Sunday, 19 April 2020

SUA-Call for PhD and MSc Scholarship applications under the Climate Smart Rice Research Project

Call for PhD and MSc Scholarship applications under the Climate Smart Rice Research Project SOKOINE UNIVERSITY OF AGRICULTURE College of Agriculture Department of Crop Science and Horticulture The College of Agriculture at the Sokoine University of Agriculture (SUA), in collaboration with the International Rice Research Institute (IRRI), of the Philippines and the University of Copenhagen, Denmark has received… Read More »

The post SUA-Call for PhD and MSc Scholarship applications under the Climate Smart Rice Research Project appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Watu 34 Waruhusiwa Kutoka Karantini Mkoani Simiyu

Na Stella Kalinga, Simiyu RS
Mkuu  wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amesema kuwa jumla ya watu 34 kati ya watu 120 waliokuwa kwenye uangalizi maalum (Karantini) mkoani Simiyu wameruhusiwa mara baada ya kupimwa na kukutwa hawana maambukizi ya Virusi vya Corona vinavyosababisha homa kali ya mapafu (COVID-19).

Mtaka ameyasema hayo Aprili 18, 2020 wakati akizungumza na waumini wa Kanisa la Waadventista Wasabato (SDA) Bariadi Mjini, ambao wameitikia wito wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kwa Watanzania kuingia katika maombi ya siku tatu (Aprili 17-19, 2020) kuliombea Taifa ili Mungu aliponye na janga la Corona.

“Tulikuwa na watu 120 waliokuwa chini ya uangalizi ambao pia wamekuwa wakipata elimu kuhusu maambukizi ya virusi vya Corona ili wakitoka wakawe msaada kwa familia zao; mpaka sasa watu 34 wameruhusiwa baada ya kupimwa na kuthibitika kwamba hawana maambukizi ya Corona, sisi kama mkoa tunaendelea kuchukua tahadhari zote,”alisema Mtaka.

Ameongeza kuwa waliowekwa karantini ni pamoja na wanaofanya biashara nchi jirani ambao waliomba wenyewe ili wajitenge na familia zao; pia wapo baadhi ambao familia ziliomba Serikali iwaweke kutokana na kujua kuwa wametoka nchi zenye maambukizi kwa hofu ya kupeleka maambukizi kwa familia zao ikiwa itatokea wameambukizwa virusi vya Corona.

 Aidha, Mtaka amesema kuwa mpaka sasa mkoa wa Simiyu hauna mtu mwenye maambukizi ya Virusi vya Corona na kutoa wito kwa wananchi kuendelea kuchukua tahadhari huku wakimuomba Mungu bila kukoma ili aliponye Taifa na janga la kidunia la ugonjwa wa COVID 19.

Katika hatua nyingine Mtaka amewahimiza wazazi kuwasimamia watoto wao na kuhakikisha wanajisomea wakiwa nyumbani huku akiwaasa kutunza chakula na kuepuka kuuza mazao pasipo na ulazima wa kufanya hivyo.

Mchungaji wa Kanisa la SDA Bariadi Mjini, Marco Mlingwa amesema Kanisa hilo limepokea maelekezo ya Serikali na linaungana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kuliombea Taifa Mungu aliponye na janga la Corona.

Kwa upande wao waumini wa Kanisa la SDA Bariadi Mjini wamemshukuru Mhe. Rais kuruhusu ibada kufanyika kwa kuzingatia maelekezo ya watalaam wa afya na kubainisha kuwa wataendelea kumuomba Mungu aliepushe Taifa na Corona wakiamini kuwa Mungu atasikia wakiomba kwa imani na kwa bidii.

“Tunamshukuru Mhe. Rais kuruhusu ibada kuendelea kufanyika huku tukichukua tahadhari,  sisi Wakristo tunaamini watu tukiomba kwa bidii Mungu anasikia maombi, hivyo tukikutana na kuomba kwa bidii Mungu atasikia na kutuokoa na ugonjwa huu wa COVID 19,” alisema Paul Jidayi muumini SDA na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Maswa.

“Sisi kama Wasabato tuna vipindi vyetu vya afya na kupitia vipindi hivyo tumeshajifunza na kuchukua tahadhari dhidi ya Corona kanisani na majumbani; pia tunaungana na Rais kuliombea Taifa tukiamini kuwa Mungu atatusikia maana hata zamani, nchi ya Ninawi walipelekewa taarifa kuwa wataangamizwa lakini walipomlilia Mungu aliwasikia na  hawakuangamia,” alisema Mariam Manyangu.


Share:

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumapili April 19














Share:

Saturday, 18 April 2020

NARCO IJIANDAE KUWA KITOVU CHA KUUZA MIFUGO NA BIDHAA ZAKE BAADA YA CORONA” PROF.OLE GABRIEL


Kaimu Meneja Mkuu wa hifadhi ya ranchi za taifa (NARCO) CPA Masele Mipawa akitoa ufafanuzi juu ya namna walivyoanza kutekeleza agizo la kuweka alama za kuonekana kwenye ranchi hizo wakati wa kikao baina ya Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo) Prof. Elisante Ole Gabriel, viongozi wa Wilaya ya Muleba na timu ya wataalam wanaoendelea na zoezi la kurekebisha ramani ya ranchi ya Mwisa II leo.
Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo) (Katikati) Prof. Elisante Ole Gabriel akiwa kwenye picha ya pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Muleba Bw. Emmanuel Shelembi (Kushoto), Mkuu wa Wilaya ya Muleba Mhe. Mhandisi Richard Ruyango leo (18.04.2020) huku wakitekeleza agizo la Wizara ya afya, la kusimama mita moja baina ya mtu mmoja na mwingine ili kuepuka maambukizi ya virusi vya Corona.

Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo) (Katikati) Prof. Elisante Ole Gabriel akiwa kwenye picha ya pamoja na timu ya wataalam wanaoendelea na zoezi la kurekebisha ramani ya ranchi ya Mwisa II muda mfupi baada ya kumalizika kikao baina yao leo
...................................................................................
Na.Mwaandishi Wetu,Muleba
Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo) Prof. Elisante Ole Gabriel ameitaka hifadhi ya ranchi za taifa (NARCO) kwa kushirikiana wadau wengine wa sekta ya Mifugo kuhakikisha Nchi inakuwa na Mifugo ya kutosha na yenye afya kwa ajili ya kukidhi mahitaji ya bidhaa zitokanazo na mifugo wakati huu wa janga la Ugonjwa wa homa kali ya mapafu unaosababishwa na virusi vya Corona (Covid 19) na hata mara baada ya janga hilo kuisha.
Prof. Elisante Ole Gabriel aliyasema hayo mapema leo alipofanya ziara katika Wilaya ya Muleba mkoani Kagera lengo likiwa ni kukagua utekelezaji marekebisho ya upimaji wa ramani ya Ranchi ya Mwisa II ili kutenga eneo lililopendekezwa kuhamishia wananchi waishio ndani ya Ranchi hiyo.
"Wakati huu wa hili janga la Corona mahitaji ya nyama Afrika na duniani ni makubwa sana na yanaweza kuongezeka maradufu mara baada ya janga hili kuisha hivyo ni lazima tujipange ili kuhakikisha tunakuwa kitovu cha usambazaji wa bidhaa zitokanazo na mifugo duniani na NARCO mnapaswa kujitokeza kifua mbele kuwa hilo mnaliweza na lipo ndani ya uwezo wenu" Aliongezea Prof. Ole Gabriel.
Alisisitiza katika kutekeleza hilo NARCO wanapaswa kutafakari vizuri na kuchagua ranchi moja ya kimkakati kati ya 14 zilizopo hapa nchini ambayo watawekeza kwa dhati ili waweze kunenepesha ng'ombe wengi watakaosafirishwa nje ya nchi zenye mahitaji makubwa ya mifugo na bidhaa zake kwa sasa.
"Lakini pia katika kuelekea kwenye uchumi wa kati unaotegemea viwanda 2025 ni lazima NARCO iainishe ranchi tano za mfano ambazo wananchi na wadau mbalimbali watafika kwa ajili ya kujifunza juu ya ufugaji wa kisasa na pia zitumike kama shule hata kwa wanaokodisha ranchi nyingine ili nao wafike kujifunza namna ya ufugaji bora utakaolenga kuzalisha mifugo itakayowawezesha kunufaika kiuchumi" Alisisitiza Prof.Ole Gabriel.
Awali akisoma taarifa ya utekelezaji wa marekebisho ya upimaji wa ramani ya Ranchi ya Mwisa II, kiongozi wa timu ya wataalam wanaofanya kazi hiyo Bw. Fikiri Mwasenga alisema kuwa kazi hiyo inatarajiwa kukamilika ndani ya siku 30 kuanzia hivi sasa na mpaka sasa tayari timu hiyo imeshakamilisha kumega maeneo ya vitongoji vitatu ambavyo ni Butera, Bionza na Rwenzige na kazi ya kupima maeneo mawili yaliyobaki inaendelea ili kuweza kukamilisha maeneo yote matano yaliyopendekezwa kutengwa.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Muleba Mhe. Mhandisi Richard Ruyango aliishukuru Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa hatua yake ya upimaji wa maeneo hayo ya ranchi ya Mwisa II kwani hatua hiyo itaondoa na kumaliza kabisa migogoro iliyokuwepo baina ya wakulima na wafugaji waliopo kwenye maeneo ya ranchi hiyo.
Ranchi ya Mwisa II ni miongoni mwa ranchi 14 zilizopo chini ya hifadhi ya ranchi za taifa (NARCO) ambapo ina ukubwa wa hekta 133,000 na inatajwa kuwa ranchi kubwa kuliko zote hapa nchini.
Share:

DEREVA BODABODA MWENYE VIRUSI VYA CORONA AKAMATWA AKISAFIRISHA JENEZA FEKI

Polisi nchini Kenya imemkamata dereva aliyekuwa na virusi vya corona pamoja na abiria watatu waliojidai kuwa waombolezaji wanaoelekea kwa mazishi.

Watatu hao waliokuwa wamesafiri zaidi ya kilomita 370 kutoka kutoka Nairobi wakiwa na jeneza bila maiti walikamatwa katika jimbo la Homa Bay magharibi mwa Kenya.

Tukio hilo la kushangaza liliangaziwa na Waziri wa Afya wa Kenya Bw. Mutahi Kagwe ambaye pia alithibitisha kuwa kundi hilo lilifanikiwa kuhadaa polisi kwa kutumia jeneza tupu na kupita vizuizi kadhaa njiani.

Aliongeza kuwa dereva huyo ametengwa na abiria wake kuwekwa karantini.

Karibu wiki mbili zilizopita serikali ya Kenya ilitangaza hatua kali za kudhibiti watu kuingia na kutoka katika mji mkuu wa Nairobi pamoja na majimbo menginine matatu ambayo yanasadikiwa kuwa na viwango vya juu vya maambukizi ya ugonjwa wa Covid-19.

Waziri wa Afya alisema serikali inachunguza madai kwamba baadhi ya watu wanatoa hongo kwa polisi wanaolsimamia vizuizi vya barabarani.

Malori yanayoenda safari za mwendo mrefu pia pia zinachunguzwa kutokana na madai ya kuwasafirisha watu kinyemela kutoka jijini Nairobi

Kufikia sasa Kenya ina jumla ya wagonjwa 262 wa covid-19 baada ya watu 16 wapya kuthibitishwa kuwa na virusi Jumamosi.
Chanzo - BBC
Share:

Kanisa Katoliki Kagera lasitisha ibada na Sala za Jumuiya Ili Kukabiliana na Kusambaa kwa Corona

Kanisa Katoliki Jimbo Katoliki la Rulenge- Ngara mkoani Kagera, limesitisha ibada za misa, maadhimisho mengine yanayokusanya waumini wengi kanisani na sala za jumuiya kwa muda wa mwezi mmoja kuanzia Jumapili Aprili 19

Katika taarifa yake Askofu wa jimbo hilo, Severine Niwemugizi amesema baada ya muda uliopangwa kumalizika wataangalia hali itakavyokuwa na ikibidi muda wa kusitisha ibada utaongezwa.

“Baada ya kutafakari alama za nyakati na kujifunza kutoka kwa wenzetu Ulaya na Marekani, nchi jirani zetu na hatua ambazo Baba Mtakatifu alizichukua kwa kutoa maelekezo kwa Maaskofu Wakatoliki duniani namna ya kuadhimisha ibada katika kipindi hiki cha vita dhidi ya corona, nimebeba dhamana ya kutoa uamuzi mgumu.

“Tutaomba redio Kwizera irushe adhimisho la misa fupi ili waumini wafuatilie redioni na baada ya muda huo kumalizika tutaona hali itakuaje na ikibidi tuongeze muda tutafanya hivyo,” amesema Askofu Niwemugizi.

Aidha amewataka mapadre kuadhimisha misa peke yao kwa niaba ya waumini kuwaombea na kuiombea dunia ili Mungu atunusuru na janga hili na kuagiza sala za Jumuiya kufanyika ndani ya familia kwa familia moja moja.



Share:

Wenye Virusi Vya Corona Nchini Kenya Wafika 262....Ni Baada ya Wengine 16 Kuongezeka Leo

Watu 262 wamebainika kuwa na ugonjwa wa virusi vya Corona nchini Kenya baada ya kuongezeka maambukizi mapya 16 ndani ya saa 24.

 Vifo sasa vimefikia 12, waliopona Corona 60. Watu hao 16 waliobainika kuwa na Corona nchini humo 15 wanatoka Kenya na mmoja ni raia wa kigeni.


Share:

Tume ya Ushindani nchini (FCC) Yatoa ONYO Kwa Wafanyabiashara wanaopandisha bei ya Sukari

Tume ya Ushindani Nchini (FCC) imetoa onyo kwa Wasambazaji na Wauzaji wa jumla na rejareja wa sukari nchini kuwa ni kosa kisheria kujihusisha na vitendo vya upandishaji bei na kuwataka kuacha mara moja

Imesema kitendo cha hivi karibuni cha baadhi ya Wafanyabiashara kupandisha bei ya sukari hadi kufikia Tsh. 4,000 kwa KG 1 ili kujipatia faida kubwa isivyo halali kwa kuwaumiza walaji pindi mahitaji ya sukari yatakapoongezeka ni kosa


Share:

Uganda kumrejesha Nchini Mtanzania aliyekutwa na corona

Wizara ya Afya ya Uganda imesema kuwa itamrejesha nchini Mtanzania aliyebainika kuwa na maambukizi ya virusi vya corona baada ya kufanyiwa vipimo katika mpaka wa Mutukula.

Aprili 17 wizara hiyo ilithibitisha kisa kimoja ambapo taarifa ya awali ilieleza kuwa maambukizi hayo yametokea miongoni mwa jamii nchini humo, taarifa ambayo baadae ilikanushwa kuwa haikuwa sahihi.

Katika taarifa mpya wizara hiyo imesema aliyebainika kuwa na maambukizi hayo ni dereva wa lori mwenye miaka 34 ambaye ni raia wa Tanzania, na aliwasili Mutukula Aprili 16 akitokea jijini Dar es Salaam.

Dereva huyo hakuwa na dalili yoyote yenye kuonesha kuwa alikuwa na maambukizi ya homa ya mapafu (COVID-19), na sasa jitihada za kumtafuta na kurejesha nchini Tanzania zinaendelea, wizara imesema.

Kutokana na msahihisho hayo, visa vya watu wenye maambukizi ya COVID-19 nchini Uganda vinabaki kuwa 55.

Hatua ya Uganda kuwarudisha nyumbani raia wa kigeni waliopatikana na ugonjwa wa corona imezua gumzo kali katika mitandao ya kijamii ndani na nje ya nchi hiyo.

Siku ya Alhamisi waziri wa Afya wa Uganda  Ruth Jane Aceng alisema kuwa Uganda kila siku huwapokea hadi madereva 3,000 wa malori kutoka mataifa ya kanda ya Afrika Mashariki na kwamba nchi hiyo haitaweza kuwapa huduma za matibabu. 


Share:

Hospitali Ya Amana Ipo Tayari Kupokea Wagonjwa Wa Corona

NA ZAMARADI KAWAWA, MAELEZO
Serikali imehamisha wagonjwa wote waliokuwa wakipata huduma za afya katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dar es Salaam, Amana iliyopo Manispaa ya Ilala, ili kuanza kutekeleza jukumu la kutumia hospitali hiyo kutoa huduma za afya kwa wagonjwa wa Corona (COVID – 19).

Akizungumza na Watumishi wa hospitali hiyo mara baada ya kutembelea majengo yatakayotumika kuwalaza wagonjwa wa Corona (COVID-19), Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Zainab Chaula amesema wagonjwa waliokuwa wanapata huduma katika hospitali hiyo wamehamishiwa katika hospitali nyingine za Serikali jijini Dar es Salaam.

Amesema Serikali imetoa kiasi cha Shilingi Milioni Mia Mbili (200m/-=) kwa ajili ya ukarabati mdogo wa baadhi ya majengo ya hospitali hiyo. Dkt. Chaula amewataka watumishi wa sekta ya afya kukumbuka kujikinga na maambukizi ya ugonjwa huo kwa kuvaa vifaa vya kujikinga na maambukizi wakati wa kuwahudumia wagonjwa
wa COVID-19 hospitalini hapo.
 
Amewakumbusha watumishi wa sekta ya afya nchini kutimiza wajibu wao katika kipindi hiki cha janga la ugonjwa wa Corona huku wakizingatia kiapo cha utii wa majukumu yao ya utoaji huduma za afya kwa wagonjwa.

Amesema Serikali ipo tayari kuwezesha huduma za afya kutolewa kikamilifu kwa wagonjwa wa Corona nchini na kuwa Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imefanya juhudi mbali mbali za kupunguza maambukizi ya virusi vya ugonjwa huo nchini zilizosababisha kuwa na wagonjwa wachache hadi sasa ukilinganisha na nchi nyingine.

Akizungumzia uamuzi huo wa Serikali Ijumaa wiki hii, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Bi Ummy Mwalimu alisema Serikali imeelekeza Hospitali ya Taifa Muhimbili kuacha kupokea wagonjwa wenye dalili za virusi vya Corona (CODIV-19) ili iweze kutekeleza majukumu yake ya kutoa huduma za kibingwa na huduma bobezi kwa wagonjwa wa magonjwa mengine nchini.

Alisema, badala yake Serikali imeamua kutumia Hospitali ya Amana kama kituo maalum cha matibabu ya ugonjwa wa CODIV-19. Wananchi wa mkoa wa Dar es Salaam wanaohitaji kupata huduma za matibabu ya magonjwa mengine katika Hospitali ya Amana wanatakiwa kutumia hospitali nyingine zilizopo mkoani humo.


Share:

Michango ya bilioni 3.2 yakusanywa kutoka kwa wadau mbalimbali kuunga mkono juhudi za Serikali katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa Corona.




Share:

Makonda: Kuanzia Jumatatu kila mtu lazima avae mask na biashara zote zifanyike kwa 'take away'

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda leo Aprili 18, 2020 amesema, kuanzia Jumatatu, Aprili 20, 2020 kila anayekwenda sehemu ya manunuzi, lazima avae barakora na kuwataka wafanyabiashara kufanya biashara  zote kwa njia ya 'take away'.

“Anayekwenda eneo la manunuzi yotote lazima awe amevaa barakoa (mask), ununue,ukate leso, ukate kanga utaamua wewe, lakini lazima uwe umevaa


"Pia kuanzia Jumatatu biashara zote zifanyike katika mfumo wa ‘take away’ ukienda sehemu nunua ondoka, lazima pia kuwe na hatua mita mbili katika msongamano wa Watu”- Amesema RC Paul Makonda 

Amewataka wenye masoko kutumia njia mbadala wa kufanya kazi kwenye masoko yao ili kujikinga na corona


Share:

Serikali Yazindua Muongozo Wa Mpango Huduma Za Afya Katika Jamii Pamoja Na Matumizi Ya Dashbodi Ya Viashiria Ya Afya

Serikali ya awamu ya Tano imesema kuwa itaendelea kutoa kipaumbele katika kuimarisha huduma za kinga, ikiwemo elimu ya afya na uhamasishaji, lishe, udhibiti wa magonjwa ya kuambukiza kama Ukimwi na afya ya mama na mtoto.

 Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu katika uzinduzi wa muongozo wa mpango wa huduma za afya katika jamii na matumizi ya dashibodi ya viashiria vya elimu ya afya kwa umma jijini Dar es Salaam leo.

“Hii itasaidia juhudi za kupunguza mzigo wa gharama za matibabu unaowatesa wananchi na kuongeza matumizi ya serikali katika tiba ya magonjwa yanayoweza kuzuilika au kuepukwa,” alisema waziri.

Alisisitiza kuwa umuhimu wa huduma za kinga ambao umezingatiwa katika Sera ya Taifa ya Afya ya mwaka 2007 na Mpango Mkakati wa Sekta ya Afya wa Mwaka 2015 – 2020 utakuwa kipaumbele katika maandalizi ya Sera Mpya ya Afya ya Mwaka 2020.

 Mkakati huu wa kutumia watoa huduma za afya kwa jamii utawezesha kuwepo kwa huduma imara za kinga katika ngazi zote ikiwemo utoaji elimu ya afya na uhamasishaji kama njia muhimu ya kusaidia jamii zetu kujikinga na magonjwa.

Serikali inatambua kuwa jamii yenye elimu sahihi juu ya vyanzo vya afya bora na masuala yanayoweza kuathiri afya hufanya maamuzi sahihi juu ya mambo yanayohusu afya zao. 

Hii itawezesha Taifa letu kuwa na wananchi wenye afya njema wanaochangia katika maendeleo yao, familia zao, jamii wanayoishi na nchi yetu kwa ujumla.

Amesema kuwa serikali imeendelea kuimarisha huduma za afya ili kufikia malengo ya upatikanaji wa huduma za afya kwa wananchi wote yaani Universal Health Coverage ambavyo itajumuisha utoaji elimu ya afya juu ya mambo yahusuyo lishe, afya ya uzazi, watoto na vijana ikijumuisha magonjwa ya mlipuko kama COVID-19 pamoja na magonjwa yasiyoambukiza.

 Pia jitihada hizi zinalenga kuhamasisha matumizi ya bima za afya ili kuwawezesha wananchi kutumia huduma mbalimbali za afya wanapohitaji. 

Kwa mfano katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita tumeshuhudia ongezeko la idadi ya watu waliopatiwa huduma za magonjwa yasiyoambukizakutoka watu milioni 3.4 (3,386,067) mwaka 2016 hadi wagonjwa Milioni 4.2 (4,190,467) mwaka 2018 ikiwa ni sawa na ongezeko la asilimia 24 ya wagonjwa hao.

Sambamba na takwimu za wagonjwa, pia tumeshuhudia ongezeko la vifo vitokanavyo na magonjwa yasiyoambukiza hadi kufikia asilimia 33 ya vifo vyote nchini kwa mwaka 2017, ambapo jumla ya vifo 134,600 viliripotiwa na kuhusishwa na magonjwa yasiyoambukiza.

 Huku vifo vitokanavyo na magonjwa ya moyo na shinikizo la damu vikichangia kwa asilimia 13, idadi ambayo ni kubwa kuliko ile itokanayo na magonjwa kama Ukimwi, Kifua Kikuu au Malaria.

 Waziri Mwalimu alisema kuwa matatizo yote haya yanaweza kupunguzwa kwa kiasi kikubwa sana endapo tutaimarisha mifumo ya kutoa elimu na taarifa sahihi kwa jamii zetu juu ya namna ya kuepuka kwa kufuata kanuni bora za afya pamoja na kuwatumia vyema wahudumu afya za jamii kuanzia ngazi za kijiji na mtaa.

 Na hayo yote sasa serikali inataka yakafanywe  na wahudumu wa afya wa jamii ambao baada ya tathmini mpya kufanyika wataongezwa kwa baadhi ya vijiji ambavyo ni vikubwa na pia watapatiwa mafunzo maalumu namna ya kukabiliana kutoa elimu sahihi kwa wananchi kuhusu magonjwa Haya.

“Pia Wahudumu wa afya ya jamii hawa waende wakahamashishe jamii zetu kujenga desturi ya kutafuta huduma rasmi za afya ikiwa ni pamoja na kujiunga kwenye mifuko yetu ya bima za afya ili kurahisisha upatikanaji wa huduma za afya,” alisisitiza.

Wakati huo huo, Mkurugenzi wa Miradi ya USAID Tulonge Afya Bw Waziri Nyoni ameipongeza serikali kwa maamuzi ya kuufanya mfumo huu wa wahudumu wa afya wa jamii kwa kuufanya uwe rasmi tofauti na awali ambapo kila mdau alikuwa akitumia mfumo wake hivyo kuwa na changamoto nyingi.

Alisema kuwa USAID Tulonge Afya imekuwa ikitumia mfumo wa wahudumu wa afya ya jamii kufanikisha miradi yake mingi ya afya hapa nchini.

Kwa mfano hadi sasa kuna takribani watoa huduma wa afya ya jamii 2200 waliopo katika mikoa 12 na wilaya 29 huku wakitoa baadhi ya huduma wanazozitoa ikiwa ni pamoja na uhamasishaji masuala ya Afya kama malaria, Afya ya mama na mtoto, ukimwi, kifua kijua, na mengine mengi.

Naye Mkurugenzi wa Utafiti, tathmini na Ufuatiliaji, FHI360, Dr Joseph Msofe alisema kuwa kupitia mradi wa USAID Tulonge Afya, wameshirikiana na wizara kuandaa mfumo wa upokeaji na utoaji wa taarifa ambao umeunganishwa katika mfumo rasmi wa Wizara yaani DHIS2.

Kutokana na hili, watoa huduma za afya ngazi ya Jamii au mdau yoyote atakua anafanya shughuli za uhamasishaji jamii ina maana atatakiwa kufuata mfumo na utaratibi huu mzuri na taarifa zote zitaonekana katika ngazi ya wilaya hadi taifa na hivyo kuwawezesha watendaji na watoa maamuzi kujua ni nani anafanya nini na wapi na hivyo kusaidia katika kufanya maamuzi sahihi..

 Lakini pia mfumo huu wa ufuatiliaji na utoaji taarifa utasaidia watendaji ngazi zote katika masuala ya afya kuufanya ufuatiliaji ili kubaini penye mapungufu hivyo kuongeza kufahamu maeneo ambayo ufanisi.


Share:

Idadi ya maambukizo ya Corona Marekani yapindukia laki saba

Idadi ya watu waliombukizwa virusi vya Corona nchini Marekani imepindukia laki saba huku idadi ya wanaoaga dunia kwa ugonjwa wa Covid-19 ikiongezeka kwa kasi nchini humo.

Takwimu za hivi punde zinaonyesha kuwa, watu 710,272 wameambukizwa virusi vya Corona nchini Marekani huku 37,175 wakiaga dunia na kuifanya nchi hiyo kuwa ndio iliyoathiriwa zaidi na virusi hivyo duniani.

Italia inashika nafasi ya pili kwa idadi kubwa ya watu walioaga dunia kwa virusi vya Corona ambapo hadi sasa watu 22,745 wamefariki dunia nchini humo, ingawa kwa upande wa idadi ya maambukizo inashika nafasi ya tatu. 

Uhispania yenye idadi 20,002 ya vifo vya Corona, jumla ya watu 190,839 wameambukizwa virusi vya Corona katika nchi hiyo ya bara la Ulaya.

Nchi zinazofuata ni Ufaransa, Ujerumani na Uingereza na kulifanya bara la Ulaya kwa sasa kuwa kitovu cha virusi vya Corona.


Share:

WHO: Afrika huenda ikaathirika zaidi na virusi vya Corona

Shirika la Afya Duniani, WHO, limeonya kwamba bara la Afrika huenda likawa na idadi kubwa ya maambukizi ya virusi vya Corona. 


WHO inabashiri kuwa hali ikiendelea ilivyo sasa, huenda idadi ya vifo ikafikia 300,000 na watu wengine zaidi ya Milioni 30 kuwa masikini.

Kufikia sasa Afrika ina vifo karibu elfu moja vinavyohusishwa na Corona, huku watu zaidi ya elfu 19 wakiambukizwa ugonjwa huo.

Wakati huo huo Shirika la Fedha la Kimataifa, IMF, limetaka Afrika isaidiwe kukabiliana na ugonjwa hatari wa Covid-19.

IMF imetoa wito wa msaada wa haraka wa kimataifa kwa nchi za Afrika ambazo zinakabiliwa na janga hilo.

Mkurugenzi mkuu wa IMF Kristalina Georgieva amewaambia mawaziri, maafisa wa Umoja wa Mataifa na wengine kwamba bara la Afrika halina raslimali za kutosha na miundo mbinu ya kutosha ya afya ili kukabiliana na janga hilo na kwamba linahitaji karibu dola bilioni 114.

Maambukizi ya virusi vya Corona kote ulimwenguni sasa yamepindukia milioni 2.18 na watu 150,000 wamepoteza maisha.


Share:

Mkuu Wa Mkoa Wa Mbeya Albert Chalamila Atoa Amri Baa Zote Zifungwe Saa Tatu Usiku Ili Kukabiliana Na Corona

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Albert Chalamila ametoa amri kwa wamiliki wa maeneo yote yanayouzwa pombe (Bar) kufunga biashara zao kila ifikapo saa tatu kamili usiku kuanzia jumatatu  kwa lengo la kuepusha misongamano inayoweza kusababisha watu kuambukizana corona. 

Ametoa agizo hilo jana April 17, 2020 baada ya kutembelea bar kadhaa na kukuta watu wakiwa kwenye misongamono iliyopigwa marufuku

"Walevi wanaoanza kunywa pombe kuanzia saa tatu kwenda mbele huwa hawana utambuzi wa kuachiana nafasi na kwa mantiki hiyo hupiga story na kushikashikana" -Alisema


Share:

ASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA KUINGIZA SUKARI YA MAGENDO KUPITIA BANDARI YA KIGOMBE MUHEZA


 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Polisi (ACP) Blasius Chatanda akizungumza na waandishi wa habari ambao hawapo pichani kuhusu operesheni walioiendesha ya kupambana na biashara haramu za magendo


Sehemu ya waandishi wa habari Jijini Tanga wakifuatilia matukio mbalimbali kwenye mkutano huo

JESHI la Polisi Mkoani Tanga linamshikilia mkazi wa Kijiji cha Kigombe Kata ya Kigombe wilayani Muheza mkoani Tanga ambaye aliyeshirikiana na wenzake ambao walikimbia wakiwa wameingiza bidhaa za magendo kutoka nchini India kwa kutumia bandari Bubu ya Kigombe.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Polisi (ACP) Blasius Chatanda alisema kwamba hatua ya kukamatwa kwa mkazi huyo ni kutokana na operesheni zinazoendelea kufanywa na Jeshi la Polisi kuhakikisha wanazibiti biashara za magendo.

Alisema kwamba tukio hilo lilitokea Aprili 17 Saa tisa mchana kwenye maeneo ya Mwarongo Kata ya Marungu Tarafa ya Pongwe ambapo wakiwa kwenye operesheni hiyo walifanikiwa kumkamata mtu huyo akiwa na mifuko 88 ya sukari yenye kg 50 ambayo imeonekana kutenegenezwa nchini India ikiwa inaingizwa nchini kwa njia za magendo.

Kamanda huyo alitaja bidhaa nyengine ambazo zilikamatwa kuwa ni Madumu 45 ya Oili ya Magari yenye kg 20 kila mmoja na mifuko mitano ya mchele yeye ujazo wa kg 50 kila mmoja ikitokea nchini Pakistani.

Kamanda Chatanda alimtaja mtuhumiwa ambaye alikamatwa kuwa ni Hassani Tausilo aliyeshirikiana huku wenzake ambao alikuwa akishirikiana nao kukimbia na kutokomea kusikojulikana ambao kwa sasa bado wanasakatwa na jeshi hilo kutokana na kufanya biashara haramu ya magendo

“Sehemu ya sukari ilikamatwa inasafirishwa kwenye pikipiki tayari ilishashuhwa kwenye Ngalawa na kwenda kufichwa kwenye mapori yaliyopo kwenye kijiji cha Kigombe na kuanza kusafrisjwa kwa kutumia pikipiki ambazo pia nazo tulifanikiwa kuzikamata na mpaka sasa tunazishikia”Alisema kamanda huyo.

Aidha alisema hivi sasa wanachoendelea nacho ni msako ulioanza kwenye mapori na kufanikiwa kukamatwa mifuko mengine 78 baada ya mifuko 10 kukamatwa kwenye pikipiki na mtuhumiw aliyekuwa kwenye pikipiki hiyo naye alikimbia huku pia na mafumu 45 na huo mchele.

Hata hivyo Kamanda huyo alitoa wito kwa wafanyabiashara watambue kwamba biashara ya magendo sio biashara tena na itawaingiza kwenye umaskini hivyo waachane nayo huku akisisitiza kwamba operesheni hiyo ni endelevu na kamwe haitawapa nafasi na kila anakayejiingia atambua kwamba kwenye biashara hiyo atambua kwamba atakamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya dola.

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger