Sehemu ya wajumbe wa kamati hiyo wakiwa kwenye ukumbi wa mikutano
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) Mhandisi Deusdedit C.V. Kakoko akipata maelezo
Sehemu ya wajumbe wa kamati hiyo
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) Mhandisi Deusdedit C.V. Kakoko katikati akiwaongoza wajumbe wa kamati hiyo kutembelea maeneo mbalimbali ya Bandari hiyo
Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Uwekezaji wa Mitaji ya Serikali Umma (PIC) imeipongeza Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) kwa kutekeleza kwa ufanisi maboresho na miradi mbalimbali katika Bandari ya Tanga.
Maboresho ya miradi hiyo hususani mradi wa kuchimba na kuongeza kina cha gati ya Bandari hiyo lengo likiwa ni kuongeza tija, ufanisi pamoja na ushindani na nchi jirani zenye Bandari.
Lengo la ziara ya Kamati ya PIC ilikuwa ni kuangalia kama uwekezaji wa mitaji ya Serikali unaleta manufaa yaliyokusudiwa na kutoa ushauri wa kimkakati wa namna ya kusaidia katika kuongeza thamani ya mitaji husika inayotewa na Serikali.
Pamoja na kutembelea meli maalum ya kuchimbia (Dredging Vessel) na kujionea wenyewe shughuli za uchimbaji na kuongeza kina zinavyoendelea walitembelea pia miradi ifuatayo:-
• Mradi wa Ukarabati wa Miundombinu na Majengo Bandarini
• Mradi wa maboresho wa gati la mafuta Ras Kazone.
0 comments:
Post a Comment