Tuesday, 13 August 2019

WAKULIMA WA NDIZI,PARACHICHI KAGERA WATAKIWA KUCHANGAMKIA SOKO UGANDA




Na Lydia Lugakila - Malunde1 blog Bukoba

Wakulima wa zao la ndizi mkoani Kagera wametakiwa kuchangamkia fursa ya mazao ya kilimo cha ndizi pamoja na upandaji wa miti ya parachichi kutokana na mazao hayo kuwa na soko kubwa la kiuchumi nchini Uganda.


Kauli hiyo imetolewa na jana Agosti 12,2019 na Balozi wa  Tanzania nchini Uganda Bwana Azizi Mlima wakati akitoa salamu za ubalozi wa Uganda katika mkutano wa wiki ya Uwekezaji Kagera ambao umewaunganisha  wafanyabiashara wa Tanzania (Kagera) na wafanyabiashara wa kutoka nchi za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Burundi,  Rwanda Uganda na Kenya katika Ukumbi wa ELCT uliopo katika Manispaa ya Bukoba Mkoani Kagera.

Mlima alisema uchumi wa Uganda umekua kwa 6% huku mazao ya kilimo cha ndizi na parachichi yakiwa na soko kubwa kiuchumi nchini humo ukilinganisha na nchi nyingine.

Kutokana na mazao hayo kuonekana kuwa na soko la kutosha  nchini Uganda hivyo  Balozi huyo aliwahimiza wakulima wa mazao hayo mkoani Kagera kulima kilimo kwani soko hilo linaweza kumkomboa Mtanzania kutoka katika hali ya umaskini.

Alisema kutokana na mkoa wa Kagera kupendeza na kuonekana wa rangi ya kijani lazima kijani hiyo ionekane katika ubora wa upandaji  miti ya maparachichi ambapo alisema nchini Uganda kilo moja ya parachichi huuzwa kwa shilingi 1200 hadi 1300.

Kuhusu suala la ugonjwa wa mnyauko wa migomba ambao unasumbua zao la ndizi mkoani Kagera,Mlima aliwataka wana Kagera kujitahidi kupambana ili kuutokomeza kwani nchini Uganda haupo kabisa.

Hata hivyo balozi huyo alimpongeza mkuu wa mkoa wa Kagera Brigedia Elisha Marco Gaguti katika jitihada anazozifanya za kimaendeleo ambazo zimeubadili mkoa huo huku akitaja ushirikiano uliopo kati ya nchi ya Tanzania na Uganda kuwa wa kuridhisha ambao umeunganishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa kumtembelea Rais wa Uganda Yoeri Museveni na kubadilishana mawazo yenye kuleta tija kwa wananchi wa pande zote mbili.

Alizitaja fursa zingine za kiuchumi zilizopo nchini humo kuwa ni fursa ya elimu ya Chuo Kikuu kuwa na unafuu sana na yenye ubora , fursa ya Bandari ya Dar es salaam – Uganda , fursa za kitalii, bomba la mafuta na bomba la gesi usafiri wa anga utokao Dar es salaam  Kia -Entebe nchini humo.

Wiki ya uwekezaji Kagera yenye lengo la kutangaza fursa zilizopo mkoani Kagera imeanza Agosti 12 mwaka huu itamalizika rasmi Agosti 17 mwaka huu.

Share:

Kutana na Sheikh Omary Mwenye Uwezo wakufanya Dua mbalimbali za Matatizo Yako Na Kutafsiri Ndoto kwa kutumia Vitabu vya QUR-AN

Sheikh Omary Ni bigwa wa kutatua matatizo kwa haraka, ni mtu aliye jaliwa kubuli Shufaa pia anatoa Duah  za Ruhia. Ukija na Maradhi yanaondoka hapo hapo bila kungoja kesho,  UKIPEWA MKONO  na Sheikh Omary .
 
Wasiliana na Mtaalam Huyu Kwani yeye hufaulu Pale wote waliko Shindwa na Pia Humaliza kazi zilizo Shindikana ama Zilizo Achwa ndani ya Siku Moja 1.
 
Sheikh Omary ni Mtaalamu wa Nyota za Binadamu  Mwenye Uwezo wa Kubaini Tatizo lako tu Pindi Utakapo Fanya Mawasiliano Kupitia Wasaa Husika.
 
Je una NUKSI  zisizo kwisha.!? JE umekimbiwa na Mume/Mke na Anaishi na Mtu Mwingine..!? Muone Akutatulie,
 
Una kosa bahati ya wanaume au mume wa kukuoa..Unataka nyota ing'ae Au huna hamu na Mkeo/ Mumeo.
 
Jini mahaba. Kama Unakasirika ovyo ukiwa na bwana au mwanamke wako na  kumchukia Mpaka  kushindwa kufanya nae tendo la ndoa.
 
Njoo umuone Sheikh Omary  na ujuwe  yanayo kusibu.Anatibu kwa Kutumia  Vitabu vya QUR-AN

Mawasiliano: Sheikh Omary 0673531992. WhatsApp/Call
Tembelea Page ya @Mtabibu_Omar  @Mtabibu_Omar
Usome Makala Tofauti Tofauti Kama.


Share:

MBUNGE WA CHADEMA AMMWAGIA SIFA MKUU WA MKOA WA KAGERA

Mbunge wa jimbo la Bukoba Mjini Mhe. Wilfred Muganyizi Rwakatare (Chadema) amepongeza Mkuu wa mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Elisha Marco Gaguti kwa kasi nzuri ya utendaji kazi inayochangia mkoa huo kuwa na maendeleo makubwa kwa muda mfupi huku akiwataka watendaji wa taasisi mbalimbali mkoani Kagera kutambua majukumu yao.
Rwakatare ametoa kauli hiyo katika mkutano wa wafanya biashara wa Tanzania (KAGERA ) na wafanya biashara kutoka nchi za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Burundi,Kenya Rwanda na Uganda uliofanyika katika ukumbi wa Elct uliopo Manispaa ya Bukoba wakati wa wiki ya uwekezaji Kagera.

Mbunge huyo ametaja kushangazwa na kasi ya utendaji kazi wa mkuu huyo wa mkoa kitendo ambacho kimesababisha mkoa huo kusonga mbele kwa haraka.

Aidha alimuomba mkuu huyo kuwa anakutana na wafanyabiashara wadogo na wakubwa mara kwa mara ili kujua changamoto zinazowakabili kupitia majadiliano na  kuzifanyia kazi ili Kagera ikue kiuchumi

Rwakatare pia alikemea tabia ya baadhi ya wafanyakazi wanaofanya kazi kwa mazoea kwani wanachangia kurudisha nyuma maendeleo.

Hata hiyo aliwataka viongozi mbalimbali wa vyama vya siasa kujenga umoja na ushirikiano ili mkoa wa Kagera usonge mbele.
Na Lydia Lugakila - Malunde1 blog Bukoba
Share:

Kutana na Mohamedi Buruhani Mwenye KUBRI kutoka kwa ALLAH .....Anauwezo wakufanya Dua mbalimbali Na Kutafsiri Ndoto

Kutana  na Mtabibu Mwenye KUBRI kutoka kwa ALLAH Mohamedi Buruhani Mtabibu wa Nyota za Binadamu  Mwenye UWEZO Kubaini tatizo lako Pindi tu Utakapo Fanya Mawasilino Kupitia Wasaa Husika..

JE UNASUMBULIWA NA Mapenzi? (Umeachwa na Umpendae,Awe Mume,Mke na Bado unampenda?Na  Umejaribu Sehemu nyingi Bila Mafanikio?Wasilina na Mohamed Buruani Ujione muujiza wa Papo kwa Papo.. 

Anauwezo WA KURUDISHA MAHUSIANO NA KUIMARISHA NDOA YAKO . Umekimbiwa na Mumeo,mkeo au Mpenzi na anaishi na mtu mwingine? Muone akutatulie ..Atamfanya Atimize Ahadi zote kwa Muda Mfupi.

Mohamed Buruhan Anatumia Jina la Muhusika au Picha Kumaliza Tatizo lako..

Anatibu kwa Kutumia  Vitabu vya QUR-AN, Anatafsiri Ndoto. ,KUSAFISHA NYOTA, Mvuto wa Mwili na BIASHARA, ...MIGUU Kufa GANZI na mengi zaidi (+255  715971688 au (+255  756914036

NB: TIBA KWA DINI ZOTE NA IMANI ZOTE...


Share:

KIONGOZI MBIO ZA MWENGE AGOMA KUZINDUA MRADI WA MAJI MPWAPWA

Na Mary Eliasi, Mpwapwa.
KIONGOZI wa mbio za Mwenge wa uhuru kwa mwaka 2019 Mzee Mkongea Ally amegoma kuzindua mradi wa maji wa Mzase uliopo wilayani Mpwapwa kutokana na kasoro mbalimbali za mradi huo, ikiwamo kukosekana kwa vielelezo vya  majibu ya vipimo vya mabomba kutoka maabara ya serikali.

Akizungumza  mara baada ya kukagua miundombinu ya mradi huo Mkongea amesema baada ya ukaguzi wao wameona kuna baadhi ya vitu walivyoomba kwenye mradi huo havipo lakini fedha zinaonyeshwa zilitengwa.
“ Tulifanya ukaguzi kwa pamoja tumeona kuna baadhi ya vitu vielelezo vyake havipo kama test za nondo kutoka maabara ya serikali haipo,test za zege haipo,test za bomba kutoka maabara ya serikali hazipo,ubaya wa hapa ni kwamba kazi hazikufanyika lakini kwenye certificate fedha zimelipwa,”amesema Mkongea.
Amesema kutokana na kasoro hizo inaonyesha utaratibu ulikiukwa kwa kufanya malipo hewa hivyo Mwenge wa Uhuru 2019 hauwezi kuzindua mradi huo.
Kutokana na kasoro hizo amemtaka  mkuu wa Wilaya hiyo Jabir Shekimweri kumpa taarifa za mradi mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na rushwa(TAKUKURU)wilaya ili ajiridhishe na matumizi ya pesa zilizotumika.
“Tunajua mkuu wa wilaya hili sio kosa lako  wala sio kosa la waheshimiwa wabunge,kuna wataalam ambao wanataalum ya injinia kuweza kusimamia miradi hii ndio wanakiuka utaratibu,mh mkuu wa wilaya tunakukabidhi taarifa ya mradi ili umkabidhi afisa Takukuru,kila eneo liangaliwe ili kujiridhisha matumizi ya fedha na baada ya wiki mbili taarifa itumwe makao makuu ya Takukuru,”amesema.
Pamoja na kasoro hizo Mkongea amesema wameangalia ubora wa maji kwa mujibu wa vipimo vya maabara na vimeonyesha kwamba maji ni salama kwa matumizi hivyo wananchi waendelee  kuyatumia.
Kwa upande wake waziri wanchi ofisi ya makamu wa Rais Muungano na Mazingira George Simbachawene amesema kitendo hicho kimekuwa ni fundisho kwa wao wanaoongoza jamii na kwa wataalam ili wanapoyasikia mapungufu hayo waweze kusema na katika vikao vya halmashauri.
Simbachawene ambaye ni mbunge wa Kibakwe ametumia nafasi hiyo kusisitiza wananchi kutunza vyanzo vya maji kwa kuheshimu sheria iliyopo ya kutofanya shughuli za kibinadamu ndani ya mita 60 kutoka katika vyanzo vya maji.
Akizungumza baada ya maelekezo hayo Shekimweri amesema wamepokea taarifa ya ukaguzi na watazingatia maelekezo yaliyotolewa na kuyafanyia kazi.
Mradi huo umegharimu kiasi cha sh mil 432.2 ukihusisha baadhi ya ujenzi wa miundombinu ikiwemo ujenzi wa kisima,nyumba ya mashine,ujenzi wa tanki la kuhifadhi maji,ujenzi wa mlango,ofisi ya jumuiya ya watumiaji maji na njia ya umeme mpaka eneo la kisima.
Share:

MAJERUHI MWINGINE AJALI YA MOROGORO AFARIKI....13 BADO HAWAJITAMBUI NA WAKO ICU


Mkuu wa Mkoa wa Morogoro  (RC) nchini Tanzania, Dk Stephen Kebwe amesema vifo vinavyotokana na ajali ya mlipuko wa moto iliyotokea Jumamosi iliyopita ya Agosti 10, 2019 mkoani humo vimeongezeka na kufikia 76.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumanne Agosti 13,2019 nje ya chumba cha kuhifadhia maiti cha Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Morogoro, RC Kebwe amesema idadi hiyo imefikia baada ya majeruhi mmoja aliyelazwa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Dar es Salaam kufariki usiku wa kuamkia leo.

Amesema majeruhi waliosafirishwa kwenda Muhimbili wengi walikuwa katika hali mbaya kwa sehemu kubwa ambapo mpaka sasa (asubuhi) wamebakia 38 wakiendelea na matibabu na katika Hospitali ya Rufaa Morogoro wamebaki 16 nao wakiendelea na matibabu.

Kwa upande wake, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Umma Hospitali ya Taifa Muhimbili, Aminieli Aligaesha  amesema  Majeruhi 13 kati ya hao  38 walionusurika katika ajali hiyo, waliolazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), hali zao bado ni  mbaya na wamelazwa katika Chumba cha wagonjwa Mahututi (ICU) wakiwa hawajitambui.

“Hadi leo Agosti 13, hiyo ndiyo idadi ya wagonjwa waliolazwa MNH, na wale ambao wamefariki tayari miili yao imepelekwa Morogoro na mmoja umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti hapa Muhimbili,” amesema Aligaesha.

Share:

Dereva lori la mafuta lililoteketea kwa moto Ruvuma Apatikana

Dereva Hurbet Mpete aliekuwa anaendesha lori la mafuta lililopata ajali Mkoani Ruvuma amepatikana akiwa hai.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma, Simon Marwa  amesema dereva huyo ana michubuko kidogo na amevunjika mbavu, hivyo wamempeleka Hospitali kwa matibabu zaidi.

RPC Marwa amesema uchunguzi zaidi unaendelea kujua chanzo cha ajali hiyo ingawa  shehena ya mafuta lita 33,000 alizobeba zimekutwa salama na mmiliki wa mafuta hayo ameshahamisha.

Lori hilo mali ya James Mwinuka ambaye ni mmiliki wa kampuni ya Njombe Filling station  lilipata ajali juzi Jumapili Agosti 11,2019 saa 4 usiku  baada ya kuacha  njia na kugonga mti Kijiji cha Hangangadinda mkoani Ruvuma. 

Katika ajali hiyo, kichwa chote cha Lori hilo kiliteketea kwa moto na kubakiza tank pekee lililokuwa na Lita 33, 000 za Petrol.


Share:

Matumaini ya Kupatikana Dawa ya Kutibu Ugonjwa wa Ebola Yaanza Kuonekana

Wizara ya Afya katika jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo imesema dawa mbili za majaribio ya kuutibu ugonjwa wa Ebola zinaonekana kuyanusuru maisha ya wagonjwa. 

Dawa hizo zinazotokana na kingamwili ,za watu walionusurika na ugonjwa huo hatari zimeonyesha mafanikio mema miongoni mwa wagonjwa waliozitumia, katika juhudi za kupambana na mripuko wa sasa wa Ebola Mashariki mwa Kongo. 

Aina nne za dawa zilikuwa zikifanyiwa majaribio, lakini aina mbili, REGN-EB3 na mAb114 zilionekana kuleta tija. Mbili nyengine, ZMapp na Remdesivir sasa imeamuliwa zisitumiwe. 

Mkurugenzi wa Taasisi ya Kimarekani kwa ajili ya magonjwa ya kuambukiza Antony Fauci amesema mafanikio ya dawa hizo ni habari njema, ambazo zinaashiria kupatikana tiba dhidi ya maradhi ambayo katika kipindi cha hivi karibuni hakuna aliyekuwa akifikiria. 

Shirika la Afya Ulimwenguni WHO limewahimiza wagonjwa wa Ebola kutafuta dawa hizo haraka.


Share:

Umoja wa Mataifa unachunguza visa 35 vya mashambulizi ya kimtandao ya Korea Kaskazini

Wataalam wa Umoja wa mataifa wanasema wanachunguza visa visivyopungua 35 kutoka nchi 17 ambazo raia wa Korea Kaskazini wanatumia mashambulizi ya mtandao kupata fedha kinyume cha sheria ili kufadhili mpango wake wa nyuklia na kutoa wito wa kuwekewa vikwazo kwa meli zinazoipatia mafuta nchi hiyo.

Wiki iliyopita shirika la habari la Associated Press liliripoti likinukuu ripoti iliyotolewa na wataalam hao wa Umoja wa Mataifa kuwa Korea Kaskazini imekuwa ikijipatia hadi dala bilioni mbili kutoka kwenye shughuli zake za kufanya mashambilizi ya mtandao dhidi ya taasisi za kifedha na maduka ya kubadilishia fedha.

Ripoti hiyo imefichua kuwa taifa jirani la Korea Kusini ndiyo limeathiriwa zaidi na shughuli hizo za uvamizi wa kimtandao ikirikodi visa 10, ikifuatiwa na India iliyoshambuliwa mara 3 huku Bangladesh na Chile zilirekodi kila moja visa viwili. 

Mataifa mengine 13 yamerikodi kisa kimoja kimoja cha mashmbulizi ya mtandao kutoka Korea Kaskazini.

-DW


Share:

TANZIA: Katibu BAWACHA Jimbo la Kawe afariki dunia




Share:

Tanzania kufanya jitihada Kiswahili iwe lugha ya SADC

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Profesa Palamagamba Kabudi amesema katika Mkutano wa 39 wa wakuu wa nchi na Serikali na kwenye mwaka mmoja ujao Tanzania itafanya jitihada kuhakikisha Kiswahili kinakuwa lugha rasmi ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).

Waziri Kabudi ameyasema hayo jijini Dar es Salaam baada ya kukabidhiwa uenyekiti wa Baraza la Mawaziri wa nchi za SADC na ataifanya kazi hiyo kwa mwaka mmoja.

Profesa Kabudi amewaeleza waandishi wa habari kuwa, katika mwaka mmoja ujao, SADC pia itaendeleza harakati za kuitaka jumuiya ya kimataifa ishinikize Zimbabwe iondolewe vikwazo vya kiuchumi.

"Zimbabwe imewekewa vikwazo vya kiuchumi kwa muda na tunadhani vikwazo hivyo havina sababu ya kuendelea kwa sababu Zimbabwe imekwishafanya uchaguzi, Rais amechaguliwa na maendeleo wananchi wanaendelea vizuri sasa ni wakati wa vikwazo vya kiuchumi kuondolewa kwa Zimbabwe ili Zimbabwe iendelee" amesema Waziri Kabudi.




Share:

Shehena ya malori ya dawa Yatua Muhimbili Kuwasaidia Majeruhi Ajali ya Moto Morogoro

Bohari ya Dawa (MSD) imekabidhi dawa na vifaa tiba kwa Hospitali ya Taifa Muhimbili, kwa ajili ya kuwahudumia majeruhi wa ajali ya moto waliohamishiwa hospitalini hapo kutoka mkoani Morogoro baada ya Kutokea kwa mlipuko wa mafuta Msamnvu Morogoro. 

Makabidhiano haya ya dawa ni mwitikio wa maombi ya dharura yaliyoombwa na Hospitali Muhimbili kwa ajili na majeruhi hao.

Meneja wa MSD, Kanda ya Dar es Salaam Bw. Celestine Haule amesema mpaka sasa jumla ya shehena ya malori matano yameshakabidhiwa Muhimbili zikiwemo dawa muhimu zinazotumika kwa ajili ya kuokoa maisha ya majeruhi hao.



Share:

Acacia yaruhusiwa kuendelea kusafirisha Dhahabu kutoka mgodi wa North Mara

Kampuni ya Acacia imeruhusiwa kuendelea na utaratibu wa kusafirisha dhahabu baada ya kuzuiliwa kwa takribani mwezi mmoja na Tume ya Madini Tanzania

Taarifa iliyotolewa na Acacia inaeleza sasa wataanza kusafirisha madini kutoka North Mara baada ya kutimiza masharti

Hata hivyo, Tume ya Madini imesema inaamini baadhi ya vipengele vya kanuni ya madini ya mwaka 2010 vilikiukwa na imewataka kuwasilisha mpango wa uchimbaji na ripoti ya upembuzi yakinifu ifikapo Ijumaa ya wiki hii

Acacia imekuwa kwenye mvutano wa muda mrefu na Serikali baada ya kuzuiwa kusafirisha Makinikia nje ya nchi kwa madai ya kutolipa mrabaha stahiki


Share:

Serikali Yaagiza Mashamba Makubwa ya Tumbaku Yapimwe

Serikali  imeuagiza uongozi wa mkoa wa Tabora kuhakikisha mashamba makubwa ya tumbaku yanapimwa.

Akizungumza na viongozi wa mkoa wa Tabora leo Jumanne Agosti 13, 2019, Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi nchini Tanzania, Angelina Mabula amesema kwa kutopimwa mashamba hayo ina maana Serikali  inakosa mapato.
 
Awali, mkuu wa mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri amemweleza naibu waziri kuwa migogoro ya ardhi mkoani Tabora imepungua kwa kiwango kikubwa kutokana na jitihada mbalimbali zilizofanywa na mkoa pamoja na wilaya kwa kushirikiana na ofisi ya Ardhi kanda ya Magharibi.


Share:

CHAVITA TANGA WATAKA WAKALIMANI KILA KITUO WAKATI WA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA



CHAMA cha Viziwi mkoani Tanga (Chavita) wametoa wito kwa serikali kuweka wakalimani katika kila kituo cha kupigia kura wakati wa uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu ili kurahisisha mawasiliano kwao.

Hayo yalisemwa jana na Katibu wa Chama hicho mkoani Tanga Nassoro Ally wakati akizungumza na gazeti hili ofisini kwake ambapo alisema pia wanatoa wito kwa serikali kuwaboreshea mazingira kwa kuwapatia elimu ya uraia

Alisema kwani uwepo wao kwenye maeneo husika itawasaidia na kuwawezesha kuweza kutekeleza wajibu wao kwa waledi mkubwa kwa kutimiza haki yao ya kikatiba kuchagua viongozi ambao wanaweza kuleta maendeleo kwao na jamii zinazowazunguka kwenye chaguzi hizo.

“Kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa nitoa wito kwa serikali kuona namna bora ya kuweza kuweka wakalimani kwenye vituo vyote vya kupigia kura kwa lengo la kurahisisha mawasiliano “Alisema.

Akizungumzia changamoto ambazo zinawakabili alisema kwamba kubwa inayowakabili ni kukosekana kwa ushirikishwaji katika vyombo vya kutoa maamuzi ngazi ya mkoa na wilaya.

Aidha alisema pia vikwazo nyengine wanavyokutana navyo ni kuwepo kwa urasimu katika utoaji wa huduma za kijamii unaofanywa na maafisa ustawi wa jamii pindi wanapofuatilia hazi zao kwa kupewa majibu ya kuwakatisha tamaa.

Katibu huyo alisema pia vikwazo vingine kwao ni kutokuwa na uwazi katika utoaji wa huduma kwa makundi maalumu jambo ambalo limekuwa likiwakwamisha kwenye baadhi ya mambo muhimu kwao. 

“Katika hili tunatoa ushauri kwa serikali iwe inafuatilia kwa undani watoaji wa huduma kwani baadhi yao wanafanya kwa mazoea jambo ambalo linawapa wakati mgumu “Alisema

Hata hivyo alisema licha ya serikali kutenga asilimia 2 ya mapato ya ndani kwa ajili ya huduma kwao lakini wananyimwa fungu hilo kwa mwaka na asilimia 4 kwa ajili ya kukopesha walemavu upatikaji wake sio wa haki kwa sababu wanaunganishwa wasio na ulemavu.

Mwisho.
Share:

Takukuru Dodoma Yaokoa Zaidi Ya Tsh.milioni 135

Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa[TAKUKURU] mkoa wa Dodoma imeokoa Jumla ya Tsh.Milioni 135,laki 9 ,48 elfu  na mia 193 kwa kipindi cha miezi 6.

Akizungumza na  Mtandao  Wa Mpekuzi Blog Mapema leo Agosti 13,2019  Ofisini  kwake jijini Dodoma,Mkuu wa TAKUKURU Mkoani Dodoma ,Bw.Sosthenes Kibwengo amesema Fedha hizo zimeokolewa kwa kipindi cha Miezi 6 kuanzia  Mwezi Januari,hadi Juni ,2019.

Bw.Kibwengo amesema kwa kipindi cha miezi sita pia zimedhibibitiwa Jumla ya Tsh.Milioni 322,laki 3 ,48 elfu na mia 989.

Aidha,Bw.Kibwengo amebainisha kuwa katika kipindi hicho cha miezi 6 kuanzia Januari hadi Juni ,2019 TAKUKURU Mkoa wa Dodoma  imepokea jumla ya Malalamiko 231  ya vitendo vya rushwa .

Bw.Kibwengo amesema asilimia 28% ya Malalamiko hayo yanatoka Serikali za mitaa[TAMISEMI],Ardhi kwa asilimia 26.5%,Polisi 7% na mahakama   malalamiko kwa asilimia 6% na asilimia zilizobaki ni kwa sekta nyingine huku akitaja Wilaya iliyo na Malalamiko mengi ni Wilaya ya Dodoma Mjini.

Pia amesema kuanzia mwezi huu wa Agosti ,2019 wanatarajia kufungua ofisi za TAKUKURU Eneo la Chemba huku akitoa wito kwa wananchi kuwa na ushirikiano na Taasisi hiyo na kuweza kuitumia namba ya bure 113 pindi wanapoona vitendo vya rushwa.


Share:

PICHA: Waziri Kabudi Akabidhiwa Uenyekiti Wa Mawaziri Wa SADC

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Tanzania, Profesa Palamagamba Kabudi amekabidhiwa uenyekiti wa Baraza la Mawaziri wa jumuiya hiyo na Naibu Waziri Mkuu wa Namibia na Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo Mhe. Netumbo Nandi- Naitwah aliyemaliza muda wake ikiwa ni sehemu ya mkutano huo utakaohitimishwa na wakuu wa nchi wanachama Agosti 17 na 18, 2019.
Naibu Waziri Mkuu wa Namibia na Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo Mhe. Netumbo Nandi- Naitwah (kulia) akimkabidhi Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Tanzania, Profesa Palamagamba Kabudi kijiti cha uenyekiti wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) iliyofanyika mapema leo Agosti 13, 2019 wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Mawaziri wa Nchi za SADC unaondelea jijini Dar es Salaam, Tanzania. Ambapo Tanzania ni mwenyeji wa Mkutano huo wa 39.
Naibu Waziri Mkuu wa Namibia na Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo Mhe. Netumbo Nandi- Naitwah akimpa maneno ya usia  kwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Tanzania, Profesa Palamagamba Kabudi (kushoto).
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Tanzania, Profesa Palamagamba Kabudi (kushoto) akipokea ngao ikiwa ni ishara ya kuupokea uenyekiti wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Tanzania, Profesa Palamagamba Kabudi (kushoto) akipokea ngao ikiwa ni ishara ya kuupokea uenyekiti wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).
Naibu Waziri Mkuu wa Namibia na Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo Mhe. Netumbo Nandi- Naitwah akitoa hotuba yake wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Mawaziri wa Nchi za SADC unaondelea jijini Dar es Salaam, Tanzania. Ambapo Tanzania ni mwenyeji wa Mkutano huo wa 39.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Tanzania, Profesa Palamagamba Kabudi akitoa hotuba yake mara baada ya kukabidhiwa uenyekiti wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) iliyofanyika mapema leo Agosti 13, 2019 wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Mawaziri wa Nchi za SADC unaondelea jijini Dar es Salaam, Tanzania. Ambapo Tanzania ni mwenyeji wa Mkutano huo wa 39.
Mawaziri wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) wakifuatilia kwa makini ufunguzi huo.
Mawaziri wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) wakiwa katika picha ya pamoja.


Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger