Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amethibitisha kisa cha tatu cha maambukizi ya virusi vya corona na kuamuru shule zote zifungwe.
Rais Uhuru ameamuru shule zote za kutwa kufungwa kuanzia siku ya Jumatatu. Shule za mabweni zimepewa muda hadi Jumatano kuhakikisha wanafunzi wote wanarejea nyumbani kwao kwa sababu ya homa ya Corona.
Vyuo vikuu na vile vya amali vimepewa muda hadi Ijumaa kuwapa nafasi wanafunzi wote kurejea kwao.
Rais Uhuru kadhalika amethibitisha kuwa watu wengine wawili wameambukizwa virusi vya corona nchini Kenya.
Rais Uhuru kadhalika amethibitisha kuwa watu wengine wawili wameambukizwa virusi vya corona nchini Kenya.
Mmoja aliambatana na aliyeambukizwa akiwa kwenye karantini hospitalini Kenyatta. Wahudumu wa afya wanaendelea kuwatazama walioambukizwa na pia kuwatibu.
Kutokana na hali hii, wasafiri wanaotokea nchi za kigeni zilizoathiriwa na homa hiyo ya Corona wamepigwa marufuku kuingia ndani ya mipaka ya Kenya.
Kutokana na hali hii, wasafiri wanaotokea nchi za kigeni zilizoathiriwa na homa hiyo ya Corona wamepigwa marufuku kuingia ndani ya mipaka ya Kenya.
Watakaoruhusiwa kuingia nchini ni wakenya na wageni walio na vibali rasmi.
Wakenya wote watakaorejea nyumbani katika muda wa saa 48 zijazo watalazimika kujiweka kwenye karantini na kusalia ndani.
0 comments:
Post a Comment