Friday, 10 April 2020

RC Wangabo awataka wananchi kulinda mipaka huku 49 wakiwekwa karantini Mkoani Rukwa

Mkuu wa mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo amewataka viongozi wa vitongoji, vijiji pamoja na watendaji wao wa kata za Korongwe na Kabwe kuhakikisha wanawahamasisha wananchi katika maeneo yao kuwa mstari wa mbele katika kuilinda nchi kutokana na ugonjwa wa Corona kwa kuzuia uingiaji holela wa wageni wanaoweza kuuleta ugonjwa huo kutoka nchi za jirani.

Mh Wangabo amesema kuwa hadi sasa mkoa wa Rukwa umewaweka Karantini watu 49 ambapo kati ya hao watanzania 36 na wageni 13 ambao walipita katika bandari na mipaka rasmi ya mkoa huo na kusisitiza kuwa katika utekelezaji wa kuwaweka watu Karantini hauangalii uraia wa mtu wala hadhi yake, na kuongeza kuwa inachokijali serikali ni usalama wa wananchi wake dhidi ya ugonjwa hatari wa Corona.

Hivyo amewataka viongozi hao kuwaelimisha wananchi kuwakataa wageni wasiotumia mipaka na bandari rasmi kuingia katika nchi kwani kutofanya hivyo kutailetea nchi maafa makubwa na hivyo na hivyo kuwataka viongozi na wananchi kuacha matumizi ya bandari bubu zilizopo katika vijiji vya mwambao wa ziwa Tanganyika.

“Waende wakapite katika maeneo ambayo ni rasmi, waje hapa kwenye bandari ya Kabwe, wapite hapo na taratibu nyingine za kiafya zitafanyika, lakini sio kwenye bandari bubu huku, bandari bubu ni marufuku kutumika, ndani ya wilaya hii ya Nkasi kuna bandari bubu 46, Nkasi peke yake na katika kata zenu mbili hizi, ya Korongwe na Kabwe kuna bandari bubu 13, ndio maana nikasema viongozi ninyi wa kata mbili hizi mje hapa, ili muone umuhimu wa kuzuia watu kiholela holeal kuja kwenye bandari hizi bubu,” Alisisitiza.

Mh. Wangabo ameyasema hayo wakati wa kikao na wenyeviti wa vitongoji na vijiji vyenye bandari bubu pamoja na watendaji wa kata Kabwe na Korongwe zinazobeba vijiji hivyo katika kikao kilicholenga kutoa elimu ya ugonjwa wa Corona kwa viongozi hao pamoja na kutoa maelekezo ya serikali dhidi ya mapambano ya ugonjwa huo.

Kwa upande wake Kamanda wa Jeshi la Uhamiaji Mkoa wa Rukwa Kamishna Msaidizi Elizeus Mushongi alitahadharisha matumizi mabaya ya madaraka ya viongozi hao ambao huwapokea wageni hao na kuwaruhusu kuingia katika nchi bila ya kufuata utaratibu wa serikali na kuongeza kuwa matumizi ya bandari bubu ni haram una hivyo atakayekamatwa anahalalisha matumizi ya bandari hizo hatua kali zitachukuliwa dhidi yake.

“Wageni kutoka nje ya nchi, iwe Kongo, iwe Burundi, iwe Zambia, mnawapokea kule na nyinyi ndio mnakuwa maafisa uhamiaji, mnakuwa maafisa forodha, kila kitu mnamaliza wenyewe kule, sasa kama mtampokea mtu anaumwa ule ugonjwa, ninyi ndio mtakaoanza kuupokea ule ugonjwa kabla ya wote na bila ya kujua mtaenda kuambukiza familia na familia kama dokta alivyosema, niwaombe sana msipokee watu kutoka nje ya nchi kama hawajapita katika vituo vilivyoainishwa kisheria,” Alisema.

Aidha wakati akitoa salamu zake kwa mkuu wa mkoa, Diwani wa Viti Maalum Mh. Christina Simbakavu alisema kuwa kuna baadhi ya watu wenye ndugu zao nchi ya jirani ya Kongo huwa na kawaida ya kuingia katika vijiji hivyo nyakati za usiku na ndugu zao huwapokea katika utaratibu ambao unaweza kuhatarisha maisha yao.

“Kuna boti zinazoingia usiku kama alivyotamka mjumbe wa Kijiji cha Kalila, zile boti zinaingia lakini wenyeji wenye ndugu zao kutoka nchi jirani ya kongo wanawapokea katika mazingira ambayo sio Rafiki sana na hawatoi taarifa, na hili nalo linafukuta lakini hatujapata uhakika uliowazi, tunajaribu kuongea na wananchi kuwa tusipokee wageni wa aina yoyote na nawaomba viongozi wangu tuhamasishe utumiaji wa maji na sabuni kunawa na katika nyumba zetu tuweke vifaa hivyo,” alisema.

Naye Diwani wa Kata ya Korongwe Mh. Venus Bamilitwaye wakati akitoa neno la shukurani ka mkuu wa mkoa wa rukwa aliwasisitiza viongozi wa kata hizo kuhakikisha wanashirikiana na wananchi katika kulinda bandari bubu pamoja na kuzuia uingiaji wa kiholela wa wageni jambo ambalo ni hatari kwa afya ya wananchi wa mkoa wa Rukwa na Tanzania.


Share:

Tanzania Yatoa Biilioni 10 Kuifufua Upya Tazara

Serikali ya Tanzania imetoa kiasi cha shilingi bilioni 10 ikiwa ni kuhakikisha inaifufua upya Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA) ili kuiongeza mtaji na kufikia lengo la kujiendesha kibiashara.

Akizungumza mkoani Mbeya mara baada ya kukagua vichwa viwili vilivyokamilika baada ya kufungwa mashine mpya za kufua umeme (traction motor) Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe, amesema kuwa kukamilika kwa ukarabati huo kutaongeza usafirishaji wa mzigo kwa mamlaka.

“Makusudi makubwa ya Serikali kuwekeza fedha hizi ni kuhakikisha mnafanya biashara na kurejesha mzigo wa tani milioni tano mnaotakiwa kuusafirisha kwa mwaka”, amesema Mhandisi Kamwelwe.

Kamwelwe amefafanua kuwa fedha hizo zilizotolewa zimeshanunua mashine mpya za kufua umeme takribani arubaini na mbili ambazo zitafungwa kwenye vichwa saba.

Meneja Karakana ya TAZARA mkoani humo, Mhandisi Ezekiel Mong’ateko, amesema mpaka sasa vichwa viwili vimeshakamilika na mwishoni mwa mwezi huu kichwa cha tatu kitakamilika ambapo kichwa kimoja kina uwezo wa kusafirisha tani laki mbili na nusu kwa mwaka.

“Kukamilika kwa vichwa hivi kutaongeza mzigo tunaotakiwa kuusafirisha kwa mwaka kwani kwa sasa mzigo tunasafirisha umepungua sana na hauzidi tani laki tatu, tunaishukuru sana Serikali kwa kuiwezesha mamlaka”, amesema Mhandisi Mong’ateko.

Mhandisi Mong’ateko ameongeza kuwa sambamba na ukarabati wa vichwa hivyo mkoani humo, Mamlaka inaendelea na ukarabati wa mabehewa katika karakana ya mamlaka jijini Dar es Salaam ili kuhakikisha ukamilikaji wa vichwa hivyo unaendana na ongezeko la usafirishaji wa abiria na mizigo.

Kukamilika kwa ukarabati wa vichwa hivyo kutaongeza idadi ya vichwa kumi na tatu vilivyopo kwa sasa na kufikia vichwa 20 ambapo kila kichwa kina uwezo wa kubeba tani elfu thelathini.

Utoaji wa fedha hizo ni utekelezaji wa makubaliano ya nchi Mbili ya Tanzania na Zambia ambazo kwa pamoja zilikubaliana kutoa bilioni 20 ambapo kila nchi ilitakiwa kuchangia bilioni kumi ili kuifufua upya mamlaka hiyo na kuiwezesha kujitegemea mara baada ya kushuka kwa usafirishaji kutokana na upungufu wa vichwa.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.


Share:

TAMASHA LA BIASHARA LA WATOTO



• • Una Biashara au Wazo la Biashara??!! 

Una Umri kati ya 5-17yrs?? “Tunakutafuta”  • • Jiandikishe sasa kupitia @monpetitplace No.0755 828 302 ili uweze kuonyesha biashara yako kwa watoto na wazazi zaidi ya 500.  

 Ewe mzazi tumia Fursa hii kumuwezesha mtoto wako na kuendeleza au kuanza Biashara.... • •  Pia kutakua na mafunzo ya ujasiriamalia kwa watoto watakaoshiriki kwenye Tamasha hili la Kidspreneur...   

OUR SECOND BUSINESS FAIR COMING SOON.... 

 Are you a kid Vendor or Business owner?  Age 5-17 years?? • • A Business Fair for children ages 6-17years,who are already Entrepreneurs or desire to be one.. We are looking for you!! We will give you a space to sale and show case your products and book your space now call 0755 828 302 • • Tell a friend to tell a friend...
Share:

DOWNLOAD - PAKUA APP YA MALUNDE 1 BLOG ...TUWE TUNAKUTUMIA HABARI ZOTE BURE MOJA KWA MOJA KWENYE SIMU YAKO

Kuwa wa Kwanza kupata habari na matukio yanayojiri Tanzania na dunia kwa ujumla kwa kupakua/ kudownload App ya Malunde 1 blog tukuhabarishe masaa 24.


Tembea na dunia kiganjani mwako sasa.

Pakua App mpya ya Malunde 1 blog imeboreshwa zaidi ili kukidhi mahitaji ya wasomaji wetu. Hii ndiyo mpya kabisa,ina alama hii ↡↡
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Ni rahisi sana : Ingia Play store kisha Andika Malunde 1 blog halafu bonyeza Install

https://bit.ly/2Qb7qyF

Tafadhali fuata maelekezo hapo juu... Usikubali kukosa habari kizembe..Pakua app yetu Mpya ya Malunde1 blog Sasa
Share:

WATENDAJI SEKTA YA ARDHI OFISI ZA MIKOA WATAKIWA KUEPUKA URASIMU


Na Munir Shemweta, WANMM DODOMA
Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mary Makondo amewataka watendaji wa sekta ya ardhi katika ofisi za mikoa kuepuka urasimu na kufanya kazi kwa kuzingatia sheria ili kutoa huduma bora na zenye tija kwa wananchi.



Alisema, pamoja na kutenda kazi kwa kuzingatia sheria, watendaji hao pia wanapaswa kuhakikisha wanashughulikia kero za wananchi kwa kukaa nao pamoja hasa pale wananchi wanapokosea kwa lengo la kuwasaidia badala ya kuwakatisha tamaa.

‘’Urasimu uishe, lengo hapa ni kumhudumia mwananchi na cha msingi ni kukaa pamoja na mteja na kumueleza alipokesea badala ya kumkatisha tamaa kwa kumzungusha, tuwaonee huruma na kuacha urasimu usio wa lazima’’. Alisema Mary.

Akizungumza wakati wa kufunga mafunzo ya Maofisa wa sekta ya ardhi katika mikoa ya Morogoro, Manyara, Singida na Dodoma katika ofisi za Wizara zilizopo Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma jana, Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mary Makondo aliwataka watendaji hao kuwa wabunifu na kutenda kazi kwa kasi na kusisitiza kuwa kazi katika maeneo wanayotoka ni nyingi na zinahitaji kushughulikiwa.

Kwa mujibu wa Mary Makondo, watendaji hao ambao ni Makamishna na Wasajili Wasaidizi wa ofisi za ardhi za mikoa wahakikishe wanatoa kipaumbele katika kushughulikia migogoro ya ardhi kwa haraka pamoja na kutilia mkazo mafunzo ya ndani kwa watumishi.

Aidha, alihimiza utoaji huduma nzuri kwa wateja wanaokwenda kupata huduma katika ofisi za mikoa na kubainisha kuwa suala hilo linahitaji uvumilivu mkubwa na wakati mwingine kushirikisha  wataalamu wengine wa ofisi moja ili kuja na uamuzi  utakaohusisha mawazo ya wengi.

Akigeukia utoaji hati za ardhi, Mary Makondo aliwataka watendaji hao kuhakikisha wanaongeza idadi ya utoaji hati miliki za ardhi kwenye maeneo yao zikiwemo hati za kimila, urasimishaji  na leseni za makazi sambamba na kuhakikisha fidia zinalipwa kwa wakati hususan maeneo yaliyotwaliwa kwa shughuli mbalimbali.

Vile vile, katibu Mkuu Wizara ya Ardhi aliwataka watendaji hao wa sekta ya ardhi kuhakikisha wanapata taarifa zote za makampuni ya urasimishaji na mikataba yao na wakati huo makampuni hayo kufuata miongozo ikiwemo bei elekezi ya urasimishaji.

Mthamini Mkuu wa Serikali Evelyne Mugasha alieleza kuwa mafunzo hayo ya watendaji wa sekta ya ardhi kutoka ofisi za mikoa ya Morogoro, Dodoma, Singida na Manyara yatawawezesha watendaji wa ardhi wa mikoa kufanya kazi kwa ufanisi kutokana na aina ya mafunzo waliyoyapata ikiwemo namna ya kuongeza mapato ya serikali kupitia kodi ya ardhi.

Alisema, watendaji hao walipatiwa mafunzo katika masuala ya ukusanyaji kodi ya pango la ardhi, upimaji na ramani, mipango miji sambamba na masuala ya maendeleo ya makazi aliyoyaeleza kuwa watakuwa wakikutana nayo katika utendahji wa kazi za kila siku.


Share:

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Ijumaa April 10



















Share:

Picha : MWILI WA MWANDISHI WA HABARI ELIYA MBONEA WAZIKWA MKOANI ARUSHA

Mwili aliyekuwa Katibu wa Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Arusha (Arusha Press Club APC), na mmoja wa waandishi wa habari waandamizi wa Kampuni ya New Habari (2006) Limited, Eliya Mbonea,umezikwa leo Alhamis Aprili 9,2020 mkoani Arusha.

Eliya Mbonea amefariki dunia siku ya Jumatatu Aprili 6,2020 wakati akiendelea kupata matibabu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es salaam.
Share:

Picha : POLISI SHINYANGA WAKAMATA WATU 48 MATUKIO YA WIZI,UGANGA BILA KIBALI...ANGALIA MALI ZILIZOIBIWA



Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba akionesha mali mbalimbali zinazodhaniwa kuwa ni za wizi zilizokamatwa  wakati wa Misako na Operesheni mbalimbali zilizofanywa na Jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga katika kipindi cha kuanzia Mwezi Desemba 2019 hadi Machi,2020 katika wilaya ya Shinyanga - Picha zote na Marco Maduhu - Malunde 1 blog
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba akionesha mali mbalimbali zinazodhaniwa kuwa ni za wizi zilizokamatwa  wakati wa Misako na Operesheni mbalimbali zilizofanywa na Jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga katika kipindi cha kuanzia Mwezi Desemba 2019 hadi Machi,2020 katika wilaya ya Shinyanga.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba akionesha mali mbalimbali zinazodhaniwa kuwa ni za wizi zilizokamatwa  wakati wa Misako na Operesheni mbalimbali zilizofanywa na Jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga katika kipindi cha kuanzia Mwezi Desemba 2019 hadi Machi,2020 katika wilaya ya Shinyanga 
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba akionesha mali mbalimbali zinazodhaniwa kuwa ni za wizi zilizokamatwa  wakati wa Misako na Operesheni mbalimbali zilizofanywa na Jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga katika kipindi cha kuanzia Mwezi Desemba 2019 hadi Machi,2020 katika wilaya ya Shinyanga 
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba akionesha pikipiki zinazodhaniwa kuwa ni za wizi zingine zikidaiwa kutumika katika matukio ya uhalifu zilizokamatwa  wakati wa Misako na Operesheni mbalimbali zilizofanywa na Jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga katika kipindi cha kuanzia Mwezi Desemba 2019 hadi Machi,2020 katika wilaya ya Shinyanga 
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba akionesha mali mbalimbali zinazodhaniwa kuwa ni za wizi zilizokamatwa  wakati wa Misako na Operesheni mbalimbali zilizofanywa na Jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga katika kipindi cha kuanzia Mwezi Desemba 2019 hadi Machi,2020 katika wilaya ya Shinyanga 
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba akionesha mapipa matatu na mtambo wa kutengeneza pombe ya Moshi.

Picha zote na Marco Maduhu - Malunde 1 blog


Jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga limefanikiwa kukamata watuhumiwa 48 wa makosa mbalimbali wakiwa na mali zinazodhaniwa kuwa ni za wizi katika wilaya ya Shinyanga.

Akitoa taarifa kwa Vyombo vya Habari Aprili 9,2020,Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba amesema watuhumiwa hao wamekamatwa wakati wa Misako na Operesheni mbalimbali zilizofanywa na Jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga katika kipindi cha kuanzia Mwezi Desemba 2019 hadi Machi,2020.


Kamanda Magiligimba amesema kati ya watuhumiwa hao 48 wanaotuhumiwa kujihusisha na vitendo vya kuvunja nyumba na kuiba,kupatikana na mali zidhaniwazo kuwa ni za wizi,kufanya shughuli za uganga bila kibali, kukamatwa na bangi,mirungi,pombe ya moshi na tuhuma mbalimbali, 

Amesema watuhumiwa 28 wamefikishwa mahakamani na 20 bado wapo chini ya upelelezi.

Amezitaja mali zilizokamatwa kuwa ni Magodoro 7,TV 9, pikipiki 4,baiskeli 5,sabufa 3, vitenge pea 9,Laptop 4,pasi moja ya umeme,Inverter moja,CPU 2 na King’amuzi kimoja.

Vingine ni Bangi mafurushi matatu,mirungi mabunda 32,sabuni B29 Boksi 3, mchele kilo 43.5 na vifaa vya kufanyia shughuli za uganga na mapipa matatu na mtambo wa kutengeneza pombe ya Moshi.

Share:

Thursday, 9 April 2020

POLISI SHINYANGA WAONYA WAHALIFU SIKUKUU YA PASAKA…RPC ATAKA WANANCHI KUSHEREHEKEA MAJUMBANI KUKABILIANA NA CORONA



Kamanda wa Jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba akizungumza na waandishi wa habari Aprili 9,2020 - Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Kamanda wa Jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba akizungumza na waandishi wa habari Aprili 9,2020 - Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog 
Katika Kusheherekea Sikukuu ya Pasaka Aprili 12,2020, Kamanda wa Jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba amesema ni vyema wananchi wakakaa nyumbani ili kujiepusha na mikusanyiko isiyo na ulazima ambayo inaweza kusababisha kusambaa kwa Virusi vya Corona ‘Covid 19’. 

Kamanda Magiligimba ametoa rai hiyo leo Alhamis Aprili 9,2020 wakati akizungumza na waandishi wa habari kuelekea Kipindi cha Sikukuu ya Pasaka kwa ajili ya kuwashirikisha wananchi kuhusu mambo mbalimbali ya ulinzi na usalama huku wito wake ukiwa ni kuwataka wananchi kusherekea kwa amani na utulivu mkubwa. 

“Kutokana na Ugonjwa wa Corona ni vyema wananchi wakasherehekea Sikukuu ya Pasaka Aprili 12,2020 majumbani mwao na waendelee kunawa mikono kwa sabuni na kutumia Sanitizer ili kukabiliana na ugonjwa huu”,amesema Kamanda. 

Katika hatua nyingine amesema Jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga limejipanga kikamilifu kuhakikisha wananchi wote wanasherehekea kwa amani na utulivu bila kujihusisha na vitendo vya uhalifu ama vitendo vingine vyenye viashiri vyovyote vya uvunjivu wa sheria akibainisha kuwa ulinzi umeimarishwa katika maeneo yote ya ibada. 

“Nawatahadharisha watumiaji wote wa barabara kuwa makini kwa kuzingatia sheria na kanuni za usalama barabarani,ikiwa ni pamoja na madereva kutoendesha vyombo vya moto kwa mwendo kasi,kuepuka kuendesha vyombo hivyo wakiwa wametumia vilevi. Jeshi la polisi halitawajibika kumuonea mtu huruma ama upendeleo mtu yeyote atakayekwenda kinyume cha sheria”,amesema Kamanda Magiligimba. 

Aidha amewaasa wazazi,walezi na jamii kwa ujumla kuendelea kuwa makini zaidi na uangalizi wa watoto wao,watoto wa majirani na watoto wa jamii kwa ujumla waepuke kuwaacha watembee peke yao au kuzurura barabarani na maeneo mengine ili kuepuka ajali na maafa ama matukio yanayoweza kujitokeza na kusababisha madhara kwa watoto. 

“Napenda pia kuwakumbusha wananchi watakaolazimika kutoka katika makazi yao kwenda katika ibada wahakikishe kuwa hawaziachi nyumba/makazi yao wazi pasipo uangalizi ili kama ni lazima kufanya hivyo ni vyema waone umuhimu wa kutoa taarifa kwa majirani zao ili kutekeleza kikamilifu dhana ya Ulinzi Jirani”,ameongeza. 

Amewataka wananchi waendelee kushirikiana na Jeshi la polisi kwa kutoa taarifa mapema pale watakapowatilia mashaka watu wasiowafahamu ama wanaowafahamu kuwa ni wahalifu pindi watakapobaini katika maeneo yao ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa haraka iwezekanavyo. 

“Nawasisitiza wananchi kuchukua tahadhari kwa kushirikiana na Jeshi la polisi ili kuhakikisha kuwa vitendo vyote vya uhalifu na wahalifu katika maeneo mbalimbali vinadhibitiwa mapema iwezekanavyo iwapo vitajitokeza kwani uzoefu unaonyesha kwamba baadhi ya watu hutumia kipindi cha Sikukuu kufanya matukio ya uhalifu”,amefafanua Kamanda Magiligimba. 

Share:

Ummy Mwalimu: Tumeanza Kupata Maambukizi Ya Ndani Ya Virusi Vya Corona, Tuongeze Tahadhari

Na Mwandishi Wetu WAMJW Dar es Salaam
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amesema Tanzania imeanza kupata maambukizi ya Virusi vya Corona ya ndani kuanzia maambukizi yaliyopatika tarehe 08/04/2020.

Amesema kuwa tahadhari kubwa inahitajika katika kuhakikisha kuzuia kuendelea kwa maambukizi ya kijamii itasababisha kuongezekana kwa kasi ya maambukizi katika jamii.

Ameyazungumza hayo leo jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano na viongozi wakuu wa madhehebu ya dini katika kujadiliana namna ya kukabiliana na maambukizi ya virusi ya Corona nchini.

Ameongeza kuwa Serikali itatangaza hivi karibuni wananchi kuchukua tahadhari kwani tafiti zinaonesha virusi vya Corona vinaweza kusambaa na kuambukizwa kwa njia ya hewa hivyo maelekezo ya kutumia barakoa yatatolewa ili kuondokana na maambukizi.

“Tafiti zimeonesha kuna uwezekano wa Virusi vya Corona vinaweza kuenezwa kwa njia ya hewa hivyo tutaleta muongozo wa kuanza kutumia Barakoa (Mask) kwa jamii ili kuzuia  maambukizi kuenena kwa njia ya hewa” alisema

Aidha amewataka viongozi wa dini kutoa rai kwa wazazi na walezi kuwalinda watoto kutowaruhusu Watoto kuzurula na kuhangaika ovyo mitaani ili kupunguza uwezekano wa kuongezeka kwa maambukizi ya virusi vya Corona.

“Imani ya watanzania wengi kufikiri kuwa hatuwezi kupata maambukizi ni suala sahihi tunaweza kupata maambukizi kama watu wengine wanavyopata” alisema.

Kwa upande wake Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu amesema kuwa viongozi ni watu muhimu katika kuleta mabadiliko katika Jamii yetu kwani wanasikilizwa zaidi na waumini katika sehemu za ibada.

Ameongeza kuwa lengo ni kuwashirisha viongozi wa kidini katika kuhakikisha wanatimiza wajibu wao katika kuhakikisha maambukizi ya virusi vya Corona yanatokomea nchini.

"Viongozi wa kidini ni watu muhimu sana katika mapambano katika kuondokana na maambukizi ya Virusi vya Corona nchini tunaomba mtusaidie katika hili" alisema

Naye Mkurugenzi wa Shirika la World Vision Gilbert Kamanga amewaomba vingozi wa dini kutofanya suala la virusi vya Corona kuwa la kisiasa bali waunganishe nguvu pamoja ili kuondokana na maambukizi ya virusi vya Corona.

Ameongeza kuwa jamii inatakiwa kupewa elimu kila mahali ikiwemo katika nyumba za ibada ambapo watu wengi ukusanyika pamoja kuabudu itakuwa sehemu sahihi kufikisha ujumbe kuhusu kuondokana na maambukizi ya virusi vya Corona.

"Viongozi wetu wa dini nawaomba tushikamane katika hili kwani virusi vya Corona ni hatari sana lakini tukisimama pamoja hakika tutafanikiwa katika kutokomeza virusi vya Corona" alisema

Akitoa salam za mkoa wa Dar es Salaam Mganga Mkuu wa Mkoa huo Dkt. Rashid Mfaume amesema mkoa umejidhatiti katika kupambana kwa kuenea na maambukizi ya Virusi vya Corona mkoani humo kwa kuzingatia maelekezo yanayotokea na wataalam wa Afya  na Serikali kwa ujumla.

Naye Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Alhaji Musa Salum amesema janga la Corona ni kubwa na kama watu wa imani tunaamini katika kumuonba Mwenyezi Mungu na tunaamini litatokomea.

Pia amemshukuru Rais John Magufuli kuendelea kuruhusu ibada kuendelea katika kama kawaida ni jambo ambalo litasaidia kuzidisha maombi katika kupambana na Virusi vya Corona.

Mkutano huu kati ya Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu na viongozi wakuu wa madhehebu ya dini umekuja wakati Tanzania ikiendelea kupambana na maambukizi ya virusi vya Corona huku ikiwa na jumla ya watu 25 waliombukizwa virusi hivyo.

MWISHO.


Share:

RPC MAGILIGIMBA AZUNGUMZIA TUKIO LA MWANAUME KUKATWA KORODANI KWA WEMBE NA MKEWE



Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba
Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga linamtafuta mwanamke aliyejulikana kwa jina moja la Mwajuma kwa tuhuma ya kumkata na wembe sehemu za korodani ya kulia mme wake aitwaye Shaibu Jabuka (36) mkazi wa mtaa wa Mabambasi kata ya Ndembezi Manispaa ya Shinyanga. 

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba amesema tukio hilo limetokea Aprili 6,2020 majira ya saa saba usiku. 

“Shaibu Jabuka alijeruhiwa kwa kukatwa na wembe sehemu za siri korodani ya kulia na mke wake aliyefahamika kwa jina moja la Mwajuma”,amesema Kamanda Magiligimba. 

“Chanzo cha tukio hilo ni Mwajuma kunyimwa pesa za matumizi shilingi 10,000/=. Majeruhi amepatiwa matibabu katika hospitali ya rufaa mkoa wa Shinyanga na kuruhusiwa kutoka”,ameeleza Kamanda Magiligimba. 

Amesema jeshi la polisi linaendelea na juhudi za kumtafuta Mwajuma aliyekimbia baada ya kumkata na wembe mmewe sehemu za siri. 

“Natoa wito kwa wananchi wote mkoa wa Shinyanga hususani wanandoa na watu wenye mahusiano ya kimapenzi kuacha kujichulia sheria mkononi pale inapotokea mzozo/mgogoro wasikilizwe wazee wenye busara katika maeneo wanayoishi,wafike ofisi za ustawi wa jamii au Ofisi za Dawati la Jinsia na watoto zilizopo vituo vya polisi ili wasikilizwe kuondoa tofauti zao”,amesema Kamanda huyo wa Polisi.
Share:

Jeshi La Polisi Dodoma Lawanasa Wahalifu Mbalimbali Akiwemo Mwanamke Mmoja Anayetuhumiwa Kwakosa La Wizi Kwa Njia Ya Mtandao

Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Jeshi la polisi mkoani Dodoma limemkamata  mwanamke mmoja Grace  Rauwo   Miaka 31 mkazi wa  MTONI KWA AZIZI ALLY  Jijini Dar Es Salaam kwa kosa la wizi kwa njia ya mtandao  na akiwa na gari  lenye namba za usajili  T.745  DSS aina ya TOYOTA CROWN rangi nyeupe  alilokuwa anatumia katika uhalifu  na likidhaniwa kuwa ni la wizi.

Akizungumza na Waandishi wa Habari leo April,9,2020 jijini Dodoma Kamanda wa Polisi mkoani hapa  SACP Gilles Muroto amebainisha kuwa ,Mwanamke huyo huwa anafanya uhalifu huo na timu ya  wenzake  wanaojihusisha na wizi wa fedha kwa njia ya mtandao na wamejisajili kama mawakala .

Kamanda Muroto amesema wahalifu hao wamechonga laini za simu ,wanaingilia mifumo ya neno la siri za wateja  na kuwaibia fedha ambapo kabla ya kukamatwa  waliiba fedha kwa njia ya mtandao  Tsh.Milioni  27  na kugawana fedha hizo  na yeye kuamua kununua gari  hilo  lenye Namba za usajili T.745 DSS ambalo pia wanalitumia kufanya uhalifu katika mikoa mbalimbali.

Katika tukio jingine Kamanda Muroto amebainisha kuwa huko mtaa wa Chinyoya kata ya Kilimani jijini Dodoma katika msako na kwa msaada wa askari wa jeshi la wananchi Tanzania[JWTZ]aliweza kumkamata Godfrey Francis Shirima [22]mpiga picha na mkazi wa Image jijini Dodoma akiwa na silaha  Bastola  aina ya Browning  yenye Na.016975  akiimiliki kinyume cha sheria na kuitumia katika uhalifu na atafikishwa mahakamani muda wowote.

Aidha ,Kamanda Muroto ameendelea kufafanua kuwa ,tarehe   7/04/2020 kijiji cha Chilungulu tarafa ya Bahi mkoani Dodoma  aliuawa Mwalimu  Eradius Mgaya  kwa kupigwa na kitu chenye ncha kali  na kutupwa kwenye shamba la shule  baada ya kuviziwa njiani  wakati akirejea nyumbani kwake ambapo watu watano wamekamatwa kwa tuhuma hizo.

Kamanda Muroto ametoa rai kwa wananchi wa Dodoma  na watu wote wanaochukia uhalifu kushirikiana na jeshi hilo  kwa kutoa taarifa za uhalifu .


Share:

Walioambukizwa Virusi Vya Corona Afrika Wafika 10,692.

Watu wengine 535 wamethibitishwa kuambukizwa virusi vya corona barani Afrika na kuifanya idadi ya watu wenye ugonjwa wa COVID-19 katika nchi 52 za bara hili kufikia 10,692.

Hayo ni kwa mujibu wa taarifa ya Kituo cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa cha Afrika (Africa CDC) ambayo pia imethibitishwa na Shirika la Afya Duniani (WHO).

Misri ilikuwa nchi ya kwanza ya Afrika kuripoti kesi za ugonjwa wa COVID-19 mwezi Februari na tokea wakati huo ugonjwa huo umeenea kwa kasi katika wiki za hivi karibuni.

Katika taarifa, Matshidiso Moeti, mkurugenzi wa WHO barani Afrika amesema ugonjwa wa COVID-19 si tu kuwa unaweza kusababisha vifo vya maelfu ya watu bali pia unaweza kusababisha janga la kiuchumi na kijamii. 

Ametahadharisha kuwa iwapo ugonjwa wa corona utaenea nje ya miji barani Afrika basi itakuwa changamoto kubwa kwa bara hilo.

Moeti amesema kuna haja ya kuziwezesha jamii mashinani kwa kuzingatia mazingira ya kila eneo. 

Aidha amesema WHO inafanya kazi kwa pamoja na serikali za Afrika ili kuimarisha kiwango cha upimaji, karantini, kuwafuatilia wale waliokutana na walioambukizwa, kuzuia maambukizi zaidi na kujumuisha jamii katika kuzuia kuena ugonjwa huo.

-Parstoday


Share:

Waziri Jafo awasilisha makadirio ya bajeti 2020/2021 TAMISEMI

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo ameliomba bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kuidhinisha kiasi cha shilingi Trioni 7.02 kwa ajili ya utekelezaji wa majukumu katika mwaka wa fedha 2020/2021.

Akiwasilisha hoja hiyo Bungeni jana Jijini Dodoma Mhe Jafo amesema  makadirio hayo  yanahusisha Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa-(OR-TAMISEMI), Tume ya Utumishi wa waalimu, Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa.

Akifafanua zaidi Mhe Jafo amesema kiasi cha shilingi Trilioni 3.8  kitatumika  kwa ajili ya mishahara, Bilioni 851 kwa matumizi mengine na kiasi cha shilingi trilioni 2.29 kitatumika  kwa ajili ya miradi ya maendeleo.

Amesema katika mwaka wa fedha wa 2020/2021 Serikali imepanga kusimamia utawala bora, kukuza demokrasia, ushirikishwaji wa wananchi na Ugatuaji wa Madaraka kwa Umma (D by D)

Ameendelea  kufafanua kuwa Serikali itaendelea kuratibu na kusimamia utekelezaji wa shughuli za utoaji wa Elimu ya Msingi na Sekondari  katika Mamlaka ya Serikali za Mitaa ikijumuisha utekelezaji wa mpango wa utoaji wa Elimumsingi Bila Ada

Akifafanua zaidi Mhe.Jafo amesema Serikali inampango wa kuratibu ujenzi wa miundombinu ya maeneo ya utawala katika Mikoa, Wilaya, na Halmashauri mpya na za zamani zipatazo 30 ambazo zinatakiwa  kuhamia katika maeneo yao ya Utawala

Kuhusu ujenzi wa  majengo ya utawala na nyumba za viongozi amesema Serikali itaendelea na ujenzi, ukarabati na ukamilishaji wa majengo ya Ofisi na nyumba za makazi ya Wakuu wa Mikoa, Makatibu Tawala wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya, Makatibu Tawala wa Wilaya, Makatibu Tawala Wasaidizi, Maafisa Tarafa na watumishi waandamizi

Hata hivyo amesema itafanya matengenezo ya barabara zenye urefu wa Kilometa  23,175.11,  Makaravati2, 052 na mifereji ya maji ya mvua  yenye urefu wa 79.9, Ujenzi wa Madaraja 80  yaliyopo  vijijini na mijini ili kuimarisha miundombinu ya barabara nchini .

Kwa upande wa Ujenzi wa Miundombinu ya Barabara Mhe. Jafo amesema Serikali itajenga barabara zenye urefu wa kilometa 35.3 kwa kiwango cha lami na ukarabati urefu wa kilometa 321 kwa kiwango cha changarawe , kukamilisha ujenzi wa barabara zenye urefu wa kilometa 47.59 kwa kiwango cha lami Jiji la Dar-es-salaam.

Wakati Huohuo Mhe. Jafo amesema Serikali itaanza  ujenzi wa barabara ya Nzasa-Kilungule-Buza,Ulongoni-Bangulo-Kinyerezi  na Magomeni Mapipa- Urafiki na ujenzi wa barabara zenye urefu wa kilometa 11.7 kwa kiwango cha lami katika Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni

Mhe. Jafo amesema katika suala la afya Seikali  itaendelea kujenga miundombinu ya afya  ambapo  kutajengwa  wodi tatu  katika kila Hospitali ya Halmashauri, kuendelea na ujenzi wa  Hospitali  27, ujenzi wa Zahanati 3 katika kila Halmashauri na ununuzi wa vifaa tiba katika Hospitali 67 zilizojengwa.

Aidha  Mhe. Jafo  amesema katika mwaka wa Fedha wa 2020/2021 Serikali imepanga  kutumia shilingi bilioni 42.3 kwa ajili ya ujenzi wa maabara za sekondari ambazo zitajengwa katika kila Halmashauri.


Share:

Kambi ya Marekani Nchini Afghanistan Yashambuliwa Kwa Makombora

Makombora matano yameipiga kambi ya jeshi la angani la Marekani ya Bagram nchini Afghanistan leo, lakini hakujawa na ripoti za vifo wala majeruhi na mpaka sasa hakuna kundi lolote lililodai kuhusika na shambulizi hilo. 

Shambulizi hilo limetokea wakati serikali ya Afghanistan ikianza kuwaachilia huru wafungwa wa Taliban kutoka gereza la karibu na kituo cha Bagram, kama sehemu ya hatua ya kujenga imani katika mpango wa amani kati ya Marekani na Taliban unaolenga kumaliza karibu miongo miwili ya vita nchini Afghanistan. 

Ujumbe wa kijeshi unaoongozwa na Jumuiya ya kujihami ya NATO umesema kuwa makombora hayo yaliyoilenga kambi hiyo ya jeshi la Marekani yalifyatuliwa leo asubuhi kutoka kwenye gari lililokuwa limeegeshwa katika kijiji kilicho karibu. 

Wafungwa 100 wa Taliban wanatarajiwa kuachiliwa huru leo kutoka gereza moja la karibu na kambi hiyo, baada ya wanamgambo wengine 100 wa kundi hilo kuachiwa jana.

Credit:DW


Share:

Museven ataka Wenye Nyumba Wasiwafukuze Wapangaji wakati huu wa mlipuko wa Corona

Rais wa Uganda, Yoweri Museveni ametoa onyo kwa wapangaji nchini humo na kuwataka wasiwafukuze wapangaji wanaoshindwa kulipa kodi katika wakati huu ambapo nchi hiyo inakabiliana na janga la Corona

Museveni amesema huu sio mwisho wa dunia na kwamba wenye nyumba wanapaswa kuwa wavumilivu na waelewa kwani janga hili litakapoisha, madeni yote yatalipwa

Pamoja na hayo, Rais Museveni pia amewaagiza Polisi nchini humo kuingilia kati pale wanapokuta mpangaji anafukuzwa

Wiki iliyopita Rais Museveni alitangaza amri ya kutotoka nje na kusalia nyumbani kwa siku 14 kuanzia 1.000 usiku hadi 12.00 asubuhi.

Pia, Rais Museveni alipiga marufuku watu kuendesha magari yao isipokuwa ya kusafirisha mizigo na kutokufunguliwa kwa maduka na kuruhusu biashara ya vyakula pekee.


Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger