Wednesday, 22 April 2020

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatano April 22



















Share:

Tuesday, 21 April 2020

Senior procurement Officer at NRC Tanzania

Senior procurement Officer NRC Tanzania is looking for Senior Procurement Officer base at Kibondo ,kigoma The purpose of the Senior Procurement Officer position is to manage the day to day implementation of the procurement support functions responsibilities. All NRC employees are expected to work in accordance with the organization’s core values: dedication, innovation, inclusivity and accountability. These attitudes… Read More »

The post Senior procurement Officer at NRC Tanzania appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Junior Business Development Manager Job at Sculpt Army Sports Tanzania

Position: Junior Business Development Manager  Location: Dar es salaam This is what you’ll do: You are responsible for promoting sculptarmy.com in Tanzania Track and find events we can participate and manage preparations for the same Prepare Market analysis , SWOT, PESTEL analysis for competition and retail industry in Tanzania & East Africa Prepare Marketing campaign and materials Create new… Read More »

The post Junior Business Development Manager Job at Sculpt Army Sports Tanzania appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

 Logistics Officer vacancy at NRC Tanzania

 Logistics Officer   NRC Tanzania is looking for Logistics Officer base at Nyarugusu ,Kigoma The purpose of the Officer position is day to day implementation of the Logistics responsibilities and overall Logistics contact person for Nyarugusu Camp thus supervising other NRC Logistics personnel in the camp and reporting to the Logistics Coordinator in Kibondo. The Officer will have very… Read More »

The post  Logistics Officer vacancy at NRC Tanzania appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Muhimbili yasambaza vazi la PPE kwa kamati za dharura Jijini Dar es salaam ili Kuendelea Kukabiliana na Corona

Na Sophia Mtakasimba & Angela Mndolwa
Hospitali ya Taifa Muhimbili imeanza kusambaza  mavazi maalumu (coverall) ambayo ni sehemu ya mavazi ya watoa huduma (PPE) kuvaa ili kujikinga wakati wanatoa huduma wagonjwa wenye maambuki mbalimbali ikiwemo Covid 19 kwa kamati za dharura za Jiji la Dar es Salaam.

Akizungumza na wanahabari jana, Mkurugenzi wa Huduma za Uuguzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Bi. Zuhura Mawona  alisema kuwa baada ya kujadiliana na Serikali bei elekezi itakuwa Tzs. 50,000 kwa kila vazi moja.

Manispaa ya Kinondoni imenunua mavazi 15 yenye thamani ya Tzs. 750,000, Ilala mavazi 20 yenye thamani ya Tzs. 1,000,000 huku Manispaa nyingine zikiendelea kulipia ili kupata mavazi hayo.

"Kwa sasa tunaanza na vituo vilivyopo katika Manispaa za jiji la Dar es Salaam na mikoa mingine itafuata" alisema Bi. Mawona

Alisema kuwa mahitaji ni makubwa katika mikoa mbalimbali hivyo kwa sasa Muhimbili imejikita katika kuongeza uzalishaji ili kukidhi mahitaji.

Mapema wiki iliyopita Muhimbili ilizindua vazi hilo maalumu liloshonwa na wataalamu wa MNH kwa kutumia malighafi za ndani ya nchi lengo ikiwa ni kukabiliana na upungufu wa bidhaa hizo duniani.


Share:

Korea Kusini Kuchunguza Madai Ya Marekani Kuwa Rais Wa Kora Kaskazin Kim Jong Un Ana Hali Mbaya Baada Ya Kufanyiwa Upasuaji.

Serikali ya Korea Kusini inaangalia undani wa taarifa zilizoripotiwa na Vyombo vya Habari vya Marekani kuwa Kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong Un ana hali mbaya baada ya kufanyiwa upasuaji.

Maafisa wa Korea Kusini wamesema hawawezi kudhibitisha ripoti hiyo mara moja. 

CNN kimemnukuu Afisa wa Marekani ambaye alisema Kim yupo katika hali mbaya baada ya kufanya upasuaji ambao haukuwekwa wazi.

Kumekuwa na sintofahamu kuhusu afya ya Kim baada ya Kiongozi huyo kushindwa kuhudhuria hafla ya Kumbukumbu ya Marehemu babu yake, Kim Il Sun ambaye pia ni muasisi wa Taifa hilo wiki iliyopita.

Inaelezwa kuwa afya ya Kim Jong Un imezorota miezi ya hivi karibuni kutokana na uvutaji sigara, unene uliopitiliza na kufanya kazi kwa muda mrefu.

Alionekana kwa mara ya mwisho Aprili 11 ambapo aliongoza kikao na kisha kuelekea hospitali, chanzo kimoja kimesema kuwa Kim amekuwa akiugua tangu Agosti mwaka jana.


Share:

Picha : SHUWASA YATOA MSAADA WA NDOO 15 KUKABILIANA NA CORONA KATIKA MANISPAA YA SHINYANGA



Mkurugenzi wa SHUWASA Bi. Flaviana Kifizi (kulia) akimkabidhi Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko (kushoto) ndoo 15 zenye ujazo wa lita 45 kila moja kwa ajili ya kunawia mikono katika maeneo ya huduma za kijamii ili kukabiliana maambukizi ya Virusi vya Corona (Covid -19) 

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog  
Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA) imetoa msaada wa ndoo 15 zenye ujazo wa lita 45 kwa ajili ya kutumika kunawia mikono katika maeneo ya huduma za kijamii ili kusaidia katika mapambano dhidi ya maambukizi ya Virusi vya Corona (Covid -19) katika Manispaa ya Shinyanga.

Ndoo hizo zimekabidhiwa leo Jumanne Aprili 21,2020 na Mkurugenzi wa SHUWASA Bi. Flaviana Kifizi kwa Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko ambaye pia amemkabidhi Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Geofrey Mwangulumbi kwa ajili ya kuzisambaza katika maeneo yenye huduma za kijamii.

Akikabidhi ndoo hizo, Kifizi alisema SHUWASA inaunga mkono juhudi zinazofanywa na serikali katika kukabiliana na Maambukizi ya Virusi vya Corona na wananchi wahakikishe wananawa mikono kwa maji tiririka na sabuni.

“Tumezunguka katika maeneo mbalimbali katika Manispaa ya Shinyanga na kubaini kuwa baadhi ya maeneo yenye huduma za kijamii mfano sokoni wananchi wanatumia ndoo ndogo na chache kunawia mikono yao ndiyo maana tumeona ni vyema nasi tuchangie kwa awamu ya kwanza ndoo hizi 15 zenye ujazo wa lita 45 kila moja”,alisema Kifizi.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko aliishukuru SHUWASA kwa mchango huo wa ndoo za kunawia mikono huku akiwaomba wadau wengine kujitokeza kushirikiana na serikali katika kukabiliana na ugonjwa wa Corona kwani ni jukumu la kila mwananchi kuhakikisha maambukizi ya Virusi vya Corona havisambai katika jamii.

“Kwa niaba ya uongozi wa serikali niwashukuru sana SHUWASA kwa mchango huu ambao unaongeza juhudi za  katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa Corona. Tutazisambaza ndoo hizi katika maeneo yenye huduma za kijamii ikiwemo kwenye masoko ili kupunguza foleni lakini pia kuimarisha zaidi usafi”,alisema Mboneko.

“Naomba tuendelee kuhamasisha wananchi kunawa mikono kwa maji na sabuni kabla ya kupata huduma za kijamii katika maeneo mbalimbali ikiwemo masoko na vituo vya mabasi na kuhakikisha maji yanakuwepo kila wakati”,aliongeza Mboneko.

Katika hatua nyingine Mkuu huyo wa wilaya aliwataka wazazi,walezi na jamii kuwazuia watoto wasizulule mtaani badala yake watulie majumbani ili kuwaepusha wasipate maambukizi ya Virusi vya Corona.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga, Geofrey Mwangulumbi alisema atahakikisha maji ya kunawa yanakuwepo kila wakati na kwamba wataweka askari wa Jeshi la Akiba ‘Mgambo’ katika maeneo ya huduma za kijamii ili kusimamia zoezi la kunawa mikono kwa kila mtu anayefika katika maeneo hayo.

ANGALIA PICHA
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA) Bi. Flaviana Kifizi (kulia) akimkabidhi Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko (kushoto) ndoo 15 zenye ujazo wa lita 45 kila moja kwa ajili ya kunawia mikono katika maeneo ya huduma za kijamii ili kukabiliana maambukizi ya Virusi vya Corona (Covid -19) leo Jumanne Aprili 21,2020. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA) Bi. Flaviana Kifizi akimkabidhi Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko (kushoto) ndoo 15 kwa ajili ya kunawia katika maeneo ya huduma za kijamii kukabiliana na ugonjwa wa Corona. Wa Kwanza kushoto ni Katibu Tawala Wilaya ya Shinyanga, Boniface Chambi,wa kwanza kulia ni Afisa Mahusiano wa SHUWASA, Bi. Nsianel Gelard,wengine ni wafanyakazi wa SHUWASA.
Ndoo 15 zenye ujazo wa lita 45 zilitolewa na SHUWASA kwa ajili ya kunawia katika maeneo ya huduma za kijamii kukabiliana na ugonjwa wa Corona katika wilaya ya Shinyanga.
Kulia ni Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA)  Bi. Flaviana Kifizi akimwelezea Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko lengo la SHUWASA kuchangia ndoo za kunawia mikono katika maeneo ya huduma za kijamii.
Kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akiwashukuru viongozi wa SHUWASA kuchangia ndoo za kunawia mikono katika maeneo ya huduma za kijamii.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akisisitiza umuhimu wa kuhamasisha kila mwananchi anayefika katika maeneo ya huduma za kijamii ananawa mikono kwa maji safi na sabuni ili kukabiliana na maambukizi ya Virusi vya Corona.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akipiga picha ya kumbukumbu na viongozi wa SHUWASA baada ya kupokea ndoo 15 zilizotolewa na SHUWASA kwa ajili ya kukabiliana na maambukizi ya Virusi vya Corona katika maeneo ya huduma za kijamii.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko  (katikati) akiomuonesha Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga, Geofrey Mwangulumbi ( wa pili kushoto) ndoo zilizotolewa na SHUWASA kwa ajili ya kukabiliana na maambukizi ya Virusi vya Corona katika maeneo ya huduma za kijamii.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko  (kulia) akimkabidhi Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga, Geofrey Mwangulumbi  ndoo zilizotolewa na SHUWASA kwa ajili ya kukabiliana na maambukizi ya Virusi vya Corona katika maeneo ya huduma za kijamii.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga, Geofrey Mwangulumbi (wa pili kushoto) akizungumza baada ya kukabidhiwa na Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko ndoo 15 zilizotolewa na SHUWASA kwa ajili ya kukabiliana na maambukizi ya Virusi vya Corona katika maeneo ya huduma za kijamii.

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Share:

Chief Operations Officer Vacancy at CRDB Bank PLC

JOB VACANCY CRDB Bank PLC is looking for a suitable person to fill a vacant position of Chief Operations Officer (COO) at the Head Office, in Dar es Salaam. Job Purpose Reporting to Group Chief Executive Officer & Managing Director, COO is responsible for managing all operational activities, ensuring delivery of timely, reliable, quality and secured services to… Read More »

The post Chief Operations Officer Vacancy at CRDB Bank PLC appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Stress Counsellor at UNDP – United Nations Development Programme, Kasulu, Tanzania

Stress Counsellor at UNDP – United Nations Development Programme, Kasulu, Tanzania   Organization: UNDP – United Nations Development Programme Country: Tanzania Field location: Kasulu, Tanzania Office: UNDP in Kasulu Grade: NO-A Background The administrative supervision of the UNDSS security advisor and technical supervision of the UNDSS CISMU regional stress counsellor, the field stress counselor will implement a wide… Read More »

The post Stress Counsellor at UNDP – United Nations Development Programme, Kasulu, Tanzania appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Kinara wa Usafirishaji Wahamiaji Haramu Akamatwa Kyela, Mbeya

Mbeya, Tanzania: Idara ya Uhamiaji Mkoa wa Mbeya Imefanikiwa Kumkamata mtuhumiwa wa usafirishaji wa wahamiaji haramu Bwana Paul Edward Kawilo, alimaarufu Mwakaniemba Mtanzania mwenye umri wa miaka 36 mkazi wa Kasumulu Wilaya ya Kyela Mkoani Mbeya.

Mtuhumiwa alikamatwa tarehe 16 Aprili ambapo anatuhumiwa kwa makosa ya kusafirisha wahamiaji haramu ambao idadi yao ni 06 raia wa  Ethiopia, raia  hao walipitishwa katika vipenyo vya Mpaka wa Isongole uliopo Wilayani Ileje Mkoani Songwe unaotenganisha nchi ya Tanzania na Malawi, kwa kutumia usafiri wa pikipiki (Bodaboda) zenye namba za usajili wa Tanzania ambazo nazo zinashikiliwa na Uhamiaji.

Akitoa taarifa kwa vyombo vya Habari Afisa Uhamiaji Mkoa wa Mbeya Kamishna Msaidizi Mwandamizi (SACI) Msafiri Alan Shomari alieleza kwamba Mtuhumiwa alikamatwa na Afisa Uhamiaji akishirikiana vyema na askari wa Jeshi la Magereza na wananchi katika eneo la Busare Wilaya ya Kyela Mkoani Mbeya,  hata hivyo mtuhumiwa  amerudishwa Mkoani Songwe kwa ajili ya kupelekwa mahakamani Kujibu shitaka lake.

Afisa uhamiaji Mkoa wa Mbeya ametoa wito Kwa wananchi kutojihusisha na biashara hiyo kwani ni hatari kwa usalama wa nchi na mipaka yetu na hivyo amewahimiza kufanya shughuli nyingine halali zinazoweza kuwaingizia vipato.

Aidha kwa kushirikiana na Ofisi ya Uhamiaji Mkoa wa Songwe SACI Shomari amesema mtuhumiwa ananendelea kufanyiwa mahojiano ya kina kwa lengo la kubaini mtandao wa usafirishaji wa wahamiaji haramu ili kusambaratisha kabisa mtandao huo katika Mikoa hiyo ya kusini.
(Picha na Ofisi ya Uhusiano Uhamiaji Mkoa wa Mbeya).


Share:

Waliofariki Kwa Corona Marekani Wafika 42,518....Trump Asitisha Kupokea Wahamiaji Ili Kulinda Ajira za Wamarekani

Idadi ya watu walioaga dunia kutokana na maambukizi ya virusi vya corona nchini Marekani imepindukia 42,518.


Vyombo vya habari vya Marekani vimeripoti kuwa, idadi ya watu walioambukizwa virusi vya corona nchini humo imefikia 792,938  na kwamba 72,389 miongoni mwao wamepona

Kwa sasa Marekani inashika nafasi ya kwanza duniani kwa kuwa na idadi kubwa zaidi ya watu walioambukizwa virusi vya corona na vilevile kwa kuwa na idadi kubwa zaidi ya wahanga wa virusi hivyo.

Kutokana na hali mbaya iliyosababishwa na ugonjwa wa Covid-19, kwa mara ya kwanza kabisa katika historia ya Marekani Rais wa Nchi hiyo Donald Trump ametangaza mkakati wa  "kulinda ajira" za Wamarekani. 

"Kwa kuzingatia shambulio la adui asiyeonekana, na kutokana na haja ya kulinda ajira za raia wetu wakuu wa Marekani, nitasaini agizo la rais la kusitisha kwa muda zoezi la kupokea wahamiaji nchini Marekani, "Trump ameandika kwenye ukurasa wake wa Twitter.

Mapema mwezi wa Januari, alizuia safari zozote kwenda China ambapo virusi vya Corona vilianzia mwezi wa Desemba mwaka jana, kabla ya kupiga marufuku safari kati ya Marekani na nchi nyingi za Ulaya katikati mwa mwezi Machi.


Share:

Temporary Job Opening (Duration until 31 December 2020) Messenger / Mail Clerk, G-2

United Nations International Residual Mechanism for Criminal Tribunals Temporary Job Opening (Duration until 31 December 2020) Messenger / Mail Clerk, G-2 DEADLINE FOR APPLICATIONS : 21 April 2020 DATE OF ISSUANCE : 15 April 2020 OFFICE : Registry/ General Services Section (GSS) LOCATION : Arusha JOB OPENING NUMBER : 2020/IRMCT/REG/GSS/103-GS   United Nations Core Values: Integrity, Professionalism, Respect… Read More »

The post Temporary Job Opening (Duration until 31 December 2020) Messenger / Mail Clerk, G-2 appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Messenger/ Mail Clerk, G-2 at United Nations International Residual Mechanism for Criminal Tribunals

United Nations International Residual Mechanism for Criminal Tribunals Messenger/ Mail Clerk, G-2 DEADLINE FOR APPLICATIONS : 15 May 2020 DATE OF ISSUANCE : 16 April 2020 OFFICE : Registry/ General Services Section (GSS) LOCATION : Arusha JOB OPENING NUMBER : 2020/IRMCT/REG/GSS/068-GS United Nations Core Values: Integrity, Professionalism, Respect for Diversity Organizational setting and Reporting: This position is located… Read More »

The post Messenger/ Mail Clerk, G-2 at United Nations International Residual Mechanism for Criminal Tribunals appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Programme Assistant (Library) at RMT Arusha, Tanzania

Organization: International Residual Mechanism for Criminal Tribunals Country: Tanzania City: Arusha, Tanzania Office: RMT Arusha Closing date: Friday, 15 May 2020 Posting Title: Programme Assistant (Library), FS4 Job Code Title: Library Assistant Department/Office: International Residual Mechanism for Criminal Tribunals Duty Station: ARUSHA Posting Period: 16 April 2020 – 15 May 2020 Job Opening Number: 20-Documentation and Information -RMT-134249-R-Arusha… Read More »

The post Programme Assistant (Library) at RMT Arusha, Tanzania appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

UPDATED EMPLOYMENT OPPORTUNITIES: MIZENGO PINDA CAMPUS-KATAVI & SUA MAIN CAMPUS-MOROGORO

UPDATED EMPLOYMENT OPPORTUNITIES: MIZENGO PINDA CAMPUS-KATAVI & SUA MAIN CAMPUS-MOROGORO (This advertisement replaces the previous advertisement dated 14th April, 2020 in Mwananchi, Daily News and Uhuru Newspapers and SUA Website)   The Management of Sokoine University of Agriculture (SUA) invites suitable qualified Tanzanians to apply for the positions of Assistant Lecturers and Tutorial Assistants. All applications should be addressed to the… Read More »

The post UPDATED EMPLOYMENT OPPORTUNITIES: MIZENGO PINDA CAMPUS-KATAVI & SUA MAIN CAMPUS-MOROGORO appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Tanzania Impact Ventures Program Associate at One Acre Fund Morogoro, Tanzania

About One Acre Fund Founded in 2006, One Acre Fund supplies 1 million smallholder farmers with the agricultural services they need to make their farms vastly more productive. We provide quality farm supplies on credit, delivered within walking distance of farmers’ homes, and agricultural trainings to improve harvests. We measure our success by our ability to make farmers… Read More »

The post Tanzania Impact Ventures Program Associate at One Acre Fund Morogoro, Tanzania appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Kuongoza maombi ya Kitaifa kesho tarehe 22/04/2020 katika Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.

Dodoma,  Jumanne 21 Aprili, 2020 
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa kushirikiana na Viongozi wa madhehebu ya Dini nchini, imeandaa maombi maalum Kitaifa kuiombea Nchi dhidi ya maambukizi ya homa kali ya mapafu inayotokana na Virusi vya Corona.

 Maombi hayo  yatakayoongozwa na Viongozi Wakuu wa  madhehebu ya Dini nchini, yatafanyika Jumatano tarehe 22 Aprili, 2020 katika Viwanja vya Karimjee Jijini Dar Es Salaam, kuanzia Saa 3.00 Asubuhi ambapo Mgeni Rasmi atakuwa Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

 Hatua hii ni utekelezaji wa maazimio ya Mkutano wa viongozi wa Dini na Serikali uliofanyika tarehe 9 Aprili, 2020 Jijini Dar Es Salaam kuwa yafanyike maombi ya kitaifa yanayojumuisha madhehebu yote nchini kuomba dhidi maambukizi ya Corona.

 Aidha, maombi haya ni mwendelezo wa maombi ya siku tatu mfululizo yaliyotangazwa na Mhe. Rais, Dkt. John Pombe Magufuli kuanzia tarehe 17-19 Aprili, 2020.

 Viongozi wachache watahudhuria maombi haya kuwakilisha wananchi ikiwa ni katika hali ya kuchukua tahadhari ya maambukizi hivyo, wananchi mnasisitizwa kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya Corona na kufuatilia maombi haya mkiwa katika maeneo yenu kupitia vyombo mbalimbali vya habari.

JIKINGE, WAKINGE WENGINE CORONA INAZUILIKA.
 
IMETOLEWA NA
   
Prudence Constantine,
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
(Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii).


Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger