Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli, amesitisha mbio za Mwenge wa Uhuru kwa mwaka 2020.
Mbio hizo zilitarajiwa kuanza hivi karibuni.Uamuzi huo ni tahadhari ya kuepukana na maambukizi ya CORONA.
Ugonjwa huo uliosababisha vifo vya zaidi ya watu 6,513 katika nchi mbalimbali umeingia Afrika Mashariki katika nchi za Kenya, Rwanda.
Rais Magufuli ametoa maagizo hayo leo jijini Dar es Salaam baada ya kutembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa daraja la juu eneo la Ubungo linalounganisha barabara za Morogoro, Sam Nujoma na Mandela.
“Nina fahamu kitu kingine kinacholeta mkusanyiko ni mwenge na tulitegemea kuwasha mwenge karibuni kule Zanzibar ambapo ungewezwa kutembezwa nchi nzima, nimeamua mbio za mwenge hazitafanyika mpaka corona iwe imeondoka” amesema Magufuli.
Rais Magufuli amesema fedha za mwenge ambao ulitakiwa kuwashwa Zanzibar zitatumika katika kujiandaa na tahadhari zaidi ya corona ambayo ishafika Kenya na Rwanda.
Amesema hadi sasa hakuna mgonjwa wa corona Tanzania na mbio za mwenge zitaendelea itakapothibitishwa ugonjwa huo umeisha duniani.
0 comments:
Post a Comment