Monday, 16 March 2020

PIC YAIPONGEZA TPA KWA KUTEKELEZA KWA UFANISI MRADI WA KUCHIMBA NA KUONGEZA KINA KWENYE LANGO LA KUINGILIA NA KUGEUZIA MELI CHA BANDARI YA TANGA

 Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) Mhandisi Deusdedit C.V. Kakoko akitoa taarifa ya Mpango wa Kitaasisi na Utendaji wa Bandari ya Tanga kwa Mwaka wa Fedha 2018/19 na Nusu Mwaka ya Kwanza ya Mwaka wa Fedha 2019/2020 kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) ilipotembelea Bandari ya Tanga hivi karibuni.

 Sehemu ya wajumbe wa kamati hiyo wakiwa kwenye ukumbi wa mikutano


  Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) Mhandisi Deusdedit C.V. Kakoko akipata maelezo

  Sehemu ya wajumbe wa kamati hiyo 
 Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) Mhandisi Deusdedit C.V. Kakoko katikati akiwaongoza wajumbe wa kamati hiyo kutembelea maeneo mbalimbali ya Bandari hiyo
 
Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Uwekezaji wa Mitaji ya Serikali Umma (PIC) imeipongeza Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) kwa kutekeleza kwa ufanisi maboresho na miradi mbalimbali  katika Bandari ya Tanga.
 
Maboresho ya miradi hiyo hususani mradi wa kuchimba na kuongeza kina cha gati ya Bandari hiyo lengo likiwa ni  kuongeza tija, ufanisi pamoja na ushindani na nchi jirani zenye Bandari.

Lengo la ziara ya Kamati ya PIC  ilikuwa ni kuangalia kama uwekezaji wa mitaji ya Serikali unaleta manufaa yaliyokusudiwa na kutoa ushauri wa kimkakati wa namna ya kusaidia katika kuongeza thamani ya mitaji husika inayotewa na Serikali.  

Pamoja na kutembelea meli maalum ya kuchimbia (Dredging Vessel) na kujionea wenyewe shughuli za  uchimbaji na kuongeza kina zinavyoendelea walitembelea pia miradi ifuatayo:-
• Mradi wa Ukarabati wa Miundombinu na Majengo Bandarini 
• Mradi wa maboresho wa gati la mafuta Ras Kazone.

Share:

BREAKING: Tanzania Yathibitisha Kupata Mgonjwa Wa Corona.....Aliingia Nchini Jana Kupitia Uwanja wa Ndege KIA

Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amesema mtanzania mmoja ambaye aliingia nchini Machi 15 kupitia uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro akitokea Ubelgiji amethibitika kuwa na virusi vya Corona. Ummy amesema ni mwanamke mwenye miaka 46. 

Tazama hapo chini


Share:

Makonda Atoa Maagizo Katika Kukabiliana na Virusi vya Corona...."Kuwe na Ndoo za Kunawia, Misongamano Marufuku"

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amepiga marufuku msongamano wa abiria katika vyombo vya usafiri, maeneo ya ibada, benki na mengineyo jijini humo ili kujikinga na ugonjwa wa virusi vya corona.

Aidha, ametoa maelekezo katika kujikinga na virusi hivyo kuwa ziwekwe ndoo za kunawia mikono zenye maji yanayotiririka na dawa za kusafishia mikono katika maeneo yote ya hoteli na nyumba za kulala wageni, kumbi za starehe na kwenye mashine za kutolea fedha (ATM).

Maeneo mengine ni kwenye baa, maduka, maeneo ya ibada, maeneo ya taasisi za serikali na zisizo za serikali, shule, vituo vya afya, bandari, viwanja vya ndege na katika kila kaya.

“Wamiliki wote wa mabasi makubwa na madogo ya kubeba abiria yanayoingia na kutoka na yaliyopo ndani ya Mkoa wa Dar es Salaam, boti za mwendo kasi, treni/Shirika la Reli Tanzania (Tazara), Uongozi wa Stendi kuu ya Mabasi Ubungo na mengineyo waweke sehemu za kunawa mikono kwa maji yanayotiririka na kwa sabuni na utekelezaji wa suala hili ukamilike ndani ya siku tatu kuanzia leo Machi 16.

Ameongeza kuwa ugonjwa huo haupo Tanzania lakini kutokana na muingiliano mkubwa wa Mkoa wa Dar es Salaam, mikoa mingine na nchi nyingine ni muhimu kuchukua tahadhari ili kuzuia ugonjwa huo usiingie nchini.


Share:

Head of Products and Sales at National Bank of Commerce (NBC)

Position: Head of Products and Sales Location: Head Office NBC Job ID: R-15901142 NBC is the oldest serving bank in Tanzania with over five decades of experience. We offer a range of retail, business, corporate and investment banking, wealth management products and services. Job Description​ Head of Sales and Product is responsible to ; To develop Products by identifying Potential… Read More »

The post Head of Products and Sales at National Bank of Commerce (NBC) appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Markets Sales Dealer at National Bank of Commerce (NBC)

Position: Markets Sales Dealer Location: Head Office NBC Jib ID: R-15907531 NBC is the oldest serving bank in Tanzania with over five decades of experience. We offer a range of retail, business, corporate and investment banking, wealth management products and services. Job Description​ Accountability : Markets Sales Dealing. Time split : 80% Key actions to include: Lead on development… Read More »

The post Markets Sales Dealer at National Bank of Commerce (NBC) appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Dkt. Mpango Atahadharisha Wafanyakazi Kujikinga Na Corona Na Kutaka Ifanyike Tathimini Ya Athari Za Ugonjwa Huo Kiuchumi

Na. Farida Ramadhani na Saidina Msangi, WFM, Dodoma
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango, amewaagiza Wataalamu wa Wizara hiyo kushirikiana na Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kuangalia madhara ya Corona yanayoweza kujitokeza katika uchumi wa nchi pamoja na namna ya kukabiliana nayo.

Agizo hilo amelitoa jijini Dodoma alipokuwa akizungumza na watumishi wa Wizara hiyo kuhusu umuhimu wa kujikinga na Virusi vya Corona vinavyosababisha ugonjwa hatari wa COVID-19.

“Nilikuwa naangalia taarifa ya Tume ya Uchumi ya Afrika “Economic Commission of Africa” inayoelezea madhara ya ugonjwa wa COVID 19 unaosababishwa na Virusi vya Corona, kwa kweli inatisha, wanasema uchumi wa Africa unaweza ukaanguka na kufikia asilimia 1.8, wastani huwa ni asilimia 3.2”, alisema Dkt. Mpango.

Dkt. Mpango alisema kuwa ugonjwa huo ni hatari ni vema Taifa liandaliwe upande wa uchumi ili kujiweka sawa ma kutafuta namna ya kuchukua hatua katika kukabiliana na madhara yanayoweza kutokea kiuchumi hususani kwenye biashara na utalii.

Aliwataka Watumishi wa Wizara ya Fedha na Mipango kuchukua tahadhari za kujikinga na ugonjwa huo kwa kuzingatia taratibu za afya katika maeneo ya kazi na kwenye familia zao.

“Kila mmoja ana wajibu binafsi, wajibu katika familia na wajibu kazini ili tuendelee kukaa salama. Sitapenda kupoteza mtumishi hata mmoja wala mtumishi kupoteza mwanafamilia wake kutokana na ugonjwa huu”, alisema Dkt. Mpango.

Aliwaasa watumishi kuchukua tahadhari kwa kuiga mfano wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, wa kuacha mazoea ya kushikana mikono wakati wa kusalimiana.

“Kiafrika unaonekana unaringa kweli usipompa mtu mkono, lakini kwa dharura tuliyonayo, muwafundishe na watoto wenu hakuna kupeana mikono” alisisitiza Dkt. Mpango.

Alifafanua kuwa katika kupambana na ugonjwa huo, Wizara imeweka Kemikali maalum ya kunawia mikono (Sanitizer) inayoweza kuua vijijidudu kwenye maeneo mbalimbali ya Majengo ya Wizara hiyo, hivyo aliwataka watumishi wahakikishe wanaitumia wakati wanapoingia ofisini na kwa wenye uwezo wainunue kwa ajili ya matumizi ya familia zao.

Aidha, Aliwataka watumishi hao kutoa elimu ya afya kwa familia zao pamoja na kuepuka mikusanyiko na safari zisizokuwa za lazima za ndani na nje ya nchi ili kujikinga na ugonjwa huo.

Alisema ugonjwa huu ni kama vita na kwasasa kwani umeshafika katika nchi jirani za Kenya na Rwanda, hata hivyo alibainisha kuwa, kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na Wizara ya Afya, Tanzania iko salama.

Mwisho.


Share:

TANGA UWASA YAWATAKA WATEJA KUCHUKUA TAHADHARI WAKATI WA KUPATA HUDUMA KWA KUEPUKA MIRUNDIKANO

 Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Mhandisi Geofrey Hilly akizungumza na wakati wa mkutano wake na vyombo vya habari kuhusu maadhimisho ya wiki ya maji inayoanza Machi 16 hadi 22 mwaka huu kulia  ni Meneja wa Ruwasa Mkoa wa Tanga Mhandisi Upendo Lugongo
 Meneja wa Ruwasa Mkoa wa Tanga Mhandisi Upendo Lugongo kulia akisistiza jambo wakati wa mkutano huo kushoto ni Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Mhandisi Geofrey Hilly
 Sehemu ya waandishi wa habari wakichukua matukio mbalimbali
 Mwandishi wa Gazeti la Citizen Mkoa wa Tanga George Sembony kushoto akiwa na Amina Omari wa gazeti la Mtanzania wakifuatilia mkutano huo kwa umakini


MAMLAKA ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) imewataka wateja wao kuchukua tahadhari na kufuata maelekezo kama watakavyoongozwa wakati wakupatiwa  huduma ikiwemo kuepuka kurundikana kwa pamoja kwenye madirisha ili kukabiliana  na maambukizi ya ugonjwa wa Corona.

Amesema tahadhari hiyo wameichukua ikiwa ni hatua mojawapo kuunga mkono juhudi serikali kuzuia kuingia nchini ugonjwa huo kwa kutoa elimu  kwa njia ya jumbe mbalimbali katika maeneo ya ofisi zao,hususani majengo ya huduma kwa wateja pamoja na kuwa na sehemu za wateja pamoja na watumishi kuosha mikono yao

Hayo yalisemwa leo na Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Mhandisi Geofrey Hilly wakati wa mkutano wake na vyombo vya habari kuhusu maadhimisho ya wiki ya maji inayoanza Machi 16 hadi 22 mwaka huu.

Alisema kwamba kwa kuwa maeneo yao hususani kwenye ofisi za kutolea huduma ni mojawapo wa maeneo yenye mwingilio mkubwa wa watu hivyo ni wajibu wao kuhakikisha wanachukua tahadhari ya kukabiliana na ugonjwa huo.

“Kufuatia na maagizo mbalimbali yanayotolewa na viongozi wa nchi juu ya ugonjwa huo sisi kama mamlaka tumeona ni muhimu kuanza kuchukua hatua mapema za kukabiliana nao”Alisema Mkurugenzi huyo.

Alisema miongoni mwa tahadhari ambazo zimeanza kuchukuliwa na mamlaka ni pamoja na kuunga mkono serikali kwa kutoa elimu juu ya ugonjwa huo kwa njia ya ujumbe mbalimbali katika maeneo ya ofisi ,majengo ya huduma kwa wateja kuwa na sehemu za wateja na watumishi kwa ajili ya kuosha mikono.

“Sisi tumekuwa na madirisha ya huduma kwa wateja hivyo ndio maana tumeamua kuchukua tahadhari hivyo kutokana na kwamba wakati mwengine wateja wanakuwa na fujo wanarundikana wanataka kila mmoja asikilize kwa wakati na ndio maana tumeamua kufanya hivyo”Alisema

Mkurugenzi huyo alisema kwamba wataweka huduma ya kunawa mikono kwa sababu ugonjwa huo asilimia kubwa unatokana na kugusanagusana kwa hiyo kila wakati mtu ahakikisha amenawa mikono na sabuni.

“Tunasisitiza kuchukua tahadhari watumishi na wateja wote lakini pia tutaweka maeneo ya kunawa mikono kwenye ofisi zao kuwasaidia watu ambao wanakuja kupata huduma kunawa mikono “Alisema

Awali akizungumza wakati wa mkutano huo Meneja wa Ruwasa Mkoa wa Tanga Mhandisi Upendo Lugongo alisema upatikanaji wa maji vijijini kwa wastani ni asilimia 52 lakini kwenye mikuu ya wilaya ni asilimia 54 na Jiji la Tanga ni asilimia 89 na watu wanapata maji safi.

Alisema kwa Tanga wapo vizuri na wanajitahidi miradi yote inakwenda kutekeleza kupitia njia ya uwezo wa ndani na wakandarasi watatumika kwa uchache ili wananchi waweze kupata huduma kwa haraka ndani ya muda mfupi.
Share:

Head of SME at National Bank of Commerce (NBC)

Position: Head Of SME Location: Head Office NBC Job ID: R-15907527 NBC is the oldest serving bank in Tanzania with over five decades of experience. We offer a range of retail, business, corporate and investment banking, wealth management products and services. Job Description​ Accountability: Driving Business Development and Growth -40% The role holder will have specific accountability for delivering… Read More »

The post Head of SME at National Bank of Commerce (NBC) appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Collateral Risk Assessment Manager at National Bank of Commerce (NBC)

Position: Collateral Risk Assessment Manager Location: Head Office NBC Job ID: R-15907568 NBC is the oldest serving bank in Tanzania with over five decades of experience. We offer a range of retail, business, corporate and investment banking, wealth management products and services. Job Description​ Team Leadership (10% to 30%) Responsibilities: Develop highly motivated team maintaining excellent relationships with own… Read More »

The post Collateral Risk Assessment Manager at National Bank of Commerce (NBC) appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Wauguzi wa wagonjwa waliombukizwa virusi vya corona Kenya waanza mgomo baridi

Wauguzi wanaofanya kazi katika wodi iliyotengwa kwa watu walioambukizwa virusi vya corona nchini Kenya wameanza mgomo baridi kulalamikia kile wanachodai kuwa ukosefu wa vifaa vya kujikinga na mafunzo ya kutosha.

Hospitali ya Mbagathi katika mji mkuu wa Nairobi, ni moja ya hospitali zilizo na wodi ya kutibu wagonjwa waliombukizwa virusi hivyo hatari.

Katibu mkuu wa muunganowa wauguzi nchini Kenya,Seth Panyako ameiambia BBC kwamba wauguzi watarejea kazini ikiwa watapewa mavazi maalum na mafunzo ya jinsi ya kuwashughulikia wagonjwa.

Credit -BBC


Share:

Wabunge Waunga Mkono Zuio La Serikali Uagizaji Vifaa Vya Umeme Nje Ya Nchi

Veronica Simba – Dar es Salaam
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini imesema inaendelea kuunga mkono zuio la serikali kwa wakandarasi wa miradi mbalimbali ya umeme nchini kuagiza vifaa husika nje ya nchi.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Machi 14 mwaka huu, baada ya Kamati hiyo kufanya ziara katika viwanda vya Europe Inc. Industries Ltd (Tropical) na Kilimanjaro Cables (T) Ltd (Africab), vinavyozalisha nyaya za umeme na mashine umba (transfoma), Mwenyekiti wa Kamati husika, Dunstan Kitandula alisema uamuzi huo ni mzuri na unapaswa kuungwa mkono.

“Baada ya kutembelea viwanda hivi, tumejiridhisha pasipo shaka kuwa uwezo wake wa uzalishaji unatosheleza mahitaji ya ndani hivyo hakuna sababu ya kuagiza vifaa hivyo nje ya nchi,” alisema Kitandula.

Akieleza zaidi, Mwenyekiti alisema lengo la ziara yao lilikuwa ni kujiridhisha kuhusu uwezo wa uzalishaji wa viwanda husika kutokana na mkanganyiko uliopo kutokana na baadhi ya wakandarasi kulalamika kuwa vifaa vinavyozalishwa ndani ya nchi havitoshelezi mahitaji yao.

Alisema kumekuwepo na malalamiko kutoka kwa wananchi kuwa kasi ya utekelezaji miradi ya umeme vijijini hairidhishi na wakandarasi husika wanapoulizwa wamekuwa wakijitetea kuwa hali hiyo inasababishwa na zuio la serikali kuagiza vifaa nje ya nchi.

Hata hivyo, Kitandula alisema mara zote Serikali imekuwa ikisisitiza kuwa viwanda vya ndani vina uwezo mkubwa kiuzalishaji kwani unakidhi mahitaji ya soko la ndani na hata kuwepo ziada.

Katika hatua nyingine, Mwenyekiti huyo wa Kamati, alitoa wito kwa Wizara ya Nishati na Wakala wa Nishati Vijijini (REA), kuwasaidia wazalishaji wa ndani katika utafutaji masoko ya vifaa husika ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na katika Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC).

“Ni lazima sasa ninyi Wizara na REA mvichukulie viwanda hivi kama sifa kwa nchi na mvisaidie kupata masoko nje ya nchi ili kuwawezesha wawekezaji hawa wazalendo kuzalisha kwa tija zaidi na kuepuka hasara inayoweza kuwafilisi,” alisisitiza.

Akizungumzia hatua zilizochukuliwa na Serikali katika suala hilo, Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgalu, alisema Wizara imeendelea kuwasaidia wawekezaji wa ndani katika utafutaji masoko nje ya nchi akitoa mfano namna serikali ilivyoisaidia kampuni ya Africab ilipotaka kuwekeza nchini Zambia.

“Niwapongeze Africab kwa uthubutu wao ambao umewawezesha kuanzisha kiwanda nchini Zambia. Walipoenda huko mara ya kwanza, tuliwasaidia kuzungumza na Serikali ya nchi hiyo tukawaeleza uwezo wao wa ndani hatua iliyowasaidia kufanikisha lengo lao. Tutaendelea kufanya hivyo kwa kampuni zetu nyingine,” alisema Naibu Waziri.

Kuhusu suala la baadhi ya wakandarasi wanaosemekana kuendelea kuagiza vifaa nje ya nchi, Naibu Waziri alisisitiza kuwa msimamo wa Serikali ni kutoa adhabu kali za kimkataba na kisheria kwa yeyote atakayebainika kama alivyobainisha Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani hivi karibuni.

Kiwanda cha Africab kina uwezo wa kuzalisha (kwa mwaka) nyaya za umeme kilomita 75,000 transfoma 6,500 na insulators 660,000 wakati Kiwanda cha Tropical kikiwa na uwezo wa kuzalisha transfoma 75,000 na nyaya zinazozidi kwa kiasi kikubwa mahitaji ya soko la ndani.

Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini iko katika ziara jijini Dar es Salaam na Mkoa wa Pwani, kukagua miradi mbalimbali inayotekelezwa chini ya Wizara ya Nishati.


Share:

Rais Magufuli afanya ziara ya kushtukiza Ubungo Jijini Dar es Salaam.....Atangaza kuahirisha Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka huu

Rais  wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli, amesitisha  mbio za Mwenge wa Uhuru kwa mwaka 2020.
 
Mbio hizo zilitarajiwa kuanza hivi karibuni.Uamuzi huo ni tahadhari ya kuepukana na maambukizi ya CORONA.

Ugonjwa huo uliosababisha vifo vya zaidi ya watu 6,513 katika nchi mbalimbali umeingia Afrika Mashariki katika nchi za Kenya, Rwanda.

Rais Magufuli ametoa maagizo hayo leo jijini Dar es Salaam baada ya kutembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa daraja la juu eneo la Ubungo linalounganisha barabara za Morogoro, Sam Nujoma na Mandela.


“Nina fahamu kitu kingine kinacholeta mkusanyiko ni mwenge na tulitegemea kuwasha mwenge karibuni kule Zanzibar ambapo ungewezwa kutembezwa nchi nzima, nimeamua mbio za mwenge hazitafanyika mpaka corona iwe imeondoka” amesema Magufuli.


Rais Magufuli amesema fedha za mwenge ambao ulitakiwa kuwashwa Zanzibar zitatumika katika kujiandaa na tahadhari zaidi ya corona ambayo ishafika Kenya na Rwanda.

Amesema hadi sasa hakuna mgonjwa wa corona Tanzania na mbio za mwenge zitaendelea  itakapothibitishwa ugonjwa huo umeisha duniani.


Share:

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatatu March 16











Share:

Tanzania Yaendelea Kuaminiwa Kimataifa

Na. Immaculate Makilika- MAELEZO
 Tanzania imeendelea kuaminiwa kimataifa kufuatia jitihada mbalimbali inayofanya kwa ajili ya kupiga vita vitendo vya rushwa pamoja kuwekeza katika miradi mbalimbali inayolenga na kuboresha maisha ya wananchi, pamoja na kukuza uchumi wa nchi.

 Akizungumza na Waandishi wa habari jana jijini Dodoma, Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi alisema kuwa Machi 5, 2020 Shirika la Fedha Fedha Duniani (IMF) lilikamilisha taarifa yake ya tathmini kuhusu uchumi wa Tanzania.

“Katika taarifa hiyo IMF imesisitiza kuwa Uchumi wa Tanzania uko imara na wamefurahishwa na akiba ya kutosha ya fedha za kigeni, mfumuko wa bei kuwa chini ya asilimia 5, mauzo ya bidhaa nje ya nchi kuongezeka, kuongezeka kwa kasi ya mabenki kutoa mikopo kwa sekta binafsi na kuwa na deni la taifa ni himilivu” alisema Dkt. Abbasi

“Katika kuonesha Tanzania inaaminika kimataifa, hivi karibuni tumesaini mikataba mitano na Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB), inayohusu utekelezaji wa miradi mitatu ya kimkakati kwa mkopo wa masharti nafuu ya Dola za Marekani milioni 495.59 ambayo ni sawa na TZS trilioni 1.14.” alisititiza Dkt. Abbasi

Aidha, alifafanua kuwa fedha hizo zitawezesha kutekeleza ujenzi wa miradi ya Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Msalato Jijini Dodoma kwa gharama ya dola za marekani milioni 271.63, ujenzi wa barabara ya Bagamoyo – Horohoro – Lungalunga – Malindi kwa kiwango cha lami yenye urefu wa km 120. 8 kwa gharama ya dola za marekani milioni 168.76 na dola milioni 55.2 kwa ajili ya Programu ya utawala bora na kuendeleza sekta binafsi.


Share:

Tabora Waanza Kunufaika na Mradi wa Maji Ziwa Victoria

Na. Immaculate Makilika- MAELEZO
Mradi wa maji kutoka ziwa Victoria umeanza kufanya kazi na kuwanufaisha wananchi ambao wamepitiwa na mradi huo katika mkoa wa Tabora, na unatarajiwa kunufaisha wakazi wakazi Milioni 1.8 utakapokamilika.

Akizungumza na Waandishi wa habari jana jijini Dodoma, Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ambaye pia ni Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi amesema  mradi huo unaogharimu shilingi bilioni 600 utawanufaisha wakazi wa vijiji zaidi ya 90 vilivyopitiwa na bomba la maji.

Amefafanua kuwa, maeneo ambayo mradi huo umepitisha bomba la maji hadi kufikia Tabora mjini ni pamoja na Igunga na Nzega. Amesema, kukamilika kwa mradi huo kutaondoa tatizo la upatikanaji wa maji ya uhakika na salama kwa matumizi ya nyumbani na shughuli nyingine ambazo zinahitaji maji ya uhakika.

Dkt. Abbasi amesema kuwa Serikali inaendelea kuboresha Sekta ya maji kwa kuimarisha miundombinu yake ili kutoa huduma ya maji safi na salama mijini na vijijini.  Amefafanua kwamba, hadi sasa jumla ya miradi 875 inatekelezwa sehemu mbalimbali nchini ambapo kati ya hiyo miradi 802 ipo mijini na miradi 73 ipo vijijini. Jumla ya miradi  ya maji 75 ya vijijini imekamilika.

Wakati huo huo Dkt. Abbasi amesema kwamba, kutokana na mageuzi makubwa yaliyofanyika katika sekta ya ardhi, hadi kufikia Machi 2020 jumla ya migogoro ya ardhi 10,000 imetatuliwa. Pia, ufanisi katika mifumo ya upimaji na utoaji wa hati umewezesha kukusanya mapato kutoka shilingi bilioni 54.1 mwaka 2014/15 hadi shilingi bilioni 100 mwaka 2018/19.

Kuhusu Serikali kuhamia Dodoma, Dkt. Abbasi amesema, hadi sasa jumla ya Watumishi wa Umma 15,361 wa Wizara na Taasisi za Serikali wameshahamia Makao Makuu ya Serikali, Dodoma. Aidha, maandalizi ya awamu ya pili ya ujenzi wa majengo ya ofisi za Serikali na barabara kwa kiwango cha lami kwa urefu wa kilometa 40 katika mji wa Serikali ulioko Mtumba unaendelea.


Share:

Wagonjwa wa Corona Waongezeka Kenya.....Rais Kenyatta Aamuru Shuoe Zote, Vyuo Vifungwe

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amethibitisha kisa cha tatu cha maambukizi ya virusi vya corona na kuamuru shule zote zifungwe.

Rais Uhuru ameamuru shule zote za  kutwa kufungwa kuanzia siku ya Jumatatu. Shule za mabweni zimepewa muda hadi Jumatano kuhakikisha wanafunzi wote wanarejea nyumbani kwao kwa sababu ya homa ya Corona. 

Vyuo vikuu na vile vya amali vimepewa muda hadi Ijumaa kuwapa nafasi wanafunzi wote kurejea kwao.

Rais Uhuru kadhalika amethibitisha kuwa watu wengine wawili wameambukizwa virusi vya corona nchini Kenya. 

Mmoja aliambatana na aliyeambukizwa akiwa kwenye karantini hospitalini Kenyatta. Wahudumu wa afya wanaendelea kuwatazama walioambukizwa na pia kuwatibu.

Kutokana na hali hii, wasafiri wanaotokea nchi za kigeni zilizoathiriwa na homa hiyo ya Corona wamepigwa marufuku kuingia ndani ya mipaka ya Kenya.

 Watakaoruhusiwa kuingia nchini ni wakenya na wageni walio na vibali rasmi.

 Wakenya wote watakaorejea nyumbani katika muda wa saa 48 zijazo watalazimika kujiweka kwenye karantini na kusalia ndani.


Share:

Wizara ya Ujenzi Yatoa Ufafanuzi Kuhusu Taarifa za Kukatika Tena Daraja la Kiegeye Morogoro




Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger