Monday, 27 April 2020

Wenye Virusi Vya Corona Nchini Kenya Wafika 363....Ni Baada ya Wengine 8 Kuongezeka

Waziri wa afya nchini Kenya Mutahi Kagwe ametangaza kwamba watu 8 zaidi wamethibitishwa kuambikizwa virusi vya corona. Idadi ya Walioambukizwa Virusi hivyo nchini humo sasa imefika 363

Wanne kati ya hao 8 wanatokea Mombasa huku waliosalia wakiwa ni wakazi wa Nairobi

Aidha, watu 8 pia wamethibitishwa kupona na kufikisha jumla ya idadi hiyo kufikia 114.

Wote walioambukizwa hawana historia ya kusafiri  nje ya nchi ikiwa ni sawa na kusema kwamba maambukizi hayo sasa ni ya ndani kwa ndani.


Share:

Mahakama Kuu Yatupilia Mbali Kesi ya Tundu Lissu Kupinga Kuvuliwa Ubunge

Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam kwa mara ya pili, imetupilia mbali maombi ya aliyekuwa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu ya kujaribu kupinga uamuzi wa kuvuliwa ubunge.

Maombi hayo yalitupwa mwishoni mwa wiki mbele ya Jaji Yose Joseph Mlyambina, baada ya kukubaliana na pingamizi la awali lililowasilishwa na jopo la mawakili kutoka ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali.

“Baada ya kusikiliza hoja za mapingamizi na majibu, mahakama inakubaliana na hoja za Serikali na inaona  maombi hayana msingi kisheria  kwa kuwa sheria hairuhusu rufaa kwa kesi inayofafana na hiyo,”alisema.

Katika maombi hayo namba 42 ya mwaka 2019 ya kutaka ridhaa ya Mahakama Kuu kumruhusu kukata rufaa yaliyofunguliwa Oktoba 10, 2019,Tundu Lissu alikusudia kupinga uamuzi wa yeye kuondolewa ubunge kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Kanuni za Kudumu za Bunge kutokana na kushindwa kuhudhuria vikao zaidi ya vitatu vya Bunge pasipo ruhusa ya maandishi ya Spika.

Maombi hayo yalipingwa vikali na mawakili wa Serikali kutoka Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali kwa madai hayakustahili kusikilizwa kwa kuwa yalikinzana na kifungu cha 5(2) cha Sheria ya Rufani kama ilivyorekebishwa na Sheria ya Marekebisho ya Sheria Na. 25 ya mwana 2002.

Upande wa Serikali, ulidai Lissu hakuwa na haki kisheria kupinga uamuzi wa Jaji Sirilius Matupa ulitolewa Septemba 9, mwaka jana wa kumnyima ridhaa kufungua shauri la mapitio ya kiutawala uamuzi ambao uliishia kwa yeye kupoteza  ubunge.

Ilielezwa na mawakili wa Serikali, uamuzi wa Jaji Matupa haukupaswa kupingwa kwa njia ya rufaa kwa  kuwa uamuzi huo haukumaliza shauri kama inavyopaswa kisheria.

Upande wa Serikali uliishawishi mahakama katika kesi mbalimbali, Mahakama iliamua kuwa rufaa haiwezi kukatwa kwa shauri ambalo limeisha katika hatua za awali kama ilivyokuwa kwa kesi ya Lissu ambaye alikuwa akiomba ridhaa ya kuwasilisha maombi ya mapitio na akanyimwa ridhaa kwa kuwa maombi yake hayakuzingatia Sheria.


Share:

Korea Kusini Yasema Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un Ni Mzima Wa Afya Njema !!

Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un yuko katika hali nzuri ya kiafya  kwa mujibu wa Moon Chung In, mmoja wa washauri wa usalama wa rais wa Korea Kusini Moon Jae-in.

Chung amesema kiongozi huyo wa Korea Kaskazini amekuwa katika mji wa Wonsana tangu april 13 na hajafanya ziara nyingi kama ilivyo ada yake, na kuwa yuko salama kinyume na uvumi kuwa amefariki.

Wakati huo picha za satelaiti zimeonyesha treni inayodhaniwa kuwa ni ya kiongozi huyo ikiwa imeegeshwa kwenye makazi yake yaliyoko pwani ya mashariki mwa nchi hiyo tangu wiki iliyopita.

Picha hizo za satelaiti zilizochapishwa na tovuti ya 38 North ambayo ni maalumu kwa masomo kuhusu Korea Kaskazini, hata hivyo hazielezi chochote kuhusu matatizo ya kiafya ya Kim Jon-un, lakini zinaendeleza taarifa za kiintelijensia za Korea Kusini kwamba Kim yuko nje ya mji mkuu, Pyongyang.

Uvumi kuhusu hali yake ya kiafya, kwa sehemu kubwa umesababishwa na kutoonekana kwake hadharani kwa kipindi kirefu.

Credit:RFI


Share:

Mgodi wa kuchimba dhahabu wa Geita (GGM) Kuanza Kutumia Umeme Wa Gridi Ya Taifa Mwezi Juni Mwaka Huu

Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani amesema kuanzia Mwezi Juni mwaka huu, Mgodi wa kuchimba dhahabu wa Geita (GGM) utaanza kutumia umeme wa Gridi ya Taifa kuendesha shughuli zake baada ya Kituo cha kupoza na kusambaza umeme cha Mponvu mkoani Geita kukamilika mwishoni mwa Mwezi Mei, 2020.

Aidha alisema ameridhishwa na kasi ya ujenzi wa kituo hicho ambacho awali kilipangwa kukamilika mwezi Juni lakini kutokana na kasi ya ujenzi wake kitakamilika mwishoni mwa Mwezi Mei na kuanza kusambaza umeme kwa wateja ikiwemo GGM.

Dkt. Kalemani alisema hayo, alipofanya ziara ya kikazi Aprili 25, 2020, mkoani Geita ya kukagua ujenzi wa kituo cha kupoza na kusambaza umeme cha Mponvu, Kituo cha kuchenjua dhahabu cha Geita na kuwasha umeme katika Kijiji cha Buyagu na Zahanati ya Musasa.

“Kituo hiki cha Mponvu kitakuwa mkombozi mkubwa wa nishati ya umeme ya kutosha na kwa gharama nafuu kwa wakzi wa Mkoa wa Geita na mikoa jirani,pia Mgodi wa GGM utajiendesha kwa faida zaidi na kuliongezea mapato taifa kwa sababu wataacha kutumia majenereta kuzalisha umeme ambao ni wa gharama kubwa sana ukilinganisha na umeme unaozalishwa hapa nchini” alisema Dkt. Kalemani.

Dkt. Kalemani alifafanua kuwa, mgodi wa GGM utatumia umeme wa gridi ya taifa kutoka kituo cha Mponvu ambacho kitapokea umeme wa njia ya kusafirisha umeme wa Kilovolti 220 kutoka kituo cha Bulyanhulu mkoani Shinyanga hadi mkoani Geita yenye urefu wa kilomita 55.

Vilevile alieleza kuwa tayari njia ya kusafirisha umeme wa Kilovolti 33 utakaotumiwa na mgodi huo yenye urefu wa Kilomita 6.5 kutoka katika kituo hicho hadi ndani ya mgodi huo imekamilika na kinachosubiriwa sasa ni kuunganisha umeme punde kituo hicho kitakapokamilika.

Dkt. Kalemani pia aliwasha umeme katika Kijiji cha Buyagu,ambacho ni moja ya vijiji vinavyopitiwa na njia ya kusafirisha umeme wa Kilovolti 220 kutoka Bulyanhulu hadi Geita ikiwa ni ishara ya kukamilika kwa njia hiyo kwa asilimia 80.

Katika kukagua maendeleo ya usambazaji umeme vijijini, aliwasha umeme katika zahanati ya Musasa na kuwataka wananchi wa eneo hilo kuendelea kulipia ili waunganishiwe umeme.

Hata hivyo aliliagiza Shirika la Umeme Nchini, ( TANESCO) kuharakisha ufungaji wa Mashineumba( Transfoma) katika kituo cha kuchenjua dhahabu mkoani Geita ambacho kiko katika hatua za mwisho kukamilika.

Dkt. Kalemani alirejea kusema kuwa lengo la serikali ni kuhakikisha kuwa wachimbaji wote nchini wanaendesha shughuli za uchimbaji kwa kutumia nishati ya umeme unaozalishwa nchini kwa gharama nafuu.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Geita, Robert Gabriel alisema kuwa kituo hicho kikikamilika kitakuwa uwezo wa kuchenjua dhahabu inayotakiwa katika ubora wa kimataifa na kitawasaidia wachimbaji wadogo kunufaika zaidi na shughuli zao za uchimbaji tofauti na ilivyo sasa.

Gabriel aliwaomba wawekezaji kwenda kuwekeza zaidi katika mkoa huo wa Geita kwa kuwa kuna umeme mwingi wa kutosha na gharama nafuu kuendesha shughuli mbalimbali vikiwemo viwanda.

Vilevile aliishukuru Wizara ya Nishati kwa kuhakikisha kuwa mkoa huo unakuwa na umeme wa kutosha ili kuvutia wawekezaji wengi, kuwaunganishia umeme wa bei nafuu wananchi wa mkoa huo pamoja na kujengwa kwa kituo cha kupoza na kusambaza umeme cha Mponvu ambacho kitawezesha migodi yote katika mkoa huo kutumia umeme, na kuugawa katika mikoa jirani. 


Share:

Wenye Virusi Vya Corona Nchini Uganda Wafika 79....Ni Baada ya Madereva 04 Toka Tanzania Kuongezeka

Wizara ya Afya nchini Uganda imetangaza ongezeko la visa vipya 4 vya maambukizi ya COVID-19 baada ya kufanya vipimo vya sampuli 1578

Wote ni Watanzania ambao ni madereva wa malori walioingia kupitia mpaka wa Mutukula.

 Idadi ya wagonjwa wa COVID-19 nchini humo sasa ni 79.


Share:

JITIBU TATIZO LA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME KWA KUTUMIA FULL POWER.. UUME MDOGO ZAT 50 NDIYO SULUHISHO


Zati 50
Full Power

Sababu za upungufu wa nguvu za kiume na maumbile madogo ya uume:

⇒Ngiri,

⇒Henia

⇒Kisukari

⇒Tumbo kujaa gesi

⇒Kutopata choo vizuri

⇒Utumiaji madawa kwa muda mrefu

⇒Unywaji wa pombe kupita kiasi

⇒Msongo wa mawazo 

⇮⇒Haya yote hupelekea mwili kutokuzalisha homoni ya gesrtogine au kuwa chache na kushindwa kupata mzunguko mzuri wa damu na vichocheo vingine kama madini ya zinki ambayo hukufanya kuwa na msisimko  na kufanya kuwa na muda  mrefu na nguvu za kutosha.

ZAT 50

⇨ Inarutubisha maumbile ya uume  na kunenepesha urefu nchi 6,unene sentimita 4

⇨Dawa hii ni ya kutibu kabisa tatizo hilo.

FULL POWER

⇨Ni dawa ya vidonge ya miti shamba inaongeza nguvu za kiume na kutibu kabisa tatizo hilo.

⇨Inaongeza hamu ya tendo la ndoa
⇨Inakufanya uchelewe kufika kileleni zaidi ya Dakika 30 na kurudia tendo zaidi ya mara nne na zaidi.

Pia tunatibu Magonjwa mengine Kama

Matatizo ya pumu,Bawasiri, vidonga vya tumbo,Kisukari,Magonjwa sugu ya zinaaa,Kaswende,U.T.I , kiuno,miguu kuwaka moto, Fangasi sehemu za Siri, kupunguza unene wa mwili,tumbo kuunguruma,kujaa gesi, matatizo ya uzazi kwa wanawake, kurutubisha mbegu za uzazi kwa akina baba, matatizo ya meno tunatibu bila kungoa

Kliniki yetu inapatikana Zanzibar, Dar es salaam na Shinyanga.

Wasiliana nasi kwa simu namba 071770 22 27
Share:

Tanzia: Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Evord Mmanda afariki Dunia




Share:

WAZIRI BITEKO AZINDUA VIWANDA VIWILI VYA MFANO VYA UCHENJUAJI WA DHAHABU



WAZIRI wa Madini Doto Biteko katikati akijiandaa kukata utepe hafla ya uzinduzi wa viwanda hivyo vya Mfano





Waziri wa Madini, Doto Biteko akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili kilipojegwa kiwanda cha kuchenjua dhahabu bila kutumia kemikali ya zebaki cha Katente wakati wa uzinduzi wa kiwanda hicho uliofanyika tarehe 26 Aprili, 2020



Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Prof. Simon Msanjila akiongea jambo wakati wa hafla ya uzinduzi wa viwanda vya kuchenjua dhahabu vya Katente na Lwamgasa uliofanyika Katente mkoani Geita tarehe 26 Aprili 2020


Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idrisa Kikula akizungumza jambo wakati wa hafla ya uzinduzi wa kiwanda cha kuchenjua dhahabu cha Katente wilayani Bukombe mkoani Geita tarehe 26 Aprili, 2020



Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Mipango wa Wizara ya Madini, Augustine Ollal (mwenye mic) akimkaribisha Waziri wa Madini, Doto Biteko (katikati)tayari  kwa ajili ya kukata utepe ili kuelekea katika hatua ya kukagua kiwanda cha kuchenjua dhahabu  cha Katente Mkoani Geita wakati wa hafla ya uzinduzi wa kiwanda hicho tarehe 26 Aprili, 2020.





Viongozi wa Serikali kuanzia kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Geita, Robert Gabriel akifuatiwa na Waziri wa Madini, Doto Biteko, Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Profesa Simon Msanjila na mwisho ni Mshauri mwelekezi aliyesimamia ujenzi wa viwanda vya kuchenjua dhahabu Rogers Sezigwa wakiendelea na ukaguzi wa kiwanda hicho kabla ya kukikabidhi rasmi kwa Shirika la Madini la Taifa (Stamico)



Mshauri Mwelekezi, Rogers Sezigwa wa kampuni ya Tan Discovery Mineral Consultancy Limited akieleza namna maji yenye sumu ya kemikali ya sayonide inavyotuzwa pasipo kusababisha madhara kwa jamii inayozunguka kiwanda hicho kilichopo Katente Wilayani Bukombe mkoani wa Geita



Waziri wa Madini, Doto Biteko (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa wa Geita mara baada ya hafla ya uzinduzi na makabidhiano ya kiwanda cha kuchenjua dhahabu cha Katente na Lwamgasa Mkoani Geita. Kiwanda hicho kimekabidhiwa kwa Shirika la Madini la Taifa (Stamico) ili kukisimamia na kukiendesha.

Stamico wakabidhiwa rasmi



Waziri wa Madini, Doto Biteko amelitaka Shirika la Madini la Taifa (Stamico) kusimamia ipasavyo Viwanda vya Mfano vya Uchenjuaji wa madini ya dhahabu vya Katente-Bukombe na Lwamgasa-Geita alivyovizindua leo APRIL 26 na kuvikabidhi rasmi kwa shirika la Stamico..

Ujenzi wa viwanda hivyo visivyotumia kemikali hatari ya zebaki ulifanywa na kampuni ya Tan Discovery MineralConsaltancy Limited inayosimamiwa na Rogers Sezigwa iliyoanza ujenzi wa mradi mwezi Disemba, 2016 ikianziaLwamgasanakufuatianaKatentenaItungi- Chunya.

Akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa viwanda hivyo vya Mfano,Waziri Biteko amesema, itakuwa aibu kubwa kwa Stamico endapo Viwanda hivyo vitafia mikononi mwao kwani Serikali imetumia gharama kubwa katika ujenzi wa viwanda hivyo.

“Afe Kipa, afe beki ni lazima viwanda hivi vifanye kazi” Biteko alisisitiza.

Aidha,Waziri Biteko amewahakikishia wananchi na wachimbaji wadogo wa madini nchini kuwa, serikali ya Rais John Magufuli inawajali na itawahudumia kwa gharama nafuu hivyo wasisite kupeleka mawe kiwandani hapo ili waweze kuchenjuliwa dhahabu kwa kutumia teknolojia mpya na ya kisasa na hivyo kuepuka kutumia zebaki na kuachana na utumiaji wa matimba kwenye mashapo.

Amesema matumizi ya matimba wakati wa uchimbaji yanasababisha uharibifu wa mazingira wakati zebaki huathiri afya za wachimbaji hivyo waitikie na kuvitumia viwanda hivyo kwa faida zao.

“Tumetengeneza viwanda hivi kuwavutia ninyi fanyebiashara” Biteko alisisitiza.

Pamoja na hayo, Waziri Biteko alimtaka Mwenyekiti wa Bodi ya Stamico kuhakikisha wanasimamia ipasavyo miradi hii pasipo kucheka na watu wasiotimiza wajibu wao kwenye viwanda hivyo.

Sambamba na hayo amewataka Bodi pamoja na Stamico kuhakikisha wananchi wanaozunguka viwanda hivyo wananufaika na uwepo wa viwanda katika maeneo yao kwa kupata ajira ndogo ndogo kwa kufanya hivyo kutainua uchumi wao.

Akizungumzia faida zitokanazo na uwepo wa viwanda hivyo vya mfano, Waziri Biteko alisema ni pamoja na utoaji wa mafunzo na maarifa kuhusu sheria, kanuni, taratibu na miongozo mbalimbali kwa wachimbaji wadogo, kutolewa elimu ya mfumo wa kuthamini mashapo ya madini yaliyopo ilikufanya uchimbaji wenye tija, kuchenjua dhahabu pamoja na kukodishwa vifaa vinavyotumika katika shughuli za uchimbaji kwa gharama nafuu pamoja na kutolewa elimu juu ya uongezaji thamani madini na upatikanaji wa masoko.

Akizungumzia mchakato wa ujenzi wa viwanda hivi vya mfano, Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Mipango, Augustine Ollal amesema, ujenzi huo nimatokeo ya Utekelezaji wa Sera ya Madini ya mwaka 2009 iliyosisitiza zaidi juu ya uendelezaji wa sekta ya madini hususani wachimbaji wadogo.

Amesema katika kutimiza azma hiyo, Serikali ilianzisha mradi wa Usimamizi Endelevu wa Rasilimali Madini (SMMRP) uliokuwa na awamu mbili, ya kwanza ni kuanzia 2009 hadi 2014 na awamu ya pili mwaka 2015 hadi 2018 ambapo awamuya pili ya mradi ndipo viwanda vitatu vya mfano vya uchenjuaji wa dhahabu vya Katente- Bukombe, Lwamgasa- Geita na Itumbi –Chunya vilipoanza kujengwa baada ya kufanyika kwa utafiti wa kijiolojia chini ya ushirikiano baina ya uongozi wa mradi, Stamico, Taasisi ya Utafiti na Jiolojia Tanzania (GST) na wachimbaji wadogo.

Akizungumzia gharama ya ujenzi wa viwanda hivyo Ollal alisema mradi wa Katente umegharimu kiasi cha shilingi bilioni 1.7 na Lwamgasa umegharimu kiasi cha shilingi bilioni 1.3 wakati mradi wa Itumba Uligharimu kiasi cha shilingi bilioni 1.7 na hivyo kufanya miradi yote kutekelezwa kwa kiasi cha shilingi bilioni 4.7.

Ollal ameongeza kuwa, uwepo wa tekinolojia hii kwa wachimbaji wadogo itakuwa na manufaa kama vile; kupunguza kwa kiasi kikubwa ajali migodini kwa kutumia sementi katika kuimarisha kuta, kurahisisha utoaji wa mbale mgodini(Haulage system) kupunguza athari za kimazingira kwa kutokata miti hovyo na kurahisisha ufungaji wa migodi.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara y aMadini, Prof. Simon Msanjila amelitaka Shirika la Madini la Taifa (Stamico) kuisaidia jamii inayozunguka viwanda hivyo vya mfano kuondokana na changamoto ya maji kwa kuchimba kisima kiwandani hapo na kuiruhusu jamii kunufaika na huduma hiyo.

Aidha, Prof. Msanjila amewataka Stamico kutoa nafasi za ajira kwa wananchi kutokana na ukweli kwamba wao ndio walinzi wa viwanda hivyo. “Nitashangaa sana kuona wafanyakazi wakawaida wanatoka km 200 kutoka hapa wakati kijiji kimezungukwa na vijana mahiri na wachapa kazi” alisistiza Prof. Msanjila.

Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Geita, Robert Gabriel ametoa wito kwa watendaji na wasimamizi wa vituo hivyo kuwa wazalendo katika usimamizi wa Viwanda hivyo vya uchenjuaji wa dhahabu.

Sanjari na hilo, ameelezea mikakati ya mkoa wake kuelekea maonesho ya Tekinolojia ya uchimbaji wa madini kwa mwaka huu kuwa ni pamoja na mkoa wake kuandaa uwanja maalum kwa ajili ya maonesho hayo ambapo tayari ujenzi wa jengo la ofisi mbalimbali ikiwepo ya wataalamu wa Sekta ya madini umefanyika.

Mkuu wa Mkoa ametoa wito kwa wataalamu na timu nzima ya Ujenzi wa viwanda hivi kushiriki kikamilifu katika maonesho hayo ili kuachilia utaalamu wao kwa watanzania wengine wenye nia ya kujiendeleza kupitia sekta ya Madini.

Share:

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatatu April 27




















Share:

Sunday, 26 April 2020

CHAMA CHA WALIMU IRAMBA MKOANI SINGIDA CHAPATA VIONGOZI WAPYA


Viongozi wapya wa Chama cha Walimu nchini (CWT) Wilaya ya Iramba wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kuchaguliwa kupitia mkutano mkuu uliofanyika jana.


Na Godwin Myovela, Singida

WAJUMBE wa Chama cha Walimu nchini (CWT) Wilaya ya Iramba, mkoani hapa kupitia mkutano mkuu wamefanya mabadiliko ya safu ya juu ya uongozi wake kwa kumchagua Anania Mbuta kuwa mwenyekiti mpya wa chama hicho, huku aliyekuwa akishikilia nafasi hiyo Hamis Kumara kujikuta akipata kura pungufu.

Pia kupitia mkutano huo wa uchaguzi, wajumbe waliamua kumwondoa madarakani aliyekuwa mwekahazina wa muda mrefu wa chama hicho William Gunda, na nafasi yake kuchukuliwa na Sebastian Gunda-huku nafasi ya Mwenyekiti wa Kitengo cha Walimu Wanawake (KE) akikakabidhiwa Dorcus Mungulu.

Katika uchaguzi huo wa kikatiba uliofanyika jana kwenye ukumbi wa halmashauri wilayani hapa, na kusimamiwa na Mwenyekiti wa CWT Mkoa wa Singida, Aran Jumbe, jumla ya wajumbe takribani 120 ambao wanawakilisha zaidi ya walimu 1200 walishiriki na kuwa sehemu ya mabadiliko hayo.

“Nawashukuru wajumbe kwa kuniamini na kunikabidhi jukumu hili la kuhakikisha haki na maslahi ya walimu vinazingatiwa kwa vitendo na kwa wakati, timu yote ya uongozi mliyonipa iko vizuri, nawahakikishia tutachapa kazi sintawaangusha,” alisema Mwenyekiti mpya Mbuta.

Aidha, wajumbe wengine waliochaguliwa kupitia mkutano huo uliokuwa na mvutano mkali baina ya wagombea ni pamoja na Grace Shirima ambaye ameshinda kwa nafasi ya mwekahazina Kitengo cha Wanawake, huku Damiano Awali akiaminiwa kushika nafasi ya uwakilishi wa Taasisi na Uongozi.

Hata hivyo, nafasi ya uwakilishi nafasi ya chuo alipewa Thomas Sekenga, na uwakilishi wa wenye Ulemavu ukienda kwa Emanuel Suwi, huku Vijana nao wakimpata mwakilishi wao Griflin Kaleshu. Ushindi wa nafasi ya uwakilishi wa cwt kwa walimu wanawake wilayani hapa hatimaye umekwenda kwa Veleriana Masangya.

Walimu wanne ambao ni Clemensi Pegia, Makilagi Makalanga, Godfrey Athuman na Elia Sumbi wamechaguliwa kuwakilisha walimu wa Shule za Msingi, huku walimu wawili Seaclif Msagaha na mwenzake Magreth Gregory wao watawakilisha walimu wa shule za sekondari .
Share:

ALIYEDAI KAPITIWA NA SHETANI WA MAPENZI AKABAKA MTOTO WA MIAKA 8 ATUPWA JELA MAISHA


Mkazi wa Kata ya Wailes, Halmashauri ya Manispaa ya Lindi, Selemani Hassani (29) amehukumiwa kifungo cha maisha gerezani,baada ya kupatikana na hatia ya kumbaka mtoto wa miaka 8.

Hukumu hiyo imetolewa na Hakimu mkazi mwandamizi wa Mahakama ya Wilaya ya Lindi, Maria Batraine, baada ya kuridhishwa na ushahidi uliotolewa na upande wa Mashitaka. 

Kabla ya kutolewa kwa hukumu hiyo, Hakimu Batraine alimuuliza mshitakiwa iwapo ana sababu za msingi itakayoiwezesha Mahakama isimpe adhabu kali kutokana na kosa linalomkabiri mbele yake,ambapo aliomba aonewe huruma kwani ni mkosaji wa mara ya kwanza na pia anayofamilia inayomtegemea. 

"Naiomba Mahakama yako tukufu naomba inionne huruma kwani shetani wa mapenzi alinipitia na sasa najutia kosa langu" amedai Selemani.

Hakimu Betraine akitoa hukumu katika kesi hiyo namba 08/2020, amesema amesikia maombi ya pande zote mbili,lakini kutokana na kubanwa na Sheria kupitia vifungu 130 kifungu kidogo cha kwanza fungu la pili kipengele (e) pamoja na 131 fungu dogo la (1) na (3) alimuhukumu kutumikia kifungo cha maisha Gerezani.
Share:

Wenye Virusi vya Corona Nchini Kenya Wafika 355....Ni Baada ya Wengine 12 Kuongezeka

Watu wengine 12 wamepatikana na virusi vya corona nchini  Kenya ndani ya masaa 24 yaliyopita.

Sasa idadi ya watu walioambukizwa virusi hivyo nchini Kenya imefikia 355 tangu kisa cha kwanza kiripotiwe Machi 13 mwaka huu. 

Taarifa hiyo imetolewa leo Jumapili, Aprili 26, na katibu msimamizi katika Wizara ya Afya Rashid Aman. 

Aman amesema  kuwa hakuna kifo zaidi kimeripotiwa kutokana na virusi hivyo na idadi ya waliofariki imesalia watu 14.

Watu 8 wamepona virusi hivyo na kufikisha idadi ya waliopona kuwa 106


Share:

Waziri mkuu wa Uingereza kurejea ofisini kesho baada ya kupona Corona

Waziri mkuu wa Uingereza Boris Johnson atarejea ofisini kesho Jumatatu baada ya kupona maambukizi ya virusi vya corona.Msemaji wa serikali amelithibitishia shirika la habari la DPA.

Johnson alikuwa katika makazi yake yaliyoko nje ya London baada ya kuruhusiwa kutoka hospitali ya Mtakatifu Thomas Aprili 12 alikolazwa kwa wiki nzima akitibiwa COVID-19. 

Kulingana na shirika la habari la Uingereza la Press Association, siku ya Ijumaa Johnson alikutana na mawaziri waandamizi wa baraza lake kwa masaa matatu ikiwa ni pamoja na waziri wa mambo ya kigeni Dominic Raab aliyekaimu nafasi yake wakati akiwa mgonjwa.

Hata hivyo Johsnon anarejea katika wakati ambapo shinikizo linaongezeka dhidi ya serikali la miito ya kulegezwa vizuizi vya mapambano dhidi ya janga la corona. 

-DW


Share:

Tuendelee Kuchukua Tahadhari Dhidi Ya Corona- ASP Swebe

Na WAMJW- DSM
Mrakibu mwandamizi wa polisi kanda maalum ya Dar es Salaam ASP Swebe ametoa wito kwa wananchi, hususan Wana Dar es Salaam kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya maambukizi ya homa kali ya mapafu inayosababishwa na virusi vya Corona.

Ameyasema hayo wakati akiwa katika majukumu yake ya ukaguzi wa namna gani kituo cha Polisi Pangani kilichopo Ilala Jijini Dar es Salaam kimechukua hatua ya kukabiliana dhidi ya maambukizi ya virusi vya Corona.

“Tunaendelea kukumbusha Wananchi wa hususan Wanaotoka Jijini Dar es Salaam kunawa mikono na kuchukua hatua zote za tahadhari zinazotakiwa, tunaendelea kusisitiza kila mmoja katika familia yake aendelee kuchukua hatua ambazo Wizara ya Afya inapendekeza” alisema

Kwa upande mwingine, ASP Swebe ameishukuru Serikali kupitia Wizara ya Afya kwa kuja na kampeni ya “Mikono safi, Tanzania salama” inayohamasisha wananchi kuchukua tahadhari dhidi ya maambukizi ya virusi vya Corona, hali inayoonesha jinsi gani Serikali imewekeza kwenye Afya ya wananchi.

“Kwanza nitoe shukrani kwa Serikali kupitia Wizara ya Afya, kwa Kampeni inayoendelea ya “Mikono safi, Tanzania salama”, hii inaonesha ni jinsi gani Serikali imewekeza kwenye Afya ya wananchi” alisema.

Aidha, ameishukuru Wizara ya Afya kwa kuendelea kulisaidia Jeshi la polisi vifaa vya kujikinga dhidi ya maambukizi ya homa kali ya mapafu inayosababishwa na virusi vya Corona ikiwemo vitakasa mikono na Barakoa (mask).

Kwa upande wake, Sfaff sergeant (S/Sgt ) Valentine Ngowi, amewataka madereva wote wa vyombo vya moto hususan bodaboda na bajaj kuhakikisha wanavitakasa vyombo vyao vya usafiri kwa sabuni mara kwa mara ili kuua maambukizi ya virusi vya Corona endapo vitakuwepo.

Uhamasishaji huu unafanywa kupitia kampeni hii ya “Mikono safi, Tanzania salama” inaratibiwa na Wizara ya Afya, kwa kushirikiana na Shirika lisilo la kiserikali la Project CLEAR kwa kushirikiana na Msanii Mrisho Mpoto (Mjomba) kutoka Mjomba Theatre Gallery unaendelea katika Jiji la Dar es Salaam.


Share:

Mbaroni Kwa Kurekodi Na Kusambaza Video Zamtoto Akinywa Bia Baa Kwenye Mitandao Ya Kijamii Shinyanga

SALVATORY NTANDU
Jeshi la Polisi mkoa wa Shinyanga linawashikilia Watu watatu kwa tuhuma za kufanya ukatili dhidi ya Mtoto wa kike mwenye umri wa miaka  (3)na Matumizi mabaya ya Mtandao kwa kumnyesha pombe na kisha kurekodi video na kuirusha kwenye mitandao ya kijamii.

Kwa Mujibu wa Taarifa iliyotolewa leo Aprili 26 kwa Vyombo vya Habari na Kamanda wa Polisi mkoani humo, ACP Debora Magiligimba imesema kuwa limetokea lilitokea Aprili 24 katika baa itwayo Bondeni huko Mwakitolyo  ambapo watuhumiwa hao walinywesha bia  aina ya Balimi na kurekodi video hiyo kisha kuirusha katika mtandao wa Whatsapp.

Kamanda Magiligimba aliwataja   watu  hao waliohusika na tukio hilo kuwa ni pamoja na   Godius  Novat  katisha (32) baba mzazi wa Mtoto huyu,Irene Alphonce Pima mmiliki wa baa hiyo wote wakazi wa mwakitolyo na Oscar Daniel Makondo (35) mfanyabiashara na mkazi wa Mtaa wa Mayila mjini kahama.

“Baada ya tukio hilo kuripotiwa kikosi Kazi cha askari wa Uhalifu wa Makosa ya Kimtandao kilianza kazi rasmi ya kuwatafuta watuhumiwa hao ambao walifanikiwa kuwakamata Aprili 25 mwaka huu katika Kijiji cha Nyaligongo, Kata ya Mwakitolyo, Wilayani Shinyanga,” alisema Magiligimba.

Ameongeza kuwa baada ya Upelelezi kukamilika Wote kwa Pamoja watafikishwa Mahakamani kujibu Mashitaka yanaowakabili.

Sambamba na hilo Kamanda Magiligimba  alitoa  wito kwa wananchi kuheshimu haki za watoto na kutoa onyo kali kwa  atakayebainika kwenda kinyume hatua kali zitachukiliwa dhidi yake.

Mwisho.


Share:

Masoko Yadhahabu Kahama Yaingiza Shilingi Bilioni61.5

SALVATORY NTANDU
Baada  ya  Serikali  kujenga  Masoko ya Madini katika mkoa wa Madini Kahama ili kudhibiti biashara holela na utoroshwaji  wa  dhahabu imesaidia kuongeza  Mapato ambapo kwa  kipindi cha Julai 20 2019 hadi Aprili 2020  jumla  ya  shilingi  bilioni 61.5  sawa  na  asilimia 77.62 zilikusanywa.

Hayo yalibainishwa Aprili 25 Mwaka huu na Afisa Madini wa Mkoa wa Shinyanga, Mhandisi Joseph Kumburu baada ya kuzungumza  na Mwandishi wa habari  kuhusiana na hali ya  ukusanyaji wa Maduhuli ya serikali baada ya kuboreshwa kwa  masoko ya Madini mkoni humo.

Alisema, fedha hizo zimetokana na Malipo ya Maduhuli ya  mirahaba pamoja na  ada za ukaguzi wa Makinikia katika migodi midogo na mikubwa ambazo zinakusanywa kwenye Masoko na miyalo ya Uchejuaji wa madini.

“Hapo awali wachimbaji na Wafanyabiashara ya Madini walikuwa wakiibia serikali kwa kuuza madini kwa njia za panya na kusababisha serikali kokosa mapato,lakini kwasasa baada ya kujenga masoko katika maeneo ya Kahama,Kakola Mwime,Mwazimba na Mwabomba yamesaidia kuongeza ,mapato kwa asilimia 77.62,” alisema Kumburu.

Kumburu alifafanua kuwa kwa sasa wafanyabiashara na wachimbaji wa Madini wameelewa faida za kuuza kwenye masoko kwani wanaweza kuuza kwa bei ya juu ikilinganishwa na hapo awali ambapo walikuwa wakitapeliwa na madalali kwa kuuza mali zao kwa bei ya chini.

“Sheria kali zinaendelea kuchukuliwa kwa wachimbaji ama wafanyabiashara wa madini ambao wanafanya biashara hii nje ya masoko,nitoe rai kwao kwani ukikamatwa madini yako yatataifishwa na wewe kuchukuliwa hatua kali za kisheria ni vyema mkauza ndani ya masoko yaliyotengwa na serikali,”alisema Kumburu.

Sambamba na hilo Mhandisi kumburu aliwataka wachimbaji wadogo wa madini kuhakikisha wanaosha mawe yenye madini katika mialo ambayo inatambulika kisheria kwa kuwa na fomu za kujaza kiwango cha dhahabu ili kuepuka usumbufu pindi ukaguzi unapofanyika.

Mwandu Makoye ni mmoja wa Wafanyabiashara wa Madini mkoani humo ameipongeza serikali ya awamu ya Tano chini Rais Dk John Pombe Magufuli kwa  kuanzisha masoko hayo na kusema kuwa kwa sasa wanapata faida kuwa ikilinganishwa na hapo awali ambapo biashara hiyo ilikuwa imeingiliwa na matapeli.

“Sisi kama wafanyabiashara Tunampongeza Rais wetu Magufuli kwa kutambua mchango wa sekta ya Madini,tunaahidi kufanyabiashar hii kwa uaminifu mkubwa na tupo tayari kuwafichua wenzetu ambao wamezoea Magendo katika sekta hii ya Madini.

Kabla ya kuanza kwa masoko hayo katika mkoa wa Kimadini Kahama Serikali ilikuwa inakusanya shilingi milioni 593,689,214.67 za mrahaba huku ada za ukaguzi wa Madini zikiwa ni shilingi milioni 8,481,274,495.27 kwa mwaka.

Mwisho.



Share:

WALIOPELEKA MTOTO BAA KUMNYWESHA POMBE KISHA KUMREKODI VIDEO NA KUSAMBAZA MITANDAONI WAKAMATWA SHINYANGA


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba 


Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga linawashikilia watu watatu kwa kosa la kumpeleka Baa mtoto  wa kike mwenye umri wa miaka mitatu na kumnywesha pombe aina ya Balimi huku wakimrekodi video kisha kusambaza kwenye mitandao ya Kijamii yakiwemo magroup ya Whatsapp.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba amesema tukio hilo limetokea Aprili 24,2020 majira ya saa sita mchana kwenye baa iitwayo Bondeni iliyopo katika Kijiji cha Nyaligongo, Kata ya Mwakitolyo, Wilayani Shinyanga. 

“Tunawashikilia watu watatu ambao ni Godius Novat Katisha (32),mkazi wa Mwakitolyo ambaye ni baba wa mtoto huyo, mmiliki wa bondeni bar aitwaye Irene Alphonce Pima (32), mkazi wa Namba 02 Mwakitolyo na Oscar Daniel Makondo (35) mkazi wa mtaa wa Mayila Kahama kwa Makosa ya Ukatili dhidi ya Mtoto na Matumizi Mabaya ya Mitandao”,amesema Kamanda Magiligimba. 

“Siku ya tukio Mtoto wa kike, mwenye umri wa miaka mitatu, mkazi wa Mwakitolyo alifanyiwa ukatili kwa kupelekwa kwenye baa hiyo na kunyweshwa pombe aina ya Balimi na kurekodiwa video kwa kutumia simu kisha kurushwa kwenye mitandao ya kijamii na kuonekana kwenye magroup ya whatsapp”,ameeleza Kamanda Magiligimba. 

Amesema baada ya tukio hilo kikosi Kazi cha askari wa Uhalifu wa Makosa ya Kimtandao waliwakamata watuhumiwa hao akiwemo baba mzazi wa mtoto aitwaye Godius Novat Katisha. 

Kamanda Magilgimba amesema watuhumiwa watafikishwa Mahakamani baada ya upelelezi kukamilika huku akitoa wito kwa wananchi kuheshimu haki za mtoto na yeyote atakayeenda kinyume hatua kali zitachukuliwa dhidi yake.

Katika Video hiyo iliyosambaa mtandaoni ambayo Malunde 1 blog pia imefanikiwa kuiona inamuonesha mtoto huyo akiwa anakunywa pombe aina ya Balimi huku akikohoa baadhi ya watu wanasikika wakicheka pamoja na sauti ya mwanaume akimhamasisha mtoto anywe pombe akimaliza amnunulie nyingine.

"Yaani hii ni Live ..unasikia Nkurunzinza..halafu Nkurunzinza usicheke sana Nkurunzinza..Kunywa kunywa nyingine nikununulie", sehemu ya maneno yanayosikika katika video hiyo ambayo imeibua hisia tofauti kwa watumiaji wa mitandao ya kijamii.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger