Thursday, 23 April 2020

Serikali Imetangaza Ukomo Wa Kiwango Chajuu Cha Bei Ya Sukari Kwa Reja Reja Kwa Kila Mkoa....Tazama Hapa

Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga na Waziri wa Viwanda na Bishara Mhe Innocent Bashungwa wamekutana na waandishi wa habari ili kuzungumza  na umma wa Watanzania wote kuhusiana na Hali ya sukari nchini na mwenendo wa bei yake  katika msimu huu wa uzalishaji wa sukari wa 2019/2020.

Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga ameanza kwa kueleza mahitaji na matumizi ya sukari nnchi ‘‘Mahitaji ya sukari ya matumizi ya kawaida Nchini yanakadiriwa kufikia tani 470,000 kwa Mwaka. Kiasi hiki ni kwa wastani wa mahitaji ya kiasi cha tani 38,000 kwa kila Mwezi pamoja na kiasi cha tani 14,000 kwa ajili ya dharura. 
 
Uwezo wa viwanda vyetu vya ndani kwa msimu wa 2019/20 kwa mujibu wa makadirio ya mwanzoni mwa msimu yaani Julai, 2019 ni kuzalisha takribani tani 378,000 za sukari. Kiasi hiki ni sawa na asilimia 82.9 ya mahitaji halisi ya tani 456,000 ambayo hayajumuishi kiasi cha dharura cha tani 14,000. 
 
Uwezo huu wa uzalishaji wa viwanda vya ndani unaacha pengo la kiasi cha tani 78,000 ili kuweza kutosheleza mahitaji halisi ya tani 456,000 bila kiasi cha dharura cha tani 14,000.
 
Hata hivyo, uwezo huu wa uzalishaji wa viwanda vya ndani ulitarajiwa kufikiwa pale tu panapokuwa na hali nzuri ya hewa na ufanisi mzuri wa viwanda’’

Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga ameendelea kwa changamoto ambazo zimekumba msimu wa uzalishaji sukari wa Mwaka 2019/2020
 
‘‘Kutokana na ukweli kwamba msimu wa uzalishaji sukari wa Mwaka 2019/20 umekumbwa na changamoto kadha wa kadha zikiwemo
      i.         Mvua nyingi kupita kiasi ambayo imepelekea uvunaji wa miwa kuwa mgumu,
    ii.         Mlipuko wa magonjwa ya miwa kama vile viding’ata wa njano n.k,
   iii.         Uharibifu wa mitambo ya baadhi ya viwanda na kuchelewa kupatiwa vipuri.
Sababu hizo zote kwa pamoja zimechangia kwa kiasi kikubwa Viwanda vyetu vya ndani kushindwa kufikia malengo ya kuzalisha tani 378,000 za sukari kwa msimu wa 2019/20.’’

Waziri wa Viwanda na Bishara Mhe Innocent Bashungwa ametoa hali ya uzalishaji wa viwanda vya sukari nchini:
Na.
Jina la Kiwanda
Malengo ya Uzalishaji (tani)
Kiasi kilichozalishwa (tani)
Uzalishaji (%)
1
Kilombero Sugar Co. Ltd
                    120,183
                    103,122
85.8
2
TPC Ltd
                      90,815
                      88,968
98.0
3
Kagera Sugar Ltd
                      95,000
                      79,403
83.6
4
Mtibwa Sugar Estates Ltd
                      33,513
                      20,705
61.8
5
Manyara Sugar Co. Ltd
                       5,785
                        6,750
116.7

JUMLA
                   345,296
                   298,949
86.6

‘­­­‘Kutokana na hali halisi ya uzalishaji wa ndani wa sukari kuwa pungufu ya malengo ya uzalishaji, Serikali ilifanya makadirio ya kiasi cha sukari ya kuziba pengo la uzalishaji (gap sugar) na kutoa vibali kwa wazalishaji ili kuweza kuagiza na kuingiza sukari hiyo Nchini kwa wakati kwa ajili ya kukidhi mahitaji. Hadi hivi sasa tunazungumza na nyinyi, sukari iliyoagizwa kuja kuziba pengo la uzalishaji takribani tani 10,710 imeshaingia nchini na inaendelea  kusambazwa katika Mikoa yote.
 
Mnamo tarehe 24, 28 na 30 Aprili, 2020 tunategemea kupokea jumla ya tani 13,500 za sukari ya kuziba pengo na tutaendelea kupokea kiasi kingine cha sukari Mwanzoni mwa Mwezi Mei, 2020. Kiasi chote cha sukari kilichopo Nchini na tunachoendelea kupokea kinatosheleza kabisa mahitaji ya sukari nchini. Kwa taarifa hii, tuwaombe Wananchi wote kuwa watulivu kwa sababu Nchi yetu inayo sukari ya kutosha.’’

Waziri wa Viwanda na Bishara Mhe Innocent Bashungwa amesema serikali haitakubali kuona wafanyabiashara kupandisha bei kiholela
 
‘‘Tunapenda kuwatangazia Wafanyabiashara wote Nchini wenye tabia hizi za kupandisha bei kiholela waache mara moja kwani Serikali haipo tayari kuona Wananchi wake wanaumia kwa manufaa ya watu wachache.
Serikali itachukua hatua kali kwa Mfanyabiashara yeyote ambaye atabainika kujinufaisha kwa kuuza sukari bei ya juu kulikoni bei ya kawaida ya soko.’’

Aitha, Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga kabla ya kutangaza bei ya sukari ya reja reja Katika Mikoa yote nchini amesema;
 
Kwa mujibu wa Sheria ya Sukari  Na. 26 ya Mwaka 2001(Cap. 251) chini ya kifungu cha 11A inampa Mamlaka Waziri mwenye dhamana ya Kilimo kutangaza bei ya ukomo wa juu ya sukari.
 
Kutokana na changamoto ya wafanyabiashara kupandisha kiholela bei ya sukari nchini, Serikali tumeamua kuutangazia Umma wa Watanzania bei Kikomo ya sukari katika Mikoa yote Nchini Tanzania. Bei hizi kikomo zinalenga kukabaliana na changamoto ya kupanda kiholela kwa Bei ya Sukari Nchini ambayo kwa sasa imefikia wastani wa Shilingi 4,000/= hadi 4,500/= kwa kilo. Bei hii kikomo ya sukari imepangwa kwa kuzingatia gharama zote za uagizaji wa sukari ya kuziba pengo zinazotumiwa na wazalishaji kuagiza sukari kutoka nje ya Nchi.
 
Hivyo, kwa niaba ya Serikali tunapenda kuutangazia umma wa Watanzania kuwa bei ya sukari ya reja reja Katika Mikoa yote nchini itakuwa kama ifuatavyo;

KIWANGO CHA JUU CHA BEI YA SUKARI KWA REJA REJA KWA KILA MKOA

NA.
MKOA
BEI YA  KILO (Tsh)




  1.  
IRINGA
2,900

  1.  
MBEYA
3,000

  1.  
RUKWA
3,200

  1.  
KATAVI
3,200

  1.  
RUVUMA
3,200

  1.  
NJOMBE
2,900

  1.  
LINDI
2,800

  1.  
MTWARA
2,800

  1.  
ARUSHA
2,700

  1.  
KILIMANJARO
2,700

  1.  
MANYARA
2,700

  1.  
TANGA
2,700

  1.  
DAR ES SALAAM
2,600

  1.  
PWANI
2,700

  1.  
MOROGORO
2,700

  1.  
KAGERA
3,000

  1.  
MWANZA
2,900

  1.  
SIMIYU
2,900

  1.  
SHINYANGA
2,900

  1.  
GEITA
2,900

  1.  
MARA
3,000

  1.  
KIGOMA
3,200

  1.  
SINGIDA
2,900

  1.  
TABORA
2,900

  1.  
DODOMA
2,900

  1.  
SONGWE
3,000

Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga amemaliza kwa kusisitiza kuwa;
‘‘Bei hizi za ukomo za sukari zimezingatia umbali wa kila eneo katika Mikoa yote nchini. Niwaombe Wafanyabiashara wote nchini kuzingatia maelekezo haya ya Serikali. Yeyote atakayekiuka maelekezo haya atakuwa ametenda kosa na hivyo atafikishwa katika vyombo vya sheria ili apate adhabu ambayo itahusisha ama kunyang’anywa leseni ya biashara, kulipa faini au adhabu zote kwa pamoja. Tutachukua hatua kali za kisheria kwa mfanyabiashara yeyote ambaye atakiuka masharti haya.’’


Share:

Mwongozo Wa Usafirishaji Wa Bidhaa Muhimu Na Huduma Katika Nchi Za SADC Kwa Kipindi Hiki Cha Janga La Virusi Vya Corona (Covid – 19)

Tarehe 6 Aprili, 2020 ulifanyika Mkutano wa Dharura wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC). 

Mkutano huo ulijadili janga la mlipuko wa ugonjwa wa homa kali ya mapafu (COVID-19) unaosababishwa na virusi vya Corona. Mkutano huo ulihusisha Mawaziri wenye dhamana ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Fedha,Viwanda,Biashara, Utalii, Mambo ya Ndani na Uchukuzi, kutoka nchi 16 wanachama wa SADC ambazo ni Angola, Botswana, Malawi, Mauritius, Msumbiji, Namibia, Jamhuri ya Visiwa vya Ushelisheli, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Zambia.

Katika mkutano huo, Baraza la Mawaziri lilitoa mwongozo kuhusu Usafirishaji wa Bidhaa Muhimu na Huduma Katika Nchi za SADC katika kipindi hiki cha janga la Virusi vya Corona. 

Mwongozo huu utatumika katika kipindi hiki unalenga kupunguza safari zisizo za lazima na usafirishaji wa bidhaa ambazo ni za muhimu tu na unazitaka Nchi Wanachama kuzingatia na kutekeleza sera na miongozo mbalimbali iliyotolewa na inayoendelea kutolewa na Shirika la Afya Duniani (WHO), Shirika la Forodha Duniani (WCO), Shirika la Usafiri wa Anga Duniani (ICAO) na Shirika la Usafiri wa Maji Duniani (IMO).

Kwa mujibu wa Muongozo huo Malori na magari yatakayoruhusiwa kusafirisha mizigo ni yale yatakayobeba bidhaa za Vyakula; Vifaa tiba na Dawa, vifaa binafsi vya kujikinga; Mafuta na makaa ya mawe; Pembejeo za kilimo; vifungashio, vipuri vya magari na mashine.

Raia wanaorejea katika nchi zao wanatakiwa kuzingatia sheria za nchi zilizowekwa za kupimwa na ikiwa atagundulika mgonjwa mwenye Virusi vya Corona, atatakiwa kutengwa kwa kuwekwa kizuizini kwa muda uliowekwa; Kupunguza idadi ya wasafiri katika mabasi na vyombo vingine vya usafiri; Kutumia miongozo ya WHO ya usafi katika vyombo vya usafiri, vituo vya mabasi na maeneo mengine ambayo mabasi yatasimama; Madereva/waendeshaji kutoa taarifa mbalimbali kuhusu njia za kupambana na COVID-19 kwa wasafiri katika lugha za wasafiri na; Kujaza fomu zinazohoji maeneo waliopita wasafiri na kuhakikisha fomu hizo zinawasilishwa kwa kituo cha maafisa afya.

Vyama vya wasafirishaji vinatakiwa Kushirikiana na maafisa afya kuandaa na kutekeleza programu ya uhamasishaji kwa wasafirishaji magari na waajiri wake;Kuwaelekeza madereva wa malori kujaza fomu maalum zinazoonyesha maeneo ambayo watapita, maeneo watakayosimama wakati wa safari na kituo cha mwisho cha safari ambazo zitawekwa katika ofisi za maafisa afya zilizopo mipakani ili kuweza kuwasiliana na kufuatilia madereva kwa uchunguzi;

Wasafirishaji magari wanatakiwa kushirikiana na Serikali kuangalia jinsi taarifa za gari zinavyoweza kutumika wakati wa kuifuatilia; Kuhakikisha madereva wanaovuka mipaka wanabeba sabuni na maji ya kunawa; Kuwaelekeza madereva kutobeba watu wasiohusika katika magari yao; Kuelekeza madereva wa malori kuzingatia umbali wa mita moja kati yao wakati wa safari; na; Kugawa vifaa maalum kwa wafanyakazi na waajiriwa ambao wapo katika mazingira hatarishi ya kupata maambukizi.

Madereva wa malori watalazimika kuweka bayana kituo cha mwisho cha safari yao na wanaaswa kusimama katika vituo maalum vilivyopangwa na endapo dereva au wahudumu wa chombo husika wataonesha dalili za kuugua COVID-19 lori hilo litalazimika kupitia hatua za usafishaji kabla ya kuruhusiwa kuendelea na safari, watoa huduma wa chombo hicho watengwa katika eneo maalum (Quarantine) au kupelekwa kituo cha matibabu kwa gharama zao; Mmiliki wa lori atalazimika kuandaa dereva na watoa huduma wengine ili kuwezesha bidhaa kufika mahali zilipokusudiwa.

Dereva na wasaidizi wake wakishusha mzigo watapaswa kukaa watengwa katika eneo maalum ( Quarantine) kwa siku 14 na kutofanya safari nyingine ya nje katika kipindi hicho na wataalamu wa afya waliopo mpakani mwa nchi husika watalazimika kuwasiliana kwa kina na wataalamu wa afya wa nchi mwenyeji wa lori husika ili kupata taarifa zitakazo saidia kuchukua hatua ya kuwatenga katika eneo maalum dereva na wasaidizi wake wakati wa kushusha au kupakia mzigo.

Vyombo vya usafiri wa majini kutoka nchi ambazo zipo hatarini zaidi katika maambukizi au zenye wasaidizi au abiria waliopo kwenye hali hatarishi zaidi ya maambukizi watalazimika kutengwa katika eneo maalum kwa siku 14 kwa gharama zao kabla ya kuruhusiwa kutoka eneo ambalo chombo hicho kilitia nanga na chombo kilichobeba abiria na wasaidizi walioathirika na COVID-19 hakitaruhusiwa kutia nanga.

Ndege zinazofanya safari katika maeneo mbalimbali zitalazimika kufuata hatua zote za usafishaji kwa kupuliziwa dawa na hatua zingine za kujikinga ambazo kila ndege iliyobeba abiria walioathirika au washukiwa wa COVID 19 inapaswa kuzipitia.

SADC ilikubaliana kuwa hakutakuwa na zuio dhidi ya wasafirishaji wa nje waliosajiliwa la kuingia nchi mwanachama endapo wanaendesha shughuli zao kwa kuzingatia taratibu, kanuni na sera za usalama za nchi husika.

Imetolewa na:
 Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali
WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI


Share:

Picha : MWILI WA ASKOFU GETRUDE RWAKATARE WAZIKWA KANISANI KWAKE MIKOCHENI B DAR


Jeneza lenye mwili wa Askofu na mbunge wa Viti maalum CCM Mkoa wa Morogoro mama Getrude Rwakatare likiwa tayari kuingizwa kaburini huku likiwa limefunikwa bendera ya bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati wa mazishi yaliyofanyika kwenye kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni B jijini Dar es salaam leo.

***************
Aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Morogoro na Kiongozi wa Kanisa la Mikocheni B Assembly of God (Mlima wa Moto), Mama Getrude Rwakatare leo Alhamis Aprili 23,2020 amepumzishwa kwenye nyumba yake ya milele katika Kanisa lake lililopo Mikocheni B.

Waombolezaji waliouhudhuria ni wachache wakiwemo wawakilishi wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na baadhi ya ndungu kuepuka msongamano kutokana na kusambaa kwa maambukizi ya Virusi vya Corona.
Baadhi ya Waombolezaji wachache wakiwa katika mazishi ya aliyekuwa Askofu na mbunge wa Viti Maalum CCM Mkoa wa Morogoro Mama Getrude Rwakatare yaliyofanyika kwenye kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni B jijini Dar es Salaam leo.
 
Share:

Tanzania government postpones 2020 Form Six exams indefinitely

Tanzania government postpones 2020 Form Six exams indefinitely   Tanzania’s ministry of education has postponed the Advanced Certificate for Secondary Examinations Education until further notice due to the outbreak of the novel coronavirus. Permanent Secretary, Dr Leonard Akwilapo on April 22, 2020 responded to questions from parents and form six students about their fate over final exams that… Read More »

The post Tanzania government postpones 2020 Form Six exams indefinitely appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema Azungumzia Taarifa za Wagonjwa wa Corona Kutoroka Hospitali ya Amana

Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema amethibitisha kutokea kwa vurugu za wagonjwa waliowekwa katika uangalizi wa maambukizi ya corona katika Hospitali ya Amana wakitaka kutoroka hospitalini hapo na kurejea nyumbani.

Leo asubuhi katika mitandao ya kijamii, ilisambaa sauti ikielezea wagonjwa katika Hospitali ya Amana ambayo ndiyo kituo cha wagonjwa wenye maambukizi ya virusi vya corona wametoroka na wengine kupanda daladala hali iliyozua hofu katika jamii.

Wagonjwa hao wanadaiwa kutoroka hospitalini hapo leo Alhamisi Aprili 23, wakidai kuna msongamano wa wagonjwa wengi huku kukiwa hakuna dawa wala chakula na wao wanaendelea vizuri lakini hawaruhusiwi kurejea nyumbani.

Akitoa ufafanuzi wakati akihojiwa na Kituo cha Televisheni cha ITV, Mjema amesema si wametoroka ila walikuwa wamechoka hawataki kuendelea kukaa hospitalini hapo.

“Kuna wagonjwa walikuwa wamefika pale wakasema wao hawaumwi sana kwa hiyo walikuwa wanataka waruhusiwe, sasa ukifika pale kama una dalili za maambukizi ya corona lazima ukae kwanza uangaliwe, sasa wao hawataki wanataka waruhusiwe walikuwa wanapiga kelele wanataka kuondoka.

“Walikuwa wanasema wanataka kuondoka tufuatilie kwa maaskari wanaolinda hapo. Kama wametoroka kubwa ni kuwafuatilia maana wanajulikana wanapotoka ili wasiende kueneza ugonjwa sehemu nyingine, ni kuwaambia tu wafuatilie maelekezo ya hospitali kwa wale watakaoonekana wagonjwa na watakaokuwa na nafuu waruhusiwe.

“Kama mtu ana viashiria au ana dalili za corona, ana wasiwasi wa kujiona ni mzima. Mimi nawashauri wasiwe wanaamini mambo yanayosemeka huko, wasikilize serikali inavyosema kufanya vurugu sioni kama inasaidia maana kama mtu ana viashiria aende mtaani hata huko mtaani hawakutaki, tunataka tuwaelimishe kwamba wanapoletwa pale si jela ila wanawaangaliwa na kutibiwa kama wameambukizwa,” amesema Mjema.

==>>Msikilize hapo chini


Share:

Temporary Jobs at Bahi District Dodoma Tanzania (NEC Jobs April, 2020)

Temporary Jobs at Bahi District Dodoma Tanzania (NEC Jobs April 2020)   OVERVIEW: In accordance with Section 7A (4) of the National Electoral Law, Chapter 343 and Section 10 (6) of the Local Government Elections Act, Chapter 292, reads as well as Rule 9 of the Rules for Improving the Permanent Register of Voters Polls, Presidential and Parliamentary… Read More »

The post Temporary Jobs at Bahi District Dodoma Tanzania (NEC Jobs April, 2020) appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

32 National Electoral Commission (NEC) Temporary Jobs Songea

The National Electoral Commission is the national election commission of Tanzania.  Songea is the capital of Ruvuma Region in southwestern Tanzania. It is located along the A19 road. The city has a population of approximately 203,309, and it is the seat of the Roman Catholic Archdiocese of Songea.   Deadline: 26th April, 2020

The post 32 National Electoral Commission (NEC) Temporary Jobs Songea appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

32 NEC Employment opportunities at Songea District (Temporary Jobs)

32 NEC Employment opportunities at Songea District (Temporary Jobs) BVR Kit Operators nafasi 16 Waandishi Wasaidizi nafasi 16 X

The post 32 NEC Employment opportunities at Songea District (Temporary Jobs) appeared first on Udahiliportal.com.

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger