Sunday, 19 April 2020

Fisi Ajeruhi Watu Wawili Kahama Mkoani Shinyanga

SALVATORY NTANDU
Wakazi wawili wa Kijiji cha Ngogwa halmashauri ya Mji wa Kahama mkoani Shinyanga wamenusurika kuuawa baada ya kushambuliwa na  Fisi wakati wakijaribu kumfukuza fisi huyo aliyekuwa amevamia kundi la mbuzi katika kijiji hicho.

Akizungumza na waandishi wa Habari leo Aprili 19, 2020 Afisa mtendaji wa Kata hiyo Upendo Shirima alisema tukio hilo limetolea  leo saa mbili asubuhi ambapo Fisi  huyo  alivamia zizi la Mbuzi  kabla ya wananchi kuanza kumpiga na ndipo alipowajeruhi sehemu za mikononi wananchi hao ambao wamepelekwa katika hospitali ya halmashauri ya mji wa Kahama kwa matibabu.

Aliwataja walioshambuliwa Fisi huyo kuwa ni Pamoja na Donald Simoni (27) na Furaha Ngusa (46) na ameiomba Wizara ya Maliasili kutenga siku maalumu ili kwenda kuwawinda fisi hao ambao wamekuwa ni wengi kwa wakati huu.

“Tunaomba tu watu wa maliasili watusaidie kufanya oporesheni  juu ya wananyama hao maana kutokana na mvua hizi Maji yameingia kwenye mapango yao hali ambayo inawafanya waje kwenye makazi ya watu”alisema Shirima.

Alisema kuwa watu wameanza kupata hofu kutokana na wananyama hao kuanza kuvamia nyakati za mchana kwani walizoea kuwaona wakivamia mifugo wakati za usiku.

Diwani wa Kata ya Ngogwa  Kamuli Mayuga alisema  baada ya kuwafikisha hospitalini wamepatiwa matibabu kwa kushonwa nyuzi kwenye majereha na kuruhusiwa kuerejea nyumbani huku akiwataka wananchi waendelee kuchukua tahadhari.


Share:

Wanamgambo 44 wa Boko Haram Wafariki Gerezani Nchini Chad

Wafungwa 44 wa kundi la wapiganaji wa msimamo mkali la Boko Haram waliokamatwa na jeshi la Chad mwanzoni mwa mwezi huu katika mkoa wa Lac wamekutwa  wamefariki dunia katika gereza usiku wa Alhamisi kuamkia Ijumaa wiki hii

Wafungwa hao walikabidhiwa mahakama siku ya Jumatano baada ya kukamatwa katika operesheni ya jeshi la Chad dhidi ya shambulio baya lililogharimu maisha ya askari wa chad katika moja ya kambi za jeshi la nchi hiyo.

Wafungwa 48 kutoka kundi la Boko Haram walizuiliwa katika kituo kimoja nje ya mji mkuu wa Ndjamena na kukabidhiwa mahakama siku ya Jumatano. Lakini Alhamisi asubuhi, 44 kati yao walikutwa wamefariki dunia katika  chumba walimo kuwa wamezuiliwa, kulingana na mamlaka ya Chad.

Kulingana na uchunguzi wa daktari, wapiganaji hao walikunywa sumu. Ripoti yake ya vipimo, kulingana na taarifa ya mwendesha mashtaka wa Ndjamena, Youssouf Tom, inaonysha kwamba walitumia vidonge vyenye sumu iliyosababisha  washindwe kupumua


Wote walikamatwa wakati wa operesheni iliyoitwa "Hasira ya Bohoma", iliyotekelezwa na jeshi la Chad kuanzia Machi 31 hadi Aprili 8. Karibu wanajeshi 52 wa Chadi na wapiganaji kadhaa wa Boko Haram waliuawa katika mapigano hayo


Credit:RFI


Share:

ODO UMMY FOUNDATION YATOA MSAADA WA VIFAA VYA KUJIKINGA NA CORONA KWA TAASISI ZA DINI JIJINI TANGA

 MKUU wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa kulia akizungumza wakati akishukuru Taasisi ya Odo Ummy Foundation kwa msaada ndoo 120 na sabuni 60 ikiwemo vifaa vyake vya kuwekea ndoo hizo ili kuwawezesha kuzitumia katika kuhakikisha wanajikinga na maambukizi hayo ambayo kwa sasa yamekuwa yakilitikisha dunia katikati ni  Katibu wa Taasisi ya Odo Ummy Foundation Khatibu Kilenga
 Katibu wa Taasisi ya Odo Ummy Foundation Khatibu Kilenga kulia akiteta jambo na Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa kushoto kabla ya kuona msaada ndoo 120 na sabuni 60 ikiwemo vifaa vyake vya kuwekea ndoo hizo ili kuwawezesha kuzitumia katika kuhakikisha wanajikinga na maambukizi hayo ambayo kwa sasa yamekuwa yakilitikisha dunia ambayo vimetolewa na Taasisi ya Odo Ummy Foundation kwa nyumba za ibada misikiti na makanisa Jijini Tanga
 Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa kushoto akiangalia koki zilizopo kwenye ndoo hizo ambazo zilitolewa na Taasisi ya Odo Ummy Foundation kwa ajili ya kupelekwa kwenye misikiti na makanisa kusaidia kwenye mapambano dhidi ya Ugonjwa wa Corona

 Sehemu ya vifaa ambavyo vimetolewa na Taasisi ya Odo Ummy Foundation kwa ajili ya kupelekwa kwenye misikiti na makanisa kusaidia kwenye mapambano dhidi ya Ugonjwa wa Corona


NA MWANDISHI WETU,TANGA.

TAASISI ya Odo Ummy Foundation ya Jijini Tanga imetoa msaada wa vifaa vya kujikinga na maambukizi ya virusi vya Corona kwa taasisi za dini zilizopo Jijini humo ikiwa ni mkakati wa kuhakikisha wanaepukana na maambukizi hayo kwa kuchukua tahadhari.

Msaada uliotolewa ni ndoo 120 na sabuni 60 ikiwemo vifaa vyake vya kuwekea ndoo hizo ili kuwawezesha kuzitumia katika kuhakikisha wanajikinga na maambukizi hayo ambayo kwa sasa yamekuwa yakilitikisa dunia.

Akizungumza wakati wa halfa hiyo ambayo ilihudhuriwa na Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa, Katibu wa Taasisi ya Odo Ummy Foundation Khatibu Kilenga ambayo ilianzishwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga Ummy Mwalimu ikiwa na lengo l kujenga hamasa kwenye jamii na kusaidia masuala mbalimbali ya kijamii.

Alisema kwamba taasisi hiyo imekuwa ikiwasaidia kwenye mambo mengi ikiwemo elimu,afya na makundi madogo madogo ya kijamii ikiwemo vijana na wanawake ili kuweza kuhakikisha wanajikwamua kiuchumi kupitia fursa zilizopo kwenye maeneo yao na hivyo kuharakisha maendeleo.

“Kwenye janga hilo lililoikumba dunia la Corona hatukuwa nyuma tumeona angalu tutoa ndoo na sabuni kwa ajili ya kusaidia kupunguza maambukizi ambao yanaonekana kukua kwa kasi kwenye maeneo mbalimbali lakini pia ni sehemu ya kutoa elimu pamoja na kwamba kuna maelekezo mbalimbali yanayotolewa ya kujilinda kwa kunawa mikono vizuri pamoja na kutumia maski ”Alisema

Aidha alisema wao wameona wagawe ndoo 60 maana ya zenye maji na za kukingilizia 60 hivyo kufikia ndoo 120 na vifaa vyake vya kuwekea ndoo hizo ambayo watazigawa kwenye maeneo ya misikitini na kanisani ambapo wameona kutakuwa na uhaba mkubwa.

“Katika maeneo ya ibada misikitini na kanisani tuliona vifaa hivyo havijawafikia na ndio maana tuliona tusambaze huku akisisitiza kwamba hiyo ni hatua ya kwanza ya kusaidia jambo hilo lakini hapo mbeleni wanakusudia kufanya jambo mkubwa zaidi”Alisema Kilenga

Hata hivyo alisema pia wataendelea kuchangia mambo mbalimbali kwa jamii kwani matatizo yao ni yetu na hivyo ndio kauli mbiu ya Taasisi yetu kwamba “Tanga yetu ni wajibu wetu” huku akimkaribisha Mkuu huyo wa wilaya ashiriki nao katika kuliunga mkono jambo hilo akiwa kama msimamikzi mkuu wa wilaya.

Awali akizungumza wakati wa alipotembelea na kuona vifaa hivyo Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa aliishukuru Taasisi ya Oddo Ummy Foundation na Mbunge Ummy kwa kuja na mpango huo wa kusaidia msaada huo ambao umefika wakati muafaka ambapo kwa sasa wamekuwa wakikabiliana na ugonjwa wa Corona.

Alisema ni faraja kubwa kwa kuja na mpango huo wa kutusaidia watu wa Tanga vifaa hivyo kufanyia jambo la usafi ambalo ni sharti la umuhimu katika mapambano dhidi ya Ugonjwa wa Virusi vya Corona.

“Lakini nishukuru Taasisi ya Oddo Ummy foundation kuianisha msaada huo ujieleze kwenye maeneo gani hilo ni jambo la msingi sana na muhimu hivyo tunakushukuru sana kwa hili ambalo umelifanya kupitia Taasisi yenu na tunafurahi kuona umeelekeza hili liende kwenye jumba za ibada”Alisema

Aidha alisema kwamba wamefurahi sana kuona msaada huo uelekezwe kwenye nyumba za ibada na itakuwa ni mchango mkubwa sana kwao kuweza kuimarisha jitihada mbalimbali za kukabiliana na ugonjwa huo ambao ni hatari duniani.

“Msaada huo umekuja kutupa nguvu kwa juhudi ambazo tumekuwa tukizifanya hivyo tunakushukuru sana huku akizitaka taasisi za dini ambazo zitanufaika na msaada huo kuhakikisha wanavitumia kwenye matumizi yaliyokusudiwa na sio vyenginevyo “Alisema DC Mwilapwa.
Share:

FULL POWER , ZATI 50 NI SULUHISHO LA KUDUMU TATIZO LA NGUVU ZA KIUME NA UUME MDOGO



Sababu za upungufu wa nguvu za kiume na maumbile madogo ya uume


⇒Ngiri,

⇒Henia

⇒Kisukari

⇒Tumbo kujaa gesi

⇒Kutopata choo vizuri

⇒Utumiaji madawa kwa muda mrefu

⇒Unywaji wa pombe kupita kiasi

⇒Msongo wa mawazo 



⇮⇒Haya yote hupelekea mwili kutokuzalisha homoni ya gesrtogine au kuwa chache na kushindwa kupata mzunguko mzuri wa damu na vichocheo vingine kama madini ya zinki ambayo hukufanya kuwa na msisimko  na kufanya kuwa na muda  mrefu na nguvu za kutosha.



FULL POWER



⇨Ni dawa ya vidonge ya miti shamba inaongeza nguvu za kiume na kutibu kabisa tatizo hilo.



⇨Inaongeza hamu ya tendo la ndoa
⇨Inakufanya uchelewe kufika kileleni zaidi ya Dakika 30 na kurudia tendo zaidi ya mara nne na zaidi.

Zati 50

⇨ Inarutubisha maumbile ya uume  na kunenepesha urefu nchi 6,unene sentimita 4

⇨Dawa hii ni ya kutibu kabisa tatizo hilo.

Pia tunatibu Magonjwa mengine Kama

Matatizo ya pumu,Bawasiri, vidonga vya tumbo,Kisukari,Magonjwa sugu ya zinaaa,Kaswende,U.T.I , kiuno,miguu kuwaka moto, Fangasi sehemu za Siri, kupunguza unene wa mwili,tumbo kuunguruma,kujaa gesi, matatizo ya uzazi kwa wanawake, kurutubisha mbegu za uzazi kwa akina baba, matatizo ya meno tunatibu bila kungoa

Kliniki yetu inapatikana Zanzibar, Dar es salaam na Shinyanga.

Wasiliana nasi kwa simu namba 071770 22 27
Share:

WASAMBAZAJI NA WAUZAJI WA SUKARI NCHINI TANZANIA WAPEWA ONYO


Share:

Naibu Waziri wa Afya Dr Faustine Ndugulile Ametoa Ufafanuzi Kuhusu Barakoa (Mask) Na Matumizi Yake

NA Dkt Faustine Ndugulile
Kuna clip inazunguka mitandaoni nikiongelea kuhusu barakoa za kitambaa. Napenda kutoa ufafanuzi ufuatavyo:

1. Barakoa za N95 zinapaswa kutumika na watoa huduma wa afya wanaohudumia wagonjwa wa Covid-19. Barakoa hizi hazipaswi kuvaliwa mitaani, majumbani wala maofisini.
 
2. Barakoa za upasuaji (surgical masks) hizi zinapaswa kuvaliwa na watumishi wa afya ambao hawana direct contact na wagonjwa. Barakoa hizi pia zinaweza kuvaliwa na jamii kwenye maeneo ya mikusanyiko kwa muda wa masaa 4-6. Barakoa hizi hazipaswi kuvaliwa kutwa nzima na kurudia matumizi (re-use). 
 
Aidha, kumekuwa na sintofahamu kuhusu namna ya uvaaji wa barakoa za upasuaji. Barakoa hizi zinapaswa kuvaliwa kama ifuatavyo:
(a). Upande wenye rangi (blue, kijani, zambarau nk) unapaswa kuwa nje.
(b). Upande wenye chuma unapaswa kuwa juu.
 
3. Barakoa za kitambaa (cloth masks) *hazina ubora wa kinga kama N-95 au  surgical masks*, lakini *zinaweza kutumika kupunguza uwezekano wa maambukizi toka kwa mtu mmoja kwenda mwingine majumbani na sehemu za mikusanyiko*. 
Mambo ya kuzingatia ni pamoja na:
1. Kutumia vitambaa vya pamba.
2. Kutumia layers zaidi ya mbili katika utengenezaji wa barakoa hizo.
3. Kuwa na  barakoa angalau mbili ili kuruhusu kufanyiwa usafi wa mara kwa mara.
4. Barakoa zifuliwe kwa maji na sabuni na kupigwa pasi.
 
NI MUHIMU KUKUMBUKA KUWA BARAKOA SIO MBADALA WA KUNAWA MIKONO NA KUZINGATIA UMBALI KATI YA MTU NA MTU (SOCIAL DISTANCING) BALI NI NYONGEZA YA HATUA HIZI. 
 
Aidha, tuhakikishe barakoa zilizotumika hazitupwi ovyo na badala yale zichomwe moto ili kuepuka kuokotwa na kutumiwa na watu wengine.
 
 Vile vile, watu hawapaswi kuazimana barakoa iliyokwisha kutumika. Kila mtu awe na yake.
 
Mwisho, tuendelee kuzingatia maelekezo yanayotolewa mara kwa mara na Wizara ya Afya kuhusu hatua mbali mbali za kujikinga na ugonjwa huu.
 
Dkt Faustine Ndugulile (Mb)
19.04.2020


Share:

Tumefanya Maboresho Kwenye App Yetu ya Mpekuzi Ili Kukuwezesha Kupata Habari zetu Haraka hasa Wakati huu wa janga la Corona

Tumefanya maboresho katika App yetu ya MPEKUZI ili kuendana na changamoto ya sasa ya janga la Corona inayoikumba dunia Nzima

Usikubali kupitwa na taarifa muhimu zinazoendelea hapa nchini na Duniani  kwa Ujumla . Tumejipanga vizuri sana kukupatia taarifa sahihi na kwa wakati.

👉1. Tumebadili muonekano na kuufanya kuwa mzuri zaidi
👉2. Kila habari tunayoweka kuanzia sasa utapata notification kwenye simu yako 
👉3. Habari zote kwa sasa zinafika kwa haraka kwenye simu yako kuliko ilivyokuwa hapo awali

KUMBUKA: App yetu ni BURE. Unachotakiwa kukifanya ni kuingia Playstore na kupakua MPEKUZI APP

Kama tayari unayo, basi Ingia Playstore kwa ajili ya kupata UPDATE hii ya Toleo Jipya

Tumekurahisishia, Unaweza pia ...<<KU BOFYA HAPA>> Kupata toleo hili Bure Kabisa


Share:

DK. NDUGULILE ATOA UFAFANUZI KUHUSU BARAKOA NA MATUMIZI YAKE


UFAFANUZI KUHUSU BARAKOA NA MATUMIZI YAKE

Kuna clip inazunguka mitandaoni nikiongelea kuhusu barakoa za kitambaa. Napenda kutoa ufafanuzi ufuatavyo:


1. Barakoa za N95 zinapaswa kutumika na watoa huduma wa afya wanaohudumia wagonjwa wa Covid-19. Barakoa hizi hazipaswi kuvaliwa mitaani, majumbani wala maofisini.

2. Barakoa za upasuaji (surgical masks) hizi zinapaswa kuvaliwa na watumishi wa afya ambao hawana direct contact na wagonjwa. Barakoa hizi pia zinaweza kuvaliwa na jamii kwenye maeneo ya mikusanyiko kwa muda wa masaa 4-6. Barakoa hizi hazipaswi kuvaliwa kutwa nzima na kurudia matumizi (re-use). 

Aidha, kumekuwa na sintofahamu kuhusu namna ya uvaaji wa barakoa za upasuaji. Barakoa hizi zinapaswa kuvaliwa kama ifuatavyo:

(a). Upande wenye rangi (blue, kijani, zambarau nk) unapaswa kuwa nje.

(b). Upande wenye chuma unapaswa kuwa juu.

3. Barakoa za kitambaa (cloth masks) hazina ubora wa kinga kama N-95 au  surgical masks, lakini zinaweza kutumika kupunguza uwezekano wa maambukizi toka kwa mtu mmoja kwenda mwingine majumbani na sehemu za mikusanyiko.  

Mambo ya kuzingatia ni pamoja na:

1. Kutumia vitambaa vya pamba.

2. Kutumia layers zaidi ya mbili katika utengenezaji wa barakoa hizo.

3. Kuwa na  barakoa angalau mbili ili kuruhusu kufanyiwa usafi wa mara kwa mara.

4. Barakoa zifuliwe kwa maji na sabuni na kupigwa pasi.

NI MUHIMU KUKUMBUKA KUWA BARAKOA SIO MBADALA WA KUNAWA MIKONO NA KUZINGATIA UMBALI KATI YA MTU NA MTU (SOCIAL DISTANCING) BALI NI NYONGEZA YA HATUA HIZI. 

Aidha, tuhakikishe barakoa zilizotumika hazitupwi ovyo na badala yale zichomwe moto ili kuepuka kuokotwa na kutumiwa 
na watu wengine.

 Vile vile, watu hawapaswi kuazimana barakoa iliyokwisha kutumika. Kila mtu awe na yake.

Mwisho, tuendelee kuzingatia maelekezo yanayotolewa mara kwa mara na Wizara ya Afya kuhusu hatua mbali mbali za kujikinga na ugonjwa huu.

Dkt Faustine Ndugulile (Mb)
19.04.2020
Share:

Bodi Ya Pamba Yashauriwa kudhibiti Uuzaji Holela Wa Pembejeo Kishapu.

SALVATORY NTANDU
Baada ya Kuwepo kwa Malalamiko ya Wakulima wa zao pa Pamba Wilayani Kishapu mkoani Shinyanga ya kuwatuhumu Viongozi wa vya Msingi (AMCOS) kuuza pembejeo zilizotolewa na serikali kwa mkopo kwa wakulima hatimaye Bodi ya Pamba Tanzania imeanzisha  msako  mkali katika maduka ya pembejeo ili kubaini undani wa suala hilo. .

Akizungumza na Waandishi wa Habari kabla ya kuanza msako huo Aprili 18 mwaka huu, Mkaguzi bodi ya pamba, Thomas Daudi alisema kuwa watafanya ukaguzi kwenye maduka ya pembejeo ya watu binafsi pamoja na minada na magulio yote wilayani humo ambayo pembejeo hizo huuzwa kwa wakulima.

Daudi alifafanua kuwa ofisi yao imepokea malalamiko kutoka kwa wakulima wa pamba kuwa wapo baadhi ya  viongozi wa AMCOS wanauza kuuza pembejeo za kuulia kinyume na maelekezo ya serikali kwani pembejeo hizo zinatolewa kwa mkopo kwa wakulima kupitia vyama vyao vya msingi.

“Niwatake viongozi AMCOS kuacha tabia hiyo pamoja kwani watakapobainika katika msako huo watachukuliwa hatua kali za kisheri na pia wafanyabiashara walionunua  pembejeo hizo kunyume na utaratibu wanapaswa kuzisalimisha kwa Bodi ya pamba mara moja”,alisema Daudi.

Rajabu Masunga ni mkulima wa Zao la Pamba wilayani Kishapu aliyeshuhudia msako huo aliipongeza Bodi ya Pamba kwa kuwabana wauzaji wa pembejeo za ruzuku zilizotolewa na serikali ambapo wengi wao walikuwa wakipanga pembejeo hizo chini kwenye minada na kuwauzia wakulima kwa bei ya juu.

Alisema kuwa pembejeo hizo ambazo ni sumu za kuulia wadudu katika zao la pamba katika minada mbalimbali huku kishapu zimekuwa zikiuzwa kiholela tena kwa kuanikwa juani na wakulima wengi wamekuwa wakizikosa katika AMCOS zao na kulekezwa kununua katika minada kinyume na maalekezo ya serikali.

“Tunashangaa siku ya mnada ambayo ni alhamisi ya kila wiki katika manada huu  mkubwa wa mifugo ambao pia wafanyabiashara huleta biashara mbalimbali hususani dawa za kuulia wadudu kwenye mazao ya mifugo ambayo wengi wetu hatujui kama ni yanavigezo vinavyotakiwa ama ni yale ya ruzuku yaliyotolewa na serikali,” alisema masunga.

Sambamba na hilo Masunga aliishauri bodi ya pamba kila siku ya Alhamisi ambayo ni siku ya mnada kufanya ukaguzi wa pembejeo zinazouzwa  ili kuhakiki kiwango cha ubora wa dawa zinazouzwa kwa wakulima ili kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya tano ya kumkomboa mkulima.

Mwisho.


Share:

VH.SHAH WAUZA SUKARI KWA BEI "CHEE" KANDA YA ZIWA


WAKALA na msambazaji mkubwa wa sukari katika mikoa ya kanda ya ziwa VH. Shah, ameendelea kuuza sukari katika mikoa hiyo kwa bei elekezi inayotakiwa na Serikali.



Hivi karibuni, Waziri wa Viwanda na Biashara, Innocent Bashungwa, aliwaonya baadhi ya mawakala "wapigaji" wa sukari nchini kuacha kupandisha bei kwa madai ya kwamba bidhaa hiyo imeadimika nchini huku akisisitiza kuwa Serikali haitasita kuchukua hatua kwa atakaebainika.

Msimamo huo wa SHAH ni njia moja wapo ya utekelezaji wa agizo la Serikali la kuwataka wasambazaji (mawakala) wa sukari nchini kuuza sukari kwa mjibu wa taratibu.

Akizungumza jana, amesema sukari yote iliyopo katika magahara yake, inatauzwa kwa watu wote bila kubagua mtu au mfanyabiashara yeyote yule.

Pia amesema, bei ya sukari inayouzwa (na wao) ni bei ya chini ya bei elekezi iliyoelekezwa na Serikali huku akisisitiza kuwa hakuna sababu ya wao kupandisha bei.

"Sisi tunauza sukari mpaka chini ya bei elekezi, lakini unaweza kushangaa leo tumeuza sukari ya kilo 50 kwa Tsh.130000 lakini kesho ukakuta tumeuza chini au zaidi ya hapo.

"V.H.Shah hatujawahi kupandisha bei na tunafanya kazi kwa mjibu wa sheria hatuwezi kufanya kosa la kupandisha bei ya sukari, tunafahamu tukipandisha bei ni kosa na tunaweza kufutiwa hata leseni na tunafanya kazi hii kwa kusasaidia wananchi wetu " amesema Shah.


Amesema kazi ya kusambaza sukari kanda ya ziwa wanaifanya kwa kufuata sheria na kanuni za biashara za nchi pamoja na kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania DK. John Magufuli, anaepambana kuhakikisha Tanzania inafikia uchumi wa kati.

"Rais wetu Magufuli anafanya kazi ya kuhakikisha nchi hii inakuwa na uchumi kupitia viwanda, sasa sisi tunafanya kazi hii ili kusaidiana nae, lakini unakuta kuna watu wanaongea mambo ya kwamba sisi tumepandisha bei kitu ambacho sio kweli," amesema.

Pia amewaondoa wasi wasi wakazi wa mikoa ya kanda ya ziwa na kuwahakikisha kuwa sukari ipo ya kutosha na hakuna bei iliyopandishwa ya uuzwaji wa sukari.

Mkoa wa Mwanza, sukari ya KG 50 inauzwa kwa Tsh. 130000 huku mfuko wa KG 25 ukicheza kwa Tsh. 60000, ambapo bei hiyo ni kwa jumla. 
Share:

22 WAPONA CORONA 1,126 WAPIMWA KWA SIKU


Nchi ya Uganda mpaka sasa imeripoti visa 55 vya waathirika wa Virusi vya Corona, na 22 kati yao tayari wamekwishapona huku 33 waliobaki wakiendelea na matibabu.

Aidha kwa mujibu ya taarifa ya vipimo vya sampuli vya watu 1,126, vilivyochukuliwa siku ya jana ya Aprili 18, 2020, vimeleta majibu ya kwamba wote hawana maambukizi ya Virusi vya Corona, ambapo kati yao madereva wa malori ni 837 na waliosalia ni wale watu waliokuwa wakifuatiliwa kwa ukaribu.

Aidha mpaka sasa nchi ya Uganda haijaripoti kifo chochote cha mgonjwa wa COVID-19, tangu nchi hiyo ianze kupata maambukizi hayo.
Share:

BREAKING: Wagonjwa wa Corona Zanzibar Wafika 58....Ni Baada ya Wenginge 23 Kuongezeka




Share:

Ununuzi wa Tiketi Kufanyika Kwa Njia ya Mtandao ili Kukabiliana na Corona

Katika  kukabiliana na mambukizi ya virusi vya Corona katika vituo vya mabasi serikali imesema mfumo wa ukatishaji tiketi kwa njia ya mtandao utaanza hivi karibuni kwa mabasi yote yanayofanya safari zake mikoani.
 
Mbali na mabasi hayo, daladala pamoja na mabasi ya mwendokasi yanatarajiwa (Data center) ambapo mfumo huo utarahisisha huduma na kuondoa adha ya wapiga debe vituoni.
 
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano , Mhandishi Isack Kamwele, wakati wa ukaguzi wa mifumo hiyo jana Dar es Salaam alisema hatua hiyo itafikiwa hivi karibuni ambapo kiu ya serikali ni kuona wananchi wananufaika kwa kuondoshewa adha ya usafiri.
 
Mhandisi Kamwelwe alisema serikali imefikia hatua ya mwisho ya kuanza kutumika kwa mfumo huo ambapo wananchi watatumia simu kukata tiketi za mabasi na hawatolazimika kutembelea vituoni jambo litakalowaepusha na wizi unaofanywa kupitia ulanguzi wa tiketi na wapiga debe.
 
“Nimeridhishwa na mfumo, huu ambao utasimamiwa na serikali kupitia kituo chetu cha Data center ukweli utasaidia sana wananchi wetu hususani wale wa chini ambao walikuwa wanaingia gharama kwenda katika vituoni kukata tiketi, tumefika wakati wa kuwa kisasa zaidi wapiga debe walikuwa wakiongeza gharama lakini wakati huu wa maambukizi ya corona ni muhimu kutafuta njia mbadala katika usafirishaji,”alisema.
 
Mhandisi Kamwele alisema, mfumo huo ameungahikia kwa muda mrefu hatimaye sasa unafika mwisho ambapo ameridhaka na uandaaji wa kimifumo kwakuwa taarifa zitatunzwa vizuri na kufanya kazi kwa ushirikishi wa wadau wa usafiri nchini.
 
“Hakuna sababu ya msafiri kutembea na pesa mkononi, hata wanaopandia njiani ni wakati wa kuwa na pesa kwenye simu, kwakuwa hatuna uhakika iwapo ugonjwa huu utaenea hadi kwenye noti ni lazima kuwa na njia nyingi za udhibiti,”alisema.
 
Alisema wamiliki wa mabasi walikuwa na maswali mengi wakati wa mchakato wa mfumo huo, wakihofia kupata hasara lakini ni wazi utendaji wake utanufaisha pande zote.


Share:

Rose Ndauka Afunga Ndoa na Mpenzi Wake wa Muda Mrefu Haffiyy Mkongwa

Muigizaji wa filamu za Bongo Movie, Rose Ndauka ameingia rasmi kwenye maisha ya ndoa na aliyekuwa mchumba wake wa muda mrefu anayefahamika kwa jina la Haffiyy Mkongwa.

Rose amefunga ndoa ya siri iliyohusisha watu wachache tu wa familia za wawili hao kutokana na kuwepo hatari ya mlipuko wa Ugonjwa wa Covid-19 unaosababishwa na Virusi vya Corona.



Share:

Waziri Zungu Akagua athari zilizosababishwa na korongo kubwa kando ya Mto Shaban Robert, Mpwapwa

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa Azzan Zungu mwishoni mwa wiki amefanya ziara ya kikazi wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma kukagua athari zilizosababishwa na korongo kubwa kando ya Mto Shaban Robert. 

Akizungumza wakati wa ziara hiyo aliagiza Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kufanya tathmini ya haraka kupata ufumbuzi wa tatizo hilo ili kunusuru wananchi kuzingirwa na maji yanayojaa katika mto huo. 

Waziri Zungu alisema pamoja na hayo Serikali kupitia Ofisi yake imeichukua changamoto hiyo na kuahidi kukaa na wataalamu wa mazingira kuanza utekelezaji wake. 

"Athari hii sio ndogo ni kubwa na inahitaji uangalifu mkubwa katika kuitatua kwani kila siku maji yanaongezeka katika mto huu, pia sisi kama Serikali tumetenga fedha za kukabiliana na maafa kama kupitia mifuko ya kitaifa na ya kimataifa hivyo tutazama tuone nini tunafanya," alisema. 

Aidha Waziri Zungu aliwataka wananchi kuendelea kushiriki katika suala zima la uhifadhi wa mazingira ikiwemo upandaji wa miti na kuitunza ili kuepusha athari za mabadiliko ya tabianchi. 

Aliongeza kuwa shughuli za binadamu zinachangia kwa kiasi kikubwa kwa matatizo hayo ambayo yamewaletea madhara ikiwemo kukatika kwa mawasiliano baina ya eneo moja hadi lingine baada ya madaraja kusombwa na maji ya mto yaliyofurika isivyo kawaida. 

Pia waziri huyo aliwaahidi wananchi kuwasiliana na Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) Mkoa wa Dodoma kufahamu wana mkakati gani katika kurudisha mawasiliano ya daraja lililosombwa na maji.  

"Ombi langu kwenu muendele kulinda mazingira kwani tukiharibu mazingira watoto wetu watateseka na dini zote zimesisitiza kulinda mazingira. Pia tuendelee kumuomba Mwenyezi Mungu atunusuru na janga hili la Corona ili Taifa letu liendelee na shughuli za kawaida na pia tuendelee kujikinga kama wanavyoelekeza wataalamu wa afya," alisisitiza. 

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Mpwapwa Mhe. George Lubeleje aliishukuru Serikali kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais kwa kutenga fedha kiasi cha sh. bilioni 17.4 kwa ajili ya wilaya tano ikiwemo Mpwapwa kutekeleza miradi ya kuhimili athari za mabadiliko ya tabianchi. 

Mbunge huyo aliwaomba wananchi kuacha kufyeka na kuchoma miti kwa ajili ya mkaa hususan katika maeneo ya milima kwa kuwa hatua hiyo inasababisha kuharibiwa kwa vyanzo ya maji.  

Meneja wa Wakala wa Barabara Mijini na Vijijini (TARURA) Wilaya ya Mpwapwa, Emmanuel Lukumay aliahidi kuwa watafanyia kazi changamoto hiyo kunusuru eneo la korongo kwa kutenga sh. milioni 457 kwa ajili ya kujenga daraja la kudumu. 

Lukumay alibainisha kuwa daraja hilo lililojengwa zaidi ya miaka 60 iliyopita na kusombwa na maji hivi karibuni lilikuwa ni kiungo muhimu kwa wananchi wa wilaya hiyo. 

Aliongeza kuwa TARURA daraja liko chini ya mradi wa barabara ya lami iliyoanza kujengwa katika wilaya hiyo na kusema kuwa tayari wameomba fedha kwa ajili ya kulijenga.


Share:

Waziri Wa Kilimo Japhet Hasunga Atembelea Kiwanda Cha Mbolea Cha Minjingu Mkoani Manyara

Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Manyara
Waziri wa kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) tarehe 18 Aprili 2020 ametembelea kiwanda cha mbolea cha Minjingu (Minjingu Mines and Fertilizer Ltd) kilichopo katika eneo na Kata ya Minjingu Mkoani Manyara ambapo pamoja na mambo mengine amejionea hali ya uzalishaji wa mbolea asilia ya kupandia aina ya Minjingu.

Mhe Hasunga ameshuhudia uzalishaji ukiwa umeongezeka kufikia Tani 100,000 kwa mwaka ambapo uongozi wa kiwanda hicho umetii agizo la Waziri Mkuu la kuwasihi kuboresha teknolojia ili kuzalisha Tani zaidi ya 150,000 ambazo zitaongeza kiwango cha upatikanaji wa mbolea hapa nchini kwwani bado upo chini kuliko mahitaji

Sambamba na hayo pia Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga ametoa mwito kwa uongozi wa kiwanda hicho cha mbolea Minjingu (Minjingu Mines and Fertilizer Ltd) kutoa elimu kwa umma juu ya ubora na umuhimu wa mbolea hiyo ya kupandia.

Mbolea hiyo inatokana na miamba inayochimbwa katika eneo la Minjingu Mkoani Manyara ambayo husagwa na kufungashwa kwenye kiwanda kilichojengwa katika eneo hilo. Mbolea ya Minjingu imeboreshwa kwa kuongezwa virutubisho vya Nitrogen, Salfa, Magnesi, Zinki na Boron (N, S, Mg, Zn, na B).

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda cha Mbolea cha Minjingu (Minjingu Mines and Fertilizer Ltd) Ndg Pardeep Singh Hans (Tosky) ameiomba serikali kupitia wizara ya kilimo kuwaruhusu maafisa ugani kote nchini kupatiwa mafunzo maalumu yatakayowaimarisha ili waweze kuwa sehemu ya kuitangaza mbolea bora ya Minjingu ambayo inazalishwa nchini.

Alisema kuwa serikali inapaswa kutazama upya utozaji wa VAT kwa wazalishaji wa bidhaa mbalimbali hapa nchini kwani tozo ya VAT wanayotozwa ni kubwa huku waagizaji wa mbolea nje ya nchi wao wanaingiza pasipo tozo kama hiyo.

Aidha, alisema kuwa tayari makala za vipindi vya Redio, Televisheni na Magazeti mbalimbali zimeanza kuandaliwa kwa ajili ya kuelimisha wakulima juu ya umuhimu wa mbolea hiyo ya Minjingu ambayo ni bora kuliko mbolea nyingine yoyote nchini na nje ya nchi.

Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga amesema kuwa serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli imejidhatiti katika viwanda, hivyo inathamini bidhaa zinazozalishwa na viwanda vya ndani.

Takribani asilimia 80 ya Watanzania ni wakulima. Shughuli hiyo ndiyo inawaingizia kipato ili waweze kukidhi mahitaji yao muhimu, ikiwamo kusomesha watoto wao, kugharamia matibabu na kadhalika.

Hata hivyo, wengi wamejikuta wakiishia kupata mazao yanayowatosha kwa chakula tu – bila ziada, huku wengine wakiishia kutupa nguvu na muda wao bure, hata hivyo Wizara ya Kilimo imeanzisha usajili wa wakulima ili kuwatambua na kuongeza ufanisi wa namna ya kuwahudumia, kadhalika kuanzisha bima ya Mazao ili wakulima wanapokumbwa na kadhia ya mavuno kidogo wawe na ahueni ya kulipwa kutokana na kuwa na bima.

Hali hiyo inatokea licha ya kulima eneo kubwa la ardhi ambalo kimsingi lingepaswa liwapatie chakula cha kutosheleza mahitaji yao katika familia pamoja na kupata ziada ambayo kama ingeuzwa ingewasaidia kwa mahitaji mengine muhimu.


Share:

SUA-Call for PhD and MSc Scholarship applications under the Climate Smart Rice Research Project

Call for PhD and MSc Scholarship applications under the Climate Smart Rice Research Project SOKOINE UNIVERSITY OF AGRICULTURE College of Agriculture Department of Crop Science and Horticulture The College of Agriculture at the Sokoine University of Agriculture (SUA), in collaboration with the International Rice Research Institute (IRRI), of the Philippines and the University of Copenhagen, Denmark has received… Read More »

The post SUA-Call for PhD and MSc Scholarship applications under the Climate Smart Rice Research Project appeared first on Udahiliportal.com.

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger