Tuesday, 28 April 2020

Rais Magufuli Atuma Salamu za Rambirambi Kufuatia Kifo cha Jaji Mkuu Mstaafu, Augustino Ramadhani




Share:

Kitwanga Atishia Kuigomea Bajeti Wizara Ya Maji

Mbunge wa Misungwi, Charles Kitwanga, amesema atapiga kura ya hapana kwenye bajeti kuu na Wizara ya Maji, iwapo hawatafafanua kuhusu mgawanyo wa mradi wa India utakaotekelezwa katika miji 28 wakati ungeweza kutekekezwa katika miji 50.

Amesema kuwa mradi huo hauna thamani ya fedha kwa kuwa kila mmoja unagharimu dola milioni 17 sawa na Shilingi Bilioni 39 wakati kiuhalisia unatakiwa kugharimu Sh.Bilioni 12," amesema.

"Chukua dola Bilioni 50 gawanya kwa miji 28 utapata milioni 17.2 sawa na Bilioni 39 na zaidi, bila kufanya marekebisho sitaunga mkono hoja kwa kuwa najua kinachoendelea na ushahidi nikishauleta...kama mlisema mkataba wa Lugumi ni mbaya sasa hii ni zaidi ya Lugumi na siku nikipewa nafasi nitasema kuhusu Lugumi, "amesema.


Share:

Wenye Virusi Vya Corona Zanzibar Wafika 105......Ni Baada ya Wengine 7 Kuongezeka




Share:

TANZIA: Jaji Mkuu Mstaafu, Augustino Ramadhani afariki dunia

Jaji Mkuu Mstaafu wa Tanzania, Augustino Ramadhani amefariki dunia leo asubuhi katika Hospitali ya Aga Khan, jijini Dar baada ya kuugua maradhi ya moyo.

Familia yake imesema hali ya Jaji Ramadhani ilibadilika jana usiku na kukimbizwa hospitalini hapo ambapo mauti ilimkuta leo asubuhi.
 
Jaji Augustino Ramadhani pia alikuwa Brigedia Jenerali kabla ya kuitwa katika sekta ya Sheria na kutumikia Mahakama.

Alipostaafu ujaji, alipewa kazi ya ukasisi, akatawazwa rasmi kuwa Mchungaji wa Dayosisi ya Kanisa la Anglikana lililopo Mkunazini Zanzibar na hivyo kuitwa “Mchungaji Augustino Ramadhani”


Share:

Bodi Ya Mkonge Yatekeleza Agizo La Waziri Mkuu

Na.Bashiri Salum,Wizara ya Kilimo,Tanga
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Gerald Kusaya ameipongeza Menejimenti ya Bodi ya Mkonge na watumishi kwa kutekeleza agizo la Waziri Mkuu la kuhamia katika ofisi iliyotwaliwa na serikali hivi karibuni kutoka kwa wamiliki binafsi.

Kusaya ametoa pongezi hizo jana (tarehe 27.O4.2020) Jijini Tanga wakati alipokwenda kufanya ufuatiliaji wa utekelezaji wa maagizo yaliyotolewa na Waziri Mkuu mwezi Machi mwaka huu kufuatia ripoti ya kamati ya uchunguzi kuhusu mali za bodi ya mkonge kumilikishwa kwa watu binasfi kinyume cha utaratibu.

“Nawapongeza menejimenti mpya ya Bodi ya Mkonge kwa kutekeleza kwa vitendo agizo la Waziri Mkuu Kassim Majaliwa la kuhamia katika jengo hili na kuendelea na kazi za kusimamia zao la mkonge”alisema Kusaya

Waziri Mkuu aliagiza kuwa jengo lililokuwa linamilikiwa visivyo halali na Willian Kimweli Madundo na kulitumia kama Medicare hospital Tanga litumike kuwa makao makuu ya bodi kwani miaka ya nyuma ndipo palikuwa makao makuu ya Mamlaka ya Mkonge Tanzania .

Aidha,Katibu Mkuu huyo aliigiza bodi ya mkonge kuhakikisha inafuatilia mali zake ikiwemo nyumba 32 ambazo zilirejeshwa serikalini “ nataka waliokuwa wamiliki wapewe notisi na kuondoka au wapewe mikataba ya upangaji  haraka” alisisitiza

“Bado kuna nyumba mbili nchini Uingereza,nataka zirejeshwe serikalini na zile nyumba mbili jirani na Mkonge hotel hapa Tanga zifuatiliwe kujua uhalali wa umiliki wake “ alisema Katibu Mkuu huyo

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Mkonge Saad Kambona alimweleza Katibu Mkuu kuwa tayari wameanza kufanya kazi kwenye jengo jipya la ofisi kama walivyoagizwa na wamefanya ukarabati mdogo kuwezesha jengo hilo kutumika kama ofisi badala ya ofisi za zamani uwanja wa gofu Tanga .

Kambona alisema kwa sasa wanaiomba serikali kuendelea kuiwezesha bodi ili iweze kuhudumia zao la mkonge wakati ikijipanga kuanza kujitegemea kimapato.

‘Tuna lengo baada ya kuimarisha usimamizi wa zao la mkonge nchini,bodi iweze kutoa gawio kwa serikali “alisema Kambona.

Katika hatua nyingine Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martin Shigela aliipongeza Wizara ya Kilimo kwa jitihada zake za kufufua zao la mkonge kwani ndio uti wa mgongo wawananchi wa Tanga.

Shigela alisema ni wakati sasa wizara ya kilimo ikaongeza msukumo katika kuhakikisha mbegu za mkonge zinapatikana kwa wingi na wakulima wanazipata kwa gharama nafuu. Mwisho

Imetolewa na ;
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Wizara ya Kilimo
TANGA
28.04.2020


Share:

Kumbuka Kuiharibu Vizuri Barakoa Yako Baada Ya Kumaliza Kuitumia Ili Kuepuka Kusambaza Magonjwa

Na WAMJW- DSM
Serikali kupitia Wizara ya Afya, imetoa wito kwa wananchi kuteketeza Barakoa zao vizuri baada ya kumaliza matumizi yake kisha kuitupa sehemu salama ili kuepusha kusambaa kwa magonjwa ya mlipuko hususan ugonjwa wa homa kali ya mapafu inayosababishwa na virusi vya Corona.

Wito huo, ameutoa Mkuu wa Kitengo cha maji na usafi wa mazingira, Wizara ya Afya, Ndg. Anyitike Mwakitalima wakati akitoa elimu kwa wakazi wa Jiji la Dar es Salaam kuhusu kuchukua tahadhari za kujikinga dhidi ya maambukizi ya virusi vya Corona.

“Wale ambao mmevaa Barakoa (mask) zile ambazo zinatakiwa kutupwa baada ya kutumika (disposable mask) , ukumbuke kabla hujaitupa uitoboe ili mtu mwingine asiweze kuiokota na kuisafisha na kuirudisha katika mzunguko jambo litalosaidia kuepusha magonjwa ya mlipuko hususan ugonjwa wa Corona” alisema.

Alisema, katika baadhi ya nchi imethibitika kuwa, mgonjwa mmoja wa Corona anaweza kuambukiza mpaka watu kumi kwa wakati mmoja hii inatokana na mwingiliano uliopo baina ya watu, hivyo kutoa wito juu ya kuchukua tahadhari kwa hali ya juu.

“Kwa baadhi ya nchi zilizopata maambukizi, inasemekana kuwa, mtu mmoja aliyeambukizwa virusi hivi anauwezo wa kuambukiza mpaka watu kumi kwa wakati mmoja” alisema.

Aidha, alisema kuwa, kwa wale ambao wanatumia Barakoa za kitambaa, kuhakikisha wanabadirisha mask hizo kila baada ya masaa manne ili kuepusha kupata magonjwa mengine, huku akisisitiza kuwa, ni muhimu kabla ya kuivaa zifuliwe kwa maji na sabuni kisha ipigwe pasi ili kujiweka salama zaidi dhidi ya magonjwa.

“Kwa wale ambao mnavaa Barakoa (mask) za kitambaa basi mkumbuke kuwa, mask hiyo inatakiwa ivuliwe kila baada ya masaa manne mpaka sita, na hakikisha kuwa, unaifua kwa maji na sabuni, umeinyoosha ili kama kuna virusi humo waweze kufa, usivae barakoa (mask) ambazo ni chafu” alisema

Kwa upande wake, Sfaff sergeant (S/Sgt ) Valentine Ngowi, alisisitiza kuwa, wazazi watoe elimu kwa watoto kujikinga dhidi ya maambukizi ya virusi vya Corona kwa kuhakikisha wananawa mikono kwa sabuni na maji safi yanayotiririka, huku akisisitiza waepuke kuzulula mtaani kuepusha kuokota Barakoa zilizotupwa hovyo bila utaratibu.

Nae Balozi wa kampeni ya Mikoni safi, Tanzania salama, Msanii Mrisho Mpoto (Mjomba), amewakumbusha Watanzania kuepuka msongamano katika maeneo yote, huku akisisitiza kuwa, kama hakuna sababu yakutoka nje ni vema watulie majumbani.


Share:

MBUNGE WA CHADEMA JOSEPH SELASINI ALALAMIKA KUPIGWA REMOVE GROUP LA WHATSAPP


Mbunge wa Rombo kupitia CHADEMA  ,Joseph Selasini, ameonesha kusikitishwa baada ya kuondolewa bila kupewa taarifa kwenye 'Group la WhatsApp' la Wabunge wa chama chake, ambalo pia yumo Mwenyekiti wa chama hicho Freeman Mbowe.


"Namshukuru Katibu wa Bunge kwa kuwasilisha ombi langu mbele yako, leo natoa mchango wangu nikiwa nimetengwa na familia ya kisiasa group la WhatsApp la chama changu, ambalo wapo viongozi wakuu wa chama changu, bila kupewa taarifa ya kukemewa au juu ya hatua hiyo iliyochukuliwa, alisema.

Amesema tangu kuanza kwa kikao cha bajeti ndiyo mara ya kwanza kusimama kuchangia baada ya kupata ridhaa ya meza ya Spika.



Share:

GGML YATOA SH BILIONI 1.6 KUUNGA MKONO MAPAMBANO DHIDI YA CORONA


Mmoja wa wakazi wa Mji wa Geita wakiosha mikono kwa maji tiririka na sabuni kutoka kwenye vifaa vilivyotolewa na kampuni ya GGML
Baadhi ya wakazi wa Mji wa Geita wakiosha mikono kwa maji tiririka na sabuni kutoka kwenye vifaa vilivyotolewa na kampuni ya GGML
Mkurugenzi Mtendaji wa GGML, Richard Jordinson akizungumza

***

NA MWANDISHI WETU

Kampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML) imetoa Sh bilioni 1.6 kuunga mkono juhudi za Serikali kudhibiti maambukizi ya Virusi vya Corona ambayo hadi sasa yamesambaa katika nchi 210 duniani Tanzania ikiwemo.

Pia GGML imezindua mikakati kadhaa ya kupambana na janga la virusi hivyo vinavyosababishwa ugonjwa wa Covid–19 katika eneo lake la kazi na kwa jamii zinazozunguka mgodi wake.

Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa GGML, Wayne Louw imefafanua kuwa katika fedha hizo, Sh bilioni 1.1 zitaelekezwa kwenye ngazi ya kitaifa kupitia Mfuko Maalum wa mapambano dhidi ya Covid – 19 ambao unasimamiwa na ofisi ya Waziri Mkuu.

Alisema fedha zingine kiasi cha Sh milioni 500 zitatumika kwa ajili ya kusaidia juhudi zinazofanywa katika ngazi ya mkoa na jamii, zitakazojumuisha ununuzi wa vifaa-tiba muhimu na vitendea kazi kama vile vifaa vya kujikinga, barakoa, mashine za kusaidia upumuaji, nk.

Aidha, alisema GGML kwa kushirikiana na Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Geita (GEUWASA) imeweka matanki 10 ya maji yenye uwezo wa kubeba lita 1000 kila moja kwa ajili ya kuwezesha watu kunawa mikono.

Alisema jukumu la GEUWASA litakuwa ni kujaza maji katika matenki hayoambayo yamewekwa katika maeneo yenye watu wengi mjini Geita.

“GGML pia itatoa dawa aina ya Chlorine ili kutakasa maji hayo, na kwa hiyo hakutakuwa na ulazima wa kutumia sabuni. Matenki mengine yanaendelea kutengenezwa kwa ajili ya Watoto na watu wenye ulemavu.

“Nia yetu ni kuendelea na shughuli zetu kama zilivyopangwa na tunatumaini kwamba janga hili litakwisha hivi karibuni. Kwetu sisi, shughuli zetu zinajumuisha uzalishaji wa dhahabu na pia utekelezaji wa miradi ya kusaidia jamii inayotuzunguka,” alisema.

Naye Meneja Mwandamizi anayeshughulikia masuala ya afya mahali pa kazi, Dk. Kiva Mvungi alisema katika kujenga uelewa juu ya janga hili kwa jamii zinazozunguka mgodi, kampuni hiyo imekuwa ikigawa vipeperushi vyenye taarifa za virusi ndani na nje ya mgodi.

“Katika kutumia vyombo vya habari kwa ajili ya uelimishaji juu ya janga la Covid-19, GGML imeingia ubia na Rubondo fm, ambacho ni kituo cha redio kinachomilikiwa na Halmashauri ya Wilaya ya Geita. Chini ya ubia huu, Kampuni ya GGML inagharimia uandaaji wa tangazo, na kituo cha Rubondo fm kitatoa mchango wake kwa kurusha tangazo hilo bila malipo",alisema. 

Alisema Kituo cha Rubondo fm kilianzishwa kwa ufadhili wa GGML chini ya Mpango wa uwajibikaji kwa Jamii (Corporate Social Responsibility) wa kampuni hiyo.

“Tunafanya kazi kwa ushirikiano wa karibu na Serikali. Maofisa wetu wawili wameteuliwa na Mkuu wa Mkoa kuwa sehemu ya kamati maalum iliyoteuliwa kupambana na janga hili hapa Geita. Wawakilishi wetu hawa wanahakikisha kwamba mipango yetu ya kupambana na Covid – 19 inaendana na ile ya Serikali”, alisema Dk. Mvungi.
Share:

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumanne April 28




















Share:

Monday, 27 April 2020

Serikali yapokea msaada wa shilingi bilioni 14.9 wa Kupambana na Janga la Corona

Na WAMJW-Dar es Salaam
Serikali imepokea msaada wa shilingi bilioni 14.9 kutoka Global Fund, Airtel Tanzania, Rotary Club Tanzania ambazo sehemu kubwa zitatumika kununua vifaa kinga kwa watumishi wa afya na vifaa tiba kwa ajili ya kuwahudumia wagonjwa wenye maambukizi ya COVID-19.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu ameyasema hayo leo wakati akipokea msaada wa fedha na lita 1,250 za vitakasa mikono ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono juhudi za Serikali za kupambana na maambukizi ya virusi vya Corona.

Waziri Ummy amefafanua kwamba Global Fund imetoa shilingi bilioni 14, Airtel Tanzania shilingi milioni 700 na Rotary Club Tanzania shilingi milioni 250.

“Tumepokea shilingi bilioni 14 kutoka Global Fund, shilingi bilioni 9.6 tumezitoa kwa ajili ya kununua vifaa kinga kwa ajili ya watumishi wa Afya, lakini pia fedha zilizotolewa na Airtel na Rotary Club Tanzania tutazielekeza huko. Kipaumbele chetu ni kuwalinda watumishi wa afya,” amesema Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu.

“Natumia fursa hii kuwashukuru watumishi wa afya ambao wamekuwa wakijitoa usiku na mchana katika kutoa huduma kwa watu waliopata maambukizi ya virusi vya Corona (Covid-19) pamoja na wale wahisiwa.

“Kipaumbele cha Serikali ni kuwalinda watumishi wa Afya kwa kununua vifaa kinga kwani fedha tulizozipata hapa tutazielekeza kwenye ununuzi wa vifaa kinga. Niendelee kuwaisistiza Watumishi wa Afya wazingatie miongozo ya magonjwa ya kuambukiza,” Amesema Waziri Ummy .

Amesema watumishi wa afya ambao wamepatiwa mafunzo katika vituo vya kutoa huduma kwa wenyr maambukizi ya ugonjwa huo, hakuna aliyepata maambukizi kwa kuwa wanazingatia miongozo ya Serikali ya kutoa matibabu kwa wagonjwa wa Covid-19 pamoja na miongozo ya magonjwa ya kuambukiza.

Waziri amesema ushiriki wa kila mdau katika mapambano dhidi ya maambikizi ya virusi vya Corona ni muhimu na kwamba msaada uliotolewa na kampuni hizo ni mkubwa katika mapambano ya maambukizi ya ugonjwa wa Corona.

“Napenda kurudia tena kwa niaba Mhe. Rais Dkt. John Magufuli, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, nawashukuru Airtel Tanzania, Serengenti Breweries na Rotary Club kwa hiki mlichotupatia. Asanteni sana,” amesema Waziri Ummy.

Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Airtel Tanzania, Bw. Gabriel Malata amesema Airtel Tanzania imetoa shilingi milioni 700 ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono juhudi za Serikali za kupambana na janga la Corona.

“Sisi bodi ya wakurugenzi wa Airtel na kwa niaba ya Airtel Tanzania, tunatambua juhudi za Serikali katika kupambana na ugonjwa wa Corona, lakini pia tumejitathimini na kutambua kuwa sisi kama Airtel hatuwezi kuendelea bila kuwepo watu wanaotumia huduma zetu. Watu hawa ndio mtaji wa Kampuni,” amesema Bw. Gabriel.

Mkurugenzi wa Uhusiano wa Kampuni ya Bia ya Serengenti, Bw. John Wanyancha amesema kuwa kampuni hiyo imetoa lita 1,250 ya vitakasa mikono nyenye thamani ya shilingi milioni 15 kwa ajili ya kuunga mkono juhudi za Serikali za kupambana na maambukiza ya virusi.

Mwenyekiti wa Rotary Club, Bi. Agnes Batenga amesema Rotary imetoa shilingi milioni 250 kwa ajili ya kupambana na ugonjwa wa homa ya mapafu (COVID-19).

“Shilingi milioni 183 zitatumika kutoa msaada wa vifaa vya kujikinga (PPE), vifaa vya maji safi ambavyo vitasambazwa katika vituo maalumu vya kuhudumia wagonjwa wa Corona jijini Dar es Salaam, Hospitali ya Amana, Zanzibar, Hospitali ya Mawenzi na Hospitali ya Mount Meru,” amesema Bi. Agnes.

Amesema shilingi milioni 67 zitatumika katika kutekeleza miradi ya kudhibiti ugonjwa wa Corona nchini kupitia Club za Rotary.


Share:

WAANDISHI WA HABARI WAANDIKE HABARI ZENYE MSAADA KWA JAMII KIPINDI HIKI CHA COVID - 19


Waandishi wa habari wakiendelea na majukumu yao


Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Vyombo vya Habari ni moja ya sehemu ambayo inatoa tarifa kwa wananchi na kujua hali ya nchi inavyoendelea katika kipindi husika.

Kazi ya Vyombo vya habari inalindwa na Katiba ya nchi ya mwaka 1977,ibara ya 18 kifungu a hadi d ambapo vinaeleza bila kuathiri sheria ya nchi,kila mtu yupo huru kuwa na maoni yoyote na kutoa nje mawazo yake na kutafuta ama kupokea na kutoa habari kupitia chombo chochote cha habari.

Pia ibara hiyo inaeleza kila raia anayo haki ya kupewa taarifa wakati wote kuhusu matukio mbalimbali yanayoendelea nchini na duniani ambayo ni muhimu kwa maisha na shughuli za wananchi.

Rose Reuben ni Mkurugenzi Mtendaji wa Chama Cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA),anaelezea umuhimu wa habari kwa wananchi kipindi hiki cha COVID-19.

Anasema wanahabari wanapaswa kuhakikisha wanaendelea kutoa taarifa kwa wingi zaidi na zenye kujibu maswali ya wananchi hususani katika kipindi hiki cha Mlipuko wa ugonjwa wa Covid-19(corona)

Anasema ni wajibu wa wanahabari kuhabarisha wananchi juu ya mwenendo wa ugonjwa huu kwa kutoa habari zilizo sahihi ambazo zitawatoa hofu wananchi na kuwaelimisha namna ya kujikinga na ugonjwa huo.

Anasema kwa kipindi hiki wanahabari wanapaswa kusaidia serikali katika kufikisha taarifa sahihi kwa wanajamii na kusaidia wanajamii kuchukua tahadhari.

"Ni nafasi ya wanahabari kuandika kutoa na kuandika habari za uhakika ambazo zinakuwa msaada katika jamii hususani katika kipindi hiki watu wanataka kujua umuhimu wa uvaaji wa barakoa wengine kujua namna ya kujinga wasiweze kupata maambukizi ya ugonjwa huu ni muhimu sana kutoa taarifa hizi,”anasema Rubern

Anasema Waandishi wa habari ni daraja kati ya Jamii na Serikali katika kujibu majibu yao hivyo ni jambo jema la kupokea taarifa zilizosahihi.

Kwa Upande wake Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), Kajubi Mkajanga anasema baraza limekuwa likisisitiza majukumu na uwajibikaji upo pande mbili kwa watoa habari ,Mamlaka husika na waandishi wa habari .

Anasema kwa kipindi hiki cha ugonjwa wa COVID-19 wamekuwa wakiwahimiza waandishi wa habari kuzingatia muongozo uliotolewa na Baraza hilo katika kufanya kazi kipindi hiki.

Kajubi anasema uhuru wa Kuandika habari nikuhakikisha waandishi wa habari wanaandika habari kwa usahihi kufata vigezo na misingi ,taaluma na Maadili ya uandishi wa habari katika kuwafikishia wananchi habari.

“Kwa upande wa watoa taarifa Watanzania wana haki ya kupata taarifa juu ya ugonjwa huu,taarifa zilizosahihi na kuzipata kwa haraka sio wakati wa kuonyeshana umashuhuru ni vema habari zikatolewa kwa uhakika na zisicheleweshwe,’’anasema.

Anasema wanaomba vyombo vya mamlaka kutokimbilia kutoa adhabu kwa vyombo vya habari kipindi hiki bali kiwe kipindi cha kuelimishana kutokana na kipindi hiki cha Covid-19 kuwa kipya.


Share:

DIAMOND AKABIDHI KWA SERIKALI HOTELI YAKE ITUMIKE KAMA HOSPITALI YA KUHUDUMIA WAGONJWA WA CORONA AU KAMA KARANTINI

Staa wa muziki nchini Nasibu Abdul maarufu kama Diamond Platnumz  ametoa ruhusa kwa serikali kuitumia hoteli yake mpya aliyoinunua kama hospitali ya kuhudumia wagonjwa wa corona au kama karantini.


Diamond amesema hayo leo ikiwa ni siku mbili baada kutangaza kuwalipia nyumba watu 500 ili kuondokana na adha ya kodi katika kipindi hiki cha maambukizi ya ugonjwa wa covid-19.

“Misukumo ya kusaidia watu, imetokana na malezi niliyolelewa, maisha niliyotokea na historia yangu ya nyuma. Nikikumbuka shida nilizopitia, napata moyo wa kusaidia wengine.

“Nimenunua hotel maeneo ya Mikocheni B, jijini Dar es Salaam ina vyumba zaidi ya 30, nimeshakabidhiwa documents zangu, ipo kwenye marekebisho kadhaa kisha nitaitambulisha. Kwa sababu sijaanza kui-upgrade, niko radhi niitoe kwa serikali kwa muda huu ili iweze kutumika kama Karantini au Hospital mpaka pale Corona itakapoisha,” amesema Diamond.

Aidha, Mondi amesema hajaweka kiwango cha mwisho cha kodi atakazowalipia wananchi, lakini lazima ataangalia wenye uhitaji haswa. Kwa sababu wapo wanaolipa pesa kubwa mpaka Tsh million 1 kwa mwezi, na mwengine Tsh 60,000 tu na inawashinda.

“Sitaangalia Dar es Salaam peke yake, ntajitahidi na kila mkoa nisaidie walau familia tano. Kwa sababu mikoani pia kuna watu wana shida sana. Sitaangalia jinsia moja zaidi, nitaweka usawa kwa wote. Kwa sababu suala la kodi linamgusa kila mtu, wanawake kwa wanaume.

“Ili kuweza kuwafikia walengwa halisi wanaotakiwa kufaidika na hizi kodi, tutatumia serikali za mitaa. Watu wapo wengi lakini lengo ni kuwafikia masikini, wajane, na wale wasio na uwezo. Baada ya hili la kodi kuisha, nitakuja na mpango wa kuwasaidia Ma-DJ wa ma-club na redio. Kwa sababu ni miongoni mwa kundi lilioathirika sana na kipindi hiki cha Corona,” amesema.


Share:

AFIKISHWA MAHAKAMANI KWA KUIBA PIKIPIKI YA BOSI WAKE MJINI KAHAMA

Na Salvatory Ntandu - Kahama

Mkazi wa mtaa wa Muhongolo Aron Salvatory Chubwa amefikishwa katika Mahakama ya wilaya ya Kahama kwa tuhuma ya wizi wa kuiba pikipiki ya mwajiri wake yenye thamani ya shilingi milioni tatu.


Mbele ya Hakimu mkazi wa Mahakama hiyo Christina Laurent Chovenye,Mwendesha Mashitaka wa Jeshi la Polisi Athumani Kisango alidai kuwa Salvatory alitenda kosa hilo Aprili 8 mwaka huu katika eneo la Cool breezy Mjini Kahama.

Alisema kuwa Mtuhumiwa katika shauri hilo la jinai namba 133 la mwaka huu alitenda kosa hilo la wizi wa kuaminiwa kinyume na kifungu mamba 258 (1)273(b) sura ya 16 ya kanuni ya adhabu marejeo ya mwaka 2019.

"Aron aliiba piki piki ya mwajiri wake Omary Musa yenye namba za usajili MC 747 CSC baada ya kuikabidhiwa kwa ajili ya kufanya kazi ya kusafirisha abiria katika maeneo mbalimbali mjini humo,"alisema Kisango.

Hata hivyo Aron amekana shitaka hilo na limeahirishwa hadi Mei 11 mwaka huu na amerudishwa rumande baada ya kushindwa kutimiza masharti ya dhamana.
Share:

DC MBONEKO AKABIDHI MATENKI YA MAJI YALIYOTOLEWA NA MGODI WA BARRICK BUZWAGI KUKABILIANA NA VIRUSI VYA CORONA SHINYANGA



Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko katikati, akimkabidhi Tenki la maji Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Mhe. Hoja Mahiba (kushoto) .Wa kwanza kulia ni katibu tawala wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Boniphace Chambi. Matenki hayo yametolewa na Kampuni ya Uchimbaji wa madini ya dhahabu ya Barrick kupitia mgodi wa Buzwagi uliopo wilayani Kahama ili kuendeleza mapambano ya kukabiliana na maambukizi ya virusi vya Corona. Picha zote na Marco Maduhu- Malunde 1 Blog.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko katikati, akimkabidhi Tenki la maji Kaimu mk urugenzi wa manispaa ya Shinyanga Mhe. Tito Kagize, wa kwanza kulia ni Katibu Tawala wa wilaya ya Shinyanga Boniphace Chambi.Matenki hayo yametolewa na Kampuni ya Uchimbaji wa madini ya dhahabu ya Barrick kupitia mgodi wa Buzwagi uliopo wilayani Kahama ili kuendeleza mapambano ya kukabiliana na maambukizi ya virusi vya Corona.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko katikati, akipiga picha ya pamoja mara baada ya kumaliza kukabidhi matenki ya maji katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga na manispaa, kulia ni mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Mhe. Hoja Mahiba, na kushoto ni Kaimu mkurugenzi wa manispaa ya Shinyanga Mhe. Tito Kagize.




Na Marco Maduhu- Malunde 1 Blog

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko amekabidhi matenki ya maji yaliyotolewa na Kampuni ya Uchimbaji wa madini ya dhahabu ya Barrick kupitia mgodi wa Buzwagi uliopo wilayani Kahama ili kuendeleza mapambano ya kukabiliana na maambukizi ya virusi vya Corona katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga na manispaa ya Shinyanga.


Zoezi la kukabidhi matenki hayo mawili ya maji limefanyika  kwenye Ofisi za mkuu wa wilaya ya Shinyanga leo Jumatatu Aprili 27, 2020.

Mboneko amesema Tenki moja la maji katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga litawekwa kwenye hospitali ya wilaya iliyopo Iselamagazi na kwa upande wa  manispaa ya Shinyanga tenki la maji  litawekwa kwenye Stendi kuu ya Mabasi maeneo ambayo yana msongamono mkubwa wa watu.

“Nakabidhi matenki haya ya maji ambayo yametolewa na wadau wetu wa Kampuni ya uchimbaji wa madini ya dhahabu Barrick kupitia mgodi wake wa Buzwagi, ambapo Tenki moja litakwenda halmashauri ya wilaya ya Shinyanga na jingine manispaa ya Shinyanga, lengo ni kuongeza mapambano ya kukabiliana na maambukizi ya virusi vya Corona,” amesema Mboneko.

“Naagiza pia Matenki haya ya maji yawekewe ulinzi wa kutosha na yasiharibiwe ili yadumu kwa muda mrefu kwa ajili ya kutoa huduma kwa wananchi kunawa mikono kwa sabuni na maj itiririka, ili wasipate maambukizi ya virusi vya Corona na kubaki kuwa salama”,ameongeza.

Pia ametoa shukrani kwa wadau wote mkoani Shinyanga kwa kuendelea kuunga juhudi za Serikali kupambana na virusi vya Corona, na kutoa wito kwa wadau wengine waendelee kujitokeza kutoa msaada, ikiwa bado kuna maeneo mengi yana uhitaji wa vifaa ili wajikinge na virusi hivyo na kubaki salama.

Kwa upande wao wakurugenzi hao akiwemo Mhe. Hoja Mahiba wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, na Kaimu mkurugenzi wa manispaa ya Shinyanga Mhe. Tito Kagize, wameahidi kuyalinda matenki hayo ya maji kwa kuweka ulinzi wa kutosha ili yasiharibiwe na kudumu muda mrefu.

Share:

Waziri wa Viwanda na Biashara Atangaza Ukomo Wa Bei Za Barakoa, Aelekeza Viwanda Vya Nguo Nchini Kutengeneza Barakoa

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Innocent Bashungwa amesema atachukua hatua kwa Taasisi zisizo za kiserikali (NGOs) zinazouza barakoa kwa gharama kubwa.

Bashungwa alitoa taadhari hiyo mkoani Arusha alipotembelea Viwanda vya kuzalisha nguo vya Sunflug na A to Z kuangalia hali ya uzalishaji wa barakoa katika Viwanda hivyo.

Bashungwa alitoa onyo kwa NGOs zilizoomba kibali cha kuzalisha barakoa kwa ajili ya kuwasaidia Watanzania lakini badala yake wanauza barakoa kwa shillingi 2,500 hadi 3,000

“Wamekuwa wakitoa masharti kupitia mitandao ya kijamii kuwa hawauzi barakoa chini ya bei hiyo”.

Sitawataja kwa leo lakini nikiona tu wanauza kwa bei kubwa sitasita kuwachukulia hatua, maana mnakuja kuomba vibali kumbe mnafanya mtaji.

Aliongeza kusisitiza barakoa zote ziuzwe kwa bei isiyozidi 1500 badala ya bei ya sasa ilikuwa sokoni ya 2500 ambayo watanzania wengi inawapa changamoto ya kumudu.

Kwa upande mwingine Mhe. Bashungwa alivipongeza Viwanda nguo vya A-Z na Sunflug kwa kuzalisha barakoa ambazo zinawasaidia watanzania walio wengi, na amewahaidi serikali kuwapati ushirikiano.

Aidha alivitaka Viwanda hivyo kuendelea kuzalisha kwa wingi ili wananchi walio wengi wa vijijini waweze kupata vifaa hivyo vya kujikinga na maambukizi ya ugonjwa wa korona.

Kwa upande wake mkuu wa Mkoa wa Arusha Bw. Mrisho Gambo aliwataka wananchi wote wa mkoa huo kuchukua taadhali zinazotolewa na Wizara ya afya wanapotembelea maeneo yenye mkusanyiko.

Pia, alisisitiza kuwa ni vema sasa wafanyabiashara hao wakatengeneza barakoa kwa bei nafuu ili kuwezesha wananchi kununua.

Wakitoa taarifa kwa Mhe. Waziri, Bw. Emmanuel Mgoma muakilishi wa kiwanda cha Sunflug alisema kiwanda kina uwezo wa kuzalisha barakoa 25,000 kwa siku.

Muakilishi wa A-Z Bw. Slyvester Kazi  alisema kiwanda kina uwezo wa kuzalisha barakoa 15,000 kwa siku.


Share:

WAFIKISHWA MAHAKAMANI KWA TUHUMA ZA KUKUTWA NA BANGI KAHAMA

SALVATORY NTANDU
Wakazi wawili wa Kijiji cha Mseki kata ya Bulungwa Joseph Maweda (24) na Fabian Petro (20) wamefikishwa katika Mahakama ya wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga wakituhumiwa kupatikana na dawa za kulevya aina ya bangi kilo nane.


Mbele ya Hakimu mkazi wa Mahakama hiyo Christina Laurent Chovenye Mwendesha Mashitaka wa Jeshi la Polisi Evodia Baimo alidai kuwa wawili hao walitenda kosa hilo Aprili 21 mwaka huu katika eneo la Mwabomba .

Amefafanua kuwa watuhumiwa hao walitenda kosa hilo kinyume na Vifungu 17(1)(b) na 2 namba 5 vya sheria ya kuzuia na kupamba na dawa za kulevya ya mwaka vya mwaka 2017.

Watuhumiwa hao wote kwa pamoja wamekana shitaka linalowakabili  namba 132 la mwaka huu na limeahirishwa hadi Mei 25 mwaka huu litakapoanza kusikiliwa baada ya upelelezi wake kukamilika

Washitakiwa wote kwapamoja wako nje  baada ya kukidhi Masharti ya dhamana ambapo walitakiwa kuwa na wadhamini wawili kila mmoja.



Share:

SERIKALI YASEMA UHAI WA BINADAMU UNA THAMANI KUBWA KULIKO UHAI WA WANYAMAPORI


Serikali imetolea ufafanuzi wa kauli iliyotolewa na  baadhi ya Wananchi  wanaodai kuwa Wizara ya Maliasili na Utalii imekuwa ikithamini uhai wa wanyamapori kuliko uhai wa Binadamu.



 Akizungumza na viongozi wa vijiji vitano vinavyopakana na Hifadhi ya Taifa ya Serengeti katika wilaya ya Serengeti mkoani Mara, Naibu Waziri Mhe.Constantine Kanyasu amesema  uhai wa binadamu una thamani kubwa na kamwe hauwezi kufananishwa na uhai  wa wanyamapori

Amesema licha ya  kuwa  Binadamu anaaminika kuwa akili kuliko Wanyamapori hata hivyo Wizara hiyo imekuwa ikifanya kila liwezekalo ili kuondoa migogoro kati ya Wanyamapori na binadamu.

" Tunaamini kila binadamu angetamani kuona yupo salama na ndio madhumuni na matamanio ya serikali" Amesisitiza Mhe.Kanyasu.

 Amesisitiza  kuwa  binadamu ana uwezo wa kukwepa mienendo ya wanyamapori na  kuwa katika mazingira salama kuliko mnyama mwenyewe na ameongeza kuwa  wanyamapori hao wapo kwa ajili ya Binadamu na sio vinginevyo.

Akitaja baadhi ya mikakati iliyochukuliwa na Serikali  ili kunusuru uhai wa binadamu ni pamoja na kuhamisha jumla ya Simba 36 kutoka Hifadhi ya Taifa ya Serengeti na kupelekwa katika Hifadhi nyingine lengo likiwa ni kupunguza madhara kwa binadamu wanaoishi karibu na Hifadhi hiyo.

Amesema jitihada hizo zilizochukuliwa na Serikali kufuatia Simba kula  ng'ombe wapatao  360 kwa kipindi cha mwezi Januari na Februari mwaka huu  huku  baadhi ya Wananchi kuuawa na wengine kujeruhiwa na wanyamapori wakali na waharibifu ni mkakati wa kuona maisha ya binadamu yanakuwa salama.

Licha ya jitihada hizo zilizofanywa na Serikali, Mhe.Kanyasu amewataka wananchi kuchukua tahadhari kwa kujiepusha kulima mazao  pamoja kujenga nyumba karibu na vigingi ili kuepuka athari za wanyamapori hao    kwa vile wanyamapori  wanakapokuja hawajui kuwa wamevuka mpaka.

 Amesema maamuzi hayo ni moja ya jitihada za Serikali kuhakikisha  uhai wa binadamu unalindwa kwa gharama yoyote ile.

Amesema licha ya kuwa moja ya jukumu la msingi la Wizara hiyo ni kulinda na kuendeleza Wanyamapori kwa ajili ya kizazi cha sasa na cha badae lakini hata hivyo thamani ya  Uhai wa binadamu ipo pale pale .


Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger