Tuesday, 5 November 2019

Kimataifa | Marekani kujiondoa rasmi makubaliano ya tabia nchi ya Paris

Marekani imeanza rasmi mchakato wa kujitoa kutoka katika makubaliano ya Paris ya mazingira, kulingana na waziri wake wa mambo ya kigeni Mike Pompeo.

Rais wa  Marekani Donald Trump  alikuwa  mpinzani  mkubwa  wa makubaliano  hayo  wakati  alipokuwa  anawania  kiti  cha  urais, na utawala  wake  umekuwa  ukifanya  kila  unaloliweza kubadilisha sheria  za  mazingira, ukisema zinazuwia  biashara  na  kutoa  kwa nchi  nyingine  nguvu  ya  ushindani.

Pompeo alielezea  kuhusu kile  alichokiita "mzigo usio wa  haki wa kiuchumi uliowekwa  kwa  wafanyakazi wa  Marekani, biashara, na walipa  kodi, kwa  ahadi za Marekani  zilizotolewa  chini  ya makubaliano  hayo," wakati  akitangaza  kujitoa  huko. Amesema ,"mfano bora  na  wenye  uhalisia" utapendekezwa  na  Marekani kupinga  makubaliano  hayo  ya  dunia.

Makubaliano  ya  mwaka  2015 yalitiwa  saini  na  karibu  nchi  zote, na  kuuweka  utawala  wa  Trump  dhidi  ya  karibu  washirika  wake wote  pamoja  na  washindani  wake  wakuu  kuhusiana  na  suala  la mabadiliko  ya  tabia  nchi. Trump  binafsi  ni  mtu  mwenye  shaka na  mabadiliko  ya  tabia  nchi.

Utawala  wa  Trump rasmi uliuarifu  Umoja  wa  mataifa  hatua  yake hiyo  ya  kujitoa  siku ya Jumatatu, ukianza  mchakato  wa  mwaka mmoja  ambao  utakamilika  siku  moja  baada  ya  uchaguzi  wa  rais wa  Marekani  mwaka  2020.

Msemaji  wa  Umoja  wa  mataifa  alilithibitishia shirika  la  habari  la Ujerumani dpa kuwa  taasisi  hiyo  ya  dunia  imepokea  barua ya Marekani.

Credit:DW


Share:

Video Mpya | Harmonize - UNO

Video Mpya |  Harmonize - UNO


Share:

Video Mpya | Walter Chilambo - God Of Mercy

Video Mpya | Walter Chilambo - God Of Mercy


Share:

Video Mpya | Kayumba Ft Linah - UMENIWEZA

Video Mpya | Kayumba Ft Linah - UMENIWEZA


Share:

NAIBU WAZIRI WA AFYA AFUNGUA WARSHA YA WADAU WA UTAFITI KANDA YA ZIWA

Share:

Ofisi Yavunjwa, Nyaraka mbalimbali zikiwemo fomu za uchaguzi Zaibiwa

Mnamo tarehe 31.10.2019 majira ya saa 19:50 usiku huko Kijiji cha Pashungu, Kata ya Itawa, Tarafa ya Isangati, Wilaya ya Mbeya Vijijini, Mkoa wa Mbeya. JACKSON MATONYA [28] Afisa mtendaji wa Kijiji cha Pashungu, mkazi wa Pashungu aligundua kuvunjwa ofisi ya Kijiji cha Pashungu na kuibiwa nyaraka mbalimbali kama ifuatavyo;

1. Fomu za wagombea wenyeviti wa vijiji na vitongoji.
2. Fomu za wajumbe wa kundi maalum la wanawake zilizojazwa 21 za
wagombea wa chadema 7 za wagombea wa ccm.
3. Fomu 24 za wenyeviti wa vijiji na vitongoji ambazo hazijajazwa.
4. Fomu 46 za kundi maalum la wanawake ambazo hazijajazwa.
5. Mhuri wa msimamizi msaidizi wa uchaguzi.
6. Faili moja la mihtasari ya malipo ya walengwa wa TASAF.
7. Faili la mihtasari ya vikao vya Halmashauri ya Kijiji na mikutano ya hadhara.
 
Kutokana na tukio hilo, jumla ya watuhumiwa nane [08] wamekamatwa ambao ni:-
1. MWAWA POSTA [40] katibu wa CHADEMA Kata ya Itawa
2. ENOCK JECK MWASILE [25]
3. ALEX JECK MWASILE [21]
4. AMONI SIFUKU MWASILE [40]
5. ALUWA JOHN NGELEKA [37]
6. BAHATI SIFUKU YANJILWA [45]
7. MOSKO ALLAN MWASELE [32]
8. CHARLES MANGENI MWASILE [31] wote wakazi wa Kijiji cha Pashungu.


Share:

RC MONGELLA AZINDUA MAADHIMISHO YA MAULID KITAIFA JIJINI MWANZA

Share:

Msimamo Wa Ligi Kuu Tanzania Bara Ulivyo Kwa Sasa




Share:

PICHA: CAG Mpya Akabidhiwa Ofisi Rasmi

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) mpya Charles Kichere, aliyeapishwa jana Novemba 04, amekabadhiwa ofisi na Mtangulizi wake Prof. Mussa Assad leo Novemba 05, katika makao makuu ya ofisi hiyo yaliyopo jijini Dar es Salaam.

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) mpya Charles Kichere, aliyeapishwa jana Novemba 04, akikabidhiwa Rasmi ofisi na Prof. Mussa Assad aliyemaliza muda wake leo Novemba 05, 2019 katika makao makuu ya ofisi hiyo yaliyopo jijini Dar es Salaam.



Share:

LIVE: Kutoka Bungeni Dodoma Kwenye Kipindi Cha Maswali Na Majibu

LIVE:  Kutoka Bungeni Dodoma Kwenye Kipindi Cha Maswali Na Majibu


Share:

Iran yatangaza hatua mpya za kukiuka mkataba wa silaha za nyuklia

Iran imetangaza leo hatua zake mpya za kukiuka makubaliano makubwa ya silaha za nyuklia yaliyosainiwa mwaka 2015 kati ya mataifa yenye nguvu kubwa duniani. 

Iran imesema kwa sasa inatumia nyenzo ambayo ina kasi ya mara 50 zaidi ya ile iliyokubaliwa na mkataba huo. 

Tangazo hilo limetolewa wakati Iran ikianzisha maadhimisho ya kumbukumbu ya miaka 40, tangu Marekani ilipoukamata ubalozi wake mnamo mwaka 1979, mzozo uliodumu kwa siku 444. 

Mkuu wa shirika la kitaifa la nishati ya Atomiki nchini Iran Ali Akbar Salehi amesema kwa kuanza kutumia nyenzo hizo za kasi kubwa, Iran itapunguza muda wa mwaka mmoja ambao wataalam walisema Iran itauhitaji ili kuwa na vifaa vyote vya kutengeneza silaha za nyuklia endapo itaamua kufanya hivyo. 

Iran ilishakiuka makubaliano hayo kuhusu urutubishaji madini ya urani kama hatua ya kuushinikiza Umoja wa Ulaya kupata mkataba mpya, mwaka mmoja tangu Marekani ilipojiondoa katika mkataba huo.

-DW


Share:

Waziri wa Kilimo: Tumejipanga Kudhibiti Sumukuvu

Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Arusha
Hivi karibuni, Serikali ya Tanzania ilipata fedha za kutekeleza mradi wa kuzuia kuenea kwa sumukuvu hapa nchini (TANIPAC). Mradi huo unalenga kupunguza kutokea kwa madhara ya sumukuvu katika mfumo wa chakula kupitia udhibiti husishi kwenye mnyororo wa thamani wa mazao ya mahindi na karanga, hivyo kuboresha uhakika na usalama wa chakula na hatimae kuimarisha afya na lishe ya jamii yetu na kuimarisha biashara kati ya Tanzania na nchi zinazotuzunguka.

Mradi huo unatekelezwa kwa kuzingatia mkakati Madhubuti kwa kushughulikia masuala yote yanayohusu sumukuvu hapa nchini. Mkakati huo unazingatia udhibiti wa sumukuvu katika hatua za uzalishaji, uvunaji, udhibiti wa kibilojia, teknolojia baada ya kuvuna na njia za ukaushaji, uhifadhi, kujenga uwezo wa kitaasisi, uratibu na kutoa elimu ya kuhamasisha wadau muhimu. Ushiriki wa sekta binafsi ni muhimu katika uhaulishaji wa teknolojia pamoja na kuhakikisha mradi unakuwa endelevu.

Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) ameyasema hayo leo tarehe 4 Novemba 2019 wakati akifungua Mkutano wa kwanza wa Afrika wa kudhibiti Sumkuvu (Alfasafe) kwenye vyakula uliofanyika katika Hoteli ya Mount Meru Jijini Arusha.

Mhe Hasunga amesema kuwa Ushirikiano wa kiutafiti, kati ya sekta binafsi na watunga sera, ni muhimu katika kufanikisha mageuzi ya kilimo.

Waziri Hasunga amesema kuwa Tangu kuibuka kwa tatizo la sumukuvu mwaka 2016, Tanzania imechukua hatua mbalimbali za kupunguza kusambaa kwa sumukuvu hapa nchini. Kwa kutambua changamoto za kukabili sumukuvu, ambapo kunahitajika kutumia njia mbalimbali kuanzia kwenye hatua za uzalishaji, uvunaji, uhifadhi, usindikaji na kuhusisha sekta za Umma na Binafsi katika kupunguza upotevu wa chakula na kuongeza upatikanaji wa chakula salama na lishe bora.

Amesema, Tanzania imeanzisha Kamati  Jumuishi ya Uendeshaji inayohusisha sekta na taaluma kutoka taasisi mbalimbali chini ya Uenyekiti wa Wizara ya Kilimo ambayo ina mamlaka ya kusimamia masuala yote yanayohusu sumukuvu.

Kadhalika, amewahakikishia washiriki hao kuwa kinga ya sumukuvu - Alfasafe TZ01;  imeshasajiliwa kwa matumizi hapa nchini Tanzania.  "Aidha, nimefarijika kuwa kazi hii inafanywa na Kampuni Binafsi ambayo imewekeza katika uzalishaji, na usambazaji wa bidhaa hii ambayo itaokoa Maisha ya watu hapa nchini" Alisisitiza

"Napenda kuwahakikishia utayari wa Wizara yangu katika kuyatumia maazimio mtakayokubaliana katika mkutano huu. Aidha, Serikali ya Tanzania, inatilia maanani na inaunga mkono hatua zinazochukuliwa katika kuhimiza biashara ya chakula salama, usalama wa chakula na lishe" Alisema Mhe Hasunga

Tanzania kwa sasa inatekeleza Awamu ya Pili Programu ya Uendelezaji wa Sekta ya Kilimo (ASDP II) yenye lengo la kuleta mageuzi ya sekta ya kilimo kuwa na kilimo chenye tija na kibiashara, pamoja na kukuza uchumi wa wakulima wadogo na kuboresha maisha, uhakika wa chakula na lishe bora.

Uhakika wa chakula na lishe ni muhimili ambao ni muhimu wa ASDP II Katika kufikia malengo hayo, uwekezaji katika utafiti wa kilimo ni muhimu katika kuleta matokeo kwa wakulima na wadua wengine katika mnyororo wa thamani.

Waziri Hasunga amesema kuwa kutokana na takwimu za Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) za mwaka 2017, Tanzania inaongoza katika uzalishaji wa mahindi na karanga katika ukanda wa nchi za Afrika Mashariki, kwa kuzalisha tani milioni 6 na tani milioni moja mtawalia.

Amesema, Pamoja na mafanikio hayo, Serikali inatambua kuwa, ingawa mazao hayo ni muhimu kwa chakula cha kila siku, lakini yanakabiliwa na ukubwa wa tatizo la sumukuvu ambalo linahatarisha usalama wa chakula na kuwa kikwazo cha biashara ya mazao hayo kwa nchi jirani na Tanzania.

Mkutano huu ambao umewaweka pamoja watafiti, wafanyabiashara, watunga sera na wadau wa maendeleo, ambao unalenga kupanga mikakati ya kuongeza kasi ya matumizi ya kinga ya sumukuvu (Alfasafe), na kukabili sumukuvu barani Afrika, unadhihirisha mabadiliko chanya ya kimtazamo tunayoyahitaji.


Share:

Shehena Ya Mifuko Isiyokidhi Viwango Yakamatwa

Ofisi ya Makamu wa Rais inaendelea kusimamia marufuku ya katazo la matumizi ya mifuko ya plastiki kwa kushirikiana na Kikosi kazi cha Kitaifa. 

Kwa siku za hivi karibuni kumekuwepo na wimbi la uzalishaji, utengezaji na uingizaji na usambazaji wa mifuko isiyokidhi viwango vilivyowekwa na Shirika la Viwango Tanzania (TBS).

Kikosi kazi cha Kitaifa cha kuzuia matumizi ya mifuko ya plastiki pamoja na Kamati za Mikoa na Wilaya wanaendesha oparesheni maalumu nchi nzima kwa lengo la kusaka mifuko isiyokidhi viwango.

Tarehe 30/10/2019 NEMC ilikamata marobota 21 katika Wilaya ya Misenyi, Mkoani Kagera na marobota 7 Mkoani Arusha ambayo yanashikiliwa katika kituo cha polisi cha Arusha. Upelelezi wa mashauri haya bado unaendelea.

Tarehe 4/11/2019 Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi kwa Mazingira (NEMC) kwa kushirikiana na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Mwanza wamekamata shehena ya mifuko isiyokidhi viwango gunia 8 yenye thamani ya Shilingi 10,000,000/-  Mifuko hiyo iliingia kupitia bandari bubu ya Bwiru jijini Mwanza ikitokea nchi jirani. Watuhumiwa watafikishwa mahakamani na mifuko hiyo itateketezwa kwa mujibu wa sheria kama itakavyoelekezwa na NEMC.

Ofisi ya Makamu wa Rais, inatoa wito kwa wafanyabiashara wote wanaojihusisha na uingizaji, usambazaji na uuzaji wa mifuko mbadala kuhakikisha wanazingatia matakwa ya Sheria. Aidha, wafanyabiashara wanasisitizwa kuacha kuzalisha, kuingiza nchini, kuuza na kusambaza mifuko isiyokidhi viwango. Hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya wote wanaokiuka agizo hilo.


Share:

Grant Coordinator Job at Norwegian Refugee Council (NRC)

Grant Coordinator  NRC is looking for a Grant Coordinator base at Kibondo, The purpose of the Grants Coordinator position is to provide essential grant management support to HoP and AM in delivering quality programmes in line with the NRC COs strategy and PoA for Tanzania. All NRC employees are expected to work in accordance with the organization’s core… Read More »

The post Grant Coordinator Job at Norwegian Refugee Council (NRC) appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Sales Agents Job at Jubilee Insurance

Job Location. DAR ES SALAAM Position: Sales Agents  Jubilee Insurance was established in August 1937, as the first locally incorporated Insurance Company based in Mombasa in 1937. Jubilee Insurance has spread its sphere of influence throughout the region to become the largest Composite insurer in East Africa, handling Life, Pensions, General and Medical Insurance. Today, Jubilee is the… Read More »

The post Sales Agents Job at Jubilee Insurance appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Procurement Officer Job at HelpAge International

Procurement Officer Dar es Salaam District Salary Range (Tsh)2,500,001 – 3,000,000 Person Specification At least Bachelor’s degree in Procurement and Supplies Chain Management or related discipline. Preferred at least 3 years procurement management experience. Working with INGO will be added advantage. Computer skills is required especially good command in excel and word. Facilitation and training skills. Donor funding… Read More »

The post Procurement Officer Job at HelpAge International appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Global Procurement Associate Job at One Acre Fund

Global Procurement Associate  Mbeya About One Acre Fund Founded in 2006, One Acre Fund supplies smallholder farmers with the agricultural services they need to make their farms vastly more productive. We provide quality farm supplies on credit, delivered within walking distance of farmers’ homes, and agricultural trainings to improve harvests. We measure our success by our ability to… Read More »

The post Global Procurement Associate Job at One Acre Fund appeared first on Udahiliportal.com.

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger