Friday, 24 April 2020

Makubwa Haya!! WANANCHI WAVUNJA AMRI YA CORONA KUSHUHUDIA CHIFU MAARUFU AKIZIKWA NDANI YA GARI AKIWA AMEKAA KWENYE USUKANI

Mazishi ya Tshekede Pitso

Chifu Tshekede Pitso wa kijiji kimoja Jozanashoek Sterkspruit, Eastern Cape nchini Afrika Kusini amewaacha wengi vinywa wazi baada kuzikwa ndani ya gari lake alilopenda sana enzi za uhai wake la Mercedes Benz.

Inaelezwa  kuwa chifu huyo alikuwa ameagiza familia yake kuheshimu matakwa yake kwa kumzika ndani ya gari hilo lenye gharama ghali.

Chifu Pitso, ambaye alifariki akiwa na miaka 72, alivutwa na trela hadi katika kaburi lake akiwa amevalia suti nyeupe huku mikono yake yote ikiwa imeshikilia 'steering' kana kwamba alikuwa hai. 

Kulingana na binti wa chifu huyo, Sefora Letswaka, marehemu alipenda sana gari hilo la Mercedes Benz E500 licha ya kuwa lilikuwa limeharibika.

 "Kwa wakati mmoja baba yangu alikuwa mwanabiashara tajiri ambaye alikuwa na kundi la magari ya Mercedes. Miaka miwili iliyopita, alijinunulia Mercedes Benz iliyokuwa imetumika. 

Haikuchukua muda kabla ya gari hilo kuharibika, lakini muda wake mwingi alikuwa akiketi ndani ya gari hilo. Hakuwa analiendesha lakini hapo ndipo alikuwa anapata furaha na kusema wakati utakapofika angependa kuzikwa ndani yake. Tulimsikiza na kutimiza matakwa yake na ninatumai amefurahi," alidokezea Sefora.

 Baba huyo wa watoto sita alifanyiwa mazishi rasmi ya dini ya kikristu katika boma la familia hiyo Afrika Kusini. 

Mazishi ya mwanasiasa huyo wa Chama cha United Democratic Movement iliwashuhudia watu wengi wakihudhuria ambao waliamua kuvunja sheria ya kutoka nje kutokana na Janga la Corona. 

Share:

Wenye Virusi Vya Corona Zanzibar Wafika 98.....Ni Baada Ya Wengine 15 Kuongezeka

Wizara ya Afya Zanzibar imetoa taarifa ya ongezeko la Wagonjwa wapya 15 wa corona na kufikisha idadi ya wagonjwa 98 kutoka 83.

Taarifa hiyo imesema wagonjwa wote ni Raia wa Tanzania (Unguja 10 na Pemba watano).

Kwa ongezeko hili sasa idadi ya visa vya corona Tanzania nzima imefikia 299 kutoka 284.


Share:

WALIMU WACHAPWA FIMBO KISHIRIKINA..WALAZWA NJE BILA KUJIJUA


Walimu wanaofundisha katika shule mbalimbali zilizopo katika Halmashauri ya Mji wa Geita, wamelazimika kukimbia makazi yao kwenye maeneo ya shule kutokana na kuchapwa mijeredi na wakati mwingine kujikuta wakiwa wamelazwa nje.

Hoja hiyo imeibuka katika kikao cha baraza la madiwani wa Halmashauri ya Mji wa Geita, ambapo Diwani wa Kata ya Kanyara, Mapande Enock amesema kuwa walimu wanapitia shida hiyo kutokana na imani za kishirikina.

Diwani huyo akaenda mbali zaidi akitaka nyumba hizo zijengwe uraiani na si kwenye maeneo ya shule ambayo anaona ni hatarishi kwa maisha ya walimu, kwani shule nyingi zipo mbali na makazi ya watu.

Modest Alpolnary ambaye ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Geita, akakiri kuwepo kwa changamoto hiyo huku Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo akishauri jamii kuacha tabia ya kuwapiga na kuwalaza nje walimu kwani inaathiri mkakati wa Serikali wa kuhakikisha walimu wanaishi katika mazingira mazuri.
 Chanzo - EATV
Share:

Wenye Virusi Vya Corona Nchini Kenya Wafika 336....Ni Baada ya Wengine 16 Kuongezeka Leo

Watu 16 zaidi wameambukizwa  corona  nchini Kenya na kufanya idadi ya wagonjwa nchini Kenya kufikia 336.

Katibu wa Kudumu katika Wizara ya Afya Dkt Rashid Aman amewaambia waandishi wa habari leo Ijumaa, Aprili 24 kwamba wagonjwa hao walithibitishwa baada ya sampuli 946 kupimwa katika saa 24 zilizopita. 

Amesema Visa 11 vimetokea Nairobi huku wagonjwa wengine 5 wakiwa Mombasa.


Share:

WAGONJWA WENGINE 37 WAPONA CORONA NCHINI TANZANIA


 Wagonjwa 37 waliokuwa wameambukizwa virusi vya Corona (COVID-19) wamepona na kuruhusiwa kurejea nyumbani baada ya vipimo vya mwisho kuthibitisha kwamba hawana maambukizi ya COVID-19.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amesema kuwa wagonjwa hao 37 ni kati ya wagonjwa 108 waliothibitika kuwa na maambukizi ya virusi vya Corona lakini sasa hawana dalili zozote za ugonjwa kama homa, mafua na kikohozi.

Waziri Ummy Mwalimu amewataka watu waliopona ugonjwa huo kuzingatia maelekezo ya wataalamu wa afya ili kujikinga na maambukizi mapya ya COVID-19 kwani zipo tafiti zilizofanyika nchi mbalimbali ikiwamo China zimeonyesha kuwa watu wanaweza kupata  maambukizi mapya kama asilimia 14.

Waziri pia ametoa wito kwa watumishi wa afya kuendelea kutoa huduma za afya kwa watu wote wanaohitaji huduma za matibabu wakiwamo wenye dalili za ugonjwa wa Corona.

“Tumeona kumeanza tabia ambayo ni kinyume na taratibu za afya, hatutakiwi kuwakataa wagonjwa wenye dalili za maambukizi ya virusi vya Corona. Nasisitiza kwamba watumishi wa afya wanakumbushwa kutekeleza wajibu wao kwa kuzingatia nwongozo wa Taifa wa kudhibiti maambukizi (National Infection Prevention and Control Guidelines for Health care Services in Tanzania) wa Juni, 2018 pamoja na mwongozo wa Menejimenti ya Matibabu ya Ugonjwa wa COVID-19 wa Januari, 2020 ili kujikinga na maambukizi wakati wa utoaji wa huduma kwa wagonjwa,” amesema Waziri Ummy Mwalimu.


Share:

Rufaa ya Freeman Mbowe na Vigogo Wengine CHADEMA Kusikilizwa May 13 Mwaka huu

Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, inatarajia kuanza kusikiliza rufaa iliyokatwa na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na viongozi wenzake saba wakipinga hukumu na adhabu iliyotolewa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Machi 10 mwaka huu.

Kesi hiyo ilitajwa jana na kupangwa kutajwa tena mbele ya Lameck Mlacha Aprili 28 mwaka huu na rufaa itasikilizwa Mei 13 mwaka huu mbele ya Jaji Ilvin Mugetta.

Machi 10 Mbowe na wenzake nane walihukumiwa kulipa faini ya Sh milioni 350 au kutumikia kifungo cha miezi mitano gerezani baada ya kutiwa hatiani kwa makosa 12 kati ya 13 yaliokuwa yakiwakabili.

Uamuzi wa kuwatia hatiani ulitolewa na Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Kisutu, Thomas Simba baada ya kupitia ushahidi wa upande wa mashtaka na ule wa utetezi.

Mbali na Mbowe, viongozi wengine wa Chadema waliohukumiwa katika kesi hiyo ni Mbunge wa Iringa Mjini Peter Msigwa, Naibu Katibu Mkuu Zanzibar, Salum Mwalimu, Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika na Mbunge wa Tarime mjini Ester Matiko.

Wengine ni Mbunge wa Kawe, Halima Mdee, Mbunge wa Bunda, Esther Bulaya na mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche na aliewahi kuwa Katibu wa chama hicho Dk Vincent Mashinji, ambaye sasa amejiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Hata hivyo viongozi wote kwa nyakati tofauti walifanikiwa kulipa faini na kukwepa kutumikia kifungo hicho.


Share:

Kuingia Hospitali Ya Bugando Kuanzia Leo Ni Lazima Uvae Barakoa (Mask)

Kuanzia leo Aprili 24, 2020, mtu yeyote yule, wakiwemo wagonjwa ama ndugu za wagonjwa atakayeingia katika Hospitali ya Bugando  jijini Mwanza, atatakiwa kuvaa barakoa na kuirejesha getini kabla ya kutoka, ikiwa ni hatua ya kujikinga na maambukizi ya Virusi vya Corona.



Share:

Wenye Virusi Vya Corona Uganga Wafika 74....Ni Baada ya Madereva 06 wa Tanzania na Wengine 05 wa Kenya Kukutwa na Virusi Hivyo

Watu 74 wabainika kuwa na virusi vya Corona nchini Uganda baada ya kuongezeka maambukizi mapya 11, ambapo kati ya watu hao 11 Watanzania wapo 6, watano wanatoka nchini Kenya.

Wizara ya Afya nchini Uganda imesema kati ya wagonjwa 74 wa Corona 46 wamepona na kuruhusiwa.


Share:

Mvua Yaua Watu Wawili Mkoani Arusha

Mvua zinazoendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Arusha, zimesababisha vifo vya watu wawili wilayani Arumeru.

Akitoa taarifa za ya mwendendo wa mvua ambazo zimenyesha kwa siku tatu mfululizo, Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Jerry Muro, alisema mvua hizo zimeleta madhara makubwa baada ya watu wawili kufariki jana katika Halmashauri ya Meru.

Muro aliwataja waliofariki kuwa ni Terevaeli Nasari (65) Mkazi wa kitongoji cha Meto Kijiji cha Mulala Kata ya songoro.

Alisema mtu huyo alifariki dunia asubuhi ya jana baada ya maporomoko ya udongo kutoka mlimani kuvunja ukuta wa chumba alichokuwa amelala na kusababisha kifo chake na kwamba mwili wake upo katika Hospital ya Mount Meru.

Alisema kifo kingine ni cha mtoto Tumaini Simon mwenye miaka miaka mitatu kutoka Kijiji cha Valeska Kitongoji cha Mwamko, ambaye amesombwa na mafuriko ya maji wakati akiwa katika harakati za kuokolewa na mzazi wake.

Alisema mzazi wa mtoto huyo, Mzee Simon alifanikiwa kuokoa mtoto mmoja na mwingine kufariki dunia na mwili wa mtoto aliyefariki umepatikana na taratibu za mazishi zinaendelea.


Share:

Serikali Kutoa Ajira Zaidi ya 4000 kwa Polisi, Magereza, Uhamiaji, Zimamoto

Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, imetangaza ajira zaidi ya 4,400 kwa vyombo vya ulinzi na usalama nchini.

Akiwasilisha makadirio ya bajeti ya mwaka 2020/21, Waziri wa wizara hiyo, George Simbachawene, alisema ajira hizo zitakwenda pamoja na mafunzo mbalimbali kwa askari na watumishi mbalimbali.

Alisema kwa mwaka huo, Jeshi la Polisi linatarajia kuajiri askari 2,725, askari Magereza 685, Uhamiaji 495 na Zimamoto 501.

Simbachawene alisema katika mwaka 2020/21 Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na wadau wa ndani na nje ya nchi limepanga kuendelea kutoa mafunzo mbalimbali kwa maafisa, wakaguzi na askari 9,465 pamoja na watumishi raia 25.

Alisema kati ya hao 9,051 watapata mafunzo ndani ya nchi kupitia vyuo vya polisi na 414 nje ya nchi kwa udhamini wa taasisi na nchi mbalimbali.

Aidha, alisema katika kuimarisha kuimarisha utendaji kazi wa watumishi wa Jeshi la Polisi jumla ya maofisa, wakaguzi, askari na watumishi raia 5,470 wamepata mafunzo mbalimbali, kati ya hao 5,461 walipata mafunzo ndani ya nchi na tisa nje ya nchi.

Kwa upande wa Jeshi la Magereza, alisema katika kipindi cha Julai,2019 hadi Machi, 2020 jumla ya maofisa naaskari 1,537 walipata mafunzo ya uongozi wa kijeshi katika Vyuo vya Magereza nawatumishi 951 walihitimu mafunzo ya taaluma mbalimbali katika vyuo vya ndani na nje yaJeshi.

“Jeshi linatarajia kuajiri askari 685 wenye fani mbalimbali watakaopatiwa mafunzo ya awali katika Chuo cha Magereza Kiwira (Mbeya), mafunzo ya uendeshaji wa Magereza na Taaluma ya Urekebishaji kwa Maafisa na Askari 3,270 katika ngazi mbalimbali za uongozi,” alisema.

Waziri Simbachawene alisema kuhusu hali ya ulinzi na usalama magerezani, hadi kufikia mwezi Machi, 2020 kulikuwa na jumla ya wafungwa na mahabusu 32,438 katika magereza yote nchini na kwamba kati ya hao, wafungwa ni 14,464 na mahabusu 17,974 ambapo ni asilimia 9 zaidi ya uwezo uliopo wa kuhifadhi wafungwa na mahabusu 29,902.

Simbachawene alisema mwaka 2020/21Idara ya Uhamiaji inatarajia kuajiri askari 495 na kuwapa mafunzo ya awali, ikiwamo kuendelea kutoa mafunzo mbalimbali kwa maofisa, askari na watumishi raia ili kuwaongezea ujuzi wa utendaji kazi kwa ufanisi zaidi.

Alisema katika kukabiliana na changamoto ya upungufu wa rasilimaliwatu, Jeshi la Zimamoto na Uokoaji linatarajia kuwapandisha vyeo Maoafisa na askari 1,311 na kuajiri askari wapya.


Share:

China yaipa WHO dola milioni 50 baada ya Marekani kulikatia misaada shirika hilo

China inasema itatoa mchango wa Dola Milioni 30 kwa Shirika la Afya Duniani WHO, kulisaidia kupambana na maambukizi ya virusi vya Corona, ugonjwa unaosubua ulimwengu.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya nje nchini humo Hua Chunying kupitia ukurasa wake wa Twitter amethibtisha hilo na kusema mchango huo unalenga kulisaidia shirika hilo kupambana virusi katika nchi zinazoendelea.

Aidha, amesema kuwa tayari China imetoa Dola Milioni 20, mchango uliotoa kwa WHO mwezi Machi.


Hatua hii ya China imekuja wiki moja baada ya rais wa Marekani Donald Trump kutangaza kuwa nchi yake inasitisha mchnago Wake kwa Shirika hilo kwa madai ya kushindwa kudhibiti mapema virusi hivyo.

Hatua hiyo ya Marekani  ilaaniwa na China na mataifa mengine ya Magharibi huku WHO ikisema huu sio wakati wa kusitisha mchango  huo wa fedha.


Share:

Hali ya Ukusanyaji wa Mapato kwa Halmashauri Zote Hapa Nchini

Kwa mwaka wa fedha 2019/20 Halmashauri zilipanga kukusanya shilingi bilioni 765.48 kutoka kwenye vyanzo vyake vya ndani na katika kipindi cha Julai, 2019 hadi Machi, 2020 Halmashauri zimekusanya Jumla ya Shilingi bilioni 527.31 ambayo ni asilimia 69 ya makisio ya mwaka.

Uchambuzi wa taarifa za mapato ya ndani ya Halmashauri katika kipindi cha Julai, 2019 hadi Machi, 2020 umeonesha ongezeko la mapato yaliyokusanywa kutoka Shilingi Bilioni 449.82 kwa kipindi cha Julai, 2018 hadi Machi, 2019 na kufikia Shilingi bilioni 527.31 katika kipindi cha Julai, 2019 hadi Machi, 2020 ambalo ni ongezeko la  Shilingi bilioni 77 sawa na asilimia 17 .

Vile vile uchambuzi unaonesha kuwa katika kipindi cha Julai, 2019 hadi Machi, 2020 Halmashauri 58 zimekusanya mapato ya ndani kwa asilimia 75 au zaidi kwa kulinganishwa na makisio kwa mwaka wa fedha 2019/20.

Aidha, Halmashauri 96 zimekusanya asilimia 50 au zaidi lakini chini ya asilimia 75 na Halmashauri 31 zimekusanya chini ya asilimia 50 ya makisio ya mwaka.

Halmashauri hukusanya mapato mengi au kidogo kwenye vyanzo tofauti kulingana na hali halisi ya shughuli za kiuchumi za kila Halmashauri ikiwemo mavuno na mauzo ya mazao mbalimbali na katika kipindi hiki ushuru wa Huduma umekusanywa vizuri na umechangia asilimia 26 ya mapato yote katika kipindi cha Julai, 2019 hadi Machi, 2020 na usimamizi wa ukusanyaji wa mapato katika eneo hili unaonekana kuimarika.

Akitoa taarifa ya mapato na matumizi ya Halmashauri Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais – TAMISEMI Mhe. Selemani Jafo  jana  amesema katika kipindi cha miezi tisa (Julai, 2019 – Machi, 2020), Halmashauri ya Mji wa Njombe imevunja rekodi kwa kukusanya mapato kwa asilimia 130 ya makisio ya mwaka 2019/2020 huku Halmashauri ya Wilaya ya Shinyangaikiwa ya mwisho kwa kukusanya  asilimia 30 tu ya makisio yake kwa kipindi cha miezi tisa.

Mhe. Jafo alifafanua kuwa halmashauri zote zilizokusanya zaidi ya asilimia 100 hadi Machi, 2020 na zile ambazo zimejitathmini na kuona upo uwezekano wa kuzidi asilimia 100 ya bajeti za mapato ya ndani ifikapo Juni, 2020 zinaelekezwa kufanya mapitio ya Bajeti kwa mujibu wa Kifunga cha 29 (1) cha Sheria ya Bajeti ya mwaka 2015 ili ziweze kuongeza Bajeti za mapato na matumizi ya fedha hizo.

“Halmashauri itakayoshindwa kufanya hivyo haitaweza kutumia fedha hizo kwa kuwa Bajeti ya mwaka wa fedha 2020/2021 imekwisha idhinishwa na Bunge” alisisitiza Jafo.

Katika kuzipima Halmashauri zote kwa kigezo cha wingi wa mapato (pato ghafi), Waziri Jafo ameeleza kuwa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala imekusanya mapato mengi zaidi kuliko Halmashauri zote kwa kukusanya Shilingi 43.14 na Halmashauri ya Wilaya ya Gairo imekusanya mapato kidogo kuliko Halmashauri zote kwa kukusanya Shilingi Milioni 343.70. 

Aidha Waziri Jafo amesema  mapato ya ndani ya Halmashauri Kimkoa kwa kuzingatia asilimia kuwa Mkoa wa Njombe umefanya vizuri kwa kukusanya wastani wa asilimia 87 ya makisio ya Halmashauri za Mkoa huo huku Mkoa wa mwisho kwa kigezo hicho ni Mkoa wa Simiyu ambao umekusanya wastani wa asilimia 51 ya makisio ya mwaka ya Halmashauri za Mkoa huo.

Katika kigezo cha mapato ya ndani ya Halmashauri Kimkoa kwa kuzingatia wingi wa Mapato amesema Mkoa wa Dar es Salaam umefanya vizuri kwa kukusanya kiasi cha Shilingi 126.77 huku Mkoa wa mwisho katika wingi wa ukusanyaji wa mapato ni Mkoa wa Rukwa ambao umekusanya Shilingi 6.34.

Jafo alibainisha ukusanyaji wa Mapato ya Ndani ya Halmashauri kwa kuzingatia aina za Halmashauri kwa Kigezo cha Asilimia ya Makusanyo ukilinganisha na makisio kuwa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam imeongoza kundi la Halmashauri za Majiji kwa kukusanya mapato kwa asilimia 78 ya makisio yake ya mwaka huku halmashauri ya Jiji la Dodoma ikiwa ya mwisho kwa kukusanya asilimia 55 ya makisio yake.

“Kwa upande wa Asilimia Halmashauri ya Manispaa ya Iringa imeongoza kundi la Halmashauri za Manispaa kwa kukusanya  asilimia 100 ya makisio yake huku Manispaa ya Lindi ikiwa ya mwisho akwa kukusanya asilimia 49  kwa mwaka wa Fedha 2019/20” amesema Jafo.

Katika kipengele cha Halmashauri za Miji, Jafo amesema Halmashauri ya Mji wa Njombe imeongoza kwa kukusanya asilimia 130 ya makisio ya mapato ya ndani kwa mwaka na Mji wa Handeni imekuwa ya mwisho kwa kukusanya asilimia 43 ya makisio yake kwa mwaka.

Aidha, kwa kundi la Halmashauri za Wilaya amesema, Halmashauri ya Wilaya ya Masasi imeongoza kwa kukusanya asilimia 126 ya makisio ya mapato ya ndani na Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga imekuwa ya mwisho katika kundi hilo kwa kukusanya asilimia 30 ya makisio ya mapato yake ya ndani.

Waziri Jafo aliongeza kuwa ukusanyaji wa mapato ya ndani ya Halmashauri kwa kuzingatia wingi wa makusanyo ni Jiji la Dodoma ambalo limeongoza kundi la Majiji kwa kukusanya Shilingi bilioni 36.04 na Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam limekuwa la mwisho ambapo kwa kukusanya Shilingi bilioni 8.83.

Kwa upande wa Manispaa, Halmashauri ya Manispaa ya Ilala imeongoza kwa kukusanya Shilingi bilioni 43.14 na Manispaa ya Kigoma Ujiji imekuwa ya mwisho katika kundi hili ambapo imekusanya Shilingi Bilioni 1.20 amesisitiza Jafo.

Pia aliongeza kuwa  halmashauri ya Mji wa Geita imeongoza kwa wingi wa mapato kwa kukusanya Shilingi Bilioni 7.02 na Halmashauri ya Mji wa Mbulu imekuwa ya mwisho katika kundi kwa kukusanya Shilingi Milioni 671.78.

Na kwenye Halmashauri za Wilaya, Halmashauri  ya Chalinze imeongoza kwa kukusanya mapato mengi ya Shilingi Bilioni 5.78 na  Halmashauri ya Wilaya ya Gairo imekuwa ya mwisho katika kundi hili ambapo imekusanya Shilingi Milioni 343.70.

Halkadhalika Jafo alibainisha matumizi ya vyanzo vya ndani vya Halmashauri kwa kipindi cha Julai 2019 – Machi 2020 kuwa  Halmashauri zimetumia kiasi cha Shilingi Bilioni 329.53 ambayo ni asilimia 63 ya mapato halisi yaliyokusanywa na kati ya matumizi hayo, Shilingi Bilioni 186.75 zimetumika kwenye matumizi ya kawaida na Shilingi Bilioni 142.80 zimetumika kwenye matumizi ya maendeleo.

Amehitimisha  kuwa  Shilingi Bilioni 34.83 zimetumika kwenye miradi ya maendeleo ikiwa ni bakaa ya mapato ya ndani ya mwaka wa fedha 2018/19 ambayo ni asilimia 76.5 ya bakaa yote (Shilingi Bilioni 45.54), hivyo kufanya jumla ya matumizi ya miradi ya maendeleo kufikia Shilingi Bilioni 169.20.

Mwisho.


Share:

Baraza la Ulamaa BAKWATA Latoa Tamko kuhusu Ibada za Ramadhwaan na janga la Corona

Wakati tukikaribia Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, Baraza la Ulamaa BAKWATA Taifa limefanya vikao kadhaa kupitia, kutafakari na kuzingatia mwenendo wa COVID 19 nchini Tanzania na hali ya utekelezaji wa Ibada za Swala za Jamaa, Ijumaa na Tarawehe hususan wingi wa watu wanaojitokeza Misikitini katika mwezi wa Ramadhani.

Baada ya tafakari iliyozingatia ushauri wa kitaalamu na miongozo ya kiafya katika kujikinga na kudhibiti ugonjwa wa Corona (COVID 19); pia baada ya kuzingatia kuwa funga ya Ramadhani ni nguzo muhimu ya Uislamu, na kuwa ni kipindi muhimu sana kwa waumini kutubu kwa Mungu, toba ambayo ni nyenzo pekee ya kuondosha majanga kwa mujibu wa mafunzo ya Uislamu, Baraza la Ulamaa linatoa maelekezo yafuatayo:

1. Mwezi wa Ramadhani ni fursa adhimu kwa Waislamu kuleta toba na kufanya wingi wa Ibada.  Hivyo Misikiti iendelee kuwa wazi na waumini waendelee kutekeleza Ibada zao kwa utaratibu wa kufuata maelekezo na ushauri wa wataalamu wetu wa afya ikiwemo kunawa mikono kwa sabuni na maji tiririka, kutumia vitakasa mikono (Sanitizers), kuchukua udhu majumbani na kwenda Misikitini na miswala yao binafsi, kuacha nafasi ya angalau mita moja kati ya mtu na mtu katika swafu wakati wa kuswali na ukaaji misikitini, uvaaji wa barakoa kwa kila Muislamu aingiapo Msikitini, kuwepo msikitini kwa muda mfupi kadri inavyowezekana, kupulizia dawa Msikiti baada ya Swala, kuifungua misikiti muda mfupi kabla ya wakati wa Swala na kuifunga muda mfupi mara baada ya Swala.

Aidha pia Misikiti iandae utaratibu wa kutumia maeneo yao ya wazi kwa kuweka mahema ili kuzuia msongamano ndani ya Misikiti na kuunda kamati za usafi zinazowahusisha wataalamu wanaoswali katika Misikiti hiyo.

2. Baraza la Ulamaa linawaagiza Masheikh wa Mikoa, Wilaya na Kata na Maimamu wa Misikiti kote n chini kuhakikisha utekelezaji wa maelekezo yote yanayotolewa na wataalamu wetu wa Afya katika kujikinga na maambukizi ya CORONA (COVID 19) yanafatwa na kuhakikisha kiwango cha juu cha usafi katika Misikiti yetu, na kwamba hatua stahiki za kinidhamu zitachukuliwa kwa viongozi watakaoshindwa kutekeleza na kusimamia maagizo haya.

3. Baraza la Ulamaa linasisitiza Waislamu kutumia mwezi huu kuleta toba za kweli kwa ajili ya maslahi yao kesho Kiama na maslahi yao hapa Duniani kwani toba zikiswihi janga lolote hata liwe kubwa vipi huondoka kwa nguvu za Allah. Aidha Baraza linawataka Waislamu kuendelea kumuomba Mwenyezi Mungu kwa Dua na Qunuti kila Swala ili atunusuru na janga hili la CORONA na kwamba tuutumie mwezi Mtukufu wa Ramadhani kwa kufanya wingi wa Ibada, dua, nyiradi na kutoa Swadaka tukiwa na yakini kwamba Allah S.W.T. atatusikia, atatukubalia na atatupa sisi Watanzania na nchi yetu bali na viumbe wake wote Ulimwenguni faraja yake kutokana na janga hili.

4. Baraza la Ulamaa linawahamasisha wafanyabiashara na wenye uwezo, kote nchini kujitolea vifaa vya usafi na vifaa kinga vya COVID 19 ikiwemo mashine za upuliziaji Dawa katika Misikiti pamoja na Barakoa ili Ibada zitendeke bila mazingira hatarishi.

5. Baraza la Ulamaa linaziagiza ngazi zote kuanzia Kata, Wilaya na Mikoa kuunda kamati za kusimamia utekelezaji wa maagizo haya.  Kamati hizo zitaundwa na Sheikh, Mwenyekiti na Katibu wa kila ngazi husika kwa lengo la kuhakikisha maagizo haya yanatekelezwa.

6. Kwa Ramadhani ya mwaka huu Baraza la Ulamaa linaagiza utaratibu wa kufuturisha kwa pamoja usitishwe badala yake linawaelekeza wale wote wenye nia ya kufuturisha watu wasiokuwa na uwezo waandae futari za kubeba mikononi (Take away) au kuwapa watu chakula hicho wapike wenyewe majumbani kwao kuepuka maambukizi.

7. Baraza la Ulamaa BAKWATA Taifa limepitisha mpango wa Baraza Kuu la Waislamu wa Tanzania unaohusu taratibu za mazishi ya Waislamu wanaokufa kutokana na ugonjwa wa CORONA ili wapate haki yao ya kuzikwa kwa mujibu wa taratibu za Uislamu.  BAKWATA imefanya mazungumzo na Nyanja husika ili kushirikiana kwa pamoja kuunda kamati za maziko zisizozidi watu 7 katika kila Halmashauri kuhakikisha Muislamu anaefariki na janga hili anatekelezewa mambo yote muhimu kidini katika mazingira salama bila maambukizi.

8. Pia Baraza litatoa muongozo wa kielimu kuhusu kinga unaozingatia mtazamo wa dini na ushauri wa wataalamu wa Afya dhidi ya ugonjwa wa CORONA (COVID 19) ili Waislamu wapate mafunzo na mwongozo utakaowawezesha kujikinga na janga hili bila kigegezi.

9. Nimalizie kwa kusema Ramadhani ni mwezi wa toba hivyo kila Muislamu bali Watanzania wote, tuhakikishe tunatubu toba ya kweli huku tukimbembeleza Mungu wetu atuondolee janga hili kwa wema wake na huruma zake – Aamin.

Imewasilishwa kwa niaba ya Mufti na:-
sheikh Hassan Chizenga
Katibu Baraza la Ulama


Share:

Waziri wa Afya Ummy Mwalimu Awataka Wahudumu wa Afya Kutowakimbia Wagonjwa

Na WAMJW – Dar es Salaam
Serikali imewataka wahudumu wa afya nchini kufuata kanuni na miongozo iliyopo katika kutoa huduma kwa wagonjwa kwa kufanya hivyo wataweza kuepuka kupata maambukizi kutoka kwa wagonjwa wanaowahudumia.

Rai hiyo imetolewa jana jijini  jijini Dar es Salaam na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu wakati akipokea msaada wa vifaa vya kunawia mikono 100 vyenye ujazo wa lita 500 kutoka kwa Shirika  lisiyo la kiserikali la Water Mission Tanzania .

Waziri Ummy alisema kama mtaalamu wa afya atafuata mwongozo wa kuzuia maambukizi wa mwaka 2018  na muongozo wa uzuiaji wa maambukizi ya Virusi vinavyosababisha ugonjwa wa Corona (COVID-19) wa mwezi wa kwanza mwaka 2020 hataweza kupata maambukizi kutoka kwa mgonjwa .

“Wakati tunaendelea kukabiliana na janga la ugonjwa wa COVID -19  tukumbuke kuwa kuna magonjwa mengine kama ya moyo, kisukari, maralia, figo na ya kuambukiza ikiwemo Ukimwi na kifua kikuu.  Hivyo basi mgonjwa wa aina hii akifika katika kituo cha kutolea huduma za  afya anatakiwa kutibiwa na siyo kukimbiwa”,.

“Baadhi ya wahudumu wakimpokea mgonjwa mwenye joto kali wanamkimbia kwa kudhani kuwa  ana ugonjwa unaosababishwa na virusi vya Corona. Mwongozo wa utoaji wa huduma za afya hauwataki kuwakimbia wagonjwa jambo la muhimu ni kufuata miongozo iliyopo hii ikiwa ni pamoja na kunawa mikono, kuvaa barakoa na glovu wakati una muhudumia mgonjwa ”, alisisitiza Waziri Ummy.

Aidha, Waziri Ummy alishukuru kwa msaada uliotolewa na Shirika hilo na kuwataka wananchi kuzingatia maagizo wanayopewa na wataalamu wa afya ikiwa ni pamoja na kunawa mikono kwa maji safi yanayotiririka na sabuni pamoja na kuvaa barakoa katika kukabiliana na ugonjwa wa Corona.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkazi wa Taasisi ya Water Mission Tanzania Benjamin Filskov alisema Taasisi yake imetoa msaada huo wa vifaa vya kunawia mikono   100 ambavyo vitatumika katika vituo vya kutolea huduma za afya vilivyopo katika mkoa wa Dar es Salaam.

Filskov alisema, “Tafiti zinaonesha kuwa kama mikono itaoshwa vizuri kwa maji safi yanayotiririka na sabuni ni rahisi kuepuka kupata maambukizi ya ugonjwa wa Coron. Hivyo basi nasi tukaona ni vyema tuweze kukabiliana na ugonjwa huu kwa kutoa msaada wa  vifaa vya kunawia mikono ambavyo ni matanki 100 yenye ujazo wa lita 500 vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 124”,.

Naye Katibu Tawala wa mkoa wa Dar es Salaam  Abubakar Khunenge alisema  watahakikisha vifaa hivyo vya kunawia mikono 100 vinatumika kama ilivyokusudiwa katika kupambana na maambukizi ya COVID -19.

“Tutahakikisha vifaa hivi vinapelekea katika vituo vya kutolea huduma za afya 100 vilivyokusudiwa  na vitawekwa katika mlango wa mbele wa kuingilia katika kituo husika”, alisema Khunenge.


Share:

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Ijumaa Aprill 24



















Share:

Thursday, 23 April 2020

Infection Prevention and Control STTA for COVID-19 at Management Sciences for Health (MSH)

Infection Prevention and Control STTA for COVID-19 at Management Sciences for Health (MSH) Overview In the advent of Public Health Emergency of International Concern (PHEIC) related to COVID-19 outbreak, USAID through its Medicines, Technologies, and Pharmaceutical Services (MTaPS) program is providing technical assistance to the  Tanzania Ministry of Health, Community Development, Gender, Elderly and Children (MOHCDGEC) to support… Read More »

The post Infection Prevention and Control STTA for COVID-19 at Management Sciences for Health (MSH) appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

TAKUKURU yawaonya wanasiasa kutoa zawadi zenye harufu ya rushwa

Na Amiri kilagalila,Njombe
Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa Takukuru mkoa wa Njombe imewaonya wanasiasa walioanza kujitokeza kwa wananchi kugawa zawadi kabla ya muda wa uchaguzi na kutangaza kuto kusita kuwachukulia hatua kali za kisheria.

Akizungumza na vyombo vya habari kamanda wa TAKUKURU mkoa wa Njombe Domina Mukama wakati akitoa taarifa ya utekelezaji wa majukumu katika kipindi cha miezi mitatu ya januari hadi machi amesema kuwa tayari kuna baadhi ya wanasiasa wameanza kujitokeza kuwahonga wananchi kinyume cha sheria.

“Mwaka huu ni mwaka wa uchaguzi,nchi yetu itafanya uchaguzi mkuu mwezi Oktoba kuwachagua madiwani,Wabunge na Rais kwa mujibu wa katiba ya Nchi.Taasisi imebaini kuwa kuna baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa wanaokiuka sheria,kanunina taratibu za uchaguzi ambao wameanza kufanya kampeni za kuwashawishi wananchi kabla ya muda unaotolewa kwa mujibu wa sheria”alisea Mukama

Baadhi ya wanasiasa na viongozi wa vyama vya siasa mkoani Njombe akiwemo Edwin Mwanzinga na Alatanga Nyagawa wanakiri kuwa rushwa ina madhara makubwa katika chaguzi mbalimbali lakini wametaka TAKUKURU iangazie macho yao katika vyama vyote vya siasa badala ya kujikita na vyama vichache ili hali uchaguzi unahusisha vyama vyote.

“Sisi kwenye chama chetu cha mapinduzi unapotaka kutoa msaada hutakiwi kutoa kwa kificho,unatakiwa uwasilishe kwenye ofisi za chama upate utaratibu ukienda tofauti na hapo inatafsirika ni rushwa vinginevyo usigombee”amesema Mwanzinga

“Kweny chaguzi zipo dalili za rushwa ni vyema vyombo vya kiserikali katika kipindi hiki vikafanya kazi kikamilifu kwenye vyama vyote”alisema Alatanga

Erasto Ngole ni katibu mwenezi wa CCM mkoa wa Njombe na Rose Mayemba ni mwenyekiti wa CHADEMA mkoa ambao nao wamewaonya wanachama wao wenye nia ya kugombea kwa kuanza kukiuka kanuni kabla ya mchakato kutangazwa.

Mwezi Oktoba mwaka huu Tanzania inatarajia kuingia kwenye mchakato wa uchaguzi mkuu utakaowahusisha madiwani,wabunge na Rais


Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger