, taarifa rasmi toka taasisi za Serikali, Bunge, Mahakama, jeshi la polisi, vyombo vya habari na asasi mbalimbali za kiraia zisizo za Serikali. Taarifa hii pia hutumia taarifa mbalimbali za kitaifa lakini pia na za kimataifa, hasa zinazolenga kuelezea hali ya haki za binadamu nchini”, amesema Anna Henga.

Kwa mujibu wa Ripoti hiyo, haki tano zilizokiukwa zaidi kwa mwaka 2019 ni pamoja na:

Haki ya Kuishi ambapo matukio kama vile mauaji ya wanawake, mauaji ya watoto, mauaji yanayotokana na kujichukulia sheria mkononi, mauaji yanayotokana na imani za kishirikina pia yameendelea kuripotiwa.

Uhuru dhidi ya ukatili; ambapo matukio yaliyoripotiwa ni Ukatili wa kingono na kimwili dhidi ya watoto; ukatili wa kingono na kimwili dhidi ya wanawake. Katika kipindi cha kuanzia mwaka 2017 hadi mwezi Juni 2019, jumla ya matukio 88,612 ya ukatili wa kijinsia yameripotiwa.Matukio ya ukatili wa kingono dhidi ya watoto jumla ya matukio 3,709 ya ubakaji yaliripotiwa katika vituo vya polisi nchini ikiwa ni matukio 126 zaidi ya yale yaliyoripotiwa katika kipindi kama hicho mwaka 2018. ukatili dhidi ya watu wenye ulemavu na wazee nao umeendelea kushika kasi katika tukio moja, bibi wa miaka aliripotiwa kubakwa hadi kufariki. 

Uhuru wa Kujieleza; muendelezo wa uminywaji wa uhuru wa kujieleza ambapo kumekuwepo na Sheria kandamizi, ukamataji na uwekaji kizuizini waandishi wa habari kinyume na sheria pamoja na kufungiwa kwa vyombo vya habari

Haki ya kuwa Huru na Salama; Ripoti imeripoti matukio kadhaa yanayopelekea kuminywa kwa haki hiyo kama vile Mashambulizi na mauaji ya madereva bodaboda pamoja na Matukio ya utekaji, watu waliopotea na matukio ya ukamataji na uwekaji kizuizini kinyume na sheria.

Haki ya Kujumuika na Kukusanyika; zimeendelea kukiukwa hasa kipindi hiki ambapo tunaelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2020. Vyama vya siasa, hususan vya upinzani, viliendelea kulalamikia maamuzi haya kwamba yanakiuka haki yao inayolindwa na Katiba, jambo linaloathiri pia ushindani wao kwenye Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020. Vyama hivi pia vililalamika kwamba marekebisho ya Sheria ya Vyama vya Siasa yanaminya uhuru wao wa kujumuika na kukusanyika.

LHRC kupitia Mkurugenzi Mtendaji wake, Anna Henga wametoa rai kwa serikali na wanajamii kwa ujumla kuchukau hatua katika kulinda na kudumisha haki za binadamu. 

“Tunatoa rai kwa serikali, taasisi na jamii ya Watanzania kuendelea kulinda haki za binadamu na kuwawajibisha wale ambao wameshindwa kuheshimu haki hizo bila ubaguzi wa kikabila, kidini, kisiasa na kijinsia ili tuweze kuifikia jamii yenye haki na usawa”,amesisitiza Anna Henga.

Ripoti ya Haki za Binadamu Tanzania 2019 ni muendelezo wa ripoti za kituo hicho zinazotolewa kila mwaka kwa lengo la kuonesha hali na kutoa mapendekezo ya maboresho.
Share:

RAIS MAGUFULI ATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KUFUATIA KIFO CHA MBUNGE WA SUMVE, RICHARD NDASSA




Share:

JITIBU TATIZO LA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME KWA KUTUMIA FULL POWER.. UUME MDOGO ZAT 50 NDIYO SULUHISHO



Zati 50
Full Power


Sababu za upungufu wa nguvu za kiume na maumbile madogo ya uume:

⇒Ngiri,


⇒Henia


⇒Kisukari


⇒Tumbo kujaa gesi

⇒Kutopata choo vizuri


⇒Utumiaji madawa kwa muda mrefu


⇒Unywaji wa pombe kupita kiasi


⇒Msongo wa mawazo 

⇮⇒Haya yote hupelekea mwili kutokuzalisha homoni ya gesrtogine au kuwa chache na kushindwa kupata mzunguko mzuri wa damu na vichocheo vingine kama madini ya zinki ambayo hukufanya kuwa na msisimko  na kufanya kuwa na muda  mrefu na nguvu za kutosha.

ZAT 50

⇨ Inarutubisha maumbile ya uume  na kunenepesha urefu nchi 6,unene sentimita 4

⇨Dawa hii ni ya kutibu kabisa tatizo hilo.


FULL POWER

⇨Ni dawa ya vidonge ya miti shamba inaongeza nguvu za kiume na kutibu kabisa tatizo hilo.

⇨Inaongeza hamu ya tendo la ndoa
⇨Inakufanya uchelewe kufika kileleni zaidi ya Dakika 30 na kurudia tendo zaidi ya mara nne na zaidi.

Pia tunatibu Magonjwa mengine Kama

Matatizo ya pumu,Bawasiri, vidonga vya tumbo,Kisukari,Magonjwa sugu ya zinaaa,Kaswende,U.T.I , kiuno,miguu kuwaka moto, Fangasi sehemu za Siri, kupunguza unene wa mwili,tumbo kuunguruma,kujaa gesi, matatizo ya uzazi kwa wanawake, kurutubisha mbegu za uzazi kwa akina baba, matatizo ya meno tunatibu bila kungoa

Kliniki yetu inapatikana Zanzibar, Dar es salaam na Shinyanga.

Wasiliana nasi kwa simu namba 071770 22 27
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger