Sunday, 26 April 2020

36 Job Opportunities at Tanzania Automotive Technology Centre (TATC) “Shirika la Nyumbu“


Overview
Tanzania Automotive Technology Centre (TATC), synonymously known as “Shirika la Nyumbu“, was formally established on the 14th December 1985, through a Presidential Order, made under the Public Corporations Act 1969.

TATC’s mission is to develop a reputable capacity” for automotive engineering by conducting research and innovation, technology transfer and quality assurance services.
 
TATC is wholly owned by the Government of the United republic of Tanzania through the Ministry of Defense and National Service (MoDNS)



Share:

Marekani Yaanza Kufungua Baadhi Ya Majimbo Yake Licha Ya Kuendelea Kuongoza Duniani Kwa Vifo Vya Corona

Majimbo matatu nchini Marekani yameruhusu baadhi ya maduka kufunguliwa tena baada ya hatua zilizowekwa za kukabiliana na kusambaa kwa virusi vya corona.
 
Saluni za wanaume na wanawake sasa zinaweza kufunguliwa tena katika majimbo ya Georgia Oklahoma huku Alaska ikiondoa masharti iliyokuwa imewekea migahawa.

Vifo vinavyotokana na corona vimeendelea kuongezeka Marekani ambapo hadi asubuhi hii wamefariki Watu 54,265.

Marekani inaongoza kwa vifo vingi Duniani pia kwa visa ambapo leo vimefikia 960,896 na wamepona 118,162,

Rais wa nchi hiyo Donald  Trump amekabiliwa na ukosoaji mkubwa baada ya kupendeza kuwachoma sindano ya kemikali za kuua vimelea au za usafi wagonjwa wa corona

Kauli zake zimekua zikilaaniwa na madaktari pamoja na watengenezaji wa bidhaa wanaozitaja kuwa ni za hatari. 

Kemikali za kuua vijidudu au vimelea zinaua na zinaweza kuwa sumu zikiingizwa katika mwili wa binadamu , na hata matumizi yake ya nje ya mwili yanaweza kuwa hatari kwa ngozi, macho na mfumo wa kupumua.


Share:

TANZIA: Aliyewahi kuwa Mbunge wa Mafia, Abdulkarim Shah(Burji) afariki dunia

Aliyewahi kuwa mbunge wa Jimbo la Mafia (2005-2015), Abdulkarim Shah (59) amefariki dunia akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Hindu Mandal, jijini Dar as Salaam.

Akiwa mbunge, Shah alipata kuwa Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Ardhi, Maliasili na Utalii na pia alikuwa Kamishna wa Tume ya Utumishi ya Bunge.

Marehemu Abdulkarim Shah atazikwa leo Aprili 26, 2020 sasubuhi katika makaburi ya Kisutu jijini Dar


Share:

Diamond atangaza kuzilipia kodi familia 500 zilizoathirika na Corona kwa miezi mitatu

Msanii wa mizki wa Bongo Fleva Diamond Platnumz ametangaza kuwalipia kodi watu 500 walioathirika na Corona kwa miezi mitatu kila mmoja.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Diamond ameandika ujumbe huu.

“Najua katika kipindi hiki cha Corona, mambo mengi hayajakaa sawa, hususan upande wa biashara….nyingi zimeshuka na kupelekea hali ya kifedha kuyumba na mambo kuwa kidogo Magumu kwa wengi wetu…ijapokuwa na mimi ni Miongoni mwa walio ndani ya janga hili, lakini nimeona walau kwa kidogo changu nilicho nacho, nitoe kusaidia kulipia kodi za Nyumba kwa miezi Mitatu mitatu kwa familia 500, walau kusaidiana Katika kipindi hiki kigumu cha kupambana na Virusi hivi vya Corona…Licha ya kuwa Tiafa moja lakini siku zote mmekuwa Familia yangu kupitia Muziki wangu, hivyo naamini Shida yenu ni yangu, na Tabasamu lenu ni Langu pia….Jumatatu nitaweka rasmi Utaratibu wote wa namna gani Familia Hizi Miatano zinaweza kupata kodi hizo ya Nyumba….🙏🏼
#HiliNaloLitapita#ShidaYakoNiYangu #PamojaTutaishindaCorona
.
.
(I pretty much know that at these terrible times where we are all fighting global pandemic COVID-19,countless life circumstances have changed especially in businesses, many businesses are drowning hence rendering to financial difficulties and life becoming a little bit tough to many of us. Although I am amongst those affected by this pandemic on Economy, with the little that God has blessed me with, I have decided to atleast offer a helping hand by paying 3 Months house rent to 500 families as my kind gesture of helping one another during these terrible times of fighting COVID-19 for I believe i should share your troubles and your happiness too. On Monday i shall announce procedure on how these 500 families shall receive house rent. 🙏🏼)”


Share:

Serikali Kuendelea Kushirikiana Na Asasi Za Kiraia katika kupambana na janga la ugonjwa wa Corona

Na.WAMJW,Dar es Salaam.
Serikali imesema itaendelea kushirikiana na Asasi za Kiraia (AZAKI) katika kupambana na  janga la ugonjwa unaosababishwa na Virusi vya Corona (COVID-19).

Hayo yamesemwa jana  jijini Dar es Salaam  na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile  wakati akipokea andiko na mpango mkakati wa Asasi za Kiraia(AZAKI) kuhusu  janga la COVID -19 nchini.

Naibu Waziri Ndugulile alisema AZAKI pamoja na wananchi  wanao wajibu wa kushirikiana na Serikali katika kupambana na ugonjwa wa Corona ambao ni janga la kidunia lililoleta athari za kiuchumi na kiafya na kusabisha vifo vingi kwa muda mfupi.

“Ninawapongeza kwa kuona umuhimu wa kushirikiana na Serikali katika kukabiliana na janga hili , andiko lenu tumelipokea tutalifanyia kazi na kuangalia maeneo ambayo mmeyafanyia utafiti nasi tutaona ni namna gani tutaweza kushirikiana kwa pamoja katika kuudhibiti ugonjwa huu”, alisema Ndugulile.

Kwa upande wake Mratibu wa Kitaifa  Mtandao wa watetezi wa haki za binadamu Tanzania (THRDC) Onesmo Olengurumwa aliipongeza Serikali kwa hatua wanazochukuwa katika kukabiliana na ugonjwa huo na kusema kuwa ipo haja ya kuunga mkono juhudi zinazochukuliwa na Serikali.

Alisema  wameandaa mpango huo kwa kufanya  tathmini na kuainisha changamoto zilizojitokeza,  kuangalia  madhara mbalimbali yaliyotokea na kuona ni kwa jinsi gani wanaweza kuwa sehemu ya kuendeleza hatua zinazochukuliwa na Serikali katika kupambana na janga hilo.

“Katika mpango mkakati wetu maeneo ambayo azaki imepanga kushirikiana na serikali ni pamoja na uhamasishaji juu ya hatua za kujikinga, utoaji wa huduma,ushauri na kusaidia pale changamotozinapojitokeza, mikakati ya kupunguza matokeo hasi , pamoja na kuweka mpango wa pamoja baina ya Serikali na AZAKI”,alisema Olengurrumwa.

Naye  Mwenyekiti Shirikisho la vyama la watu wenye ulemavu Tanzania (SHIVYAWATA) Ummy Nderiananga aliwashukuru wataalamu wa afya kwa huduma wanayoitoa kwa wananchi waliopata maambukizi ya ugonjwa huo.

Ummy alisema ,”Sisi kama watu wenye ulemavu ugonjwa huu umetuathiri ndio maana tukaona tushirikiane katika kutoa elimu na kuainisha aina ya vifaa vitakavyohitajika kwa  walemavu ili kuhakikisha nchi yetu inakuwa salama bila kupata madhara makubwa ya ugonjwa huu.”

Jumla ya AZAKI 200 kutoka maeneo yote nchini zimeshiriki katika kuandaa andiko hilo, lengo likiwa ni  kuongeza ufanisi wa kukabiliana na janga hili.


Share:

Katika Kupambana Na Maambukizi Ya Corona CCM Yazindua Ushonaji Wa Barakoa Chuo Cha Ihemi Mjini Iringa

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wanawake wa CCM Tanzania (UWT) Mama Queen Mlozi, amezindua ushonaji wa Barakoa (Mask) katika Chuo cha Mafunzo Ihemi cha CCM Mkoani Iringa.

Mama Queen Mlozi amefanya Uzinduzi huo  tarehe 25 Aprili, 2020 akimuwakilisha Katibu Mkuu wa CCM Dkt. Bashiru Ally.

Katibu Mkuu wa UWT, akizundua utengenezaji huo wa Barakoa, ameeleza kuwa, "CCM imeamua kutengeneza barakoa kwa bei nafuu, kulinganisha na bei za maeneo mengine ili kutoa huduma na kuwasaidia wananchi kujikinga na maambukizi ya virusi vya Korona ikiwa ni jitihada za kuunga mkono mapambano ya kuutokomeza ugonjwa huo."

Ameongeza kwa kuwaomba wananchi kote nchini kununua barakoa zinazotengenezwa katika kiwanda hiko cha Ihemi, kutokana na bei nafuu ya shilingi elfu moja tu, zikizingatia ubora na viwango vinavyohitajika na mamlaka za viwango nchini.

Kwa sasa kiwanda hicho kina uwezo wa kuzalisha barakoa takribani elfu 4000 kwa siku na uzalishaji  unaongezeka kulingana na mahitaji ya wananchi.

Uzinduzi huo umehudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Katibu Mkuu wa UVCCM Mwl. Raymond Mangwala na viongozi wengine wa Chama na Serikali Mkoa wa Iringa.


Share:

Waziri Bashungwa Amewaagiza TEMDO Kutengeneza Mashine Za Kukamua Miwa Na Kuchakata Zao La Mkonge.

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Innocent Bashungwa ametoa rai kwa Taasisi ya Uhandisi na Usanifu wa Mitambo Tanzania (TEMDO) kuhakikisha wanawasaidia wajasiliamali wadogo  na wa kati kubuni  mashine za kutengeneza sukari pamoja na kuchakata katani ili kufungua fursa ya ajira na ongezeko la viwanda nchini.

Mhe. Bashungwa aliyasema hayo mkoani Arusha alipokuwa akizindua mashine 14 za kisasa zinazoendeshwa kwa mfumo wa kompyuta yaani CNC zikiwa na  thamani ya shilingi milioni 600 zilizotolewa kwa fedha za Maendeleo za Serikali na za ufadhili wa shirika la kimataifa la UNIDO.

Akizungumza na watumishi wa taasisi hiyo Mhe. Bashungwa aliwataka TEMDO kuongeza kasi ya kubuni mtambo mdogo wa kuchakata miwa ili kupata sukari ili kuongeza uzalishaji na upatikanaji wa wa bidhaa hiyo sokoni.

Aliongeza kwa kusema wafanyabiashara wanapandisha bei ya bidhaa hususani sukari sokoni, lakini endapo TEMDO itatengezeza mashine za kutengeneza sukari kwa wajasiriamali wadogo  itawasaidia kujikwamua kiuchumi na kusaidia upatikanaji wa sukari nchini.

Aidha amewataka pia kuongeza kasi ya kubuni mashine  ndogo ndogo za kuchakata zao la mkonge kwa kiwango cha upatikanaji wa nyuzi ili kuwasaidia wajasiliamli wadogo kutengeneza nyuzi wao wenyewe ili waweze kuziuza na  kujiongezea kipato badala ya hali ilivyo hivi sasa ambapo wakulima wanategemea wazalishaji wakubwa kununua bidhaa hiyo kwa kiasi kikubwa ambapo mkulima amekuwa hanufaiki.

Sambamba na hilo Mhe. Bashungwa alikabidhi barakoa zenye thamani ya Tsh.500,000 zilizotolewa na TEMDO  kwa mkoa wa Arusha ikiwa ni sehemu ya kuungana na Serikali kupambana na ugonjwa wa Korona kwa watoa huduma ya afya.

Awali Mkurugenzi Mkuu wa TEMDO, Prof. Fredrick Kahimba aliishukuru serikali kwa kuwawezesha kupata mashine hizo ambazo zitawezesha kuunda mitambo na mashine mbalimbali kwa urahisi zaidi kuliko awali.

Aliongeza kuwa “taasisi ya TEMDO imeendeleza shughuli mbalimbali zinazochangia maendeleo ya Viwanda Tanzania na kuwawezesha wakulima na wajasiliamali wadogo, wa kati na wakubwa kujipatia teknologia ya kuogeza uzalishaji mali.

Pia alimuomba Waziri Bashungwa kusaidia kuharakishwa uundwaji wa bodi mpya ya Wakurugenzi ya taasisi kwa kuwa liyokuwepo imemaliza muda wake.

Kwa upande wake bi Restuta Mrosso ambaye ni mnufaika wa utaalamu unaotolewa na TEMDO aliishukuru taasisi hiyo kwa kuwapatia ujuzi  wajasiriamali kutengeneza bidhaa mbalimbali na kuwasaidia kupata nembo ya Ubora (TBS).



Share:

Waziri wa Viwanda na Biashara Awataka Wenye Viwanda Vya Sukari Kurejea Mikataba Ya Ubinafsishwaji

Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Innocent Bashungwa amewataka wenye viwanda vya sukari nchini kurejea mikataba ya uzalishaji walioafikiana na Serikali kujiridhisha iwapo inaenda  sambamba na masharti waliokubaliana.
 
Mhe. Bashungwa aliyasema hayo mkoani Kilimanjaro alipofanya ziara katika kiwanda cha cha kuzalisha sukari cha TPC ili kujiridhisha na hali ya uzalishaji viwandani hapa.
 
Kuna viwanda vinne Kagera sugar,  Mtibwa Sugar, Kilombero Sugar na TPC wakati vinabinafsishwa vilipewa malengo ya kuongeza uzalishaji wake.
 
TPC  kilipobinafsishwa mwaka 2007 kilipewa malengo ya kuzalisha tani 75,000 lakini kwa sasa kinazalisha tani 100,000 kwa mwaka.
 
"Baada ya kutembelea TPC wanawatumia ujumbe viwanda vingine kama Kagera Sugar, mtibwa Sugar, kilombero Sugar kurejea mikataba ya ubinafsishaji ili kujiridhisha kama wanaenda sambamba na mikataba hiyo."
 
Bashungwa aliongeza kuwa viwanda vya Kagera sugar, Mtibwa sugar na Kilombero kurejea mikataba ya uzalishaji kuna malengo ya serikali, nitapita kuangalia kama mmezingatia mnafuatilia mikataba ya uzalishaji.
 
"Kama watakuwa wameshindwa kutimiza malengo hayo basi watakuwa wanatukwamisha.
 
"Mhe Rais Dk John Pombe Magufuri alipoingia madarakani mwaka 2015, aliweka malengo ya kuwa nchi ya viwanda ili tujitegemee katika uzalishaji wa vitu kama sukari."
 
Mhe Bashungwa aliendelea kusema "viwanda hivi vinatoa ajira kubwa kwa kinamama na vijana, mfano hapa TPC peke yake wanatoa ajira elfu nne za moja kwa moja achilia mbali zile zinazokuja kutokana na uzalishaji na usafirishaji.
 
"Endapo viwanda vya kuzalisha sukari vya kagera , Mtibwa na Kilombero vitazingatia mkataba wa uzalishaji basi hakutakuwa na uhaba wa sukari hapa nchini. Tutaachana na masuala ya kuagiza sukari kila mwaka pamoja na upungufu wa bidhaa hiyo.

"Nia ya Serikali ni kuzalisha sukari kwa wingi ili kuuza ndani ya nchi na nje ya nchi katika masoko ya EAC, SADC,COMESA kwa kuwa nchi yetu ni mwanachama wa jumuiya hizo zote".

Aidha amewaonya wafanyabiashara wanaosambaza sukari nchini ambao wanatumia kipindi cha mfungo  kuongeza bei ya sukari, kuwa serikali haitawafumbia macho kwa kufanya kitendo hicho.

Ole wenu tukiwabainisha tutawawafutia leseni za biashara ,hamtafanya biashara tena kama mkibainika kupandisha bei ya sukari.
Aliongeza kusema serikali imetoa ukomo wa bei za sukari ya kiwango cha juu si lazima mtu akauza bei hiyo.



Share:

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumapili April 26
















Share:

Saturday, 25 April 2020

CCM YAIBUKA NA USHONAJI WA BARAKOA KWA BEI NAFUU KUKABILIANA NA CORONA


Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wanawake wa CCM Tanzania (UWT) Mama Queen Mlozi, akizungumza jambo wakati wa kuzindua ushonaji wa Barakoa (Mask) katika Chuo cha Mafunzo Ihemi cha CCM Mkoani Iringa.
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wanawake wa CCM Tanzania (UWT) Mama Queen Mlozi, akishiriki ushonaji w Barakoa wakati wa kuzindua ushonaji wa Barakoa (Mask) katika Chuo cha Mafunzo Ihemi cha CCM Mkoani Iringa.
Baadhi ya Mashine za kushoea Barakoa kama zionekanavyo pichani
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wanawake wa CCM Tanzania (UWT) Mama Queen Mlozi pamoja na Katibu Mkuu wa UVCCM Mwl. Raymond Mangwala wakionesha barakoa zilizoshonwa tayari kwa kutumika na Wananchi,mara baada ya kuzindua ushonaji wa Barakoa (Mask) katika Chuo cha Mafunzo Ihemi cha CCM Mkoani Iringa.
***
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wanawake wa CCM Tanzania (UWT) Mama Queen Mlozi, amezindua ushonaji wa Barakoa (Mask) katika Chuo cha Mafunzo Ihemi cha CCM Mkoani Iringa.

Mama Queen Mlozi amefanya Uzinduzi huo leo tarehe 25 Aprili, 2020 akimuwakilisha Katibu Mkuu wa CCM Dkt. Bashiru Ally.

Katibu Mkuu wa UWT, akizindua utengenezaji huo wa Barakoa, ameeleza kuwa, "CCM imeamua kutengeneza barakoa kwa bei nafuu, kulinganisha na bei za maeneo mengine ili kutoa huduma na kuwasaidia wananchi kujikinga na maambukizi ya virusi vya Korona ikiwa ni jitihada za kuunga mkono mapambano ya kuutokomeza ugonjwa huo."

Ameongeza kwa kuwaomba wananchi kote nchini kununua barakoa zinazotengenezwa katika kiwanda hiko cha Ihemi, kutokana na bei nafuu ya shilingi elfu moja tu, zikizingatia ubora na viwango vinavyohitajika na mamlaka za viwango nchini.

Kwa sasa kiwanda hicho kina uwezo wa kuzalisha barakoa takribani elfu 4000 kwa siku na uzalishaji unaongezeka kulingana na mahitaji ya wananchi.

Uzinduzi huo umehudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Katibu Mkuu wa UVCCM Mwl. Raymond Mangwala na viongozi wengine wa Chama na Serikali Mkoa wa Iringa.
Share:

Video Mpya : SUMU KALI - CORONA

Msanii Sumu Kali anakualika kutazama video ya wimbo wake mpya unaitwa Corona.
Tazama hapa chini
Share:

UMOJA WA KLABU ZA WAANDISHI WA HABARI TANZANIA (UTPC) KUGAWA VIFAA VYA KUJIKINGA NA CORONA KWA WAANDISHI WA HABARI

Umoja wa  klabu za waandishi wa habari Tanzania  (UTPC),umetangaza mpango wa kugawa  vifaa maalumu vya kujikinga  na ugonjwa wa Covid 19 kwa klabu zote za waandishi wa habari Tanzania.


Hayo yamesemwa na Rais wa UTPC bwana Deogratias  Nsokolo kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanyika leo   April 25 Jijini Mwanza, kwenye ofisi za umoja huo.

Nsokolo amebainisha kuwa, utekelezaji wa mpango huo ni matokeo ya tathimini ya usalama kwa waandishi uliofanywa na UTPC na kubaini uwepo wa changamoto za vifaa kwa waandishi wa habari Nchini.

Nsokolo amebainisha kuwa klabu zote ishirini na nane zitapatiwa vifaa vya kujikinga, ikiwemo barakoa, vitiririsha maji na vitakasa mikono.

Pia UTPC imeiomba serikali na wadau wengine wa kimaendeleo Nchini kuliingiza kundi la waandishi wa habari kwenye migao ya vifaaa vya kujikinga na Corona vinavyotolewa wakati huu, kwa kuwa uhitaji wa vifaa  kwa kundi hilo ni mkubwa zaidi.

Pia UTPC imewaomba waandishi kuzingatia maelekezo ya kujikinga yanayotolewa na wataalamu wa Afya Nchini ili waendelee kufanya kazi zao wakiwa salama.

Kundi la waandishi wa habari ni moja kati ya makundi yanayofanya kazi kwenye mazingira ya hatari na hivyo kuwa na mikakati ya kujilinda ni mushimu.

Edwin Soko
Watetezi Tv
Mwanza
25.04.2020

Share:

SERIKALI KUENDELEA KUSHIRIKIANA NA ASASI ZA KIRAIA KUPAMBANA NA CORONA



NA. WAMJW, Dar es Salaam
Serikali imesema itaendelea kushirikiana na Asasi za Kiraia (AZAKI) katika kupambana na  janga la ugonjwa unaosababishwa na Virusi vya Corona (COVID-19).


Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam  na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile  wakati akipokea andiko na mpango mkakati wa Asasi za Kiraia(AZAKI) kuhusu  janga la COVID -19 nchini.

Naibu Waziri Ndugulile alisema AZAKI pamoja na wananchi  wanao wajibu wa kushirikiana na Serikali katika kupambana na ugonjwa wa Corona ambao ni janga la kidunia lililoleta athari za kiuchumi na kiafya na kusabisha vifo vingi kwa muda mfupi.

“Ninawapongeza kwa kuona umuhimu wa kushirikiana na Serikali katika kukabiliana na janga hili , andiko lenu tumelipokea tutalifanyia kazi na kuangalia maeneo ambayo mmeyafanyia utafiti nasi tutaona ni namna gani tutaweza kushirikiana kwa pamoja katika kuudhibiti ugonjwa huu”, alisema Ndugulile.

Kwa upande wake Mratibu wa Kitaifa  Mtandao wa watetezi wa haki za binadamu Tanzania (THRDC) Onesmo Olengurumwa aliipongeza Serikali kwa hatua wanazochukuwa katika kukabiliana na ugonjwa huo na kusema kuwa ipo haja ya kuunga mkono juhudi zinazochukuliwa na Serikali.

Alisema  wameandaa mpango huo kwa kufanya  tathmini na kuainisha changamoto zilizojitokeza,  kuangalia  madhara mbalimbali yaliyotokea na kuona ni kwa jinsi gani wanaweza kuwa sehemu ya kuendeleza hatua zinazochukuliwa na Serikali katika kupambana na janga hilo.

“Katika mpango mkakati wetu maeneo ambayo azaki imepanga kushirikiana na serikali ni pamoja na uhamasishaji juu ya hatua za kujikinga, utoaji wa huduma,ushauri na kusaidia pale changamotozinapojitokeza, mikakati ya kupunguza matokeo hasi , pamoja na kuweka mpango wa pamoja baina ya Serikali na AZAKI”,alisema Olengurrumwa.

Naye  Mwenyekiti Shirikisho la vyama la watu wenye ulemavu Tanzania (SHIVYAWATA) Ummy Nderiananga aliwashukuru wataalamu wa afya kwa huduma wanayoitoa kwa wananchi waliopata maambukizi ya ugonjwa huo.

“ Ummy alisema ,”Sisi kama watu wenye ulemavu ugonjwa huu umetuathiri ndio maana tukaona tushirikiane katika kutoa elimu na kuainisha aina ya vifaa vitakavyohitajika kwa  walemavu ili kuhakikisha nchi yetu inakuwa salama bila kupata madhara makubwa ya ugonjwa huu.”


Jumla ya AZAKI 200 kutoka maeneo yote nchini zimeshiriki katika kuandaa andiko hilo, lengo likiwa ni  kuongeza ufanisi wa kukabiliana na janga hili.

Share:

RAIS MAGUFULI ATOA MSAMAHA KWA WAFUNGWA 3,973... 256 WALIOHUKUMIWA KUNYONGWA WABADILISHIWA ADHABU



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewatakia heri Watanzania wote katika kuadhimisha kumbukumbu ya miaka 56 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar huku akiwataka kutumia siku ya kesho Aprili 26,2020 kuutafakari Muungano ulioasisiwa na Viongozi wakuu Baba wa Taifa, Hayati Mwl Julius Kambarage Nyerere na Hayati Sheikh Abeid Amani Karume pamoja na kumuomba Mwenyezi Mungu aepushe janga la Ugonjwa wa Corona.

Aidha katika kuadhimisha miaka 56 ya Muungano,Rais Magufuli ametoa msamaha kwa jumla ya wafungwa 3,973 ambapo kati yao wafungwa 3,717 wamesamehewa vifungo vyao na wafungwa 256 waliokuwa wanakabiliwa na adhabu ya kunyongwa hadi kufa wamebadilishiwa adhabu hiyo.
Share:

MARUFUKU YA KUTOTOKA NJE USIKU NCHINI KENYA YAONGEZWA KWA SIKU 21..WAGONJWA WA CORONA NCHINI WAMEFIKA 343


Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ameongeza muda wa marufuku ya watu kusafiri na kuingia au kutoka katika mji wa Nairobi na miji mingine minne kwa muda wa siku 21 ili kuendelea kukabiliana na Virusi vya Corona.

Marufuku ya kutoka nje nyakati za usiku kwa taifa zima pia imeongezwa kwa siku 21.
 
Kenyatta  ametangaza kuwa Kenya sasa ina visa 343 baada ya wengine 7 kuongezeka leo  na wagonjwa waliopona ni 94


Share:

Hatua Zilizochukuliwa na Serikali Katika Mapambano Dhidi ya Virusi Vya Corona




Share:

MAAMBUKIZI YA UGONJWA WA MALARIA YAPUNGUA KWA ASILIMIA 50





Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger