Thursday, 21 November 2019

Technical Specialist / Demand Planning Specialist at Abt Associates

Organization Overview The International Development Division focuses on improving the lives and economic well-being of people in lower and middle-income countries. We command technical expertise in health, agriculture, climate change, food security and governance—as well as in international evaluation. Our multi-layered health portfolio includes policy, health promotion and disease prevention, health finance, and health systems management. In partnership… Read More »

The post Technical Specialist / Demand Planning Specialist at Abt Associates appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Transport Director at Trade Mark East Africa (TMEA)

Transport Director, Northern Cluster Countries & Horn of Africa The Transport Director, Northern Cluster Countries & Horn of Africa will be responsible for providing strategic and operational support in delivering and managing TMEA’s infrastructure programme and activities in the Northern Cluster Countries & Horn of Africa. S/he will ensure that TMEA’s strategic objective of reduced trade barriers, and… Read More »

The post Transport Director at Trade Mark East Africa (TMEA) appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Project Director Job at PATH

PATH is currently seeking a qualified Project Director for an upcoming CDC-funded program, “Health Information System Development, Project Management and Coordinated Deployment for National HIV and Health Sector Systems in the Republic of Tanzania under the Global Health Security Agenda and under PEPFAR”. The project’s goal is to increase the ability of information systems to support high quality… Read More »

The post Project Director Job at PATH appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Consultancy – Forestry and Sustainability expert – Job at WeForest

Job Opportunity at WeForest – Consultancy – Forestry and Sustainability expert Consultancy – Forestry and Sustainability expert Tanzania CONTEXT WeForest is fast growing international non-profit association with headquarters in Belgium and projects in Brazil, Ethiopia, India, Tanzania, and Zambia. Our aim is to demonstrate, through the restoration of entire regions, that well-planned reforestation can be the solution to… Read More »

The post Consultancy – Forestry and Sustainability expert – Job at WeForest appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

MAASKOFU MWANZA WACHEKELEA KANISA LA MFALME ZUMARADI KUFUNGWA...WATAKA SERIKALI IKOMAE ZAIDI



Mkuu wa Wilaya Nyamagana alipofanya ziara kwenye Kanisa la Mfalme Zumaradi.

Viongozi wa Umoja wa Makanisa (UMJM), jijini Mwanza, unaoundwa na Mabaraza matatu ya TEC, CCT na CPCT, umeitaka Serikali kuyapitia upya Makanisa mengine ambayo usajili wake haueleweki, ili kuondoa sintofahamu kwa waumini wa madhehebu hayo.

Hatua hiyo inakuja ikiwa ni siku chache baada ya Kamati ya ulinzi na Usalama Wilaya ya Nyamagana, ikiongozwa na Mkuu wa Wilaya Dkt. Philis Nyimbi, kufungia Kanisa la Mfalme Zumaridi lililopo eneo la Iseni jijini humo ambalo linadaiwa kuendesha Ibada zake kinyume cha sheria na Katiba ya nchi.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Mwanza, Mwenyekiti wa umoja huo, Askofu Philipo Mafuja amesema hatua hiyo iliyofanywa na viongozi wa Serikali kuyafungia Makanisa yanayoendeshwa kinyume cha sheria yanabaraka hata kwa Mungu.

"Maandiko matakatifu yanasema tuilinde imani na kulinda imani ni hii kuyachukulia hatua baadhi ya Makanisa ambayo yanafanya kazi kinyume na utaratibu" amesema Askofu Philipo Mafuja

Novemba 18, 2019 Uongozi wa Wilaya ya Nyamagana Mkoani Mwanza umepiga marufuku ibada zinazoendeshwa na kiongozi wa kanisa la Mfalme Zumaridi hadi hapo Serikali itakapojiridhisha kuwa ibada hazikinzani na sheria za nchi.
Share:

Download App Yetu Kwenye Simu Yako Ili Uweze Kupata Habari Zetu Kwa Haraka Zaidi

Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa urahisi kabisa kupitia simu yako ya mkononi muda wowote hata usiku wa manane au ukiwa kazini...

Pata kurasa za mbele Magazetini, habari za kitaifa, matukio yote ya kisiasa, burudani na udaku   kupitia simu yako ya mkononi.

Huhitaji tena kuwa na Computer. Ingia Play Store, pakua App yetu  tukuhabarishe masaa 24.



Share:

Taarifa Kwa Umma Ya Kusitisha Matumizi Ya Dawa Zenye Kiambata Hai Cha Ranitidine




Share:

Mahakama Yaelezwa Kuwa Tundu Lissu Amepona Lakini Anahofia Usalama Wake Kurudi Nchini

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, imeelezwa kuwa aliyekuwa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu ameshapona ila anashindwa kurudi nchini kwa kile alichokidai ni kuhofia usalama wake.

Hayo yameelezwa leo Novemba 21,2019 na Mdhamini wa Lissu, Ibrahim Ahmed, alipokuwa akiieleza mahakama hiyo juu ya afya ya Mwanasheria huyo wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Ahmed ameieleza mahakama hiyo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba, wakati wa kesi ya uchochezi inayomkabili mshtakiwa huyo na wenzake watatu ilipoitwa.



Share:

Msanii Baba Levo Ashinda Rufaa Yake na Kuachiwa Huru

Msanii wa Muziki na Diwani wa Mwanga Kaskazini, Clayton Chipando ‘Baba Levo’ ameachiwa huru leo baada ya kumaliza hukumu yake ya miezi mitano huku Mahakama ikijiridhisha kuwa kifungo alichoongezewa kilikuwa batili.

Kabla ya kuachiwa huru leo, Baba levo alihukumiwa kwenda jela Miezi mitano Agosti 01, 2019 na Mahakama ya Mwanzo Mwandiga, Kigoma baada ya kupatikana na hatia ya kumshambulia Askari wa Usalama Barabarani, baadae alikata rufaa kupinga hukumu hiyo na akaongezewa hukumu


Share:

Naibu Waziri Mabula Azitaka Halmashauri Nchini Kudhibiti Ujenzi Holela

Na Munir Shemweta, WANMM MOROGORO
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula amezitaka halamashauri nchini kuhakikisha zinadhibiti ujenzi holela kwa kuhakikisha utoaji vibali vya ujenzi ktika maeneo yao unazingatiwa na kusimamiwa ipasavyo.

Dkt Mabula alitoa kauli hiyo kwa nyakati tofauti jana katika halmashauri za wilaya za Morogoro, Mvomero pamoja na Manispaa ya Morogoro wakati wa ziara yake ya kukagua utendaji kazi wa sekta ya ardhi katika mkoa wa Morogoro.

Alisema, halmashauri nchini zina wajibu wa kudhibiti ujenzi holela katika maeneo mbalimbali kwa kushirikiana na Watendaji wa Mitaa na kuweka taratibu ambazo hazitamruhusu mtu kufanya ujenzi wowote bila kupata kibali cha ujenzi kutoka halmashauri husika.

‘’ ili kuondokana na ujenzi holela katika halmashauri zenu mwananchi asifanye ujenzi wowote bila kupata kibali cha ujenzi kutoka halmashauri ‘’ alisema Dkt Mabula

Kwa mujibu wa Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, zoezi la urasimishaji linaloendelea sasa katika maeneo mbalimbali siyo zoezi la kudumu na kulegalega kudhibiti ujenzi holela kutasababisha zoezi hilo kutokuwa na maana kwa kuwa ujenzi holela utakuwa ukiendelea.

Akigeukia suala la utoaji hati za ardhi, Dkt Mabula aliagiza Hati zilizokamilika katika ofisi za Msajili wa Hati wamiliki wake watangaziwe kupitia njia mbalimbali zikiwemo radio  za Kijamii (Local Radio) sambamba na hati hizo kutolewa kwa wamiliki wake katika eneo maalum litakaloandaliwa  karibu na maeneo wanaoishi wamiliki wa hati hizo.

Alisema, njia ya kuwatafuta wananchi ambao hati zao zimekamilika itasaidia kupunguza mlundikano wa Hati za Ardhi zilizokamilika kwenye Ofisi za Msajili wa Hati tofauti na utaratibu wa sasa unaomtaka mwenye hati kuifuata ofisi za ardhi au ile ya Kamishna Msaidizi wa Ardhi za Kanda kwenda kuchukua.

Awali Mkuu wa Idara ya Ardhi katika halmashauri ya wilaya ya Morogoro Patrick Mwakilili alisema halmashauri yake imepanga kupima viwanja 1,000 kwenye  makao makuu ya wilaya Mvuha na viwanja 3,900 katika mji mdogo wa Kisaki ambao ni lango la kuingilia Mradi wa Kufufua Umeme wa Stiglers George na Hifadhi ya Taifa ya Mwl Nyerere zamani Selous.

Kwa mujibu wa Mkuu huyo wa Idara ya Ardhi Halmashauri ya wilaya ya Morogoro,  tayari maeneo tisa ya kufanyiwa urasimishaji makazi yameanishwa aliyoyataja kuwa ni Pangawe, Mkambarani, Fulwe, Ngerengere, Mvuha, Kisaki , Mtamba, Mkuyuni na Dhutumi na kubainisha kuwa halmashauri yake imepokea na kuridhia maombi kutoka makampuni manne kwa ajili ya kazi hiyo.

Wakati huo huo, Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula amekagua maendeleo ya ujenzi wa Ofisi za Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) zilizopo katika wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro, ujenzi unaofanywa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC).

Akiwa katika ukaguzi huo, Dkt Mabula mbali na kulipongeza Shirika la Nyumba la Taifa kwa kuisimamia vyema miradi yake ya ujenzi katika maeneo mbalimbali nchini ameridhishwa na kasi ya ujenzi wa Ofisi hizo za TFS hasa baada ya kuelezwa na Msimamizi wa ujenzi huo Mhandisi Grace Musita kuwa hatua iliyofikiwa sasa na Shirika lake katika kujenga ofisi hizo za TFS ilitakiwa kufikiwa tarehe 13 Desemba 2019.


Share:

Mwijage Amwaga Milioni 74 Kagera.

Na Avitus Benedicto Kyaruzi,Kagera.
Zaidi ya shilingi milioni 74 zimetolewa na mbuunge wa jimbo la Muleba Kaskazini mh Charse Mwijage katika kuchangia maendeleo ya kata Kamachumu  iliyopo Wilayani Muleba Mkoani Kagera.
 
Hayo yamesemwa na Mbunge wa jimbo hilo Mh Charse Mwijage Nov 20, 2019 wakati akiongea na wananchi kwenye ufunguzi wa kuwatambulisha na kuwanadi wagombea wanao wania nafasi mbalimbali katika  uongozi wa serikali za mitaa kupitia chama cha mapinduzi CCM Wilayani humo mkutao uliofanyika katika kata ya  Kamachumu.
 
Aidha Mh Mwijage amesema kuwa licha ya yeye kuchangia kiasi hicho cha fedha kwa lengo la kuunga mkono jitihada za kuchangia maendeleo kwenye kata hiyo ameongeza kuwa zaidi ya shilingi bilioni moja zimetolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano Wa Tanzania Mh John Pombe Magufuri kwenye kata hiyo.
 
Mbali na kiasi icho pia mh Mwijage amechangia ujenzi wa vyumba vinne pamoja na mabati 180,katika hospitali ya Ndorage iliyopo Wilayani humo.
 
Ameongeza kuwa wananchi wa jimbo hilo watazidi kunufaika na miradi mbalimbali ya kimaendeleo uku akitaja uzinduzi wa Chuo  Cha Ufundi  Cha Wilaya Ya Muleba Veta kitakacho funguliwa  rasmi na Waziri wa Elimu Mh Joyce Ndalichako mnamo tarehe 28/11/2019.
 
Amewataka viongozi watakao chaguliwa  kupitia chama hicho kufanya kazi kwa bidii na kufuata sheria na ilani ya chama cha Mapinduzi ili kuwaletea wananchi maendeleo pasipo kufuata kabila wala itikadi za kisiasa.
 
Kwa upande wake mwenyekiti wa chama cha mapinduzi CCM Kata ya Kamachumu bwana Abdunuru Bengesi amesema kuwa ana mashaka na viongozi wanao wania nafasi hizo kwa kuwa walio wengi wana uzoefu katika uongozi na kuongeza kuwa mara baada ya kuchaguliwa viongozi hao watapewa semina elekezi ili kuweza kufanya kazi kuendana na kasi ya mh Rais.
 
Kwa upande wa wananchi wa kata hiyo wamempongeza mbunge wao kwa juhudi kubwa anazo zifanya za kuwaletea maendeleo huku wakihaidi kumpatia ushirikiano katika Chuo  Cha Ufundi  Cha Wilaya Ya Muleba Veta kwa kuwapeleka watoto wao kupata ujuzi mbali mbali katika chuo hicho.


Share:

Serikali Imeilekeza TPDC Kushawishi Viwanda Nchini Kutumia Gesi Asilia

Na Robert Hokororo, Mtwara
Serikali imeelekeza Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) kushawishi viwanda mbalimbali nchini kutumia gesi asilia inayozalishwa hapa nchini hatua itakayosaidia kupunguza matumizi ya nishati zinazoharibu mazingira.
 
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa Sima ametoa maelekezo hayo alipotembelea miradi ya kuchakata gesi katika maeneo ya Mnazi Bay na Madimba mkoani Mtwara wakati wa ziara ya kukagua shughuli za mazingira zinavyofanyika katika miradi hiyo.
 
Sima pamoja na kupongeza miradi ya uzalishaji wa nishati hiyo alisema kuwa hakuna sababu ya viwanda kuharibu mazingira kwa kutumia nishati kama mafuta ambayo imezoeleweka na badala yake vianze kutumia gesi asilia ambayo ni rafiki wa mazingira.
 
“Katika ziara hii tumejifunza mambo mengi na hapa tunaona juhudi zinazofanyika kuhakikisha tunapata gesi asilia na tumeambiwa hapa kinazalishwa, kuchakatwa na kusafirishwa kiwango kikubwa cha gesi hivyo Serikali inaelekeza ninyi TPDC (Shirika la Petroli Tanzania) mkae na CTI (Shirikisho la Viwanda) muwashishi kuona sasa namna ya kutumia gesi asilia na kuachana na mafuta kwani yanaharibu mazingira,” alisema.
 
Aidha, Sima ambaye aliambatana na Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) alitoa maelekezo kwa kampuni zinazojihusisha na uchakataji wa gesi asilia kuomba kibali cha viwango cha uchafuzi wa hewa vinavyozalisha katika shughuli zao za kila siku.
 
Alifafanua kuwa viwanda hivi vina jukumu la kufuata Sheria ya Mazingara ya Mwaka 2004 hivyo pamoja na kuishirikisha jamii kujua madhara yanayoweza kutokea kutokana na nishati hiz lakini pia ni lazima NEMC watambue viwango vya uchafuzi wa mazingira hususan katika hewa zinazotokana na shughuli za uckakataji wa gesi.
 
“Hi sasa dunia inakabiliwa na changamoto ya mabadiliko ya tabianchi ambayo yana athari kubwa kwa mazingira yetu hivyo tunapoanzisha miradi kama hii lazima tuombe vibali ili tujue standards za pollution tunazozalisha na kama ikizidi utaratibu basi tuanze kulipa tozo kwa mujibu wa taratibu.
 
“Tunatambua juhudi kubwa zinazofanywa na viwanda hivi vya gesi na hapa,tunaambiwa kuna visima takriban vitano na vinafanya vizuri ambapo takriban futi za ujazo zaidi milioni 90 sawa na asilimia 90 ya pure gas inasambazwa katika maeneo mengine ya nchi na hapa tayari tuna hazina kubwa ya nishati hii,” alisema.
 
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa NEMC Dkt. Samuel Gwamaka alitaka viwanda vyote vinavyojishughulisha na shughuli kama hizo za uchakatiji wa gesi kuwa na mpango wa jinsi wanavyoratibu uchafuzi wa hewa ili kuweza kukabiliana na changamoto kama hizo katika mazingira.
 
Pamoja na mambo mengine pia Dkt. Gwamaka alitaka ziungwe mkono juhudi za uzalishaji wa gesi zinazofanyika katika miradi hii ili kuweza kuhifadhi mazingira kutokana na kuepukana na ukataji wa miti kwa ajili ya nishati.
 
Naibu Waziri Sima na NEMC wako katika ziara kwenyue mikoa ya Lindi na Mtwara kukagua miradi ya visima vya gesi kuona kama inafuata Sheria ya Mazingira ya mwaka 2004 na namna mabavyo wanatoa elimu kwa wananchi kuhusu namna ya kuchukua hatua pindi yanapotokea maafa yakiwemo kuvuja kwa nishati hiyo katika mabomba.


Share:

TAKUKURU Geita yawakamata viongozi wa AMCOS waliotafuna fedha za wakulima.

NA SALVATORY NTANDU
Taasisi ya Kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU) mkoani wa Geita imefanikiwa  kurejesha shilingi milioni 23 kati ya 49 zilizokuwa zimeibwa na baadhi ya  viongozi wa vyama vya Ushiriaka (AMCOS) 8 katika wilaya Mbogwe.

Kauli hiyo imetolewa jana na Kamanda wa TAKUKURU mkoa wa Geita, Leonidas Felix katika hafla maalumu ya kukabidhi shilingi milioni 15 kwa wakulima wa chama cha ushirika Mwanza madaso zilizorudishwa na baadhi ya viongozi wa AMCOMS hizo.

Amesema TAKUKURU iliendesha zoezi la ukaguzi katika AMCOS zote katika mkoa wa Geita na kubaini baadhi ya viongozi wake kutumia fedha za wakulima wa zao la pamba kujinufaisha wao na kutowalipa kwa kuwahadaa kuwa kampuni za ununuzi bado hazijalipa licha ya kuwa wao tayari wameshalipwa.

“Mpaka sasa tunawashikilia viongozi 22 wa AMCOS mbalimbali katika mkoa wetu ambao wameiba fedha za wakulima tumewapa wiki mmoja tuu kurejesha fedha hizo wengine tayari wameanza kutiii agizo hili na kurejesha shilingi milioni 23”alisema Felix.

Amefafanua kuwa katika zoezi la ufuatiliaji wa madeni ya wakulima wa zao la pamba katika mkoa huo wamebaini baadhi ya kampuni za ununuzi wa zao la pamba kutowalipa wakulima ambapo katika halmashauri ya wilaya ya  Geita wakulima wanadai zaidi ya shilingi bilioni 1 ambazo wanapaswa kuzilipa kwa muda wa wiki mmoja ili kuwawezesha kujiandaa na msimu mpya wa kilimo.

Katika hatua nyingine Mkuu wa Wilaya Mbogwe,  Matha Mkupas  amewataka viongozi wa AMCOS kwa kushirikiana na Maafisa Ushirika kuhakikisha wakulima wanalipa madeni ya pembejeo ya msimu uliopita kabla ya kulipwa fedha zao  baada ya kampuni za ununuzi wa pamba kuwalipa.

“serikali ya awamu ya Tano haiwezi kukubali wakulima wake kuendelea kunyanyaswa na viongozi wa AMCOS ambao ni wabadhilifu wanaowaibia wakulima tutahakikisha tunawakamata wote hadi walipe fedha za wakulima”alisema Mkupas.

Nao baadhi ya wakulima wa Zao la Pamba katika AMCOS ya Mwanza Madaso, Suzana Nkinjiwa na Rafael Shizya wamesema kucheleweshwa kwa malipo ya zao hilo kwa msimu huu yatasababisha kushuka kwa uzalishaji kutokana na wakulima wengi kukata tamaa.


Share:

Serikali Yaahidi Kuendelea Kusimamia Maslahi Ya Wafugaji Na Kuwataka Kufuata Sheria Za Nchi

Na. Edward Kondela
Serikali imewataka wafugaji katika Wilaya za Chunya na Mbarali Mkoani Mbeya kufanya shughuli zao kwa kufuata sheria na taratibu za nchi ikiwemo ya kutoingiza mifugo katika maeneo ya Hifadhi za Taifa ya Ruaha na Pori la Akiba la Ruangwa, hali ambayo imekuwa ikisababisha migogoro kati ya wafugaji na askari wa Hifadhi za Taifa (TANAPA), wanaolinda hifadhi hizo ambapo baadhi ya migogoro hiyo imesababisha vifo vya wafugaji, askari na mifugo.

Akizungumza Jumanne hii (19.11.2019) wakati wa kuhitimisha ziara ya siku mbili ya makatibu wakuu kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Wizara ya Maliasili na Utalii pamoja na Wizara ya Sheria na Katiba, waliozuru baadhi ya maeneo yenye migogoro katika wilaya hizo, Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo) Prof. Elisante Ole Gabriel amewataka wafugaji kuacha tabia ya kuingiza mifugo katika maeneo ya hifadhi kwa ajili ya malisho kwa kuwa ni kinyume na taratibu za nchi.

“Serikali inawataka wafugaji wote kufanya shughuli zao kwa kufuata sheria na kutoingiza mifugo katika maeneo ya hifadhi za taifa kwa kuwa ni kinyume cha sheria pia serikali itaendelea kuhakikisha wafugaji wanafanya shughuli zao kwa amani bila kubughudhiwa ili mradi wanafuata sheria na taratibu za nchi ikiwemo ya kutoingiza mifugo katika mashamba ya wakulima.” Amesema Prof. Gabriel

Akizungumza kwa niaba ya makatibu wakuu wa wizara hizo, Prof. Gabriel amefafanua kuwa kutokana na Tangazo la Serikali (GN) Na. 28 la Tarehe 14 mwezi Machi mwaka 2008, ambalo liliongeza eneo la Hifadhi ya Taifa ya Ruaha kutoka Kilometa za Mraba 5,878 hadi kufikia Kilometa za Mraba 20,226 hali hiyo imesababisha eneo la malisho kupungua kutoka hekta 259,000 za awali hadi 154,000 katika Wilaya za Chunya na Mbarali ambapo amewataka wafugaji katika wilaya hizo kuheshimu tangazo hilo wakati serikali ikifanyia kazi maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ya kuainishwa kwa vijiji vilivyopo katika maeneo ya hifadhi ili maboresho yaweze kufanyika kwa maslahi ya vijiji hivyo.

Katika ziara hiyo ya makatibu wakuu kutoka wizara nne Mkoani Mbeya uongozi wa TANAPA umekubali kutengeneza barabara za kuainisha mipaka ya maeneo ya hifadhi na vijiji mara baada ya kuainishwa kwa mipaka mipya kufuatia agizo la Rais Dkt. John Magufuli la kutambuliwa kwa  maeneo ya vijiji na hifadhi za taifa ambalo tayari linafanyiwa kazi.

Kufuatia matukio ya mauaji ya askari mmoja wa TANAPA na askari mgambo mmoja mwaka 2018 waliouawa na wafugaji wakati wakiswaga ng’ombe waliokamatwa katika Hifadhi ya Ruaha kuelekea Kambi ya Nyota ya TANAPA  iliyopo Wilaya ya Mbarali na tukio la hivi karibuni la Tarehe 11 Mwezi Oktoba 2019 la kuvamiwa kwa kambi hiyo na baadhi ya wafugaji wakiwa na silaha za jadi kwa nia ya kukomboa mifugo iliyokamatwa katika Hifadhi ya Ruaha hali iliyosababisha kijana mmoja wa wafugaji (19) kupigwa risasi na askari wa TANAPA na ng’ombe 14 kuuawa, Katibu Mkuu Prof. Gabriel amewataka wafugaji kutumia njia zisizo halali kukomboa mifugo iliyokamatwa.

Akizungumza na baadhi ya wafugaji katika Kijiji cha Igunda, Kata ya Igava Wilayani Mbarali, katibu mkuu huyo amefafanua kwa wafugaji hao kuwa kutokana na sheria na haki za wanyama duniani ni makosa kuua mnyama bila kuwa na sababu za msingi hali iliyosababisha serikali kuchukua hatua kwa askari wa TANAPA waliohusika kupiga ng’ombe hao risasi na hivyo kuwataka wafugaji hao kuwa watulivu kwa kuwa suala hilo linashughulikiwa na vyombo vya dola.

Aidha ameeleza kuwa kuwa pindi mifugo inapokamatwa na askari wa TANAPA inapobainika kuingia kwenye maeneo ya hifadhi, wamiliki wa mifugo hiyo wanapaswa kufuata taratibu za kisheria za kulipa faini na kukabidhiwa mifugo yao na kusisitiza kuwa ni muhimu kwa wafugaji kujiepusha kuingiza mifugo maeneo wasiyoruhusiwa yakiwemo ya Hifadhi za Taifa.

“Sisi viongozi wa Wizara za Mifugo na Uvuvi, Maliasili na Utalii, Mambo ya Ndani ya Nchi na Sheria na Katiba tunasikitishwa sana na matukio haya ya mauaji kijana mdogo amefariki dunia kwa sababu ambazo zingeweza kuepukika kwa kutaka kumdhuru askari kwa kutumia silaha za jadi akiwa na wenzake takriban 20 ili kukomboa ng’ombe waliokamatwa hifadhini, tunawaomba mjiepushe na matukio ya namna hii fuateni sheria na taratibu za nchi ili mfuge bila bughudha.” Amefafanua Prof. Gabriel

Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo) Prof. Elisante Ole Gabriel akiwaongoza viongozi wenzake katika ziara hiyo akiwemo Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Bw. Ramadhan Kailima, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Sheria na Katiba Bw. Amon Mpanju na Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori Dkt. Maurus Msuha akimwakilisha Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Prof. Adolf Mkenda wamefika pia katika Kijiji cha Lualaje Kata ya Lualaje Wilayani Chunya na kuzungumza na baadhi ya wafugaji kufuatia matukio ya wafugaji hao kuingiza ng’ombe katika Hifadhi ya Ruaha.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Bw. Ramadhan Kailima amewataka wafugaji hao kufuata sheria na taratibu za nchi na kwamba jeshi la polisi litazidi kutoa ushirikiano kwa wafugaji hao katika matukio mbalimbali yakiwemo ya kuwabaini baadhi ya wafugaji ambao wamekuwa wakiingiza mifugo katika maeneo ya hifadhi pamoja na kujihusisha na uhalifu.

Naye Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Sheria na Katiba Bw. Amon Mpanju amewataka wafugaji kuwa watulivu na walitambue Tangazo la Serikali Na. 20 la Tarehe 14 mwezi Machi mwaka 2008, ambalo liliongeza eneo la Hifadhi ya Taifa ya Ruaha na kupunguza eneo la malisho katika Wilaya za Chunya na Mbarali hali iliyosabisha baadhi ya maeneo waliyokuwa wakiyamiliki kubadilishwa matumizi na kuwa ya hifadhi, ambapo suala hilo tayari linafanyiwa kazi kwa maelekezo ya Rais Magufuli na kuwataka kutoingiza mifugo yao katika eneo la hifadhi hadi serikali itakapotangaza maamuzi mengine.

Kuhusu kuainishwa kwa mipaka kati ya vijiji na Hifadhi ya Taifa ya Ruaha pamoja na Pori la Akiba la Ruangwa, akizungumza kwa niaba ya katibu mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori kutoka katika wizara hiyo Dkt. Maurus Msuha amesema serikali kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii itahakikisha inatuma timu ya wataamu katika maeneo hayo ili kuweka alama maeneo ambayo wananchi yanawatatiza kufahamu mipaka ya vijiji na maeneo ya hifadhi ili kuondoa migogoro kati ya maeneo ya wakulima na wafugaji na mipaka ya Hifadhi ya Ruaha na Pori la Akiba la Ruangwa.

Baadhi ya wananchi katika Wilaya za Chunya na Mbarali waliopata fursa ya kuzungumza wakati wa ziara ya makatibu wakuu kutoka Wizara za Mifugo na Uvuvi, Maliasili na Utalii, Mambo ya Ndani ya Nchi na Sheria na Katiba wamesema wamefurahishwa na ziara hiyo na kwamba watazingatia maelekezo waliyopatiwa ili kuhakikisha wanafuga kwa kufuata sheria na kwamba watashirikiana na serikali ili kuwabaini baadhi ya wafugaji wanaokiuka sheria na kuingiza mifugo katika maeneo ya Hifadhi ya Ruaha na Pori la Akiba la Ruangwa.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti wamefafanua kuwa wamefurahishwa kwa viongozi hao wa juu kutoka wizarani kufika hadi katika maeneo yao na kujionea changamoto mbalimbali zinazowakabili ikiwemo ya maji na malisho pamoja na kupata taarifa za matukio ambayo yamejitokeza katika wilaya hizo kutoka mamlaka mbalimbali za serikali wakiwemo viongozi wa serikali, wafugaji pamoja jeshi la polisi.

Awali kabla ya makatibu wakuu hao kutembelea wafugaji katika Wilaya za Chunya na Mbarali, wamefika katika Ofisi ya Mkuu wa Mbeya na kuwa na mazungumzo na mkuu wa mkoa huo Mhe. Albert Chalamila pamoja Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Mbeya, ambapo Mhe. Chalamila amewaambia serikali ya mkoa huo itaendelea kufanya kazi kwa kusimamia sheria na kuwaasa viongozi wenzake wanapofika mkoani hapo kupata taarifa sahihi ya mkoa kabla ya kufika katika maeneo mbalimbali kuzungumza na wananchi.

Aidha Mhe. Chalamila amebainisha kuwa migogoro ya wafugaji katika Wilaya za Chunya na Mbarali ambao wamekuwa wakiingiza mifugo kwenye maeneo ya Hifadhi ya Ruaha na Pori la Akiba la Ruangwa katika Mkoa wa Mbeya unatokana na wafugaji kuwa na mifugo mingi tofauti na maeneo ya malisho, hali ambayo imekuwa ikiulazimu uongozi wa mkoa kutoa elimu kwa wafugaji juu ya ufugaji wa kisasa na wenye tija kwa wafugaji kuwa na ng’ombe wachache wanaoweza kuwapatia matokeo mazuri.

Ameongeza kuwa uongozi wa Mkoa wa Mbeya utazidi kusimamia na kutoruhusu mifugo kuingizwa katika maeneo ya hifadhi pamoja na maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya uhifadhi wa mazingira ili kuhakikisha mkoa huo unakuwa na mpango wa matumizi bora ya ardhi.

Katika ziara hiyo ya makatibu wakuu wanne Mkoani Mbeya, ikiongozwa na Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo) Prof. Elisante Ole Gabriel akiambatana na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Bw. Ramadhan Kailima, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Sheria na Katiba Bw. Amon Mpanju na Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori Dkt. Maurus Msuha akimwakilisha Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Prof. Adolf Mkenda, ilikuwa na lengo la kupata taarifa sahihi ya hali ya wafugaji katika Wilaya za Chunya na Mbarali pamoja na kupata hadidu za rejea ambazo wataalam watatumia katika kufanya mapitio na maboresho ya Tangazo la Serikali (GN) Na. 28 la Mwaka 2008 ili iwe shirikishi na kupata suluhu ya migogoro ya wakulima na wafugaji.

MWISHO


Share:

Watu 6 Wafikishwa Mahakamani na TAKUKURU Kwa Uhujumu Uchumi

Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa (Takukuru) kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi, Jumatano Novemba 20, imewakamata na kuwafikisha mahakamani wafanyabiashara sita wakiwamo raia wa kigeni kutoka nchini China kujibu mashtaka ya Rushwa na uhujumu uchumi.

Kaimu Mkurugenzi wa Uchunguzi), Wli Mfuru amewataja watuhumiwa hao waliofikishwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kibaha mkoani Pwani kuwa ni You Hattao, Zhang Zhi Xin wote raia wa China, wengine ni John Mnyele, Loncolin Ilungu, Andrew Kowelo na Emmanuel Maro, ambao wote ni watanzania.
 
Amesema watuhumiwa hao wamekuwa wakimiliki kampuni maeneo ya Kibaha inayotengeneza na kuuza mafuta aina ya Dizeli yaliyo chini ya kiwango na kuyauzia baadhi ya kampuni zinazofanya biashara hiyo bila kufuata taratibu za ufanyaji biashara.

"Uchunguzi uliofanywa na Takukuru kwa kushirikiana na jeshi la polisi limebaini kampuni ya SHIN UP iliyopo Visiga imejihusisha na vitendo vya rushwa pamoja  na uhujumu uchumi na kusababisha serikali hasara ya zaidi ya 1.2 bilioni," amesema Mfuru

"Pamoja na mambo mengine, kampuni hii imeghushi vyeti vya kuwawezesha kufanya biashara nchini, inakwepa kodi pamoja na watuhumiwa kujihusisha na mtandao wa uhalifu," alisema

Amewataja watuhumiwa hao ni Yu Hattao na Zhang Zhi ambao wote ni raia wa China, John Mnyele, Lincolin Ilungu, Andrew Kowelo na Emmanuel Maro ambao ni Watanzania.

Mfuru amesema Oktoba 3O, 2019 Takukuru iliwafikisha mahakamani watuhumiwa watatu kati ya hao ambapo washtakiwa wengine wameeunganishwa nakuongezewa mashtaka yakiwemo utakatishaji fedha na uhujumu uchumi.


Share:

Mzee wa miaka 70 ashambuliwa na Fisi akiwa amelala usiku.

NA SALVATORY NTANDU
Mkazi wa kijiji cha chela katika Halmashauri ya Msalala Mkoani Shinyanga, Buluba Jilasa (70) amejeruhiwa na fisi kwa kung’atwa sehemu mbalimbali za mwili wake akiwa amelala.

 Akizungumza na waandishi wa habari akiwa anapatiwa matibabu katika hospitali ya Halamashauri ya Mji wa kahama Jilasa amesema tukio hilo limetokea jana usiku wakati akiwa amelala, nyumbani kwake alishituka mlango ukivunjwa na fisi huyo ambaye aliingia hadi chumbani na kuanza kumjeruhi.

 “Nimepambana naye ili asimdhuru,lakini alifanikiwa kuning’ata kiganja cha mkono wa kushoto na kunisababishia majeraha makubwa katika maeneo mbalimbali ya mwili wangu”alisema Jilasa.

Amesema aliweza kumdhibiti fisi huyo  ambaye baadae alianza kushambulia kuku na ndipo alipotoka na kwenda kumgongea mjukuu wake Charles Bushemeli kwaajili ya kuomba msaada.

Nae afisa Mtendaji wa kijiji cha Chela Zaphline Samweli amesema tukio la fisi kuvamia kwenye mkazi ya wananchi sio lakwanza na wamekuwa wakivamia nyakati za usiku na kushambulia mifugo kama vile Ng’ombe, Mbuzi pamoja na Punda kutokana na uwepo wa milima mingi.

Amesema  mapango yaliyopo kwenye milima iliyopo kijijini hapo ndio makazi ya wanyama hao  wanapojificha na kuwataka wananchi kuchukua tahadhari na kutoa taarifa kwa maafisa maliasili pindi wanapowaona wanayama hao.

Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Halmashauri ya mji wa kahama Dk George Masasi amethibitisha kumpokea  majeruhi huyo ambaye alikuwa na majeraha sehemu mbalimbali za mwili wake na ameshaapatiwa huduma ya  matibabu na anaendelea vizuri.

“Tumemchoma sindano ya  kuzuia asipate kichaa kinachotakana na kung’atwa na fisi(Anti Rabies)na  mkono wake wa kushoto umeshambuliwa vibaya unatakiwa kukatwa kiganja alisema Masasi.


Share:

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi November 21

















Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger