Thursday, 9 April 2020

Jeshi La Polisi Dodoma Lawanasa Wahalifu Mbalimbali Akiwemo Mwanamke Mmoja Anayetuhumiwa Kwakosa La Wizi Kwa Njia Ya Mtandao

...
Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Jeshi la polisi mkoani Dodoma limemkamata  mwanamke mmoja Grace  Rauwo   Miaka 31 mkazi wa  MTONI KWA AZIZI ALLY  Jijini Dar Es Salaam kwa kosa la wizi kwa njia ya mtandao  na akiwa na gari  lenye namba za usajili  T.745  DSS aina ya TOYOTA CROWN rangi nyeupe  alilokuwa anatumia katika uhalifu  na likidhaniwa kuwa ni la wizi.

Akizungumza na Waandishi wa Habari leo April,9,2020 jijini Dodoma Kamanda wa Polisi mkoani hapa  SACP Gilles Muroto amebainisha kuwa ,Mwanamke huyo huwa anafanya uhalifu huo na timu ya  wenzake  wanaojihusisha na wizi wa fedha kwa njia ya mtandao na wamejisajili kama mawakala .

Kamanda Muroto amesema wahalifu hao wamechonga laini za simu ,wanaingilia mifumo ya neno la siri za wateja  na kuwaibia fedha ambapo kabla ya kukamatwa  waliiba fedha kwa njia ya mtandao  Tsh.Milioni  27  na kugawana fedha hizo  na yeye kuamua kununua gari  hilo  lenye Namba za usajili T.745 DSS ambalo pia wanalitumia kufanya uhalifu katika mikoa mbalimbali.

Katika tukio jingine Kamanda Muroto amebainisha kuwa huko mtaa wa Chinyoya kata ya Kilimani jijini Dodoma katika msako na kwa msaada wa askari wa jeshi la wananchi Tanzania[JWTZ]aliweza kumkamata Godfrey Francis Shirima [22]mpiga picha na mkazi wa Image jijini Dodoma akiwa na silaha  Bastola  aina ya Browning  yenye Na.016975  akiimiliki kinyume cha sheria na kuitumia katika uhalifu na atafikishwa mahakamani muda wowote.

Aidha ,Kamanda Muroto ameendelea kufafanua kuwa ,tarehe   7/04/2020 kijiji cha Chilungulu tarafa ya Bahi mkoani Dodoma  aliuawa Mwalimu  Eradius Mgaya  kwa kupigwa na kitu chenye ncha kali  na kutupwa kwenye shamba la shule  baada ya kuviziwa njiani  wakati akirejea nyumbani kwake ambapo watu watano wamekamatwa kwa tuhuma hizo.

Kamanda Muroto ametoa rai kwa wananchi wa Dodoma  na watu wote wanaochukia uhalifu kushirikiana na jeshi hilo  kwa kutoa taarifa za uhalifu .


Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger