Thursday, 23 April 2020

PAKA WAAMBUKIZWA CORONA NYUMBANI

Picha ya maktaba ya paka akiwa katika kliniki ya wanyama

Paka wawili wamekutwa na virusi vya corona katika jimbo la New York , wanyama wa kwanza wa kufugwa nchini Marekani kukutwa na maambukizi, maafisa wameeleza.

Wanyama hao ambao wanaishi kwenye maeneo tofauti ya New York , wote walikuwa na dalili za wastani za kushindwa kupumua lakini wanatarajiwa kupona.

Wanasayansi wanafikiri kuwa hakuna uwezekano wa mnyama kumuambukiza binadamu virusi vya corona.

Awali, simba saba na chui katika bustani ya wanyama ya Bronx walikutwa na virusi vya corona.

Idara ya kilimo ya Marekani (USDA) na kituo cha kudhibiti na kuzuia magonjwa (CDC) zilitangaza taarifa kuhusu paka hao siku ya Jumatano.

Mmoja kati ya paka hao alipimwa na kuonesha dalili za homa ya mapafu baada ya mmiliki wake kukutwa na maambukizi.

Mmiliki wa paka wa pili hajapimwa virusi vya corona.

Kumekuwa na idadi ndogo ya wanyama waliotengwa kutokana na kupata maambukizi ya virusi vya corona nchini Marekani.

Hakuna wanyama ambao waliokuwa na maambukizi ya virusi ambao waliumwa sana. Wanasayansi wanafanya uchunguzi kuhusu sababu ya hali hiyo.

Kituo cha kupambana na kudhibiti magonjwa kimesema kuwa wamiliki wa wanyama hawa wa kufugwa nyumbani wawaache wanyama hawa kuchangamana na watu au wanyama wengine nje ya nyumba wanamoishi.
Chanzo- BBC
Share:

Child & Youth Development Officer Jobs at SOS Children’s Villages Tanzania

Job Title: Child & Youth Development Officer The main responsibility: The Child and Youth Development Officer is responsible for guiding SOS Youth (within the Village) towards independence, so that they may eventually become self-sufficient, contributing members of society. In achieving this, the Child and Youth Development Officer should be seen as a peer and a role model providing guidance,… Read More »

The post Child & Youth Development Officer Jobs at SOS Children’s Villages Tanzania appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Human Resource Manager Job vacancy at Fabec Investment LTD

Human Resource Manager  HUMAN RESOURCE MANAGER Employer: Fabec Investment LTD LOCATION: GEITA (GGM) Date Published: 22/04/2020 Application Deadline: 05/05/2020 QUALIFICATION AND EXPERIENCE: Bachelor degree in Human resource from any recognized institution with working experience of at least 3 years and Must also be computer literate and fluent in English and Swahili languages. Managerial experience with strong leadership skills… Read More »

The post Human Resource Manager Job vacancy at Fabec Investment LTD appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Assistant Project Manager at Exim Bank Tanzania

Job Position: Assistant Project Manager Job Purpose: To partner with key business stakeholders and multiple external vendors to ensure successful initiation and completion of Change Projects in line with the approved project baselines. In this role, the Assistant Project Manager will plan, coordinate, and monitor medium to large-scale projects with high degree of complexity and risk. Qualities: Self-driven… Read More »

The post Assistant Project Manager at Exim Bank Tanzania appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

CRDB Tenders: Supply Of Branded Staff Uniforms For CRDB Banks Staff, April 2020

Supply Of Branded Staff Uniforms For CRDB Banks Staff EXPRESSION OF INTEREST (EOI) FOR SUPPLY OF BRANDED STAFF UNIFORMS FOR CRDB BANKS STAFF FOR THE YEAR 2020/2021 CRDB Bank Pic is an African bank and a leading Financial Services Provider in Tanzania with current presence in Tanzania and Burundi, East Africa.The Bank was established in 1996 and was… Read More »

The post CRDB Tenders: Supply Of Branded Staff Uniforms For CRDB Banks Staff, April 2020 appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Program Officer Job vacancy at SHIVYAWATA

Program Officer Job vacancy at SHIVYAWATA Program Officer Job Description Main Purpose of Role: The Kukuza Uwezo project is currently recruiting for the position of Program Officer for the implementation of a capacity building project which focuses on strengthening key capabilities of DPOs and increasing DPO capacity to respond to needs and rights of people with disabilities (PWDs),… Read More »

The post Program Officer Job vacancy at SHIVYAWATA appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

MAGUFULI : WAPO WENGINE WANATOA MAWAZO YA KUIFUNGA DAR ES SALAAM,HILI HALIWEZEKANI

Rais John Magufuli amewatoa hofu Watanzania kwa kusisitiza kuwa: ''Kila anayekufa sio mgonjwa wa corona''

Katika hotuba yake iliyopeperushwa mubashara jana na vyombo vya habari nchini Rais Magufuli ameongeza kuwa Watanzania wengi wanatakiwa kuhamasishwa kuhusu ugonjwa corona.

Idadi ya watu walioambukizwa virusi vya corona nchini Tanzania imefikia 284.

Wito wa kutaka serikali kuweka marufuku ya usafiri ili kukabiliana na kuenea kwa maambukizi ya virusi vya corona umekuwa ukitolewa na baadhi ya watu nchi humo.

Lakini akiangazia suala la kuweka marufuku ya kutotoka nje yaani ''Lockdown'' Rais Magufuli alisema: "Wapo wengine wanatoa mawazo ya kuifunga Dar es Salaam, hili haliwezekani. Dar es salam ndio centre pekee ambapo collection ya revenue inapatikana kwa nchi yetu"

Zaidi ya asilimia 80 ya mapato yanakusanywa Dar es Salaam.

Dar es Salaam ni jiji la watu milioni 6, hivyo kitakwimu tu lazima wawe na wagonjwa wengi zaidi.

Rais Magufuli pia ametoa wito kwa wa nchi zote za Afrika kuungana kuziomba taasisi za kifedha ikiwemo Benki ya Dunia kutoa msamaha wa madeni badala ya kutaka kukopesha madeni mengine.

"Niziombe taasisi za Fedha Duniani kwasisi nchi maskini badala ya kutoa unafuu wa Mikopo kwa ajili ya kupambana na Corona watufutie baadhi ya madeni au kupunguza riba katika mikopo tunayolipa kusudi mapato tunayopata yakapambane na corona na si kulipa madeni"

Alitaja Benki ya dunia ambayo imeguswa na janga la corona kusaidia mataifa ya Afrika kwa kusamehe madeni japo kwa asilimia kidogo ili fedha zinazolipwa na mataifa hayo na pamoja na riba wanazolipa katika fedha walizokopa zitumike kupambana na corona.

Baadhi ya Watanzania wakiwemo viongozi wa upinzani wamekuwa wakiitaka serikali kutangaza marufuku ya usafiri wa watu baina ya jiji la Dar es Salaam na sehemu zengine za nchi.

''Nawapongeza wanasiasa kwa kuonesha moyo wa mshikamano kuhusu ugonjwa huu'' alisema Bw. Magufuli.Dar es Salaam inaongoza kwa kasi ya maambukizi nchini humo, kiongozi wa chama cha upinzani ACT Zitto Kabwe ameileza BBC hivi karibuni kuwa kama Dar es Salaam haitafungiwa basi kasi ya maambukizi kwa mikoa mingine ya nchi hiyo itakuwa kwa kasi.
Chanzo- BBC
Share:

Bunge Limeridhia Na Kupitisha Zaidi Ya Tsh.bilioni 40 Kwa Wizara Ya Habari,sanaa ,utamaduni Na Michezo Kwa Mwaka Wa Fedha 2020/2021

Na.Faustine Gimu Galafoni ,Dodoma.
Katika  kutekeleza majukumu ya Wizara kwa mwaka 2020/21 Bunge limeridhia  na kuidhinisha Bajeti ya Wizara ya Habari ,Sanaa,Utamaduni na Michezo  kwa mwaka 2020/21 ya jumla ya Shilingi Bilioni Arobaini, Milioni Mia Moja Arobaini, Mia Sita Arobaini na Moja Elfu (Sh. 40,140,641,000).

Akiwasilisha  hotuba ya Madirio na Matumizi  ya Wizara hiyo kwa Mwaka 2020/2021      Bungeni jijini Dodoma leo April 22,2020 Waziri Wa Habari,Sanaa ,Utamaduni na Michezo Dkt.Harrison Mwakyembe  amesema Kati ya fedha hizo Mishahara ni Shilingi Bilioni Ishirini, Milioni Mia Tisa Sabini na Tisa, Mia Mbili Thelathini na Moja Elfu (Sh. 20,979,231,000), Matumizi Mengineyo ni Shilingi Bilioni Kumi na Moja, Milioni Mia Nne Arobaini na Sita, Mia Nne na Kumi Elfu (Sh. 11,446,410,000) na Miradi ya Maendeleo ni Shilingi Bilioni Saba, Milioni Mia Saba Kumi na Tano (Sh. 7,715,000,000).

Aidha,Dkt Mwakyembe amesema kwa Mwaka  wa fedha 2020/21 Wizara inatarajia kukusanya jumla ya Shilingi Milioni Mia Tisa Sitini (Sh. 960,000,000) kupitia Idara ya Habari-MAELEZO na Maendeleo ya Michezo.

Katika kuendelea kuhifadhi na kudumisha Utamaduni wa Mtanzania,Waziri Mwakyembe amesema , Wizara imefanya utafiti wa awali wa maktabani wa lugha ambazo zipo katika hatari ya kupotea ambapo ametaja lugha hizo kuwa  ni Kizaramo, Kisegeju, Kividunda na Kiburunge kutokana na kupungua kwa idadi ya wazungumzaji wa lugha hizo.

Kuhusu Chuo cha Maendeleo ya Michezo Malya Dkt.Mwakyembe  amesema kimeendelea kutoa mafunzo ya muda mfupi na muda mrefu kwa ajili ya kuwapatia wadau mbalimbali wa michezo ujuzi wa kufundisha michezo ambapo Katika kipindi cha Mwezi Julai, 2019 hadi Machi, 2020 chuo kimetoa mafunzo ya muda mfupi kwa washiriki takribani 203 kwenye mikoa ya  Njombe (wilaya ya Wangingombe washirki 83), Rukwa (wilaya ya Kalambo washiriki 48) na Mwanza (Wilaya ya Kwimba washriki 72).

Aidha, Katika kipindi cha Julai, 2019 hadi Februari, 2020 jumla ya wanafunzi 110 walidahiliwa katika Chuo hicho kwa ajili ya mafunzo ya muda mrefu (Stashahada).

Katika Taasisi ya Sanaa na Utamaduni[TaSUBa] Waziri Mwakyembe amesema imeendelea kuongeza udahili wa wanafunzi kutoka 235 mwaka wa masomo 2018/19 hadi kufikia 411 mwaka wa masomo 2019/20 (ongezeko la 75%).

Aidha, katika mwaka wa masomo 2019/20 Taasisi imetoa ufadhili kwa Watanzania wa kike wapatao kumi (10) ambapo Ufadhili huu ni wa awamu tatu, ambapo awamu ya mwisho ni mwaka wa masomo 2020/21, na  Taasisi itafanya tathmini ya endapo malengo ya kuanzishwa kwa utaratibu huu
yamefikiwa.

Akiwasilisha  Hotuba Ya Kamati Ya Kudumu Ya Bunge Ya Huduma Na Maendeleo Ya Jamii  Kuhusu Utekelezaji Wa Majukumu Ya Wizara Ya Habari ,Utamaduni, Sanaa na Michezo Kwa Mwaka Wa Fedha 2019/2020 Pamoja na Maoni Ya Kamati Kuhusu Makadirio Ya Mapato na Matumizi Ya Wizara Hiyo Kwa Mwaka Wa Fedha 2020/2021 Mwenyekiti wa   Kamati  hiyo   Mhe.Peter  Joseph Serukamba  ameishauri serikali Kuongeza Bajeti Ya  Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo [TASUBA] Ili  kukarabati Miundombinu Yake Ambayo Ipo Kwenye Hatari Ya Kuharibika Zaidi Kutokana na Mawimbi Ya Bahari  pamoja na  Kuongeza bajeti ya  Baraza la Kiswahili Tanzania[BAKITA ]Ili Iweze Kujiandaa Katika Kutoa Huduma mbalimbali Kama Ukalimani na Tafsiri Mbalimbali.


Share:

JBS Fuel Company Yatoa Msaada Kwa Watoto Wenye Ualbino Busega Kukabili Corona

Na Stella Kalinga, Simiyu RS
Mkurugenzi wa Kampuni ya JBS Fuel Company Limited ya Mjini Bariadi, Bi. Lucy Sabu ametoa msaada chakula na vifaa mbalimbali vya kujikinga na maambukizi ya virusi vya Corona, katika kituo cha kulelea watoto wenye mahitaji maalumu cha Bikira Maria kilichopo Lamadi wilayani Busega.

Akizungumza wakati wa kukabidhi msaada huo Bi. Sabu  amevitaja vifaa hivyo kuwa ni pamoja na Vitakasa mikono, sabuni za maji, ndoo kwa ajili ya maji ya kunawia mikono, mahindi na sukari vyote vikiwa na thamani ya shilingi milioni mbili (2,000,000/=).

Amesema wito uliotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli wa maombi ya siku ya tatu umemsukuma kutoa msaada huo kwani ameona ipo haja ya kuwasaidia wahitaji katika kipindi hiki cha Janga la Corona na kutoa wito kwa Watanzania kuendelea kuchukua tahadhari na kufuata maelekezo ya wataalam wa afya.

"Namshukuru sana Mhe. Rais kwa maono yake kwa Watanzania kufanya maombi ya siku tatu kumuomba Mungu atuepushe na Janga la Corona, maombi haya yamenikumbusha kuwakirimu wahitaji na ndiyo maana nimeguswa kufika katika kituo hiki; nitoe wito kwa Watanzania wote kuwakumbuka wahitaji katika kipindi hiki cha Janga la Corona," alisema Bi Lucy Sabu.

Akipokea msaada huo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka, Mkuu wa Wilaya ya Busega Mhe. Tano Mwera amemshukuru Bi. Lucy Sabu kwa namna alivyoguswa kusaidia kituo hicho huku akiendelea kusisitiza wananchi kuchukua tahadhari na kumwelekeza Mkurugenzi wa kituo kuwa makini kudhibiti watu wanaoingia kituoni hapo ili kuwalinda watoto.

Naye Mratibu wa mapambano dhidi ya maambukizi ya Virusi vya Corona Mkoani Simiyu, Dkt. Khamis Kulemba ameutaka Uongozi wa kituo hicho kuongeza maeneo ya watoto kunawa mikono pamoja na kuwasisitiza kunawa mara kwa mara.

Mkurugenzi wa kituo cha Bikira Maria, Sister Helena Ntambulwa amemshukuru Bi. Lucy Sabu kwa msaada aliotoa na kuwashukuru viongozi wa Wilaya ya Busega na Mkoa wa Simiyu kwa namna wanavyokisaidia kituo hicho chenye jumla ya watoto 71 ambao wanatoka maeneo  mbalimbali ya Tanzania wakiwemo waliopoteza wazazi na waliotelekezwa.

Kwa upande wake Mjumbe wa Bodi ya wadhamini ya Kituo hicho, Bw. Belensi China amesema kituo hicho kinakabiliwa na changamoto mbalimbali, ikiwa ni pamoja na upungufu wa fedha za kulipa matibabu ya watoto na mishahara ya wafanyakazi; hivyo amewaomba Watanzania wenye mapenzi mema kuendelea kuwasaidia watoto hao wenye mahitaji maalum.


Share:

Wanahabari Rukwa watakiwa kuwa makini kujikinga na Corona ili kuendelea kuihabarisha jamii

Mkuu wa mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo amewataka wanahabari Mkoani humo kuhakikisha wanajikinga kwa namna yoyote ile ikiwemo kufuata maelekezo ya wataalamu kwa kuvaa barakoa pamoja na kunawa mikono yao kwa maji tiririka na sabuni kwani kazi zao zinahusisha kukutana na watu katika kutafuta habari mbalimbali zinazohusiana na Corona na habari nyinginezo katika kijamii.

Amesema kuwa mara kadhaa amekuwa akiwashuhudia wakitumia kipaza sauti kimoja wakati wa kuwahoji watu na hutumia kipaza sauti hicho kuripoti habari kwenye vyombo vyao, hivyo amewataka kuwa makini zaidi na kuongeza kuwa kutokana na uwezo mdogo wa waandishi hao kujikimu kuwa na vifaa vya kujikinga, ametoa wito kwa mashirika ya serikali na yasiyo ya kiserikali kuona umuhimu wa kuwawezesha wanahabari ili wafanye kazi zao kwa usalama.

“Muwe makini sana, vinginevyo maambukizi yatawapata sana, kwasababu ugonjwa huu hauchagui, hauna Mwanahabari, hauna Mkuu wa Mkoa, hauna DC(Mkuu wa Wilaya), hauna Waziri, hauna mtu yeyote yule, isipokuwa unapenya kwa mtu ambaye hajachukua tahadhari, na tahadhari mojawapo ni kuvaa barakoa, Wanahabari vaeni Barakoa kila mahali, mjilinde, nafahamu wanahabari wa Rukwa uwezo ni mdogo hivyo nitoe wito kwa amashirika ya ndani na nje ya nchi, tutaanzia na ofisi yangu hapa ya mkoa, Katibu Tawala utafute hata boksi mbili, tatu tuwape wanahabari ili wajilinde,”Alisema.

Aidha, Mh. Wangabo amemuagiza Katibu Tawala wa Mkoa kuhakikisha kuwa Taasisi zote ndani ya Mkoa zinakuwa na Vipima joto (Thermal Scanner) na kuongeza kuwa Mkoa umesambaza vifaa vya kujikinga (Personal Protective Equipment – PPE) 139 katika halmashauri nne za mkoa pamoja na kusambaza vipeperushi 12,200 vya kutolea elimu kwa jamii juu ya ugonjwa wa Corona.

Mh. Wangabo ameyasema hayo katika semina fupi iliyowakutanisha waandishi wa Habari katika Mkoa wa Rukwa na wataalamu wa afya ngazi ya mkoa pamoja na wadau wa mradi wa Lishe Endelevu unaosimamiwa na Shirika la Save the Children ambapo katika semina hiyo waandishi walipata kuelewa aina tofauti za barakoa na utendaji kazi wake, Elimu ya Lishe ya mtoto katika kipindi hiki ambacho ugonjwa wa Corona umekuwa tishio pamoja na njia za kufuata wanapotafuta habari kuanzia ngazi ya halmashauri, Wilaya na mkoa.

Kwa upande wake Kaimu Afisa Lishe wa mkoa Teddy Swallo alitoa ufafanuzi juu ya namna ya kuendeleza lishe yam toto kutoka kwa mama endapo mmoja kati yao atakuwa ameambukizwa ugonjwa wa Corona na kusisitiza kuwa mtoto hatakiwi kuachishwa kunyonya kwasababu ya maambukizi na kusisitiza kuwa mama na walezi wa mtoto wanawe kabla na baada ya kumshika mtoto na wavae barakoa wakati wa kumhudumia mtoto.

“Kuna maswali yanayoulizwa mara kwa mara kuhusiana na unyonyeshaji na ugonjwa Covid – 19, swali, virusi vya Corona vinapatikana kwenye maziwa ya mama? jibu ni kwamba hadi sasa tafiti zinaonyesha kuwa virusi vya corona havipatikani kwenye maziwa ya mama, swali, mtoto aliyepata Covid-19 ataendelea kunyonyeshwa? Jibu ni ndio ataendelea kunyonyeshwa ili aweze kupata king ana virutubishi muhimu kutoka kwenye maziwa ya mama yake na muhimu mtoto anayeumwa anyonye mara nyingi zaidi ya kawaida,” Alisisitiza.

Halikadahalika, Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa Dkt. Emanuel Mtika wakati akijibu swali kuhusu dawa inayosemekana inatibu Corona ya kuchanganya malimao na tangawizi alisema kuwa, mchanganyiko huo utamsaidia mtumiaji kusafisha na kuimarisha kinywa chake lakini sio kujitibu ugonjwa wa Corona na kusisitiza wale wanaojisikia dalili za mafua makali waharakishe kufika katika vituo vya kutolea huduma na sio kubaki nyumbani wakitegemea ugonjwa huo utapona wenyewe.

Katika kuhakikisha elimu ya ugonjwa wa Corona inawafikia wananchi Mh. Wangabo ameshafanya vikao na viongozi wa makundi mbalimbali ya jamii, kuwaelimisha na kutoa maelekezo kwa viongozi wa kata za mwamabo wa Ziwa Tanganyika zenye bandari bubu 57, na kuunda timu za wataalamu kutoka katika sekta mbalimbali 11 kuanzia ngazi ya mkoa hadi halmashauri pamoja na kusimamia uandaaji wa mpango wa dharura wa kukabiliana na Corona uitwao Regional Covid -19 Contingency Plan ulioanza utekelezaji wake mwezi Machi mwaka huu.


Share:

Malkia Elizabeth II Wa Uingereza afuta mpango wa kusherehekea siku yake ya kuzaliwa

Tarehe 21 Aprili ilikuwa siku ya kutimiza umri wa miaka 94 kwa Malkia Elizabeth II. 

Kwa kawaida mtawala wa Uingereza anasherehekewa siku ya kuzaliwa mara mbili kila mwaka. 

Moja ni siku yake halisi ya kuzaliwa, na nyingine ni siku ya kusherehekea kuzaliwa kwa Malkia iliyowekwa na serikali.

Kutokana na hali mbaya ya maambukizi ya virusi vya Corona, malkia Elizabeth ameamua kufuta sherehe za kutoa heshima ya mizinga mwaka huu.


Share:

DC Atoa Siku Saba Kwa Mhandisi Wa Jiji La Arusha Kuweka Maji Kwenye Jengo La Kituo Cha Afya Muriet

Na Ahmed Mahmoud Arusha
Mkuu wa wilaya  Arusha Gabriel  Daqarro ametoa siku saba kwa kaimu mhandisi  wa halmashauri ya jiji la Arusha Samwel mshuza    kuweka maji katika jengo la upasuaji  lililopo katika kituo cha afya  Cha Muriet ili kuanza shughuli za upasuaji.
 
Akizungumza katika siku ya pili ya ziara yake alipotembelea kituo hicho  katika kukagua ujenzi wa njia yakutembea kwa miguu inayounganisha majengo yote uliokamilika tarehe 4 March  mwaka huu wenye ghara a ya shilingi milion 100  .
 
Mkuu huyo amesema kuwa anatoa siku saba kwa mhandisi huyo kwani maji ni  sehemu kubwa ya kukwamisha  wananchi kupata huduma ya upasuaji pamoja na shughuli nyingine ndani ya majengo hayo.
 
Akiwa katika shule ya sekondari Taret mkuu huyo  amesema kuwa kabla ya mwaka wa fedha kuisha  majengo hayo  yawe tamekamilika  ili kuanza mwaka mwingine wa fedha isiokuwa na Madeni ya nyuma.
 
” Haitaleta maana nzuri kuona tunaanza  mwaka mwingine tukiwa na Madeni na kutokukamilisha  baadhi ya majengo tunatakiwa kuanza mwaka na miradi mingine sio ya viporo”. Alisema daqqaro
 
Hata hivyo mkurugenzi wa  jiji  Hilo Maulid Madeni amesema kuwa jiji limesimamisha shughuli zote za kawaida ili kuweza kukamilisha majengo yote .
 
” Mheshimiwa mkuu wa wilaya tunatambua wewe ni msaidizi wa Rais ndani ya eneo Hilo naomba nikuahidi jengo hili  ndani yasiku 30 litakuwa limekamilika”.
 
Akizungumza mmoja wa wananchi wa eneo Hilo Abdala maguta amesema kuwa wanaishukuru  serikali  kwa kuendelea kuboresha sekta ya elimu na kuwarahisishia wanafunzi wengi kutokwenda mashule ya mbali .


Share:

Habari Zilizopo Katika Magaxeti ya Leo Alhamisi April 23


















Share:

Wednesday, 22 April 2020

Mambo 13 MUHIMU Aliyoyaongelea Rais Magufuli Leo Kuhusu Mapambano Dhidi ya Corona


Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, amesema kuwa haitatokea hata siku moja Mkoa wa Dar es Salaam, ukafungwa kutokana na maambukizi ya Virusi vya Corona, kwa kuwa ndiyo kitovu cha mapato ya Taifa.

Hayo ameyabainisha leo Aprili 22, 2020, wakati akizungumza na viongozi mbalimbali wa vyombo vya ulinzi na usalama wa nchi, Ikulu ndogo ya Chato mkoani Geita 


==>>Hapo chini ni Baadhi ya Mambo Muhimu aliyoyasema leo

“Nawapongeza viongozi wa Dini na watanzania kwa ujumla kwa kuitikia wito wa kuliombea taifa kwa siku 3 dhidi ya ugonjwa wa COVID-19, nina amini Mungu wetu ni wahuruma atatusikiliza na siku moja tutalishinda hili gonjwa

“Navipongeza vyombo vya ulinzi na usalama kwa kuchukua hatua mbalimbali za kuilinda nchi yetu hasa katika kipindi hiki cha mapambano dhidi ya COVID-19, nimekubaliana na hatua mnazoendelea kuzichukua katika kipindi hiki

"Wananchi tuondoe hofu, hofu ni ugonjwa mkubwa kuliko Corona. Niwaombe watu wa mitandao, waache kupotosha kuhusu ugonjwa huu na wananchi pia nawaomba wawapuuze hawa wanaopotosha. IGP upo hapa kawashughulikie hao, ndiyo saizi yako

"Wengine wanatoa mawazo ya kuifunga DSM, hili haliwezekani hii ndiyo center pekee ya mapato, tuendelee kuchukua hatua lakini si ku-lockdown DSM never, kwahiyo ufungie watu Mil.6 ikitokea Mwanza na yenyewe tuifungie, tutafungia watu wangapi

“Hauwezi kuua corona kwa kupuliza dawa kwenye mabasi na mitaani ile unaua mende na wadudu wengine, ila hatujiulizi kwamba labda kupuliza ndio tunaongeza corona, maana DSM imepulizwa dawa tu na kasi ya wagonjwa imeongezeka.

“Baadhi ya Watanzania wanajishonea wenyewe mask, shona mask yako tumia badala ya kutegemea unazouziwa na hujui wanaouza wana dhamira gani?, viwanda vyetu navyo vianze kutengeneza mask, hizi mask za nje narudia tunaweza kuambukizwa corona kwa mask kutoka nje

“Kuna tunaowaweka katarantini ‘Hosteli za Magufuli’ liangaliwe upya hakuna sababu ya Mtu unamuweka pale anakaa siku 14 wakati unamuona hana tatizo, tushughulike na wagonjwa, badala ya kuwakalisha muda mrefu pale wakati hata mtaani atakuta wanaoumwa, tunapoteza rasilimali
 
"Benki ya Dunia najua wametoa ofa ya nchi zinazosumbuliwa na Corona kukopa pesa, badala ya kukopesha tena, wasamehe madeni kwa nchi hizi, mfano sisi huwa tunalipa karibu Bil 700, watusamehe ili hizi pesa zikatumike kupambana na hili janga


"Nimemteua Katibu Mkuu mpya ili atoe pia na taarifa za wanaopona, sio kwamba ukipata ugonjwa lazima ufe, tuwaondolee hofu wananchi

"Tuanze kushughulikia hata vitu tunavyoletewa kama zawadi visije kutuletea madhara, unapopewa mask lazima ujue aliyetengeneza, aliyesambaza na misingi ya kutuletea tusije kujikuta tunaambukizwa corona kutoka kwenye mask zinazotoka nje
 
“Tutangaze pia na wanaopona sio wanaokufa tu, inawapa Watu hofu kwamba ukipata corona lazima ufe, kwani Maralia haiui?, na nimegundua baadhi ya wanaopotosha kwenye mitandao wengine sio Watanzania, namba zao ziko nyingine kwenye Nchi za jirani wanawachafua tu Watanzania

“DSM, na Mwanza niliona mabasi yanapulizwa dawa na hasa DSM, hakuna upuliziaji dawa unaoweza kuua corona, ingekuwa pakipulizwa corona wanakufa, Nchi zinazoendelea wangemwagia Nchi zao kwa Ndege na wasingekuwa wanakufa, kule kupuliza dawa ni upuuzi tu

 


Share:

LIVE: Rais Magufuli Anahutubia Taifa Muda Huu Kuhusu Corona

Live: Rais Magufuli Anahutubia Taifa Muda Huu Kuhusu Corona


Share:

Rais Magufuli Kuzungumza na Viongozi wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama kuhusu hali ya ugonjwa wa Corona Kuanzia Saa Tisa dk 45

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli atazungumza na Viongozi wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama kuhusu hali ya ugonjwa wa Corona. 

Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais-IKULU Gerson Msigwa imesema matangazo ya kikao hicho yatarushwa mubashara kutoka Chato Mkoani Geita kuanzia saa 9:45 alasiri leo Aprili 22, 2020.


Share:

Taarifa Kwa Umma: Ewura Yatoa Ufafanuzi Kuhusu Kushuka Bei Za Mafuta

Katika siku za hivi karibuni, kumekuwepo na taarifa katika mitandao ya kijamii kuhusu kushuka kwa bei ya mafuta ghafi nchini Marekani, hali iliyosababisha watu kuanza kuhoji kwanini bei za mafuta hapa nchini hazishuki kwa kiwango kinachoonekana kushuka katika soko la Marekani. 
 
Ufafanuzi ni kwamba; bei za mafuta nchini Marekani zinazotangazwa kupungua kwa kiwango kikubwa ni zile za mafuta ghafi (crude oil) na siyo mafuta yaliyosafishwa (refined petroleum products). Punguzo hili la bei linatokana na kukosa mahali pa kuhifadhia mafuta hayo nchini Marekani. 
 
Ni vyema ikafahamika kuwa hivi sasa, Tanzania haina mitambo ya kusafisha mafuta (refineries), hivyo mafuta yanayoingizwa nchini ni yale yaliyosafishwa tu. Pia hakuna Hifadhi ya Taifa ya kuhifadhi mafuta kwa wingi. 
 
Maghala yote yaliyopo nchini ni ya kampuni binafsi na yanauwezo wa kuhifadhi mafuta kwa matumizi ya ndani kwa takribani siku miamoja ishirini (120). Hata hivyo, Kanuni zinazosimamia biashara ya mafuta zinamtaka kila mfanyabiashara wa mafuta kwa jumla awe na hifadhi ya mafuta kwa muda wa siku zisizopungua kuminatano (15) kulingana na hisa zake katika soko. 
 
Hata hivyo, Serikali kupitia Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) na Shirika la Maendeleo ya Petroli (TPDC) inafanya mchakato wa kujenga maghala ya kuhifadhi mafuta. 
 
Vilevile, kwa taratibu zilizopo, mafuta yanaingizwa nchini na mshindi wa zabuni za uagizaji mafuta kwa pamoja, ambapo kwa kiasi kikubwa; mafuta yanayoletwa nchini hutokea nchi za Uarabuni. Hivyo basi, kushuka kwa bei za mafuta Marekani kunaweza kusilete unafuu katika soko la Tanzania, kwa kuwa mafuta yetu yananunuliwa Uarabuni. 
 
Hata hivyo; ikiwa mafuta hayo yatashuka katika Soko la Dunia (Uarabuni), itachukua kipindi cha miezi miwili ndipo watanzania waone faida. 
 
Imetolewa na:
MKURUGENZI MKUU
22 Aprili, 2020


Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger